Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

KIWANDA CHA PAMBA AMBACHO PAMBA YAKE ILITEKETEA KWA MOTO MKOANI SHINYANGA CHAPATA BIMA YAKE TOKA UAP

$
0
0
Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Bima ya UAP wakiwa na Meneja wa Kiwanda cha JIELONG Holdings Tanzania LTD Kiki Huwa Xu (kushoto) wakitenbelea kiwanda hicho kujionea shughuli za utendaji ikiwa ni pamoja na kuzungumza na uongozi wa kiwanda hicho mara baada ya kukipatia bima ya shilingi milioni themanini (80,000,000/=)  kufuatia kuunguliwa na pamba yake katika ghala la kuhifadhia lililopo kiwandani hapo.
Mwanzoni mwa mwaka huu 2015 pamba iliyokuwa imehifadhiwa kwenye moja ya maghala katika kiwanda cha pamba JIELONG Holdings Tanzania LTD iliungua na kuharibika kabisha mara baada ya kuhifadhiwa kwa muda mrefu hali iliyosababisha pamba hiyo kuchemka na kuwaka moto.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MKUYA KUZINDUA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA PPRA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Saada Salum Mkuya anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 10 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) yatakayofanyika Mei, 19 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga, amesema lengo la maadhimisho ni kukutanisha wadau wa manunuzi ya umma nchini kujadili mafanikio katika udhibiti wa manunuzi ya umma na changamoto wanazokabiliana nazo katika sekta hiyo.

Lumbanga amesema katika maadhimisho hayo kutafanyika warsha maalum ya wadau wa habari ambao ni waandishi ,wahariri wawakilishi wa kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) pamoja na Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) itakayofanyika Mei 18 ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amewataja wahusika katika uzinduzi wa maadhimisho hayo kuwa ni Wakandarasi,Wataalam wa Ushauri,Watoa Huduma katika sekta hiyo,Wagavi na Taasisi Nunuzi ,wanasiasa asasi za kiraia wanataaluma, wanafunzi wanaosomea taaluma ya manunuzi pamoja na wananchi kwa ujumla.

Lumbanga amesema katika maadhimisho hayo Mei 20 itakuwa ni maalumu kwa wadau wa manunuzi kutoka Halmashauri zilizoko katika Mikoa ya Dodoma,Pwani,Tanga,pamoja na Kigoma ikiwa ni mpango wa kuzijengea uwezo wa manunuzi chini ya miradi inayofadhiliwa na serikali ya Ubelgiji.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Miaka 10 ya PPRA,Tumethubutu ,Tumeweza ,Tushirikiane kuboresha zaidi manunuzi ya Umma, hivyo wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano chanya katika kuzuia upotevu wa fedha za umma kwenye manunuzi yasiyo na tija.
Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Balozi Dk. Matern Lumbanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandimisho ya miaka 10 ya PPRA katika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam leo, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Laurent Shirima.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA leo jijini Dar es salaam. Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Vijana wametakiwa kukopa na kurudisha marejesho kwa wakati

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh.Norman Sigala King aliyesimama akiongea na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma akifungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana (hawapo pichani) ya kujikomboa kiuchumi yanayotolewa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,wa kwanza kutoka kushoto ni KaimuMkurugenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria Bi. Ester Riwa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo aliyesimama akitoa mada ya ujasiriamali kwa Vijana wa Halmashauri Songea wakati Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara ya mafunzoa ya kujikomboa kiuchumi Mkoani Ruvuma.

Kumbukumbu ya Amina Ngaluma kufanyika Jumamosi jijini Dar

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

KISOMO cha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwimbaji mahiri nchini, marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’ kinatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Kitunda, Machimbo Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili, baba mzazi wa marehemu,  Kassim Ngaluma, alisema kisomo hicho kitafanyika nyumbani kwa wazazi wake marehemu na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali wa marehemu wakati wa uhai wake wahudhurie.

“Tunaomba wote tulioshiriki kwa namna mbalimbali wakati wa msiba wa marehemu mwanangu, tushirikiane pia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake,” alisema Mzee Ngaluma na kuongeza kuwa kisomo hicho kitafanyika saa saba mchana baada ya swala ya adhuhuri.

Aliwaomba waliokuwa wanamuziki wenzake na marehemu, mashabiki wake, pamoja na wadau wengine wa muziki na marafiki wote, washirikiane katika tukio hilo.

Ngaluma aliyepata kung’ara na bendi mbalimbali nchini, alifariki dunia Mei 15 mwaka jana kwa shinikizo la damu akiwa Thailand alikokuwa akifanya shughuli za muziki katika bendi ya Jambo Survivor na kuzikwa Mei 24 mwaka huo, Dar es Salaam.

Wakati wa uhai wake alitamba na bendi mbalimbali zikiwemo African Revolution ‘Tamtam’,  Double M Sound ‘Mshikemshike’ na TOT Plus zote za Dar es Salaam.Pia alipigia makundi ya Arusha Sangoma, Sayari Band na Less Mwenge yote ya Arusha na Mangelepa na Sky Sound za Kenya.

Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake ni Manyanyaso Kazini na Mapendo alizotunga akiwa Tamtam, wakati Double M Sound alitunga nyimbo za Wajane na Ukewenza.Pia alitoa albamu yake binafsi iitwayo Jitulize.

Baadhi ya nyimbo alizopata kuimba na kumpatia umaarufu mkubwa ni Mgumba, Maisha Kitendawili,  Ndugu Lawama, Zawadi ya Watanzania, Ugumu wa Maisha na Call Box zote zikitungwa na Muumin Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’.

WAZIRI WA FEDHA ZANZIBAR ASOMA BAJETI YA FEDHA YA MWAKA KWA MWAKA 2015/16 LEO

$
0
0
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee akionesha Mkoba wa Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee akisoma Hutuba ya Mapato na Matumizi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee aliyokuwa akiisoma kuhusu Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Waalikwa walioshiriki wakifuatilia Hotuba ya Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee aliyokuwa akiisoma kuhusu Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 leo katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

EAC SUMMIT DISCUSSES THE SITUATION IN BURUNDI 13TH MAY 2015

BAMAGA -AFRIKA SANA SINZA TAABAN KWA MAFURIKO.!

$
0
0
Pichani ni sehemu ya barabara kutoka Bamaga kuelekea Afrikasana Sinza jijini Dar ikiwa hoi bin taaaban baada ya kufunikwa na maji kufuatia mvua ambazo zimekuwa zikiendelea kunyesha jijini,aidha mafuriko hayo yamekuwa yakisababishwa pia na mitalo mingi ya eneo hilo kuzibwa na takataka zinazotupwa holela,matokeo yake maji yamekuwa yakikosa muelekeo.Idara husika wanapaswa kulifanyia kazi ipasavyo eneo hilo kwani limekuwa ni kero kubwa kwa wanaotumia barabara hiyo kila wakati kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.
 Hali halisi ndio hivi mvua ikinyesha jijini Dar,kwa eneo la Bamaga.
Maji yakiwa yametuama tuliiii eneo la bamaga kuelekea Afrikasana

MWENYEKITI WA VUGUVUGU ZA KUMPINGA RAIS WA BURUNDI AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI USIKU HUU SERENA HOTEL JIJINI DAR

$
0
0
Mwenyekiti wa vuguvugu za Maandamano Burundi kwa Mara ya kwanza amefika Nchini Tanzania ili kuweza kushuhudia Mkutano wa Dharula kati ya viongozi watano kuhusu nchi ya Burundi ambayo sasa imeingia katika machafuko baada ya Rais aliyeopo Madarakani kutaka kuongeza muda wake.

Akiongea na Waandishi wa Habari usiku huu Mkuu huyo wa vuguvugu wa Burundi amesema kuwa wananchi hawaridhiki na Rais wao kuendelea kuwa madarakani ambapo hata sheria hairuhusu na pia sasa ni wiki ya tatu ambapo wananchi wanaendelea kupinga Rais kuendelea kuwania kwa Muhula wa Tatu.

Amezungumzia juu ya waandamanaji  baada ya wiki tatu bado wapo barabarani ambapo wameweza kuwa ni kiungo, wameweza kuwa ni njia kwa sababu wanadai kumekuwa na mabadiriko kuhusu Rais wao, na kuwashukuru waandamanaji hao kwa kuonesha moyo wa uzalendo na kuwa wameweza kudhihilisha na kuwa walikuwa ni watulivu na kutulia kungoja utekelezaji wa mambo ambayo yamezungumziwa.

Amesema kwamba anaomba vurugu hizi zipate kwisha ambapo watu zaidi ya laki mbili wamekimbia nchi na anaomba vurugu ziishe ili wapate kurejea nchini kwao.

Pia ameiomba Jumuiya ya kimatafa iweze kufuatilia kwa karibu hali inayoendelea kwa sasa  Nchini Burundi ambapo jumuiya hiyo tangia zamani imeweza kusimamia mambo ya usalama nchini Burundi na amani ili Burundi iweze kufikia malengo ya Mkataba wa amani wa Arusha na kufikia malengo ya katiba ambayo ndio uti wa mgongo wa taifa hilo.

Kuhusu jaribio la Mapinduzi kiongozi huyo amesema hayupo Miongoni mwa wale ambao wameandaa tukio hilo 

Kuhusu jambo baya alilofanya Rais wa Burundi Kiongozi huyo amaesema kwamba ni kuongezea Muhula wakati tayari alisha tawala kwa Miaka 10, na katika miaka hiyo alishindwa kuweka usawa baina ya warundi, hajatekereza swala la haki za Binadamu , aliongeza kuwa Muhula wake ni Haramu hauko sambamba na Katiba wala Sheria ya Burundi pamoja na Mkataba wa Arusha na angetekeleza yote hayo hizi vurugu zisinge kuwepo.

 Pia hata makubaliano ya Arusha yanasema hakuna Rais ataenda Mihula mitatu. Pia warundi wanafanya hivyo kwa sababu hawataki shuhudia tena Damu inamwagika.

Mwisho amewaomba Marais watano wamalize salama Mkutano na kuhakikisha maamuzi yote yanafanyiwa kazi.

Nae Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa amewashukuru kwa uvumilivu wao na kuendelea kupinga Rais wao kuendelea kuwa madarakani kwa awamu ya Tatu. 
 Mwenyekiti wa Vuguvugu kutoka nchini Burundi Bw. Mugwengezo Chauvineau akiongea na waandishi wa Habari Usiku huu Serena Hotel Dar.
 Dr. Christine Mbunyingingo Mwenyekiti wa wanawake na wasichana katika harakati za usawa nchini Burundi, Akiongea na waandishi wa Habari usiku Huu. 
Kikao Kikiwa kinaendelea usiku Huu.

SWAHILI BLUES BAND WAKANDAMIZA VILIVYO KATIKA TAMASHA LA DOADOA

$
0
0

Mkamuzi yalikuwa siyo ya kitoto kama unavyoona kwenye picha
 Watu wakiserebuka mwanzo mwisho

Leo Mkanyia Ang'aa katika Tamasha la DoaDoa

Baada ya ziara ya mafanikio katika jiji la maraha la Nairobi, kundi zima la Swahili Blues Band chini ya uongozi wa Leo Mkanyia walielekea mjini Jinja Uganda kushiriki katika Tamasha la muziki la DoaDoa.
Tamasha la DoaDoa ni maalumu kwa wanamuziki kutoka Afrika ya Mashariki kushiriki na kutambulishwa kwenye jukwaa la kimataifa. DoaDoa wanatoa fursa mahsusi kwa wasanii hao kuonyesha kazi zao kwa wadau mbalimbali wa kimataifa wa muziki pamoja na wapenzi kutoka nchi husika.
Baadhi wa wadau wakimataifa walioshiriki ni pamoja na wawakilishi kutoka Songlines Magazine(UK), Sheer Publishing(Ethiopia), Visa for Music(Morocco), Selam festival(Ethiopia/Senegal), Sarakasi Trust(Uholanzi), Sound Diplomacy(UK) na ONGEA(Australia/Kenya).
Vikundi vilivyo shiriki vilijumuisha pamoja na Leo Mkanyia and Swahili Blues Band, Nandujja(Uganda), Abeneko(Tanzania), Octave Band(Kenya), Strong Voice Band(Rwanda), Jemimah Sanyu(Uganda), Idi Masaba(Uganda), H_Art the Band(Kenya), Moutcho(Burundi) na Makadem(Kenya).
Tamasha hilo lilifanyika kati ya tarehe 6 hadi 9 May 2015 na Swahili Blues Band walipanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 8 majira ya saa nne kamili usiku.
Walirusha karata yao ya kwanza kabisa kupitia kibao chao maarufu kinachojulikana kama "Afrika". Afrika inayopigwa katika mirindimo mahsusi ya Blues, ina mashairi yaliyojaa dhana ya kizalendo na kimapinduzi. Katika wimbo huu Leo aliyepiga gitaa na kuongoza uimbaji, alihamasisha hadhara yote kuwa bara la Afrika siyo bara la migongano na migogoro wala vita bali ni bara la amani lililoshereheshwa na ngoma pamoja na muziki. Wadau waliohudhuria walikunwa vilivyo pale Leo alipowahamasisha wadau kusema Hapana kwa Boko Haram na Al Shabaab.
Baada ya wimbo huo uliomithiri ya hotuba kutoka kwa mwanadiplomasia aliyebobea, Leo aliamua kuwarudisha wapenzi wote katika vitongoji vya Jiji la Dar es Salaam pale aliposhusha kibao chao cha Mdundiko. Ndani ya kibao hicho, bendi haikuhitaji steji shoo kwani kadamnasi ilivamia jukwaa na kunengua mdundiko vilivyo.
Kibao cha tatu kilitii kiu ya wadau wanaozungumza lugha ya kifaransa waliohudhuria kama vile vile kutoka nchi za Ufaransa, Burundi, Algeria na Senegal. Kibao hicho kinaitwa "Mon Ami".
Baada ya Mon Ami, wapenzi wa rhumba la asili lililojaa mirindimo ya ngoma za asili kutoka makabila ya Kitanzania walipewa ladha hiyo kupitia kibao kinachoitwa Moro Moro.
Moro Moro ilipoisha, ukawa muda mwingine wakupata Blues pale bendi ilipongurumisha kibao kingine maarufu kinachoitwa "Wazazi Wangu". Katika kibao hiki Leo na baba yake mzazi Henry Mkanyia walibishana vilivyo katika magitaa pale kila mmoja wao alipocheza solo kwa kupishana. Wapenzi walidataje?
Ngoma iliyomaliza shoo siku hiyo iliwarudisha wapenzi kwenye viunga vya kizaramo pale "Shikandwambwe" ilipotupwa hewani. Jukwaa halikutosha maana wadau mbalimbali walijialika ili kuonyesha vimbwanga vyao vya kucheza mirindimo hiyo kutoka kabila maarufu la Wazaramo. Leo aling'aa kwa mara nyingine pale alipoweka gitaa pembeni na kuchukua kinanda cha mdomoni "harmonica" na kuwakumbusha wadau jinsi mwanamuziki mkongwe Stevie Wonder alipoanza maisha yake marefu ya muziki.
Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kuongea na meneja wa Leo Mkanyia ofisi ya Ulaya na America bwana Samia X na kumuuliza ni nini mipango yao baada ya Tamasha hili. Akiongea katika kiswahili fasaha na kilichonyooka Samia X alijibu; Baada ya Tamasha la DoaDoa, bendi itarudi katika uwanja wa nyumbani wa Hoteli ya nyota tano ya Serena Dar es Salaam. Na mipango thabiti inaendelea ili kuratibu ziara ya bendi katika bara la Ulaya kwenye kipindi kijacho cha majira ya joto. Alimalizia Samia X.

WIZARA YA FEDHA YAWAPA SEMINA WAANDISHI WA HABARI JUU YA MRADI WA MABORESHO YA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

$
0
0
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma akifafanua jambo wakati wa warsha ya siku tano kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli Njuweni Kibaha. Bi.Ingiahedi alisema kuwa Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Alisema kuwa Mpaka sasa mradi huo umepata mafanikio makubwa hasa ya  kuweka mfumo mzuri wa malipo, muda wa kupitishwa kwa bajeti ya Taifa umeimarika na fedha zinatoka kwa  wakati,Alibainisha kuwa bajeti ya mwananchi inatangazwa katika Tovuti ya Wizara ya fedha na kuwa mfumo wa malipo umefika mpaka katika Serikali za Mitaa.
Washiriki wa warsha kuhusu maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakiwa katika warsha ya siku tano kuhusu kuhusu mradi wa maboresho ya matumizi ya fedha za umma inayoendelea katika Hoteli ya Njuweni Kibaha. 

===========  =======  ========
Serikali ya Tanzania ilianzisha mradi huo kwa madhumuni ya kuimarisha mifumo ya matumizi ya fedha katika ngazi zote.  Mradi huu umekuwa wa awamu 4 kutokana na mafanikio yanayojitokeza na changamoto.

Awamu ya kwanza (I) ilikuwa kutoka mwaka
1998 – 2004 huu ulikuwa na malengo ya kudhibiti matumizi,
kuweka nidhamu ya fedha pamoja na kukuzana kuimarisha uchumi mpana.

Awamu ya pili (II)
ilikuwa kutoka mwaka 2004 – 2008 malengo ya mradi huo yalikuwa ni kuimarisha na kuendeleza mifumo na njia zinazotumika katika malipo ya fedha za umma kwa kutumia njia rahisi na nyepesi. Aidha awamu hiyo ilizingatia pia uimarishaji wa njia ya ukusanyaji mapato na jinsi ya kuweka mbinu ya kuzitumia rasilimali fedha na kuweka mikakati ya kipi kianze kwanza.

Awamu ya tatu (III)
ilikua kuanzia 2008 – 2011, mradi huu ulikua na malengo ya kuhakikisha kuna kuwa na upatikanaji rasilimali fedha kutoka katikaTaasisi mbalimbali za kifedha.

Awamu ya nne (IV)
ya mradi ni kuanzia June 2012, mradi ulizinduliwa na kuanza rasmi tarehe 1 Julai, 2012. Madhumuni ya mradi huu katika awamu ya nne umelenga katika kuonge za nguvu ambayo itawezesha kufikia malengo ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025, 
 hiyo inaenda sanjari na mpango wa maendeleo wa miaka mitano yaani 2011/2012 – 2015/2016 na MKUKUTA (MkakatiwaKukuzauchumi Tanzania)/ MKUZA (Mkakati wa Kukuza uchumi Zanzibar), ili kufika malengo ya ukuaji wa uchumi.


HABARI ZAIDI INGIA HAPA

Article 24

Mahakama nchini spain yazuia mgomo wa wachezaji uliopangwa kufanyika kuanzia Jumamosi

$
0
0
Na Sultani Kipingo 

Mahakama nchi Spain imeamuru mgomo wa wachezaji nyota nchi hiyo uliopangwa kufanyika Jumamosi wakipinga sharia mpya ya haki za mapato kwenye TV, hivyo ndio kusema fainali timu ya Barcelona itaweka msumali wake wa mwisho wa La Liga dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumapili.

Mahakama hiyo ya National Court imesema katika uamuzi wake leo kwamba kuruhusu mgomo huo uendelee kutazuia kumalizika kwa michuano ya ubingwa ya nchi hiyo na pia kusababisha mvurugano mkubwa wa kiutawala. 

"Mgomo huo utavuruga mikataba ya kimataifa ya Spain na vilabu vyake, kadhalika na likizo za wachezaji”, Mahakama hiyo imeongezea. 

Muungano wa wachezaji nchini Spain (AFE) ulitangaza wiki iliyopita kwamba wachezaji watagoma kuanzia Jumamosi na uongozi wa La Liga uliweka pingamizi na kuuita mgomo huo kama kinyume cha sharia. 
Mgomo huo, unaoongozwa na nyota wakubwa kama Iker Casillas wa Real Madrid na Adres Iniesta wa Barcelona, una nia ya kushinikiza kwamba vilabu vidogo vipatiwe donge kubwa Zaidi kutoka mapato yanayotokana na haki za kuonesha michezo kwenye TV. 
Mahakama hiyo imesema uamuzi wa kuzuia mgomo huo ni hatua ya muda mfupi wakati ikiendelea kuipitia kesi hiyo, na hukumu itatolewa Juni mwaka huu.

Mtu Mmoja apoteza maisha kwa Mafuriko jijini Dar

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwepo kwa mtu mmoja mwanaume aliyetambulika kwa jina la EXAVERY S/O MICHAEL, Miaka 19, Mkazi wa Kingugi Mbagala, aliefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akiwa katika harakati za kuvuka mto Kizinga, na kufikia idadi ya Watu 13 waliopoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari ya mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. 

Tukio hili lilitokea tarehe 13/05/2015 majira ya saa nane kamili mchana huko maeneo bonde la Mto Kizinga Kata ya Kiburugwa Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam. Maiti yake iliopolewa na wasamaria wema na imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi na utambuzi.

Nawashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea na kushiriki kushughulikia maafa yanayoendelea kutokea ikiwa ni matokeo ya mafuriko yaliyosababisha na mvua zinazonyesha mfululizo katika jiji la Dar es Salaam.

Nawaomba wakazi wa maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam waendelee kuchukua tahadhali kwa kuwa madhara zaidi yanaweza kutokea kutokana na kwamba mvua bado zinaendelea kunyesha. Aidha, waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona hali yoyote isiyo ya kawaida ili hatua za haraka ziweke kuchukuliwa.

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
S. H. KOVA
DAR ES SALAAM

BALOZI WA FINLAND NCHINI TANZANIA AZINDUA KITUO CHA MSAADA KWA WAHANGA WA UKATILI

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka akifurahia jambo mara wakati akitembelea majengo ya kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ambayo yamejengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo chini ya shirika la UKUMBI.
Balozi wa Finland Tanzania Mh. Antila Sinikka alikabidhi kitabu cha "Politics of Gender "kwa mkurugenzi wa Kwieco ,Elizabeth Minde.

WANAHABARI NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI CHANGAMOTO ZA NCHI ZAO

$
0
0
 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano la kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha demokarasia na mambo mbalimbali yanayogusa jumuiya hiyo Dar es Salaam leo
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Felix Mosha akizungumza katika kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Assa Mwambene akijibu maswali ya wanahabari.


UTARATIBU WA UTEUZI WA WAGOMBEA NDANI YA CHAMA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015 CHADEMA

Changamoto maboresho usimamizi wa fedha za umma zatajwa

$
0
0
Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali. Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada mbalimbali.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani. Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.
---------------------------------------------

PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. 
 Mratibu wa Mradi huo ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. 
 Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa fedha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi. Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu. 
 Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma. Mradi pia umefanikiwa kuimarisha ushirikishaji wa utayarishaji wa bajeti kuanzia ngazi za chini, kutumika kwa mfumo wa SBAS ambao unatoa fursa ya kuingiza mahitaji ya Mpango wa miaka mitano na kugawa rasilimali na pia kuchapishwa kwa taarifa ya utekelezaji wa bajeti, ukaguzi mbalimbali hivyo kuongeza kiwango cha uwazi. 
 Mengine ni pamoja na kutungwa kwa sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya 2011 badala ya sheria iliyokuwepo Na. 21 ya 2004. Sheria hii pamoja na mambo mengine imeiweka PPRA kutoshughulikia masuala ya michakato ya ununuzi, na kubaki na shughuli yake kuu ya kutoa miongozo ya ununuzi wa umma. Vile vile sheria imeongeza kiwango cha uwazi zaidi katika michakato ya ununuzi wa umma. 
 "...Kujenga uwezo wa watumishi katika kufanya kazi zao zinazohusiana na usimamizi wa fedha za umma. Kwa mfano mafunzo kadhaa yalitolewa kwa wahasibu, wakaguzi, wachumi; maafisa wa ununuzi...kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kulitumikia taifa. Kuandaa na kutoa taarifa za kifedha chini ya mfumo wa IFMS ili kufikia vigezo vya kimataifa (IPSAS), Kuwekwa kwa mfumo wa kusimamia mali za serikali (Asset tracking software) katiak ofisi zote za kurugenzi ya Usimamizi wa Mali za Serikali." Alisema Mratibu huyo. 
 Mafanikio mengine ni kuongezeka kwa uwezo wa NAOT hata kufikia kiwango cha hatua ya 3 ya AFROSAE, uhuishwaji wa mifumo ya fedha kama EPICOR ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi (k.m. mfumo wa EPICOR toleo la 7.3.5 ulibadilishwa na kuingizwa toleo la 9.05 wenye modules nyingi zaidi kuliko ule wa mwanzo, Kufanyika kwa zoezi la uhamishaji wa fedha kwenda serikali za mitaa na kuweka Mpango Kazi ili kuboresha uhamishaji wa fedha toka serikali kuu kwenda kwenye LGAs. 
 Mratibu alibainisha kwa sasa Ofisi ndogo za hazina zote nchini zimewekewa mfumo wa IFMS, na hivyo kuongeza ufanisi, Uandaaji na utoaji wa taarifa ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo wa IFMS na kwa kufuata mifumo ya kimataifa ya International Public Sector Accounting Standards Cash Basis (IPSAS). 
 Mradi wa PFMRP ulianzishwa mwishoni mwa miaka ya 1990, ukiwa na lengo la kuimarisha usimamizi, kuongeza uwazi na uwajibikaji na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika serikali na taasisi zake, huku ikitekelezwa sambamba na programu nyingine za kitaifa katika sekta ya umma. *Imeandaliwa na www.thehabari.com

introducing "amechelewa" by Dream

$
0
0
Artist - Dream 
Song - Amechelewa 
Directed by Aj 
 Contact Phone number +255 652 124848 
email address dreammswazi@gmail.com

Balozi mpya wa Malawi nchini Marekani atembelea Ubalozi wa Tanzania Washington DC

$
0
0
 Mhe balozi mpya wa Malawi Nector Mhura akipokelewa na Afisa ubalozi Bi. Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, jijini Washington DC.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Malawi Mhe. Nector Mhura.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani akiweka saini kwenye kitabu maalum cha wageni.

  Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi Bi. Jane Nankwenya.
 Mhe, balozi wa Malawi nchini Marekani Nector Mhura akiwa ameambata na mkuu wa utawala wa ubalozi wa Malawi bi, Jane Nankwenya, kulia ni balozi wa Tanzania nchini Marekani Liberata Mulamula na Afisa wa ubalozi Bi. Swahiba Mndeme. Picha  na Ubalozi

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA BANDARI YA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Kulia) akiukaribisha ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Kushoto ni Kiongozi wa Msafara huo, Bibi Florence Mwanri. Wengine pichani ni Bw. Aloyce Andrea (Wapili Kushoto), Bw. Robert Senya (Katikati) na Bw. Abel Shirima.  
 Meneja wa Mipango na Mikakati wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Ntandu Mathayo (Wapili Kushoto) akizungumza wakati ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bibi Lucy Kazibure (Kushoto) na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. 
 Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) wakati walipotembelea kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
 Mkuu wa Sehemu ya Kushushia Mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, Kapteni P. R. Paul (Kulia) akitoa maelezo kuhusu hali ya upakuaji wa mafuta kwa ugeni kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kiongozi wa Msafara kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akizungumza wakati walipokwenda kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images