Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 837 | 838 | (Page 839) | 840 | 841 | .... | 3284 | newer

  0 0

  BENKI ya NMB, imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma vyenye thamani ya shilingi milioni 10 ikiwa na lengo la kusaidia uboreshaji wa huduma katika hospitali hiyo kubwa kwa mikoa ya kanda ya kati – Singida na Dodoma. Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni magodoro 22 na mashuka 422 ambayo kwa maelezo ya mganga mkuu wa hospitali hiyo – Dr Ezekiel Mpuya vitasaidia sana kuweka mazingira rafiki kwa wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo hususani akina mama wajawazito na watoto.
  Meneja wa NMB  Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto), akikabidhi sehemu ya  magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma  Kapteni Mstaaafu  - Chiku Galawa zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye silele cha siku ya wauguzi Duniani. Kulia ni Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Dodoma - Anatolia  Mkindo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma - Ezekiel Mpuya
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Kapteni Mtaaafu - Chiku Galawa  (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya shuka  422 na godoro  22 yenye thamani ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa NMB  Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto). Vifaa hivyo vilitolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma  katika hafla iliyofanyika kwenye kilele cha siku ya wauguzi duniani - Dodoma.
  Meneja wa NMB  Kanda ya Kati - Gabriel ole-Loibanguti (kushoto), akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi  magodoro 22 na shuka 422 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10 kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma  Kapteni Mstaaafu  - Chiku Galawa zilizotolewa na NMB kwaajili ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. 

  0 0  0 0

  Tuzo za Watu 2015 zinatarajiwa kufanyika Ijumaa ya May 22 kwenye hoteli ya Hyatt Regency (The Kilimanjaro) jijini Dar es Salaam.  Tuzo za mwaka huu zinahusisha vipengele 13 vilivyopo kwenye muziki, filamu, redio, televisheni na blogs.

  Washindi watapatikana kwa asilimia 100 ya kura za wananchi zinazoendelea katika hatua hii ambapo wamebaki washiriki watatu katika kila kipengele.

  Kila mshindi atapokea tuzo na zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja.

  Pamoja na utoaji wa tuzo hizo, hafla hiyo itasindikizwa na burudani moto moto kutoka kwa wasanii watakaotangazwa hapo baadaye. Hakuna kiingilio kwenye tuzo hizo bali itatolewa mialiko kwa baadhi ya watu kwenye tasnia ya burudani na zingine nchini. Pia mialiko 100 itatolewa  kwa wananchi waliopiga kura zaidi.

  Haya ndio majina yaliyoingia kwenye fainali ya tuzo za watu:

  Mtangazaji wa redio anayependwa 

  D’Jaro Arungu - TBC FM - TZW1C
  Maryam Kitosi – Times FM - TZW1D
  Millard Ayo – Clouds FM - TZW1E


  Kipindi cha redio kinachopendwa 

  Amplifaya – Clouds FM - TZW2B
  Hatua Tatu – Times FM - TZW2C 
  Papaso – TBC FM - TZW2D

  Mtangazaji wa runinga anayependwa

  Abdallah ‘Dullah’ Ambua – EATV - TZW3A
  Salama Jabir – EATV/Maisha Magic - TZW3B
  Salim Kikeke - BBC Swahili - TZW3C

  Kipindi cha runinga kinachopendwa

  In My Shoes – EATV - TZW4B
  Mkasi – EATV - TZW4C
  Planet Bongo – EATV - TZW4D

  Blog/Website inayopendwa 
  Hassbabytz.com - TZW5C
  Millardayo.com - TZW5D
  timesfm.co.tz - TZW5E

  Muongozaji wa video anayependwa
  Adam Juma - TZW6B
  Hanscana  - TZW6D
  Nisher - TZW6E

  Muongozaji wa filamu anayependwa

  JB - TZW7A
  Leah Mwendamsoke - TZW7B
  Vincent ‘Ray’ Kigosi - TZW7D

  Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa 

  Jacqueline Wolper - TZW8C
  Riyama Ally - TZW8D
  Wema Sepetu - 

  Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa 

  Hemedy PHD - TZW9A
  JB – TZW9B
  King Majuto - TZW9C

  Mwanamuziki wa kike anayependwa TZW10

  Lady Jaydee - TZW10A
  Linah - TZW10B
  Vanessa Mdee - TZW10E

  Mwanamuziki wa kiume anayependwa

  Alikiba - TZW11A
  Barnaba - TZW11B
  Diamond Platnumz - TZW11C

  Filamu inayopendwa 

  Chausiku - TZW12A
  Kigodoro - TZW12B
  Madam - TZW12C

  Video ya muziki inayopendwa

  Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz - TZW13C
  Wahalade -  Barnaba - TZW13D
  XO – Joh Makini - TZW13E

  Kupiga kura andika code ya jina ulipendalo na tuma ujumbe wa simu kwenda namba 15678 au tembeleawww.tuzozetu.com.


  0 0

   Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mhe. Sophia M. Simba (Mb.) akikata utepe kuzindua Kitini cha Zana za Mawasiliano kuhusu Elimu ya Malezi kwa Familia, kushoto kwake ni Mhe. Dk. Pindi H. Chana (Mb) Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, kulia kwake ni Georgina Mtenga kutoka UNICEF na Anna T. Maembe Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
    Waziri akikabidhi Kitini hicho kwa Muwakilishi wa Watoto.

  Wawakilishi wa Watoto, Wazazi, Waandishi wa Habari na Taasisi mbalimbali wakiwa katika Mkutano huo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0

   RAis mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin Mkapa akifungua Mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi leo jijini Dar es salaam
    Baadhi ya Wahandisi waliohudhuria mkutano huo wakiapishwa leo jijini Dar es Salaam. 
    Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia masuala mbalimbali. Picha/Aron Msigwa -MAELEZO. 

  Na Aron Msigwa, 
  MAELEZO .


  Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamin Mkapa amewataka Wakandarasi kote nchini kufanya kazi zao kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ujenzi ili miradi wanayoisimamia na kuitekeleza iweze kuwa na manufaa kwa taifa.

  Mhe.Mkapa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB) uliowawajumuisha pia wadau wa sekta ya Ujenzi kutoka nchini Malawi na Kenya.

  Amesema umakini katika usimamizi wa kazi za wakandarasi na uwepo wa wataalam waliobobea katika sekta ya ujenzi umechangia kwa kiasi kikubwa kasi maendeleo inayotokea sasa nchini Tanzania.
  Ameeleza kuwa sekta ya ujenzi ndiyo iliyolifikisha taifa hapa kutokana na mchango wake katika Pato la Taifa unaofikia asilimia 14.1 ikifuatiwa na sekta nyingine na kuongeza kuwa ili nchi iweze kuendelea lazima wakandarasi wazalendo wajengewe uwezo ili kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa katika sekta ya ujenzi zinabakia Tanzania na kuwanufaisha wazawa badala ya wageni.

  0 0

  Inline image 3  Waziri Mkuu Mweshmiwa Mizengo Pinda akijadili jambo na Mama  Bertha Semu-Somi(Mama madawati) na Project Officer Kayemarie Bukila alipotembelea Banda la Hassan Maajar Trust   Inline image 1

  Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Dr. Shukuru Kawambwa alipotembelea banda la Hassan Maajar Trust
  Inline image 4
  Naibu waziri Elimu-Tamisemi Mhe. Kassim M. Majaaliwa alipotembelea kibanda cha hassanmaajartrust 
  Inline image 2


  Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Anna Kilango akimsikiliza Mama Madawati(Bertha Semu-Somi) katikati , na Project Officer Kayemarie Bukila kulia alipotembelea banda la hassan maajar Trust

  0 0

  PROGRAMU ya Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) imetaja changamoto zinazoukabili mradi huo licha ya mafadikio mengi iliyoyapata wakati mradi huo ukiingia awamu ya nne ya utekelezaji wake. 

  Mratibu wa Mradi huo,Bwa.Sebastian Ndandala ametaja changamoto hizo leo mjini Kibaha alipokuwa akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari pamoja na waendeshaji wa mitandao ya jamii ikiwa ni hatua ya kushirikisha vyombo vya habari juu ya utekelezaji wa mradi huo. 

   Mratibu huyo alizitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ugumu wa kuunganisha mifumo mbalimbali ya kifedha inayotumika serikali ili mifumo hiyo iweze kuongea kwa pamoja, ugumu wa kujenga uwezo katika maeneo ya kitaalamu kama E-procurement na ICTs, Uhaba wa ferdha za ndani katika kutekeleza program na changamoto nyingine katika utekelezaji mradi.

   Alisema mradi huo unaofadhiliwa kwa pamoja na washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania tayari umeingia awamu ya nne ambapo lengo kuu la awamu hii ni kudumisha nidhamu katika usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa umma ili kuleta maendeleo endelevu. 

   Aidha alisema licha ya changamoto zilizopo katika utekelezaji mradi huo yapo mafanikio hasa katika awamu ya nne ambayo ni pamoja na programu kufanikiwa kuunganisha mfumo wa usimamizi wa fedha nchi nzima katika serikali kuu na serikali za mitaa, kufanikiwa kufanya utafiti wa namna Halmshauri za Wilaya/Miji inavyoweza kuongeza mapato na kufanyika kwa zoezi la PEFA mwaka 2013 na hivyo kuibua mapungufu yaliyopo katika usimamizi wa fedha za umma.
  Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari. Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma (katikati) akiuliza swali kwa Mratibu wa Mradi wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) hayupo pichani.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.Kulia ni Mratibu wa Moboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management Reform Progamme – PFMRP) ,Bwa.Sebastian Ndandala akifafanua jambo juu ya utekelezaji wa mradi huo kwa wanahabari.  0 0

   Patients and relatives who went to seek medical attention at African Medical Investment Ltd (AMI Hospital, also known as Trauma Center) in Dar es Salaam were yesterday in shock to see court brokers attaching hospital belonging after AMI failed to pay its rental bills for the past 26 months that accumulated to $1.6million.

  Speaking to journalists who went to witness the eviction court broker from MEM Auctioneers and General Brokers Ltd, Mr Elieza Mbwambwa, said they were carrying out a court order issued by the High Court of Tanzania, Commercial Division, following a long commercial legal battle involving AMI and a local businessman, Mr Navtej Singh Bains, (the land Lord).

  He said that the court ordered for attachment of AMI hospital properties to compensate for the dept, mentioning that as at yesterday, a number of AMI properties were confiscated including three ambulances, one Saloon car (Mark II), special hospital beds, computers, chairs and other hospital gadgets.

  “Although we were given an order to confiscate everything at once after the elapse of 14 days notice, which falls today, we have considered humanity in executing this assignment because this is an hospital. We have only taken items that are not used by inn-patients (those who are already admitted).

  “We have given the hospital a notice to evacuate admitted patients by 22nd this month of May. If they don’t comply by this time, we will transfer them to other hospitals and hand over the building to the landlord. This has been done in a humanitarian level. We have not disturbed already-admitted patients, but from today onwards, not any other new patient will be allowed in,” he said.

  Mr Mbwambwa said that machines like city-scan, x-ray machines and others           that are still being used by in-patients have been recorded and will be attached immediately after transferring the patients.When contacted for his comments on behalf of AMI Hospital management, Mr Lawrence Ochola said briefly that they are still continuing to attend to admitted patients and that he could not comment further.

  Families and friend of patients admitted at AMI hospital were seen processing documents to transfer their patients. Those who were bringing in new patients were returned by the gate.  There is also information that AMI Hospital Bank accounts at EXIM Bank which were attached by the Courts were found to have been unfrozen and most funds emptied.

  It is now clear that AMI hospital will be closed down despites its several appeal attempts to stop eviction, leaving its loyal patients in limbo.
  The hospital had failed to comply with Tanzania Court of Appeal order that wanted it to deposit in court $1.514 million plus a monthly rent to a tune of $64,000 per month following a tenancy agreement dispute.

  AMI Plc Chief Executive Officer (CEO), Mr Theunis Peter Botha, also a Director and CEO of the local AMI Hospital in Tanzania, subsequently filed the Bankruptcy application in the High Court of Tanzania stating that it was operating insolvently having incurred losses for the past two years.

  AMI Tanzania is wholly owned by its London Company AMI Plc.
  In a bankruptcy petition filed in March this year before the High Court's Main Registry, the company alleges that it has been incurring losses in terms of billions to the extent of having several outstanding liabilities and debts which are now exceeding its ability to pay to different creditors.

  "The petitioner (AMI) incurred a net loss of $1.146 million in the year ended February 28, 2013, while in the year ended February 28, 2014, the petitioner incurred a net loss of 775,000 US dollars," reads a section of the petition document. 

  It is stated that the company was also required to pay outstanding dues to institutes, notably the National Social Security Fund (NSSF) and the Tanzania Revenue Authority (TRA) and individuals.

  According to the petition, given the value of the assets of the company and the amount of money owed to it by creditors, there was no way it would be able to raise enough funds for paying them as well as meeting her obligations.  
  There are also records showing that Lancet Laboratory (T) Ltd filed for an urgent application against AMI Hospital eviction claiming over Sh150 million owed to them by AMI Hospital.

  Inside information has it that several creditors are now in a limbo as the Hospital owes over $4m to them including the biggest creditor being the Landlord Mr Bains, Doctors, Staff, TRA, Pharmaceutical suppliers and other suppliers.

  0 0

    
  MAULID BARAKA KITENGE WITH CO HOST  IBRAHIM MASOUD “MAESTRO” NA OMAR KATANGA.
  WACHAMBUZI  OSCAR OSCAR,  MUSSA KAWAMBWA  NA SUDI  MKUMBA

  WATAYARISHAJI : YUSUPH MKULE, FRANCIS MHANDO, DR PANJUAN NA  WENGINEO....


  1.    MAULID KITENGE NI NANI?,

  Huyu ni mtangazaji nguli wa Sports Tanzania, aliyetumia kipindi cha miaka kumi na nne(14) kwenye moja kati ya vituo maarufu nchini Tanzania, na mwanzilishi wa Sports E FM Radio, ambae anafahamika sana kwa utangazaji wake maridhawa, na maswali yenye kutia kashkashi ambayo huleta mvuto mkubwa kwa wasikilizaji..na ambae anaamini kile anachokiamini yeye, na akiwa ni mwenye kujiamini kwa mapana na marefu kitu kikubwa alichonacho Kitenge ni hupenda kushauriwa na kumsikiliza kila mwenye kuhitaji kujifunza kutoka kwake.

  2.    IBRAHIM “MAESTRO” MASOUD ..

  Mtangazaji mwingine Nguli wa sports Tanzania, akiwa muongozaji na mchambuzi mahiri wa sports kwenye Radio na Television, uzuri wa huyu bwana aliwahi kuwa mchezaji wa klabu kadhaa za ligi mbalimbali Tanzania bara na Visiwani, na ambae pia ni mwalimu wa soka wa Ngazi ya kati, na mwenye taaluma ya soka la vijana aliyebobea, akiwa nauzoefu wa miaka isiyopungua kumi na minne (14) kwenye kiwanda cha habari za michezo Tanzania... 
  3.    OMARY KATANGA…

  Mtayarishaji na muongozaji pia muanzilishi wa E-Sports ya E-fm mbali na umahili wake katika sports, lakini pia ni msomaji mzuri wa Taarifa za habari, anatumia  style ya kipekee inayopendwa na wasikilizaji  ya kwenda speed wakati wa kutangaza  michezo, ana maswali ya mtego yenye kuleta burudani masikioni mwa wasikilizaji wakati akifanya mahojiano na watu waliomo kwenye familia ya michezo, ni mtangazaji makini sana kwa kila akipelekacho hewani.

  4.    OSCAR OSCAR..

  Kitaaluma ni mwalimu, na ambae ameibuka kuwa mmoja kati ya wachambuzi wanaokuja juu sana kwenye michezo Tanzania kutokana na kuwa mfuatiliaji sana wa masuala ya soka,  na mara nyingine hufanya  uchambuzi kwenye vipindi vya TV kama Kabumbu show, na uchambuzi wa mechi za Premier ya England, kwenye kituo cha Utangazaji  cha Kimataifa-BBC.

  5.    MUSSA KAWAMBWA..

  Ni mchambuzi na muaandaji wa kipindi cha michezo hapa 93.7 EFM mwenye uzoefu wa hali ya juu katika tasnia hii akiwa amepita katika vituo mbalimbali vikubwa hapa nchini, pia ni muandaaji wa kipengele cha HISABATI ndani ya Sports Headquarters na Chakuchabo. Sauti yake ya kuvutia pamoja na historia kubwa aliyonayo hasa katika soka la barani Ulaya ni moja kati ya vitu vinavyomfanya awe wa kipekee. Mwisho kabisa ni uelewa wake juu ya michezo kama Tennis, Cricket, Rugby, Masumbwi na Langalanga. 
  1.    FRANCIS MUHANDO.

  Ni mtayarishaji na reporter  wa vipindi vya michezo hapa 93.7 EFM, unayeweza kumsikia katika kipengele cha Robo saa ya nguvu akifanya mahojiano na wanamichezo mbalimbali. 
  2.    YUSUPH MKULE.

  Mtayarishaji na muongozaji wa vipindi vya michezo hapa Efm, E.Sports & Sports HQ na amekuwa mtangazaji wa michezo tangu mwaka 2009 kwakufanya kazi katika redio mbalimbali  hapa nchini Tanzania. Pia amewahi kuwa msimamizi wa vipindi katika mmoja ya redio aliyowahi kufanya kazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania.  

  Kwaujumla ni kati ya watangazaji na waongozaji wa vipindi vya michezo  ambaye  kwasiku za usoni atakuwa moto wa kuotea mbali na hilo analithibitisha katika kipinchi cha E.Sports na Sports HQ hapa E.FM.

  3.    SUDI MKUMBA.

  Mtayaarishaji na mchambuzi wa vipindi vya  E Sports na Sports HQ ni ni miongoni mwa walioanzisha vipindi hivi  vya michezo hapa 93.7 EFM pia ndiye mchambuzi wa kipengele cha michezo katika kipindi cha UBAONI kinachoongozwa na mtangazaji Gadner G Habash.

  Ni mchambuzi anaechipukia na anaekuja kwa kasi kubwa katika tasnia hii ya uchambuzi na uandaaji wa vipindi vya michezo radioni.

  SPORTS HEADQUATERS..

  Ni show ambayo imekusanya michezo yote duniani, ambayo Platfom yake ni E Sports, ikiwa na Vipengele mbalimbali kama vile habari za nyumbani na uchambuzi yakinifu, Robo saa ya nguvu ya kwanza ambayo inahusisha mahojiano ya wanamichezo mbalimbali, Hisabati, Maswali ya Dr Panjuani, Robo saa ya pili ya nguvu kwa habari za kimataifa, ikiwemo Soka, Basketball, Boxing,Tennis, Rugby,Formula 1,Golf, Cricket, Netball na kadhalika, na mwisho kuna kitu kinaitwa, Cha kuchabo,,ambacho kinapekua habari zilizojificha.

  Pamoja na yote hayo, bado pia kuna burudani ya kutosha ua muziki uliopangika vizuri toka kwa ma Dj waliobobea kwenye Burudani, RDJ’S.  0 0  0 0  0 0

  Huwezi  kufikiria  umiliki  wa kampuni  kabla  ya kufikiria  kuhusu  mtaji  wa  kampuni. Mtaji  wa kampuni ni  suala  nyeti  kwa  wenye  wazo  la  kumiliki  kampuni  au  wanaomiliki  kampuni  tayari.  Mtaji  ndio  kila  kitu  katika  kampuni. Tangu  unapokuwa  katika  harakati  za  kusajili kampuni  utalisikia  neno  hili  mtaji  karibia katika  kila  hatua  unayopita. Niseme  mapema  kuwa  mtaji  mdogo  ndio  kampuni ndogo  na  mtaji  mkubwa  ndio  kampuni  kubwa.  Kwa  hili  mitaji  imegawanyika  mara  mbili upo  mtaji  wa  maandishi unaokuwa  kwenye   katiba  na  waraka  wa  kampuni( MEMAT)   na  upo  mtaji  wa  mali  halisi ( physical assets).
  Mtaji  wa   unaokuwa  kwenye  nyaraka nilizotaja  mara  nyingi  hautambulishi  ukubwa  au udogo  wa  kampuni. Hii  ni  kwasababu  mtaji  huu  huwa  ni  maandishi  tu na  yawezekana  kiwango  cha fedha  kilichoandikwa   humo  kama mtaji   hakipo  kabisa  katika  kampuni.  Hivyo  mtaji  wa  aina  hii  hauna  uhusiano wowote   na  ukubwa  au  udogo  wa  kampuni.  Kwa  upande  wa  mtaji  wa  mali   halisi   huu  ndio  mtaji  ambao  huweza  kutambulisha  ukubwa  au  udogo  wa  kampuni.  Hii  ni  kwasababu mtaji  huu  huwa   sio  maneno  tu  au maandishi  bali  mali kwa  maana  ya  mali . Na  kisheria  mali  kama  mali  za  kampuni  ndio  mtaji  wa  kampuni  na  ndio  nitakaozungumzia  hapa.  Nitazungumzia  mtaji  lakini  zaidi   ni  kujua  mtaji  hujumuisha  nini. 

  0 0
 • 05/14/15--23:00: kiwanja kinauzwa pugu
 •  Ukubwa: mita 20 kwa 36 ( 20m X 36m )
  Eneo: Bangulo CCM, Pugu Dar es Salaam
  Bei: Milioni 9 na laki 5  ( 9.5m/- ) Tshs/
  Mawasiliano: +255 657 582 510 


  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa Shirika lisilo la kiserikali la Al Muntada lenye makao yake makuu jijini London Uingereza wanaoendesha zoezi la upasuaji na tiba ya moyo kwa zaidi ya watoto 70 katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Picha na Freddy Maro

  Mei 14, 2015 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  ametembelea kitengo cha upasuaji wa moyo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuwaona watoto ambao wamepata matibabu ya moyo kwa njia ya upasuaji na kuziba tundu la moyo bila kupasua, zoezi ambalo limeendeshwa na timu ya madaktari kutoka Taasisi ya Al Muntanda ya London, Uingereza, kwa kushirikiana na madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili. Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU imetayarisha video ya ripoti hii kuhusiana na ziara hiyo. Bofya mshale kuendelea...

  0 0


  0 0
 • 05/15/15--00:56: MCHUMA UKO SOKONI
 • Bei Milioni 6.5 
  Maelewano yapo. 
  Kwa maelezo zaidi 
  cheki kwa namba hii: 0713262902. 
  Karibu.


  0 0

  Majenerali wawili waliotekeleza jaribio la mapinduzi nchini Burundi dhidi ya rais Pierre Nkurunziza wametiwa mbaroni baada kushidwa kwa jaribio lao hilo, huku kiongozi mkuu wa mapinduzi hayo jenerali Godefroid Niyombare akidaiwa kuingia mititi na sasa anasakwa.

  Hayo yemeelezwa leo hii na Msemaji wa Rais Nkurunziza,Willy Nyamitwe.

  Awali Jenerali Niyombare alikaririwa akikiambia chombo cha habari cha AFP kwamba yeye na wafuasi wake watajisalimisha kwa serikali ya Rais Nkurunziza, huku akiongezea kuwa ''natumai hawatatuua''.
  Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
  Naibu kiongozi wa jaribio la mapinduzi nchini Burundi, alikiri kuwa jaribio lao limeshindwa kufanikiwa, baada ya kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa jeshi la taifa hilo. Habari za kushindwa huko zimetolewa wakati rais Pierre Nkurunziza akitangaza kuwa amerejea nchini Burundi.

  Akitangaza kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nkurunziza aliwashukuru wanajeshi na polisi kwa ''uzalendo wao'', na wananchi wa Burundi kwa ''subira'' waliyoidhihirisha.

  Majaribio ya kuiangusha serikali ya rais Pierre Nkurunziza yalitokea yeye akiwa nchini Tanzania, alikokuwa amekwenda kuhudhuria mkutano wa marais wa kikanda kuhusu hali ya kisiasa nchini mwake.
  Kiongozi mkuu wa Jaribio la Mapindizi nchini Burundi,Meja Jenerali Godifroid Niyombare
  Lakini mpaka wakati huu, haijulikani hasa wapi alipo rais huyo, na taarifa za kurejea kwake hazikuthibitishwa na vyanzo huru.

  Kufuatia mkutano wa dharura jana Alhamisi, Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika, lililaani jaribio lolote la kutwaa madaraka kupitia vurugu nchini Burundi, na kuhimiza mazungumzo kati ya makundi yanayohasimiana.

  Mjini New York, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon na maafisa wake waandamizi, walikuwa wanafuatilia matukio nchini Burundi kwa wasiwasi mkubwa, alisema msemaji wake.

  Nalo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa litawachukulia hatua wale wote wanaowafanyia vurugu raia na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria.

  0 0

  Mkuu wa shule ya sekondari Maua seminari ,Erastus Tesha akizungumza katika mahafali ya 33 kwa wahitimu wa kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.
  Mgeni rasmi katika mahafali hayo ,mbunge wa kuteuliwa na rais ,Mh James Mbatia akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wageni waalikwa .
  Wahitimu wa kidato cha sita shule ya sekondari Maua Seminari.
  Baadhi ya wageni waliofika shuleni hapo kwa ajili ya mahafali ya ndugu zao wanaotarajia kuhitimu kidato cha sita katika shule ya sekondary ya Maua.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Familia ya marehemu mzee Japhet Mbaga, wa Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, NENDIWE MBAGA, kilichotokea hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, siku ya Jumatano mchana, tarehe 13 Mei 2015 kwa ugonjwa wa pneumonia. 
  Mama Nendiwe ni mama mzazi wa MARY RUSIMBI, Hillary Mbaga, Michael Mbaga, Rose Mshana, Stella Mbaga na John Mbaga.
  Mazishi yanatarajiwa kufanyika makaburi ya Kinondoni, siku ya Jumapili tarehe 17 Mei 2015 saa 10.00 jioni. 
  Ratiba ya kutoa heshima za mwisho itafanyika siku hiyo hiyo, saa 7.00 mchana nyumbani kwa Mary Rusimbi (Mkurugenzi Mkuu, WOMEN FUND TANZANIA) eneo la Tabata, nyumba za TAZARA. 
  Baadaye saa 9.00 Ibada ya kumuaga itafanyika Kanisa la KKKT Mwananyamala B.

  "Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake na lihimidiwe."

older | 1 | .... | 837 | 838 | (Page 839) | 840 | 841 | .... | 3284 | newer