Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live

BAADA YA KUKWAMA KWA MASAA KADHAA, MV MAENDELEO YATIA NANGA SALAMA UNGUJA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, 
Swahilivilla
Meli ya Mv Maendeleo imetia nanga salama katika bandari ya Unguja ikitokea kisiwani Pemba baada ya kukwama kwa muda wa masaa kadha katika eneo la bandari ya Mkoani.
 Mv Maendeleo ikiwa imetegesha katika katika eneo la bandari ya Mkoani Pemba.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka bandarini Unguja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari nchini Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji Ali, Afisa wa ngazi za juu katika MV Maendeleo alithibitsha kuwa meli hiyo imetia nanga ikiwa na abiria wote salama.
"Siwezi kuzungumza sana kwa sasa kwa vile bado tumo katika harakati za kushusha abiria", alisema afisa huyo na kuongeza kuwa atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuongea baadaya mkutano na maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Zanzibar utakaofanyika mara tu baada ya kumaliza ushushaji wa abiria hao.
Mawasiliano ya Ndugu Omar Ali na maofisa wa ngazi za juu katika Serikali ya Zanzibar na MV Maendeleo, yanakuja katika juhudi za kuwapatia taarifa za uhakika wanachama wa ZADIA na Wazanzibari kwa ujumla nchini Marekani, kufuatia khofu na mtafaruku vilivyojitokeza miongoni mwa wanajumuiya hiyo baada ya habari za kukwama kwa meli hiyo kisiwani Pemba.
Bwana Ali amewataka wanajumiya hiyo kutokuwa na khofu yoyote juu ya ndugu na jamaa zao waliokuwa katika meli hiyo, kwani abiria wote wamefika salama salmini.
Meli ya Mv Maendeleo ilikwama baada ya kukosea njia wakati ikitoka katika banndari ya Mkoani kisiwani Pemba ikiwa na abiria zaidi ya 260. 
Bado haijajulikana rasmi ni hasara gani za kiuchumi zilizosababishwa na mkwamo huo wa abiria ambao baadhi yao walikuwa katika safari za kibiashara.

TAWLA YAADHIMISHA MIAKA 25 YA KUJENGA UWEZO NA KUFANYA UCHECHEMUZI WA HAKI ZA WANAWAKE NCHINI

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 CHAMA cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) wamefanya maadhimisho  ya miaka 25 ya kujenga uwezo  na  kufanya uchechemuzi juu ya  haki za  wanawake, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1990 hapa nchini.

 Akizungumza katika uzinduzi wa Maadhimisho ya Chama hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa jengo la  YWCA jijini Dar es Salaam leo,  Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria (TAWLA), Magreti Ringo amesema kuwa  chama hicho kimefanikiwa kutoa msaada wa kisheria kwa wanawake wasiopungua milioni tano kupitia vituo vilivyopo Dar es Salaam,Tanga,Arusha na Dodoma.


 Pia chama hicho kimefanikiwa kutoa mafunzo kwa wasaidizi wa kisheria 402 ili kuhakikisha jamii  inapata msaada wa kisheria na kuhamasisha jamii, kujua masuala ya kisheria kupitia machapisho mbalimbali.


 Ringo amesema kuwa  chama chicho  kinaratibu  muungano wa  jukwaa la jinsia la katiba, ambalo limefanya kazi na kuchangia kuwepo kwa ibara nyeti zinazolinda haki za kijinsia kwenye katiba inayopendekezwa.


 Katika maadhimisho ya miaka 25 ya chama hicho kimehamasisha uandikaji wa wosia bila gharama yeyote.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wanasheria (TAWLA), Magreti Ringo akizungumza na wandishi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi wa chama hicho,Tika Mwambipile na kushoto ni Mjumbe wa Baraza uuguzi wa TAWLA,Annamaria Moreybo.


 Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 25 ya  Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA).(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)

MAALIM SEIF AHIMIZA WAZANZIBAR KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad amewataka Wazinzibari kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura linalotarajiwa kuanza Mei 16 mwaka huu, ili waweze kutumia haki zao  kikatiba za kushiriki uchaguzi mkuu kwa kupiga kura.


Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Cha  Wananchi (CUF),amesema kuwa uchaguzi mkuu uliopita ulikuwa wa uhuru na wa amani lakini ulikuwa na kasoro katika daftari la wapiga kura, kwamba wapiga kura walikuwa na kadi mbili hali ambayo kwa sasa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inapaswa kuliangalia jambo hilo kwa umakini.


Amesema kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu  Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ipitie upya wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki kuhakiki makosa yaliyokuwa yakijitokeza kwa watu kujiandikisha mara mbili.


Maalim Seif amesema kuwa katika kasoro hizo ZEC iharakishe kutangaza majimbo ya uchaguzi kutokana na kazi hiyo ilishafanywa muda mrefu kupitia Wizara ya  Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.



Amesema katika kasoro zilizokuwemo kwenye daftari la wapiga kura ni pamoja watu waliofariki kuendelea kupiga kura kutokana na mfumo  huo wa kutohakiki wapiga  kura pamoja na watu wasio wakazi wa Zanzibar kupiga kura.


Hata hiyo amesema kuwa atagombea katika uchaguzi mkuu na yaye ana sifa na wengine wenye sifa wanaweza kuomba ridhaa ndani ya chama kugombea .


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo,juu ya harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu Zanzibar, kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Salim Biman na kushoto ni Naibu katibu Mkuu Zanzibar (CUF),Nassoro Ahmed Mazrui.

Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CUF Ismail Jussa, akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa kitengo cha Sera,Utafiti na Mafunzo, Hassan Jani Masoud akielezea  juu ya utafiti walioufanya kupitia kitengo hicho cha CUF juu ya changamoto ya daftari la wapiga kura Zanzibar katika mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waandishi habari wailiohudhuria katika mkutano na ulioitishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad ,(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII).

DRFA YACHEKELEA TIMU ZAKE KUMALIZA TATU BORA LIGI KUU

$
0
0
Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam kimeonesha furaha yake baada ya timu tatu zilizo katika himaya yake, kumaliza katika nafasi za juu kwenye ligi kuu Tanzania bara iliyomalizika jumamosi mei 9,2015.

Kamati ya utendaji ya DRFA chini ya mwenyekiti wake Almas Kasongo,imesema ni jambo la kufurahisha kuona mkoa wa Dar es salaam unafanya vizuri kisoka na kuwa mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine.

Timu hizo zimepongezwa kutokana matayarisho waliyoyafanya tangu kuanza kwa msimu,ambapo mabenchi ya ufundi yameonesha kuwa na nia ya dhati kuleta ushindani katika ligi.

Yanga SC na Azam Fc ndizo zitakazoiwakilisha nchi katika michuano ya vilabu barani afrika,ambapo Yanga itakwenda huko kuwania kombe la klabu bingwa baada ya kutwaa uchampioni,huku Azam ikiwania kombe la shirikisho baada kumaliza katika nafasi ya pili,wakati Simba imemaliza katika nafasi ya tatu.

Aidha DRFA imeipongeza Tff na kamati ya bodi ya ligi kwa usimamizi mzuri wa ligi msimu huu licha ya kuwepo na changamoto ndogondogo kwa vilabu kulalamikia miundombinu ya vyumba vya kubadilishia nguo viwanjani,na uonevu wa baadhi ya waamuzi.

Hata hivyo imeishauri Tff kuangalia kwa kina na kuzifanyia kazi changamoto hizo zilizojitokeza msimu huu ili zisijirudie tena katika msimu ujao,kwa lengo la kuiboresha ligi ya Tanzania,ambayo kuanzia msimu ujao itakuwa na jumla ya timu 16.

Pamoja na hayo DRFA imezishauri Yanga na Azam kujipanga vizuri kwaajili ya mashindano ya vilabu afrika msimu ujao, ili kuandika historia na kuleta vikombe hivyo kwa mara ya kwanza hapa nyumbani.

MBUNGE WA KINONDONI AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA KATIKA MATATIZO

$
0
0
MBUNGE wa Kinondoni,Idd Azzan amewataka wananchi kuwa na ushirikiano wakati wa matatizo ili kuwafariji wahanga waliopata majanga.

Mh.Azzan aliyasema hayo jana wakati alipowatembelea wananchi wake waliopata mafuriko pamoja na wale ambao nyumba zao zimezingirwa na maji,amesema kuwa sasa ni wakati wa watu kusaidia wenzao waliopata na maafa.

Amesema kuwa ametoa mpira wa kutolea maji kutokana na kuepusha na magonjwa ya mlipuko yatakayotokana na maji  yaliyojaa katika mitaa iwamo Kipindupindu na Maralia.

Mh.Azzan amesema kwa jimbo lake sehemu kubwa limeathiriwa na mafuriko hata maeneo ambayo huwa maji hayafiki, hivyo kila mtu anawajibu wa kusaidia kwa nafasi yake.
Mbunge wa Kinondoni,Idd Azzan akishiriki kutoa maji katika Mtaa wa Kanazi,Kinondoni 'B' jana yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

RIDHIWANI ATOA MSAADA WA FEDHA NA SARUJI UJENZI WA WODI

$
0
0
Mwenyekiti wa Kijiji cha Pongwekiona Rajab Mgaya kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja na mifuko 70 ya Saruji toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Iddy Swala ambaye alimwakilisha Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete, fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili kwenye zahanati ya Kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Kimange Hussein Hadingoka kushoto akipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja toka kwa katibu wa Mbunge wa Chalinze Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge kwa ajili ya ofisi ya kata fedha zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete.

Na John Gagarini, Chalinze

ADHA ya akinamama wajawazito kujifungua mbele za wanaume kutokana na zahanati ya Kijiji cha Pongwe Kiona wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuwa na chumba kimoja cha matibabu huenda ikaondoka baada ya kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni moja na mifuko 70 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume.

Kutokana na zahanati hiyo kuwa na chumba kimoja imesababisha akinamama kujifungua huku kukiwa na wanaume jambo ambalo limesababisha kutokuwa na usiri hivyo utu wa mwanamke kutokuwepo. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambapo fedha na Saruji vilikabidhiwa na Katibu wa Mbunge huyo Iddy Swala kwa niaba ya Mbunge.

Akizungumzia changamoto hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Rajab Mgaya alisema kuwa zahanati hiyo ilijengwa mwaka 1964 na ina wodi moja tu.

“Tunamshukuru Mbunge kwani hii ilikuwa changamoto kubwa kwa akinamama wanaojifungua huku kukiwa na akinababa nao wanapata matibabu humo hivyo usiri kutokuwepo kutokana na hali hiyo,” alisema Mgaya. Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kimange Husein Hadingoka alisema kuwa mbunge huyo ameonyesha upendo wa hali ya juu kwa kutoa vitu hivyo ambavyo vitasaidia ujenzi huo.

Hadingoka alisema kuwa wananchi watafanya ujenzi huo ambapo yeye alitoa 100,000 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo na kusema atafurahi kuona uujenzi huo unakamilika mapema.

Naye moja ya wakazi wa Kijiji hicho ambaye ni mwanamama Sikudhani Ally alisema kuwa kujifungua huku wanaume wakiwepo ni mtihani mkubwa lakini kwa mpango huo utakuwa umeweka stara ya mwanamke.

Kwa upande wake katibu wa Mbunge Swala alisema kuwa mbunge ametoa msaada huo baada ya kutemebelea hivi karibuni akiwa kwenye ziara zake za kikazi na wananchi kutoa kilio chao juu ya hali hiyo.

CCM ARUSHA YATOA ONYO KWA WALIOTANGAZA NIA ARUSHA MJINI

$
0
0
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Arusha,Feruz Bano (kushoto) akimkabidhi kitabu cha kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea aliyetangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute jana ofisini kwake mara alipofika kujitambulisha na kutangaza nia.
mgombea aliyetangaza kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM katika jimbo la Arusha mjini,Kim Fute akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya katibu wa chama hicho wilayani Arusha jana alipofika kujitambulisha na kutangaza nia(picha na moses mashalla).

Chama Cha Mapinduzi(CCM)  wilayani Arusha kimetoa  onyo kwa wagombea waliojitokeza kutangaza nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupiti chama hicho kuacha tabia ya kuchafuana na kuanza kampeni kabla ya muda.

Onyo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na katibu wa chama hicho wilayani Arusha,Ferooz Bano wakati akimkabidhi kanuni za uchaguzi wa CCM mgombea alliyetia nia ya kugombea jimbo la Arusha mjini kupitia chama hicho,Kim Fute .

Mgombea huyo alifika mbele ya ofisi za CCM wilayani hapa kujitambulisha  na kutia nia ambapo mbali na kufanyiwa ukaguzi wa kadi zake za uanachama pia alikabidhiwa kitabu chenye kanuni hizo na kupewa agizo la kutoshiriki kampeni kabla ya muda.

Hadi sasa jumla ya wagombea saba  ambao ni Kim Fute,Phillemon Mollel”Monaban”,Mustapha 
Panju”Bushbuck”,Victor Njau,David Rwenyagira,Deo Mtui,Francis Laiser pamoja na mbunge mstaafu wa jimbo la Arusha mjini,Felix Mrema wamejitokeza kutia nia kuwania jimbo la Arusha mjini.

Akizungumza mara baada kumkabidhi kanuni hizo katibu huyo wa wilaya aliwataka wagombea wote waliojitokeza kutia nia kupitia chama hicho kuacha tabia chafu ya kupakana kuandaa sherehe kwa wapiga kura.

“Muda wa kampeni bado haujafika hatutaki  nyinyi wagombea muanze kuchafuana huko mitaani na wala kuandaa vijisherehe”alisema Bano

Hatahivyo,kwa upande wake mgombea huyo mbali na kushukuru mapokezi ofisini hapo pia alihaidi kufuata maagizo ya chama hicho na kusisitiz kwamba atafuata maagizo ya kanuni hizo kwa umakini mkubwa.

Fute,alitangaza rasmi kuinga katika kinyang”anyiro hicho kupitia CCM huku akijitapa kwamba amejipima na kubaini anatosha kuwa mwakilishi wa jimbo la Arusha mjini kwa kuwa amegundua kuna ombwe la uongozi.

Dkt. Shein aongoza mamia ya waombolezaji kwenye Maziko ya WANA CCM Waliopata ajali jana

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akishiriki katika swala ya maiti kumswalia Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja katika msikiti wa marehemu aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la Marehemu Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu walioshiriki katika maziko ya Marehemu Bi Mwanaidi Zamir Haji miaka 28 mkaazi wa Magogoni Mjini Unguja aliyefariki kwa ajali ya gari iliyopinduka huko Mtowapwani Kaskazini jana na kuzikwa leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe.


TFF YAKUBALI UENYEJI KAGAME CUP

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, leo hii imekubali kuwa wenyeji wa  michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya Vilabu maarufu kama CECAFA Kagame Cup.

CECAFA ambao ndio wamiliki wa mashindano haya watatoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki na wakipokea uthibitisho wa ushiriki wao watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo.

Michuano hii inatarajiwa kuafanyika nchini kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

MAONYESHO YA KUUNGANISHA WAKULIMA NA FURSA ZA MITAJI YAFANYIKA WILAYANI BABATI

$
0
0

Asasi zisizo za kiserikali zinazojishughulisha na shughuli za Kilimo biashara za masharika ya TAHA, SNV,MVIWATA, AGRO PRO FOCUS,HIVOS, TCCIA na  TRIAS leo zimefanikisha kufanya maonesho ya Kuunganisha Wakulima na Fursa za Mikopo ambayo yamelenga kuwakutanisha wakulima na wafanya biashara wa mazao ya kilimo pamoja na Taasisi za kifedha na zile zinazotoa mikopo kwa ajili ya shughuli za Kilimo Biashara. Katika picha ni Eneo la viwanja vya Kwaraa Halmashauri ya Wilaya ya Babati ambavyo vinatumika kwa ajili ya kuwakutanisha wakulima na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wakulima(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
2
Afisa wa NMB akifafanua jambo kwa mkulima wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika Katika Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwenye Viwanja vya Kwaraa na yamefunguliwa na Mwenyekiti wa chemba ya biashara Mkoa wa Manyara ndugu Athumani Karunde.

Kulia Mkurugenzi wa TAHA Bi. Jacqueline Mkindi akiwa na Mgeni rasmi ndugu Athumani Karunde wakati wa kutembelea mabanda ya waoneshaji

Wakulima wakipokea maelezo ya namna ya kuunganishwa na fursa za Mikopo toka kwa maafisa wa TAHA.

NAPE AZINDUA KIKUNDI CHA MICHEZO CHA TEGETA JOGGING.

$
0
0
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi cha michezo cha Tegeta Jogging and sports club ambapo aliwaambia vijana wajiandikishe kwenye daftari la kupiga kura kwanza na kuweka itikadi za vyama pembeni, pia alitoa pongezi kwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi William Lukuvi kwa kazi nzuri ya kusimamia viwanja vya wazi vilivyovamiwa hasa katika wilaya ya kindondoni virudi visaidie katika kukuza michezo.
Kada wa CCM Gabriel Munasa akiwasalimia wana vikundi vya Jogging na kuahidi kuvisaidia katika kila hali katika kufanikisha malengo yao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Club .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye pamoja na viongozi wengine na makada wa CCM wakishiriki mazoezi ya kukimbia mchaka mchaka yalioandaliwa na kikundi cha Tegeta Jogging and Sports Clubikiwa sehemu ya uzinduzi wa klabu hiyo ya michezo na mazoezi ya Tegeta.


Taasisi ya Imetosha yatoa msaada kwa kituo cha Buhangija Shinyanga

$
0
0

Toka kushoto ni Kathrin Hoff, kijana Paulo, Masoud Kipanya na Balozi Henry Mdimu.


Taasisi ya Imetosha ya jijini Dar es Salaam leo hii imepeleka misaada mbali mbali katika kijiji cha watoto wasioona cha Buhangija, mkoani Shinyanga ambacho kwa sasa kinahifadhi pia watoto na vijana wenye ualbino takriban 300. 
Misaada hiyo ikiwemo mabelo ya mitumba 2 moja la masweta na jingine la suruali za jeans, unga, mchele, maharage, sukari, chumvi, ndoo 3 za mafuta ya kupikia, sabuni za kufulia box 8, vile vile box 3 za vifaa vya hedhi vitakavyodumu miezi miwili pamoja na nguo za ndani dazeni 12 vyote hivo  imegharimu Tsh milioni mbili na elfu sitini(2,060,000) ambazo zimetolewa na wanachama wa taasisi hiyo iliyojikita kupambana na mauaji ya watu wenye ualbino kwa njia ya elimu.


Akiongea na watoto na vijana hao Mwenyekiti Masoud Kipanya alisema taasisi hiyo inaangalia jinsi ya kutengeneza mazingira kwa kituo hicho kujijengea uwezo wa kujipatia chakula badala ya kutegemea wasamaria wema huja pale watakapojisikia wakati watoto katika kituo hicho wanahitaji kula kila siku.
Mkuu wa kituo hicho aliishukuru taasisi ya Imetosha kwa kuonesha mapenzi ya dhati na watoto wa kituo hicho na kuguswa na changamoto zinazowakuta, kwani si mara nyingi sana watu au taasisi kurudia kupeleka misaada kituoni hapo kitu ambacho Imetosha wamekifanya. Wiki 3 zilizopita taasisi hiyo ilipeleka msaada wa chakula kituoni hapo.
Awali mtafiti wa masuala yahusuyo watu wenye ualbino mJerumani Bi Kathrin Hoff alielezwa kufurahishwa na jitihada zinazooneshwa na Imetosha kwa uhamasishaji inayoufanya kwa jamii ya Ki Tanzania, pia amepongeza sana hatua ya Imetosha kutaka kukifanya kituo cha Buhangija kujitegemea badala ya kubaki tegemezi kama ilivyo sasa. Kathrin Hoff ni mhitimu toka chuo kikuu cha Mainz nchini Ujerumani.

MTAA KWA MTAA JIJINI MBEYA NA MR PENGO WA MICHUZI TV

DUNIA KUJADILI CHANGAMOTO NA ATHARI YA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0
Bw. Sam Kutessa, Rais  wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Na  Mwandishi Maalum, 
New York 
Jumuiya ya Kimataifa  inajiaanda  kwa  mkutano maalum na  wa aina yake kufanyika, ambapo  nchi wanachama watakutana  na  kujadiliana kwa kina kuhusu  changamoto na adhari kubwa  zitokanazo na  biashara haramu na matumizi ya dawa za kulevya.

 Mapema wiki iliyopita,    wajumbe wanaoziwakilisha nchi  zao  hapa  Umoja wa Mataifa, walikuwa na mkutano wa siku moja ambao ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano huo maalum utakaofanyika mwezi Aprili  2016.

Mkutano huo wa maandalizi uliofanyika hapa  Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo mawaziri kadhaa kutoka nchi hasa  za  Amerika ya Kati ambako   nchi nyingi zinakabiliwa  na changamoto kubwa ya  biashara hiyo, uliandaliwa na Bw. Sam Kutessa, Rais  wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Katika  majadiliano ya  mkutano huo ,  ilidhihirika wazi kwamba hakuna nchi hata moja   duniani  iwe tajiri au maskini ambayo  haijakumbwa  na  janga  la biashara na  matumizi ya dawa za kulevya.

“ Hakuna nchi ambayo imepona kutokana na biashara hii yenye thamani  ya mabilioni  ya dola. Licha ya juhudi kubwa na raslimali nyingi ambazo mataifa yanatumia   kukabiliana na janga hili, lakini tatizo  linaendelea kukua” akasema Bw. Sam Kutessa wakati akifungua mkutano huo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA

Hospitali ya AMI hatarini kufurushwa kwa kutolipa kodi ya pango ya bilioni tatu

$
0
0
Mahakama Kuu, Kitengo cha Biashara imeamuru kufurushwa kwenye jengo hospitali ya African Medical Investment Ltd (AMI) maarufu kama Trauma Center ya Msasani Jijini Dar es Salaam, baada ya kushindwa kulipa kodi ya pango kwa zaidi ya miezi 26, inayofikia zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.6 (zaidi ya Shilingi Bilioni tatu za Kitanzania).

Hatua hii imefikiwa baada ya mabishano ya muda mrefu ya kisheria baina ya AMI na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa jengo hilo, Bw. Navtej Singh Bains. Akaunti za Benki za Hospitali hiyo ya AMI katika Benki ya EXIM  zilizoambatanishwa na Mahakama zimekutwa zikiwa zimefungwa na fedha zote zikiwa zimetolewa.

Amri hiyo iliyotolewa wiki iliyopita (tarehe 7 Mei, 2015) na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, imeipa mamlaka kampuni ya mnada ya MEM (MEM Auctioneers and General Brokers Limited) kuifurusha Hospitali ya AMI kutoka kwenye jingo ambapo kampuni hiyo inafanya biashara yake.

Amri hiyo ya kutoka kwenye jengo itaanza mara baada ya kuisha kwa kipindi cha notisi cha siku kumi na nne ambacho kimeshatumiwa na AMI. “Ikiwa mdeni aliyetajwa katika hukumu hapo juu (African Medical Investment Limited –AMI) ameamuriwa kwa amri ya mahakama hii ya tarehe 9 mwezi Septemba, 2014 kuondoka na kukabidhi jengo, na ikiwa bado hajaondoka na kukabidhi jengo lenyewe.

“Unaelekezwa kumwondoa mdaiwa/wadaiwa au mtu yeyote anaefanyakazi chini yake atakayekataa kuondoka kwenye jengo na kumuweka anaemiliki amri hii ya mahakama (Navtej Singh Bains- Mwenyenyumba) kwenye nyumba yake,” inasomeka sehemu ya amri ya mahakama iliyoelekezwa kwa kampuni ya mnada ya MEM (MEM Auctioneers).

Amri hii sasa inapelekea kufungwa kwa Hospitali ya AMI, licha ya rufaa zake za kujaribu kuzuia kufukuzwa, imefikiwa baada ya hospitali hiyo kushindwa kutimiza amri ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania iliyoamuru kulipwa kwa dola za kimarekani milioni 1.514 mahakamani pamoja na kodi ya kila mwezi ya kiasi cha dola za kimarekani 64,000 kila mwezi kufuatia mgogoro wa kodi ya jengo.

Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Mbarouk, Salum Massati na Katherine Oriyo waliiamuru Hospitali ya AMI kufanya malipo hayo ndani ya mwezi mmoja baada ya hukumu iliyotolewa Februari 12, 2015, agizo ambalo halijatekelezwa.


Mahojiano na Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kuhusu KISWAHILI

$
0
0
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi zaidi kusini mwa jangwa la Sahara.

Ni lugha ya taifa kwa nchi za Kenya na Tanzania na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda, Visiwa vya Comoro na nchi nyingine Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika.

Ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa. Lakini , licha ya ukubwa wake, lugha hii inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Hivi karibuni, Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kilifanya mkutano wake wa nne, ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi. Na amekuwa mkarimu sana kujiunga nasi kuzungumzia juu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zake.

“NIPO STUDIO” YA JENNIFER MGENDI KUACHIWA

$
0
0
Mtayarishaji wa filamu na mwimbaji wa siku nyingi Jennifer Mgendi anakusudia kuachia filamu yake ya “Nipo Studio” mapema wiki hii. Akiongea na blogu hii Jennifer amesema filamu hiyo imekamilika kwa kila kitu na itaingia sokoni wiki hii ikiwa imewashirikisha wasanii mbalimbali akiwamo shosti wake wa siku nyingi Bahati Bukuku, Bibi Esta, Hassan Mbangwa, Gwamaka Kametta na wengine wengi.

Jennifer amesema filamu hii inazungumzia changamoto mbalimbali anazokutana nazo Bibi Esta pale anapokuwa na ndoto ya kuwa mwimbaji huku umri na kipato vikiwa kikwazo kwake.

Wakati huo huo Jennifer  amesema maandalizi ya tamasha lake la uzinduzi wa video ya Wema ni akiba yanaendelea vizuri na tamasha hilo litafanyika kama ilivyopangwa tarehe 28 Juni katika kanisa la DCT Tabata Shule huku Mgeni Rasmi akitarajiwa kuwa Askofu Mkuu wa kanisa la Tanzania Assemblies of God , Dr. Barnabas Mtokambali.

JK akutana na Rais wa Algeria Mhe Abdelaziz Boureflika jijini Algiers

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MAREHEMU JOHN NYERERE DAR

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu John  Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John 
anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati alipowasili  nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu John Nyerere, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati  alipowasili nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu John Nyerere.  Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo cha msiba wa marehemu John Nyerere, wakati  wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Msasani, jijini Dar es Salaam leo Mei 11, 2015. Marehemu John anatarajia kuzikwa  keshokutwa nyumbani kwao Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na baadhi ya viongozi na waombolezaji nyumbani kwa Mama Maria  Nyerere Msasani jijini Dar es Salaam, leo wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu John Nyerere. Marehemu John anatarajia kuzikwa keshokutwa nyumbani kwao Butiama. Picha na OMR

NEC KUGAWA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI KWA VIGEZO

$
0
0

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi Nchini(NEC),inatarajia kuchunguza mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi na kuyagawa kwa ajili ya uchaguzi wa Wabunge unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa NEC,Jaji Mstaafu Damian Lubuva wakati alipokutana na viongozi wa Vyama vya Siasa kujadili masuala mbalimbali ya Tume katika kuelekea uchaguzi Mkuu.

Amesema  ugawaji wa Majimbo,Tume imezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo idadi ya watu,upatikanaji wa mawasiliano hali ya kijiografia na vigezo vingine kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge ya mwaka 2010.

Jaji Lubuva amesema ugawaji wa majimbo hufanyika kila baada ya miaka 10 na ugawaji huo utafanywa kabla ya Oktoba na hii inatokana na kuongezeka kwa idadi ya watu katika majimbo na kuona kuna umuhimu wa kugawa majimbo kwa mujibu wa sheria.

Aidha amesema ugawaji wa majimbo sio kwa kuangalia idadi ya watu,bali upatikanaji wa mawasiliano inayojumuisha miundombinu,simu na vyombo vya habari kwa ajili ya kupata mwakilishi atakayeharakisha maendeleo katika eneo husika.

Lubuva amesema kuwa uchaguzi mkuu utafanyika kama ulivyokuwa umepangwa kutokana na zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaendelea katika mikoa iliyoainishwa.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC),Jaji Mstaafu,Damian Lubuva akizungumza katika Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka  huu uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmoud Hamid.
  Kamishina wa Tume ya uchaguzi,Profesa Amon Chaligha akizungumza katika mkutano wa viongozi vyama vya Siasa katika ukumbi wa Hoteli ya New Africa leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Julius Malaba.
 Mwenyekiti wa Taifa Chama cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba akichangia maada katika Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka  huu uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Part (TLP),Nancy Mrikaria akitoa ufafanuzi juu ya viti maalumu Bungeni katika Mkutano wa Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini kujadili masuala mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka  huu uliofanyika leo katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)
Viewing all 110182 articles
Browse latest View live




Latest Images