Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 866 | 867 | (Page 868) | 869 | 870 | .... | 3348 | newer

  0 0
 • 06/10/15--02:57: shi Kistaa na Rich Mavoko


 • 0 0

  Gulio la Airtel Smartphone lililofanyika wiki iliyopita pale Mlimani City wikiendi iliyopita .Baadhi ya Wateja waliofika katika Mlimani City kujipatia Ofa kabambe inayotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel na Huawei katika banda la Mlimani City jijini Dar Es Salaam wiki iliyopita. Gulio linalomuwezesha mteja kujishindia zawadi mbali mbali pale anaponunua simu ya Huawei.
  Airtel Bazaar Gulio lililoanza wiki iliyopita pale Mlimani City siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili litaendelea tena wiki hii kutoa ofa kabambe za simu za kisasa. Wiki hii Bazaar la Airtel na Huwawei ni pale Kibo Complex Tegeta na Mlimani City kuanzia saa tatu na nusu Asubuhi hadi saa moja usiku siku zile zile za Ijumaa Jumamosi na Jumapili.

  Huu ndio wakati wako wewe kujismartifonisha kwa simu kali kwa gharama nafuu ikiambatana na Bando la bure la mwaka mzima la Airtel.

  Bazaar hili sio lakukosa kwani linamwaga ofa ambazo huwezi kupata popote zaidi ya Airtel.

  Karibuni Kusmatifonika na Airtel

  0 0

  Mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Taifa la Sweden, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi wa Sweden hapa nchini. Mhe. Lennarth Hjelmaker (hayupo pichani).
  Balozi wa Sweden hapa nchini, Mhe.Balozi Lennarth Hjelmaker akifungua hafla hiyo iliyofanyika usiku wa tarehe 09/06/2015 katika Makazi ya Balozi huyo Masaki Jijini Dar es Salaam.
   Balozi Lennarth akimkaribisha Balozi Mulamula katika hafla hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akikaribishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Nd. Moh’d Omar Nyawenga kuyafunga Mafunzo elekezi ya siku 5 kwa Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Dolfin By Kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja.
  Katibu wa UWT Wilaya ya Mjini Bibi ASHA Mzee Khamis akizoa maazimio ya washiriki wa mafunzo elekezi ya Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini mbele ya mgenzi rasmi Balozi Seif.
  Katibu wa CCM Jimbo la Magomeni Nd. Makame Khamis Ame akiwa miongoni mwa washiriki wa mafunzo elekezi ya Viongozi na watendaji wa CCM kuanzia ngazi ya Matawi hadi Mkoa Mjini akipokea cheti kutoka kwa Balozi Seif mara baada ya kumaliza mafunzo yao hapo Dolfin Bay Hoteli Kizimkazi.


  0 0

  Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Andrew Lyimo (katikati), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya akaunti za mishahara iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao’ yenye lengo la kuhamasisha wafanyakazi kuchukulia misharahara benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter na Meneja Malipo ya Mishahara na Maendeleo, Amos Lyimo.
  Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Andrew Lyimo na Meneja wa Malipo ya Mishahara na Maendeleo, Amos Lyimo.
  Meneja Malipo ya Mishahara na Maendeleo wa Benki ya NBC Tanzania, Amos Lyimo (kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya akaunti za mishahara iliyopewa jina la ‘Mcheza Kwao’ yenye lengo la kuhamasisha wafanyakazi kuchukulia misharahara benki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NBC, Andrew Lyimo na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.
  Baadhi ya waandishi waliohudhuria uzinduzi huo wakisikiliza maelezo kuhusu kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akizungumza na wanahabari (hawako pichani) juu ya tuhuma zilizoibuliwa bungeni dhidi yake.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali ya habari mkoani Kilimanjaro.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  SIKU moja baada ya kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kumlipua mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama kwa madai ya kufanya udalali na ufisadi katika uporaji wa ardhi ya wananchi ,mkuu huyo amejitokeza
  mbele ya wanahabari na kukanusha tuhuma hizo.

  Katika utetezi wake Gama alirejea kauli yake aliyoitoa miaka sita iliyopita ya kuwa yeye ni msafi huku akiitupia mzigo halmashauri ya wilaya ya Rombo tuhuma za kiasi cha sh Mil 500 zilizotajwa kutolewa wawekezaji wa Kichina kama fidia kwa wananchi katika ardhi
  kilipojengwa kiwanda cha kutengeneza Saruji.

  Alisema tuhuma zilizotolewa Bungeni dhidi yake si za kweli na kwamba ni za kisiasa huku akitaja sababu ya kuibuliwa kwa tuhuma hizo kuwa ni kutokana na juhudi zake za kupambana na Pombe haramu katika wilaya ya Rombo pamoja na Urejeshwaji wa wafanyabiashara katika soko la kati la mjini Moshi.


  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa (BOA), Masia Mushi, akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, kuhusu mradi mkubwa wa mikopo nafuu ya nyumba zilizojengwa na kampuni hiyo, zilizopo eneo la Somangira, Kigamboni jijini Dar es Salaam, ambao utawanufaisha watanzania hususani wateja wa benki ya BOA, ambao ulisainiwa rasmi jana. Katikati ni Naibu Meneja Mkuu wa AVIC, Liu Dexiang na kushoto ni Mwanasheria wa kampuni hiyo, Li Jiayin.
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakisaini mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigambini jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania (BOA), Masia Mushi (kulia), na Naibu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uendelezaji wa Ardhi ya AVIC, Liu Dexiang, wakibadilishana hati za mktaba wa makubaliano ya mikopo na uuzaji wa nyumba za bei nafuu kupitia BOA jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusaini leo, zilizojengwa na kampuni hiyo eneo la Somangira, Kigambini jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwanasheria wa BOA, Patrick Malewo na kushoto ni Mwansheria wa AVIC, Li Jiayin.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (katikati) akionyesha kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwaonyesha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabrasha lenye fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kabla ya kuanza kuzungumza na kujibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari. Kulia ni mkewe Waziri Chikawe, Profesa Amandina Lihamba. Tukio hilo la uchukuaji wa fomu lilifanya katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Waziri Chikawe ambaye alijibu maswali ya waandishi wa habari kiufasaha huku akishangiliwa na wanachama hao, alisema yeye ni kiongozi mwenye uzoefu mkubwa na pia akiteuliwa na chama chake kugombea nafasi hiyo ataendeleza mapambana zaidi dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini pamoja na adui mwingine rushwa ambaye ni adui wa maendeleo. Kulia ni mkewe, Profesa Amandina Lihamba.


  0 0

  Na Georgina Misama, MAELEZO-Dodoma

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameombwa kumwajibisha mara moja Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bwn. Leonidas Gama kwa kutumia vibaya madaraka yake na kujiingiza kwenye biashara chafu ya kupora na kuwapa wawekezaji wageni ardhi ya wananchi mkoani humo. Ombi hilo limetolewa leo na Mbunge wa Rombo, Mkoani Kilimanjaro Mhe. Joseph Selasini alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari wa Bunge, Mjini Dodoma.

  Aidha, Mhe. Selasini ameitaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) imchunguze mkuu huyo wa mkoa pamoja na watendaji wote wa serikali ambao amedai wametumia madaraka yao vibaya, kuwatapeli wananchi ardhi na kutumia isivyo halali fedha za Halmashauri za Wilaya ya Rombo shilingi million 168 kuanzisha kampuni binafsi.

  Amesema Mkuu huyo wa Mkoa aliilazimisha halmashauri ya Rombo kutoa fedha hizo shilingi millioni 168 kuwalipa fidia wanaushirika wa Lokolova waliotoa kwa hiyari yao, kwa Rais Jakaya Kikwete ardhi heka 140 kwa ajili ya kujenga soko la kisasa.

  Amesema hata hivyo, bwana Gama ameshiriki katika kuanzisha kampuni binafsi ya ubia ya kujenga na kuendesha soko hilo inayomilikiwa na wananchi wawili raia wa China na Mtoto wa Mkuu huyo wa Mkoa. Kampuni hiyo imeanzishwa bila kushirikisha Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambayo alitoa fedha za kulipa fidia wala wananchi wa rombo.

  Amesema wakati alipokwenda China kuwatafuta wawekezaji hao, Bwn. Gama alitumia fedha za Halmashauri ya Rombo na nembo ya serikali ya mkoa imetumika katika kuanzisha kampuni hiyo binafsi.

  Mhe. Selasini amesema pia kuwa, Bwn. Gama amefuta ushirika wa Lokolova na kuunyang’anya ardhi uliokuwa nayo eka 2100 ingawa Waziri Mkuu ameagiza ushirika huo urejeshwa. Mhe. Selasini aliyeambatana na Mbunge wa Vunjo, Mhe. Augustine Mrema amesema kuwa, kuna tetesi kwamba kampuni hiyo binafsi imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kulipa fidia lakini shilingi milioni 168 zilizotolewa na Halmashauri ya Rombo haijulikani zimefanyiwa nini. Mbunge huyu amesema yeye hapingi uwekezaji katika jimbo la Rombo lakini anataka uwekezaji huo uwe shirikishi wananchi waukubali na wawe wabia au wanufaike na ajira zinazotokana na uwekezaji huo.

  Ushauri huo ulitolewa pia juzi na Waziri kivuli wa Wizara wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Halima Mdee wakati akiwasilisha bajeti ya kambi ya upinzani. Pia Mhe. Mrema amewasilisha leo Hoja binafsi kuhusu suala hilo.

  Hata hivyo, Spika, Mheshimiwa Anna Makinda amesema kama alivyoahidi Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Ardhi juzi kuwa hawezi kulitolea jibu suala hilo mpaka ufanywe uchunguzi kupata ushuhuda na wabunge hao wawe wavumilivu ili wizara iweze kulifuatilia suala hilo.
  Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mhe. Joseph Selasini, akiwaonyesha waandishi wa habari mkataba wa ubia kati ya Raia wa China na anayedai ni Mtoto wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.

  0 0

  Mratibu wa tamasha la michezo na Afya ,Dimo Dembwe (katikati) akiwa ameshikana mikono na waratibu wenzake kama ishara ya umoja wa kufanikisha tamasha hilo. Wakati walipokuwa wakiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Meneja Utawala wa benki ya CRDB, Leevan Maro,Mwandaaji msaidizi wa Tamasha hilo Fakii Majipino,Rais wa TAFF Simon Mwakifuamba na Mratibu wa Tamasha hilo Josephine Kayombo.Tamasha hilo litafanyika jumapili kwenye viwanja vya Leaders club jijini.
  Mratibu wa tamasha la michezo na Afya,Dimo Dembwe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) Wakati walipokuwa wakitangaza siku maalum ya kufanya tamasha hilo kwenye ukumbi wa mikutano wa MAELEZO jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo litafanyika ijumapili kwenye viwanjavya Leaders Club kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya mazoezi jijini Dar es Salaam.Wengingine toka kushoto ni Meneja Utawala wa benki ya CRDB, Leevan Maro, na Mratibu wa Tamasha hilo Josephine Kayombo.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano wa kutangaza Tamasha la Michezo na Afya uliofanyika Kwenye ukumbi wa Habari Maelezo . Tamasha hilo litafanyika jumapili katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Musoma.
  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Kagera.
  Zoezi la udhamini katika wilaya ya Magu likiendelea huku Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akifatilia kwa makini.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Njombe, waliofika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Njombe Jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 360.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Iringa, waliofurika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Iringa mjini Jana, kwa ajili ya kutia saini fomu za kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini 317.

  0 0

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman na msafara wake ukielekea kukagua mradi wa maji uliopo katika kata ya Bundaza,wilayani Missenyi mkoani Kagera.Ndugu Kinana  na ujumbe wake wapo katika ziara za kujenga na kuimarisha chama, kukagua,kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenda kuona chanzo cha maji kwenye eneo la Ukolobe kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwika ndoo ya maji kwa mmja wa wana kijiji  cha Rukurungo,wilayani Missenyi,wakati wa uzinduzi wa huduma ya maji itakayohutumia wakazi zaidi ya 1884 na itakua na vituo zaidi ya 16 katika kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera. 
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Bwanjai mbele ya ofisi ya Kata ya CCM .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhiwa silaha za jadi na wazee wa Kimila wa Kata ya Bwanjai,wilaya ya missenyi mkoani Kagera,kulia kwake ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishuhudia tukio hilo.
    Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mzee Omari Hussein ambaye ni mmoja wa Walezi waliomlea wakati wa ujana wake.
   Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Assumpta Mshama (kulia) akiongea na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Balozi Dkt. Diodorus Kamala kwenye eneo la mkutano katika kata ya Bwanjai,wilani Missenyi mkoani Kagera.

  PICHA NA MICHUZI JR-MISSENYI - KAGERA 


  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwamuwakilisha Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, katika ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa muziki kwa nchi za jahazi, inaofanyika chuo cha muziki Forodhani Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Chuo cha Muziki Zanzibar bibi Fatma Kilua, akimkaribisha mgeni rasmi Maalim Seif katika ufunguzi za mkutano huo.
  Muandaaji wa mkutano huo Profesa Raymond Vogals, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.


  0 0


  0 0  0 0  0 0

  Hatimaye siku imewadia, tarehe iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab wa jiji la Mwanza ndio hii hapa - ni Mzee Yussuf na Isha Mashauzi katika onyesho la kukata na shoka ndani ya Villa Park leo usiku.
  Ni onyesho linalokutanisha miamba miwili ya taarab ambapo licha ya kuchukuliwa kama mtu na mwanae lakini upinzani mkubwa unatarajiwa kutawala katika onyesho hilo lililopewa jina la usiku wa baba na mwana.

  Wasanii wote wawili (Isha na Mzee) wameahidi kumimina uhondo wa aina yake Alhamisi ya leo hapo Villa Park - Mwanza huku kila mmoja akikataa kuanika silaha (nyimbo) zake za maangamizi.


  Hii ni mara ya kwanza kwa Mzee Yussuf na Isha Mashauzi kukutana jukwaa moja nje ya Dar es Salaam tangu Isha alipojiengua Jahazi Modern Taarab ya Mzee Yussuf zaidi ya miaka minne iliyopita.


  0 0  Umesha jiulizaga kwanini kuna .co, .or, .go, .ac, nakadhalika. Katika Domain Name System (DNS) yani mfumo wa domain kuna ngazi tofauti. Leo nataka tuongelee SLD yani Second Level Domain au ngazi ya pili ya domain ambayo hii iko punde tuu baada ya Top Level Domain (TLD). 

  Mfano .co katika .co.tz ni SLD wakati .tz ni TLD (Top Level Domain).  Kwa kawaida Second Level Domain (SLD) huwa ina tambulisha shirika (organization) linalo sajili hio domain liko katika mfumo gani au ni la aina gani.  Kwa hapa Tanzania, tzNIC wamepanga SLD (Second Level Domain) kama ifutavyo.
  • .co.tz – hii ni kwaajili ya kampuni au biashara zilizo sajiliwa kulingana na sheria za usajili wa makampuni ya biashara Tanzania.
  • .or.tz – hii ni kwaajili ya mashirika ya sio tafuta faida katika kuendesha shuguli zao.
  • .go.tz – hii ni kwaajili ya mashirika ya kiserikali ambayo yame undwa na bunge la Tanzania au yametokana na sera ambazo zimepitishwa na serikali ambayo hufanya kazi ya kuhudumia wananchi kama vile wizara na kadhalika.
  • .ac.tz – hii ni kwaajili ya taasisi za elimu ya juu na ufundi.
  • .ne.tz – hii ni kwaajili ya makampuni ya mawasliano kwa njia za mtandao.
  • .mil.tz – hii ni mahususi kwaajili ya Jeshi la Tanzania na taasisi zinazo husika maswala ya ulinzi.
  • .sc.tz – hii ni kwaajili ya shule za awali, msingi pamoja na sekondari.
  Hivyo basi kama unataka kuregister domain yako unatakiwa kuzingatia mfumo huo ili kuwa rahisi kwa wewe kupatikana pale wateja wako wanapo kutafuta mtandaoni.  0 0

   Kingine kipya kutoka Star Times kinadondoka kwako! App kali ya Tenbre; sasa itakufanya uzipate habari zote kali, chat room inakayokupa uwezo wakualika marafiki, kupiga stori mbalimbali za vipindi vya Startimes ambapo tabasamu hutawala.

  Orodha yote ya vipindi vya wiki nzima itakuwa kiganjani mwako kupitia smartphone yako, unapata uwezo wakipekee kupanga channel uzipendazo kutegemeana na nchi; au mkoa. Si hilo tu, wale wapenzi wa filamu na muziki na habari zataifa hatuja waacha nyuma. 
                                                                                                                                                                                   
   Utaona vipindi vikiruka live, vipindi vifuatavyo kwenye ratiba na pia kukusaidia kuweka kumbukumbu ya vipindi vyako bora unavyo vipenda.

  Tazama salio lako la pochi yamtandaoni kwaurahisi zaidi, kujua salio kiasi gani limebaki kwenye akaunti yako. Yote ndani yaTenbre, huduma bora toka StarTimes.

  Ukitaka kudownload bonyeza hapa bofyahapa
  Kama unaswali au ungependa kujua zaidi, tembelea kurasa za Startimes hapa chini.

older | 1 | .... | 866 | 867 | (Page 868) | 869 | 870 | .... | 3348 | newer