Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 867 | 868 | (Page 869) | 870 | 871 | .... | 3348 | newer

  0 0

  WAANDAAJI wa Tamasha la Pasaka wamesema kuwa DVD ya onesho la Miaka 15 ya tamasha hilo lililofanyika Aprili mwaka huu ipo mtaani.
   
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa DVD imeonesha shughuli nzima ya tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mgeni rasmi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
   
  “Nawaomba mashabiki wa muziki wa Injili ambao walikuwa wakiniulizia kuhusiana na DVD hiyo kwamba sasa ipo mtaani na ni jukumu lao kuitafuta katika maduka yetu.
   
  “Wale waliohudhuria tamasha hilo na wale ambao hawakuhudhuria wote watambue kuwa sasa wanaweza kuona tamasha hilo wakiwa sebuleni kwao,” alisema Msama.
   
  Alisema tamasha la mwaka huu lilikuwa tofauti na matamasha mengine yaliyopita kwani liliendana na sherehe za miaka 15 tangu waanze tamasha hilo.
   
  Alisema DVD hiyo inaonesha waimbaji wote mahiri waliohudhuria na kwamba ana matumaini makubwa mashabiki watakuwa na kumbukumbu kubwa ya shughuli hiyo.Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje walishiriki tamasha la mwaka huu akiwemo Mwingereza, Ayobami David na Rebecca Maloppe wa Afrika Kusini.
   
  Mwaka huu Tamasha la Pasaka lilitimiza miaka 15 tangu kuasisiwa kwake na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, ambapo limekuwa likijiongezea umaarufu na kukubalika zaidi kutokana na ubunifu wake wa kufanya maadhimisho ya Sikukuu za Pasaka na Krismasi kwa umahiri na mguso wa kiroho kupitia matamasha hayo.

  0 0

  Bendi ya African Stars maarufu kama Twanga Pepeta Ijumaa Juni 12 itafanya onyesho maalum la kumtambulisha mwanamuziki maarufu nchini Ali Choki na wengine waliorejea kwenye bendi hiyo.

  Onyesho hilo litafanyika usiku katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
  Mratibu wa onyesho hilo Joseph Kapinga wa Keen Arts na Bob Entertainment amesema kuwa onyesho hilo pia litakuwa ni la vunja jungu kabla ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Kapinga alisema pia Choki atatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zake mpya ambazo ni “Kichwa Chini” na “No Discussion”.

  Wanamuziki wengine ambao watatambulishwa pamoja na Choki ni mnenguaji wa bendi hiyo Super Nyamwela na mpiga kinanda Victor Mkambi. Choki na Nyamwela wametokea kwenye bendi ya  Extra Bongo wakati Victor Mkamba ametokea bendi ya Ruvu Stars.

  Kwa upande wake Ali Choki alisema kwenye onyesho hilo litakuwa ya aina yake kwani atapiga nyimbo zote alizizowahi kupiga akiwa na Twanga Pepeta kabla hajahamia bendi ya Extra Bongo.
  Baadhi ya nyimbo hizo ni “Kisa Cha Mpemba,” “Fainali Uzeeni,”  “Umbea Hauna Posho,” “Jirani,” “Password,” “Kuolewa,” “Busu la 2005,” “Busu la Kufunga Mwaka,”  “Aminata” na zinginezo.

  Naye Mkurugenzi wa bendi hiyo Asha Baraka amesema onyesho ya leo litakuwa ni kama zawadi kwa wakazi wa Tabata na vitongoji vyake, kwani itakuwa onyesho la mwisho la bendi hiyo kabla mfungo wa Ramadhani.

  0 0
 • 06/11/15--06:37: STARS KUWAFUATA MISRI KESHO
 • Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, kesho siku ya ijumaa jioni inatarajiwa kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku ya jumapili.

  Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na raiba yake ya mazoezi katika uwanja wa Taifa, amabpo leo imefanya mazoezi yake asububuhi tu.

  Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na  uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.

  Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.Aidha kocha Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.
  Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mapharao.


  Taifa Stars inatarajia kuondoka kesho jioni ijumaa kuelekea nchini Misri kwa shirika la ndege la Ethiopia majira ya saa 5 usiku na kufika Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha safari ya kuelekea jijini Alexandria ambapo timu mchezo huo utakapofanyika.

  Mchezo kati ya Misri dhidi ya Tanzania utachezwa katika uwanja wa Borg El Arab kuanzia majira ya saa 1 jioni kwa saaa za huku, sawa na saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
  Waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchini Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa (mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma (mwamuzi msaidizi wa kwanza), na Wolday Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili).


  0 0  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nne wa Umoja wa Kinamama wa Kikristo (UMAKI) wa Kanisa Angikana Dayosisi ya Zanzibar mjini Unguja jana. Kulia kwake ni Askofu Mkuu mstaafu wa Kanisa Anglikana.

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kulia), akipata maelezo kuhusu bidhaa za ujasiriamali za kikundi cha Umoja wa Kinamama wa Kikristo (UMAKI) wa Kanisa Angikana Dayosisi ya Zanzibar, kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa Nne wa UMAKI mjini Unguja jana. Picha zote na John Badi.

  0 0

   Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya kuhamasisha vijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na hatimaye kupiga kura ilijulikanayo kama 'Kuradili". Kampuni hiyo itafanya kampeni hiyo katika mikoa kadhaa kwa kushiriakiana na  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki. Kulia ni mwanamuziki Sinura Mushi na kushoto ni Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo. 
    Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Conctantine Magavila (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mwanamuziki Stamina, Kala Jeremia, Snura, Ofisa Elimu Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Rose Malo na Ofisa Mipango Msaidizi wa Shirika la Open Society International East Africa (OSIEA), Adam Anthony.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Profesa Mark Mwandosya, Bungeni Mjini Dodoma Juni 11, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, bungeni mjini Dodoma Juni 11, 2015.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Dr. Mary Nagu akiwasilisha taarifa ya hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2014 na Mwelekeo wa mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2015/2016 bungeni mjni Dodoma Juni 11, 2015.


  0 0

  Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bibi Felista Tirutangwa (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri yaliyofanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam. 
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (aliyesimama) akizungumza wakati wa Mafunzo ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria Juu ya Ripoti ya Ukaguzi ya CAG na Jinsi ya Kuitafsiri yaliyofanyika katika Hoteli ya Den France, Dar es Salaam.
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (aliyesimama) akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Taasisi Wadau wa Usimamizi wa Sheria na Ofisi yake katika kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za nchi. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Bibi Felista Tirutangwa na Mchambuzi wa Masuala ya Fedha kutoka Ofisi ya Rais, Bw. Stephene Likunga (Kulia).


  0 0

  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema watu 152 watafikishwa mahakamani mkoani Njombe kutokana na kujiandikisha mara mbili katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa mfumo mpya wa ‘Biometric Voter Registration Kit’ (BVR).

  Aidha, imeeleza kuwa kata 130 zimeongezeka kutokana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kufanya mabadiliko ya kiutawala katika kata, vijiji,vitongoji na Mitaa hivyo kulazimu NEC kuhairisha kwa wiki moja uandikishaji wa daftari uliokuwa ukianza jana kwa baadhi ya mikoa.

  Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk Sisti Cariah alisema hayo jana wakati akielezea kuahirishwa kwa wiki moja uandikishaji hadi Juni 16 mwaka huu kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Mara.

  Akizungumzia suala la watu kujiandikisha mara mbili, alisema katika mkoa wa Njombe ambao Daftari hilo liko tayari na wiki ijayo litawekwa wazi kwa siku tano na kisha kufanyiwa marekebisho kwa siku moja na wamebaini watu 152 waliojiandikisha mara mbili.


  0 0

  Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mtoto mwenye ualbino, Kabula Zacharia, anayetunzwa kwenye kituo cha kulea watu wenye mahitaji maalum cha Buhangija mkoani Shinyanga, mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini kufuatia kuchukua fomu za kuomba chama kimteue kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa ambaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupata wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa. (Picha na K-VIS MEDIA)
  Mh. Lowassa, akipokea fomu zilizojazwa na wana CCM waliomdhamini mkoani Shinyanga, kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Shin yanga mjini Charles Sangula, Juni 11, 2015.
  Waziri Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akipungia mkono wana CCM na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, alipokuwa akiondoka ofisi za chama hicho wilaya ya Shinyanga mjini mara baada ya kupata wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu kuomba CCM imteue kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amabaye yuko kanda ya ziwa kutafuta wadhamini, alivunja rekodi ya kupatya wadhamini 7,114, idadi kubwa hadi sasa. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM,Mh. January Makamba akiagana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Bi Jesca Mambatavangu mara baada ya January kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama.
  Mh. January Makamba akikabidhiwa fomu yenye majina ya wanachama waliomdamini na Mwenyekiti wa CCM wilya, Abeid Kiponza. Fomu hiyo in idadi ywa wanachama 630 waliojitokeza kumdhamini ikiwa ni kutoka wilaya ya Iringa Mjini na Kilolo.
  Mh. January Makamba akihutubia wananchi na wanachama wa CCM wilaya ya Iringa Mjini walijitokeza kumsapoti na kumdhamini. January amepata sahihi 630 za wanachama wa CCM kumdhamini, idadi hiyo ni ya wilaya ya Iringa Mjini na wilaya ya Kilolo. 

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   Sehemu ya Watanzania lukuki waishio Uholanzi waliojitokeza kumuona na kumaga Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa hoteli ya Crowne Plaza jijini The Hague wakiwa na furaha kwa kupata fursa hiyo adimu
   Rais Kikwete akisalimiana na Watanzania lukuki waishio Uholanzi waliojitokeza kumuona na kumaga JK katika ukumbi wa hoteli ya Crowne Plaza jijini The Hague 
   Wakubwa kwa wadogo walikuwepo

   Hongera sana mkuu...
  Tutakumiss sana mhishimiwa....

  0 0

  NYIMBO ZA KUMUAGA RAIS JAKAYA KIKWETE HEWANI ! SI WENGINE NI NGOMA AFRICA BAND AKA FFU -Ughaibuni yenye maskani kule ujerumani 
   Mtunzi:Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja 
  Waimbaji: Kamanda Ras Makunja Afande Chris-B ambaye pia ni mpiga solo gitaa Bendi: 
  Ngoma Africa band aka FFU wasiliana nao at ngoma4U@gmail.com

  0 0


  0 0

  Kampuni ya Acacia Mining Ltd imetiliana saini ya Makubaliano (MoU) na Halmashauri za Wilaya ya Tarime, Kahama na Msalala ili kuweza kutekeleza ulipaji wa ushuru wa huduma (service levy) kwa kiwango cha asilimia 0.3 ya mapato ghafi ya kampuni hiyo kwa mwaka mzima kwa mujibu wa sheria ya Serikali za Mitaa. 
   Tukio hilo limefanyika tarehe 10 Juni, 2015 jijini Dar es Salaam makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika, Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje na baadhi ya watendaji wa wizara hiyo. 
  Akizungumza mara baada ya tukio hilo, Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje alisema lengo la kuingia katika makubaliano hayo ni kuhakikisha ushuru unaolipwa na kampuni hiyo unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuendeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya halmashauri hizo. 
  Alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha ushuru unaolipwa na makampuni unaleta tija katika kuibua na kuendeleza miradi mbalimbali kwenye halmashauri husika ili kuepusha fedha hizo kutumika tofauti na makusudio yake. “Pande hizi zimeingia katika makubaliano ili kuhakikisha fedha inayolipwa na mgodi inatumika kwa malengo iliyokusudiwa na si vinginevyo,” alisema Mhandisi Samaje. 
  Alisema makubaliano hayo pia yamelenga kuongeza uwazi wa matumizi ya fedha zitakazolipwa na mgodi huo katika uendelezaji wa miradi ambayo imeibuliwa kwa makubaliano ya pamoja na ya wazi. “Makubaliano hayo yanasisitiza sana suala la uwazi na uwajibikaji kwani imeelezwa wazi kuwa fedha hizo zitatumika kufadhili na kuendeleza miradi ambayo imeibuliwa kwa uwazi na kwa ushirikiano na makubaliano maalumu ya mabaraza ya Halmashauri hizo,” alifafanua Mhandisi Samaje. 
   Mhandisi Samaje alieleza kwamba kumekuwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi waishio kwenye maeneo ilipo migodi husika ya kuwa hakuna faida ambayo wananchi hao wanapata kutokana na uwepo wa migodi hiyo. Alisema ili kuondokana na malalamiko hayo na kuhakikisha kunakuwa na tija iliyokusudiwa, miradi itakayofadhiliwa kwa fedha hizo itakuwa chini ya uangalizi (overseer) wa Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI pamoja na Wizara ya Nishati na Madini. 
  Alisema katika makubaliano hayo, halmashauri hizo zinatakiwa kukaa kwa pamoja na kampuni hiyo kujadili maendeleo ya miradi husika na vilevile kutoa taarifa za maendeleo ya miradi husika mara mbili kwa mwaka kwa waangalizi wa miradi husika ambao ni Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Wizara ya Nishati na Madini. 
  Aidha, kwa upande mwingine, Mhandisi Samaje alisema kwa kupitia makubaliano hayo, Kampuni ya Acacia itawasilisha kwa halmashauri hizo taarifa ya wakandarasi na watoa huduma wengine wanaofanya kazi na kampuni hiyo na pia itasaidia halmashauri hizo kuwafikia ili nao waanze kulipa ushuru huo kwa halmashauri husika.
  “Hatua ya kampuni hii kukubali kutoa taarifa za wakandarasi itasaidia halmashauri kuwabana wakandarasi hao ili nao walipe ushuru stahiki kwa maendeleo ya halmashauri hizo na taifa kwa ujumla,” alisema. 
  Mhandisi Samaje alizipongeza pande hizo mbili kwa kuingia makubaliano hayo na kueleza kuwa makubaliano hayo yanatarajiwa kuleta tija katika kuendeleza miradi mbalimbali nchini na hivyo kukuza uchumi wa halmashauri husika na taifa kwa ujumla. 
  Ilielezwa kuwa utekelezaji wa makubaliano hayo unaanza mara moja ambapo kampuni hiyo itakuwa inalipa ushuru huo kwa awamu mbili ambazo ni mwezi Julai na mwezi Januari. Aidha, makabidhiano ya makubaliano hayo yanatarajiwa kufanyika wilayani Kahama tarehe 12 mwezi Juni, mwaka huu na yatashuhudiwa na wadau wote.
   Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje akifafanua jambo kabla ya tukio la utiaji saini ya Makubaliano (MoU) ya ulipaji wa ushuru wa huduma (Service Levy) baina ya Kampuni ya Acacia Mining Limited na halmashauri za wilaya ya Tarime, Kahama na Msalala lililofanyika tarehe 10 mwezi Juni mwaka huu.
  Makamu wa Rais wa Acacia, Deo Mwanyika (wa pili kushoto waliokaa) akitiliana saini ya Makubaliano na wawakilishi wa halmashauri za Wilaya ya Msalala na halmashauri ya Mji wa Kahama. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Patrick Karangwa anaemfuatia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama, Felix Kimaryo. Wanaoshuhudia ni Kamishna Msaidizi wa Madini- Ukaguzi wa Migodi, Ally Samaje (wa kwanza kulia waliosimama) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya (wa tatu kutoka kulia- waliosimama).


  0 0

  Mh January Makamba na mkewe wakiwasili katika ofisi za CCM Mkoa wa Njombe  ambapo walipokelewa na wanachama wa CCM aliokuwa na kikundi cha ngoma
  Mh January Makamba na mkewe wakisalimana na baadhi ya wanachama wa CCM katika ukumbi mdogo wa CCM mkoani Njombe.
  Mh January Makamba akiwaka sahihi katika kitabu cha wageni katika ofisi za CCM mkoa wa Njombe.
  Mh January Makamba akipokea fomu yenye majina ya wanachama wa CCM wa Njombe waliomdhamini kutoka kwa katibu wa CCM moa wa Njombe, ndugu Mponzi. idadi ya wanachama waliojitokeza kuweka sahihi ya kumdhamini ni 72.

  0 0  0 0

   Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine, Dkt. Silvia Materu akitoa mafunzo juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Nkoarisambu, wilayani Arumeru mkoani Arusha, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia mradi wa  Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini,  Tarehe 12 Juni, 2015. 
   Mwezeshaji kutoka Wizara ya maji, Diana Kimbute akifafanua umuhimu wa vifaa vya kisasa vya kupima viwango vya maji na kutoa taarifa za hali ya hewa wakati wa mafunzo yautekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, kwa kamati za maafa za kata ya Nkoarisambu, wilayani Arumeru mkoani Arusha, kulia kwake ni Mwakilishi wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Vendelin Basso na kushoto ni mtaalam kutoka bonde hilo, William Luanda, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tarehe 12 Juni, 2015
   Mtaalamu wa masuala ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Tanzania, Bwire Masinde akitoa mafunzo juu ya mabadiliko ya tabianchi kwa wajumbe wa kamati za maafa za kata ya Nkoarisambu, wilayani Arumeru mkoani Arusha, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia mradi wa  Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini,  Tarehe 11 Juni, 2015.
   Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, kutoka kamati za maafa za kata ya Nkoarisambu, wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiandika maudhui ya mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, wa kwanza ni, Elieka Akyoo, Tarehe 12 Juni, 2015.
   
  Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji mradi wa Kuimarisha mfumo wa habari za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema nchini, kutoka kamati za maafa za kata ya Nkoarisambu, wilayani Arumeru mkoani Arusha, wakiandika maudhui ya mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, wa kwanza ni, Eliyona Mugure, Tarehe 12 Juni, 2015

  0 0


  0 0


older | 1 | .... | 867 | 868 | (Page 869) | 870 | 871 | .... | 3348 | newer