Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 874 | 875 | (Page 876) | 877 | 878 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Leo ni siku ya kuzaliwa Mhandisi David E.P.Ngula. Familia yake, ndugu, jamaa, marafiki na majirani wanamtakia Heri ya Siku hii na kumuombea kwa Mungu ambariki afya njema katika maisha yake ili apate kuzima  mishumaa mingi zaidi. 

  0 0

   Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin W. Mkapa (kushoto) akisalimiana na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback (kulia) mara tu alipowasili katika uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itayoanza kutumiwa rasmi na wateja wa benki hiyo. (Katikati) ni Mkurugenzi mkuu wa benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker
   Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumiwa na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam .
   Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa wadau wa NMB wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Mastercard itakayoanza kutumika hivi karibuni kwa wateja wake. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency jijini Dar es Salaam.  
   Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini W. Mkapa akihutubia wadau wa benki ya NMB kabla ya kuzindua rasmi huduma mpya ya Mastercard ya benki ya NMB ambayo itatumika rasmi kwa wateja wake hivi karibuni. Hafla iliyofanyika katika hoteli ya Haytt Regency Kilimanjaro Hotel.
  Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara tu baada Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin W. Mkapa kuzindua rasmi huduma mpya ya NMB Mastercard. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency, jijini Dar es Salaam.

  0 0

    Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), akiwasilisha kwa Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza maamuzi ya Mkutano wa  Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 31 Mei, 2015 Jijini Dar es Salaam. Mhe. Mwakyembe  aliongoza ujumbe wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ziara ya kikazi nchini Burundi tarehe 15 Juni, 2015.
  Rais Nkurunziza akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula walipowasili kwa ajili ya kuzungumza nae.
  Mhe. Rais Nkurunziza akizungumza na Ujumbe uliomtembelea. 
  --------------------------
  Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) aliongoza ujumbe wa Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ziara ya kikazi iliyofanyika nchini Burundi tarehe 15 Juni, 2015.

  Ziara hiyo imefanyika kufuatia maelekezo ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (The Emergency Meeting of the EAC Heads of State) ambao ulifanyika tarehe 31 Mei, 2015, Dar es Salaam kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa nchini Burundi hususan katika kipindi hiki ambacho wanaelekea kwenye uchaguzi Mkuu.

  Dhumuni la ziara ya Mawaziri hao nchini Burundi lilikuwa ni kuwasilisha rasmi maamuzi yaliyotokana na kikao hicho ambacho kiliwaelekza Mawaziri kuwasilisha mara moja maamuzi yaliyotokana na kikao hicho kwa Serikali ya Burundi.

  Kwenye Jopo hilo la Mawaziri hao alikuwepo Mhe. Shem Bageine, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda ambaye alifuatana pia na Mhe. Philemon Mateke Waziri wa Nchi anayesimamia masuala ya Mtagamano na Mhe. Elen Molekane, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini. Pia Katika Ujumbe huo alikuwepo Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
  Serikali ya Rwanda na Kenya ziliwakilishwa na Balozi zao nchini Burundi. Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo alimwakilisha Katibu Mkuu. Kwa upande wa Serikali ya Burundi alikuwepo Mhe. Leontine Nzeyimana, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Edourd Nduwimana Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.

  Akiwapokea Mawaziri hao, Mhe. Pierre Nkurunziza, Rais wa Burundi alisema kuwa amepokea maamuzi ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na tayari utekelezaji wake ulianza mara moja. Aliongeza kusema kuwa karibu asilimia themanini ya maamuzi hayo yameshatekelezwa ikiwemo kusogezwa mbele kwa tarehe za Uchaguzi Mkuu ambapo  kwa kuzingatia kalenda mpya, uchaguzi wa Wabunge na Madiwani utafanyika tarehe 29 Juni, 2015 na Uchaguzi wa Rais utafanyika tarehe 15 Julai, 2015.

  Mhe. Rais Nkurunziza alifafanua kuwa, asilimia ishirini iliyosalia itatekelezwa baada ya Uchaguzi Mkuu kwa sababu inahitaji ushirikishwaji wa wananchi wote. Moja ya maamuzi hayo ni suala la kufanyia marekebisho Katiba ya Nchi; kuendeleza mazungumzo ya mustakabali wa Burundi na kufanyia marekebisho Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

  Aidha Mhe. Rais Nkurunziza alieleza kuwa, Serikali imeanza utaratibu wa kuvinyang’anya silaha vikundi vyote na hadi sasa tayari wamekusanya silaha laki moja. Pia Serikali imeanza kuchukua hatua za dhati za kuwarejesha Wakimbizi na kwamba mpaka sasa zaidi ya wakimbizi 40,000 wamesharejea Burundi na vilevile Vyama vyote vya siasa viko tayari kuendelea na uchaguzi kama ilivyopangwa na vinaendelea na kampeni.  Imetolewa na: Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dar es Salaam

  18 Juni, 2015


  0 0

  MSHAMBULIAJI wa timu ya Stand United, Abasarim Chidiebele akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga leo mara baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuitumikia timu ya Coastal Union.
  Habari na picha na 
  Mwandishi wetu, Tanga
  SHAMBULIAJI wa timu ya Stand United,Abasarim Chidiebele amesaini mkataba wa kuitumikia timu ya Coastal Union kwa mkataba wa miaka mmoja katika msimu ujao wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
  Chidiebele atua mkoani Tanga juzi kwa ajili ya kuingia makubaliana na uongozi wa timu ya Coastal Union ambapo utiliaji saini huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi, Meneja wa Coastal Union, Akida Machai na viongozi wengine.
  Akizungumza mara baada ya kusaini,Chidiebele amesema kuwa amefurahi kusajiliwa na Coastal Union na kuhaidi kutumia uwezo wake aliokuwa nao kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao.
    “Nashukuru kusajili Coastal Union kikubwa niwahaidi tu wapenzi,wanachama na mashabiki kutumia uwezo wangu katika kuipa mafanikio timu yetu “Alisema Mshambuliaji huyo ambaye ni tishio hapa nchini.
  Kwa upande wake,Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema kuwa msimu huu timu hiyo imedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakaowawezesha kuhakikisha wanachukua ubingwa wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
     “Unajua usajili wetu sio wa kukurupuka hivyo lazima tuwe makini kwani hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuhakikisha tunatimiza mipango yetu ya kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao “Alisema.
  Hata hivyo aliwataka wapenzi mashabiki kuweka mshikamano wa pamoja ambao utatuwezesha kufanikisha malengo yao ya mwakani kushiriki kombe la shirikisho kwa kuanza kufanya vizuri katika michuano ya Ligi kuu.

  0 0

  Mchumi Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Octavian Rutta akizungumza na TBC1 kuhusu masuala ya Uwekezaji na Uwezeshaji wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam. 
  Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisalimiana na Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa sasa Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima  muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga Ndugu Chima na kumkaribisha Ndugu Smythies Pangisa (katikati) aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara sasa Mkoa wa Rukwa. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 13 Juni 2015 katika ukumbi wa Kanyau Sumbawanga Mkoani Rukwa.
  Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo ambaye pia ni Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Chang'a akitoa salam za utangulizi katika hafla hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza katika hafla hiyo. Aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na ubunifu mkubwa na kwamba  ndiyo siri pekee ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Na Mchungaji Ipyana Mwakabonga
  Tembelea Tovuti ya Ibada ya Kiswahili - Ohio 

  0 0
 • 06/18/15--07:58: ......LOADING


 • 0 0

  Kampuni ya Kitanzania inayomilikiwa na Bw. Twalib Lubangula imepata tenda kubwa nchini Zambia ya kukarabati viwanda vya Cement Ndola na sehemu nyingine nchini. 
  Ni jambo la kujivunia kuwa Kampuni inayomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100 kupata tenda kubwa nchi za nje na kampuni hiyo inafanya vizuri sana. 
   Mhe. Grace J. E. Mujuma Balozi wa Tanzania nchini Zambia  akipata maelezo kuhusu mafanikio ya Kampuni ya Pan African Refractory Services Co. Ltd ya Tanzania kutoka kwa mmiliki wa kampuni hiyo Bw. Twalib A. Lubangula baada ya kuutembelea Ubalozi jijini Lusaka kwa ajili ya kujitambulisha leo.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyarandu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015. Picha zote na CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
  Balozi wa Mpya wa Kampeni ya Kupambana na Ujangili wa Tembo, Msanii wa mziki wa kizazi kipya Ali kiba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kampeni mpya ya kupambana na ujangilli wa Tembo uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.
  Afisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation, Dk. Patrick Bergin akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya sifa ya wanyamapori katika hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam Juni 18, 2015.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Ole Porokwa akitambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) kwa umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Mkoa wa Manyara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya Mkoa huo wilayani Babati Juni 18.2015, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,200.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akikabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Babati, Daniel Ole Porokwa fomu zilizotiwa saini na wanachama wa CCM, nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Manyara Juni 18.2015, kwa ajili kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,200.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akionyesha fomu yenye orodha ya majina ya wadhamini wake baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Babati, Daniel Ole Porokwa (kushoto), nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Manyara Juni 18.2015, kwa ajili kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,200.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa Mkoa wa Manyara, waliofika katika Ofisi ya CCM ya Mkoa huo wilayani Babati Juni 18.2015, kwa ajili ya kumdhamini iliaweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 1,200.

  0 0

  Hon. Adel Al Jubeir, Minister of  
  Foreign Affairs of Saudi Arabia
  Hon. Bernard K. Membe (MP), Minister of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to Hon. Adel Al Jubeir, Minister of Foreign Affairs of the Royal Kingdom of Saudi Arabia following his appointment as Minister of Foreign Affairs of the Royal Kingdom of Saudi Arabia.

    The message reads as follows;

  “Hon. Adel Al Jubeir,

  Minister of Foreign Affairs of the Royal Kingdom of Saudi Arabia,

  RIYADH

  Honourable Minister,

  On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I would like to take this opportunity to extend to you Honourable Minister our warmest congratulations for your appointment as Minister of Foreign Affairs of the Royal Kingdom of Saudi Arabia. Your appointment is a clear testimony of the trust His Royal Highness the King of Saudi Arabia has on your vast and rich knowledge on international affairs and ability to guide foreign policy of the Kingdom of Saudi Arabia.

  I would like to assure you of my personal commitment as well as that of my Government to continue working closely with you and the Royal Government of the Kingdom of Saudi Arabia at both bilateral and multilateral levels.

  While wishing you continued personal good health, happiness and prosperity and great achievements in your new roles, please accept the assurances of my highest consideration”.

  Issued by: Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam.

  18th June, 2015


  0 0

   Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kushoto akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM  kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro mjini
   Dkt. Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa Wanachama na udhamini likiendelea katika Ofisi za CCM Wilaya ya Morogoro mjini.

   Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Morogoro Mjini akikagua kadi za wanachama waliojitokeza kumdhamini Waziri Magufuli.

   . Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akinyoosha juu fomu zake za wadhamini walijitokeza kumdhamini katika Mkoa wa Morogoro.

   Dkt. Magufuli akisalimiana na baadhi ya Wanachama wa CCM mkoani Morogoro waliojitokeza kumdhamini.

   Vijana wa Morogoro wakimshangilia Waziri Magufuli mara baada ya kutoka kwenye Ofisi za CCM Wilaya.  0 0  Mtangaza nia kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao Charles Makongoro Nyerere leo amekamilisha ziara ya  kutafuta wadhamini mikoani.Ziara yake ameikamilisha katika mkoa wa Shinyanga.Katika hotuba yake ya kukamilisha ziara yake,Makongoro Nyerere amekemea vitendo vya mafisadi aliodai hawazidi 20,anaowafahamu sura,majina na tabia zao ambao wamekuwa kikwazo hata kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete,aliodai kuwa wengi ni marafiki zake na rais.
   
  Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akikabidhi fomu ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere
  Makongoro Nyerere akishikana mkono na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid
  Makongoro Nyerere akionesha mkoba uliobeba Fomu zake baada ya kukamilisha zoezi la kupata wadhamini na kuelekea Dodoma kwa ajili ya kukabidhi fomu hizo makao makuu na kubiri jina lake lipitishwe na kikao cha halmashauri kuu ya CCM Julai,12 mwaka huu. Mwandishi Kadama Malunde, ametuletea hizi picha na h0tuba ya Mhe Makongoro BOFYA HAPA

  0 0

   Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha  Leonce Matley akikabidhi  misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika .
  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Meru jijini Arusha  Leonce Matley akikabidhi  misaada kwa Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha St.Joseph Christina Mnate juzi walipotembelea kituo hicho na kutoa misaada ya chakula na vifaa vya shule katika kituo hicho kilichopo kata ya Moshono jijini Arusha ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mtoto Afrika.

  0 0


  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780. Picha Othman Michuzi.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.
  Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Muheza sambamba na kuwatakia Heri ya Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini watakamuwezesha kupata ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 18, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa alipata wasaa wa kwenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajab, Marehemu Mzee Rajab nyumbani kwao Muheza, Mkoani Tanga. anaezungumza na Mh. Lowassa ni Mama Mzazi wa Mh. Adadi Rajab, Bi. Fatuma Omar.
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (katikati) pamoja na wananchi wa Korogwe wakiwa wamefunga barabara kuuzuia msafara wa Mh. Lowassa ili aweze kuzungumza nao, huku wakimuuga mkono katika safari ya Matumaini.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais asiye na wizara maalum Profesa Mark James Mwandosya akiwa na mkewe Mama Lucy Mwandosya wakiwasili katika ofisi za CCM za Mkoa wa Iringa kusaka wadhamini 
   Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais asiye na wizara maalum Profesa Mark James Mwandosya akilakiwa na maofisa wa chama katika ofisi za CCM za Mkoa wa Iringa kusaka wadhamini 
  Waziri wa Nchi katika ofisi ya Rais asiye na wizara maalum Profesa Mark James Mwandosya akipungia mkono wasindikizaji wake katika uwanja wa ndege wa Iringa baada ya  kusaka na kupata wadhamini wa kutosha. 
  Picha na video na Francis Godwin
  Habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiswaga Ng'ombe kuingia kwenye josho katika kijiji cha Nyakwasi, Nyang'hwale mkoani Geita.Kinana aliwapongeza wana kikundi cha Songambele kwa kupambana na magonjwa ya mifugo kwa kujenga josho la kisasa,Pia Ndugu Kinana aliwaasa Vijana kufanya kazi kwa bidii n,a kuacha kukaa vijiweni kupiga sogakwani hakuna njia ya mkato ya maisha,badala yake ni kufanya kazi kwa bidii ikiwemo suala zima la kujiletea maendeleo kama vile kujishughulisha na ufugaji,ukulima ili kujikwamua na Maisha,Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  yupo mkoani Geita akitokea mkoani Kagera katika ziara ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010-2015 pamoja na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiangalia baadhi ya miradi ya akina mama wajasiliamali wa Nyang'hwale.
  Katib Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwasha mashine ya kukoboa na kusaga,ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi huo wa akina mama Wajasiliamali,katika kijiji cha Nyamgogwa,wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kharuma ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa ili nchi isonge mbele inabidi matumizi yasiyo ya lazima yapunguzwe na vijana kuamini kuwa maisha ni kuchapa kazi na si kukaa vijiweni,aliwataka wananchi hao kuchagua viongozi wenye moyo na watu.
  Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amaliakihutubia wakazi wa Kharumwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliokusanya wananchi wengi kuliko kawaida. 
   Katibu wa Itikadi na Unezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kharumwa,wilaya ya Nyang'hwale na kuwaambia kuwa Kiongozi ni mtu mwenye moyo wa uvumilivu na usikivu, kiongozi wa siasa hapaswi kuwa na mashitaka ya kupiga watu.
   Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale akihutubia wananchi wa kaa ya Kharumwa waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa michezo wa Kharumwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.


  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na Mwaandishi wa habari wa Magazeti ya Serikali (Daily News & Habari Leo),Bwa.Pius Lugonzibwa katika kijiji cha  Nyijundu,Wilayani Nyang'hwale mkoani Geita,alipokwenda kushiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari ya Nyijundu.

  PICHA NA MICHUZI JR-NYANG'HWALE,GEITA.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha mkoba wa wenye fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa Fomu hizo katiuka Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono Wanachama wa CCM waliofika Viwanja vya Jengo la Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo  wakati alipofika kuchukua fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein

   Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakisherehekea wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokwenda kuchukua fomu kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwanndui Mjini Unguja leo
   Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipozungumza nao baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar katika Ofisi ya CCM Kisiwanndui Mjini Unguja leo

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  akionesha Fomu za kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipokuwa akizungumza nao baada ya kuchukua fomi hizo (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipozungumza na 

  Viongozi wa Chama cha Mapinduzi waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo baada ya   
  kuchukua fomu za kuomba ridhaa kwa Chama cha Mapinduzi kumteuwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar. 
  Picha na Ikulu, ZNZ

  0 0


older | 1 | .... | 874 | 875 | (Page 876) | 877 | 878 | .... | 3282 | newer