Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 860 | 861 | (Page 862) | 863 | 864 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa mapema leo katika uwanja wa shule ya msingi Nyakanazi,Wilayani Biharamulo  mkoani Kagera,ambapo pia aliwasalimia wananchi wa kijiji hicho tayari kwa kuanza ziara rasmi mkoni humo.
  Kinana yupo Mkoani humu kwa ziara ya kikazi ya siku kumi ya Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya Chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM waliofika kumsikiliza mapema leo asubuhi,mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho wako ziarani kanda ya ziwa kwa siku 28 za  Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wafuasi wa chama hicho wakikatiza kuelekea kwenye mkutano wa ndani na pia kuzungumza na kundi la Wafugaji
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake akikatika kwenye moja ya soko katika kijiji cha Nyakanazi,Wilayani Buharamulo mkoani Kagera mapema leo asubuhi,akielekea kwenye mkutano wa kupokea taarifa za Chama na serikali pamoja na kuyasikiliza makundi ya Wafugaji kuhusiana na matatizo waliyonayo.

  0 0

  Sasa ni miaka miwili tangu mama yetu kipenzi ulipoitikia sauti ya Mungu hapo tarehe 07.06.2012.

  Sisi kama familia tunatoa shukrani za pekee kwa Mungu kwa jinsi alivyoweza kutulinda na kutupa Faraja ya pekee katika kipindi chote cha majonzi na hadi sasa tunatimiza miaka mitatu bila kuwa nawe. 

  Tunakukumbuka sana mama japo kimwili haupo nasi, pengo lako daima haliwezi kuzibika. Tunakukumbuka kwa upendo wako, ushauri wako kama mama na mke. Kipekee unakumbukwa sana na mume wako mpendwa ACP Kedmond Mnubi, watoto wako Catherine, Restituta, mama ako mpendwa, ndugu, jamaa na marafiki.


  Dua ya kumuombea marehemu itafanyika nyumbani kwake Msamala, Songea tarehe 07.06.2015

  INNALILAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN.

  0 0

  Dr. Kijazi amechaguliwa tarehe 4 June 2015 bila kupingwa wakati wa Mkutano Mkuu wa kumi na saba wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO-Congress wa 17) ulioanza tarehe 25 Mei ambao unatarajiwa kumalizika tarehe 12 Juni, 2015 jijini Geneva, Uswisi.

  Kuchaguliwa kwa Dr. Agnes Kijazi kumetokana na jitihada kubwa za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Ubalozi wetu wa Kudumu Umoja wa Mataifa, Geneva.


  Dr. Kijazi anaongoza ujumbe wa Tanzania katika ushiriki Mkutano huo ambao una washiriki kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Maji na Ubalozi wa Tanzania, Geneva.


  WMO ni Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya hali ya hewa duniani na mabadiliko ya tabia nchi. WMO inatekeleza majukumu na maamuzi kuhusu maendeleo ya sayansi ya hali ya hewa na uboreshaji wake ikiwa ni pamoja na kusimamia viwango katika upimaji na utoaji wa huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama.


  Hadi wakati wa Mkutano huu unaoendelea nchini Uswisi, WMO ilikuwa na nchi wanachama 191. Katika Mkutano huu nchi za Sudani ya Kusini na Tuvalu zilikaribishwa rasmi kama wanachama wapya wa WMO. Kati ya nchi hizi 191 Wanachama wa WMO ni nchi 37 tu ambazo zina wajumbe katika Baraza hilo kuu. Hivyo hii ni nafasi adhimu na heshima kwa Tanzania, TMA na Dr Kijazi ambaye ni msomi mwenye utaalamu wa kutosha akiwa na shahada ya Uzamivu (Ph.D) katika sayansi ya Hali ya hewa.


  Kazi kuu ya Baraza la Utendaji la WMO, ambalo Tanzania imefanikiwa kuwa mjumbe ni kuchukua hatua zinazostahili, kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Shirika hilo kutekeleza maamuzi yanayotolewa na Mkutano Mkuu (WMO-Congress) ambao hukutana mara moja kila baada ya miaka minne.


  Akizungumza baada ya uchaguzi huo Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alielezea sababu ya Tanzania kugombea nafasi hiyo muhimu ni kutaka kuwa ndani ya chombo cha maamuzi na hivyo kushawishi maamuzi yatakayoinufaisha jamii nzima ya kimataifa ikiwemo Tanzania katika masuala ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na kutoa mwelekeo wa kisayansi katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa yanayoendelea maeneo mengi Duniani. Aidha, Dkt. Kijazi alieleza kuridhishwa kwake na jinsi ambavyo nchi wanachama 190 walivyoridhishwa na utendaji wa Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu (2012-2015) ambacho alikuwa mjumbe wa Baraza hili na hivyo kumchagua tena katika kipindi kingine cha miaka minne. “Hii ni heshima kubwa kwa nchi yangu ya Tanzania na ninaahidi kutumia uwezo wangu wote kutekeleza majukumu ya nafasi hii” alisema Dkt. Kijazi.

  Dr. Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), ndiye aliyechaguliwa kuwa mjumbe katika Baraza la Utendaji (Executive Council) la Shirika la Hali ya Hewa Duniani–World Meteorological Organization (WMO) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 2015 hadi 2019.
  Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Jordani mwenye makazi yake mji wa Cairo nchini Misri Mhe. Mohammed Hamza Mohammed akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mfalme Abdallah II wa Jordan.
  Balozi Hamza akimsikiliza Mfalme Abdallah II mara baada ya kumaliza kuwasilisha Hati za Utambulisho.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  WATANZANIA wameendelea kuvichangamkia viwanja vya mkopo vinavyotolewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani.

  Kuchangamkiwa kwa viwanja hivyo kumekuja siku chache baada ya kuzindua huduma mpya ya mikopo ya viwanja hivyo kutoka Bayport, ikiwa ni ishara nzuri na njia ya kuwapa fursa Watanzania ya kumiliki nyumba.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema watu wengi wamekuwa wakituma maombi ya kuomba kupewa viwanja hivyo, tangu huduma hiyo ilipozinduliwa rasmi.

  Alisema kwamba baadhi ya watu walioonyesha nia ya kuvipata viwanja hivyo pamoja na kutuma maombi yao, pia wamekuwa wakitembelea eneo kulipokuwa na viwanja hivyo ili wajiridhishe kwa ajili ya kujipatia viwanja hivyo vinavyokopeshwa kwa minajiri ya kuwakwamua Watanzania, ukizingatia kuwa ardhi inapanda thamani siku hadi siku.

  “Jana (juzi) zaidi ya watu 82 wamekwenda Vikuruti, Kibaha kujionea eneo lenyewe na kuchagua viwanja wapendavyo, ikiwa ni mwendelezo mkubwa wa wananchi wanaotuma maombi ya kukopa viwanja vya Bayport, wakichukua fomu bure z kwa kupitia matawi yetu yaliyoenea nchi nzima, bila kusahau kwenye matawi ya Bank of Afrika (BOA).

  “Huduma hii ni murua kwa Watanzania wote, tukiamini kuwa ni sehemu ya kuwapatia wananchi urahisi wa kumiliki vitu vyenye thamani ikiwamo ardhi wanayoweza kuitumia kwa mambo mengi, ikiwa nyumba za kuishi na za biashara, huku thamani ya viwanja vikianzia Sh 1,400,000 na kuendelea kwa viwanja vyenye ukubwa tofauti vya kujenga nyumba za kuishi na biashara kama vile shule, vituo vya afya, nyumba za kulala wageni na hoteli,” alisema Cheyo.

  Cheyo alisema nafasi ni chache, maana maombi yanafanyika kwa siku (20), kuanzia Mei 22 hadi Juni 10, huku fomu za maombi zikipatikana katika matawi yao yote ya Bayport Financial Services na matawi ya bank of Africa (BOA), ambapo malipo ya awali yakianzia Sh 150,000 na yatakuwa yakilipwa kwa akaunti yao ya Bayport iliyopo BOA.

  Kwa mujibu wa Cheyo, fomu ya maombi na nakala ya malipo ya awali yarejeshwe katika matawi BOA au ofisi za taasisi ya Bayport zilizoenea nchi nzima na baada ya Juni 10, mteja atatakiwa kulipia kiwanja kwa fedha taslimu au mkopo kutoka kwenye taasisi yao huku watumishi wa umma na wa kampuni binafsi wakiweza kukopeshwa kiwanja na kukabidhiwa hati miliki ndani ya siku (90) watakapokamilisha mkopo wao.

  Hawa ni miongoni mwa Watanzania waliohamasika kutembelea katika viwanja vilivyokuwa kwenye mradi wa Vikuruti kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Kibaha, mkoani Pwani, ambavyo vinatolewa kwa wananchi kwa mkopo. Wakopaji ni watumishi wa umma, kampuni binafsi na wajasiriamali.
  Eneo la viwanja vya Vikuruti vinavyoonekana huku barabara ikionekana pichani.

  0 0

  Mkuu wa mkoawa Kilimanjaro Leonidas Gama akisalimiana na baadhi ya wananchi wakati alipowasili katika shule ya Sekondari Kishumundu kwa ajili ya hafla fupi ya makabidhiano jengo la Bweni la wasichana lilojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania ,(TANAPA).
  Viongozi mbalimbali walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kishumundu wakiimba wimbo wa Tanzania wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la Bweni la wasichana lilojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA.


  Wafadhili wa shule ya Sekondari Kishumundu iliyopo wilaya ya Moshi wakisalimia mara baada ya kutambulishwa katika hafla hiyo.


  Wanafunzi wa Shule ya sekondari Kishumundu wakitoa burudani ya nyimbo mbele ya wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya makabidhiano ya jengo la Bweni la Wasichana lililojengwa ufadhili wa TANAPA.


  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza wakati wa makabidhiano ya mradi wa jengo la Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kishumundu,ujenzi uliofadhiliwa na Hifadhi za Taifa,Tanzania ,TANAPA.
  Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari ya Kishumundu lilojengwa na TANAPA.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akizindua rasmi Bweni la wasichana katika shue ya sekondari Kishumundu.
  RC,Gama akikata utepe kufungua jengo la Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Kishumundu wilayani Moshi.
  Sehemu ya ndani ya Bweni la wasichana katika shule ya sekondari Kishumundu,Jengo lililojengwa kwa ufadhili wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  Mbunge  wa  Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  akizungumza na   baadhi ya  wananchi  wa kijiji  cha Luana waliojitokeza kuungana nae katika maendeleo ya  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara yenye urefu wa km 2  aliyowachongea
  Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe  akielekea  kujumuika na  wananchi wake wa  kijiji  cha Luana  kuchimba mifereji ya kutolea maji katika barabara ya kijiji  cha Luana ambayo ameshirikiana na  wananchi hao kuichonga
  Wananchi  wa Luana  wakielekea kazini pamoja na mbunge  wao

  Wananchi  wa Luana  wakiwajibika kuchimba barabara

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi yake, Dkt. Julius Ningu, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa tatu katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utunzaji wa nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Lupi Mwaikambo, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga leo

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoa huduma wa dawa za asili, Karunde Amadi, wakati alipotembelea kwenye banda wafanyabiashara za dawa asili, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga  leo .
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi zawadi ya Pikipiki kwa mmoja kati ya washindi.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Filamu ya Mamba wa Zigi, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Kushoto kwake ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu. Picha na OMR

  0 0  0 0


  0 0  0 0

  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Michezo cha Watu wenye ulemavu wa Akili Zanzibar Bibi Saada Hamad Ali akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Medali 32 walizopata wachezaji wa Zanzibar katika mashindano ya Kitaifa Mkoani Kibaha.
  Balozi Seif akimvisha Medali Mchezaji Fahad Juma Khamis ambae alishinda kwenye mashindano ya Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Pwani Tanzania Bara.
  Mchezaji Huzaima Haji Ali wa Timu ya Mchezo wa Watu wenye ulemavu wa Akili Zanzibar akivishwa Medali na Balozi Seif baada ya kushinda mashindano ya Kibaha Tanzania Bara.


  0 0

  wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa wakubwa wa mazingira, waliadhimisha siku hii asubuhi ya leo kwa kufanya usafi barabara ya Ohio kuzunguka mpaka ufukwe wa bahari ya Hindi.

  Akiongea  mara baada ya zoezi hilo la usafi mkurugenzi mkuu wa masoko wa hoteli hiyo ndugu Seraphin Lusala aliwashukuru wafanyakazi wa hoteli hiyo kwa kushiriki katika zoezi hilo la kufanya usafi wa mazingira ili kuonyesha mfano kwa jamii kwamba uchafuzi wa mazingira haukubaliki na kuwataka wafanyakazi wa hoteli hiyo kuwa mfano hata huko wanapoishi kwa kutokutupa taka hovyo na kuwaelimisha wale wanaotupa taka hovyo na kuchafua mazingira kuacha tabia hiyo ili kufanya mazingira yetu na jiji letu kuwa safi.
   wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa wakubwa wa mazingira wakiendelea na zoezi la usafi kando ya barabara ya Ocean Road, jijini Dar katika kuadhimisha siku ya Mazingira.
  wafanyakazi wa Hoteli ya Dar es Salaam Serena ambao ni wakereketwa wakubwa wa mazingira wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akitoa malalamiko ya wafugaji kwa ukatili wanaofanyiwa na askari wa wanyamapori katika mapori mbalimbali ya hifadhi kanda ya ziwa.

  Mwenyekiti huyo alisema kuwa wafugaji wamekuwa wakifunga safari kwenda mkoani Dodoma kwa ajili ya kuonana na mawaziri wahusika akiwemo, Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk.Titus Kamani , aliyekuwa Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na Waziri Mkuu Pinda.

  Pia alisema wamefanya vikao kati yao na wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori lakini hakuna kilichoifanikiwa zaidi ya kupewa tarehe ya kwamba ufumbuzi utapatikana.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma taarifa ya vikao 17 vilivyofanyika kati ya Wafugaji hao (pichani)  na viongozi mbalimbali  wa Serikali,kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa mgogolo wao dhidi ya Askari wanyama pori lakini hakuna maamuzi ama suluhisho lililopatikana.Kinana amekutana na wafugaji hao mapema leo katika kijiji cha Nyakanazi wilayani Biharamulo na kutoa kero zao kwake juu ya manyanyaso wanayofanyiwa na askari wa wanyamapori.

  Alisema kuna mambo mawili yamemsikitisha, moja watu kutumia mwamvuli wa sheria kufanya mambo yao binafsi kwani hakuna Serikali inayoweza kutumbukiza ng'ombe kwenye shimo.

  "Wizi ,rushwa ndicho kinachoonekana ndani yake, kwa maelezo yenu kuna baadhi ya watendaji wameamua kuchukua sheria mkononi mwao.Wanachukua milioni 10 za mfugaji na kisha zinakwenda kwenye mifuko yao,"alisema.

  Alisema lazima akiri, Serikali nayo imelegea mno katika kuchukua maamuzi, kwani amehesabu vikao ambavyo wafugaji wamekaa na viongozi wa ngazi mbalimbali za juu serikali vipatavyo 17 lakini hakuna ufumbuzi na badala yake ni maneno, maneno tu.

  Alisema kama wameshindwa kutatua matatizo ya watu ni vema wakaa kando maana mishahara wanalipwa na marupurupu wanapewa lakini kushughukulikia matatizo ya watu imekuwa ngumu.

  "Watu wameuawa, ng'ombe wamekufa, ng'ombe wameporwa.Hii haiwezekani na kwamba matatizo yote yanayohusu wanyamapori wenye mamlaka ni Wizara ya Maliasili na Utalii.

  "Niombe mambo mawili yafanyike, ng'ombe waliokamatwa warudishwe kwa wafugaji na pili kesi zilizopo mahakamani zifutwe na wenye mamlaka ya kuzifuta ni Serikali maana ndio waliofungua kesi,"alisema Kinana.
  Baadhi ya wafugaji wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungumza nao katika kijiji cha Nyakanazi Wilayani Biharamulo mkoani Kagera.Kwa mujibu wa wafugaji hao wameeleza kuwa wilaya zote zilizopo Mkoa wa Kagera na hasa Wilaya ya Ngara , wafugaji wamekuwa wakipata mateso makubwa pindi mifugo yao inapokamatwa kwenye pori la Kimisi ambapo ng'ombe wamekuwa wakipigwa risasi na wengine kuingizwa kwenye shimo refu lenye tope linalojulikana kwa jina la Gwantanamo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Kanda ya Ziwa Bwa.Mugisha Murshad wakati alipokuwa akimuonyesha eneo linalotumika kuhifadhi mifugo yao mara inapokamatwa na kuwa eneo hilo ni dogo na halina chakula cha mifugo wala maji jambo ambalo hupelekea mifugo kufa kwa wingi.
  Mmoja wa wafugaji akimuonesha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana eneo ambalo mifugo inayokamatwa hupelekwa hapo na kuwekwa kwa muda mrefu bila maji wala chakula na matokeo yake mifugo hufa,iwapo mwenye mifugo hiyo hakwenda kuikomboa kwa gharama itakayokuwa imetajwa,ambayo wafugaji hao wamekuwa wakiilamimikia 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akioneshwa eneo ambalo mifugo ya Wafugaji ilikuwa ikikusanywa eneo hilo na kuacha kwa muda mrefu bila chakula wala maji na hatimae kupoteza uhai,jambo ambalo wafugaji hao wameona ni kitendo cha uonevu na unyanyasaji mkubwa,kwani kwa kukamatwa mifugo yao wamekuwa wakitozwa fedha nyingi kuikomboa mifugo yao,hivyo wameomba Ndugu Kinana kusikiliza kilio chao cha mda mrefu. MICHUZI JR-KAGERA.

  0 0


  0 0

  1
  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.
  4
  Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Diyosisi ya Kasikazini akiweka akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.
  6
  Gadi Maalum ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa katika Gwaride la mazishi yake.
  9
  Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiimba wimbo kwenye Ibada Maalum ya kumuombea kheri Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa baada ya shughuli za mazishi kukamilika(kulia) ni Mchungaji Frank Machanga kutoka Jimbo la Kasikazini(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Mwenyekiti wa taasisi ya ACCT,Milton Nyerere(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Richard Masika wakibadishana hati za makubaliano ambayo itatoa fursa kwa mafundi wengi kunolewa na kuweza kufanya kazi za ujenzi kwa ubora wa hali ya juu.
  Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Masika akizungumza katika hafla ya kusaini makubaliano ya kushirikiana na Assocition of Citizen Contractors Tanzania(ACCT)leo chuoni hapo,kushoto ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo,Milton Nyerere.Taasisi hiyo itatoa mafunzo kwa mafundi mchundo na mafundi Sanifu ili kuwawezesha Makandarasi Wazalendo kuhimili ushindani dhidi ya Makampuni ya kigeni.
  Katibu Mtendaji wa Umoja wa Makandarasi Wazalendo(ACCT)Angela Joseph akizunguza wakati wa hafla hiyo.
  Makamu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)Dk Mgaya akizungumza jambo juu ya kuwawezesha Mafundi Mchundo na Mafundi Sanifu kufanya kazi kwa ubora.Mafunzo yatatolewa katika chuo hicho.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa nyumbani kwake kwa marehemu Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.Marehemu Luangisa ni miongoni  mwa Waasisi wa Taifa na katika vipindi tofauti tofauti alikuwa mkuu wa Mkoa wa Ziwa Magharibi (Kagera),Mbunge na Meya wa Manispaa ya Bukoba pamoja na nyadhifa nyingine.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Jaji Mstaafu Samuel Luangisa mapema leo asubuhi nyumbani kwake kwa Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.
  Katibu Mkuu Ndugu Kinana na baadhi ya maofisa wa chama na ndugu na jamaa wa marehemu wakishiriki sala ya pamoja na kumuombea marehemu Mzee Samuel Luangisa nyumbani kwake Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera
  Katibu Mkuu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo ya Marehemu Mh. Samuel Luangisa nyumbani kwake mapema leo asubuhi,Kitendagulo,mjini Bukoba mkoani Kagera.

  PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA.


  0 0

  The Government of Japan has been extending support to local communities in various sectors including health, education and water supply under the Grant Assistance for Grassroots Human Security Projects (GGHSP) scheme since 1991.

  On 5th June, 2015, the handing-over ceremony for “The Project for Reconstruction of a Two-storey Classroom Block at Michakaini „A‟ Primary School in Chakechake Town, South Pemba Region (JFY2013)” was held at Michakaini A Primary School.

  The Government of Japan, in response to the request Embassy of Japan Dar es Salaam 6th March, 2014 by the Parents Committee of Michakaini A Primary School, extended a grant aid of US Dollars 159,037 the project in the Japanese Fiscal Year 2013, under the GGHSP scheme.
  Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida posing with from left Chaiman of Parent Committee of Michakaini Primary School, Mr. Nassor HArith Mohammed, Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, Headteacher Ms. Neema Mwalim Khamis, Secretary of the Committee and Head Teacher, in front of the newly constructed classroom block.
  Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Prof. Ibrahim Lipumba, CUF Chairman, posing with Michakaini primary school pupils in front of the newly constructed classroom block.
  Ambassador of Japan H.E. Mr. Masaharu Yoshida with Hon. Ms. Mwanajuma Majjid Abdallah - South Pemba Regional Commissioner, during the Handing over ceremony.


  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.

  Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS  maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa  HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31, Mfanyabiashara, Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10. Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa, wanajihusisha na unalifu wa kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha baadhi ya waandishi wa habari (hawapo pichan) Bunduki aina ya (SMG) iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10.
  Katika tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko maeneo ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya kuwakurupua vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.

  Hii ni kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa taslim TSHS. 300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Kawe na ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.
  Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha risasi zilizokamatwa katika oparesheni hiyo.

older | 1 | .... | 860 | 861 | (Page 862) | 863 | 864 | .... | 3283 | newer