Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR AZINDUA BARAZA LA WAUGUZI NA WAKUNGA

$
0
0
Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar           
Waziri wa Afya  wa Zanzibar Rashid Seif ameliagiza Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar kusimamia kwa karibu watendaji wa kada hiyo ili  waweze kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Baraza Wauguzi na Wakunga katika Chuo cha Sayanzi ya Afya Mbweni, Waziri Rashid Seif amesema wauguzi na wakunga ni walezi wanaoshughulikia matatizo ya watu  hivyo wanatakiwa  kutekeleza wajibu wao kwa uadilifu.

Amesema wananchi wanapofika Hospitali na vituo vya Afya wanategemea  hifadhi na kinga ya wauguzi kabla ya kuonana na daktari na kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambayo yanahitaji kutafutiwa ufumbuzi na Baraza hilo.
Mrajisi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Haji  Haji Khamis akieleza mchakato wa kulisajili Baraza la Wauguzi na Wakunga  katika uzinduzi rasmi uliofanyika Chuo cha Sayansi ya Afya Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza mgeni rasmi katika uzinduzi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga Zanzibar kwenye sherehe za uzinduzi wa Baraza hilo.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi Waziri wa Afya Rashid Seif na wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga mara baada ya uzinduzi rasmi.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar. 


MSIBA NEW YORK NA TANZANIA.

$
0
0
MAREHEMU MZEE ALFRED MAGEGE.


Jumuiya ya Watanzania New York,New Jersey,Connecticut na Pennsylvania inaungana na Familia ya Magege kwa masikitiko kutangaza kifo cha marehemu Mzee Alfred Magege kilichotokea jumamosi June 13,2015. Marehemu Alfred Magege alisumbuliwa na Saratani ya mifupa kwa zaidi ya miaka kumi.Marehemu ameacha Mke na watoto watatu. Kama kawaida yetu tunaombwa watanzania tujitokeze ili kuwafariji wafiwa.Ili tukamilishe Msiba huu kiasi cha $10,000 kinahitajika.Watanzania tuungane,tujitolee kwa hali na Mali tusaidiane kumzika Mtanzania mwenzetu.Michango yenu inahitajika kwaajili ya mazishi yatakayofanyika New York, Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Tuchangie kupitia www.gofundme.com/wyfewd5

 Msiba utakuwa Address hii:
 2939 Wilson Avenue,Bronx,NY,10469.
 Kwa taarifa zaidi tuwasiliane na wafuatao. 
Hajji Khamis:3476238965
 Miriam Abu:9143162814
 Seif Akida:9175573195
 Buyamba Magege(Son):6469431104 
Geoffrey Ngullu:2675826276 
Amy Magege:5169467859 

Uongozi 
NY Tanzanian Community.

BENKI YA NMB YAZINDUA RASMI FAMILIA YA KADI ZA BENKI “MASTERCARD DEBIT” ZINAZOKUBALIKA KIMATAIFA

$
0
0
 Wadau wa benki ya NMB pamoja na wageni waalikwa wakisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, akiwahutubia wadau wa Benki ya NMB wakati wa hafla ya uzinduzi wa kadi hiyo mpya ambayo itaanza kutumiwa rasmi na benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Haytt Regency zamani Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa bodi, benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa Benki hiyo, Bi. Ineke Bussemaker (katikati) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard iliyozinduliwa rasmi na benki hiyo katika hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. (Kulia) ni Afisa wa Master Card kanda ya Afrika ya kati Bw. Michael Mieback aliyehudhuria mkutano huo.
  Mwenyekiti wa bodi benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja (kushoto), Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ineke Bussemaker (katikati) pamoja na Rais wa Master Card kanda ya Afrika ya kati, Bw. Michael Mieback, (kulia) wakiteta jambo kabla ya uzinduzi wa huduma mpya ya MasterCard itakayoanza kutumika katika benki hiyo. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.

MIKOA YA SHINYANGA NA MWANZA YAENDELEA UBABE MBIO ZA BAISKELI

$
0
0
Na mwandishi wetu.
Washiriki wa mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge” kutoka mikoa ya Shinyanga na Mwanza wameendelea kuudhihirisha umma wa wakazi wa kanda ya ziwa na watanzania kwa ujumla kuwa mpaka sasa hawana mpinzani baada ya washiriki wa mbio hizo kuibuka kidedea katika fainali za kumtafuta mshindi wa kanda hiyo.

Washiriki wa mikoa hii miwili wamejinyakulia nafasi zote za juu na hivyo kuwashinda wenzao wa mikoa mingine ya Kanda ya ziwa ikiwemo Kagera, Mara, Geita na Simiyu.

Katika mbio za wanaume za umbali wa kilometa 156.6 kutoka Kahama mpaka Tinde na kisha Kurejea Kahama, mshindi wa mwaka jana Masunga Duba (Mwanza) aliibuka tena kidedea huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Lupilya Hamis(Shinyanga) na nafasi ya tatu ikimuendea Kulwa Tuki(Shinyanga), washindi hawa wamejinyakulia kitita cha pesa taslimu Sh1,500.000/- kwa mshindi wa kwanza, Sh1,200.000/= mshindi wa pili na Sh800,000/= kwa mshindi wa tatu.

Kwa upande wa mbio za wanawake za umbali wa kilometa 80, kutoka Kahama mpaka Mwakata Kisha kurejea Kahama, timu ya mkoa wa Mwanza imedhihirisha kuwa wao bado ni mabingwa kwa kuibuka tena washindi wa mbio hizo, huku mshindi wa mbio za Mwaka jana Martha Antony, akiibuka mshindi wa kwanza akifuatiwa na Laulensia Luziba na nafasi ya tatu ikienda kwa Veronica Simon. Washindi hao wamepata zawadi ya pesa taslimu Sh1,200.000/= kwa mshindi wa kwanza, Sh800,000/= mshindi wa pili na Sh600,000/= mshindi wa tatu.
 Mmoja wa washiriki wa mbio hizo akinywa maji wakati wa mashindano hayo.
Mshindi wa mbio za Acacia Tufanikiwe Pamoja Lake Zone Cycle Challenge, Masunga Duba aliyeinua mikono akishangilia mara baada ya kumaliza mbio hizo akiwa mbele ya wenzake. Mshindi huyo anatoka mkoa wa Shinyanga.
 Washindi wa mbio za wanawake (kilometa 80). Aliyesimama katikati ni Martha antony ambaye ndio aliibuka mshindi wa kwanza, akifuatiwa na Laulensia Luzuba, (mwenye mtoto) aliyekuwa mshindi wa pili na Veronica Saimon (wa kwanza kushoto) aliyejinyakulia nafasi ya Tatu.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGA RASMI MATANGAZO YA TELEVISHENI YA MFUMO WA ANALOJIA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibofya kitufye cha Lap Top kuashiria kufunga rasmi Matangazo ya Televisheni ya Analojia, baada ya kufikia ukomo rasmi hii leo Juni 17, 2015 baada ya kufanikiwa kuzima mitambo ya Analojia kwa nchi nzima. Sherehe hizo za ukomo zimefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima za Digital Tanzania, Bi. Asteria Kamara, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, wakati wa sherehe za Ukomo wa Matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Ngao ya Heshima za Digital Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano Tanzania, TCRA, Prof, John Nkoma, wakati wa sherehe za Ukomo wa Matangazo ya Televisheni ya Analojia, zilizofanyika leo Juni 17, 2015 kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa. (wa pili kulia) ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo , Dkt. Fenella Mukangara. 

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

HUAWEI TANZANIA NA WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na kampuni ya Huawei katika kongamano la Teknohama, kulia ni Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala.
Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kongamano la Teknohama kushoto ni Mkurugenzi wa ICT katika wizara ya mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba
Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally Simba (Kushoto) wakishikana mkono na Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kuashilia kuungana katika kongamano la Teknohama.

Kampuni ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Technolojia jana ilitangaza kuwepo kwa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Center JNICC tarehe 18 na 19 Juni 2015.

Kongamano hilo litajadili hali ya sekta ya tecknohama kwa sasa,sera mpya zitakazowekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini.pia kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake ya milenia kupitia tecknohama.

Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Dk. Ally Simba alisema, “tumefurahi sana kwamba Wizara na kampuni ya Huawei Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo,ambapo tutajadiliana kwa undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT.Na kwa upande wa Wizara tutaelezea sera mpya na mipango tulioweka ili kuhakikisha maendeleo ya sekta”.

Aliendelea kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba Wizara imejikita katika kukuza sekta ya Teknohama.aliongeza kwamba Makamo wa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi,huku pia ,Waziri na Katibu Mkuu wa Wizaraya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Balozi wa China nchini Tanzania watakuwepo.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana Samson Majwala alisema, “tunaishukuru sana Wizara kwa kukubali kuungana nasi katika kuandaa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference nchini Tanzania,na tunawahakikishia Watanzania wote kwamba kongamano litapendeza.

Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.

Katika kongamano hilo,Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na Fusonq.Pia kutakua na gari maalumu la kufanya maonesho,gari hilo kwa kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani,na kwa mwaka wa 2015 litazuru bara la Afrika haswa Afrika kusini na Afrika Mashariki,Tanzania ikiwemo ya nchi itakayopita.

TANAPA WAKABIDHI MRADI WA UJENZI WA DARAJA KATIKA VIJIJI VYA SINGANA SUNGU WILAYA YA MOSHI VIJIJINI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza wakati wa kuzindua rasmi mradi wa daraja uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa ,Tanzania (TANAPA) kwa ajili ya wakazi wa vijiji vya Singa na Sungu wilaya ya Moshi.
Daraja linalotenganisha vijiji vya Singa na Sungu wilaya ya Moshi vijijini ambalo kwa sasa limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kufika kwa urahisi katika hosptali ya Kibosho.  


Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Erastus Rufunguro akizungumza katika makabidhiano hayo.   



KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


          

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE AKIFUNGUA KONGAMANO LA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA LEO JIJINI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  akifungua kongamano la  Wiki ya Utumishi wa Umma lililofanyika leo  kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue  (kushoto) akipeana mkono leo  na   Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu  Balozi Dkt. Matern Lumbanga(katikati)   mara  baada   kufungua kongamano la  Wiki ya Utumishi wa Umma lililofanyika  leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna  wa Tume ya Utumishi wa Umma. George Yambesi.

ZANZIBAR YADHIMISHA SIKU YA KUPAMBANA NA USAFIRISHAJI NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA DUNIANI

$
0
0
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji amesema dawa za kulevya ni janga  la Kidunia linalopigwa vita  na Mataifa yote Duniani.

Hayo ameyaeleza huko Kiwanja cha Kombawapya Zanzibar katika Maaadhimisho ya kupiga vita  Utumiaji na Usafirishaji pamoja na  Udhalililshaji wa Dawa za kulevya Duniani.

Amesema Zanzibar inakadiriwa kuwa na watumiaji wa dawa za kulevya zaidi ya 9000 idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na visiwa hivyo pamoja na idadi ya wakaazi wake jambo ambalo linahatarisha maisha ya vijana kujiingiza zaidi katika utumiaji huo
Aidha amesema Seikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za kulevya chini ya Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais huadhimisha siku hiyo kila Mwaka kwa lengo la kuitanabahisha Jamii kuwa Dawa  hizo ni janga la Kitaifa lisilovumilika hivyo linahitaji nguvu na maarifa ili kupambana na janga hilo.

 Hata hivyo Waziri huyo amesema kuwa  Zanzibar ni sehemu ya Dunia inayounga mkono juhudi za Mataifa na Jumuiya mbalimbali za Kimataifa katika kupiga vita Dawa hizo ambazo kwa asilimia kubwa zinaathiri nguvu kazi ya Taifa lolote Duniani hasa vijana wenye umri mdogo wakiwemo Wanafunzi.
Waandamanaji katika maadhimisho ya siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani wakipita mbele ya mgeni rasmi katika kiwanja cha Kombawapya. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
 Rais wa watoto Tanzania  Ameir Haji Khamis akitoa ujumbe wa watoto na dawa za kulevya kwenye sherehe za siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani katika kiwana cha Kombawapya.
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej akitoa nasaha katika  maadhimisho ya siku ya kupambana na usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya Duniani katika kiwanja Kombawapya Mjini Zanzibar.

TANGAZO LA JKT: NYONGEZA YA MAJINA YA VIJANA 20,000 NA KAMBI WALIZOPANGIWA.

$
0
0
MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA ANA WATANGAZIA VIJANA IDADI 20000 WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2015 KUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA. WANATAKIWA KURIPOTI KWENYE VIKOSI VYA MAFUNZO WALIVYOPANGIWA KUANZIA TAREHE 08 JUNI 2015. MAFUNZO YATAANZA RASMI TAREHE 15 JUNI 2015 NA KUMALIZIKA TAREHE 15 SEPTEMBA 2015.

YAFUATAYO YAZINGATIWE
  1. VIJANA WANAOTAKIWA KUJIUNGA WAWE RAIA WA TANZANIA
  2. WARIPOTI WAKIWA NA VYETI HALISI VYA KUZALIWA NA KUMALIZA KIDATO CHA SITA (LEAVING CERTIFICATE).
  3. VIJANA WENYE ULEMAVU UNAOONEKANA WARIPOTI KWENYE KIKOSI CHA RUVU.
  4. WALE WENYE MATATIZO AMBAYO YATAPELEKEA KUTOKUHUDHURIA MAFUNZO YA JKT KWA SASA WAANDIKE BARUA YA MAOMBI YA KUAHIRISHA MAFUNZO KWA MKUU WA JKT WAKIAMBATISHA VIELELEZO VYA TATIZO ALILONALO. MWAWASILIANO YOTE YAFANYIKE KUTUMIA ANUANI IFUATAYO.

MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA
MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA
S.L.P 1694
DAR ES SALAAM.

MAJINA YA VIJANA NA KAMBI WALIZOPANGIWA

CCM KUMEKUCHA JAJI RAMADHARA AVURUGA MWELEKEO WA WAGOMBEA

$
0
0

CV YA JUDGE RAMADHANI
 Nimezaliwa Desemba 28, mwaka 1945 Zanzibar mjini nikiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanane, wa kike wanne na wanaume wanne. Ni Mkristo wa dhehebu la Anglikana. 

Nimesoma shule mbalimbali za msingi Mpwapwa mkoani Dodoma 1952 -1953 nikaenda Town School-Tabora nikasoma darasa la tatu hadi la nne mwaka 1954-1956 na darasa la sita na saba nilisoma Kazel Hill sasa inatwa Shule ya Msingi Itetemia mwaka 1957-1958. Na darasa la nane tu mwaka 1959 nikarudi kusoma Mpwawa.

Mwaka 1960-1965 nilijiunga na Tabora School kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwakuwa nilifaulu nilichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1966, na nilisoma shahada yangu ya Sheria na ilipofika Machi 1970 nilihitimu masomo.

Na mwishoni mwa Machi mwaka huo huo wa 1970 nikajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), niliingia jeshini kama mwanasheria raia mpaka kipindi cha mafunzo ya kijeshi nikaenda kwenye mafunzo na kisha nikarudi kuitumikia JWTZ.

Ilipofika mwaka 1971 nikapewa kamisheni kambi ya Mgulani nikawa Luteni (nyota mbili). Nikaendelea na jeshi hadi mwaka 1977, nikahamishiwa Brigedi ya Faru-Tabora nikiwa na cheo cha Meja.

Sasa mwaka 1978, wewe mwandishi ulikuwa hujazaliwa, ndiyo mzee Aboud Jumbe Mwinyi, wakati huo akiwa ni rais akaniita Zanzibar na kuniteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar na kipindi hicho Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva.

Aidha Oktoba 1978 niliteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar. Na ilipofika Machi 1979 nilirudishwa JWTZ na baada ya muda mfupi nikapelekwa kwenye vita ya Uganda , nikiwa na cheo cha Luteni Kanali na kwenye vita hiyo nilikuwa naendesha mahakama za kijeshi.

Vita ilipokwisha nikarudi Zanzibar. Januari 8 mwaka 1980 nikaapishwa kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati huo nikiwa na cheo cha Luteni Kanali. Nikaendelea na Ujaji Mkuu Zanzibar hadi Septemba 1989 alipoapishwa Jaji Mkuu Zanzibar Hamid Mahamod Hamid.

Hata hivyo Juni 23 mwaka 1989 niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania hadi mapema wiki hii nilivyoteuliwa kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Nilipoteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani hapa Bara ndiyo sababu ya kuacha ujaji Mkuu Zanzibar.
Januari 1993 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na niliendelea na nafasi hiyo hadi Januari 2003 na Oktoba 2002 niliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ambapo kipindi changu cha miaka mitano katika tume ZEC kinamalizika Oktoba mwaka huu.

Novemba 2001, niliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki nafasi ambayo natakiwa nimalize kipindi changu cha miaka sita Novemba mwaka huu.

Nina mke mmoja ambaye Mungu ametujalia tumebahatika kupata watoto wanne, wawili ni wasichana na wawili ni wavulana.

Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Francis (30) huyu ni mwanasheria na anafanyakazi ya uwakili Manchester, Uingereza, Brigeth, huyu ana shahada ya Uandishi wa Habari na anafanyakazi ICAP hapa nchini, Marina ni mfamasia, yuko Liverpool, Uingereza na Mathew naye ni mfamasia, anafanya kazi Liverpool.”

MKURUGENZI WA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA MAMBO YA NJE AAGANA NA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA UNDP NCHINI

$
0
0
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akimkabidhi Kitabu kinachoelezea Vivutio mbalimbali vya Utalii vilivyopo nchini Mkurugenzi wa UNDP nchini, Bw. Philippe Poinsot, alipokuja kuaga mara baada ya kupata uhamisho wa kwenda kuwa Mratibu Mkazi wa UNDP nchini Moroco.
Balozi Mushy akiwa katika mazungumzo na Bw. Philippe Poinsot mara baada ya kumkabidhi kitabu.
Balozi Mushy (wa nne kulia)  akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Poinsot (wa nne kushoto) pamoja na Maafisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa.
Picha na Reginald Philip.

YANGA KUIVAA SC VILLA JUNI 27

$
0
0

Na Mwandishi wetu.
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Yanga, Juni 27, mwaka huu wanatarajia kuvaana na SC Villa ya Uganda katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kukusanya fedha za kujengea kituo cha watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na walemavu wa ngozi, yaani albino.

Akizungumza Dar es Salaam jana katika ukumbi wa makao makuu ya Yanga yaliyopo Jangwani, jijini, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Jonas Tiboroha, alisema kuwa katika mchezo huo watachezesha kikosi chao kamili, kikiwajumuisha wachezaji wapya na nyota wa zamani.

Alisema wameamua kushiriki katika tamasha hilo kama sehemu ya kuonyesha jinsi wanavyoguswa na jamii, ikiwa ni baada ya kuombwa kufanya hivyo na Taasisi ya Nyumbani Kwanza Media kwani hata klabu kubwa Ulaya zimekuwa zikiafnya hivyo.

“Baada ya kuletewa wazo hili na wenzetu wa Nyumbani Kwanza, tulikubaliana nao kwani ni zuri. Tumeona klabu ya Yanga isipate isipate sifa kwa kutwaa ubingwa tu, bali pia hata kufanya shughuli za kijamii kama hizi. Uongozi umebariki na hata Kocha Mkuu na benchi lote la ufundi lina taarifa na ndio maana tumeanza mazoezi mapema zaidi,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Nyumbani Kwanza Media, Mossy Magere, alisema kuwa wazo la kuandaa tamasha hilo lilikuja baada ya kutafakari ni vipi wanaweza kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu na wakaona ni vema kuishirikisha Yanga wakiwa kama mabingwa wa Tanzania Bara.

“Mapato yatakayopatikana yatafanya shughuli kusudiwa kwa kuanza rasmi ujenzi wa kituo huko Bagamoyo, mkoani Pwani na tutakuwa tukifahamishana kila hatua ya mradi huo utakaogharimu Sh bilioni 1.5 ambao tumepania uwe mfano wa kuigwa na wengine,” alisema Mossy.

Aliwapongeza Yanga kwanza kwa kutwaa ubingwa wa Bara, lakini pia kukubali kushirikiana nao katika kufanikisha tamasha hilo la aina yake.
Awali mechi hiyo ilikuwa ichezwe kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, lakini kutokana na ushauri wa Tiboroha, waliamua iwe Dar es Salaam ili kupunguza gharama za maandalizi yake, hasa katika suala zima la usafiri kwa timu na mengineyo.

MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR

$
0
0
 
Afisa wa wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi , Udhamini na Ufilisi  RITA,Joseph Mwakatobe  akizungumza na Michuzi TV juu ya huduma wanazozitoa katika huduma  ya Wosia katika kuondoa migogoro ya miradhi  wakiwa katika maonyesho Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Wakili wa Serikali,Msajili wa Mkuu wa Talaka wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi , Udhamini na Ufilisi (RITA),Edna Msuya akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika katika maonyesho ya  Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Msaidizi wa Ofisi ya  Kitengo cha Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu,Lylian Mmari akitoa maelezo kwa mteja alipotembelea banda la ofisi ya Waziri Mkuu  katika maadhimisho ya  Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.  
 Watumishi wa ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja katika banda la Waziri Mkuu katika maadhimisho ya  Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Kiongozi Mkuu na Mratibu wa Sayansi na Maendeleo ya Milleniam Vijijini katika kuondoa Umasikini ,Dk.Gerson Nyadzi akizungumza na Michuzi TV katika Banda la Wizara ya Fedha  juu ya wananchi walivyoweza kunufaika na miradi mbalimbali  katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa Wizara ya Fedha akitoa maelekezo kwa mteja aliopotembelea banda la Wizara ya fedha katika maaonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhasibu wa Wizara ya Fedha Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali ,Kitengo cha Pensheni,Emelda Mzatulla akizungumza na Michuzi TV juu ya huduma wanazozitoa katika kitengo cha pensheni katika Wiki ya Utumishi inayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA WATOTO TANZANIA(TAJOC)


MFANYAKAZI WA GLOBAL, ROBERT TILLYA, AZIKWA KILIMANJARO LEO

$
0
0
Wafanyakazi wa Global Publishers wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Robert Tillya wakati wa maziko Uru-Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Watoto wa marehemu, Getruda na Niveti wakiweka shada la maua.
Mwili wa marehemu Robert Tillya ukishushwa kaburini.
Ndugu, jamaa na wafanyakazi wa Global wakifukia kaburi.
Mke wa marehemu, Daya, akisaidiwa baada ya mazishi.
Baba wa marehemu, Ridoch Tillya (kushoto) akiwa na mtoto wa marehemu, Niveti. Kulia ni baba mkubwa wa marehemu Mzee Tillya akiwa na mtoto mkubwa wa marehemu.
(PICHA: RICHAR BUKOS/GPL)

LOWASSA APATA UDHAMINI WA KISHINDO MKOANI TANGA, WANACCM 24,125 WAMDHAMINI

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkomo maelfu ya wanaCCM na wananchi wa Mkoa wa Tanga, waliojitokeza kwa wingi kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Tanga leo Juni 17, 2015. zaidi ya WanaCCM 204,125 wamemdhamini Mh. Lowassa, ili aweze kuteuliwa na CCM kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akitoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Tanga, walijitokeza kwa wingi kwenye Ofisi za Chama Cha Mapinduzi, Mkoa wa Tanga leo Juni 17, 2015, ambapo zaidi ya WanaCCM 24,125 wamemdhamini Mh. Lowassa, ili aweze kuteuliwa na CCM kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu yenye majina ya WanaCCM waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na CCM kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.anaekabidhi fomu hiyo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Tanga Mjini, Lucia Mwiru.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za ziada yenye majina ya WanaCCM waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na CCM kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. anaekabidhi fomu hizo ni Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tanga, Mathew Mganga akikabidhi. 

TAA na CCTV camera za barabarani Zanzibar

$
0
0
Zanzibar yapiga hatua ,mafundi wakifunga Taa za barabarani pamoja na cctv camera katika eneo la mataa ya kuelekea darajani,unguja.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Norway nchini

$
0
0
Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberatta Mulamula (Kulia)  akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Hanne Maria Kaarstad. Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Norway.
Balozi Kaarstad akimweleza jambo Katibu Mkuu, Balozi Mulamula
Mazungumzo yakiendelea huku Bi. Tunsume Mwangolombe (kulia), Afisa Mambo ya Nje akisikiliza kwa makini.
Picha na Reginald Philip.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI, LONDON

Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images