Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 865 | 866 | (Page 867) | 868 | 869 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Juni 09, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho Jumatano saa 11 jioni.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jumanne Juni 09, 2015 maeneo ya Stesheni za Ngeta na Ruvu mkoani Pwani ambapo mabehewa matano yenye shehena ya sukari yameanguka kabisa.

  Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.

  Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
  Mhandisi Elias Mshana,
  Dar es Salaam,
  Juni 09, 2015.

  0 0

  Mgeni rasmi katika Mkutano wa 4 wa wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibimayila, akifungua mkutano huo ulioanza leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Arusha, Jijini Arusha. Mradi huo wa kuwasaidia watu wenye magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, umefika kwenye mikoa kumi na saba na wilaya 110 mwaka 2014.
  Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) toka Geneva nchini Uswiss, Denise Mupfason akielezea ushiriki wa shirika hilo kwenye Mkutano huo wa 4 wa wadau wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele, uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Arusha, Jijini Arusha.
  Afisa mradi wa NTD upande wa vikope (trakoma), Dkt. Edward Kirumbi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi pamoja na washiriki wa mkutano huo ulioanza leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya New Arusha, Jijini Arusha.
  Sehemu ya Washiriki wa mkutano huo.
  Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.

  0 0

  Mwenyekiti wa UWT Mufindi na mjumbe wa NEC Taifa Bi Marcelina Mkini akiwapongeza  wanawake kwa kuonyesha kumkubali
  Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Bi Marcelina Mkini wa kwanza kushoto akiwa na mkuu wa wilaya ya Mufindi Mboni Mhita na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Bi Zainabu Mwamwindi wakati wa kongamano la wanawake wilayani Mufindi.

   WAKATI joto  la uchaguzi  mkuu likiendelea  kushika kasi ndani ya chama  cha mapinduzi (CCM) kwa  wanachama  wake kujitokeza kutia nia ya kuwania urais ,ubunge na udiwani , umoja  wa wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Mufindi umemuomba mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Mufindi  kusini .

  Wakizungumza mara baada ya  kumalizika kwa  kongamano la UWT wilaya ya Mufindi wajumbe wa kongamano  hilo  walisema  kuwa  toka nchi ipate  uhuru  wake  mwaka 1961  wilaya ya Mufindi mkoani Iringa haijapata  kuwa na mbunge mwanamke  hivyo kwa uchaguzi wa mwaka  huu lazima wanawake wachukue nafasi ya  kuongoza ubunge jimbo la Mufindi kusini ambalo kwa  sasa  linaongozwa na mbunge Mendrady Kigola (CCM).


  0 0

  Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (kushoto) akiteta na Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa, Bungeni mjini Dodoma Juni 9, 2015.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Juni 9, 2015.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Stephen Kebwe akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Juni 9, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia jambo katika mazungumzo kati yake na Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini na Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Mkuranga, Adam Malima (kulia) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 9, 2015.


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  ALIYEKUWA Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk.  Augustine Mahiga ametangaza nia ya kugombea urais ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), jijini Dar es salaam leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Mahiga amesema maadili yamemomonyoka na kufanya kuwepo kwa rushwa na ufisadi.

  Mahiga amesema ubadhirifu na ufisadi katika taifa kunahitajika kuwepo kwa mwelekeo katika kuweza kupambana na vitu hivyo ili maendeleo yapatikane kwa wananchi.

  “Nikipata nafasi hii nitatumikia watu katika kuujenga uchumi imara kwa kila mwananchi kutokana na kuwepo kwa dira na kuondoa matabaka yanayotokana na ubadhirifu wa mali za umma”amesema Mahiga.

  Amesema CCM itoe fursa, isifikie utawala wa watu wenye pesa hiyo sio dhamira ya CCM, na watu wanaotoa msaada uwe na kikomo chake.

  Mahiga amesema katika kuweza kufikia uchumi wa kati kunatakiwa kupambana na rushwa na ufisadi, bila kufanya hivyo uchumi huo hautafikiwa.
  Aliyekuwa Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Augustine Mahiga akizungumza wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo katika ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya waandishi wa habari na wananchi wakimsikiliza Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Dk Augustine Mahiga wakati akitangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  THE Comorian Union Chambers o Commerce, Industry and Agriculture UCCIA and their counterpart from Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture ZNCCIA put hands to gather as a symbol of unity after they have signed MoU that aiming to foster business and trade development among the two countries during the ceremony in Moron. The only lady seen in the picture is Mtwara Regional Commissioner, Halima Dendego.
  President of Comorian Union Chambers o Commerce, Industry and Agriculture UCCIA, Fahmy Thabit with spectacles sign MoU with his counterpart from Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture ZNCCIA, Vice President, Ali About Mzee in Moron yesterday. Others from left are the Chief executive Officer of Ocean Business Partners, Abdulsamad Abdulrahim, Mtwara Regional Commissioner Halima Dendego and ATCL acting Director, Jonson Mfinanga.
  President of Comorian Union Chambers o Commerce, Industry and Agriculture UCCIA, Fahmy Thabit with spectacles exchanges document with counterpart from Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture ZNCCIA, Vice President, Ali About Mzee after they have sign MoU to strengthen business between those two countries in Moron yesterday. Left is Chief executive Officer of Ocean Business Partners, Abdulsamad Abdulrahim,( R) is Mtwara Regional Commissioner Halima Dendego and ATCL acting Director, Jonson Mfinanga.

  THE Comorian Union Chambers o Commerce, Industry and Agriculture UCCIA has signed MOU with their counterpart Zanzibar National Chamber of Commerce, Industry and Agriculture  ZNCCIA which aim to foster  business and trade development among the two countries.

  The signing ceremony took place yesterday in Comoro Capital city Moroni between UCCIA President Fahmy Thabit and NCCIA Vice President, Ali About Mzee and it was witnessed by the Mtwara Regional Commissioner, Halima Dendego and Air Tanzania Limited (ATCL) Acting Director, Johnson Mfinanga.


  0 0

  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) akiwa na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Gabonese Mhe,Jean ClaudeBouyobartkabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Afrika na Wajerumani uliofanyika Mjini Berlin Nchini Ujerumani.
  Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Gabonese Mhe,Jean ClaudeBouyobart akizungumza na washiriki mbali mbali wa Mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Afrika na Wajerumani alipoufungua rasmi katika jumba la Baraza la Biashara la Ujerumani Mjini Berlin.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake YA UFUNGUZI WA katika Mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Afrika na Ujerumani uliofanyika Mjini Berlin.


  0 0

  Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya (Chadema)akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kibosho Kilima kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali katika mashindano ya Lucy Owenya Cup 2015. 
  Meza kuu wakifurahi mara baada ya mwamuzi kupuliza kipyenga cha mwisho ambapo timu ya Kibosho Kindi iliibuka na ushindi wa bao 3 kwa 1.
  Mchezo ukiendelea.
  Mashabiki wa timu ya soka ya Kibosho Kindi wakifurahia ushindi huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  IMG_0820

  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea katika kijiji cha Chasimba kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige).

  Na Modewjiblog team, Bagamoyo
  SERIKALI ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF.

  Fedha hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa nchini.

  Mashirika hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).

  Hayo yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana.


  0 0

   viti vikiwa tupu baada ya kuahirishwa kwa mdahalo huo.
   Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali (kulia), akizungumza na wadau mbalimbali waliofika kwa lengo la kuwasikiliza wagombea hao ambao hawakufika.
  Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali, akitoka ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Recency Kilimanjaro baada ya kuahirishwa kwa Mdahalo wa waliotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho kushindwa kuhudhuria Dar es Salaam juzi. Wagombea hao walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo ni Mwigulu Nchemba, Samuel Sitta, January Makamba, Lazaro Nyalandu  na Frederick Sumaye.

  BOFYA HAPA KUSOMA MKASA MZIMA 

  0 0

   As Barcelona’s incredible forward team of Messi, Neymar and Suarez take on Juventus F.C in Berlin Germany on 6th of June; Heineken Tanzania set up an exclusive VIP experience for its football lovers to champion the match from Dar es salaam.

  To bring the excitement of the world class tournament to fans, Heineken  hosted the final match screening at George n Dragon in Masaki, all Samaki Samaki venues, Club 777 in Kawe,  on exclusive events open to the public due to popular demand following past UEFA Champions League final match screenings they have hosted before. The final match screening is part of the momentum of ‘Champion the match’ campaign that Heineken had launched when the games kicked off in February 2015.

  “We have massive fans of football in Tanzania and because of timing, we understand that it may have been a bit tough to experience the excitement of the UCL in real-time,” said Heineken Tanzania Country Manager Michael Mbungu, “Throughout the tournaments we created ways to encourage football fans to enjoy the games and in the process make them feel as though they are part of the experience. The final match screening is a culmination of that experience. ” During the Quarter Finals of the UEFA Champions League, the international brewer, launched the Heineken limited edition ‘trophy’ bottle that was designed to reward consumers with a trophy of their own as part of champion the match campaign.

  The UEFA Champions League is the most prestigious club league; the premier sporting event has become a global phenomenon that fits perfectly with the Heineken brand, which is enjoyed in almost every country in the world.
  Football fans in a group photo with former Kenyan Prime Minister Raila Odinga who graced the UEFA Champions league final held at Club 777 in Kawe Dar es salaam.
  Tanzanian Football fans celebrating a decisive goal from Luis Suarez on the 68th Minute. Suarez's 68th minute goal gave Barcelona the lead after Juventus had come back to level Saturday's final at Berlin's Olympic stadium. Fc Barcelona thumped FC Juventus 3 goals to one to finally lift the UCL Trophy in Berlin
  Tanzanian Football fans celebrating a decisive goal from Luis Suarez on the 68th Minute. Suarez's 68th minute goal gave Barcelona the lead after Juventus had come back to level Saturday's final at Berlin's Olympic stadium. Fc Barcelona thumped FC Juventus 3 goals to one to finally lift the UCL Trophy in Berlin. 

  0 0


  0 0

  Baadhi ya wafanyakazi wa mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)wakipanda mti ofsini kwao Banana Ukonga jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira iliyofanyika hivi karibuni kitaifa mkoani Tanga.
  Makamu wa rais Mohammed Ghalib Bilal akikaribishwa na Katibu Mkuu wa wizara ya uchukuzi Dk. Shaban Mwinjaka wakati alipotembelea banda TCAA wakati wa maadhimisho ya wiki ya mazingira yaliyofanyika hivi karibuni mkoani Tanga.
  Wanafunizi wa shule za msingi mbalimbali mkoani Tanga waliotembelea kwenye banda la Mamlka ya Usafiri wa Anga Tanzania ,(TCAA) wakigawiwa vipeperushi vyenye ujumbe mbalimbali na Mkurugenzi mazingira wizara ya Uchukuzi Tumpe Mwaijunde wakati maadhimisho ya wiki ya Mazingira mkoani Tanga.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto) akilakiwa na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vijana, waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani Ruvuma kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000. Picha zote na John Badi.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwapungua mkono wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi, waliofurika nje ya Ofisi ya CCM Mkoa wa Ruvuma iliyopo mjini Songea jana, baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini watakaotia saini fomu zake za kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, fomu zilizotiwa saini na wanachama wa CCM mkoani humo, waliofika kwenye Ofisi hizo jana, kwa ajili ya kumdhamini ili ateuliwe kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo aliweza kupata wadhamini zaidi ya 5,000.


  0 0

   Mkuu wa mashindano ya Baiskeli na Barozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Sebregondi akizungumza na waandishi wa habari leo (hawapo pichani)katika ukumbi wa mikutano wa Ubalozi wa Ulaya jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mratibu wa Msafara wa Mkuu wa Operesheni ya umoja wa Ulaya, Eric Beaume.
  Naibu Mhamasishaji Mkuu wa Mfuko wa Fedha za Umoja wa Ulaya, Godlove Stephen akizungumza na waandishi wa habari hawapo hewani kuhusiana na mashindano ya baiskeli yatakayofanyika Juni 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam na kulia ni Mkuu wa mashindano ya Baiskeli na Barozi wa Umoja wa Ulaya Filiberto Sebregondi.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa watu walioongelea kuhusiana na mashindano yatakayofanyika jijini Dar es Salaam Juni 14 mwaka huu.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

  0 0


  0 0
 • 06/10/15--01:16: Niambie Live Show EP 4
 • Omby Nyongole, Henry Kente na Salma Moshi
  Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
  Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
  Ni Niambie Live....
  KARIBU

  0 0
 • 06/10/15--02:28: Ishi Kistaa na Rich Mavoko


 • 0 0

  Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kwa kushirikiana na wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, kesho siku ya alhamis tarehe 11/06/2015 wanatarajia kutoa zawadi kwa washindi wa Vodacom Premier League msimu wa 2014/2015.

  Hafla ya utoaji wa zawadi hizo itafanyika katika ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden Jubilee Tower (PSPF), mtaa wa Ohio eneo la Posta Mpya jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 jioni.

  Mgeni rasmi katika halfa hiyo ya utoaji zawadi kwa wachezaji, makocha, na timu washindi atakua ni Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

  Vodacom watatoa zawadi kwa Bingwa wa Ligi Kuu msimu 2014/2015, mshindi wa pili, mshindi wa tatu na mshindi wa nne, baadhi ya vipengele vitakavyotolewa zawadi pia na wadhamini hao wa Ligi Kuu ni :

  1. Mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
   Mohamed Hussein (Simba SC)
   Mrisho Ngasa (Young Africans)
   Saimon Msuva (Young Africans)

  2. Mlinda mlango bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  Mohamed Yusuph (Tanzania Prisons)
  Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
   Shaban Hassan (Coastal union)

  3. Kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  Goran Kopunovic (Simba SC)
   Hans Van Der Pluijm (Young Africans)
   Mbwana Makata - (Tanzania Prisons)

  4. Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  Israel Mjuni Nkongo
   Jonesia Rukyaa
   Samwel Mpenzu

  5. Timu yenye nidhamu Ligi Kuu ya Vodacom 2014/2015
  Mgambo JKT
   Mtibwa Sugar
   Simba SC

  MAHUNDI MCHEZAJI BORA MWEZI MEI

  Wakati huo huo mchezaji John Mahundi wa timu ya Coastal Union amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Mei, 2015 na jopo la makocha kufuatia kuwazidi wachezaji wengine 14 aliokuwa anananiwa nao nafasi hiyo.

  Kwa kuibuka mchezaji bora wa mwezi mei, Mahundi atazawadiwa fedha taslimu sh. milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa Ligi Kuu kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.  

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

   Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwa sambamba na Mbunge Jimbo la Temeke, Mh. Abbas Mtemvu (kati) kwenye viwanja vya Mwembe Yanga wakifuatilia mpambano kati ya timu ya Mtoni dhidi ya Kata ya 14, zilipokuwa zikichuana ambapo katika mchezo huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3.
   Mshambuliaji wa timu ya Mtoni, Samwel Salonge  (kulia) akimtoka beki wa timu ya timu ya Kata ya 14,katika mpambano wa Nusu Fainal  ya  Mtemvu Cup  kwenye Uwanja wa Mwembeyanga  Dar es Salaam jana,  Mtanange  huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3.
    Mshambuliaji wa timu ya Mtoni, Rajabu Zanda akimtoka beki wa timu ya timu ya Kata  14,katika mpambano wa Nusu Fainal  ya  Mtemvu Cup  kwenye Uwanja wa Mwembeyanga  Dar es Salaam jana,  Mtanange  huo, Kata ya 14 iliichapa Mtoni  mabao 4-3.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 865 | 866 | (Page 867) | 868 | 869 | .... | 3348 | newer