Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

Introducing: JOH MAKINI NEW MUSIC VIDEO - NUSU NUSU OFFICIAL


DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI

WAKUU WA WILAYA ZA KISHAPU NA SHINYANGA WATEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI MAONESHO YA SIDO KANDA YA ZIWA

0
0
Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa/kutengenezwa kutoka Viwanda Vidogo yaliyoandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo SIDO kanda ya ziwa yanaendelea katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga,watu mbalimbali wanafika kujionea mambo mazuri yanayofanywa na wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania.Leo jioni,Juni 01,2015 wakuu wa wilaya za Kishapu na Shinyanga wametembelea mabanda mbalimbali.Kilele cha maonesho hayo ni Juni 02,2015.

Hapa ni katika banda la Chuo cha VETA Shinyanga,wanafunzi wa chuo hicho wakionesha mtambo wa umeme wa jua na Tanesco kwa wakuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nkhambaku na wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Mwanafunzi wa VETA Asha Hamis akitoa maelezo namna ya kufanya shughuli mbalimbali kwa kutumia mitambo hii,hapa chini.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MWILI WA MAREHEMU MZEE SAMWELI NTAMBALA LWANGISA WAPOKELEWA BUKOBA, MAJONZI YATANDA KWA WANABUKOBA.

0
0
Gari maalum kutoka Nchini Uganda lililobeba Mwili wa Mzee Samwel Ntambala Lwangisa ukiingia Bukoba. Na Faustine Ruta, Bukoba
Mwili wa Marehemu Samuel Ntambala Luangisa uliwasili usiku wa kumkia leo katika Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera. Mauti yalimkuta akiwa Nchini Marekani na maziko yake itakuwa kesho jumatano june 3,2015. Wakati wa Uhai wake Marehe Samwel Luangisa aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa kwanza wa Mkoa wa Kagera (ukiitwa ziwa magharibi), Aliwahi pia kuwa mbunge wa Bukoba Mjini, Meya wa Bukoba na Diwani wa Kata ya Kitendaguro hadi mauti yalipomkuta.
Mtoto wa Marehemu Bi. Murungi
Kulia ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mh. Khamis Kagasheki.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
 

NMB Yadhamini Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

0
0
 Benki ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa Mwaka wa Makanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania bara ulioanza leo mkoani Mororogoro. 

Katika mkutano huo, NMB imeweka mabanda ya maonyesho yanayotoa elimu juu ya huduma mbalimbali zinazopatikana ndani ya benki ya NMB pamoja na kutoa huduma za papo kwa papo ambapo wajumbe wa mkutano huo walipata wasaa wa kufungua akaunti za chap chap pamoja na kupata huduma za NMB Wakala. 

Kwa huduma za NMB Wakala, wateja wa NMB wanaweza kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti zao za NMB bila ya kwenda kwenye tawi lolote la NMB.

Mkutano huo ulioanza leo, utafanyika kwa siku tano mpaka Ijumaa ya Tarehe 5, Juni, 2015.
Kamishna jenerali wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania bara - Pius Nyambacha akimsikiliza mfanyakazi wa benki ya NMB - Nehemiah Simba na akifafanua jambo wakati akieleza namna ya huduma ya kufungua akaunti ya NMB chapchap Instant account  mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania bara uliofanyika mkoani Morogoro leo.
 Meneja wa NMB kanda ya mashariki - Nazareth Lebbi akielezea jambo kwa Naibu Kamishna wa Utawala na Fedha jeshi la zimamoto na uokoaji - Billy Mwakatage na Mwakilishi wa mkuu wa wWilaya ya Morogoro - Ester Rugaira wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi hilo mkoani Morogoro.
Meneja wa  NMB kanda ya mashariki - Nazareth Lebbi akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani -  Mwamini Malemi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania bara uliofanyika mkoani Morogoro leo. katikati ni Kamishna jenerali wa jeshi hilo - Pius Nyambacha.
Kamishna Jenerali wa jeshi la zimamoto na uokoaji Tanzania bara - Pius Nyambacha akizungumza jambo na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Magereza - Dkt Kato Rugainunura wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa makanda wa jeshi hilo mkoani Morogoro. kulia ni Meneja wa NMB kanda ya mashariki - Nazareth Lebbi.

KISIWA CHA ZANZIBAR KUTOWEKA DUNIANI KUTOKANA NA ATHARI ZA TABIA NCHI-UTAFITI

0
0

mazingira 3Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, akielezea jambokwa wandishi wa habari (hawapo pichani) katika warsha hiyo juu ya 
mazingira

Na Andrew Chale, Nairobi, Kenya
Wataalamu wa kichunguzi na wanasayansi wa Mazingira, wameelezea kuwa visiwa vilivyopo ndani ya bahari ya Hindi vinatarajiwa kutoweka duniani kutokana na mabadiriko ya tabia nchi inayoikumba dunia kwa sasa ikiwemo upungufu wa kimo cha bahari, ukame na hali ya joto sehemu mbalimbali duniani.

Hayo yameelezwa jijini hapa katika mafunzo juu ya kuripoti habari za mazingira na mabadiriko ya tabia nchi (Climate Change) mafunzo yaliyoanza jana Juni 1, 201a5 ambayo ni maalum kwa wandishi wa habari wanaoandika katika mitandao ya kijamii blog na tovuti kutoka nchi mbalimbali za Afrika, zikiwemo Tanzania, Rwanda, Madagasca, Kenya na Ufaransa ambaoyo ni ya wiki mbili ambao pia ni mkutano wa maandalizi kuelekea katika kongamano la mazingira litakalofanyika jiji la Paris, Ufaransa, Julai na Desemba mwaka huu.

Akielezea hali hiyo, Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru, alibainisha kuwa, visiwa vingi ndani ya bahari ya Hindi ikiwemo Mombasa, Comoro na Madagasca vimo hatarini kutoweka kabisa duniani kutokana na tabia nchi (Climate Change).

“Utafiti mbalimbali umefanyika na kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Dunia itaingia katika matatizo makubwa. Hasa kwa upande wa bahari ardhi iliyo ndani yake kuja kumezwa ikiwemo visiwa vya Zanzibar, Madaga” alieleza Kabukuru ambaye pia ni mchambuzi na mtafiti wa masuala ya mazingira ya ukanda wa bahari anayefanya kazi zake nchini Kenya.

Kwa Tanzania tayari athari mbalimbali zimeanza kujitokeza kutokana na tabia nchi ambapo kwa sasa mmomonyomko wa radhi umeweza kukumba maeneo zaidi ya 148 ambayo yanaingia maji ya chumvi huku wakulima wakishindwa kuendelea na kilimo cha kawaida.

Mkutano huo ulioanza leo Juni Mosi, umeandaliwa na Media Coperation CFI kutoka nchini Ufaransa ulio na lengo la kutafuta njia mbadala juu ya kuripoti habari za mabadiliko ya tabia nchi kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Ufaransa Kenya na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kwa washiriki wa Tanzania,wanawakilishwa na Andrew Chale mtandao wa modewjiblog na Dotto Kahindi mwandishi wa habari wa kujitegemea.
mazingira2Wanahabari wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mchambuzi wa mambo ya mazingira katika ukanda wa bahari na mwandishi mwandamizi wa habari nchini Kenya, Wanjohi Kabukuru (Hayupo pichani) mafunzo hayo yanaendelea jijini Nairobi hadi Juni 11, mwaka huu.
DSC_0466Mwakilishi anayeiwakilisha Tanzania, Mwandishi mwandamizi wa mtandao wa MODEWJIBLOG.COM, Andrew Chale (kulia) akiwa katika mkutano huo... unaoendelea katika jiji la Nairobi.
wwwAfisa wa CFI, kutoka Paris, Ufaransa, Anne-Sophie Ricco akielezea jambo juu ya mkutano huo kwa wandishi wa habari wa tovuti na blog (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Safari Club, Jijini Nairobi, Kenya.

UTAFITI WA KISIASA ULIOFANYWA NDANI YA MANISPAA YA IRINGA WAMBEBA FRANK KIBIKI

0
0
Na Fredy Mgunda,Iringa
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Highland Zone Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya Mwanahabari ,  Frank Kibiki aliyetangaza nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa vijana,  wanawake, walemavu na wazee.
Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SHZER,  Patson William alisema utafiti huo umefanywa katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9, Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve 2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya kazi.
Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni, Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga, Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka 2010.
Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo, litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema
       frank kibiki akiongea na wananchi stand kuu ya mabas iringa
 
wananchi wakimsikiza frank kibiki  alipokuwa maeneo ya stand kuu

Pof.Muhongo kutangaza nia leo.

0
0
Leo ni zamu ya Profesa Sospeter Muhongo kutangaza nia ya kuombwa kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kurithi mikoba ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Profesa Muhongo anatangaza nia yake leo Mjini Musoma, kwenye Ukumbi wa Open University Hall, kuanzia saa 10 jioni.

ALI KARUME AJITOKEZA KUGOMBANI NAFASI YA URASI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

0
0
 Balozi Ali Karume akisalimiana na makada wa chamacha Mapinduzi mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya  Halmashauri  Wilaya ya  kati Dunga Zanzibar kwa ajili ya kutangaza nia ya kutaka kugombania nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Baadhi ya makada walio shirika katika kumuunga mkoko mgombea   Uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzaniakatika Ofisi ya  Halmashauri  Wilaya ya  kati Dunga  Zanzibar.
Balozi Ali Karume akiwahutubia wananchi waliofika hapo ili kujuwa lengo lake la kugombea nafasi ya Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania huko Ofisi ya Halmashauri Wilaya ya kati Dunga Zanzibar. PICHA NA MIZA OTHMAN -HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

EAC ESTABLISHES YOUTH CLUB, ENGAGES UNIVERSITY STUDENTS ON REGIONAL INTEGRATION

0
0

EAC Secretariat enhances awareness on regional integration at Tumaini University Makumira (TUMa) and launches an EAC Youth Club at the Institute of Accountancy Arusha (IAA)

East African Community Secretariat, Arusha, 1 June, 2015: In its effort to take the integration agenda closer to the students' community in Arusha, the Headquarters of the Community, the EAC Secretariat participated in the 'Youth to Cooperate World Forum' held at TUMa over the weekend. This event gave the Community a firm platform to engage and interest students in advocating for regional integration initiatives.

The Forum brought together over 1,000 university students from six different universities in Arusha. Apart from the Community's outreach, students were also stimulated on insightful topics on education, self-leadership, soft skills and business development techniques, all of which to prepare them for life after graduation.

"By involving the youth in regional integration, we will not only be increasing their capacity on the (integration) process, but will also be providing the East African region with a pool of competent and talented young men and women equipped to carry out the work of the Community,"said Mr. Owora Richard Othieno, Head of EAC Corporate Communications and Public Affairs."We're looking forward to establishing more Youth Clubs around the country and to working closely with other higher institutions in order to reach our goals," he said. 

As a way of pushing the integration agenda even further, the EAC, together with joint efforts from the EAC Youth Ambassador to Tanzania and Institute of Accountancy Arusha (IAA) faculty members, launched an EAC Youth Club at IAA campus also over the weekend.

Bringing together over 100 students to this memorable event, the newly established Club will provide students with a caring and supportive environment for access and inclusion to regional sensitization and educational activities on the EAC. 
Alice Maro, EAC Communications Expert presenting an overview of Regional Integration to IAA students.
 Group photo with IAA students and faculty staff to consecrate the launch of the EAC Youth Club at IAA campus.
 Wide-eyed TUMa students attentively listening to EAC presentations on Regional Integration.
 Raymond Maro, First EAC Youth Ambassador to Tanzania talking to TUMa students about the benefits of the EAC Youth Ambassadors Platform (YAP).

KISHAPU YAFANIKIWA KUPUNGUZA ATHARI ZA UKAME

0
0
 Mkazi wa kijiji cha Masanga wilayani Same, Magreth William akiwaangalia mbuzi wake aliowapata kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia mradi wa Kupunguza Athari za Ukame unaofadhiliwa na UNICEF,  tarehe 2, Juni 2015.
Mkaguzi Hesabu za Serikali, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu Hesabu za Serikali nchini, (kushoto), Jacob Ndaki  akimsikiliza Mkulima wa mtama, kijijini Masanga wilayani Kishapu, Magreth William (kulia ) wakati wa ufuatiliaji wa utekelezaji mradi wa Kupunguza Athari za Ukame unaoratibiwa na  Ofisi ya Waziri Mkuu, (katikati) ni Mratibu maafa wilayani Kishapu, Posian Kuhabwa,  tarehe 2 Juni,  2015.

Halmashauri ya wilaya ya Kishapu imefanikiwa kupunguza athari za maafa yanayotokana na ukame kwa kutekeleza vyema mradi  wa kujengea jamii uwezo wa kukabili maafa ya ukame unaoratibiwa na Ofisi ya waziri mkuu,  idara ya uratibu maafa.

Mradi huo wenye  kauli mbiu “Athari za Ukame zinapunguzika jamii husika ikijengewa uwezo”, umetekelezwa wilayani humo kwa mafanikio katika kata ya Mwamalasa, Masanga na Langana kutokana na vikundi vya maendeleo kumi (10) kufanikisha ufugaji wa   Mbuzi na kuku, kilimo cha viazi, mtama, mboga mboga pamoja na upandaji wa miti kwa  uhifadhi wa mazingira.

Akiongea  wilayani humo mara baada ya kuiongoza timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya waziri Mkuu inayofuatilia utekelezaji wa mradi huo tarehe 2 Juni, 2015, Mratibu maafa Wilayani Kishapu, Ponsian Kuhabwa amefafanua kuwa kwa kutumia vikundi vya maendeleo katika kata husika kwa utekelezaji, kata hizo zimefanikiwa kupata uhakika wa chakula na kipato, hali ambayo huzifanya kata hizo kutoathiriwa na ukame.

Kuhabwa; “Kikundi cha Mazingira kata ya Masanga  chenye  watu 10, kupitia mradi huu kinao mbuzi 200, kuku 200  ikiwa awali walipatiwa mbuzi 50 na kuku 50 kwa ajili ya kuanza ufugaji, lakini pia kikundi hiki kinayo mashamba ya mtama, viazi lishe na bustani za mboga mboga hali inayo ifanya jamii inayotekeleza mradi huu kufanikiwa kupunguza athari zitokanazo na ukame ”.

Akiongea na timu ya wataalamu hao, mkazi wa kijiji cha Masanga, kata ya Masanga, wilayani Kishapu, Magreth William, amefafanua kuwa ukame uliokuwa ukiikumba kata hiyo mara kwa mara, walikuwa wanapata athari za upungufu wa chakula pamoja na kutokuwa na kipato kutokana na mazao yao ya biashara kuharibikia mashambani.

William; “Tumeweza kupunguza athari za maafa ya ukame kupitia mradi huu kwa kuwa tunaouhakika wa chakula kwa kuwa tunalima mazao yanayo himili ukame kama mtama na viazi lishe lakini pia tunao uhakika wa kipato kwa kuwa tunafuga mbuzi na kuku hivyo pamoja na ukame unaendelea kujitokeza lakini kwa sasa hatuathiriki kama awali”.

Mradi wa Kuijengea Jamii Uwezo wa Kupunguza Athari za Maafa kwa Mikoa iliyoathirika zaidi na ukame unafadhiliwa na Benki ya Dunia na kusimamiwa na UNICEF chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri husika wakiwa Watendaji wakuu wa mradi huo. Mradi huo unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18, ulizinduliwa wilayani  Same, mkoani Kilimanjaro tarehe 11 Desemba, 2013.  

WATANZANA WAASWA KUTUNZA NA KUTHAMINI MAZINGIRA

0
0
002
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Binilith Mahenge akimkaribisha mgeni Rasmi ili aweze kuzindua maadhimisho ya wiki ya Mazingira duniani katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
001
Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Julius Ningu akitoa maelezo kwa mgeni Rasmi Mheshimiwa Samuel Sitta alipotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira jijini Tanga. Wengine wanaosikiliza ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh. Dkt Binilith Mahenge (kulia) na Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan (kulia).
Watanzana wametakiwa kutunza na kuthamini mazingira kwa sababu ni urithi wa thamani kubwa sana kwa kizazi cha sasa na kijacho. Hayo yamesemwa na Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya siku ya mazingira Duniani, Mheshimiwa Samuel Sita- Waziri wa Uchukuzi ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Mohammed Gharib Bilal.
Akiongea na Wananchi katika viwanja vya Tangamano vilivyopo katika jiji la Tanga Mheshimiwa Sita amesisitiza juhudi zaidi katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kuwaomba Wazazi kuelemisha watoto wao umuhimu wa kuthamini mazingira. Aidha amewapa hongera Wananchi na Viongozi wa jiji la Tanga kwa kutilia mkazo usafi wa mazingira na kufanya jiji hilo kuibuka mshindi wa tatu katika mashindano ya usafi wa mazingira kitaifa.
 Akimkaribisha Mgeni Rasmi ili kufungua sherehe hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Binilith Mahenge aliesma ni jukumu la kila mmoja kutunza na kuhifadhi mazingira hivyo basi kila Mwananchi ajitahidi katika hilo. 
Siku ya mazingira duniani hufanyika kila tarehe tano ya mwezi Juni kila mwaka. Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ndoto bilioni saba, dunia Moja , tumia Rasilimali kwa uangalifu. Hii ikimaanisha kutumia vema rasilimali zetu ili kutunza vema mazingira yetu.

KAMISHNA WA MADINI AZITAKA TAASISI ZA MAZINGIRA NCHINI KUONGEZA USHIRIKIANO KWENYE MIGODI

0
0
Na Greyson Mwase, Bagamoyo
Taasisi zinazohusika na usimamizi wa sheria na kanuni za mazingira zimetakiwa kushirikiana kwa karibu zaidi ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa mazingira migodini na kuepuka mwingiliano wa majukumu.
Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi wa Madini – Ukaguzi wa Migodi Mhandisi Ally Samaje katika mahojiano maalum kwenye mafunzo yanayohusisha Makamishna Wasaidizi wa Madini, Wakaazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini Tanzania na wataalam kutoka India yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.
Mhandisi Samaje alitaja taasisi hizo kuwa ni pamoja na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii (Misitu) na kuongeza kuwa taasisi hizo zimekuwa zikishirikiana katika masuala muhimu yahusuyo madini hususan katika masuala yenye kuhitaji uelewa wa pamoja.
 Wakati huo huo akizungumza kwa kutumia mfano wa nchi ya India, mtaalam mwelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India, Sujit Kumar alisema kuwa India ina taasisi nyingi mbalimbali zinazohusika katika usimamizi wa kanuni na sheria za mazingira hali inayopelekea ugumu katika usimamizi wa sheria na kanuni hizo.
“ Matokeo yake kila taasisi inaona kuwa sheria na kanuni zake za mazingira ni bora na sahihi na kuwataka wawekezaji wa madini kuzifuata, hivyo kupelekea ukaguzi wa migodi kuwa mgumu.” Alisisitiza Singh.
 Naye mtaalam muelekezi kutoka Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akizungumzia jinsi ya kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kutumia mfano wa nchi ya India alisema kuwa ili wachimbaji wadogo waweze kufanikiwa kupata leseni wanatakiwa kuunda vikundi vidogo vidogo na kuomba leseni ya pamoja na kuanza kumiliki vitalu.
Banerjee alishauri serikali kuendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kuwapatia ruzuku kwani wana mchango mkubwa sana katika pato la nchi kupitia sekta ya madini.
 Alisisitiza kuwa elimu ni muhimu kwa wachimbaji wadogo kwa kuwa wengi hawana elimu hali inayopelekea kuchimba katika mazingira hatarishi na kutokea kwa ajali za mara kwa mara migodini.
 Ili kuhakikisha kuwa wananchi waishio karibu na migodi wananufaika na rasilimali za madini, Banerjee alipendekeza kuanzishwa kwa mifuko ya madini ambapo fedha zinazolipwa kama kodi na wawekezaji zitawanufaisha wananchi wote.
 Alisema kuanzishwa kwa mifuko itakayowanufaisha wananchi kutachochea maendeleo katika ngazi ya halmashauri na wananchi kuondokana na dhana kuwa hawanufaiki na rasilimali za madini.
 Aliongeza kuwa fedha hizo zinaweza kutumika katika uboreshaji wa huduma za jamii kama vile maji, umeme, miundombinu, afya pamoja na kusomesha wakazi kupitia elimu za madini.1
Mijiolojia wa Wizara ya Nishati na Madini, Assa Mwakilembe akizungumzia sekta ya madini  nchini kabla ya kumkaribisha  Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje  ili aweze kufungua mafunzo kwa wataalam wa Wizara. Mafunzo hayo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini  na kufanyika Bagamoyo mkoani Pwani, yanatolewa na Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka  India, lengo likiwa ni kubadilishana  uzoefu na kuwapa uelewa katika usimamizi wa mazingira kwenye migodi.2
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini akifungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi kutoka Ofisi za Madini Nchini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.3
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa kwanza kushoto, waliokaa mbele) pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka  Taasisi ya  Sayansi na Mazingira kutoka Nchini India (hawapo pichani) katika mafunzo kuhusu usimamizi wa mazingira migodini yanayoendelea mjini Bagamoyo mkoani Pwani.4
Sehemu ya wataalam kutoka Idara ya Madini iliyopo chini ya  Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini mada kuhusu usimamizi wa mazingira kwenye migodi katika nchi  ya India iliyokuwa inawasilishwa na mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh (hayupo pichani) kwenye mafunzo  hayo.5
Mtaalam kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Srestha Banerjee akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.6
Mtaalam mwelekezi kutoka  Taasisi ya Sayansi na Mazingira ya Nchini India, Sujit Kumar Singh akisisitiza jambo katika mafunzo hayo.7
Kamishna Msaidizi – Ukaguzi wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje kutoka  Wizara  ya Nishati na Madini (wa tatu kutoka kushoto, waliokaa mbele), Mkuu wa Kitengo cha Mazingira kutoka Wizara  ya Nishati na Madini,Mhandisi  Gideon Kasege ( wa pili kutoka kulia, waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo  hayo.

TANGAZO LA KIFO

0
0

unnamedKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja anasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara kuanzia Mwaka 1996 hadi 2002, Onel E. Malisa kilichotokea leo Alfajiri tarehe 2 Juni, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dares Salaam.
Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Familia ya Marehemu linaendelea kuratibu taratibu zote za kuaga na mazishi ya marehemu. Hivi sasa msiba upo nyumbani kwake Kinyerezi, Jijini Dar es Saalam. Aidha taarifa kamili kuhusiana na msiba huu mtaendelea kufahamishwa baada ya mipango yote kukamilika.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi;
AMINA

KAMPENI YA KUTOKOMEZA MARADHI YA FISTULA YATUA WILAYANI UVINZA

0
0
 Umati wa wakazi wa kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Kigoma wakiwa kwenye mkutano wa  kampeni ya kutoa elimu kuhusiana na maradhi ya  Fistula yanayowakabili wanawake hapa nchini,Kampeni hiyo inayoendeshwa na Hospitali ya CCBRT kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation  inaendelea kufanyika katika mikoa mitatu kuwasisitiza wakina baba kuwaruhusu wakina mama wajitokeze  ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni  wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua.
 Wakazi wa Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma wakimsikiliza kwa makini  Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon (wapili kutoka kushoto ) alipokuwa akiwafafanulia jambo wakina baba hao kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha  wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze  ili wakatibiwe maradhi fistula kwani yanatibika,Inakadiriwa ni  wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.
 Meneja  Mawasiliano wa Hospitali ya CCBRT Abdul Kajumul , akiwaelezea wakazi wa kata ya Nguruka  Wilaya ya Uvinza  Kigoma waliofika kwenye mkutano na kupatiwa elimu kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha  wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze  ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika,Inakadiriwa ni  wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.
Msanii wa nyimbo za kiasili na Balozi wa maradhi ya Fistula Mrisho Mpoto akitoa elimu kwa wakazi wa Kata ya Nguruka wilaya ya Uvinza Kigoma,Kuhusiana na kampeni inayoendelea katika mikoa mitatu nchini ya kuelimisha  wakina baba na wanchi kwa ujumla kuwaruhusu wakina mama wajitokeze  ili wakatibiwe maradhi ya fistula bure katika hospitali ya CCBRT kwani yanatibika,Inakadiriwa ni  wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo  wanapojifungua.Kampeni hiyo inaendeshwa na CCBRT na Vodacom Foundation.

Dk.Shein aelekea nchini Ujerumani leo kwa ziara ya kikazi

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati wakiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume leo wakati akiondoka chini kwa ziara ya kikazi nchini ujerumani pamoja na Ujumbe wa Viongozi mbali mbali.[Picha na Ikulu,Zanzibar.]

HOTUBA YA PROFESA MARK JAMES MWANDOSYA ALIYOITOA WAKATI WA KUTANGAZA NIA YA KUNGOMBEA NAFASI YA RAIS MKOANI MBEYA

KILELE CHA MAONESHO YA VIWANDA VIDOGO KANDA YA ZIWA (SIDO) YAFANYIKA MKOANI SHINYANGA

0
0
Moto ukiwa unawaka katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Juni 2,2015 ndiyo kilele cha maonesho ya bidhaa za viwandani kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na shirika la Viwanda Vidogo nchini SIDO.Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ndiye aliyefunga maonesho hayo yaliyodumu kwa siku 5 yakihusisha wajasiriamali 260 kutoka ndani na nje ya Tanzania. 

Kabla ya kufunga maonesho hayo ambayo yamefanyika mkoani Shinyanga,mkuu wa mkoa huo Ally Rufunga alitembelea mabanda mbalimbali. Malunde1 blog,ilikuwepo eneo la tukio,mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha zifuatazo.......
Mwanafunzi Asha Hamis kutoka chuo cha VETA Shinyanga akipanda kwenye mtambo unaitwa Loader na kuonesha utaalam wake wa kufanya kazi kwa kutumia mtambo huo,baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kutembelea banda la chuo cha VETA
Mwanafunzi wa  chuo cha VETA akiendesha mtambo katika viwanja vya Shycom leo Juni 02,2015
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akimpongeza mwanafunzi wa VETA Asha Hamis  aliyeendesha Loader na  mwenzake Jafari ( katikati) aliyeendesha Greda  hapo uwanjani
Mkuu wa mkoa akiwa na vijana wa VETA ambao ni wataalam wa kuendesha magreda na Loader
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

HUU NDIO UTEUZI WA WAJUMBE WAPYA WA BODI YA WAKURUGENZI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)

MH.SITTA AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI WA BANDARI YA TANGA,WAELEZA CHANGAMOTO ZAO.

0
0
 Mhe Samuel Sitta akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi mkuu Ndg Awadh Massawe.
 Mhe Samuel Sitta pia alipata fursa kuongea na wafanyakazi wa Bandari ya Tanga ambapo walieleza changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao ikiwepo kodi inayokatwa kwenye mishahara ni kubwa ukilinganisha na kipato na  Pia Mhe Sitta ameteua wajumbe wapya wa bodi ya bandari
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images