Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 833 | 834 | (Page 835) | 836 | 837 | .... | 3286 | newer

  0 0  0 0

  Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri Chini ya Miaka Mitano wa Mkoa wa Mwanza.
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa na wananchi wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka Mitano Mkoa wa Mwanza. Mkakati unalenga kusogeza huduma za Usajili na vyeti vya kuzaliwa katika maeneo wanayoishi na huduma hiyo kutolewa bila ya Malipo.
  Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akikabidhi Cheti cha Kuzaliwa kwa Mzazi wa mtoto Irine Leon (aliyebebwa), Bw Leonidas Rwehumbiza wakati wa uzinduzi wa Mkakati huo.
  Naibu Waziri wa Katiba na sheria Mhe Ummy A. Mwalimu akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya Wageni waliohudhuria uzinduzi wa Mkakati huo.

  0 0


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salama za rambirambi kwa mama Maria Nyerere na familia yake kwa kuondokewa na mmoja wa wana familia yake, Bw. John Nyerere aliyefariki Jumamosi Mei 9,2015 katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

  Pamoja na salamu hizi, Rais Kikwete ambaye yuko nchini Alrgeria kwa ziara ya kikazi, amefanya mawasiliano binafsi na Mama Maria na kumpa pole kwa kuondokewa na kijana wake.

  “Hakuna mzazi anayependa kuondokewa na mwanae, ni kitu kigumu sana  kwa mzazi kukishuhudia , hivyo  naelewa maumivu na huzuni kubwa uliyo nayo”. Rais amemwambia Mama Maria na kumuomba akaze moyo na kumuombea Marehemu John apate pumziko la milele.

  Rais Kikwete amemhakikishia Mama Maria kuwa yeye binafsi pamoja na familia yake , wapo nae katika kipindi hiki kigumu na kuwa watashirikiana wote katika msiba huu kwa hali na mali.

  Rais Kikwete anatarajia kuwasili nchini leo usiku.

  Imetolewa na; 

  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  Ikulu- Dar es Salaam.
  11 Mei, 2015

  0 0


   Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania { RED CROSS } Bwana Shaaban Ali Iddi akikabidhi msaada wa Viatu Pair 90 kwa Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d kwa ajili ya watoto wa familia zilizopata maafa ambao wapo Kambini  Skuli ya mwanakwerekwe “C”.
   Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d akiushukuru Uongozi wa Red Cross kwa misaada yao ya Kibinaadamu waliyotoa kwa ajili ya familia zilizopatwa na maafa wiki iliyopita. 
  Uongozi wa Chama cha Msalaba mwekundu Tanzania ukimsikiliza Katibu wa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Dr. Khalid Salum Moh’d hayupo pichani akitoa nasaha zake baada ya kupokea msaada uliotolewa na Uongozi huo.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA 

  0 0

  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya Marehemu John Nyerere, mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili tarehe 9.5.2015. Shughuli ya kuaga mwili wa marehemu John imefanyika nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere huko Msasani jijini Dar es Salaam leo.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Maria Nyerere mara baada ya shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu John Nyerere huko Msasani jijini Dar es Salaam, Marehemu John anatarajiwa kuzikwa Aprili 13, katika kijiji cha Butiama,Mkoani Mara.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume (wa nne kutoka kushoto) pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro wamesimama mbele ya jeneza wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu John Nyerere iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam,Mwili wa Marehemu John unatarajiwa kusafirishwa kesho kwenda Butiama  mkoani Mara kwa mazishi.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu na Ofisa Wanyamapori akikagua meno ya tembo yaliyokamtwa na askari wa wanyamapori toka kwa majangili Likuyu Sekamaganga Namtumbo mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki iliyopita.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Lazaro Nyalandu na Ofisa Wanyamapori akikagua ngozi za wanyamapori zilizokamatwa na askari wa wanyamapori toka kwa majangili Likuyu Sekamaganga Namtumbo mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki iliyopita.

  0 0

  Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani Hai.
  Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai.
  Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai,Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  3.jpg pichaBodi ya taasisi ya UTT-PID na Menejimenti yake wakia katika picha ya pamoja na uongozi wa kampuni ya Chengdu Engineering Corporation wakati wa picha ya pamoja. Waliosimama mbele (wa pili kutoka kulia) ni mjumbe wa bodi Bi. Janeth Mmari, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Mrs Elpina Mlaki. Wengine ni wajumbe wa bodi hiyo ya UTT-PID pamoja na wenyeji wao wa nchini humo 

  Na Mwandishi Maalum
  Bodi ya Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu iliyo chini ya Wizara ya Fedha (UTT-PID), pamoja na Menejimenti yake iliyozuru nchini China katika ziara maalum ya siku tano kwa ajili ya Mafunzo na kubadilishana uzoefu imefana na tayari bodi hiyo imerejea nchini.

  Katika ziara hiyo, Bodi ya UTT-PID, ikiongozwa na mwenyekiti wake Mrs. Elipina Mlaki pamoja na Menejimenti nzima walieleza kuwa imeweza kuwa ya mafanikio makubwa huku wakiahidi kuyafanyia kazi yae yote waliojifunza nchini China.

  Katika ziara hiyo, bodi na menejimenti ya UTT-PID walipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ya miji ya nchi hiyo ikiwemo makampuni makubwa na kujifunza na kujenga na kudumisha ushirikiano wa utendaji wa kazi.
  2.jpg
  Mwenyekiti wa Bodi ya UTT-PID, Mrs. Elpina Mlaki (wa pili kulia) akilezea jambo katika moja ya mkutano wao waliofanya katika ziara hiyo nchini China. Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mkuu wa UTT-PID, Dr. Gration Kamugisha pamoja na wajumbe wa bodi na Menejimenti ya UTT-PID, Wengine kushoto ni watendaji kutoka kampuni ya Chengdu Engineering Corperation ya nchini humo.


  0 0

  Na Daniel Mbega, Mwanza

  KESI ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino) imeanza kusikilizwa tena leo hii kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya kusimama kwa miezi takriban mitano.

  Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014 liko mbele ya Jaji Robert Makaramba, ambaye ndiyo kwanza ameanza kulisikiliza baada ya jaji wa awali, Ashery Sumari, kupewa uhamisho.

  Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa watano, lakini leo hii mahakama imearifiwa kwamba mmoja – Paulo Budeba Genji maarufu kama Lumalija – alifariki dunia Novemba 22, 2014 katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, wakati akiwa mahabusu.

  Taarifa hiyo ilitolewa na kiongozi wa mawakili wa upande wa mashtaka, Emil Kiria, ambaye aliiomba mahakama, akirejea Kifungu cha 284 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kwamba inapotokea hali kama hiyo mashtaka dhidi ya mtu huyo yanafikia kikomo, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

  Washtakiwa waliobakia kwenye kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.

  Kesi hiyo ambayo inaendelea tena kesho katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iko katika hatua ya ushahidi ambapo shahidi wa sita wa upande wa mashtaka atatoa ushahidi wake.

  Leo hii mashahidi wawili wametoa ushahidi wao na kufanya idadi ya mashahidi waliokwishatoa ushahidi wao kufikia watano mpaka sasa.

  Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Sista  Flosy Sequeire, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Saint Francis ya Mbeya tuzo maalum ya kutambua  ufalu mzuri wa wanafunzi wa shule  hiyo  wakati alipofungua  maadhimisho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Wemgne kutoka kushoto ni  Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma  Mei 11, 2015  kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Mei 12, 2015.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wki ya elimu wenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo, Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.


  0 0

  Position Title: Sales And Marketing Executives

  R&N Solutions LTD is looking for Three (3) enthusiastic, passionate, and dynamic Sales And Marketing Executives to become part of our team. These positions offer growth potential, and the ability to be creative within a positive, growing environment with unlimited earning potential.  Successful candidates will also have an opportunity to build expertise through continuous training and development to ensure their success. 

  Responsibilities Include But Are Not Limited To:
  Utilize elevated levels of marketing and sales to maximize sales performance; meet sales goals.
  Develop new business opportunities through cold calls and leads generation
  Develop and execute monthly sales and marketing plans that targets expansion to our existing customers as well as new ones.

  Comply with all sales related policies and procedures
  Provide the highest level of customer service and support to customers.
  As a member of our team, you will help customers with their purchases and answer any questions they may have, as well as provide support and assistance to your colleagues.

  Qualifications/ What We Are Looking For?
  1-3 years of relevant sales and marketing experience
  University degree or College Diploma preferably in Sales/Marketing or Business Management. 
  Excellent communication & interpersonal skills. Must be fluent in English and Swahili.
  Abililty to qualify leads and opportunities whether presented to you or if you have to source your own leads.
  Candidate with openness, approachability and sincerity 
  Candidate wit enthusiasm and passion for assisting customers and helping to understand their unique needs 
  With integrity and drive to succeed with passion for continuous learning and self development. 
  With ability to get past the gate-keepers and in front of the decision-makers.
  Initiate all aspects of the sales process including scheduling appointments; making initial presentation; understanding customers needs and requirements; researching industries; building rapport with potential customers; explaining the details of our products and services capabilities;

  To Apply: Send In Your CV and Cover Letter To careers@rnsolutionsltd.com before 25th May 2015 
  Thanks in advance to all candidates for applying. 

  However,only short-listed candidates will be contacted for interview. 

  0 0

  Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ameendelea na ziara ya kikazi jimboni kwake huku Makundi mbalimbali yaliendelea kumuunga Mkono na kumshawishi achukue fomu ya Ubunge kwa kipindi kijacho.

  Katika ziara yake ya kichama amekagua kazi zinazotanywa na kikundi cha wakina mama wafinyanga vyungu, wakinamama wajasiriamali wauza kokoto na walima bustani.

  Aidha amezindua Shina la ushindi ambalo wakinamama wafinyanga vyungu ndiyo wanachama wa Shina hilo, Katika kuunga Mkono vikundi hivyo mbunge amewachangia pump ya kumwagilia na Fedha vyote kwa pamoja vinafikia sh 2,800,000.

  Wakitoa ujumbe kupitia nyimbo walimtaka mbunge wao muda ukifika achukue fomu kwani wameridhishwa na kazi nzuri alizozifanya kijijini hapo ikiwepo huduma za jamii.

  Akihutubia katika mkutano huo aliwapongeza kwa kujiunga katika vikundi na mafanikio yanaonekana. Amewapongeza kwa bidha nzuri za majiko, vyungu na upatikanaji wa kokoto kwa urahisi na kwa bei nafuu.

  Amewahakikishia ushirikiano wa dhati na atachukua fomu kutetea nafasi yake mara muda utakapofika.
  Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akilakiwa na wananchi wa jimbo lake hilo.

  Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akihutubia katika moja ya mikutano na wananchi wa jimbo lake hilo.
  Akipokea zawadi ya kuku.
  Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla akikabidhi mashine ya kuvutia maji kwa wananchi wa moja ya kijiji katika Jimbo lake la Mvomero.

  0 0

  Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa, ile band ambayo kwa walio mbali basi walikuwa wakisikia simulizi zake toka kwa wenyeji kwamba inafumua burudani ya kijanja ile kisawasawa toka kiota chenye hadhi ya kitalii Jembe Beach Resort Mwanza, JJ Band ndiyo ninao wazungumzia, basi wamekuja na single yao ya kwanza mpya inayoitwa 'NISHIKE'

  Kazi imefanyika ndani ya studio za One Love FX zilizoko Ilemela jijini Mwanza, chini ya mkono wa mtayarishaji mkali Tiddy Hotter, yule aliye tengeneza ngoma kama Changamka ya Director Shahib, Tumewaka - G Nako ft Godzillah, Mimi na wewe - Dynna Nyange, Listen - Belle Nine, Itika - Josline na nyingine kali kibao.

  Kazi tamu kwa sikio, yenye hisia na inayochezeka bado mbichi kabisa isikilize kwa nafasi ikiwa ni amsha amsha ya kuelekea tarehe 23 May 2015 ambapo barabara zote za jiji la Mwanza zitaelekea CCM Kirumba katika tamasha kubwa la burudani 'JEMBEKA FESTIVAL 2015' OYOMBA YES - PAMOJA SANA 

  0 0

   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk, Seif  Rashid (watatu kushoto),  akitetajambo na madaktari hao baada ya kufungua mkutano huo  jijini Dar es Salaam leo  unao endelea hadi Mei 15-2015 ,  (wa kwanza kulia) ni   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma, wakwanza  kushoto ni  Daktari Bingwa wa Taasisi hiyo,  Anthon Assey na anaye fatia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI), Dk. Othman Kiloloma akizungumza na wandishi wa habari (pichani hawapo), katika mkutano wa nne wa mafunzo ya upasuaji wa ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dar es Salaam leo. Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Rashid, unao endelea hadi  Mei 15-2015. 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS mkoani Morogoro. Waziri Magufuli amewapongeza TANROADS kwa utendaji kazi wao mzuri ujenzi wa Barabara nchini.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale akisoma risala kwa Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.TANROADS imepata TUZO ya mfanyakazi bora na mwajiri bora kutoka TAMICO.
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa ameshikana mikono na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara, TANROADS Eng. Patrick Mfugale kushoto pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Rajabu Rutengwe kulia wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima kabla ya ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS.


  0 0

  Msikilize Rose Ndauka akijitetea katika kabali, 
  Bofya mshale mweupe hapo chini
  SIKILIZA 93.7 EFM POPOTE ULIPO DUNIANI BOFYA HAPA
  PITIA ROZZIE MAGAZINE BOFYA HAPA

  0 0

  In loving memory of our beloved husband, father and grandfather, Lucas Zerubabel Mosha, who passed away one year ago on 12thMay 2014 in Dar es Salaam and was laid to rest at his home village in Mwika, Moshi.

  You continue to be in our hearts each and every day. You will be with us forever in our hearts and minds.  
  Your wife, children, grandchildren and family miss you.  We know the love you had for us all means that you are looking out for us.


  May your soul rest in eternal peace


  0 0
 • 05/11/15--15:06: Ngoma azipendazo ankal
 • Fid Q na video rasmi ya Bongo Hip Hop

  0 0

  BENKI ya EximTanzania imezindua kampeni inayolenga kuwahamasisha wateja wake juu ya matumizi ya kadi zake mpya za  ‘Faida Chip and PIN Debit card’ ambazo zimeundwa  kwa kuzingatia vigezo vya kiusalama zaidi.

  Kwa mujibu wa Meneja Bidhaa wa benki hiyo Bw. Aloyce Maro hatua hiyo ni sehemu ya jitiahada za benki hiyo kuhakikisha kwamba huduma zake zinatolewa kwa uhakika na usalama zaidi kwa faida ya wateja wake.

  “Lengo kubwa la kampeni hii ni kuwahamasisha wateja wetu juu ya matumizi ya kadi zetu mpya za  ‘Faida Chip and PIN Debit card’ ambazo zinatumia ‘chip’ badala ya ‘magnetic strip’ lengo likiwa kuongeza usalama wa akaunti za wateja wetu’’ alisema Bw. Maro wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana jijini Dar es Salaam.

  Matumizi ya kadi hizo yanaelezwa kuongeza usalama na amani miongoni mwa watuamiaji wake kwa kuwa zina uwezo wakipekee katika kuhifadhi na kutambua  taarifa za mtumiaji na hivyo kuondoa hofu ya wizi wa namna yoyote ile, kwa mujibu wa Bw. Maro.

  “Kadi hii inauwezo mkubwa wa kuhifadhi taarifa pamoja kumtambua mmiliki wake.Uwezo huu ndio siri ya mafanikio yake kwa kuwa inauwezo wa kuwazuia kabisa watu wenye nia ovu na akaunti ya mteja hususani kwa kufanya jaribio la namna yoyote la wizi,’’ alisema Bw. Maro.

  Akiizungumzia zaidi kadi hiyo Bw. Maro alisema inauwezo wa kumuwezesha mtumiaji wake kuweza  kuifikia akaunti yake na kufanya miamala  kutoka kwenye  mashine za kutolea fedha zenye uthibitisho wa ‘MasterCard’ pamoja na zile za POS ulimwenguni kote bila usumbufu wowote.

  Aidha Bw. Maro aliwahamasisha wateja wa benki hiyo ambao bado hawajachukua kadi zao wajitokeze kuzichukua kwenye matawi ya benki hiyo ili waanze kufaidi matumizi yake.
   Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (katikati)
  Meneja Bidhaa wa Benki Ya Exim Tanzania, Aloyse Maro (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kutangaza uzinduzi wa kampeni mpya ya benki hiyo inayolenga kuhamasisha wateja juu ya matumizi ya kadi mpya ya Faida Debit Card, ambayo imeimarishwa zaidi kiusalama, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo, Anita Goshashy (kushoto) na Zawadi Kanyawana kutoka kitengo cha Huduma za Rejareja za Kibenki (kulia).
   

  0 0
 • 05/11/15--20:30: KUMBUKUMBU


older | 1 | .... | 833 | 834 | (Page 835) | 836 | 837 | .... | 3286 | newer