Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 859 | 860 | (Page 861) | 862 | 863 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc ("swala" au "Kampuni") inayo furaha kutangaza kwamba imefikia makubaliano ya kugawana umiliki na Kampuni ya Tata Petrodyne Limited ("TPL"), kampuni ambayo ni sehemu ya Kampuni ya Kimataifa ya Tata sons Limited, ambapo TPL itakuwa ikifanya shughuli zake kwenye maeneo ya leseni ya Pangani na Kilosa-Kilombero nchini Tanzania. Hii itaiwezesha Kampuni ya swala kubaki kwenye maeneo yake ya leseni na ili kupata fedha kwa ajili ya shughuli za utafutaji hapo baadaye katika njia ambayo itapunguza hasara kwa wanahisa wake wa sasa.

  Kampuni ya Tata Sons Limited ni Mratibu wa uendeshaji wa shughuli kubwa za makampuni ya Tata na kumiliki hisa zote muhimu kwenye makampuni haya, na kwa kawaida inajulikana kama kundi la Tata (Tata Group). Kundi la Tata lina mtaji wa soko wa takribani dola za Kimarekani bilioni 110 na inawakilisha zaidi ya asilimia 8 ya jumla ya mtaji wa soko katika soko la hisa la Bombay.

  Katika sekta ya mafuta na gesi, makubaliano ya kugawiana umiliki ni makubaliano yaliyoingiwa kwa mmiliki wa leseni moja au zaidi (anayegawa umiliki huo) na kampuni nyingine ambayo inataka kupata asilimia ya umiliki wa leseni hiyo kwa ajili ya kutoa huduma (na 'kujimilikisha). Makubaliano ya kugawana umiliki yanatofautiana na shughuli za kawaida kati ya wakodishaji wawili wa mafuta na gesi, kwa sababu cha msingi kuzingatia ni utoaji wa huduma, badala ya ubadilishaji rahisi wa fedha.


  0 0

    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzomna Spika wa Bunge la nchi ya Finland Mhe Maria Lohela siku alipotembelea bunge la nchi hiyo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifanya mahojiano na wanahabari jijini Helsinki, Finland.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonganisha glasi na Mari Kiviniemi, Waziri wa Masuala ya Nje wa Finland wakati wa dhifa iliyoandaliwa kwa hashima yake jijini Helsinki
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mabalozi wa sasa na wa zamani waliopata kuiwakilisha Finland nchini Tanzania
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Finlan
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyabiashara wa Finland pamoja na washirika wao wa Tanzania baada ya mkutano wao jijini Helsinki, Finland
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo alipotembelea kiwanda cha METSO cha  kutengenezea vipuli vya mitambo ya gesi na mafuta katika jiji la Helsinki, Finland.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya mchoro kutoka kwa Msanii wa Kimataifa wa Kitanzania aishiye Sweden Bw. Charles Njau alipomutana na  Watanzania waishio Sweden alipokutana nao Alhamisi jijini Stockholm
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mtaalamu wa kimataifa wa mambo ya mapishi aishiye Sweden Chef Issa Kipande ambaye mwaka jana alikuwa katika tiu ya taifa ya Sweden kwenye mashindano ya kombe la dunia la mapishi walikoibuka na medali ya dhahabu. Chef Issa, ambaye pia anaedeesha hoteli Mtwara, hivi karibuni amefungua mgahawa mkubwa mkubwa kuliko yote wa Ki Afrika katika Ulaya yote mjini Trolhattan, nje kidogo ya jiji la Stockholm, wenye uwezo wa kuchukua watu 400 kwa wakati mmoja
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio nchii Sweden jijini Helsinki
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake akilakiwa na Mfalme Carl Gustav wa 16 wa Sweden katika kasri la Mfalme jijini Stockholm, Sweden
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi mkuu wa SIDA Bw. Torbjorn Petterson makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wafanyakazi wa SIDA  katika makao makuu ya shirika hilo la maendeleo la Sweden jijini Stockholm

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Spika wa Bunge la Sweden Mhe Urban Ahlin alipotembelea Bunge la nchi hiyo jijini Stockholm

  0 0

                             Othman Khamis Ame,Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
  Maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Msingi ya Jamii katika kijiji cha Kiwengwa Kiliomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “ B “ yanaendelea vyema katika hatua za mwisho zitakazoiwezesha skuli hiyo kuanza kuchukuwa wanafunzi wa Elimu ya maandalizi kuanzia mwezi Januari Mwaka ujao wa 2016.

  Ujenzi wa skuli hiyo uliohusisha pia vyoo na Tangi la Kuhifadhia maji ambavyo vinajengwa kwa kutumia Taaluma ya Chupa za Maji  zilizotiwa mchanga unafadhiliwa na Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Nchini Marekani.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Skuli hiyo Bwana Tahir Ali alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyepeta fursa ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo kwamba Kamati hiyo kwa kushirikiana na Wananchi kupitia ushauri wa Wizara husika ya Elimu wanatarajia kuanza usomeshaji mapema mwakani kwa hatua ya watoto wa maandalizi.

  Bwana Tahir alisema juhudi za Wanakijiji kwa kuungwa Mkono na Shirika la Kimataifa la Give la Marekani zimelenga kuwakomboa Watoto wa Kijiji hicho ambao kwa muda mrefu walikuwa wakikosa fursa muhimu za kielimu.

  Naye Meneja Mpya wa Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Marekani Bwana Joshi Winter alisema Uongozi wa Mradi huo umejipanga vyema katika kuhakikisha ujenzi wa Skuli hiyo unakamilika vizuri na kutoa fursa kwa watoto wa Kijiji hicho kupata Elimu.

  Meneja wa Mradi huo wa Give ameuomba Uongozi wa Kijiji hicho kwa kushirikiana na Serikali Kuu kuandaa mazingira ya kupata eneo kubwa zaidi kwa ajili ya matayarisho ya ujenzi wa Majengo ya Sekondari katika Skuli hiyo ya Jamii Kiwengwa ambapo Taasisi yake itakuwa tayari kusaidia ufadhili.

  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Taasisi hiyo ya Kimataifa inafaa kupongezwa na wapenda Elimu hapa Nchini kutokana na hatua yake ya kuunga mkono makundi ya jamii katika kujikomboa kielimu.

  Balozi Seif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini juhudi za taasisi na mashirika ya maendeleo ndani na nje ya nchi yaliyojitolea kusaidia Wananchi hasa wanaoishi katika mazingira magumu ya kimaisha ambayo huwa kikwazo cha kupata elimu.

  Taaluma ya matumizi ya chupa za Maji zinazotiwa mchanga iliyobuniwa Nchini Nicaragua Amerika Ya Kusini katika ujenzi wa majengo mbali mbali ya makazi na huduma za Kijamii inatumika kwa lengo la kutunza  mazingira.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akikagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya Jamii katika Kijiji cha Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Skuli hiyo Bwana Tahir Ali, Kulia yake Balozi Seif  ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi ambapo nyuma yao ni jengo la Vyoo lililojengwa kwa kutumia chupa za maji zilizotiwa mchanga.
   Balozi Seif Ali Iddi wa kwanza kulia akimpongeza Meneja wa Mradi wa Kimataifa wa Give kutoka Nchini Marekani Bwana Josh Winter kutokana na Taasisi yake kusaidia maendeleo ya Elimu Zanzibar.Picha na –OMPR – ZNZ.

  0 0  Kampuni ya matangazo ya FLAMETREE iliyojikita Africa mashariki sasa imezinduliwa upya na kupewa jina jipya la RIGHT HERE TANZANIA, mabadiliko haya yametokana na kuingia kwa mwekezaji mpya wa kimataifa ambaye ameonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwenye kampuni hii kufuatia utendaji mzuri aliouona kwenye kampuni hiyo na kuamua kuongeza nguvu zaidi katika kuinua utendaji, uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao. Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya RIGHT HERE itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.

  RIGHT HERE imechaguliwa kuwa mwakilishi kwa Tanzania wa kampuni kubwa ya matan- gazo ya PUBLICIS ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa manne duniani kama WPP, Interpublic na Omnicom.

  Akizindua jina hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana Gerald Govaerts amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka mitatu.

  Gerald aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya. 

  ”Kufuatia uwekezaji huu mpya na ubia kwa kampuni ya kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.

  Kampuni ya RIGHT HERE inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyomba vya habari,kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.

  “Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya RIGHT HERE” alisema Bi Jenny Woodier, meneja mkuu wa RIGHT HERE Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kuwa wawakilishi wa kampuni kubwa yenye nia ya kuwekeza hapa Tanzania kwa hapo baadaye. Ubia huu na kampuni ya Publicis Africa Group utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama RIGHT HERE kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.

  Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa. Mpaka sasa tumeweza kushinda tuzo mbali mbali za kimataifa.

  Bi Jenny aliendeela kusema “ Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka mitatu na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya RIGHT HERE sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.

  KUHUSU KAMPUNI YA RIGHT HERE.
  Jina la RIGHT HERE linatoa maana halisi ya jinsi sisi tunavyofanya kazi kwa kuangalia walengwa wanataka nini na kufahamu umuhimu wao, lakini pia kama unatafuta mdau mwenye ujuzi na mwenye viwango vya kimataifa, watanzania wenye ubunifu na wanaoendana na hali ya soko, suluhisho pekee ni “RIGHT HERE”
  Mshauri mkuu wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA, Gerard Govaeas akizungumza na baadhi ya waandihsi wa habari katika Ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo\, Kushoto ni Mkuu wa Hati Miliki wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA,Asnath Heriel na kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa RIGHT HERE TANZANIA Jenny Woodier.
  Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhurika katika mkutano wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA mkutano uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Wakazi wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Zipporah Pangani, alipokuwa akiwaelewesha juu ya maradhi ya Fistula wakati wa kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi hayo wilayani humo.Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu akina mama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
  Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Mh.Zipporah Pangani( katikati) akimsikiliza kwa makini Mwajuma Rashid wakati alipokuwa akiwasomea moja ya kipeperushi kuhusiana na ugonjwa wa Fistula.,Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakina mama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
  Wanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya Igunga Mkoani Tabora,Asha Omari (kushoto) na Fatma Juma wakisoma kipeperushi walichogawiwa wakati wa kampeni ya maradhi ya Fistula iliyofanyika mkoani humo,Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu ya hapa nchini na akina mama wenye maradhi hayo wanahimizwa kujitokeza wakatibiwe. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.


  0 0

   Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Bw.Frederick Sumaye alitinga katika ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi mkoani Dodoma kuchukua fomu za mbio za urais 2015 akiwa ameongozana na mke wake Mama Esther Sumaye. Hapa akiweka saini mbele ya Katibu wa Oganaizesheni wa CCM , Dk Mohamed Seif Khatib
   Mhe Sumaye akionesha fomu baada ya kukabidhiwa
   Mhe Sumaye akionesha mkoba uliobeba fomu baada ya kukabidhiwa. Pembeni ni mkewe Mama Esther Sumaye
  Mhe Sumaye akiaga baada ya kuchukua fomu

  0 0

  Mfalme wa Masauti Bongo, Christian Bella ‘Obama’ akiwa ndani ya Global TV Online.
  Christian Bella akiimba wimbo wake mpya wa 'Nashindwa' ndani ya studio za Global TV Online leo.
  Malaika Band chini ya uongozi wa Christian Bella katika moja ya shoo yao, Dar Live patakuwa hapatoshi Jumamosi hii. Mfalme wa Masauti akiimba.

  MFALME wa Masauti asiye na mpinzani Bongo, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuutambulisha Usiku wa Nashindwa, Juni 6, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
  Akizungumza na mtandao huu, Bella ambaye ni kiongozi wa Bendi ya Malaika Music alisema kuwa kuanzia saa mbili usiku wa Jumamosi utakuwa wa aina yake kutokana na walivyojiandaa na bendi yake.
  Staili mpya
  Bella aliwataka mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi kwani mbali na kuzindua wimbo huo, mashabiki watapata burudani ya kuoneshwa staili zao mpya.
  “Bella na Malaika tumewaandalia staili tatu mpya na za kitofauti ambazo kila mmoja atazipenda na kuzicheza kwani tutazizindua kwa mara ya kwanza,” alisema Bella.
  Sapraiz kumiminika
  Bella aliongeza kuwa yeye pamoja na Malaika Music wameaandalia sapraiz kibao kwa wakazi wote wa Mbagala, Temeke na pande zote jijini Dar watakaojitokeza.
  “Mara ya mwisho kupiga shoo Dar Live ilikuwa ni Usiku wa Wapendanao ‘Valentine’s Day’ na usiku ule ulikuwa maalum kwa kina mama wote nakumbuka niliwaita mashabiki wote jukwaani na kuimba nao Wimbo wa Nani Kama Mama, walifurahi sana.
  “Niwaambie safari hii ni ya kitofauti kwani nakuja na Nashindwa hivyo mashabiki wote kila mmoja nitapanda naye jukwaani na kuimba naye Wimbo wa Nashindwa.”
  Ladha ndani ya ladha
  Ukiachana na wimbo wa Nashindwa usiku huo Bella alisema utakuwa wa ladha ndani ya ladha kwani kwa mara ya kwanza atawaonjesha wimbo mwingine mpya.
  “Kuna wimbo mpya ambao nimefanya na msanii mkubwa wa kimataifa na siku hiyo mbali ya kuburudika na Wimbo wa Nashindwa pia nitawaonjesha kipande cha wimbo huo.”
  Burudani mwanzo mwisho
  Kuhakikisha burudani haikauki, kwa wale mashabiki 500 wataofika wa kwanza ndani ya Dar Live watapata bahati ya kupiga picha ‘red carpet’ na Bella sambamba na kuzungumza naye machache.
  “Hakuna msanii ambaye amewahi kufanya hivi kama nilivyofanya Valentine’s Day na safari hii natoa nafasi hii kwa mashabiki wote watakaofika mapema.”
  Mashabiki pia watarajie kupata nyimbo mpya kutoka kwa Malaika Music pamoja na nyimbo nyingine zote kali kutoka kwa Bella kama vile Nani Kama Mama, Msaliti, Nakuhitaji na nyingine nyingi.

  0 0


  0 0

  Irina_Bokova

  Director-General of UNESCO. Irina Bokova.

  Seven Billion Dreams. One Planet. Consume with Care.
  We live in a world transforming deeply, rocked by multiple crises, on a planet facing rising pressure.

  Environmental change has never been so deeply interconnected with our societies as it is today, in this era that many scientists call the Anthropocene, when human activity is the major force shaping the planetary system. The impact that individual women and men are having on the sustainability of the planet may not always be visible -- but consider the impact of seven billion women and men, and it becomes clear that daily choices matter.

  Environmental change is not just about carbon – it is, fundamentally, about women and men, it is about how we produce and consume in society. The environment is intertwined with human values and behaviour, directly linked to our livelihoods, urban development and nature conservation as well as migration patterns, affecting also the use of water and land, impacting on species survival.

  Sustainability cannot be crafted through technological or economic solutions alone. We need green societies to build green economies. We must act in a holistic manner, across the board, starting with individual women and men. 

  This year, the international community has an historic opportunity to adopt a new sustainable development agenda and to reach a global agreement on climate change. UNESCO is bringing the full force of its mandate and experience to make both a success. 

  We are promoting education for sustainable development to shape the new values, skills and knowledge that all societies need today. Sustainability will be built on the benches of schools, starting as early as possible. We work also to harness the power of science, technology and innovation to strengthen knowledge, to safeguard biodiversity through Biosphere Reserves, and to strengthen the links between the sciences and policy.

  This is one goal of the Scientific Advisory Board, an initiative of the United Nations Secretary General for which UNESCO is the Secretariat, to craft a new unity among all sciences and catalyze new synergies across disciplines, policy lines and borders, including to inform the 21st Session of the Conference of the Parties to the UN Framework Convention on Climate Change (COP21) that will be held in Paris later this year.

  There is strong global momentum – we need to act on this promise and make a new one, for development that is sustainable, in harmony with the planet. This responsibility cannot wait -- we must act now.

  0 0

  Q-Chilla baada ya kuwa kimya kwa Muda Mrefu na Pia mambo yake Kubadilika, Sasa amerudi tena katika Muziki na Safarii hii ameamua kufanya kazi yaani Muziki Biashara, Akizungumza wakati wa kupreview video yake Mpya ya For U amesema kuwa kwa sasa amerudi rasmi katika Muziki na Amebadilika Tofauti na Mwanzoni alivyokuwa pia ametoa Shukran Nyingi sana kwa QS ambaye anasimamia kazi zake za kimuziki kwa sasa, Video ya For You imefenywa na Director Adam Juma Nchini Afrika ya Kusini, Kwa Upande wa Adam amesema kuwa Video hii ameifanya kwa mapenzi na ameomba wasanii kuthamini vitu vyao vya nyumbani na ameahidi kufanya kazi na msanii yeyote ambaye atakuwa tayari kikubwa kazi iwe nzuri. by www.harakatizabongo.com Angalia video hii ya Q Chilla For You au MdogoMdogo kisha kama unacomment yeyote unaweza kuacha hapo chini....
  d

  0 0

  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katikati akionyesha kabrasha lenye Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mara baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu mkoani Dodoma leo.
  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu kabla ya kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma.
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu kushoto akimkabidhi fomu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
  Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mbunge wa Chato Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya fomu aliyokabidhiwa leo.

  0 0


  0 0
 • 06/05/15--00:00: DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

 • 0 0

  Millicom signs agreement to acquire Zanzibar Telecom

  Stockholm, June 5, 2015 – Millicom (Stockholmsbörsen: MIC), today announced that it has signed a Share Purchase Agreement to acquire an 85% stake in Zanzibar Telecom (Zantel) from Etisalat Group.


  Zantel is the leading mobile telecom operator on the islands of Zanzibar with 2014 gross revenues of $82 million and 1.7 million subscribers across Zanzibar and mainland Tanzania. It operates 2G and 3G services over 545 network sites, with 57MHz of spectrum[1]and has ownership rights to undersea fibre optic cable capacity.

    Zantel has an approximate 5%share of the Tanzania mobile market[2].   Millicom intends to retain and continue to operate the Zantel brand, while delivering cash flow growth by leveraging technical and operational efficiencies.

  Under the terms of the agreement Millicom will pay the total cash consideration of $1 dollar and assume total debt obligations of $74 million.  In addition Zantel will have up to $32 million in net current liabilities at closing.  Millicom expects the EBITDA of Zantel to reach $25 million through a combination of bringing new products and services to the existing customer base and delivering greater efficiencies. The agreement allows for an adjustment to the total consideration if that target is not reached by the end of 2019.

  Millicom has arranged with a leading international bank, the provision of a $100 million 5-year credit facility for Zantel.


  The Government of Zanzibar will continue to own the remaining 15% of the shares in Zantel. Millicom is looking forward to working with the Government of Zanzibar as a partner and as a shareholder to continue to develop the exciting opportunities for Zantel and its customers.


  Tanzania is Millicom’s biggest market in Africa and the acquisition of Zantel is a natural fit for Millicom’s strategy, strengthening our overall position in Tanzania and delivering further growth prospects for the Group:


  • further leveraging the brand power of Zantel

  • delivering technical synergies including procurement and national roaming

  • improving network service quality and coverage

  • capitalising on the growing demand for mobile data and roll out of 4G coverage

  • accessing further bandwidth capacity via the undersea fibre optic cable EASSy

  • sharing Millicom best practice such as expanding its Mobile Financial Services in Zanzibar to support financial inclusion
  The transaction remains subject to regulatory approval by the Tanzanian Communications Regulatory Authority and the Fair Competition Commission.


  Ends

  Press Enquiries

  Tabitha Aldrich-Smith, Interim Communications Director

  Tel: +44 7971 919610/ press@millicom.com


  Investor Relations

  Nicolas Didio, Director, Head of Investor Relations

  Tel: +352 277 59125 (Luxembourg) / +44 203 249 2220 / investors@millicom.com


  About Millicom

  Millicom is a leading telecommunications and media company dedicated to emerging markets in Latin America and Africa. Millicom sets the pace when it comes to providing innovative and customer-centric digital lifestyle services to the world’s emerging markets. The Millicom Group employs more than 16,000 people and provides mobile, cable and satellite services to over 56 million customers. Founded in 1990, Millicom International Cellular SA is listed on NASDAQ OMX Stockholm under the symbol MIC. In 2014, Millicom generated revenue of $6.4 billion and EBITDA of $2.1 billion.


  During its Q1 results in April, Millicom announced that its Africa operations delivered a revenue growth of 16%, up from 13% in the last quarter. In Tanzania Millicom reported strong customer growth in mobile (+508,000) delivering revenue growth of 18% to $92 million with an EBITDA margin of 36%. LTE has also recently begun roll out in Tanzania. Following this transaction, Millicom will reinforce its market position in Tanzania.


  About Zantel

  Zantel (Zanzibar Telecom) is the leading data telecommunications brand in Zanzibar and its largest internet provider. Its integrated telecom service provide International Gateway services, Fixed, Mobile and data services through its CDMA, GSM, 3G networks.


  [1]Zantel has 850MHz, 900MHz, 1800MHz and 2100MHz spectrum for Zanzibar and mainland Tanzania

  [2]Source: Tanzania Communications Regulatory Authority, December 2014


  0 0

   AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF 
  ABDUL NJAIDI AKITOA HOTUBA WAKATI WA UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII, ILIYOANZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM). UZINDUZI HUO ULIDHAMINIWA NA PSPF.
  WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) WAKIFATILIA UZINDUZI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII   ULIODHAMINIWA NA PSPF.
  BW. HASSAN ABDULRAHMAN, RAIS WA KWANZA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII AKIZUNGUMZA WAKATI WA UZUNDUZI WA ASASI HIYO, UZINDUZI HUO ULIDHAMINIWA NA PSPF.


   MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII, ANSGAR MUSHI   (WA TANO KUTOKA KUSHOTO) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA AMBAO NI WANACHAMA WAAZILISHI WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII, WA NNE KUTOKA KUSHOTO NI DR. ABDALLAH SAQWARE NA WA NNE KUTOKA KULIA NI ABDUL NJAIDI, AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA PSPF. PSPF NDIO WALIKUWA WADHAMINI WAKUU WA UZINDUZI HUO.  
  MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII ANSGAR MUSHI,    AKITOA HOTUBA WAKATI WA UZINDUZI WA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII ILIYOANZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) NA KUDHAMINIWA NA PSPF.
  MKURUGENZI WA UTAFITI, TATHIMIN NA SERA WA MAMLAKA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SEKTA YA HIFADHI YA JAMII ANSGAR MUSHI    AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI WA WA ASASI YA HIFADHI YA JAMII , KILICHOAZISHWA NA WANAFUNZI WA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) KULIA NI ABDUL NJAIDI AFISA UHUSIANO MWANDAMIZI WA PSPF.

  0 0

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba ya ufunguzi wa Maonesho ya Muziki  katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani jana ambayo hufanyika kila mwaka sambamba na utoaji wa Zawadi kwa mwaka 2015 pia kujumisha wanamuziki na wasanii mashuhuri kutoka nchi za Afrika na nchi mbali mbali Duniani.
   Baadhi ya washiriki katika ufunguzi wa  Maonesho ya Muziki wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutua yake jana  katika viwanja vya maonesho ya muziki yanayofanyika katika Mji wa Wurzburg Nchini   Ujerumani sambamba na utoaji wa zawadi kwa mwaka 2015 akiwa katika ziara ya kikazi.
  Kikundi cha Matona kutoka Zanzibar kilipokuwa kikitoa burudani yake wakati wa Tamasha la Maonesho ya Muziki wa Kiafrika yanayojumisha wasanii na wanamuziki mbali mbali kutoka Afrika na Mabara mengine Duniani wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohanmed Shein alihudhuria akiwa mgeni rasmi katika ziara hiyo.
  Baadhi ya Viongozi wa Ujumbe wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa katika maonesho ya Tamasha la Utamaduni wa Muziki lililofanyika jana na kuiwashirikisha wasanii na wanamuziki kutoka Nchi za Afrika  pamoja na mabara mengine Dunaiani katika Mji wa Wurzburg na .[Picha na Ramadhan Othman,]

  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898

  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425

  PRESIDENT’S OFFICE,
  STATE HOUSE, 
  1 BARACK OBAMA ROAD, 
  11400 DAR ES SALAAM. Tanzania.
   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Serikali ya Sweden inaridhishwa na kiwango cha maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na inadhamiria  kuinua ushirikiano  baina yake na Tanzania  ili kuleta maana zaidi katika maendeleo na kukua kwa uchumi kwa ujumla.


  Waziri Mkuu wa Sweden Stefan Lofven amesema hayo jana tarehe 4, Juni, 2015 ofisini kwake alipokutana  na Rais Kikwete.  "Tumefikia kiwango kingine, tunahitaji kuanzisha awamu mpya ya Uhusiano wetu". Waziri Mkuu Lofven amesema.


  Katika mazungumzo yao, viongozi hao wawili wamesema kuna umuhimu wa kuanzisha awamu nyingine ya maendeleo ambayo italeta maana zaidi ambapo Rais Kikwete amesema pamoja na ukweli kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa haraka, bado juhudi za kuondosha umaskini zinahitajika na zitafanikiwa kwa kuelekeza nguvu kwenye kilimo ambacho ndicho kinaajiri na kutegemewa na watanzania wengi zaidi hasa wanaoishi vijijini.


  "Tumefikia awamu nyingine na ni awamu nzuri ya kudumisha uhusiano wetu, tunaweza kushirikiana kwenye nishati, kilimo ili kukuza uchumi zaidi".Waziri Mkuu Lofven amemuambia Rais Kikwete na Rais Kikwete akaongeza 

  "Pamoja na misaada hiyo, awamu nyingine ya uhusiano baina ya Nchi mbili hizi inahitaji pia kuona makampuni ya kutoka Sweden yanawekeza nchini Tanzania na pia kukuza biashara baina ya nchi mbili hizi ili hatimaye Tanzania iweze kujitegemea zaidi na kupunguza kutegemea misaada".


  Mapema kabla ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu Rais Kikwete amekutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Maendeleo Sweden (SIDA) Bwana Torbjorn Pettersson ambaye amemueleza Rais kuwa; Sweden imeridhishwa na kiwango cha maendeleo na juhudi za kupunguza umaskini nchini Tanzania, Uchumi wa Tanzania umekua kwa wastani wa asilimia 7, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Pato la Taifa limekua kutoka sola za kimarekani bilioni 14.4 hadi kufikia dola bilioni 49.2 za kimarekani, wakati Pato la Mtu kwa mwaka 2005 lilikuwa  dola 375 na mwaka 2014 limekua hadi dola 1038.


  Rais Kikwete yuko nchini Sweden kuishukuru serikali ya Sweden na Watu wake kwa msaada wa maendeleo ambao umedumu tangu miaka ya 60. Nchi ya Sweden inaongoza kwa kuipatia  Tanzania misaada ya maendeleo na ni kutokana na misaada hiyo Rais Kikwete ameishukuru Sweden kwa kuiwezesha  Tanzania kuelekea kuwa Nchi yenye uchumi wa Kati (Middle Income Country) na kufuzu kutoka kundi la Nchi Masikini sana Duniani (Least  Developed Country).

  Rais Kikwete pia amefanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Sweden Bwana Urban Ahlin pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa nchini Sweden na kuwashukuru kwa misaada ya maendeleo kwa takribani miaka 50 sasa.


  Viongozi hao wamempongeza Rais kwa kufanya ziara ya shukrani na kuwaaga kwani ni mara chache kwa viongozi wengi wa Kiafrika kuaga na kuondoka madarakani.


  Imetolewa na;

  Premi Kibanga,

  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi

  Stockholm - Sweden.

  5 Juni, 2015.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka (mwenye flana ya mistari), akisalimiana na Watumishi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake jana katika banda la Wizara ya Uchukuzi katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira Mkoani Tanga. Maonyesho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Tanga.

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka akimsikiliza Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi, Yusuph Abdulkadir Muya  wakati akimueleza matumizi ya kifaa cha kupimia mvua jana katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira yanayofanyika Mkoani Tanga.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka(mwenye flana ya mistari), akiangalia asali katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wakati alipotembelea banda la Wizara hiyo na mabanda mbalimbali jana katika katika maonyesho ya Wiki ya Mazingira Mkoani Tanga. Maonyesho hayo yanafanyika kitaifa mkoani Tanga.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

  0 0
 • 06/05/15--02:20: Article 9
 • THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898

  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425

  PRESIDENT’S OFFICE,
  STATE HOUSE,
  1 BARACK OBAMA ROAD,
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais mpya ajaye nchini Tanzania anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha Tanzania itaendelea kubakia kuwa moja kwa kudumisha Umoja wetu na Amani kwani Tanzania inatokana na muungano wa nchi mbili.


  Rais Jakaya Kikwete ameyasema hayo jijini Stockholm - Sweden ambapo alikuwa akiongea na watanzania waishio Sweden mara baada ya kuwasili na kuanza ziara ya kikazi ya siku 3, kuanzia tarehe 3 - 5 Juni,2015.


  "Hapa tulipofikia lazima kuhakikisha Taifa linakuwa moja, kuna vyama,  na makabila mbalimbali, lazima uhakikishe Nchi inabaki moja". Rais amesisitiza.

  Watanzania mbalimbali walioko nchini Sweden kwa ajili ya shughuli za kikazi, kimasomo na ambao wanaishi nchini Sweden, walifika kumpokea na kumsalimia Rais Kikwete ambapo pia wamemsomea risala ambayo pamoja na vitu vingine wametaka kujua kuhusu haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi Mkuu ujao.

  "Swala hili linategemea Tume ya Uchaguzi, likiwekewa utaratibu linawezekana. Taratibu zake hazijawekwa, lakini ninaamini kuwa uchaguzi ujao unakuwa uchaguzi wa mwisho ambao watanzania wanaoishi nje hawapigi kura".Rais amesema.


  Rais Kikwete pia ameelezea matumaini yake kuwa Tanzania itapata kiongozi mzuri na kuelezea mafanikio ambayo serikali yake imeyapata na kutumaini kuwa yatadumishwa na kuendelezwa na Rais ajaye.


  Mapema akisoma risala ya watanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Nchini Sweden Bw. Tengo Kilumanga, amempongeza Rais Kikwete kwa kuridhia na kuonesha nia ya dhati ya kumaliza kipindi cha uongozi wake na kuwa mfano bora katika ukanda wa Afrika Mashariki.


  "Tunakupongeza mheshimiwa Rais, viongozi wengi katika Bara la Afrika huwa hawaagi, umefanya kitendo cha kishujaa sana. Viongozi wa Afrika huwa hawaagi kwa sababu siku ya kuondoka madarakani huwa haijulikani".Amesema Bwana Kilumanga. "Hii inaonesha wewe sio Mtu wa kupenda madaraka". Ameongeza.


  Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Kikwete ya kuaga Nchi wahisani na wenza katika maendeleo na Rais ameanzia Nchi za Nordic kwa sababu ya historia na uhusiano wa Nchi hizi kwa Tanzania tangu kupata Uhuru wake.


  Rais Kikwete anaendelea na ziara yake nchini Sweden ambapo anatarajia kufanya mazungumzo na wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha kuja kuwekeza nchini Tanzania.


  Imetolewa na;

   Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

  Stockholm - Sweden

  5 Juni, 2015.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akiweka saini katika daftari la rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati wa ibada iliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT), Usharika wa Kinyerezi, Manford Kijalo akiwaongoza askari waliobeba mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa wakati mwili huo ukiwasili katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa Jeshi la Magereza, Onel Malisa katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Probesheni na Huduma kwa Jamii, Aloyce Msika akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kamishna Mkuu mstaafu wa jeshi hilo, Onel Malisa wakati mwili huo ukipelekwa ndani ya gari kwa ajili ya kusafirishwa kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Tukio la kuuga mwili huo lilifanyika  katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

older | 1 | .... | 859 | 860 | (Page 861) | 862 | 863 | .... | 3270 | newer