Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 875 | 876 | (Page 877) | 878 | 879 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini India na familia zao jana muda mfupi baada ya kuzungumza nao katika hoteli ya Taj Mahal Palace jijini New Delhi India ambapo yuko kwa ziara ya kiserikali.Walioketi mbele kutoka kushoto ni baadhi ya mawaziri anaofuatana nao katika ziara hii.Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa mambo ya Nje Mahadhi Juma Maalim, watatu kushoto ni Waziri wa Maji Prof.Jumanne Maghembe,watatu kulia ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Zanzibar Haji Omar Kheri,Wanne kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr.Abdallah Kigoda, na wapili kulia ni Mbunge wa Nzega Said Nkumba.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara wa India wenye viwanda ambao wamewekeza nchini Tanzania muda mfupi baada ya kukutana nao leo. Picha na Freddy Maro

  0 0

  Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Dkt. Augustino Mahiga (kulia), akizungumza na wadhamini kushoto ni katibu wilaya na kulia aliyekuwa Katibu wa Bunge Geroge Mlawa (MSTAAFU)
  Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Dkt. Augustino Mahiga (kushoto), akipokea fomu ya wadhamini kutoka kwa Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni, Athumani Shesha, Dar es Salaam juzi, alipokwenda kuomba wadhani katika wilaya hiyo. 

  0 0


  0 0

  The Chairman of the India Tanzania Business Forum Mr.Gagan Gupta hands over a special award to President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in recognition for his efforts in promoting healthy business relations and working environment for Indian investments in Tanzania at TAJ Palace Hotel in New Delhi India.On the left is India's Minister for Agriculture Mr.Mohanbai Kalyanjibhai Kundariya. Photo by Freddy Maro

  0 0


  0 0

    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali zilizohifadhiwa kumbukumbu za aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemo Indra Gandhi wakati wa uhai wake. Marehemu Idra Gandhi aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 31.10.1984 akiwa kwenye viwanja vya nyumba hiyo ambayo alikuwa akiishi.
    Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea sehemu mbalimbali zilizohifadhiwa kumbukumbu za aliyekuwa Waziri Mkuu wa India Marehemo Indra Gandhi wakati wa uhai wake. Marehemu Idra Gandhi aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 31.10.1984 akiwa kwenye viwanja vya nyumba hiyo ambayo alikuwa akiishi.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya Marehemu Indra Gandhi wakati alipotembelea makumbusho ya waziri mkuu huyo huko New De;lhi nchini India tarehe 18.6.2015
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  akipewa taarifa mbalimbali na Bwana  Rajan Madan, Mkurugenzi wa Uzalishaji  katika Kiwanda cha New Holland Fiat Limited kuhusiana na utengenezaji wa matrekta kwenye Kiwanda hicho  huko New Delhi. Mama Salma Kikwete aliambatana na Rais Kikwete kuzuru kiwandani hapo ili kujionea utengenezaji wa matrekta.
   PICHA NA JOHN LUKUWI. 

  0 0

   Mkurugenzi wa Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Stephen Kilindo (kulia), akikabidhi mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Kimarekani kwa Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga na wafugaji wa mbuzi wa maziwa katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Fedha hizo zimetolewa na Kampuni SABMiller tanzu ya TBL.
   Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu (kulia), akifafanua jambo kuhusu msaada uliotolewa na Kampuni hiyo kwa ACE Afrika kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Mwanza. Wengine ni Meneja wa Fedha na Utawala wa ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita (kushoto) na Mkurugenzi wa Sheria TBL, Stephen Kilindo.
   Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea mfano wa hundi ya Dola 24,000  za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga katika mikoa ya Arusha,

  Meneja wa Fedha na Utawala wa Taasisi ya ACE Afrika, Bw. Oswald Mwita, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kupokea mfano wa hundi ya Dola 24,000 za Marekani zilizotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya kuongeza tija kwa wakulima wa mbogamboga katika mikoa ya Arusha, 

  0 0


  0 0


  Katibu wa ccm wilaya ya Kigoma Novati Kibadi akimkabithi form Dkt. Migiro zenye majina 45 alizodhaminiwa na wakazi wa kigoma

  Baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kumdhamini Dkt. Migiro wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa ccm mkoa wa Kigoma wakimsikiliza mgeni wao
  Mhe Migiro akishukuru baada ya kukabithiwa fomu za wadhamini. Chini akishiriki kuimba na meza kuu baada ya kukabidhiwa fomu za wadhamini
  Mhe. Migiro akiongea na wana habari baada ya zoezi la kukabidhiwa majina ya wadhamini katika ofisi za CCM mkoa wa Kigoma. 
  Picha na Edita Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma

  0 0


  0 0

  IMG_2921
  Waandishi wa habari kutoka Tanzania waliosafirishwa na Shirika la ndege lenye gharama nafuu nchini Fastjet kuhudhuria maonyesho ya Kimataifa ya Utalii ya Shanganai yanayoendelea nchini Zimbabwe. Kutoka kushoto ni Timothy Kitundu (East Africa Business Week), Mariam Said (Daily News) pamoja na Justin Damiana (The African) wakiwa wameketi kwenye mapango ya Chinhoyi huku wakibadilishana mawazo na wadau wa utalii kutoka Afrika Kusini.
  IMG_3430
  Kutoka kushoto ni Victoria Siphiwe Mamvura Gava, Cherry Sibanda na Mariam Said wakiwa wamepumzika huku wakipitia baadhi ya vipeperusha vya boti za kitalii zinazokodishwa kwa ajili ya kupumzika katika ziwa la Kariba.
  IMG_3465
  Kundi jingine likiwa kwenye ziara ya ziwa Kariba likiongozwa na Rumbidzai Mudzengerere wa Mamlaka ya Utalii ya Zimbabwe (ZTA).
  IMG_3497
  Kituo cha mafuta katika Bandari ya Marine Land kikiwa ndani ya Ziwa Kariba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0

  Na Mwandishi wetu,Globu ya Jamii
  KUONGEZEKA kwa ndoa za utotoni inatokana na sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kuendelea kutumika wakati hali yake ni mbaya kwa watoto wakike kushindwa kufikia ndoto zao.
  Akizungumza na katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Regency ,Mratibu wa Utetezi Taifa ,SOS Tanzania/Zanzibar ,John Batista amesema  kuongezeka kwa mimba za utotoni inatokana na sheria ya ndoa kuendelea kutumika.
  Amesema kuwa kuendelea kwa mimba za utotoni pamoja kuolewa kunatokana sheria kutamka kuwa mtoto anaweza kuolewa kwa miaka 14 kwa ridhaa ya wazazi.
  Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya Watu (UNFPA) inaonyesha watoto 1,3822 ambao wamezaliwa katika mwaka 2005  na 2010 ifikapo 2030 watakuwa wameolewa chini ya miaka 18.
  Katika ripoti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaonyesha wasichana 8000 wanapata ujauzito wakiwemo wanafunzi wa Shule ya msingi 3000 na ,sekondari 5000.
  Mratibu wa C-SEMA,Michael Kihongoh amesema kampeni hii ni endelevu na waandishi wametakiwa kuweka kipaumbele kupigania sheria ya ndoa ya mtoto kuondolewa kabisa ili watoto wa wakike waweze kulindwa.
  Amesema kuwa watoto wa kike wako katika hatari ambapo elimu inatakiwa kutolewa kwa jamii ikiwemo malezi kwa waoto wa kike wasiweze kuingia katika vishawishi.
  Mratibu wa Utetezi Taifa, SOS Tanzania/Zanzibar, John Batista, akizungumza katika Mdahalo wa Nijali uliolenga ndoa za utotoni na mimba za utotoni  kwa kushirikisha Chama cha Waandishi wa Habari za Watoto, (TAJOC) na wengine, uliofanyika leo katika Hoteli Regency jijini Dar es Salaam.
   Mshauri Mkuu Mwandamizi na Msimamizi wa Huduma ya Simu kwa Mtoto wa C-SEMA, Fatuma Ahmad akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.
   Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Watoto (TAJOC), Chalila Kibuda akizungumza na waandishi wa habari katika mdahalo wa Nijali uliofanyika katika leo Hoteli ya Regency Jijini Dar es Salaam.

  Washiriki wa Mdahalo wa Nijali  ulioshirikisha Chama cha Waaandishi wa habari za Watoto (TAJOC) na wadau wengine uliofanyika leo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mwenyekiti  wa  Chama cha Wajane Tanzania, Rose Sarwatt akizungumza na waandishi  wa habari hawapo pichani  juu maazimisho siku ya wajane Duniani itakayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jeshini jijini Dar es Salaam Juni 23 mwaka huu. Maadhimisho hayo yatalenga  kusaidia wajane kisheria, kupata elimu pale wanapo kwama  kushawishi  jamii kuandaa wosia ili kupunguza  au kuondoa usumbusu. Kulia ni  Katibu Chama cha Wajane Tanzania John Shabani  mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa idala ya Habari MAELEZO leo Jiji Dar es Salaam.
   Katibu Chama cha Wajane Tanzania John Shabani  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu  kutoa fursa ya kuzungumzia matatizo yanayowakumba wajane hasa wanawake na watoto wao ili kurejesha haki zao na kupambana na umaskini kwa kuwezeshwa.Kushoto ni
  Mwenyekiti  wa  Chama cha Wajane Tanzania, Rose Sarwatt.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika kikao mkutano wa chama cha wajanae hapa nchini mkutano ulifanyika katika ukumbi wa idala ya Habari MAELEZO leo Jiji Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.)

  0 0

  Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, wakiwa wamemzunguka, Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa (katikati), wakati alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya leo Juni 19, 2015, kukabidhiwa fomu zitakazomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mbeya wamevunja rekodi udhamini kwa Mh. Lowassa ya mikoa yote aliyopita, amepata wadhamini 53,156 kwa mkoa wa Mbeya pekee.
  PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya, waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, wakati alipowasili kwenye Ofisi hizo leo Juni 19, 2015, tayari kwa kupokea fomu za WanaCCM 53,156 wanaliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM na Wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya, leo Juni 19, 2015.

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu tisa wa Wilaya ya Mbeya Vijijini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Mary Kalinze.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   January Makama akiweka saini kitabu cha wageni alipotua  mkoani Tabora kusaka wadhamini. Kulia ni mkewe na kushoto ni mmoja wa viongozi wa CCM mkoani humo
   January akilakiwa na wazee wa Tabora 
   Mke wa January akimpigia debe mumewe mjini Tabora
   January akihutubia wananchi wa mkoa wa Tanga na kutoa shukrani kwa wananchi wa Tanga kwa kujitokeza kwa wingi kumdhamini na kumsikiliza  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Suleiman Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari katika banda la mamlaka hiyo kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yanayoendelea viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAA pamoja na miradi yao.
   Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa TAA, Laurent Mwigune (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu shughuli zinazofanywa na TAA.
   Kamanda Msaidizi wa Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Kamishna Msaidizi, Mpemba Magogo (katikati), akizungumza na waandishi habari kuhusu kazi za uokoaji pale unapotokea moto. Kulia ni Koplo, Brian John wa Kikosi hicho cha Zimamoto.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberatta Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi wa IFAD nchini Bw. Sana F.K. Jatta, alipokuja kumtembelea na kujadili juu ya ziara ya  Rais wa IFAD Mhe. Kanayo Nwanze mwezi Agosti 2015
  Mmoja wa wajumbe aliyeambatana na Bw. Jatta akifafanua jambo kwa Balozi Mulamula.
  Mazungumzo yakiendelea

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiweka shada katika kaburi la mpigania uhuru na muasisi wa taifa la India Mahatma Ghandi jijini New Delhi India leo asubuhi


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya leo, Ijumaa, Juni 19, 2015.


   Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika ikulu ya India kwa mapokezi rasmi
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Narendra Modi katika sherehe za kumkaribisha nchini India kwa ziara rasmi ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika Ikulu ya India mjini New Delhi, asubuhi ya leo
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Majeshi ya India liliandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika asubuhi ya leo.
  Picha na Freddy Maro

  0 0

   .Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya kushoto Akishirikiana na Mkurugenzi Mkuu wa World Lung Foundation(wa pili kushoto)Dr Nguke Mwakatundu kukata utepe wakati wa Uzinduzi wa Nyumba za Watumishi wa Afya katika kituo cha Afya Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
   Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya  akikata utepe Ikiwa ni Ishara ya ufunguzi wa Nyumba zilizo jengwa kwa hisani ya WLF kwa ajili ya watumishi wa Afya katika kituo cha Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma.
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya akikagua moja ya Nyumba za Watumishi wa Afya zilojengwa kwa hisani ya WLF Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma  Kanali Mstaafu Issa Machibya(wa tatu kushoto)akifatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WLF Dr Nguke Mwakatundu katika picha ya pamoja na Baadhi ya wataalamu wa Afya Wilayani Uvinza Mkoani.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda akionesha sehemu ya vifaa vya michezo atavyogawa kesho Jumamosi kwa timu zitazojitokeza Leaders Club jijini Dar es salaam kushiriki ligi ya Kinondoni atayoizindua kukuza vipaji.
  MH: PAUL MAKONDA MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, anawaomba Wanakinondoni wote na wakazi wa DSM katika kuandaa maandalizi ya Team za Wilaya ya Kinondoni zitakazo kuwa na wachezaji watakao lipwa mshahara; katika:

  1.Mpira wa miguu
  (Football).
  2.Netball.
  3.Basketball.

  Kushirikiana nae katika uzinduzi wa ligi hizo kesho jumamosi, saa moja asubuhi Viwanja vya Leaders. Ambapo  atazikabidhi Team 138 vifaa vya michezo. SET 2  ZA JEZZY NA MIPIRA 2 KWA KILA TEAM.

  WATAKUWAPO WATAALAMU WAKUPIMA AFYA ZA WACHEZAJI NA WATU WENGINE, KUTAKUWA PIA NA ZOEZI LA KUCHANGIA DAMU KWA ATAKAE PENDA. TEAM ZOTE ZIKISHACHEZA KWA PAMOJA BAADAE WASHINDI  WATAUNDA  TEAM ZA WILAYA....

  KWA MAELEZO ZAIDI FIKA VIWANJA VYA LEADERS MAPEMA KESHO(JMOS TAR 20 JUNE/2015) . KIPAJI CHAKO AJIRA YAKO....AJIRA SI BOMU.BOMU NI KUTOTUMIA KIPAJI CHAKO. SERIKALI HAZIWEZI KUAJIRI WATU WOTE KATIKA AJIRA ZA OFISINI.

  AJIRA INAJUMUISHA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI.NJOONI TUJIAJIRI TUPUNGUZE UGUMU WA MAISHA.

  INAWEZEKANA...TUTIMIZE WAJIBU


older | 1 | .... | 875 | 876 | (Page 877) | 878 | 879 | .... | 3272 | newer