Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA BOHARI YA KUHIFADHI MAFUTA YA GBP MKOANI TANGA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Kituo cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, wakati alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Jeti ya kupokelea mafuta na Bohari ya kuhifadhia mafuta ya kampuni hiyo, wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana Juni 5, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka katika eneo hilo baada ya kukagua kituo hicho cha kupokelea mafuta cha Kampuni ya GBP, mkoani Tanga jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongoizana na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya GBP, wakati akielekea kukagua Bohari ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya GBP, alipokuwa katika ziara yake ya siku moja mkoani Tanga jana.


MAALIM SEIF AHUTUBIA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOFANYIKA KIBANDAMAITI, ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokelewa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, baada ya kuwasili akitokea Dar es Salaam ambako aliteuliwa Rasmi kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF mwaka 2015.
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akiwahutubia wafuasi na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Kibandamaiti mjini Zanzibar.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WANA CCM MKOANI SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA WAJITOKEZA KUMDHAMINI WAZIRI MAGUFULI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika mbio za kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama hicho kutoka kwa Katibu wa CCM Wilayani Nzega Mkoani Tabora.
Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akikabidhiwa fomu yenye orodha ya Wadhamini waliojitokeza kumdhamini katika Mkoa wa Shinyanga.
Baadhi ya Wadhimini waliojitokeza kumdhamini Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Singida wakimfurahia mara baada ya zoezi la uhakiki na kumdhamini katika mkoa wao kukamilika.

MH. LOWASSA ATUA ZANZIBAR KUSAKA WADHAMINI

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamaninaMbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowasa, (kulia), akipokewa na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini Unguja, Borafia Silima Juma, wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mkoa wa Mjini, Unguja Jumamosi usiku, Juni 6, 2015. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015. (Picha na K-VIS MEDIA)
Mh. Lowassa, akifurahia jambo na Mzee Borafia, mara baada ya kuwasili kisiwani Zanzinzibar, akitokea Mwanza
Wazirti Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Mh. Edward Lowassa, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, kisiwani Unguja, Zanzibar, Borafia Silima Juma, (kulia), na aliyekuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, Simai Mohammed Jumamosi usiku Juni 6, 2015 mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar. Mh.  Lowassa, yuko Zanzibar kutafuta wana CCM wa kumdhamini baada ya kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na CCM kuwania urais wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, 2015

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI AKIMWAGA SERA ZAKE WAKATI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UDIWANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

MCC, Makampuni 10 ya Kimarekani yamaliza ziara ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania

$
0
0
Makamu wa Rais wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) Kamran Khan ( wa pili kulia)  akifafanua jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (katikati) na wawakilishi wa makampuni 10 ya Kimarekani, walipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Bw. Khan aliongoza ziara ya wawakilishi hao wa makampuni ya kimarekani, Wizara ya Biashara ya Marekani na MCC ili kuangalia fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini Tanzania.
####################
Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), Wizara ya Biashara ya Marekani na  makampuni 10 ya Kimarekani hivi leo wamemaliza kwa mafanikio mkubwa ziara yao ya kuangalia fursa za biashara na uwekezaji katika sekta ya nishati katika nchi za Tanzania.
Ziara hii ya kwanza na ya aina yake katika historia ya miaka 11 ya MCC, ililenga kukuza mauzo ya nje ya bidhaa zinazozalishwa na makampuni ya Kimarekani na kuongeza uwepo wa makampuni hayo barani Afrika kwa kutambulisha kwayo fursa mbalimbali zilizopo za uwekezaji katika sekta ya nishati. Aidha, ziara hii ililenga kuchangia katika kufikia malengo ya Mpango Maalumu wa Serikali ya Marekani wa Kusaidia Maendeleo ya Sekta ya Nishati barani Afrika uitwao “Power Africa” unaolenga kuongeza mara mbili kiwango cha upatikanaji wa umeme katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara. 
Makampuni haya yalipata fursa ya kukutana na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, pamoja na wawakilishi wa sekta binafsi ya Tanzania na asasi zisizo za kiserikali
Aidha, wajumbe wa ziara hii walikutana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress na Naibu Waziri wa Nishati wa Marekani Christopher A Smith. Aidha wajumbe walipata maelezo kuhusu fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini Tanzania kutoka kwa wawakilishi wa MCC, Wizara ya Biashara ya marekani, Shirika la Marekani la Ushirikiano wa Kimataifa (USAID) na Chama cha Wafanyabiashara wa Kimarekani nchini Tanzania.
“Sekta ya nishati ya Tanzania ipo tayari kwa wawekezaji wan je, tungependa makampuni ya Kimarekani yajionee yenyewe na kusikia kutoka kwa viongozi waandamizi wa nchi hii kuhusu fursa zilizomo nchini humu,” alisema Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Idara ya Usimamizi

WANANCHI WA MKOA WA LINDI WAJITOKEZA KWA WINGI USIKU WA SHAMRA SHAMRA ZA TWENDE NA MEMBE

$
0
0
 Shamra shamra za kutangaza nia ya kuwania urais zaendelea kunoga mjini Lindi ambapo leo June 6 kuamkia June 7, 2015 ambapo Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa anatangaza nia ya Kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2015. Wananchi wamejitokeza kwa wingi huku msanii mzee Yusuph na kikundi cha ngoma ya Deda wakitoa burudani ya kijadi.
Mfalme wa Muziki wa taarabu Mzee Yusup akitoa burudani katika shamra shamra hizi.
Mbunge wa Mchinga Mheshimiwa Said Mtanda (wa pili toka Kushoto) akicheza na wananchi waliojitokeza katika shamra shamra hizo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS WA ZANZIBAR AENDELEA NA ZIARA YAKE NCHINI UJERUMANI

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk.Ali Mohamed Shein na ujumbe wake wakiwa katika Ofisi ya Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg wakati walipotembelea kupata maelezo mbali mbali wakiwa katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitia saini kitabu cha Golden Book katika Ofisi ya Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Mhe,Christian Schuehadt wakati alipotembelea akiwa na ujumbe wake akiwa katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani wakiwepo na Viongozi wengine (kutoka kulia) Mama Mwanamwema Shein, Meya wa Mji wa Wurzburg Mhe, Christian Schuehadt,Balozi Phillip Marmo na Dr.Adolf Bauer, Naibu Meya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Meya wa Mji wa Wurzburg Mhe,Christian Schuehadt (wa pili kulia) a lipokuwa akiangalia Mji wa Zamani ulivyoharibika kwa Mabomu katika Vita vya pili vya Dunia wakati alipotembelea Ofisini kwa Meya akiwa na ujumbe wake (wa pili kushoto) Mama Mwanamwema Shein na Balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe,Philip Marmo akiwapo na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji (kulia).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akifuatana na Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Mhe,Christian Schuehadt baada ya kutembelea katika Ofisi ya Mstahiki Meya akiwa na ujumbe wake katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani (katikati) Mama Mwanamwema Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzui Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mstahiki Meya wa Mji wa Wurzburg Mhe,Christian Schuehadt baada ya kutembelea katika Ofisi ya Meya na ujumbe wake katika ziara ya kikazi nchini Ujerumani.(Picha na Ramadhan Othman.)

NAIBU WAZIRI WA MAILIASILI NA UTALII AFUNGUA MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII YA KILIFAIR 2015

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Moshi Club kwa ajili ya kufungua rasmi maonesho ya kimatifa ya Kitalii yajulikanayo kama KiliFair 2015.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Mohamed Mgimwa akisalimiana na Naibu waziri wa Habari Utamaduni,Utalii na Michezo wa Zanzabar Bi Hindi Khamis walipokutana katika maonesho hayo.
Mgeni rasmi katika maonesho hayo,Naibu waziri wa utalii,Mohamed Mgimwa akiwa katika picha ya pamoja na iongozi wengine akiwemo kaimu mkuu wamkoa wa Kilimanjaro,Dkt Charles Mlingwa,katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Seveline Kahitwa,Mhifadhi mkuu KINAPA,Erastus Rufunguro.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KAMA HUKUBAHATIKA KUMSIKILIZA MH. WASSIRA WAKATI AKITANGAZA NIA YA URAIS, MSIKILIZE HAPA

DK. STEPHEN KEBWE AHITIMISHA KAMPENI YA FISTULA MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe (aliyesimama) akizunguza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Waliokaa kutoka kushoto  ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans, Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, Rutasha Dadi. Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na dhumuni la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi ( aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana.Waliokaa ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Stephen Kebwe (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans.Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wakazi wa manispaa ya Dodoma wakihudhuria kwa wingi kwenye hitimisho la kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula. Ambapo Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe alihitimisha kampeni hizo katika viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi amewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuwa walinzi namba moja dhidi ya wenyetabia ya kuharibu mazingira

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanakuwa walinzi namba moja dhidi ya watu wenyetabia ya kuharibu mazingira katika maeneo yao, kwani kwa kutofanya hivyo ni sawa na kujiuwa wenyewe.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari na mawasiliano ya Halmashauri ya wilaya ya Mufindi Imetanabasha kuwa, mkuu wa wilaya ameyasema hayo kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Vikula Wilayani Mufindi Mkoani Iringa alipomwakilisha mkuu wa Mkoa kama mgeni rasmi.

MHITA amesema endapo wananchi hawata chukua hatua dhidi ya watu wenye tabia ya za kuvuna miti kiholela, ufugaji wa mifugo usiozingatia taratibu za kitaaluma, uchomaji moto ovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji, uwindaji haramu na ukataji mijti ovyo, kunauwezekano mkubwa wa kutoweka kwa misitu na vyanzo vya maji nchini na kuhatarisha ustawi wa mwanadamu.
Aidha, ameyataja madhara yanayotokana na uharibifu wa mazingira kuwa ni pamoja na mbadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa hewa ya ukaa, misitu kuteketea kwa moto, kupungua kwa kiasi cha mvua na majra yake kubadilika kuongezeka kwa joto sanjari na kupungua kwa mavuno mashambani.

Kaulimbiu ya siku ya mazingira mwaka huu inasema ndoto bilioni saba. Dunia moja . Tumia rasilimali kwa uangalifu.

RSA wakisaidia kitengo cha mawasiliano cha usalama barabarani

$
0
0
MABALOZI wa Usalama Barabarani nchini Tanzania (Road Safety Ambasadors-RSA) wamekabidhi misaada kwenye Ofisi ya Kitengo cha Mawasiliano cha Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi nchini (Traffic Control Center-TCC). 

 Vifaa hivyo ambavyo ni vitendea kazi katika kituo cha taarifa cha Kitengo cha Mawasiliano cha Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi nchini, vimekabidhiwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa RSA, John Seka ikiwa ni michango ya mabalozi hao. 

 Akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi, Seka alisema lengo la msaada huo ni wa Mabalozi wa Usalama Barabarani ni kutaka kuboresha mawasiliano ya Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani. 
Juu ni picha mbalimbali za mabalozi wa RSA wakikabidhi vifaa hivyo kwa maofisa wa Kitengo cha Taarifa cha Kikosi cha Usalama Barabarani cha Jeshi la Polisi.
 Alivitaja vifaa vilivyokabidhiwa kuwa ni pamoja na Radio mbili za mawasiliano za kidijitali, Simu ya mawasiliano aina ya Tablet iliyounganishwa na makundi ya RSA ya Facebook, Whatsapp na Telegram, Mtungi wa Maji ya Kunywa, Viti vya kukalia, Feni na Zulia la Ofisi ya TCC. 

 Aidha Seka alitaja msaada mwingine ni Birika la kuchemsha maji ya chai, Mfumo wa kutunza betri kwa ajili ya Tablet (Power Bank) na Gharama za Upakaji wa Rangi wa ofisi ya TCC ikiwa vyote vinalenga kuhakikisha ofisi ya TCC inafanya kazi kwa ufanisi na bila vikwazo ili kurahisisha mawasiliano kati ya RSA na TCC. 

WAZIRI MEMBE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS MKOANI LINDI LEO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwasalimia wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati akitangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati akitangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe na mkewe Dorcas wakilakiwa na wana CCM na wakazi wa Lindi alipowasili katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, kutangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa na bango lenye ujumbe wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (hayupo pichani), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati.

AIRTEL SMARTPHONE BAZAAR ILIVYOBAMBA MLIMANI CITY JIJINI DAR

$
0
0
Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Gulio la Airtel na Huawei Smartphone lililofanyika Mlimani City wikiendi hii. Gulio linalomuwezesha mteja kujishindia zawadi mbali mbali pale anaponunua simu ya Huawei.Gulio hili lilianza Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na litakaloendelea wiki ijayo siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili pale Kibo Complex Tegeta.
Baadhi ya Wateja waliofika katika Gulio la Airtel na Huawei Smartphone wakipewa maelezo kuhusiana na OFA kababe inayotolewa na Kampuni ya simu ya Airtel na Huawei katika banda la Mlimani City jijini Dar Es Salaam .Gulio linalomuwezesha mteja kujishindia zawadi mbali mbali pale anaponunua simu ya Huawei.


LIVE: JANUARY MAKAMBA NA Mwanzo wa Tanzania Mpya

Nyalandu achukua fomu ya kuwania urais wa tanzania mjini dodoma leo

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akionyesha mkoba wenye fomu za kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukabidhiwa katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Pembeni ni mkewe Bi. Faraja Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuchukua fomu za kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Pembeni ni mkewe Faraja.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akipongezwa na baba yake mzazi, Mzee Samuel Nyalandu, baada ya kukabidhiwa fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kukabidhiwa katika Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

MULONGO AZINDUA MASHINDANO YA U13 TAIFA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh Magessa Mulongo leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba amefungua mashindano ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 13.

Akifungua mashindano haya Mh Mulongo amewataka vijana hao kujituma katika michezo na masomo kwa kuwa vyote vinakwenda sambamba.

Amelisisitizia Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kuongeza juhudi katika kuimarisha soka la vijana.

Katika salam zake za utangulizi Rais wa TFF Jamal Malinzi ameeleza kuwa lengo la mashindano haya ni kuibua timu ya vijana wa umri wa miaka 13 ambao watahamishiwa kwenye shule ya Alliance, watakua pamoja hapo kusoma na kufundishwa mpira.
Mpango wa TFF ni kuwa hadi kufikia mwaka 2019 timu hii itakuwa imara kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali za Afrika umri chini ya miaka 17,fainali ambazo zitafanyika Tanzania.

Mikoa yote 25 ya Tanzania bara inashiriki mashindano haya na mkoa wa Dar es salaam umewakilishwa na timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.

TFF inaishukuru Symbion Power kwa ushirikiano wa kuendeleza mpira wa vijana

NB: Picha za uzinduzi zimeambatanishwa

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

DEATH ANNOUNCEMENT

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE ATEMBELEA VISIWA VINNE WILAYANI MULEBA MKOANI KAGERA

$
0
0

 Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana,  akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira, mjini Muleba mkoani Kagera.Ndugu Kinana yuko katika ziara ya siku kumi mkoani Kagera ya kuimarisha na kukagua utekelezwaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010,ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi katika  mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wananchi (hawapo pichani),walipokuwa wakiwasili kwa boti katika kisiwa cha Iroba-Bumbile,wilayani Muleba.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwa mtumbwi katika kijiji cha Katunguru, baada ya kutembelea visiwa zaidi ya vinne, katika wilaya ya Muleba,kulia kwake ni Prof Tibaijuka ambaye ni Mbunge wa jimbo la Muleba kusini,Kinana yuko kwenye ziara ya siku kumi kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, na uhai wa Chama katika wilaya hiyo mkoani Kagera.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasili kwenye Kisiwa cha Iroba-Bumbile wilayani Muleba mkoani kagera.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa  na Mbunge wa jimbo la Muleba Kusini Mh. Profesa Anna Tibaijuka wakijadiliana jambo katika boti wakati wakijiandaa kusafiri kwenda kisiwa cha Iroba-Bumbile,wilayani humo mkoani Kagera.

Sehemu ya umati wa watu wakiwa kwenye mkutano huo wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mjini Muleba mkoani Kagera .

PICHA NA MICHUZI JR-MULEBA-KAGERA.

KUONA PICHA ZAIDI  BOFYA HAPA

au

HAPA

Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images