Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 835 | 836 | (Page 837) | 838 | 839 | .... | 3286 | newer

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo leo asubuhi nyumbani kwa Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea hivi karibuni.Aliyesimama pembeni ya Rais ni mdogo wa marehemu Makongoro Nyerere.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya marehemu John Nyerere nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye John Nyerere kilichotokea juzi .Mwili wa Marehemu John Nyerere rubani wa zamani wa ndege za kivita nchini aliyeshiriki kikamilifu vita vya Uganda kati ya mwaka 1978 na 1979, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda kijijini Butiama mkoani Mara kwa maziko.Picha na Freddy Maro

  0 0

  Anasema Mariam Ikoa, mwanamitindo nguli wa Tanzania akiwa n mrembo Lisa Jensen. Anasema: "Najivunia u-Afrika. Vazi kujivika. Stara. Heshima. Hifadhi. Uzuri. Anapatikana katika duka lake namba 5 ghorofa ya kwanza katika jengo la Dar Free Market barabar ya Ali Hassan Mwinyi jirani na ofisi za DSTV jijini Dar es es alaam. Ama katika insta@mariam.ikoa


  0 0

  Winfrida Josephat "Recho" akijitetea baada ya kupigwa loba na 93.7 E-FM bofya hako kashale keupe hapo chini umsikie...

  0 0

  Ankal akiwa na Mkurugenzi Fredy Njeje katika jengo la Tone House ambamo kuna mambo kibao ikiwa ni pamoja na studio za  Tone Radio-TZ lililopo Mwenge jijini Dar es salaam. Hapa ndipo nyumbani pa libeneke la Blog za Mikoa kama vile Mbeya Yetu, Lindi Yetu, Mwanza Yetu na kadhalika. Hawa vijana pia ni wanachama waanzilishi wa Tanzania Bloggers Network (TBN) ambayo inazidi kukua siku hadi siku...

  0 0
  0 0


  0 0

   DENNIS SSEBO NA  ADELLA TILLYA.
   1.     12:00 HADI SAA 3:00 KAMILI ASUBUHI UNAPATA
  " JOTO LA ASUBUHI" ILI KUKUANZISHIA SIKU

  DENNIS SSEBO  NI NANI?

  Ssebo  ni moto ama baruti ya kipekee katika masuala ya Radio, akiwa ni muhitimu wa mambo ya sheria na ana  shahada ya udhamiri katika mambo ya mawasiliano ya Umma lakini akiwa na ufahamu  na mapenzi zaidi  upande wa Radio na TV.

  Ssebo amekuwa kwenye Tasnia hii kwa muda mrefu akiwa na uzoefu wa kufanya kazi Zaidi  Radio na Tv kwa muda wa miaka 15, lakini pia amekuwa akisaidia kwakiwango kikubwa sana katika  kuboreha vipindi vya Radio na Tv nchini Tanzania.

  Wapo watu wachache ambao wanatambua uwezo wake wakuburudisha na kufundisha,  Zaidi amejulikana kuwa ni mtu wa masihala au utani lakini Dennis Ssebo ni mtu makini anayejitambua na muda wake mwingi ameutolea kwenye kusoma na kufanya tafiti mbalimbali.

  Ssebo anasema “ Ninasema kile ambacho ninakiona, lakini kama hukubaliani nacho ni uamzi wako”  Mpende au umchukie lakini kwa hakika utacheka, utashangaa na utajifunza kitu  unapomsikiliza radioni.

  Ssebo ni mtangazaji ambaye EFM Radio imempa nafasi ya kukuamsha na kuwa nawe kila siku asubuhi  kuanzia saa kumi na mbili hadi saa tatu kamili asubuhi , Jumatatu hadi ijumaa. 

  MJUE ADELLA TILLYA 
  Na hiyo sauti ya kike unayoisikia kila siku pamoja naye asubuhi, si ya mwingine bali ni mwanadada  shupavu ( Iron Lady) ambaye huwezi kumpata sehemu yoyote Zaidi ya Efm Radio.

  Hapa namzungumzia Adella Tillya, ambaye  ni mtayarishaji wa Kipindi cha Joto la Asubuhi na juhudi zake mara nyingi zinatambuliwa sana na Ssebo ambaye amekuwa akimwambia  “ katika wewe ninaona taarifa”

  Adella amekuwa na uzoefu wa kuandaa na kutangaza  na ni miongoni mwa watangazaji wa chache ambao mpaka sasa wameweza kumshika Ssebo.

  Ni ajabu hata katika ofisi za Efm amekuwa akiitwa mwanamke shupavu na hata akisikika hewani  akicheka lakini haimanishi kuwa ni mwanamke wa kawaida.

  Ni watu hawa wawili,  watundu,  lakini wakiwa na taarifa za kutosha za mambo mbalimbali ambao kwa pamoja wanakupa Joto la Asubuhi.

  Katika kipindi cha Joto la Asubuhi, utapata  habari za ndani na Nje ya nchi, uchambuzi wa magazeti ya ndani na nje, mada mbalimbalimba kuhusiana na mambo yanayoendelea ulimwenguni bila kusahau zawadi zitolewazo kwa wasikilizaji.  0 0

  Wiki hii bwana Costantine Magavilla anaongelea maana nyingine ya shule. Je unajua maana nyingine ya shule zaidi ya kusoma. Bofya hapo kati tuendelee...

  0 0

  Edwin Bruno, Founder and CEO at SMART CODES

  Tanzania’s leading digital marketing agency has revamped its new website at www.smartcodes.co.tz

  The agency, which is based in Dar es Salaam, has worked on a wide variety of Tanzania’s leading brands in number of campaigns from developing its’ Digital Strategy to Creativity & Designing to Technology & Development.

  To introduce what they do, SmartCodes released this video which is one of its kind and probably the first company profile video ever in Tanzania. 

  See the video below YouTube link:

  When asked about their secret CEO and Founder Mr. Edwin Bruno said that “We have simple road map on how to serve our prestigious customers, first we meet as face to face talk has proven to be the best way of communication to hear discuss customer’s needs. Then we research proper ways to meet the needs of customers and also his current position.

  From there we prepare a unique pitch, then we develop the big ideas into action and then we launch customer’s site, or mobile app, or social media campaign or both. We don’t end there; we provide all technical and business support to our customers”

  With special skills and technology, Smartcodes has served a handful of big brands in Tanzania including telecommunication giant Huawei, super TV show Mkasi, leading Technology company StarTimes, luxurious Giraffe Ocean View Hotel, Tanzania Postal Bank and many more.

  You can catch more about SmartCodes in below links  0 0

  WOTE TUNATAKA KUSOMA HADI CHUO KIKUU! Ndivyo wanavyosema wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru mjini Dodoma baada ya kuulizwa nani kati yao angependa kusoma hadi chuo kikuu na Ofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Veneranda Malima (kulia) jana (Jumanne, Mei 12, 2015). Wanafunzi hao na walimu wao walitembelea banda la HESLB ambayo inashiriki katika maonesho ya Wiki ya Elimu yanayaoendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru mjini Dodoma Bi. Conces Shirima akisaini kitabu cha wageni cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wakati alipotembelea banda la HESLB katika maonesho ya Wiki ya Elimu yanayaoendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa akibadilishana mawazo na Dkt. Jacob Chembele wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kuhusu urejeshaji wa mikopo inayotolewa na HESLB. Dkt. Chembele alitembelea banda la HESLB ambayo inashiriki katika maonesho ya Wiki ya Elimu yanayaoendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
  Ofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Veneranda Malima (kulia) akiongea na wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru mjini Dodoma wakiwa na Mwalimu wao Bw. Ikutto Bakari (katikati). Wamafuzni hao walitembelea banda la HESLB ambayo inashiriki katika maonesho ya Wiki ya Elimu yanayaoendelea katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma. (Picha na HESLB)

  0 0

  Mkuu wa biashara kanda ya Nyanda za juu kusini Bw. Juvenal Utafu ( wa tatu kutoka kushoto) akimkabidhi moja ya komputa zilizotolewa na TTCL Bw. Nasibu Mengele aliyemwakilisha Afisa Elimu mkoa wa Iringa Bw. Eusedius Mtavangu katika halfa iliyofanyika katika kituo cha Global Outreach Tanzania mkoani Iringa.
  Mkuu wa biashara kanda ya Nyanda za juu kusini Bw. Juvenal Utafu(kushoto) akifuatilia ngonjera kutoka wanafunzi (hawapo pichani) na meneje wa TTCL mkoa wa Iringa Bw. Humprey Ngowi.
  Mwanzilishi wa Global Outreach Tanzania Bw. Stan Muessle akiongea na wageni waalikwa kutoka Marekani kupitia mtandao wa Skype uliowezeshwa na Intarnet kutoka TTCL.
  Mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano ambaye alimwakilisha afisa elimu wa mkoa Bw. Nasibu Mengele (kati) akifuatilia wimbo wa shukrani kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Lugalo(hawako pichani).


  0 0

  Wateja wa Vodacom Tanzania sasa wameanza kunufaika na huduma mpya ya Ongea iliyozinduliwa rasmi leo ambayo inatoa unafuu mkubwa wa kupata huduma za mawasiliano kwa wateja na wananchi kwa ujumla. Ambapo mteja akinunua muda wa maongezi kwa Tsh 1,000/-mteja anapata dakika 100 za maongezi kupiga simu kwa mtandao wa Vodacom kwenda Vodacom,SMS 1000 na MB 100 za data.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii mpya,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa,amesema kuwa Vodacom itaendelea kuboresha huduma mbalimbali kwa wateja wake kwani kuna umuhimu wa kuwarahisishia mawasiliano wateja ili wapate kufanya kazi zao kiurahisi zaidi. Alisema jinsi ya kujiunga na huduma hii mpya ni rahisi sana,Wateja wanatakiwa kupiga namba *149*01# .Pia  wataendelea kunufaika na huduma nyingine kama vile vifurushi vya cheka .

  “Kwa mara nyingine Vodacom imewaletea  huduma ya ongea wateja wake ili kuwawezesha  kupata huduma za mawasiliano kwa urahisi zaidi  kwa kutuma ujumbe wa maneno kwa gharama nafuu ikiwemo pia kuwawezesha kuperuzi interneti kwa gharama ya chini.Huduma hii inawahusu watumiaji wa mtandao wa Vodacom tu”Alisema Twissa.

  Dunia ya leo inahitaji kila mtu awasiliane na mwenzake na wapendwa wao kwa hivyo ni muhimu kuwawezesha kuwasiliana kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi. “Ongea itawawezesha Wateja wa Vodacom kuweza kuwasiliana zaidi na kuunganishwa popote pale walipo na kuinua uchumi wa nchi kupitia mawasiliano murua”. Alisema Twissa.

  Vodacom Tanzania imekuwa ikibuni huduma bora zenye gharama nafuu za kuwarahisishia mawasiliano wateja wake ambapo mwaka jana ilizindua huduma ya Bonga iliyowezesha wateja kupiga simu kwenda mitandao yote Tanzania kwa Tsh 1.5 kwa sekunde.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Ayoub Mohammed Mahmoud kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Ayoub Mohammed Mahmoud baada ya kumuapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Mpya ya Magharibi "B" katika Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Haji Omar Kheir (kushoto) akiwa na Washauri wa Rais Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa,Abrahman Mwinyi Jumbe na Burhani Saadat Haji wakiwa ni miongoni mwa Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi "B" Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis wakiwa hafla ya kuapishwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Magharibi "B" Ayoub Mohammed Mahmoud Ikulu Mjini Unguja leo kazi iliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.]

  0 0

  Mfuko wa Maendeleo ya jamii-TASAF kwa ushirikiano na wadau wa Maendeleo wameanza mkutano wiki mbili wa tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini nchini -PSSN  unaosimamiwa na mfuko huo.

  Zifuatazo ni picha zikionyesha wadau hao wa maendeleo na watendaji wa TASAF wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga katika ukumbi wa mikutani wa Makao makuu ya mfuko huo jijini Dar es Salaam. 
   Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakichangia mawazo kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 
   Baadhi ya watendaji wa TASAF na wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakisikiliza michango ya mawazo kutoka kwa washiriki kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga. 
   Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakifuatilia kwa makini uchangiaji mawazo kufuatia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga 
  Baadhi ya wadau wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia na taasisi zingine wakipitia taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga .

  0 0

  Ripoti kutoka Bujumbura, nchini Burundi zinasema kuwa kamanda mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa Burundi.

  Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.

  Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.

  Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya urais wa Nkurunziza.

  Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani mbali na sheria za kimataifa.

  Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya kuwania awamu ya tatu.

  Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na viongozi wengine wa jeshi la Burundi.

  Tayari wanajeshi wameshika doria nje ya makao makuu ya runinga ya taifa.

  Rais Nkurunzinza alikuwa amepuzilia mbali maombi ya kuahirisha uchaguzi huo.

  Duru kutoka Burundi zinasema kuwa raia wameshajitokeza mabarabarani wakishangilia kauli hiyo ya ''Mapinduzi''.

  CHANZO: BBC SWAHILI

  0 0

  Mwenyekiti wa Madereva Tanzania Clement Masanja (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo katika picha) leo jijini Dar es salaam ili kuwajulisha madereva wote nchini kuwa mwaka huu wamekubaliana na Mamlaka husika kuwa hakutakuwa na mafunzo kama ilivyoelezwa hapo awali. Kulia ni Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga. Picha na MAELEZO_DAR ESALAAM

  Na Pius Yalula-MAELEZO-Dar es salaam

  Serikali imesema hakutakuwa na mafunzo kwa madereva wa malori na mabasi na wala hawatakiwi kwenda kusoma kozi fupi ili kuhuisha leseni zao kama ilivyokuwa imetangazwa hapo  awali na kusababisha mgomo.
  Kauli hiyo imetolewa  na  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga wakati akitoa tamko hilo kwa waandishi wa habari leo mjini Dar es salaam.

  Alisema kuwa madereva wenye daraja E, C, C1, C2 na C3 walitakiwa kupata mafunzo ya muda mfupi kila baada ya miaka 3 kulingana na kanuni ziliandaliwa mwaka 2014 kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra),Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA),Chuo cha Taifa ya Usafishaji(NIT), Vyama vya Madereva , Ofisi ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali na Chama cha Wamiliki wa Magari ya Mizigo Tanzania (TATOA) , lakini kwa mwaka huu hawatatekeleza kanuni hiyo.

  Kamanda Mpinga alisisitiza kuwa kanuni hiyo hatatumika mwaka huu badala yake madereva wataendelea na utaratibu wao wa zamani wa kubadilisha na kuhuisha leseni zao kwa zile ambazo zitakuwa zimekwisha bila kuulizwa vyeti.

  Aliongeza kuwa hadi hivi sasa mitala ya mafunzo hayo ya muda mfupi bado haijakamilika na wala Serikali haijawahi kupanga ada za mafunzo hayo , kwa hiyo utaratibu wa zamani utaendelea kutumika kama ulivyokuwa hapo awali.

  Kamanda Mpinga alitoa wito kwa madereva wote kuwa wavumilivu kwa matatizo yao wakati Kamati ya kudumu ya kutatua matatizo ya sekta ya usafishaji ikendelea kuyatafutia ufumbuzi.

  Katika hatua nyingine Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi na wasafiri kutoa taarifa kwa viongozi wa Jeshi hilo endapo wanaona Askari wao  au dereva anatenda vitendo visivyo vya kimaadili ili aweze kuchukuliwa hatua.


  Alisema kuwa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kipo wakati tayari kupokea malalamiko ya kuyachukulia hatua ili kulinda maisha ya wasafiri na mali zao , hivyo ni vizuri wakaripoti wale wote wanaohatarisha maisha ya wenzao.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya, Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri wa Jarida wa Habari za Uchumi, Biashara na Utalii la Trends baada ya kumaliza mazungumzo Nayeli ofisini kwake Brussels leo. Mhariri huyo atatembelea Tanzania kubainisha fursa za Utalii zinazopatikana Kanda ya Kusini Tanzania.

  0 0

  BENKI ya NMB, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa na lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa kwa mikoa ya kanda ya kati – Singida na Dodoma.

  Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni magodoro 22 na mashuka 422 ambayo kwa maelezo ya mganga mkuu wa hospitali hiyo – Dr Ezekiel Mpuya vitasaidia sana kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo hususani akina mama wajawazito na watoto.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Kapteni Mtaaafu - Chiku Galawa (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya shuka 422 na godoro 22 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto). Vifaa hivyo vilitolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye kilele cha siku ya wauguzi duniani - Dodoma.
  Meneja wa NMB Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto), akikabidhi sehemu ya magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Kapteni Mstaaafu - Chiku Galawa zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye silele cha siku ya wauguzi Duniani. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Dodoma - Anatolia Mkindo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma - Ezekiel Mpuya

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Baraka Konisaga akisoma taarifa ya ufunguzi wa mkutano wa kwanza kati ya minane inayotarajiwa kufanyika kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza.
  SERIKALI imesema kutokana na Jiji la Mwanza kujengwa nyumba za kudumu bila mpangilio maalumu, imeanza mchakato wa kuainisha maeneo yote ya Wilaya ya Ilemela na Nyamagana yanayounda jiji hilo ili  sehemu makazi, biashara, viwanda na huduma za jamii zifahamike.

  Imesema kabla ya kuanisha maeneo hayo, leo itaanza kukutana na  wadau wote na wananchi wa jiji hilo ili kupokea maoni na mapendekezo kabla ya kuanza utekelezwaji wa mpango huo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa jana kwenye vyombo vya habari na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Faisal Issa,imesema  mpango huo umelenga kuondoa migogoro ya ardhi na uvamizi wa maeneo yasiyoruhisiwa.
  Wadau wa mkutano kutoka idara za serikali, viongozi wa siasa, waandishi wa habari na wafanyakazi taasisi za umma.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

   KISOMO cha kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha aliyekuwa mwimbaji mahiri nchini, marehemu Amina Ngaluma ‘Japanese’ kinatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii Kitunda, Machimbo Dar es Salaam.
   
  Akizungumza baba mzazi wa marehemu,  Kassim Ngaluma, alisema kisomo hicho kitafanyika nyumbani kwa wazazi wake marehemu na kuwaomba ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali wa marehemu wakati wa uhai wake wahudhurie.
   
  “Tunaomba wote tulioshiriki kwa namna mbalimbali wakati wa msiba wa marehemu mwanangu, tushirikiane pia katika kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo chake,” alisema Mzee Ngaluma na kuongeza kuwa kisomo hicho kitafanyika saa saba mchana baada ya swala ya adhuhuri.
   
  Aliwaomba waliokuwa wanamuziki wenzake na marehemu, mashabiki wake, pamoja na wadau wengine wa muziki na marafiki wote, washirikiane katika tukio hilo.
   
  Ngaluma aliyepata kung’ara na bendi mbalimbali nchini, alifariki dunia Mei 15 mwaka jana kwa shinikizo la damu akiwa Thailand alikokuwa akifanya shughuli za muziki katika bendi ya Jambo Survivor na kuzikwa Mei 24 mwaka huo, Dar es Salaam.
   
  Wakati wa uhai wake alitamba na bendi mbalimbali zikiwemo African Revolution ‘Tamtam’, Double M Sound ‘Mshikemshike’ na TOT Plus zote za Dar es Salaam.Pia alipigia makundi ya Arusha Sangoma, Sayari Band na Less Mwenge yote ya Arusha na Mangelepa na Sky Sound za Kenya.
   
  Baadhi ya nyimbo alizotunga wakati wa uhai wake ni Manyanyaso Kazini na Mapendo alizotunga akiwa Tamtam, wakati Double M Sound alitunga nyimbo za Wajane na Ukewenza.Pia alitoa albamu yake binafsi iitwayo Jitulize.
   
  Baadhi ya nyimbo alizopata kuimba na kumpatia umaarufu mkubwa ni Mgumba, Maisha Kitendawili,  Ndugu Lawama, Zawadi ya Watanzania, Ugumu wa Maisha na Call Box zote zikitungwa na Muumin Mwinjuma ‘Kocha wa Dunia’.

older | 1 | .... | 835 | 836 | (Page 837) | 838 | 839 | .... | 3286 | newer