Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110135 articles
Browse latest View live

TANGAZO LA DHARURA - UK

$
0
0
nna lillahi wa Inna ilayhi raaji'oun.
 
Kifo cha ndugu yetu kilichotokea Milton Keynes, UK, bado ndugu zetu hawajafikia malengo ya kufikisha kima kinachotakiwa kukidhi haja zote za maziko na malengo mengine ya kijamii, ya waliomzunguka.

Maziko yanatarajiwa Alhamis ya tarehe 04 June 2015, baada ya kupata mwili kwenye majira ya adhuhuri kutokana na wahusika, in shaa allah.
Kama kuna chochote utakachojaaliwa kutoa kama ni mchango wako, tuma kwenye akaunti ya benki ifuatayo:

Bank: Natwest
Name: Muhammad M. Y.
Account no: 36555673
Sort code: 51-70-14

Reference: Muna
Ni wajib kwetu kumzika ndugu yetu wa Kiislam, kokoyr ulipo jitolee mchango wako.

Marehem ameacha Mke nyumbani Zanzibar, na mtoto wa miezi 8, na Mkewe ni mja mzito tena anatarajia mtoto wa mwingine hivi karibuni.
Allah amghufirie madhambi yake na ampe jannat firdous na aipe subra familia yake, in shaa allah, amen.
Kwa habari zaidi wasiliana na:

Abdallah Mohammed 07716607908 (UK), Mohammed 079501307276 (UK).
Kwa niaba ya wafiwa http://www.salamatrust.com

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

ZIARA YA RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN- UJERUMANI

$
0
0

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Maritim Hotel Bw.Wissmann katika Mji wa  Wurzburg Nchini Ujerumani jana alipowasili katika Mji huo akiwa katika ziara ya Kiserikali ambapo atahudhuria ufunguzi wa maonesho ya Muziki yanayojumuisha wasanii kutoka nchi za Afrika na Mabara mengine (kulia) Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo, [Picha na Ramadhan Othman.]
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Wazanzibari waliofika kuwapokea mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani wakiwa katika ziara ya kiserikali pamoja na ujumbe wa Viongozi mbali mbali aliofuatana nao katika ziara hiyo inajumuisha na  maonesho ya Muzikiyanayojumuisha Wasanii mbali wa Nchi za Afrika na Mabara mengine ambayo hufanyika kila mwaka,
3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd,Salum Khamis Nassor mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakiwa katika ziara ya kiserikali Nchini humo,ambapo atatembelea Sehemu kadhaa za kihistoria na Kiuchumi
4
Rais wa Zanzibar na Mwenmyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar LTD Bw.Brian Thomson wakati alipowasiliMaritim Hotel akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakiwa katika ziara ya Kiserikali Nchini Ujerumani pamoja na Ujumbe waliofuatana nao,

RAIS Dk.Shein Nchi ni Ujerumani

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Wazanzibari waliofika kuwapokea mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani wakiwa katika ziara ya kiserikali pamoja na ujumbe wa Viongozi mbali mbali aliofuatana nao katika ziara hiyo Rais atafungua  maonesho ya Muziki yanayojumuisha Wasanii mbali wa Nchi za Afrika na Mabara mengine ambayo hufanyika kila mwaka,[Picha na Ramadhan Othman.]

HOSPITALI YA MNAZI MMOJA ZANZIBAR KUENDELEA KUTOA HUDUMA MASAA 24-THABIT KOMBO.

$
0
0
Na Rahma Khamis /Takdiri Ali- Maelezo Zanzibar                          

Wizara ya Afya Zanzibar imesema Kitengo cha Mifupa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kinaendelea kufanya kazi zake za kutoa Matibabu Masaa 24 kama kawaida kwa kufuata utaratibu maalum uliowekwa Hospitalini hapo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo huko katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani wakati alipokuwa akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua lini Serikali itaweka daktari katika Hospitali hiyo kwa Masaa 24.

Amesema Hospitali ya Mnazi Mmoja ni Hospitali Pekee ya Rufaa kwa Zanzibar ambayo inafanya kazi ya kutoa huduma bora za afya na kwamba kwa sasa ina Madaktari bingwa wa Mifupa Wawili wanaopatikana kwa muda wa Masaa 24.

Amefahamisha kuwa kwa sasa Hospitali ya Mnazi Mmoja inautaratibu maalum wa Madaktari wa zamu kwa kila Idara kuwepo Hospitali kwa masaa 24 ili kuweza kutoa huduma pindipo anapofika mgonjwa.

Awali Jaku alidai kuwa Wagonjwa wa Ajali wanaofika kutafuta huduma kwa Madaktari hao wa Mifupa wanasumbuka na kupata huduma siku ya pili jambo ambalo halipendezi kwa Hospitali hiyo ya Rufaa.

Hata hivyo Naibu WAziri wa Afya alisema wagonjwa wote wanaofika Hospitali wakiwemo wagonjwa wa ajali hutakiwa wapitie kitengo cha huduma za dharura (Emergency department) kwa kupatiwa matibabu ya haraka zaidi katika kitengo hicho ambacho Madaktari hupatikana kwa masaa 24 .

Waziri Mahmuud aliongeza kuwa Hospitali hiyo imeweka usimamizi maalum kwa kufuatilia kazi za kila siku kwa watendaji wake na kuweza kutatua tatizo lolote linapotokezea.

Kuhusu malalamiko ya Madaktari Naibu Waziri huyo amewashauri Wananchi kupeleka malalamiko yao katika Ofisi ya Daktari Mkuu katika Jengo la Utawala Hospitalini hapo ili yaweze kufanyiwa kazi

IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR.

Tendo la hisani la Wapendelevu’89 kwa Ocean Road Cancer Institute

$
0
0
 Wapendelevu’89 ( WaP89) ni kikundi cha Wanawake waliomaliza Kidato cha sita Mwaka 1989 katika Shule ya Wasichana Weruweru. Kikundi hiki kinaundwa na wanachama 44 ambao wanajishughulisha na ujenzi wa Taifa katika Nyanja mbalimbali wakiwamo madaktari, wahasibu, wahadhiri, wachumi, walimu/wahadhiri na wafamasia.

Kutokana na kuwa kwao sehemu ya Jamii , na kuona ombwe lililopo katika sehemu mbalimbali na hasa katika huduma za jamii na pia kuthamini uwajibikaji wa pamoja, kikundi kiliona ni vema katika mipango yake (Work Plan) ya mwaka 2015 kifanye tendo la Hisani kwa jamii -hitaji. Ndipo wazo la kusaidia eneo la ORCI, (Taasisi ya Saratani ya Ocean Road) lilipozaliwa na ukamilifu wake ukawa hapo tarehe 23 Mei 2015.

Katika tukio hili Kikundi kilikabidhi msaada wenye thamani ya takribani TShs. Milioni 12  uliotokana na michango binafsi ya kikundi pamoja na kuungwa mkono na wadau wengine wenye mapenzi mema. 

Tukio hili lilijumuisha utoaji wa vitu kwa wagonjwa wenyewe hapo hospitalini ambapo wanakikundi walikabidhi kwa mgonjwa mmoja mmoja vifaa vya matumizi binafsi, ambapo jumla ya wagonjwa waliokabidhiwa walikuwa 231 ( 68 akinababa na 163 kinamama). Lakini vile vile  WaP’89 walikabidhi vifaa mbalimbali kwa wizara kupitia mwakilishi wake Dk. Shadrack Busweru 
 WaP89 wakiwa na Mh. Alshaymaar Kwegyir, Mbunge wa Viti maalum ( Walemavu) wakiwa katika Taasisi yay a Saratani Ocean Road wakipanga vitu tayari kwa ugawaji katika wodi ya Wanaume. 

Msaada huu umeainishwa kama ifuatavyo  :
ü  Mashuka 500 ya kutumiwa na wagonjwa
ü  Mito ( pillows) ya wagonjwa
ü  Dawa za kupunguza maumivu kwa wagonjwa wanaopokea tiba hapo ORCI
ü  Nauli kwa wagonjwa walioruhusiwa lakini wanashindwa kwenda nyumbani ( mikoani)
ü  Sabuni, nguo na vifaa vya kuhifadhia chakula. 
 Awamu ya pili ya ugawaji wa nguo kwa wagonjwa katika Wodi ya Wanawake. Mh. Al Shaymaar Kwegyir akisubiri mzigo wake wa kugawa huku akipata maelekezo kutoka kwa Mwenyekiti wa WaP89 Stella ¬Emma Katende ( katikati)

Mgeni rasmi  ambaye alijumuika na WaP’89 katika zoezi zima alikuwa Mbunge wa Viti Maalum (Walemavu) Mh. Al Shaymaar Kwegyir ambaye aliwapongeza sana Wapendelevu’ 89 kwa moyo wao wa kuijali jamii na hasa ukizingatia kuwa wamama hawa ni watu wenye shughuli zao nyingi na hivyo kutoa muda na raslimali ni jambo la kutia moyo sana.

Vile vile Mh. Kwegyir alitumia fursa hiyo kuwakumbusha watu wengine kusaidia jamii na hasa wagonjwa hawa ambao wanakuwa na tiba za muda mrefu. Vile vile katika nafasi yake ya Mbunge anayewakilisha Jamii ya watu wenye ulemavu, kutilia mkazo umuhimu wa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao nao huathiriwa sana na Saratani ya ngozi kutokana na athari za jua katika nchi yetu ambayo iko karibu na Ikweta, kuwahi tiba hospitali mara waonapo dalili za awali kama vipele katika ngozi zao ili kuepuka madhara makubwa kwenye ngozi na afya zao mara vipele hivi vigekapo saratani.
 Akina mama wanachama wa WaP89 wakiwa na mgeni rasmi Mbunge wa Viti maalum Mh. Alshaymaar Kwegyir ( mwenye miwani) na Mwakilishi wa Wizara ya Afya ( Idara ya Magonjwa Yasiyoambukiza), Dr Shadrack Busweru ( mwenye shati Jeupe) wakati wa makabidhiano ya vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Kikundi cha WaP89 kwa hospitali ya Ocean Road, Dar Es Salaam  hivi karibuni.
 WaP89 na mgeni rasmi Mh. Alshaymaar Kwegyir wakiwa katika picha ya pamoja katika hospital ya Ocean Road mara baada ya kukamilisha zoezi la ugawaji wa vifaa kwa wagonjwa

USIKOSE KUCHEKI MECHI YA FAINALI YA CHAMPIONS LEAGUE KUPITIA DSTV

DC ILALA, ORIJINO KOMEDI WASHIRIKI WIKI YA MAZINGIRA KATA YA KIVUKONI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kushoto) akishiriki zoezi la usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi eneo la Aga Khan kata ya Kivukoni ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya Mazingira huku akishirikiana na viongozi wa kampuni iliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala Green Waste Pro Ltd pamoja na wafanyakazi wa manispaa ya Ilala jana asubuhi. Wa pili kushoto ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.
Mkurugenzi wa Green WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo (kushoto) akifanya usafi kwenye fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni karibu na maeneo ya Aga Khan sambamba na wafanyakazi wenzake pamoja na Muandaaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni David 'Seki' (wa kwanza kulia) katika kuadhimisha wiki ya Mazingira.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakiendelea kufanya usafi katika fukwe ya Bahari ya Hindi kata ya Kivukoni eneo la Aga Khan jijini Dar ikiwa ni wiki ya Mazingira. Katikati ni Meneja wa mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

MH. SITTA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA MAZINGIRA JIJINI TANGA

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya alipokua akiwasili kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga wakati wa maonyesho ya Wiki ya Mazingira Duniani Juni 3, 2015
Mkurugenzi wa wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya Akitoa maelezo ya moja ya DVD ya majanga mbalimbali ya maafa kwa mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mhe. Samwel Sitta alipo tembelea banda la Ofisi ya waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa maafa kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga Juni 3, 2015
Mtaalamu kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ali Mwatima akitoa maelezo kwa wanafunzi wa shule ya Darajani mjini tanga walipo tembelea banda la Ofisi hiyo tarehe 3 Juni, 2015 katika maonyesho ya wiki ya Mazingira yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Tanga.

Mh. Samia Suluhu aendelea na ziara ya kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira wilayani Muheza, Tanga

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika kijiji cha UWAMAKIZI alikoenda kwenye ziara ya kukagua shughuli za utunzaji wa mazingira katika kijiji cha Bombani kilichopo wilayani Muheza mkoani Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Bombani wilayani Muheza mkoani Tanga alipotembelea kijijini hapo katika maadhimisho ya wiki ya siku ya Mazingira duniani insyofanyika jijini Tanga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akifurahia mbegu ya milimao inayooteshwa na wanakikundi wa kikundi cha UWAMAMKIZI katika kijiji cha Shembakazi wilayani Muheza mkoani Tanga.

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Anjelina Madete akiongea na wanachama wa Kikundi cha nguvu kazi wanaohusika na uoteshaji wa mbegu za miti na matunda pamoja na kutunza mazingira katika kijiji cha Mashewa wilayani Muheza mkoani Tanga.

MCC, 10 American Companies Explore Opportunities in Tanzania

$
0
0
On June 2, 2015, the U.S. Department of Energy’s Assistant Secretary for Fossil Energy, Christopher Smith, speaking with the Tanzanian Minister for Energy and Minerals, George Simbachawane (right). Seated between the Assistant Secretary and the Minister is Kamran Khan, the Millennium Challenge Corporation’s Vice President for Compact Operations. The meeting was part of a broader visit that included ten American companies exploring trade and investment in Tanzania’s energy sector.

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO LEONIDAS GAMA AKABIDHIWA MRADI WA UJENZI WA UKUMBI WA CHAKULA ULIOFADHILIWA NA TANAPA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Rombo mara baada ya kuwasili katika shule ya sekondari Olele iliyopo kata ya Olele kwa ajili ya kukabidhi Mradi wa ujenzi wa ukumbi wa Chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa , Tanzania (TANAPA).
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama pamoja na mkuu wa wilaya ya Rombo Lembris Kipuyo wakifurahia nyimbo iliyokuwa ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya  sekondari ya Olele wakati alipofika kwa ajili ya uzinduizi na makabidhiano rasmi ya ukumbi wa chakula uliojengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenye basi kuwasalimia wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wa mkoa wa Morogoro akiwa njiani kuelekea mkoani Kagera.



 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa mkoa wa Morogoro waliojitokeza kuwasalimu wakati wa safari ya kuelekea Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi waliojitokeza kwenye kituo cha mabasi mjini Morogoro maarufu kama Msamvu ambapo aliwaambia wananchi hao huu ni wakati wa kuchagua kiongozi wa kutuongoza hivyo ni vyema wananchi kupima na kuacha ushabiki.

TANZANIA YAKABILIWA NA UKAME

$
0
0
Mgeni Rasmi katika Semina ya Kukuza Uelewa wa Usimamizi wa Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga, Bwana Salim Chima ambaye pia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga akifungua Semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu akizungumza jambo katika Semina ya Kukuza Uelewa katika Masuala ya Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga iliyofanyika jijini humo leo.
Sehemu ya Washiriki wa semina ya siku moja ya Kukuza Uelewa katika Masuala ya Mazingira kwa Watendaji wa Halmashari ya Jiji la Tanga wakisikiliza mada zinazotolewa katika warsha hiyo
Mgeni Rasmi katika Semina hiyo Bwana Salim Chima akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wote walioshiriki katika Seminas hiyo. 

 Na Victor Mariki - Ofisi ya Makamu wa Rais

Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani ya asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania imeathirika na janga la ukame ambao unaweza kupelekea uzorotaji katika ukuaji  wa uchumi  na hata kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai.

Hayo yalielezwa  na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Zainab Shaban Bungwa wakati akitoa mada katika  semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira  kwa watendaji wa Halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo leo.

Aidha Bi Bungwa alifafanua kuwa  uchumi wa Tanzania  unategemea kwa kiasi kikubwa  rasimali asili kama vile ardhi, misitu, wanyamapori na maji ambapo inakadiriwa  asilimia 75 ya wanachi waishio vijijini hutegemea zaidi ardhi katika uendeshaji wa maisha yao.

Pia aliongeza kuwa  Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira imechukua hatua mbali mbali katika kukabiliana na  janaga hilo  kwa kuunda sera, mikakati na sheria mbalimbali  za kudhibiti uharibifu wa mazingira nchini.

Baadhi ya mikakati, sera na sheria hizo  ni Mkakati wa Hatua za Haraka Kuhifadhi Mazingira na Vyanzo vya Maji, Mkakati wa Bahari na Mabwawa, Program za Kupambana kwa Kuenea Hali ya Jangwa na Ukame, Mkakati wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi pamoja na Program na Miradi inayotekelezwa na  Sekretarieti ya Mikoa katika suala la Utunzaji Mazingira.

Sanjari na hayo Bi Bungwa alienda mbele zaidi  kusema kuwa hivi sasa robo ya dunia ipo hatarini kukumbwa na hali ya jangwa kwa kuwa  zaidi ya hekta bilioni 3.6 za ardhi yake tayari zimeshaathiriwa na janga hilo ambalo mpaka sasa limeathiri zaidi  ya watu milioni 900  duniani kote .

Kwa upande wa bara la Afrika  hivi sasa hali hiyo ya jangwa imekuwa ni tatizo sugu  kwakuwa mpaka sasa tayari asilimia 73 ya ardhi yake  imeshathirika vibaya na janga hilo hali ya jangwa.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAKAGUA GHALA LA KUHIFADHI VIFAA VYA MAAFA MKOANI SHINYANGA

$
0
0
Mtunza ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa mkoani Shinyanga, Asha Issa akiwaonesha Wakaguzi wa Hesabu za Serikali, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini, Jacob Ndaki (katikati) na John Obeid, rangi zitumiwazo na wanafunzi kuchora zilizo hifadhiwa ghalani hapo, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo, tarehe 3 Juni, 2015.
Baadhi ya marobota ya mablangeti yaliyohifadhiwa katika ghala la kuhifadhi vifaa vya maafa mkoani Shinyanga, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo, tarehe 3 Juni, 2015.
Baadhi ya makasha yaliyohifadhi vifaa vya maafa katika ghala la kuhifadhi vifaa hivyo mkoani Shinyanga, wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipokagua ghala hilo, tarehe 3 Juni, 2015.

Refugees and Climate Change Within a Free Country

$
0
0
 SOMETIMES it is very difficult to believe that in a free country like Tanzania, can have Refugees. May be it is sound very difficult. But let’s define Refugee according to the Oxford dictionary, “A person who has been forced to leave their country in order to escape war, persecution, or natural disaster”. 

Here we can find those factors lead to Refugees, then you will agree with me sometimes people can leave their homes even due to particular factors to find another home or remain homeless. One among the factors can be a natural cause in which most of phenomenons are due to climate Change and here we get Climate Refugees. 
Climate refugees in a temporary camp
Climate refugees in a temporary camp
 Climate Refugees are those people who leave their homes due to climate change impacts or in simple words we can say are people who must leave their homes and communities because of the effects of climate change and global warming. I could not talk about others; I am confidently talking about my country Tanzania no matter how some people might think that, it is not necessary to talk about this. Regard once George Carlin said that “Those who dance are considered insane by those who cannot hear the music.” 

 In Tanzania people have been much affected by climate change due to Floods that happening in different regions of Tanzania. Let’s talk about what happened December 2011, where Tanzania was very much affected by heavy rainfall for the first time since its independence 1961. It was reported about sixty seven thousand (67,000) people became homeless in Kilimanjaro, Arusha and Mbeya regions while in Dar es salaam about fifty thousand (50,000) people were affected. 

 In March 2015 Tanzania also has faced a same challenge of Climate change through the floods that affected the coastal area of Lake Victoria and it was reported that about three thousand and five hundred (3,500) people were affected. It has been reported that most families became Homeless after floods that has been occurred in Tanzania. Mostly in Mwanza, Dar es salaam, Mbeya, Arusha and Kilimanjaro regions. Hence people became homeless and those people subjected as Climate refugees. Climate refugees in a temporary camp Climate refugees in a temporary camp

Then there is no need to have those refugees regarding this is a free country. 

Then a government should work on those promises like to give a special place for those who are living in Areas that can be easily affected by climate change especially floods. It is true that our government have already prepare a special place for them but it has to improve the social services to those areas because it seems that is a big challenge for those places. 

 As the year of Paris conference, UNFCCC COP 21 at France then all countries has to make sure that they participate active to make sure that they fight the climate change because it affects the whole planet. I believe that we can make it because climate change is real. Let’s echo the Bill Gates when he was saying “The climate change is terrible problem and it is absolute needs to be solved. It deserve to be a huge priority” that is one among a big quote that can be used to insist the United Nation. 

 This is just a summary of what have been happen in Tanzania, and I know every where has been affected by climate change but let me remind you, if we cannot save a living Planet then we will never manage in dead planet like Mars”.

Taasisi kutoka India yawapiga msasa wakaguzi wa migodi nchini

$
0
0
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka Wizara ya Nishati na Madini (Kushoto) akijadiliana jambo na Mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (Kulia) kwenye mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini yaliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodini nchini yaliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani wakishiriki katika zoezi la kuandaa mpango wa mazingira kwa vitendo katika mafunzo hayo.

Na Greyson Mwase, Bagamoyo

Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka nchini India (Centre for Science and Environment) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, imekamilisha mafunzo ya siku nne yaliyoshirikisha wakaguzi wa migodi nchini ambapo wakaguzi walijifunza jinsi ya kuandaa miongozo mbalimbali kwa ajili ya kutumika kwenye ukaguzi wa mazingira kwenye migodi.

Akizungumza katika mahojiano maalum wakati wa mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje alisema lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wakaguzi wa mazingira na migodi nchini wa kuandaa, kuchambua na kupitia taarifa za athari kwenye mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini.

NASSAR ASHIRIKI UJENZI WA CHANZO CHA MAJI KIJIJI CHA KARANGAI KATIKA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

$
0
0
MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.


Zoezi hilo lilo anza majira ya saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassar akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.

Akizungumza katika eneo hilo ,Nassar alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya kutoshja.


“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika ugali  na kazi ikaendelea”alisema Nassar.

Nassar aliwashukuru ijana zaidi ya 300 pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia moyo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar aiwa amepanda kwenye Lori lililokuwalikibeba mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo kipya cha maji kwa ajili ya kumwagilia katika kijiji cha Karangai kata ya Kikwe katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BENKI YA EXIM TANZANIA YASHIRIKI MAONYESHO YA 18 YA WIKI YA MAZIWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

$
0
0
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisalimiana na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara Bw. John Ndyebonera ,alipotembelea kwenye banda la maonyesho la benki hiyo ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati hivi karibuni. Wengine ni wafanyakazi pia wa benki hiyo.
 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dr, Titus Kamani, (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kwenye banda la maonyesho ya benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara ambayo ilishiriki kwenye maadhimisho ya 18 ya wiki ya maziwa yaliyofanyika kitaifa wilayani Babati. Anayeshuhudia kwa karibu zaidi ni Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera. Wengine pia ni wafanyakazi wa benki hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania tawi la Babati mkoani Manyara wakiongozwa na Meneja Uendeshaji na Huduma kwa wateja wa benki hiyo tawi la Babati  Bw. John Ndyebonera (Wa pili kulia), kwa pamoja wakishuhudia mmoja wa washiriki wa maonyesho ya 18 ya wiki ya maziwayaliyofanyika kitaifa wilayani Babati (wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni waliotembelea banda la maonyesho ya benki hiyo ambayo pia ilishiriki maonyesho hayo kwa mafanikio makubwa.

katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani awatembelea wajumbe wa kikao kazi cha mambo ya ndani mjini morogoro

$
0
0
Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil akizungumza na kuwapongeza wajumbe wa Kikao Kazi cha Uandaaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara yake wa mwaka wa fedha 2015/2016 katika kazi hicho kinachoendelea mjini Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mwamini Malemi akitoa mwongozo wa majadiliano kwa Wakuu wa Idara, Maafisa Ununuzi, Maafisa Bajeti na Wakurugenzi Wasaidizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Ununuzi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi cha wizara hiyo Mapesi Manyama katika Kikao Kazi cha Utayarishaji wa Mpango wa Ununuzi na Mpango Kazi wa wizara wa mwaka wa fedha 2015/2016 kinachoendelea katika hoteli ya Oasis mjini Morogoro. Kushoto ni Kamishna wa Fedha wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga aliyesimama ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mapesi Manyama.

Viewing all 110135 articles
Browse latest View live




Latest Images