Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

BODI YA UTT-PID NA MENEJIMENTI YAKE YAFANYA ZIARA YA MAFUNZO CHINA

$
0
0
kwana Bodi ya UTT-PID ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wakiwa na wenyeji wao katika jiji la Chengdu ambapo walifanya ziara katika maeneo tofauti ya uwekezaji na manufaa wanayopata wananchi wa jiji hilo. Ziara hiyo ya siku Tano katika Miji tofauti inatarajia kukamilika Tarehe kumi kabla ya kurejea nyumbani.

Na Mwandishi Maalum
Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake ipo nchini China katika ziara maalum ya Mafunzo na kujenga uzoefu ya siku tano ikiwa na lengo la kuimmalisha utendaji kaziw wa taasisi hiyo.

Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. E Mlaki pamoja na Menejimenti wapo katika miji mbalimbali na kutembelea maeneo tofauti ya uwekezaji ilikushuhudia manufaa wanayopata wananchi wa maeneo hayo.

Kazi za UTT-PID ni pamoja na Utoaji huduma za ushahuri katika maeneo ya upembuzi yakinifu wa miradi mbalimbali, Uratibu wa fedha na huduma zinazohusiana katika maandalizi ya mapendekezo ya miradi kwa benki au taasisi za fedha, uteuzi wa watoa huduma kuhusiana na maandalizi ya zabuni na usimamizi wa majengo na mali ambao ni utoaji wa huduma fanisi za usimamizi wa majengo yaliyochini ya uangalizi thabiti wa taasisi.
pili
Bodi ya UTT-PID pamoja na Menejimenti ikipata Maelezo kutoka wataalum wa uzalishaji nishati toka mji wa Chengdu.


Mamilioni ya Kopa Bayport yazidi kupata wenyewe

$
0
0
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Ngula Cheyo, katikati akizungumza jambo wakati wa droo ya pili ya Kopa Bayport kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ambapo jumla ya washindi watatu kila mwezi wanapatikana na kila mmoja kujishindia jumla ya Sh Milioni moja. Kulia ni Afisa wa Huduma kwa Wateja wa taasisi hiyo, Gladys John, huku kushoto akiwa ni bwana Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania. Picha zote na Mpiga Picha wetu.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHINDANO la Kopa Bayport kwa njia ya mtandao linaloendeshwa na taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, limezidi kuchanja mbuga, baada ya wateja watatu wa mwezi Mei kuibuka na Sh Milioni moja kwa kila mmoja, huku mikoa ya Bukoba, Njombe na Dar es Salaam ikichanua katika droo iliyochezeshwa jana, jijini Dar es Salaam.

Wateja hao walioshinda katika shindano hilo ni Tryphone Mashamba mkoani (Njombe), Kisa Mboya (Dar es Salaam) na Oscar Gadawu (Bukoba) ambao wote kwa pamoja wameibuka na Sh Milioni moja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz, ikiwa ni huduma nzuri kutoka kwenye taasisi hiyo ya Bayport Financial Services.
Afisa wa Huduma kwa Wateja wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Gladys John katikati akichagua koponi ya mmoja wa washindi wa shindano la Kopa Bayport linaloendelea ambapo washindi watatu wamepatikana na kila mmoja kupata bahati ya kujinyakulia Sh Milioni moja kila mmoja baada ya kukopa kwa njia ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz. Kulia ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport, wakati kushoto ni Humud Abdulhussein, Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.

MH. PINDA ATEMBELEA KIWANDA CHA DAWA ZA KUUA WADUDU, KIBAHA MKOANI PWANI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mitambo ya kiwanda cha dawa za kuua wadudu hasa mbu kinachojengwa na watalaamu kutoka Cuba, Kibaha mkoani Pwani Mei 8, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watalaamu kutoka Cuba wanaojenga kiwanda cha dawa za kuua wadudu hasa mbu, Kibaha mkoani Pwani Mei 8, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua kiwanda cha kutengeneza dawa za wadudu hasa mbu, kibaha mkoani Pwani Mei 8, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la ugonjwa wa malaria kwa kuamua kujenga kiwanda cha kisasa cha kutengeneza dawa za kuua viluwiluwi wa mbu wanaosababisha malaria.

Kiwanda hicho cha viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kimejengwa eneo la TAMCO, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua kiwanda hicho jana jioni (Ijumaa, Mei 8, 2015), Waziri Mkuu alisema ana imani kujengwa kwa kiwanda hicho kutamaliza tatizo la malaria hapa nchini na katika nchi za jirani.

“Malaria ni ugonjwa hatari na unaongoza kwa kusababisha vifo hapa nchini. Watu karibu milioni mbili wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na ugonjwa huu. Tukianza kutengeneza hizi dawa zitasaidia sana kupunguza tatizo hili na kuokoa maisha ya watoto na wanawake wajawazito ambao ndiyo waathirika wakubwa,” alisema.

Akielezea utendaji kazi wa dawa hizo, Waziri Mkuu alisema: “Dawa hizi zinapotumiwa kwenye madimbwi, viluwiluwi ni lazima watakufa katika muda wa saa 24… na mle kwenye dimbwi dawa ile inabakia ikifanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja. Hii ina maana wakizaliwa viluwiluwi wengine pia wanakufa bila hata kuweka dawa nyingine,” alisema.

Kiwanda hicho ambacho kitatoa ajira za moja kwa moja 186, kinatarajiwa kuzinduliwa Juni 25, mwaka huu na Rais Jakaya Kikwete. Kinatarajiwa kuanza uzalishaji wa majaribio mapema mwezi ujao.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na viongozi wa Mkoa wa Pwani waliofika kushiriki ukaguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bw. Evarist Ndikilo alitumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania kujenga viwanda vingi zaidi katika Mkoa huo.

Akitoa maelezo kuhusu utengenezaji wa dawa hizo wakati Waziri Mkuu akikagua kiwanda hicho, Msimamizi Mkuu wa ujenzi, Dk. Ricardo Campos Menendez alisema ujenzi wa kiwanda hicho hapa nchini utatoa fursa kwa Tanzania kuuza dawa hizo kwa nchi jirani za Kenya, Congo – DRC ambazo pia zinasumbuliwa na tatizo la malaria.  

“Tukishazaliza dawa za kutosha na kuzisambaza kwenye mikao yote, itabidi tuangalie uzalishaji wa kibishara kwa ajili ya nchi jirani zenye tatizo kama hili… hiki ni kiwanda pekee barani Afrika,” alisema.

Alisema pia kwamba kiwanda kitafanya kazi kwa karibu na vyuo vikuu kufanya tafiti na kutoa fursa za kutengeneza dawa za aina mbalimbali kulingana na mahitaji yaliyopo.


Kiwanda hicho kinachojengwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na kampuni ya LABIOFAM SA ya Cuba, kitakuwa na uwezo wa kuzalisha lita milioni sita za dawa ya Biolarvicides kwa mwaka.  

MTEMVU ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MVUA TEMEKE

$
0
0
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Yombo Relini Yusufu Marko (kulia) akimwelekeza jambo wakati alipo fika katika maeneo hayo baada ya kuzunguuka maeneo tofauti na  Mbunge Abbas Mtemvu.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Abdon Kidege, akimwelekeza jambo Mbunge wa Jimbo hilo Abbas Mtemvu wakati wa ziara ya kutembelea na kuwaona wananchi waliopatwa na mafuriko ya Mvua zinazo endelea kunyesha
 Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na wananchi walio patwa na mafuriko maeneo ya Wailesi alipo watembelea
 Magari yakipita kwa shida na eneo lililoharibiwa na mafuriko.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

AutoSueco (VOLVO) delivers Mining Equipments worth $2.9

$
0
0
 AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) proudly handing the keys for one of the Articulated Haulers when delivering mining equipments worth of US$ 2.9m to Namoya Procurement Manager, Mr. Serge Longo (centre) in Dar es Salaam recently. Witnessing (left) is Namoya Project Manager, Mr. Doyen Kwabo. 
AutoSueco (VOLVO) Commercial Manager, Mr. Alen Nkya (right) gestures with Namoya Procurement Manager, Mr. Serge Longo (centre) and Namoya Project Manager, Mr. Doyen Kwabo (left) after delivering several mining equipments in Dar es Salaam recently.

TANZIA: MSIBA UK

$
0
0
Nasikitika kutangaza kifo cha Mtanzania mwenzetu aitwaye Gertrude Matesh Hodgson. Ambaye alikuwa anakaa katika anuani 37 Cromer Street, Clifton,  York YO30 6DQ 


Marehemu amehifadhiwa katika hospitali ya  Cottingham, huko YORK. 
Ameacha binti mmoja ambae anasoma chuo kikuu hapa UK.

Anategemea kuzikwa hapa hapa UK.

Msaada wa Ushauri na hali unahitajika sana.

Mawasiliano:-

Dada Kissa +447510145626

Mwanamisi 07448755475

Asante sana Mungu na awabariki nyinyi nyote.

Kwa niaba ya ndugu zetu wafiwa  naomba kuwasilisha kwenu account namba kwa msaada wenu watanzania wa UK

Account no:39860655
Sort Code: 56-00-70
Natwest Bank.
Name: Jacqueline E. Josephat

TANZANIA YAANDIKA HISTORIA NYINGINE KWA KUZIBA MATUNDU YA MOYO BILA KUFUNGUA KIFUA

$
0
0
Mwezi Mei tarehe 9, mwaka 2015, Tanzania imeandika historia nyingine baada ya kufanya Tiba ya moyo bila ya kufanya upasuaji kwa kuziba matundu yaliyoko kwenye moyo kwa kutumia “kifaa maalum” bila kufungua kifua kama ilivyozoeleka. Tiba hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini kupitia Idara ya Tiba na Upasuaji Moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 9 hadi 16 Mei, mwaka huu. Madaktari hawa wamekuja kupitia taasisi ya Al Mutanda Islami Trust ya Uingereza. Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto amesema jumla ya wagonjwa zaidi ya 20 wanatarajiwa kupatiwa tiba hii.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto kwake ni Prof. Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 8 hadi 16 Mei, mwaka huu. Aliyepo mwisho kulia ni Sheikh Said Ahmed Abri ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kiislam la hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn Islamic Foundation na shirika hili ndilo lililoratibu timu hii ya madaktari kuja kutoa huduma.
Baadhi ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath Lab) mtambo wa kufanya uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na pia kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua kifua.

INTRODUCING Lady Jaydee - Give Me Love (Official Video)


ATHARI YA MVUA JIJINI DAR DAR ES SALAAM

$
0
0
Athari ya mvua hasa kwa miundombinu jijini Dar es salaam ni kubwa. Hii  ni sehemu ya barabara ya Mbezi Chini ikiwa imekatika kufuatia mvua kubwa ilionyesha siku nzima ya jana.
Uchafu mkubwa uliokuwa umeziba daraja la mto mbezi chini ukiondolewa baada ya maji ya mto huo yaliyokuwa yakitiririka kwa kazi,kuziba kwa daraja hilo ilipelekea maji ya mto huo kupita juu ya daraja na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na sehemu nyingine.
Pichani ni hali halisi ya maji kutuama mbele ya soko la Mboga mboga na Matunda eneo la Afrika Sana, Sinza, kufuatia mitaro ya eneo hilo kuzibwa na uchafu.PICHA NA MICHUZI JR.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Queen Mother Advocating the United Nations Global Road Safety Week - May 7th to May 11th, 2015:

$
0
0
The United Nations reminds each and everybody of us to observe its Global Road Safety Week which starts on May 7th and ends on May 11th, 2015. The week reminds us to be responsible for our actions while driving on the road. 
It reminds us that road accidents are the number one killer of our children and young people across the world. In Tanzania itself, road accidents have claimed the lives of hundreds of people in the past two months. 
 Drive responsibly and join the United Nations to stop road accidents. Dr. Delois Blakely, also known as Queen Mother who takes on the role of the Goodwill Ambassador to Africa as the Community Mayor of Harlem disseminates this important message to remind us of the United Nations Global Road Safety Week:

Susan G Komen walk 2015 a hit!

MBUNGE WA JIMBO LA HAI ATEMBELEA ENEO LA TAMBARARE WILAYANI HAI KUJIONEA ATHARI ZA MAFURIKO NA KUTOA POLE KWA WAATHIRIKA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Hai  Mhe. Freeman Mbowe akiwa na mkuu wa wilaya ya Hai Mhe. Anthony Mtaka walipotembelea katika ukanda wa Tambarare kujionea athari za mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge Mbowe akiwa na biongozi wengine wa wilaya ya Hai wakitazama miundombuni ya reli ilivyochukuliwa na mafuriko.
Baadhi ya wananchi wakisalimiana na Mbunge Mbowe katika eneo la mafuriko yaliyosomba reli.
Viongozi wa Chama cha mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kutoa pole kwa waathirika  wa mafuriko uliofanyika katika kijiji cha Kawaya
Mbunge wa jimbo la Hai Mhe. Freeman Mbowe akiwa ameshika kofia mbili, ya CCM na ya CHADEMA  ambazo alizitumia kuchangisha fedha katika mkutano huo kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika ukanda wa tambarare wilayani Hai. Picha zaidi BOFYA HAPA

basi la kampuni ya Dar Express lateketea kwa moto wilayani Bagamoyo

$
0
0
 Taarifa zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani SACP Jafari Ibrahimu kwamba basi la kampuni ya Dar Express limeteketea kwa moto likiwa safarini kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha. 
Kamanda Ibrahimu wa polisi mkoa wa Pwani amesema 
‘Ni kweli basi la Dar Express leo saa saba mchana limeteketea kwa moto katika kijiji cha Makocho katikati ya kijiji cha Mandera na Mbwewe ndani ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. 
"Lilipata hitilafu kisha likaanza kuungua lenyewe. Bahati nzuri abiria wote wamewahi kushuka salama ila basi limeteketea lote. Hawakuwahi kulizima na hakuna aliejeruhiwa..."

MKUU WA WILAYA MISSENYI MH.FADHIL NKURLU AKAMATA SHEHENA LA NGOZI ZA MAGENDO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu (kushoto) akimhoji dereva wa lori aliyejitambulisha kwa jina la Bw. Kabyemela (mwenye tisheti jekundu) baada ya kuwekewa mtego na kukamatwa na shehena ya ngozi ya magendo iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea nchi jirani. Shehena hiyo ilikamatwa katika kizuizi cha Kyaka.

 Baadhi ya ngozi ya magendo iliyokamatwa baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuweka mtego kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama. Shehena hiyo ya ngozi ya magendo inakisiwa kufika uzito wa takribani tani 10.
--------------------------------------------------------------- 
Missenyi. 8 Mei, 2015 - Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Mh. Fadhil Nkurlu amekamata shehena kubwa ya ngozi ya magendo yenye uzito unaokisiwa tani 10 ikisafirishwa kwenda nje ya nchi bila kibali wala nyaraka zozote za serikali.  
Kwa mujibu wa  taarifa za ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Missenyi ngozi hiyo ilitokea Kahama ikiwa inaelekea nchini Uganda na ilikamatwa katika kizuizi cha Kyaka, wilayani Missenyi.  
"Tulipata taarifa kutoka kwa raia wazalendo tangu jana yake kwamba kuna bidhaa za magendo ambayo huwa yanapita usiku, ndipo nikawapanga vijana kutoka vikosi vyote vya ulinzi na usalama kuweka mtego huu," alisema DC Nkurlu.


"Hiki ni kipindi ambacho magendo ya kahawa husafirishwa kwa wingi kwenda nje ya nchi na hivyo hukosesha serikali mapato yake stahiki. Lakini tumejipanga ipasavyo na tutahakikisha tunakamata kila aina ya magendo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayejihusisha katika biashara hii," alisisitiza. 
"Napenda kutoa rai kwa wananchi wote wa Missenyi kuendelea kutoa ushirikiano wao kwa serikali ili kuweza kukamata bidhaa hizi za magendo na kudhibiti mtandao huu haramu," alisema Mh. Nkurlu.  
Hii ni mara ya pili ndani ya wiki hii magendo yanakamatwa ambapo Jumatatu shehena kubwa ya mbao zilikuwa zikisafirishwa kinyemela zilikamatwa na bado zinashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kyaka.


WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA LIONS CLUB JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wakati alipofungua kongamano la 12 la Lions Club kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam  Me 9, 2015.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano la 12 la Lions Club wakimsikiliza Wairi Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua  kongamano hilo kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Mei 9, 2015.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongea   na viongozi wa Lions Club  baada ya kufungua kongamano lao la 12 kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana  na viongozi wa Lions Club  baada ya kufungua kongamano lao la 12 kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MJINI MOSHI (MUWSA) YANASA MWIZI WA MAJI ENEO LA MAJENGO MJI MPYA.

$
0
0
Zoezi la ukataji wa maji hayo lilisimamiwa na Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo Florah Nguma.
Mafundi wakifukia eneo hilo.
Eneo la nje ya nyumba hiyo ambayo wizi wa maji ulikuwa ukifanyika.
Afisa wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi, Bw. Jacob Ulotu akiondoa gunia lililokuwa limefunika sehemu hiyo ambayo kiutaratibu ilitakiwa kuwa na meta ya kusoma matumizi ya maji. Picha zaidi BOFYA HAPA

lina apigwa kabali na 93.7 EFM

$
0
0
Linah alipopigwa kabali na 93.7 EFM alijiteteaje? Bofya mshale mweupe hapo...

TIMU TANZANIA YASHIRIKI MATEMBEZI YA SUSAN G. KOMEN WASHINGTON, DC

$
0
0

Mwanahabari wa Kwanza Production na Vijimambo Media Mubelwa Bandio(kulia) akiwa sambamba na mwimbaji Matt Goss na Nancy G. Brinker CEO wa Susan G. Komen

Timu Tanzania ikiwa imemaliza matembezi yao ya maili 3 takribani na kilomita 5

Watoto wa wazazi Watanzania wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza matembezi hayo na wazazi wao.

Picha ya pamoja ya kumaliza matembezi hayo pamoja na mmoja wa kikosi cha zima moto wa TDF aliyejumuika kupiga picha na timu Tanzania.
Picha zote na Kwanza Production 
na Vijimambo Media & Entertainment.

MKUTANO WA ISHIRINI WA BUNGE LA KUMI KUANZA DODOMA TAHERE 12 MEI 2015

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA




1.0       UTANGULIZI

Mkutano wa Ishirini (20) wa Bunge la Kumi (10) unatarajia kuanza mjini Dodoma tarehe 12 Mei 2015. Mkutano huo ambao ni mahususi kwa ajili ya kujadili na kupitisha Bajeti ya Serikali ndiyo utakaokuwa mkutano wa mwisho wa Bunge hili kabla ya kuvunjwa na baadaye kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2015.


Hivyo, Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili mjini Dodoma  ifikapo Jumapili tarehe 10 Mei 2015 tayari kuhudhuria kikao cha briefing siku  ya Jumatatu tarehe 11 Mei, 2015.


2.0       SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA

Katika Mkutano huu kutakuwa na wastani wa maswali 295 ya msingi yatakayoulizwa na kupatiwa majibu. Aidha, kutakuwa na wastani wa maswali 56 atayoulizwa Waziri Mkuu na kuyapatia majibu kwa mujibu wa Kanuni ya 38(1) ya  Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013.


Aidha, katika mkutano huo, taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013/2014 itawekwa mezani na kufuatiwa na taarifa yenye majibu kuhusu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa Hesabu za mwaka wa Fedha wa 2013/2014.


Baada ya hayo, Bunge litapokea na kujadili utekelezaji wa Wizara zote 24 wa Bajeti kwa mwaka wa Fedha unaoisha pamoja na Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.


Siku ya Alhamisi tarehe 11/Juni/2015 saa 4:00 (nne)  asubuhi Waziri anayehusika na Mipango atawasilisha taarifa ya Hali ya Uchumi wa Nchi, ikifuatiwa na hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016 itakayosomwa na Waziri wa Fedha saa 10:00 jioni. Wabunge wote mnaombwa kuwepo Dodoma.


Mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2015/2016 utaanza na utafuatiwa na kupitishwa kwa Muswada wa Sheria ya Matumizi wa Mwaka 2015 pamoja na kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria wa Fedha wa Mwaka 2015.


3.0 SHUGHULI NYINGINE

Shughuli za Mkutano wa 20 zinatarajiwa kumalizika tarehe 27 Juni, 2015 na kuhitimishwa kwa hotuba ya Waziri Mkuu ya kuliahirisha Bunge.


Ratiba kamili ya shughuli za Mkutano wa Ishirini wa Bunge la Kumi itapatikana kwenye Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz




Imetolewa na:

Ofisi ya Bunge,

Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,

DAR ES SALAAM

08  Mei 2015



Rais Kikwete katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Algeria

$
0
0
Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria, Jumamosi, Mei 9, 2015 kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku tatu katika nchi hiyo rafiki wa miaka mingi wa Tanzania kwa mwaliko wa Rais Abdelaziz Bouteflika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal wakipokea salamu wakati alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria Mheshimiwa Abdelmalek Sellal wakikagua Gwaride wakati alipowasili mjini Algiers, mji mkuu wa Algeria.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images