Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 857 | 858 | (Page 859) | 860 | 861 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Na  Bashir  Yakub.

  Watu  wengi  wanaonunua  ardhi  wamekuwa  wakipata  usumbufu  mkubwa katika   kubadili  majina  yaani kutoka  mmiliki  wa  mwanzo  kwenda  kwa  mmilki mpya  aliyenunua. Upo  usumbufu ambao  husababishwa   kwa  makusudi na  maafisa  wanaohusika   lakini  pia  upo  usumbufu  ambao  husababishwa   na  watu  wenyewe  wanaotaka  kubadili  majina.  

  K,Wengi  huanza  muamala  huu  bila  kuwa  na  taarifa  kamili  za  nini kinahitajika kwa  maana  ya  nyaraka  ikiwemo  ada au  malipo  ya  kisheria jambo  ambalo  huwapotezea  muda  mwingi. Kwa wanaofanya kazi  hizi  kama  mimi  watajua  ni usumbufu  wa aina  gani  mtu  huupata anapoanza mchakato  huu bila  taarifa.  Unaposoma  makala  haya  ni  vema  basi  ukajua  inatakiwa  ujiandae  na  nini  na  hasa  ada ili  unapoanza  mchakato  huu  usijikute  unaishia  njiani.

  1.UMUHIMU  WA KUBADILI  JINA  HARAKA  BAADA  YA MANUNUZI.

  Nimewahi kuandika kuwa sheria iko wazi kuwa ambaye jina lake linaonekana kwenye hati ndiye mmiliki.

  Kwa  kauli  hii   mnunuzi  anatakiwa  kufanya  jitihada  za  haraka  na za  makusudi  kubadili  jina  mara tu baada  ya  kununua  kiwanja  au  nyumba. Sikatai  kuwa  kunakuwa  na  mkataba wa  mauziano  lakini  lazima  ieleweke  kuwa  mbele  ya  macho  ya  sheria   jina  lililo  kwenye  hati  lina  uzito  kuliko  mkataba  wa  mauziano. Usiridhike  kukaa  na  mkataba  wa  mauziano  ikiwa  hujabadili  jina. Hii  ni  kwa  ajili  ya  ulinzi  wako  na  wa  ardhi  yako.  

  Utakapotokea  mgogoro   wa  umiliki  ikiwa  hujabadili  jina waweza  kuwa  katika  hatari  kubwa  ya  kupoteza  hasa  kama  mgogoro  huo  umeanzishwa na aliyekuuzia. Huu  ndio  ukweli  na  lazima  tuonyane  ili    tuwe  salama na  mali  zetu. 

  Lakini pia  hata  ukitokea  mgogoro  mwingine  wowote  wa  umiliki  kuna  mambo  ndan ya  sheria  yataufanya  kuwa   mgumu kutokana  na sababu  tu  kuwa ulikuwa  hujabadili   jina.  Hapo  sijaongelea  faida  nyingine  za kubadili  jina  kama  kukopa  n.k. Nishauri  tu  kwa  ufupi  kuwa  unapojiandaa  kununua  nyumba  au kiwanja  jiandae  pia na  kubadili  jina  moja  kwa  moja.  Hakikisha  haya  mawili  yanakwenda   pamoja.

  2. ADA  ZA KUBADILI  HATI ZA NYUMBA/VIWANJA  HIZI  HAPA.

  Nimesema  hapo  juu  kuwa  usipojiandaa  na  ada  vyema  mara   nyingi  utajikuta  unaishia  njiani  kwa  kushindwa  kukamilisha  mchakato  huu.  Lakini  utaandaaje  ada  bila  kujua  kinahitajika  kiasi  gani . Hili  ndilo  lengo  la  makala  haya. Malipo ya  ada  tunaweza kuyagawa  mara  mbili. 

  Kwanza  kuna  ada inayolipwa  manispaa. Hii  hulipwa  katika  manispaa  ile  ambayo kiwanja  au  nyumba  ilipo. Kama  temeke  basi  ada  italipwa  manispaa  ya  temeke  halikadhalika  maeneo mengine  hivyohivyo. Na  hapa  ndipo  unapoanzia katika  ulipaji  wa  ada.  

   Ada  inayolipwa katika  manispaa  huwa ni  asilimia moja  ya  mkataba  wa  kununulia  au  ya  taarifa  ya  tathmini (valuation report). Unapokwenda  kulipa  ada  manispaa  ni  lazima  uambatane  na  mkataba  wako  ulionunulia  kiwanja/nyumba  pamoja  na  valuation  report  kwakuwa  hivi  ndivyo  wanavyotumia kama  vipimo  vya  ada. 

  Ikiwa  mkataba  wa  kununulia  una  bei  kubwa  kuliko valuation  report  basi  wanachukua  asilimia  moja  ya  mkataba  huo na  ndio  itakuwa  ada. Lakini  ikiwa  pia  valuation  report  ina bei  kubwa kuliko  mkataba  basi  wanachukua  asilimia moja  ya  valuation  report. Kwa  ujumla  wao  huchukua  asilimia moja  ya  chenye  bei  kubwa  kati  ya  valuation  report  na  mkataba  wa  kununulia  na  huifanya  hiyo  ndio  ada.

  Pili  baada  ya  kulipa  manispaa  faili  lako hupelekwa  mamlaka  ya  mapato  Tanzania ( TRA) kwa  ajili  ya  kodi. Hawa  wao  hutoza  asilimia  kumi  ya  taarifa  ya  tathmini( valuation  report). Kama  valuation  inasema  eneo  lako  lina  thamani  ya  milioni  kumi bila  shaka asilimia  kumi  yake  ni  milioni moja. Hiyo  ndio itakuwa  kodi. 

  Angalizo  hapa  ni kuwa  hizi  valuation  report  hutakiwa zile mpya. Kwa  mfano  mtu anayo  valuation  yake   aliyofanyiwa  mwaka  2000  na  sasa anataka  kupata au  kubadili  hati  leo  2015. Hii  ya  mwaka  2000  haiwezi kutumika  kutathmini  kodi itahitajika  mpya  ya mwaka 2015.  Hii  ni  kwasababu  thamani  ya  ardhi  ya  mwaka  2000 si  sawa  na  ya  sasa  mwaka 2015. Hizi  ndizo  ada  unazotakiwa  kujiandaa  nazo.  


  2.   PIA  ANDAA  NYARAKA  HIZI.

  ( a ) NYARAKA  ZA  UHAMISHO

  Nayaraka  za  uhamisho  zinajumuisha  fomu  namba 29  ijulikanayo  kama  fomu  ya  kusudio  la  uhamisho( notification  of disposition) ambayo  hueleza  nia  na  lengo  la  muuzaji  kutaka  kubadili  jina  au  kuondoa  jina  lake  katika  hati.  Hii utaandaa  nakala  tatu . Pili  ni fomu  namba  30  ambayo  hujulikana  kama  fomu  ya  idhibati  ya  uhamisho ( application  for  approval  of  disposition).  Katika  fomu  hii  muuzaji  pia  atakuwa  anatoa  idhini  kwa  mamlaka  za  ardhi  kuidhinisha  hiari  yake   ya kuachia  umiliki  kutoka kwake   kwenda  kwa  mtu  mwingine ambaye  ndiye  mnunuzi.   

  Mwisho  ni  fomu  namba  35  ijulikanayo kama fomu  rasmi  ya  kuhamisha  umiliki ( transfer of a  right  of  occupancy)  ambayo  ndiyo  rasmi  sasa  huhamisha  umiliki  kutoka  kwa  muuzaji  kwenda   kwa mnunuzi. Hii  ndiyo  humpa  mnunuzi  umiliki  rasmi . Pia  mkataba  wa  mauziano  ni  nyaraka  ambayo  itaambatanishwa  hapa.
  Kwa  kiwanja  au  eneo  ambalo  halijaendelezwa ( halijajengwa)   huandaliwa  kitu  kiitwacho  commitment  bond  kikiwa  kama  ziada  ya  nilivyotaja  hapo.  Fomu  zote  hizo  pamoja  commitment  bond  hupatikana  katika  ofisi  za  wanasheria  na  huandaliwa  na  wanasheria.

  ( b ) URAIA

  Sheria  iko  wazi  kuwa wanaotakiwa  kumiliki ardhi  ni  raia  wa  nchi  hii tu. Hivyo  unapotakiwa  kupata  hati  ya  umiliki  lazima  pia  uthibitishe  Utanzania  wako. Hapa   utatakiwa kuandaa  nakala(copy)   ya   cheti  cha  kuzaliwa ambayo  imethibitishwa( certified)  na  wakili  au  nakala  ya  pasipoti  ambayo  imethibitishwa  na  wakili  au  kama  huna  hivyo  vyote  basi  yakupasa  kuandaa  kiapo( affidavit).

  Mwisho  niseme  kuwa  ikiwa  utajiandaa vyema  na  haya  utapata  hati  kwa  urahisi   au  kama unabadili  jina  utabadili  kwa  urahisi  pia. Jiandae epuka  usumbufu.

  MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com .


                KUSOMA  ZAIDI links  goes to  sheriayakub.blogspot.com                                         
   

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo katika ziara ya siku moja kuzungumza na wananchi baada ya mwananchi mmoja kuuawa kwenye msitu wa Marang unaohifadhiwa na Shirika la Hifadhi ya Taifa(Tanapa).Waziri Nyalandu ameunda Tume ya kuchunguza mgogoro huo ambayo itatoa mapendekezo serikalini kwa utekelezaji.
   Waziri wa Maliasili na Utalii,Lazaro Nyalandu akizungumza na mmoja  wa wananchi wa Kata ya Buger wilaya ya Karatu mkoa wa Arusha leo baada ya kuhutubia wananchi hao na kuwahidi serikali kuwachukulia hatua askari waliokiuka taratibu za maadili.
   Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha,Cesilia Paresso akihutubia wananchi wa Kata ya Buger na kuitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuzingatia sheria na wananchi kulinda Msitu wa Marang kwaajili vizazi vijavyo.
   Mkazi wa Kata ya Buger,Rehema Tango akitoa kero zake mbele ya Waziri wa Maliasili na Utalii.
  sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huop ambao waliweza kutoa kero zao .

  0 0
 • 06/02/15--20:54: Niambie Live Show
 • Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi
  Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
  Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
  Ni Niambie Live....
  KARIBU

  0 0


  Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Idara ya Oganezesheni Dr Mohamed Seif Khatibu akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu Dodoma kuhushu ratiba ya kuchukua fomu leo  Wagombea Urais kupitia Chama hicho aliwataja kuwa ataanza Prof Mark  Mwandosya ,Stephen Wasira,Edward Lowasa, balozi Amina Salumu Ali na Charles Makongoro Nyerere  na Khatibu ndiye aliyepewa jukumu na Chama hicho kutoa fomu hizo.

  Wanasiasa watano  wanatarajia kuchukua fomu ya kugombea urais  katika makao makuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma.

  Kwa mujibu wa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) wa Oganaizesheni, Dk Muhammed Seif Khatib, uchukuaji wa fomu hizo unaanza rasmi leo.

  Amesema kwa mujibu wa orodha waliyonayo, wanachama watano watachukua fomu hizo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 10:30 jioni, na kila mmoja amepewa saa moja na wametenga muda wa kuzungumza na waandishi wa habari kwa wagombea ambao wataona inafaa kwao. Amemtaja wa kwanza kuchukua fomu kuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya kuanzia saa 4 kamili hadi saa 5:30.

  Profesa Mwandosya atafuatiwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira kuanzia saa 5:30 na atafuata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa atachukua fomu kuanzia saa saba kamili. Wa nne atakuwa Waziri wa zamani wa Muungano, Balozi Amina Salum Ali kuanzia saa 8:30 mchana na pazia la ufunguzi litafungwa saa 9:30 alasiri na mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere.

  Baada ya kumaliza kuchukua fomu  kwa kundi la kwanza wanasiasa  wengine ambao wametangaza nia ya kuwania urais ni Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye, Profesa Sospeter Muhongo, January Makamba, Mwigulu Nchemba na Luhaga Mpina.Wanaotajwa ni pamoja Bernard Membe, William Ngeleja, Dk Titus Kamani, Luhaga Mpina, Mizengo Pinda, Dk Asha-Rose Migiro, Shamsi Vuai Nahodha, Dk Emmanuel Nchimbi na Dk Hamis Kigwangalla.

  Katibu huyo wa Oganaizesheni amesema uchukuaji huo wa fomu utazingatia taratibu zilizowekwa na CCM na kutakuwa na fomu tatu zitakazopewa wagombea.Fomu  ya kwanza  itahusu maelezo binafsi ya mgombea, itahusu uzoefu na ujuzi wake, nyingine itakuwa ya kujaza orodha ya wadhamini wake na nyingine ya masharti kama yalivyokubaliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.

  Kwa upande wa wadhamini  amesema, mgombea atatakiwa kupata wadhamini 450 kutoka katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na mikoa mingine mitatu ya Tanzania Zanzibar. wagombea hao watakapofika kuchukua fomu, wanapaswa kuwa na ada ya Sh milioni moja na watasaini daftari maalumu kuonesha ndio waliochukua fomu.

  Amewataka  wagombea wengine wanaotaka kuchukua fomu hizo kuwasiliana mapema na ofisi yao kwani alisema wangependa kazi ya uchukuaji fomu kudumu kwa siku zisizozidi tano ili shughuli nyingine ziendelee.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimajaro,Leonidas Gama akikaribishwa na Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Erastus Rufungulo katika makabidhiano ya mradi wa maji wa ujirani Mwema uliotolewa na hifadhi za taifa nchni TANAPA.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika tanki la maji la mradi wa ujirani mwema uliotolewa na TANAPA kwa wananchi katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama akisoma kilichoandikwa katika vibao mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi huo.
  RC ,Gama akinywa maji kwa kutumia mkono mara baada ya kufungua bomba la maji katika kijiji cha Ashira wilaya ya Moshi vijijini.


  0 0


  0 0

  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425


  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshutuko na masikitiko taarifa za kifo cha mbunge wa Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam, Mheshimiwa Eugenia Mwaiposya ambaye ameaga dunia usiku wa kuamkia jana, Jumanne, Juni 2, 2015, mjini Dodoma ambako alikuwa anahudhuria Vikao vya Bunge.

  Katika salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anna Makinda, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mshutuko na masikitiko taarifa za kifo cha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Eugenia Mwaiposya ambaye nimejulishwa ameaga dunia mjini Dodoma ambako alikuwa anaendelea kuhudhuria Vikao vya Bunge.”

  Amesema Rais Kikwete: “Kwa hakika, taifa letu limepoteza kiongozi muhimu kutokana na kifo hiki. Mbunge Mwaiposya alikuwa mwakilishi hodari na mtetezi wa kuaminika wa wananchi wa Jimbo la Ukonga. Napenda kukutumia wewe Mheshimiwa Spika salamu zangu za rambirambi kwa kupoteza Mbunge mahiri sana. Aidha, kupitia kwako, nawatumia Wabunge wote salamu zangu za rambirambi kwa kuondokewa na mwenzao.”

  Ameongeza Rais Kikwete: “Kupitia kwako, Mheshimiwa Spika, napenda pia kutuma salamu zangu kwa wananchi wa Jimbo la Ukonga ambao wamepoteza mwakilishi wao. Mheshimiwa vile vile, napenda kutoa pole nyingi kwa familia, ndugu na jamaa wa Mbunge Mwaiposya kwa kuondokewa na mama na mchangiaji mkubwa katika maisha yao. Wajulishe niko nao katika msiba huu mkubwa. Naelewa uchungu wao katika kipindi hiki na nawaombea subira ili waweze kuvuka kipindi hiki. Naomboleza nao na naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Mheshimiwa Eugenia Mwaiposya. Amina.”

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  2 Juni, 2015

  0 0


  0 0

  MPANGO MBAYA ni filamu iliyochezwa na washiriki 10 waliofanikiwa kuingia katika Fainali ya shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) msimu wa kwanza 2014 na kushirikisha baadhi ya waigizaji mahiri kutoka katika kiwanda cha Filamu Tanzania.
  Filamu ya Mpango Mbaya ni filamu ambayo imetengenezwa kwa viwango vya hali ya juu huku ikikidhi viwango vya kimataifa na ni filamu ambayo ina ubora wa hali ya juu kuanzia ubora wa picha, Sauti, rangi mpangilio wa matukio na upigwaji picha wake na ubora wa washiriki wa filamu hiyo
  Filamu hii itazinduliwa mnamo tarehe 12 Juni 2015 Katika Ukumbi wa Mlimani City  na pia Filamu hii itaendelea kuonyeshwa kwa siku mbili mfululizo katika ukumbi huohuo.
  Picha chini ni baadhi ya taswira za washiriki wa filamu hiyo

  0 0


  0 0

  Mazungumzo ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini Johannesburg nchini afrika kusini yanaweza kusomeka kwa "KUBOFYA HAPA"  Mkutano ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kua ya sita kwa nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.

  Akitolea ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa kampuni ya Vodacom ya Afrika kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku aki ibua mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.

  Aidha Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurgenzi wa wakala wa usalama wa Marekani (National Security Agency – NSA) bwana William Binney pamoja na Raisi na muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika vibaya na wahalifu.

  Nikiwasilisha mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii pamoja na kiuchumi. Nilielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.

  Katika mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia waliunga mkono nilicho zungumza kua bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.


  0 0  Adama Fundikira akiwa na mama yake mdogo Mh Samuel Sitta aitwaye Ndisha Said Fundikira
  Wayege wakicheza ngoma

  Habari na picha kwa hisani ya 
  Mkala Fundikira wa TBN central zone

  0 0

  Na Asteria Muhozya, Tanga.

  Kampuni za uchimbaji madini, utafutaji mafuta na gesi wakiwemo wachimbaji wadogo nchini, wametakiwa kuzingatia sheria na kanuni za uhifadhi wa mazingira wakati wanapotekeleza shughuli zao, ili kuwezesha rasilimali zinazopatikana  ardhini ziweze kuwa endelevu  kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

  Rai hiyo imetolewa na   na Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Ephraim Mushi wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani yanayoendelea kufanyika  katika viwanja vya Tangamano  Jijini, Tanga.

  Mhandisi Mushi ameeleza kuwa, kutokana na ongezeko kubwa la idadi ya watu duniani hususan katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania    ni muhimu mahitaji yao yakaenda sambamba na rasilimali zilizopo.

  “Nafahamu uelewa wa makampuni ya uchimbaji madini na utafutaji wa mafuta na gesi katika usimamizi na kutunzaji wa mazingira ni mkubwa, kwani tayari  kampuni hizo zina mpango wa usimamizi mazingira ambao umeeleza masuala yanayopaswa kuzingatiwa, lakini bado wanapaswa kuzingatia jambo hili wakati wote kutokana na umuhimu wa wake”, alieleza Mushi.

   Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Samwel Sitta (Mb) aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt . Mohamed Gharib Bilal, wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani, akimsikiliza  Mhandisi wa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Ephraim Mushi wakati alipotembelea banda la Wizara wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijini  Tanga.
   Wanafunzi kutoka shule za msingi mbalimbali jijini Tanga, wakiangalia madini ya ujenzi wakati walipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea  katika viwanja vya Tangamano jijiji Tanga.
   Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Mhe. Stephen Masele, akiongea jambo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

  After a successful event with Brooklyn, NY hip hop artist Yasiin Bey (Mosdef) in his first East African showcase, Nairobi Rapsody is back this Thursday (4th June) with Tanzania’s hip hop wordsmith -  FID Q.


  Welcome to Ebony Lounge from 10:00 p.m. (Thursday 4thJune) for an exclusive night with Coke Studio Africa season 3 artist: FID Q of the hit Bongo Hip Hop. He will be in Nairobi, Kenya hosting a Listening Party of his upcoming third album Kitaaolojia (Streetology) for the first time. The album is set for release in July.


  Kitaaolojia album is about what’s happening on the streets and inspires the youth to be in control of their lives. It features 10 songs including Ielewe Mitaa, Neno featuring Lord Eyez, Sihitaji Marafiki featuring Yvonne Mwale from Zambia, Siri ya Mchezo featuring Juma Nature, Bendera ya Chuma with Ben Pol and Bongo Hip Hop with the producer P Funk Majani. FID Q has also worked with BET Nominated Kenyan group Sauti Sol in a song that will feature in Kitaaolojia album.


  “The first album Vina Mwanzo Kati na Mwisho was about FID Q’s prose and writing. Propaganda was a political album.  Now Kitaaolojia edutaines. It highlights FID Q’s motive to help youth and the young people from the street to make sense of their lives,” said a statement from his management.


  Welcome to a chilled-out affair with the FID Q nicknamed “The Swahili Kid” by New York hip hop artist Fat Joe. Gates open at 8:00 p.m. Entrance Free. Good vibes. FID Q will also play some of his past songs from the other albums. He will be joined on the decks by Kenya’s DJ Finalkut.

  0 0

   Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akikata utepe kuzindua rasmi kisima cha maji kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa gharama ya sh. mil 56, katika Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Kushoto ni Diwani wa Kata hiyo, Karu Karavina na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (wa pili kulia).
   Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kushoto kwake) pamoja na Diwani wa Kata ya Kiparang'anda, Karu Karavina (kushoto) wakifurahi baada kukabidhi mradi wa  kisima cha maji kwa wananchi wa Kijiji cha Magoza, wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL gharama ya sh. mil. 56.

   Akina mama wakicheza kwa furaha wakati wa hafla ya kukabidhiwa kisima chas maji na TBL
   Ofisa Elimu Wilaya ya Mkuranga, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo,  Benjamin Majoya akimtwisha ndoo ya maji Mama mkazi wa Kijiji cha Magoza, Kata ya Kiparang'anda, wilayani Mkuranga, Pwani, wakati wa hafla ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kukabidhi msaada wa kisima cha maji kilichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 56 kijijini hapo. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza mapema leo jijini Dar na Waandishi wa habari, alieleza kuwa wataondoka jijini Dar kesho kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.
   Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisisitiza jambo zaidi kwa Waandishi wa habari, kuhusiana na ziara hiyo itakayoanza kesho.


  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anatarajia kuanza ziara ya siku 28 kesho katika mikoa mitatu ya Kagera, Geita na Mwanza kukamilisha mikoa yote 30 nchi nzima.

  Ziara hizo zenye malengo ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama zimekuwa na mafanikio kwa kuondoa matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi hasa wa mikoani.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, Katibu wa NEC-CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema wataondoka jijini Dar kesho asubuhi kwa basi maalumu, ambapo watasimama njiani katika mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida na mengineyo kwa ajili ya kusalimia wananchi.

  “Ziara rasmi itaanza June 4 katika Wilaya ya Nyakanazi mkoani Kagera, lakini kesho tutakunywa chai Morogoro chakula cha mchana tutakula Dodoma halafu tutasalimia wananchi katika Mikoa ya njiani kama Singida, Nzega na tumepanga kulala Kahama mkoani Shinyanga, tukiamka ziara ndio itaanza rasmi,” alisema Nape.

  Aliongeza kuwa katika ziara hiyo watatembelea majimbo yote ya uchaguzi hivyo amewataka wana-CCM na wananchi wengine kujitokeza kwa wingi kumsikiliza Katibu Mkuu katika ziara hiyo ya kihistoria.

  “Hii ni ziara ya kihistoria kwa sababu ya mambo matatu, kwanza tutatembelea visiwa vyote vya Ukerewe ambavyo ni nadra kutembelewa na viongozi, pili huu ni mwaka wa uchaguzi kuna masuala mengi yanahitaji ufafanuzi,” alisema.

  Akitaja ratiba ya ziara hiyo Nape alifafanua kuwa, “Kuanzia Juni 5 mpaka Juni 15 tutakuwa Mkoa wa Kagera, Juni 16 mpaka 21 tutakuwa Mkoa wa Geita na Juni 22 mapaka Julai 2 tutakuwa Mwanza kuhitimisha ziara ya nchi nzima kwa mkutano mkubwa wa kihistoria.”

  Akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu faida za ziara hizi Nape alisema kuna masuala mengi ya kimaendeleo yalisimama lakini alipopita Katibu Mkuu Kinana ufumbuzi umepaikana, akitolea mfano mashamba yaliyobinafsishwa bila kufuata utaratibu alisema Rais Jakaya Kikwete, amefuta hati nyingi za mashamba ya wawekezaji na kurudishwa kwa wananchi.

  “Kuna baadhi ya maeneo kulikuwa na zahanati zimeshajengwa lakini hakuna vibali, nimepata taarifa kuwa vibali vimeshapatikana na huduma zinaendelea, kulikuwa na matatizo ya ardhi za wananchi kuchukuliwa na wawekezaji katika maeneo ya Tanga, Arusha, Babati na maeneo mengine lakini kila kitu kipo sawa sasa na wananchi wanamshukuru Kinana,” alisema.

  Aliongeza kuwa, “Nisisitize kuwa tumesema tutaondoka na basi maalumu kwa sababu kama kuna mwingine atafanya hivyo atakuwa ametuiga, mkumbuke hili wazo la kuondoka na basi ni la Katibu Mkuu.”.
  Ikiwa ziara hizi zitamalizika salama Julai 2 mwaka huu, Kinana atakuwa Katibu Mkuu pekee wa CCM tangu kuanzishwa kwake Februari 5, 1977 kuzunguka nchi nzima kuangalia uhai wa chama na kusikiliza na kutatua kero za wananchi wote bila kujali itikadi za vyama.

  0 0

   Mratibu wa Programu ya kukuza Ajira zenye Staha Dar es Salaam, kupitia Elimu ya Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Dominic Ndunguru akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa program hiyo jana jijini Dar es Salaam. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
   Mshauri wa maswala ya Sera na Miradi ya Maendeleo wa Tanzania Youth Vision Association Bw. Elly Ahimidiwe Imbyandumi akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa kutathmini utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha katika jiji la Dar es Salaam (YEID jana katika ukumbi wa Kituo cha Vijana cha Don Bosco cha jijini Dar es Salaam.Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
   Afisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akielezea jambo wakati wa mkutano wa asasi za Vijana kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo  vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa asasi za vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mkutano wa asasi za Vijana uliofanyika jana jijini Dar es Salaam ili kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) mradi huo unalenga kuwajengea uwezo  vijana ili waweze kujiajiri na kuajirika. Programu hii inaendeshwa kwa ubia wa asasi za kiraia za Tanzania Youth Vission Associataion (TYVA), Open Mind Tanzania (OMT)  na Youth For Africa (YOA).
  Washiriki wa mkutano wa asasi za Vijana ILI kujadili utekelezaji wa Programu ya Kukuza Ajira zenye Staha jijini Dar es Salaam (YEID) wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Frank Shija, WHVUM

  0 0

  TFF YAZINDUA JEZI MPYA, TOVUTI.

  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.

  Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.

  Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.

  Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.

  Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
  Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
  Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
  Ndugu wageni waalikwa
  Ndugu waandishi wa habari
  Mabibi na mabwana
  Salam aleikum.
  Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.
  Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi  maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
  La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.
  Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
  FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194. 

older | 1 | .... | 857 | 858 | (Page 859) | 860 | 861 | .... | 3285 | newer