Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 830 | 831 | (Page 832) | 833 | 834 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.

  Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa..

  Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo.

  Shitaka linalomhusisha mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba SC Juuko Mursheed, na kiongozi wa Friend Rangers Hery Chibakasa wa Friends Rangers kuhamasisha vurugu katika mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya Songea Januari 29, 2015, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.

  Kamati iliahirisha malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya kupokea taarifa za udhuru zilizosbabishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya abiria ya mikoani.

  0 0

  Mratibu wa Jumuiya ya Vijana wasio na ajira Tanzania Nd. Ussi Said Suleiman akitoa maelezo kwa Baadhi ya Vijana wasio na ajira waliohudhuria katika Mkutano wa kuitambulisha Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Water front Hall Rahaleo Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Vijana waliohudhuria katika Mkutano wa kuitambulisha Jumuiya mpya ya Vijana wasio na ajira Tanzania, wakimsikiliza Mratibu wa Jumuiya hiyo Nd. Ussi Said Suleiman (hayupo pichani).
  Mmoja wa Vijana wasio na ajira Zaituni Haji Mdigo akiuliza swali katika Mkutano huo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0
 • 05/08/15--03:39: Happy Birthday MO
 • DSC01228-Edit
  MODEWJI BLOG TEAM : Thanking you for being a great boss just isn't enough for your special day! Thank you for inspiring us to be our best! Happy birthday, boss!
  And below is a small gift from us!
  IMG_9643 
  Please join us to wish him a Happy Birthday by follow him on his twitter @moodewji and instagram @moodewji

  0 0


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WANAWAKE wametakiwa kujiunga katika taasisi za fedha ambazo zinaainisha mikopo ya wajasiriamali hiyo itasaidia wanawake kujikwamua na umasikini.

  Hayo ameyasema leo Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Sophia Simba wakati wa uzinduzi wa mpango Fanikisha Plus  wa wajasirimali unaondeshwa na benki ya Equity iliyofanyika leo katika ukumbi JB,Belmote jijini Dar es Salaam.

  Sophia amesema wanawake umefika wakati kutumia fursa ambazo taasisi za fedha zenye mikakati ya kumkomboa mwanamke kiuchumi kupitia mikopo yenye masharti nafuu.

  “Wanawake umefika wakati wa kupata elimu ya vitu mbalimbli vinavyoendelea  vya jinsi ya kuweza kujikwamua kiuchumi na sio kukaa katika luninga na kuangalia tamthilia”amesema Sophia.

  Amesema katika mipango ya Umoja wa Afrika wa wameanisha jinsi ya kuweza kumasaidia mwanamke wa Afrika kumkwamua kiuchumi kwa kutoa elimu ya kuweza kujitambua hivyo wanaweza kuendesha miradi mbalimbali.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na watoto akizungumza na Wajasialiamali mbalimbali kuhusiana na kujiinua kiuchumi katika ukumbi wa JB belomente jijiji Dar es Salaam leo.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii na Jinsia na Watoto Anna Kilango akimkabidhi tuzo Mkurugenzi wa Bodi ya wanawake wafanyabiashara Tanzania Anna Matinde katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Equity Josef Iha.
  Baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria katika warsha iliyofanyika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa JB Belomente jijiji Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakaingo, blobu ya Jamii.

  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akipiga makofi mara baada ya kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid, akizindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (wapili kulia), akiwa na baadhi ya watendaji wa Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini wakishudia uzinduzi wa mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na shirika hilo katika vituo vya Afya 13.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid (katikati), akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya kuzindua mradi wa elimu kwa mtandao unaosaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto ambao unaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la World Lung Foundation (WLF) la hapa nchini, ambapo vituo vya Afya 13 vinanufaika na mradi huo.

  0 0

   Mkurugezi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB katika ukumbi wa AICCjijini Arusha leo. 
   Mwrnyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Martin Mmari akizungumza wakati wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB.
   Mwanahisa akiuliza swali.


  0 0

  Waziri wa nchi (Ofisi ya Rais) Mahusiano na Uratibu, Mhe. Dkt. Mary Nagu (wa tatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Indonesia,Dkt. Aziz Ponary Mlima (wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Asia-Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kushoto), Afisa wa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Hatibu Makenga (kushoto), Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Indonesia, Bw. Dismass Assenga (wa pili kuliana Bwana Emmanuel Rhobi-Msaidizi wa Waziri, mara baada ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Asia na Afrika uliofanyika mjini Jakarta nchini Indonesia.Mheshimiwa Waziri Dkt. Mary Nagu alimwakilisha  pia Rais Jakaya Kikwete kwenye Mkutano huo.
  Kutoka kushoto kwenda kulia Bwana Hatibu Makenga Afisa Mambo ya Nje, Dkt. Aziz Ponary Mlima- Balozi Mteule wa Tanzania nchini Indonesia, Mheshimkwa Mary Nagu-Waziri, Balozi Mbelwa Kairuki- Mkurugenzi Asia-Australasia na Bwana Emmanuel Rhobi- Msaidizi wa Waziri.
  Waziri na Timu yake wakiwa kwenye Mkutano.

  0 0

  Ratiba Ya Mkutano Wa 20 

  0 0  Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kumpatia zawadi za kimila, Shuka ya rubega, mkuki na ngao, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (kulia), wakati wa hafla ya kuwatunuku wafanyakazi waliohudumu kwa muda mrefu kwenye kampuni hiyo, na wengine 10 walizawadiwa kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sera mpya ya Acacia ya tabia sita (six desired behavior), kama kipimo cha utendaji bora wa kazi ambapo ni pamoja na kushirikiana na kufanya kazi kwa uwazi, kutambua ubora wa mfanyakazi na kumuwajibisha anapokengeuka, kupanga kazi na kutenda, kufanya kile ulichopanga kufanya, kufanya kazi kwa wepesi, na kujiendeleza ili kuwa bora katika utendaji wa kazi wa kila siku. Katika hotuba yake, Mkuu huyo wa wilaya ambaye alikuwa mgeni rasmi, kwenye sherehe hiyo ambayo ilikuwa maalum kuwatunuku wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia, na kufanyika Alhamisi usiku wa kuamkia leo Ijumaa Mei 8, 2015, aliwamwagia sifa wafanyakazi wa mgodi huo hususan uongozi mpya chini yaa Brad, kwa kuja na sera mpya ambayo sio tu inawajali wafanyakazi bali pia wananchi wanaozunguka mgodi huo ikiwemo serikali.
  Meneja Mkuu wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia udthabiti wa kampuni hiyo, (GM-Organizational Effectiveness), Janet Reuben-Lekashingo, (kulia), akimkabidhi cheti Isack John Nkulu, kwa utumishi wa muda mrefu kwenye kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Filbert Rweyemamu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuwapa kipaumbele wakulima wadogo kwa kuandika habari zao kiundani kuliko kuegemea kwa wanasiasa peke yao.

  Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima nchini (Mviwata), Veronica Sophu aliyasema hayo jana mjini Morogoro kwenye kongamano la waandishi wa habari wanaoandika habari za wakulima.

  Sophu ambaye alikuwa mjumbe wa Bunge maalum la Katiba (BMK) kupitia kundi la wakulima alisema wakulima nchini wanatakiwa wasikilizwe kwani wana changamoto nyingi zinazowakabili.

  “Kuna changamoto ndogo kati ya waandishi wa habari na wakulima kwani vyombo vingi vya habari vimekuwa vinaegemea kwa wanasiasa na kutuacha wakulima bila kuwa na mahali pa kusemea,” alisema Sophu.

  Alisema mara nyingi habari za wakulima wadogo hazipewi kipaumbele zaidi ya migogoro kati yao na wafugaji hivyo waandishi wa habari wabadilike kwa kuwatazama na wao.

  “Asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima wadogo kwani kila kwenye watu 10 kati yao nane ni wakulima hivyo wapewe kipaumbele kwani bila mkulima mdogo hatuwezi kupata chakula nchini,” alisema Sophu.

  Naye, Mkurugenzi mtendaji wa Mviwata Stephen Ruvuga alisema mchango wa waandishi wa habari nchini kwa upande wa wakulima mdogo ni wa muhimu hivyo uzingatiwe.

  Ruvuga alisema wakulima wadogo wanatakiwa kuungwa mkono na waandishi wa habari kwa kusemewa kwa namna nzuri zaidi kuliko kuripoti tuu habari hizo bila kuingia kwa undani.

  “Wakulima wadogo wana nafasi kubwa katika kuchangia uchumi wa Taifa na jamii kwa ujumla hivyo waandishi wa habari msiangalie tabaka la juu pekee na kuacha kutoa habari za wakulima,” alisema Ruvuga.
  Mwenyekiti wa Mviwata Veronika Sophu akizungumza na waandishi wa habari wanaoandika habari za wakulima (kulia) ni Mkurugenzi wa Mviwata Stephen Ruvuga na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mviwata Usi Haji Usi.
  Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoandika habari za wakulima wakifuatia kongamano la waandishi wa habari marafiki wa wakulima lililowashirikisha waandishi mbalimbali kutoka vyombo na mikoa tofauti, lililofanyika mjini Morogoro na kuandaliwa na Mviwata.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa 17 wa siku mbili wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC – SAC uliomalizika Zanzibar Beach Resort.
  Kamanda wa Majeshi ya Anga wa Jamuhuri ya Botswana Meja General Mashinyana akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake waliotoka nje ya Tanzania kutokana na ukarimu walioupata Zanzibar wakati wa Mkutano wao wa Sadc – Sac.

  Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa Majeshi ya Anga wa Mataifa ya Kusini mwa Bara la Afrika SADC – SAC uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mzizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.


  0 0

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akisoma taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi kuhusu kuhusika kwake na kashfa ya Escrow na ile ya tume ya uchunguzi wa malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa operesheni tokomeza mapema hii leo jijini Dar es Salaam , kulia niMwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais Bi. Premi Kibanga.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati akisoma taarifa ya kukamilika kwa uchunguzi dhidi ya aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Eliakimu Maswi kuhusu kuhusika kwake na kashfa ya Escrow na ile ya tume ya uchunguzi wa malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa operesheni tokomeza. Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO.


  0 0

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin akikabidhi baadhi ya vifaa vya Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba wilayani Karatu mkoani Arusha kwa baadhi ya viongozi wa Serikali ya Kijiji hicho, ambapo Kampuni hiyo ya Bia ilitoa vifaa vyenye thamani ya Sh.Milioni 22.
   Mwananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu ambacho ni maarufu kwa ulimaji wa zao la Shayiri akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin mara baada ya kukabidhi Kituo  cha Afya cha Kijiji hicho vifaa mbalimbali vya matibabu.
   Maofisa wa TBL wakibadilishana mawazo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo wilayani Karatu, katikati ni Afisa Uhusiano Dorris Malulu, kushoto kwake ni Mkurugenzi Jarrin na kulia kwake ni Meneja mradi wa Kilimo cha Shayiri Dk. Basson.
   Afisa Uhusiano wa TBL Dorris Malulu akizungumza na baadhi ya viongozi Serikali ya Kijiji pamoja na uongozi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kambi ya Simba kilichopo Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu mkoani Arusha wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya kituo hicho vyenye thamani ya Sh. Milioni 22, Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania, (TBL), Robert Jarrin na kushoto kwake ni Meneja Mradi Kilimo cha Shayir Dk. Basson Bennie.

  0 0

  Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari za mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jiji. Mvua hizo zinazonyesha kwa siku tatu mfululizo zimesababisha vifo vya watanzania hawa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam kama ifuatavyo:

  1.    Mnamo tarehe 06/05/2015 majira ya saa moja kamili usiku huko maeneo ya Magomeni Kinondoni jijini Dar es Salaam mtu mmoja jina SHABAN S/O IDD, Miaka 73, Mkazi wa Manzese alisombwa na maji ya mto ng’ombe alipokuwa akijaribu kuvuka mto huo. Mwili wake ulipatikana siku iliyofuata 07/05/2015 akiwatayari amekwishafariki dunia na umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala.

  2.    Kifo kingine kilitokea tarehe 07/05/2015majira ya  saa sita kamili mchana huko maeneo ya Mwananyamala Mbuyuni Kata ya Mwananyamala, OysterBay, Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja aitwaye MASUMBUKO S/O DOUGLASS @ LIMAMU, Miaka kati ya 50-55, mkazi wa Mwananyamala Mbuyuni, alianguka na kufariki dunia ghafla wakati anatoa maji yaliyoingia nyumbani kwake. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa hivyo wakati akihangaika kutoa maji, ugonjwa huo ulimpata na kuanguka kwenye maji na kufariki dunia baada ya kukosa msaada wa haraka. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi.


  0 0

    Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Gwesigabo akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kupanda kwa mfumuko wa bei wa huduma na bidhaa. Kushoto ni Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei, Luth Minja.
  Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema mfumuko wa bei umeongezeka kwa asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.3 kwa Machi mwaka huu ambapo umeongezeka kwa asilimia 0.8 kutoka asilimia 0.7 Machi,2015.

  Ongezeko hilo limechangiwa na kasi ya upandaji bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Aprili, 2015 kuongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo ya Machi, 2014.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa sensa ya watu na Takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alisema farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 
  mwaka huu kutoka 150.50 Aprili mwaka jana.

  "Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinjwaji baridi kwa Machi mwaka huu umeongezeka hadi asilimia 7.1 kutoka asilimia 5.9 Machi mwaka jana, hii imetokana na kuongezeka kwa bei za bidhaa za vyakula kwa kipindi kinachoishia Aprili, 2015," alisema.

  Alisema bei za vyakula kama mchele umepanda kwa asilimia 23.3, unga wa mihogo kwa asilimia 8.4, nyama kwa asilimia 4.9, samaki kwa asilimia 5.8 ambapo maharage yamepanda kwa asilimia 6.8 na sukari kwa asilimia 5.6.

  Kwegisabo aliongeza kuwa mfumuko huo kwa Aprili, 2015 umeongezeka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na asilimia 0.7 Machi, 2015 ambapo farihisi za bei zimeongezeka hadi 157.21 Aprili, 2015 kutoka 155.88 Machi, 2015.

  "Vyakula vilivyochangia kuongezeka kwa farihisi za bei ni pamoja na mchele kwa asilimia 5.8, mahindi kwa asilimia 6.3, unga wa mahindi kwa asilimia 5.0, samaki waliokaushwa kwa asilimia 3.1, ambapo maharage kwa asilimia 2.9, na viazi mviringo kwa asilimia 7.0, mihogo kwa asilimia 6.4 pia viazi mviringo kwa asilimia 4.0," alisema Kwesigabo.

  Aidha uwezo wa shilingi 100 kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 63 na senti 61 Aprili, 2015 kutoka Septemba, 2010 ikilinganishwa na shilingi 64 na senti 15 Machi, 2015.

   Alisema mfumuko huo unamwelekeo unaofanana na nchi za Afrika Mashariki ambapo Uganda umeongezeka kwa asilimia 3.60 kutoka asilimia 1.90 Machi, 2015, Kenya umepanda kwa asilimia 7.08 Aprili, 2015 kutoka 6.31 Machi, 2015.  
   (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/JosephMsami)
  Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, amesema leo kwamba anatarajia kutoa mapendekezo juu ya mapugunfu yaliyoonekana wakati wa kupambana na Ebola.
  Akihojiwa na Priscilla Lecomte na Jospeh Msami wa idhaa hii, ameeleza kwamba wanachama wa jopo hilo baada ya kuzungumza na wataalam wa afya mjini new York, watatembelea Geneva, Uswisi, ili kujadiliana na wadau wa shirika la afya ulimwenguni, WHO na mashirika mengine, halikadhalika watasafiri kwenda nchi zilizoathirika na Ebola.
  Hapa Rais Kikwete anaanza kwa kuelezea jukumu la jopo hilo ambalo ripoti yake ya awali wataiwasilisha mwezi Septemba, ripoti ya mwisho ikitarajiwa mwisho wa mwaka .
  KUSIKILIZA BONYEZA HAPA

  0 0


  0 0

  Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii imefanya ziara kwenye ofisi za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu jijini Dar es Salaam na kuitaka Bodi kuwasilisha changamoto za kisera ili ziweze kufanyiwa kazi kwa wakati. ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti ya fedha za ukopeshaji.

  Akizungumza baada ya  taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi kuwasilishwa, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Gregory Teu amesema kuwa yeye na wanakamati wenzake wamejifunza kwa kina kupitia ziara hiyo na kwamba bila kufika Bodi ni vigumu kujua ni kwa jinsi gani shughuli za utaoji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu zinafanyika kwa weledi mkubwa na bila upendeleo.

  Awali wakati akitoa neno la utangulizi kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi; Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Consolata Mgimba alielezea umuhimu wa ziara hiyo kwa Bodi na kuwashukuru wajumbe wa Kamati ya Huduma za Jamii kwa ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiutoa kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake ikiwemo Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu.

  Baada ya taarifa ya utekelezaji wa Bodi kuwasilishwa, baadhi ya wajumbe wa kamati walichangia maeneo mbalimbali ya utoaji na urejeshwaji wa mikopo na kuitaka Bodi kuwasilisha changamoto za kisera ili ziweze kufanyiwa kazi, mojawapo likiwa ni ufinyu wa bajeti ya fedha za ukopeshaji ambapo kwa miaka mitatu mfululizo serikali  imekuwa ikitenga Shilingi bilioni 306 wakati idadi ya wahitaji wa mikopo inaongezeka kila mwaka. 

  Wajumbe hao wa Kamati ya Huduma za Jamii wametembelea idara na vitengo mbalimbali vya Bodi kushuduhudia huduma zinavyotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu wa ndani na nje ya nchi.

  Ziara hiyo imewawezesha wajumbe wake kupata maelezo kutoka kwa watendaji wa Bodi kuanzia mchakato wa maombi ya mikopo, uchambuzi na upangaji, utoaji wa mikopo na uhifadhi wa taarifa za wanafunzi kwa ajili ya urejeshwaji wa mikopo hiyo baada ya kuhitimu masomo yao.

  Ziara ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ni sehemu ya majukumu yake ya kutembelea taasisi zinazotoa huduma kwa jamii na kupokea taarifa za utekelezaji wa utoaji huduma hizo.
  Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakipata maelezo kutoka kwa mkuu wa moja ya idara za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Gregory Teu.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Sheria wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Firmat Tarimo akielezea shughuli zinazofanywa na kitengo hicho.
  Meneja wa Mifumo ya Kompyuta na Utunzaji wa Kumbukumbu wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Bahati Singa akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii jinsi ambavyo kumbukumbu za wanafunzi zinatunzwa baada ya kupokelewa Bodi.
  Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii Mhe. Christowaja Mtinda akichangia maoni yake baada ya taarifa ya utekelezaji wa Bodi kuwasilishwa mbele ya kamati.

  0 0

   Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wapili kulia) akipeana mkono na Bw. Rajpaul Singh Dhani (kulia) dereva wa gari ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga.
  Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Bw. Gabriel masanja  (wa kwanza kushoto) pamoja na Bw. Rajpaul Singh Dhani (Wa tatu kushoto) dereva wa gari (iliyopo mbele yao)ya mashindano iliyoiwakilisha benki hiyo katika mchezo wa mashindano ya magari uliyofanyika mkoani Tanga hivi katibuni. Wengine katika picha ni wafanyakazi wa benki hiyo tawi la Tanga.

older | 1 | .... | 830 | 831 | (Page 832) | 833 | 834 | .... | 3284 | newer