Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 868 | 869 | (Page 870) | 871 | 872 | .... | 3348 | newer

  0 0

  IMG_0984
  Balozi wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kushoto) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) wakikagua mitaala ya kufundishia kwenye ofisi za walimu katika shule ya msingi Yombo ambayo imejengwa na mradi wa awamu ya pili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) iliyopo katika kijiji cha Chasimba, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF wilayani humo huku Afisa Program Kitengo cha Uahulishaji Fedha (TASAF), Edith Mackenzie (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa ugeni huo.
  (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Tanzania Alvaro Rodriguez ametaka serikali za tawala za mikoa na serikali za mitaa kuwezeshwa zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi.

  Aliyasema hayo wakati alipozuru kijiji cha Chasimba mwishoni mwa juma akiwa na Balozi wa Hispania Luis Cuesta Civis kuona miradi ya maendeleo inayofadhiliwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania, Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Ubalozi wa Hispania.

  Mratibu huyo alisema kwamba mafanikio makubwa yanayoonekana katika kijiji cha Chasimba ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa wadau wa maendeleo na wanakijiji.

  Alisema ushirikiano huo ni muhimu katika kutokomeza umaskini uliokithiri katika jamii.

  Alisema pamoja na mafanikio hayo Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo wangelipenda kuona serikali za mitaa zinawezeshwa zaidi ili kuweza kusaidia jamii kama inavyofanyika sasa katika kijiji cha Chasimba.

  Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji kadhaa nchini vinavyofaidika na mpango unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, TASAF, ambao nao unachangiwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa maendeleo.

  Alisema anapenda kuona kwamba maisha ya wakazi wa kijiji hicho yanabadilika na kuwa kama ya mama Kicheko ambaye ameondoka katika umaskini uliokithiri baada ya kutumia vyema mradi uliofikishwa kijijini hapo.

  Alitoa wito kwa wadau wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kusaidia kuwezesha serikali za mitaa na mashirika yanayoapambana na umaskini nchini kuwezesha miradi ya kuondoa umaskini kufanikiwa.

  Bi. Kicheko ambaye mwaka mmoja uliopita alikuwa hohehahe kwa sasa anatengeneza sabuni, ameboresha nyumba yake kwa kuiwekea bati na ana kula mlo zaidi ya mmoja sasa.

  Katika ziara hiyo, Mratibu huyo alitaka kujua wananchi wa Chasimba katika miaka mitano hadi saba ijayo wanataka kuwaje na kujibiwa kwamba wanataka kuwa na hali bora zaidi ilivyo sasa na kuanzisha viwanda vidogo.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu.
  Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Januari Makamba amewaomba wanachama wenzake wa CCM walioko Njombe kutochukulia suala la ugombea kwa ushabiki kiasi cha kuzua mtafaruku ndani ya chama, jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wake.

  Makamba ameyasema hayo alipokuwa akiwashukuru wanachama wenzake waliojitokeza kumdhamini ili kupata ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

  "Najua katika kipindi hiki, ambacho wanachama wengi tumejitokeza kuwania nafasi hii kila mtu ametengeneza kundi la wafuasi ambao wengi wanadhani kwamba kuwa kundi la mtu mmoja basi wewe ni adui wa kundi jingine. Hili ni kosa, sote tunania njema na nchi hii, tujenge mazxingira ya kutooneana haya baada ya kupatikana kwa mgombea mmoja kwa kuungana mkono bila kuchafua wengine", alisisitiza Makamba.

  Makamba ameonya pia kuhusu kuchafuana kwa watangaza nia, wenyewe kwa wenyewe ambako kutasababisha kazi nyingine kubwa ya kuanza kumsafisha mgombesa atakayesimamishwa na chama muda utakapofika.

  Leo mchana Makamba anatarajiwa kupokea wadhamini mkoani Songea na baadae kuelekea Mbeya mjini ambako pia atafanya zoezi hilo.

  Mh January Makamba akicheza ngoma pamoja na wanachama wa CCM wilayani Njombe waliojitokeza kumdhamini.  0 0


  0 0

   Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia harakati za matengenezo ya Vitabu vya Baketi katika Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi wakati alipofanya ziara fupi ya Kutembelea kiwanda hicho.Kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bibi Hanat mohammed Aboud.
  Mkuu wa Kitengo cha Kompyuta katika Kiwanda cha uchapaji Maruhubi Nd. Moh’d Abass Rajab akimuonyesha  Balozi Seif aina za michoro tofauti  inayosarifiwa katika uchapaji wa vitabu na majarida mbali mbali yanayopelekwa  na wateja kuchapishwa kwenye kiwanda hicho.
  Picha na –OMPR – ZNZ.


  0 0  0 0

  Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (pichani) kesho Jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.
  Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .
  Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.
  Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.
  Katika kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na familia ya walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na kuwaua  wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO 
  LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0
 • 06/12/15--03:23: Article 12
 • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 96
  TAREHE 12 JUNI, 2015
  MEYA MWANZA KUFUNGA U13 KESHO
  Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.

  Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .

  Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.

  Lengo la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.

  Katika kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na familia ya walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na kuwaua  wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (pichani) , amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua.

  Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.” 

  Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.”

  Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa dead bodies, lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya uhakika, lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.” 

  “Katika safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa kila ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”

  Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano akitokea Iringa ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili kumwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.

  Akiwa uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo makada hao walipata nafasi ya kuzungumza. 

  Akiwa katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma, hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”

  “Ni lazima kina mama wawezeshwe kujiajiri ili msiwategemee kina baba kwa kila jambo lakini pia ili kufikia malengo hayo ni lazima tuwape elimu kina mama.”

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Burundi Mhe,Rajab Gamala alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha jana,[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Sensei Yoshiro Miyazato, Kancho Mwenyekiti wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu akimkabidhi cheti cha Dan ya 3 Sensei Rumadha Fundi mjini Naha, Okinawa, hivi karibuni. Sensei Rumadha sasa anashikilia Dan 3 kutoka vyama viwili vya karate – ikiwa ni Dan 3 kutoka Okinawa Goju Ryu Karate na Dan 6 kutoka Tanzania Karate do Federation.

  Sensei Rumadha akiwa Jundo Kan Dojo, chimbuko la Goju Ryu Karate duniani, lililoko Naha, Okinawa.

  Mke wa Kancho Miyazato akimfundisha mtoto wa Sensei Rumadha, Iman, juu ya Sanaa hiyo ya kujilinda.

  Sensei Rumadha akiwa mbele ya kaburi la mwanzilishi wa Naha te  Goju Ryu Karate, Master Kanryo Higashionna (Higaona) huko Okinawa.

  Sensei Rumadha na bintiye Iman wakipata chakula cha jioni na wenyeji wao mjini Naha, Okinawa.

  0 0

  Matayarisho ya awali ya maandalizi ya ujenzi wa Kiwanja cha Michezo cha Mao Tse tung kiliopo Mperani Kikwajuni Mjini Zanzibar yameanza rasmi kwa hatua ya utafiti wa uchunguzi wa udongo wa eneo hilo.

  Mhandisi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Ali Mbarouk alieleza hayo wakati akimpatia ufafanuzi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi ya kuangalia matayarisho hayo.

  Mhandisi Ali Mbaouk alimueleza Balozi Seif kwamba utafiti huo wa udongo unaofanywa kwa kuchukuwa  aina tofauti  za udongo kwenye vishimo 34 vinavyochimbwa  ndani ya eneo la uwanja huo unatarajiwa kuchukuwa muda wa siku 20.

  Alisema udongo huo utafanyia utafiti wa kina na wataalamu waliobobea ambao kukamilikwa kwake watatoa ripoti kamili itakayofuatiwa na utangazaji wa tenda kwa Makampuni yatayokuwa tayari kujenga uwanja huo.

  Alifahamisha kwamba ujenzi kamili wa uwanja wa Mao Tse Tung unatarajiwa kuanza rasmi mwezi wa Febuari mwaka 2016 chini ya ufadhili wa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China.

  Akitoa ufafanuzi wa Ramani ya  ujenzi  wa uwanja huo Mhandisi Ali Barouk alimueleza Balozi Seif kwamba uwanja huo utakapomalizika utakuwa na Viwanja viwili vya mchezo wa soka, kimoja kitakachokidhi michezo ya Pete pamoja na  Kikapu.

  Alieleza kwamba lipo eneo litakalotengwa maalum kwa michezo mbali mbali ya ndani { INDO GAMES }, Majukwaa ya watazamaji eneo la watu Maarufu { VIP } pamoja na ofisi za watendaji wa uwanja huo.

  Akielezea furaha yake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kukamilika kwa uwanja wa huo wa Mao Tse Tung kutasaidia kuupunguzia mzigo mkubwa uwanja wa michezo wa Amani.

  Balozi Seif alisema uwanja wa Amani kwa sasa ndio pekee unaobeba michezo yote ya Kimataifa na Kitaifa ,Sherehe tofauti ikiwemo ile kubwa ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na matamasha mbali mbali.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kati kati akisalimiana na wataalamu wa Kichina wanaosimamia utafiti wa udongo katika uwanja wa  Mao Tse Tung katika matayarisho ya awali na maandalizi ya ujenzi wake.
   
   Eneo la Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung likionekana kuwa katika maandalizi ya awali ya matayarisho ya ujenzi mpya unaotarajiwa kugharamiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China.


  0 0

  KITUO CHA RADIO CHA COCONUT FM ZANZIBAR CHAANDAA BONANZA LA "PEPEA" KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, KATIKA VIWANJA VYA MAISARA MJINI UNGUJA TAREHE 16 JUNE, 2015. 

  0 0

   Mkurugenzi  wa Upelelezi  wa  makosa  ya Jinai,(CP) Diwani  Athuman akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya mambo ya Ndani juu ya Operesheni  usalama  imetokana na maamuzi  yaliyofikiwa kwenye mikutano ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kati ya Nchi za Kusini  mwa Afrika na Mashariki mwa Afrika  waliokutana  chini ya mwavuli wa (SARPCCO) na (EAPCCO) uliofanyika Johanesburg nchini  Afrika  Kusini.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi  wa  Makosa  ya Jinai CP, Diwani  Athumania leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya mambo ya ndani jijini Dra es Salaam.
   ( Emmanuel  Massaka,Globu ya Jamii.
    
  Mkutano  wa maandalizi kwa ajili ya Operesheni hii ulifanyika kule Pretoria  Afrika  Kusini mnamo tarehe 23-24 April,2015. Wajumbe walikubaliana kufanya  Operesheni ya pamoja na kwa wakati  mmoja Mkutano huo uliamua pia kuwa makosa yafuatayo yapewe kipaumbele, Wizi wa magari, Madawa ya kulevya, Silaha haramu na milipuko, Wahamiaji haramu na biashara haramu ya binadam, Ugaidi , Biashara haramu ya madini, Wizi wa Miundombinu ya Umeme na Nyara za Serikali.

  0 0

  Mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza akitoa taarifa ya  idadi ya  wana CCM waliomdhamini Mbega
   
  Monica  Mbega  (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao  walijitokeza kumdhamini  kuwa mgombea wa nafasi ya  urais   kupitia CCM.


  0 0

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika  mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani  Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wa CCM Mkoani Kilimanjaro waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kumdhamini.
   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akisaini kitabu cha wageni huku Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini akihakiki kadi za wanachama kwa ajili ya udhamini.


  0 0

  Na Rahma Khamis – Maelezo Zanzibar.
  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na azma yake ya kukamilisha Mradi wa Utafiti wa Nishati mbadala ili kujuwa uwezekano wa Zanzibar kupata Umeme wake wa uhakika.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Ramadhan Abdalla  Shaaban katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  Chukwani  wakati akitoa Hutuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2015 /2016.

  Amesema Wizara yake imekamilisha kazi ya kupatikana  kwa Mkandarasi  kutoka katika Kampuni ya (AGMIN ya Italy) kwa Ujenzi wa Minara ambapo kwa sasa ameanza kazi zake.

  Aidha amefahamisha kuwa Mshauri Elekezaji wa ukusanyaji wa taarifa pamoja na kutaarisha Ripoti ya upembuzi  sahihi ( Feasibility Study) ameshapatikana ambapo kazi yao inatarajiwa kumalizika Mwaka ( 2017)
  Itakumbukwa kuwa Zanzibar bado inategemea Nishati ya Umeme kutoka Tanzania Bara na kwamba kama Utafiti huo utatoa Matokeo mazuri kuna uwezekano wa Zanzibar kuwa na Vyanzio vyake vya Umeme badala ya kutegemea Bara.

  Waziri Shabani amesema katika utekelezaji huo Wizara imeweza kushiriki katika mikutano mbalimbali iliyofanyika ndani na nje ya Nchi ikiwemo kuhudhuria katika mkutano wa kuitangaza Tanzania katika utekelezaji wa masuala ya Nishati (Den Hague-Uholanzi).

  Akielezea kuhusu utekelezaji huo amesema  kuwa ni kushiriki katika Maonesho na Warsha ya Nishati Mbadala iliyo fanyika Kahama na Tanzania, na kushiriki Vikao vya Jumuia ya Afrika Mashariki katika masuala ya Nishati na Umeme (Nairobi Entebe) sambamba na mkutano mkuu wa Mafuta na Gesi wa Afrika Mashariki (EAPCE 2015) uliofanyika Kigali –Ruwanda.

  Hata hivyo amesema katika kuhakikisha Nishati ya Mafuta inapatikana Nchini Wizara inaendelea kufuatilia shughuli za kusimamia upatikanaji wa Mafuta pamoja na utekelezwaji wa Ratiba za uagizaji wa Mafuta Nchini kwa Makampuni manne makubwa (GAPCO,UP,ZP na PUMA).

  Aidha  amefahamisha kuwa katika kulisimamia suala hilo dosari za uagizwaji wa Mafuta ya Petrol zimejitokeza baina ya Mwezi wa Februari na Machi ambazo zilichangiwa na kuchelewa kwa Meli ya Mafuta ya pamoja (Bulk Consignment) inayoleta Mafuta Nchini Tanzania.

  Sambamba  na hayo Waziri Shaaban amesema kutokana na hali iliyojitokeza ni kiashirio tosha cha kusisitiza umuhimu wa kuwepo kwa Taasisi maalum ya kushuhulikia Sekta Binafsi ya kuendesha Biashara hiyo kwa kutumia sheria.

  Waziri Shaaban ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishie Jumla ya Shl. Bilion 35 na Milioni 949 kwa ajili ya Wizara ya Ardhi Makaazi Maji na Nishati kwa mwaka wa Fedha 2015-16.  
                                                        
                                 IMETOLEWA NA  HABARI MAELEZO –ZANZIBAR.

  0 0

   Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha  Mwantumu Dossi akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo  Elisha Maghembe.Picha na Mahmoud Ahmad
  .

  0 0


  Waziri Mkuu wa Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wana CCM waliofika kumdhamini pamoja na wananchi wengine, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wana CCM 9516 kwa mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo safari yake ya kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kimteue kuwania nafasi ya urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea majina kutoka kwa Naibu Katibu wa CCM Wilaya ya Tabora Mjini, Bi. Hidaya Rashid yenye idadi wanachama wa CCM 9516 waliomdhamini ili aweze kuteuliwa na Chama kuwania Urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na WanaCCM waliofika kumdhani pamoja na wananchi wa Mji wa Tabora, kwenye viwanja vya ofisi za CCM Tabora Mjini, leo Juni 12, 2015.
  Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Mzee Juma Nkumba, aliewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tabora miaka ya nyuma.

  Mh. Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Wazee wa Mji wa Tabora.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma mara baada ya kabidhiwa fomu yenye sahihi za wanachama waliomdhamini.
  Mh January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma ndani ya ukumbi wa ofiswi kuu ya chama hicho mkoani Ruvuma. kuanzia kushoto ni mke January Makamba, Ramona Makamba, katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho na kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa, Odo Mwisho.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi fomu yenye majina na sahihi za wanachama waliomdhamini mh. January Makamba. Makabidhiano hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma.


  0 0

   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza baada ya kuchukuwa   fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni mkewe mama Tunu Pinda
  Sehemu ya wageni wakimsikiliza Mhe Pinda  wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watu waliofika kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumsikiliza wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma
    Baadhi  ya wazee wa Dodoma waliofika kwenye ukumbi wa Halmashauri kuu ya taifa ya CCM kumsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipozungumza baada  ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watu waliofika kwenye Ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kumsikiliza wakati alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukuwa fomu ya kuwania uteuzi wa CCM  ili awe mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao  kwenye ofisi kuu ya CCM mjini Dodoma.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 868 | 869 | (Page 870) | 871 | 872 | .... | 3348 | newer