Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI


KATIBU MTENDAJI WA ANGONET AZUNGUMZIA MASUALA YA LISHE NCHINI

$
0
0
Katibu Mtendaji wa Shirika lisilokua la kiserikali la ANGONET lenye makao makuu jijini Arusha, Petter Bayo (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya masuala ya lishe na kuitaka serikali iweke vipaumbele katika lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo.Katikati ni Mratibu wa Angonet, Petro Ahham na kulia ni Jovitha Mlay Mwanachama wa Shirika hilo.
Mratibu wa Angonet, Petro Ahham akifafanua juu ya Mkakati wa Lishe wa taifa wa July 2011/12 hadi Juni 2015/16 kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) jana katika mkutano na waandishi juu ya hali ya lishe nchini na namna ya kuhamasisha lishe ili kuondokana na udumavu na utapiamlo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (ANGONET), Petter Bayo. Picha na Mahmoud Ahmad

MWIGULU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS

$
0
0

Mh.Mwigulu akiwasili makao makuu ya CHAMA CHA MAPINDUZI mjini Dodoma kwaajili ya Kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.

Mh:Mwigulu akisaini kitabu cha Wagombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

BREAKING NYUZZZZ......: msafara wa makongoro nyerere wapata ajali mbaya mkoani kigoma

$
0
0
Msafara wa mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Charles Makongoro Nyerere umepata ajali wilayani Kasulu mkoani kigoma mapema leo hii.

Msafara huo uliokuwa ukielekea wilayani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini, ambapo gari walilokuwa wamepanda wasaidizi wa Makongoro ndilo lililopata ajali kwa kupinduka wakati likiwa kwenye mwendo.

Watu waliokuwepo katika gari hilo lililopata ajali wameumia vibaya sana akiwemo Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba na kukimbizwa katika hospital ya wilaya ya kasulu (mlimani) kwaajili ya matibabu.

tutaendelea kuwajuza zaidi juu tukio hilo
Gari lililopata ajali katika msafara wa Mgombea urais, Charles Makongoro Nyerere lililokuwa limebeba wasaidizi wake.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya kasulu wakishangaa ajali ya gari la wasaidizi wa mgombea urais kupitia CCM, Charles Makongoro Nyerere.

Stars yajidhatiti kuwakabili Misri

$
0
0
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.

Jana kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya Taifa kwa mazoezi.

Taifa Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.

Daktari wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya mazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.
Hali ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na kuzungukwa na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.

Wachezaji wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri, kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mapaharao. 

Wenyeji Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea nchini Misri.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

CHADEMA YATIKISA ARUSHA

$
0
0
 Profesor Jay akihamsisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIO MATUMAINI"
 Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari amewataka watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa Miaka Mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura" Pia ametambulisha AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
Mbuge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari akitambulisha  AMBULANCE 2 alizo zitoa kwenye jimbo lake
 umati wa wananchi waliouthuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS KIKWETE ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KWA RAIS WA CHINA KUFUATIA VIFO VYA WACHINA 400 KATIKA AJALI YA BOTI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping kuombeleza vifo vya zaidi ya watu 400 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya boti ya kitalii, iliyozama katika Mto wa Yangtze mwanzoni mwa wiki hii.

Meli ya kitalii ya Eastern Star ilizama katika Mto wa Yangtze, karibu na mji wa Jianli, Jimbo la Kati la Hubei, Jumatatu usiku ikiwa na abiria 456 waliokuwa wanafanya safari ya kitalii ya siku 11 kutoka Nanjing kwenda Chongqing. Mpaka usiku wa jana, Ijumaa, Juni 5,2015, miili ya watu 369 ilikwishapatikana, watu 46 walikuwa hawajulikani walipo na 14 walikuwa wameokolewa.

 Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amemwambia Rais Jinping: “Nimepokea kwa mshituko na masikitiko taarifa ya vifo vya mamia ya watu waliopoteza maisha yao katika ajali ya boti ya kitalii ya Eastern Star katika Jimbo la Hubei iliyotokea mwanzoni mwa wiki hii wakiwa katika safari kutoka Nanjing kwenda Chongqing.”
“Kwa hakika, haya ni maafa ya kitaifa. Kwa niaba ya Watanzania wenzangu, Serikali yangu na mimi mwenyewe, nakutumia wewe binafsi, Serikali yako na wananchi wote wa China salamu za dhati ya moyo wangu na naungana nanyi katika kuomboleza tukio hili la huzuni kubwa.”

Ameongeza Rais Kikwete katika salamu zake alizozituma usiku wa jana, Ijumaa, Juni 5, 2015 “Tanzania ikiwa nchi rafiki na China na Watanzania wote wanaungana na wenzao wa China kuwapa pole nyingi wote ambao wamepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo.”

Wakurugenzi watendaji na maofisa wa uchaguzi Mkoani Manyara wala viapo

$
0
0
Wakurugenzi watendaji na maofisa wa uchaguzi wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Manyara, wakila viapo kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliyofanyika jana mjini Babati.
Mchambuzi mwandamizi wa kompyuta wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) Joseph Mally akionyesha vifaa vya Biomertic Voter Registration (BVR) vitakavyotumika kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Manyara, jana mjini Babati.

KAMANDA MSTAAFU WA UVCCM KINONDONI ASHIRIKI KATIKA USAFI WA MAZINGIRA

$
0
0
 
Kamanda Mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya Kinondoni (UVCCM),Jumaa Mhina akichukua mbolea kwa ajili ya kupanda miti katika Zahanati Mbopo  baada ya mazoezi ya vijanawa Mbopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
Kamanda Mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya Kinondoni (UVCCM),Jumaa Mhina akishiriki katika usafi wa mazingira katika zahanati ya Mbopo iliyopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Kamanda Mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  Wilaya Kinondoni (UVCCM),Jumaa Mhina akishiriki mazoezi ya kukimbia na Vijana wa Mbopo katika eneo la Shule ya Msingi Mbopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 

BIASHARA KWANZA, USALAMA BAADAE....

$
0
0
BIASHARA KWANZA, USALAMA BAADAE: Kauli hiyo ndio inayoonekana kwa vijana hawa wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo ya kuuza machungwa eneo la Segera, Mkoani Tanga. maana wakiona basi limesimama mahala hapo, basi hawaangalii kabisa usalama wao, bali wanavuka tu kulifata hata kama kuna magari mengine yanapita.

LOWASSA ASHIRIKI JUBILEE YA MIAKA 50 YA SEMINARI YA MTAKATIFU KALOLI LWAHANGA, HUKO NGARA

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, (wapili kushoto), akiwa na Askofu  wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, mkoani Kagera, Severine Niwemuguzi baada ya kuzindua jiwe la msingi kuashiria maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50, Seminari ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Jumamosi Juni 6, 2015
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa, akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Severine Niwemuguzi, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege Biharamulo Mkoani Kagera kwa ajili ya kusherekea Miaka 50 ya Seminari ya Katote.
Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa, akiwasha kompyuta baada y kuzindua chumba cha mafunzo ya Kompyuta katikaKuadhimisha Jubilei ya Miaka 50 Seminari ya Mtakatifu Kaloli Lwahanga Katote Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara mkoani KageraJumamosi Juni 6, 2015. Kushoto ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lulenge Ngara, Severine Niwemuguzi.

Balozi Seif Iddi afungua Semina ya usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiifungua Semina ya siku moja ya Usafiri Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyofanyika kwenye ukumbi wa juu wa Baraza la Wawakilishi Mbweni.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Mh. Juma Duni Haji akitoa maelezo kwenye Semina ya Usafiri wa Barabarani kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kabla ya ufunguzi wa Senmina hiyo.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wadau wa usafiri walioshioriki semina ya usafiri wa bara barani wakifuatilia Horuba ya Mgeni rasmi Balozi Seif hayupa Pichani.

HOTUBA YA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE (MB.), ILIYOWASILISHWA BUNGENI LEO

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Mh. George Simbachawene.

NYALANDU ATANGAZA NIA KUGOMBEA URAIS

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi mkoani Singida baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua leo. (Picha na Loveness Bernard)

Umati wa watu ukimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu baada ya kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida leo. (Picha na Loveness Bernard)
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto) akiwa na mkewe Faraja kabla ya kuzungumza na wananchi mkoani Singida wakati wa kutangaza nia.

SENENE KIGANJA KIMOJA CHA MKONO 'JERO' MJINI BUKOBA.

$
0
0
 Baadhi wachuuzi wa kitowea maarufu kwa wakazi wa Bukoba,kiitwacho senene,wakiwaandaa tayari kwa kuwauza kwa wateja wao,ambapo hupima kwa kiganja cha mkono kwa kiasi cha shilingi 500.
 Kijana akiandaa senene wake kwa ajili ya chakula,kama alivyokutwa na Camera ya Globu ya Jamii nje ya soko la Bukoba mjini,ambako Senene hao hupatikana na kuuzwa kwa wingi. 
Wachuuzi wa kitoweo cha Senene wakimuuzia mteja wao,ambapo hupima kwa kiganja na kuuzwa 500 .
 Wengine wanauwaza wakiwa bado hai kama hivi
Baadhi ya akina mama wakiwa kwenye ujasiliamali wao biashara ya mbogamboga nje ya soko la Bukoba mjini,mapema leo mkoani Kagera.

PICHA NA MICHUZJI JR-BUKOBA

Introducing "End of the World" by Tarmo and Md Ice

$
0
0
Ankal with Mad Ice at the middle and Edwin Ndaki in Helsinki, Finland, last week where the crooner is now based

DKT. BILAL AONGOZA WANANCHI KWENYE MAZISHI YA MBUNGE WA JIMBO LA UKONGA MAREHEMU EUGENE MWAIPOSA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Maiposa kabla ya mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho kwenye Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa aliyefariki Ghafla nyumbani kwake Dodoma juzi, wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo Juni 06, 2015 nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekua Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa wakati wa mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya Mbunge wa Ukonga Marehemu Eugene Mwaiposa baada ya mazishi yake yaliyofanyika nyumbani kwake Ukonga Dar es salaam leo Juni 06, 2015. (Picha na OMR)

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AUNGURUMA MJINI BUKOBA LEO,KESHO MULEBA.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Mkutano wa hadhara leo, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na ilani ya Uchaguzi ya CCM.Ndugu Kinana yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku kumi akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho
  Mbunge wa Bukoba mjini Hamis Kagasheki (kushoto) akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba mkoani Kagera.
 Wananchi wa mji wa Bukoba mjini na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pichani katikati alipokuwa akizungumza
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba leo, akiwa katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mkoani Kagera.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Mh.John Mongella akiwasalimia Wananchi na  Wanachama wapenzi wa CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Mashujaa,mkoani Kagera.

PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA


WAGOMBEA URAIS CCM WAPO HURU KUSHIRIKI MIDAHALO - COMRADE KINANA

MHE. BERNARD MEMBE ANAKUALIKA LEO JUMAPILI KUMSIKILIZA ATAKAPOKUWA ANATANGAZA NIA YA URAIS

Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images