Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 829 | 830 | (Page 831) | 832 | 833 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti cha kutambua mchango wa serikali ya Zanzibar katika mradi wa ujasiriamali, ndugu Ameir Ali Ameir, ambaye ndiye Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Rais Kazi na Utumishi wa Umma, Zanzibar.
  Naibu waziri wa kazi na ajira, Mheshimiwa Makongoro Mahanga akizungumza na waandishi wa habari.
   Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Philippe Poinsot akizungumza wakati wa kongamano.
   Mkurugenzi Mkuu wa ILO Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda Bwana Alexio Musindo akizungumza na waandishi wa habari.
     Baadhi ya wahudhuriaji wa kongamano la kuadhimisha Miaka mitano ya mradi wa Ujasiriamali uliokuwa unaendeshwa na Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO).

  ILO Tanzania yaadhimisha miaka 5 ya kuwawezesha vijana Tanzania kupitia ujasiriamali. Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) leo limeadhimisha miaka 5 toka kuanzishwa kwa mfuko wa ujasiriamali wa vijana (YEF) kwa kuandaa kongamano katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulizinduliwa mwaka 2010 ukilenga katika kutengeneza ajira kwa vijana kwa kupitia ukuzaji wa sekta binafsi pamoja na kuongeza ushindani kwenye uchumi wa Afrika.

  Mradi ulijikita katika kuwatengenezea vijana ajira nzuri, kukuza ujasiriamali na kuwatengenezea fursa vijana wa kiafrika kupitia elimu, kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji wa mtaji. Kwa kupitia mradi huu wa Kuwezesha Ujasiriamali, Mfuko wa Ujasiriamali kwa vijana ulilenga kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.

  Msingi mkuu wa mradi ulikuwa kukuza utamaduni wa ujasiriamali miongoni mwa vijana, kuingiza elimu ya ujasiriamali katika mitaala, kuongeza uwingi wa mambo yanayowezekana katika ajira kwa vijana, kuwezesha taasisi za vijana kutekeleza mawazo mazuri ya ujasiriamali na kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana walio nje ya shule.

  Toka mradi umeanzishwa, umewezesha zaidi ya vijana 30,000 ambao ni wajasiamarali wapya na waliopo kupitia utoaji wa elimu ya biashara, kusaidia uanzishwaji wa biashara zaidi ya 17,000 pamoja na utengenezaji wa zaidi ya ajira 40,000 kwa vijana, ambayo vyote kwa pamoja vimevuka malengo ya mradi yaliyoaninishwa mwanzo.  0 0


   Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.  MAFURIKO,Mafuriko,Mafuriko .! Jiji la Dar limejaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha wengine kukosa makazi.  Maeneo yaliyokumbwa kwa mafuriko ni Mnyamani (Ilala),Bonde la Mpunga (Kinondoni) ,Kigogo (Kinondoni),Mikocheni ( Kinondoni),Vingunguti (Ilala) Tabata Kisiwani (Ilala)na Kurasini (Temeke) na maeneo mengine ambayo hayajawahi kupata mafuriko yamefika.  Mvua hizo zimeharibu miundombinu katika barabara ya Morogoro kwa kujaa maji na kufanya kutokuwepo kwa usafiri kuelekea katikati ya jiji la Dar es Salaam.  Wilaya ya Kinondoni ndio inaongoza kwa maeneo mengi kukumbwa na mafuriko kutokana na watu kujenga katika mikondo ya maji na baadhi ya watu kujenga nyumba katika miundombinu ya maji mitalo ya  maji taka na  kufanya maeneo mengine kutapakaa maji na kuleta adha ya usafiri.  Kwa Wilaya Ilala ni eneo moja ndilo limekuwa likisababisha mafuriko, ni kwa wale waliojenga karibu na bonde la mto Msimbazi  ndio wamekuwa waathirika wa mafuriko kila mwaka.  Wananchi wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko hawana msaada wowote huku mvua ikiendelea kunyesha kuanzia majira ya saa 10 jioni na kuamkia leo hadi katika muda huu mvua inatikisa.


  Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick amesema kuwa serikali msaada wake ni wale waliopata madhara kutokana na mvua hizo na sio kuwapa makazi na chakula kutokana na kukataa kuhama maeneo hayo na kuishia kuipeleka serikali mahakamani.  Mkuu wa Mkoa amesema serikali ilitoa maeneo mbadala ya kwenda kujenga na kuishi kwa watu wa maeneo ambayo mara kwa mara wamekuwa wakipata mafuriko, walikataa na kuipeleka serikali mahakamani hivyo sasa haiwezi kuwasaidia.


  “Sasa sisi tufanye nini tutawaombea sala,lakini msaada kwetu ni wale waliopata madhara ya kiafya kwa ajili matibabu,Serikali ndio itafanya hivyo”amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP),Suleiman Kova amesema katika mvua zinazoendelea mtu mmoja amepoteza maisha kwa kuanguka katika mto ng’ombe uliyopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.  Kamanda Kova amesema aliyepoteza maisha ni Shaban Idd (73) Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam na mwili wake umeopolewa na kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke,Sophia Mjema amesema ,daraja wa mwanatopa limekatika na kufanya mawasiliano kati ya Kijichi na Mbagala kukosekana.

  Katika mvua hizo,wilaya ya Temeke Mtoto mmoja ambaye jina lake halijaweza kupatikana alipoteza maisha kutokana na kuchuliwa na maji.  0 0

  WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wenye uwezo wa kifedha waangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda hapa nchini badala ya kuendelea kuwa wachuuzi wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na kuziuza hapa nchini.

  Ametoa wito huo jana jioni (Jumatano, Mei 6, 2015) baada ya kutembelea maonyesho ya biashara ya Syria yanayoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania pamoja na wafanyabiashara kadhaa, Waziri Mkuu Pinda alisema mtindo unaoendelea wa kuuza mazao ghafi nje ya nchi hauisaidii Tanzania kama nchi na badala yake unanemeesha viwanda na uchumi wa nchi zinazonunua mazao hayo.

  “Watazania lazima wajiulize hivi bidhaa zote wanazoagiza kutoka nje ya nchi haziwezi kabisa kuzalishwa hapa nchini ili kupunguza matumizi mkubwa ya fedha za kigeni, kukuza uchumi na kuongeza ajira?,” alihoji Waziri Mkuu.

  Alisema wakati umefika sasa wa Tanzania kufikiria kuanzisha mpango mahsusi wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuweka vivutio vitakavyowashawishi wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi inayozalishwa hapa nchini hatua ambayo itawafanya wafanyabiashara wasiende nje kununua bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa hapa nchini.

  Mapema, Balozi wa Syria nchini, Mhe. Abdulmounem Annan alimweleza Waziri Mkuu kuwa nchi yake inavyo viwanda vya nguo za pamba zaidi ya 100 na pamba ghafi yote inayotumika kwenye viwanda hivyo inalimwa nchini humo.

  Balozi Anan alisema yuko tayari kuandaa utaratibu utakaowawezesha wafanyabiashara, wawekezaji na viongozi wa Serikali kwenda Syria ili kukutana na wenzao kwa lengo la kujifunza na kuwashawishi waje kuwekeza Tanzania kwenye viwanda vya nguo na vya kusindika vyakula.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM
  ALHAMISI, MEI 7, 2015.

  0 0

  Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran ina wajibu  wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika harakati za maendeleo kutokana na Historia ndefu iliyopo ya mwingiliano wa kibiashara baina ya baadhi ya Wananchi wa pande hizo mbili.

  Gavana  Mkuu wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana  Ali Osat Hashemi akiuongoza Ujumbe wa Viongozi saba wa Jimbo hilo alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

  Gavana  Ali Osat Hashemi alisema muingiliano huo wa biashara kati ya Irani na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla umepelekea watu wa pande hizo mbili pia kuwa karibu zaidi kwa kuchanganya damu.

  Alisema wiki chache zijazo pande hizi mbili zinatarajia kusaini Mkataba wa ushirikiano katika kuendeleza mradi wa mafunzo ya amali   ambao utagharimiwa na Iran kwa kiasi cha Dola  za Kimarekani Laki 500,000 zitakazotumika katika ununuzi wa vifaa vya kufundishia.

  Gavana huyo wa Jimbo la Sistan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran alifahamisha kwamba sekta binafsi hasa miradi ya amali inafaa kuungwa mkono kwa vile inasaidia kutoa ajira kubwa kwa Jamii hasa Vijana.
  Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema miradi ya Amali na Sekta ya Afya inayofadhiliwa na Iran kwa Zanzibar ni uthibitisho wa uimarishaji wa uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili.

  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikutana kwa mazungumzo na Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania  Bibi Hawa O. 

  Ndilole aliyefika kujitambulisha rasmi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
  Akizungumza na Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japani Balozi Batilda Buriani aliyefika Ofisini kwake Vuga kumuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo Balozi Seif  alimuomba Balozi Batilda kuhakikisha kwamba Tanzania inafaidika kutokana na ushirikiano wake wa Kidiplomasia ya Japan.
   Balozi Mpya wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan Balozi Batilda Buriani akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika kuaga rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jakaya Mrisho Kikwete.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkaribisha Balozi Mpya wa Malawi Nchini Tanzania Bibi Hawa Ndolowe aliyefika Ofisini kwake kujitambulisha rasmi.
   Balozi Seif akisalimiana na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi wakati alipofika na ujumbe wake kwa mazungumzo ya uhusiano  kati ya nchi hizo mbili.

  Balozi Seif akibadilishana mawazo na Gavana Mkuu wa Jimbo la Siustan na Balachestan Nchini Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran Bwana Ali Osat Hashemi  ambae yupo Zanzibar na Ujumbe wake kwa ziara ya siku mbili.
  Picha na OMPR – ZNZ.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipotambulishwa rasmi na viongozi wa bodi ya benki hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Muda wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein.
   Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alipotambulishwa rasmi na viongozi wa bodi ya benki hiyo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Muda wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein na baadhi ya viongozi wa benki hiyo.
    Mwenyekiti wa Muda wa Bodi ya Benki ya NBC Tanzania, Dk. Kassim Hussein (kulia) akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa benki hiyo, Edward Marks (kulia kwake) jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Benki ya NBC Tanzania, Edward Marks (kulia) alisalimiana na baadhi ya wanahabari waliohudhuria hafla ya utambulisho wake jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Waziri Mkuu wa Israel,Benjamin Netanyah.

  Waziri Mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu,ameunda serikali mpya ya mseto kabla ya kumalizika muda uliopangwa kwa kiongozi huyo kuwasilisha serikali yake.
  Netanyahu alifanikiwa kukishawishi chama cha kiyahudi cha mrengo wa kulia cha Jewish Home Party baada ya Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali inayoondoka madarakani, Avigdor Lieberman, kukataa chama chake cha Yisrael Baitenu, kuwa sehemu ya muungano wa Likud.

  Makubaliano hayo ya serikali ya mseto yanamhakikishia kupata wingi wa viti 61 katika bunge la nchi hio lenye viti vya wabunge 120. 

  0 0

  Na Ismail Ngayonga
  MFUKO wa wakfu wa kuendelezazao la Korosho nchini umetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kubangulia korosho vitakavyojengwa katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga.

  Taasisi zitakazojenga viwanda hivyo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Kitivo cha Biashara na Chuo Kikuu  cha Ardhi (ARU).


  Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba baina ya mfuko huo na wataalamu washauri jana (Jumatano Mei 6, 2015), Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfukohuo, Athuman Nkinde katika bajet iiliyopo kiwanda kimetengewa kiasi cha Tsh Bilioni 2 na pia fedha hizo zinatarajia 
  kuongezeka kila mwaka kulingana na mahitaji yatakavyojitokeza.


  Nkinde alisema ujenzi wa viwanda hivyo unatarajia kuanza katika kipindi cha miezi mitatu ijayo ambapo pindi vitakapomalika kila kiwanda kinataraji kuzalisha tani 10000 kwa mwaka, na kuongeza kuwa Ofisi yake ina imani kubwakuwa  ujenzi wa viwanda hivyo utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya zao la koroho nchini.


  Aliongeza kuwa madhumuni ya kuanzisha viwanda hivyo ni kuliongezea thamani zao la korosho ili liweze kuchangia kikamilifu katika kukuza uchumi wananchi pamoja na wakulima wa zao hilo nchini.


  Kwa mujibu wa Nkinde alisema taasisi zilizopewa kazi ya ujenzi wa viwanda hivyo havina budi kutambua thamani ya viwanda hivyo, kwani zipo taasisi nyingi zikiwemo za umma na zile za sekta binafsi zilizoomba zabuni kwa ajili ya ujenzi huo.


  “Tumeingia katika historia mpya leo hii, dunia nzim itasikia taarifa hizi za ujenzi wa viwanda hivi, hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa kuzingatia uwezo wa kitaaluma mliokuwanao” alisemaNkinde.


  “Tanzania imekuwa ikisafirisha nje ya nchi korosho ghafi, kwa kujenga viwanda hivi kutatusaidia kupunguza gharama hizo sambamba na kuongeza thamani ya zaohilo” alisema Nkinde

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Mfuko huo, Suleiman Lenga aliwataka wataalamu washauri hao kuzingatia viwango, ubora na muda katika kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo kwani taasisi hizo zina uzoefu mkubwa katika kusimamia na kundeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.


  Alisema katika mikataba iliyosainiwa, Chuo cha Ardhi kitahusika zaidi katika kuandaa michoro, ramani na usanifu wa majengo wakati, Chuo cha Biashara kitahusika katika kuandaa andiko la mradi litakalohusiana na masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa masoko.


  Naye Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kitivo cha Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba alisema taasisi itafanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha kuwa ujenzi huo utafikia katika ubora na viwango vilivyokusudiwa.


  “Zao la korosho limekuwa kwa sasa limekuwa ni zao muhimu kwa uchumi wa Tanzania na wananchi kwa ujumla, hivyo tutahakikisha kuwa kupitia  ujenzi huu zao hili linazidi kuongezewa thamani yake” alisema Dkt. Mbamba.


  Aidha Makamu Mkuu wa Taaluma katika Chuo Kikuu cha Ardhi, Prof. Gabriel Kassenga alisema wa Chuo kitahakikisha kuwa viwanda hivyo vitaleta tija kwa kukuza uchumi wa Taifa na wakulima wa zao la koerosho nchini.
  Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Nchini,Mundhir Mundhir 
  akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa viwanda vitatu vya kubangulia korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga kati ya Mfukowa Wakfu wa kuendeleza Zao la Korosho Nchini na wataalamu washauri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Mfuko huo Bw.SuleimanL enga.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa wakfu wa kuendeleza Zao la Korosho Nchini Bw. Athuman Nkinde akizungumza na waandishi wa habari (hawapopichani)Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga kati ya Mfuko huo na wataalamu washauri wa kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam na Shule ya Elimu ya Biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara . Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Mundhir Mundhir na Katibu Mtendaji wa mfuko huo Bw. Suleiman Lenga.
   Mwadili wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitivo cha Biashara, Dkt. Ulingeta Mbamba (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw. Suleiman Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leoJumatano (Mei 6, 2015) Jijini Dar es Salaam.
  1 Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi cha Jijini Dar es Salaam, Prof. Gabriel Kassenga (kulia) na Katibu Mtendaji wa Mfuko wakfu wa Kuendeleza zao la Korosho Nchini, Bw. Suleiman Lenga wakionyesha mkataba wa ujenzi wa viwanda vitatu vya korosho katika Wilaya za Mtwara, Tunduru na Mkuranga. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatano (Mei 6, 2015) Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

  0 0

  Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali hapa jijini Dar, imepekea baadhi ya njia kufungwa kutokana na wingi wa maji kwenye baadhi ya madaraja, hali iliyopelekea kuwepo kwa msongamano mkubwa la magari kama ionekanavyo pichani hapa katika Barabara ya Azikiwe, kutokea kwenye kipita shoto cha Askari.Picha zote na Othman Michuzi.
   Mjini leo hakuna kutoka, maana foleni ni kila kona.
   Azikiwe hiyo.

  Mzee wa Feva kaamua kukaa kando, maana hakuna hata anaetaka kumsikiliza.
   Barabara ya Ohio street nako mambo ni kama hivi.
   Trafiki wa kujitolea akizizuia gari zisiingie katikati ya barabara kuhofea kuendeleza msongamano.
   Baadhi ya Madereva wa magari yaliopo kwenye msongamano wakimsikiliza mzee wa Feva juu ya hali ya barabara.
   Mtaa wa Chimala 


  0 0

  Vijana wakiwa katika Maandamano nchini Burundi

  Watu wanne wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kuwania Urais kwa Mhula wa tatu.
  Mamia ya watu wamejitokeza kwenye maandamano hayo huku baadhi wakichoma moto baadhi ya vitu katika nchi hiyo.

  Siku ya jumanne Mahakama ya Katiba ilikubali kuwa Rais Nkurunziza anaweza kugombea urais ambapo ilisema ni halali yeye kuwania tena urais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

  Katika hotuba yake siku ya jumatano Rais Nkurunziza alisema kama atachaguliwa tena kuongoza nchi hiyo, mhula huu utakuwa wa mwisho kwake kuwa madarakani.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kituo cha redio cha 93.7 E-Fm, Denis Ssebo (kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sherehe za kuadhimisha miaka 16 ya muziki ya Msanii Juma Kassim Kiroboto "Juma Nature" (kulia) yatakayoambatana ya sherehe za mwaka mmoja za Kituo cha redio cha 93.7 E-Fm.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Kituo cha redio cha 93.7 E-Fm, Lydia Moyo
  Msanii Juma Kassim Kiroboto "Juma Nature" (kulia) akizungumzia sherehe hizo.

  0 0


  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akimkabidhi kitabu kinachozungumzia Hifadhi za Taifa zilizopo nchini Tanzania Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchni, Bwa. Alvaro Rodriguez alipomtembelea ofisini kwake
  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akimwelezea Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchni, Bwa. Alvaro Rodriguez juu ya Kahawa inayozalishwa Tanzania  na Kampuni ya Panone (Panone Fresh Coffee) 
  Balozi Mushy akimkabidhi Bwa. Rodrigues Kahawa iliyofungwa vizuri na kampuni ya Panone
  Picha na Reginald Philip

  0 0

  Katika kukabiliana na vitendo vya mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino),leo jeshi la jadi sungusungu katika halmashauri ya manispaa ya Shinyanga limekabidhiwa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja, laki 6 na elfu 50 kwa ajili ya kuhimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yao.

  Zoezi la makabidhiano limefanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.
  Pikipiki hiyo imetolewa na mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam kupitia kwa mfanyabiashara Ndegesela na kukabidhiwa kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga, James Deshi.Pichani katikati ni meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akikabidhi ufunguo wa pikipiki kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro ambaye naye alikabidhi ufunguo huo kwa katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi.

  Akikabidhi pikipiki hiyo meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam alisema pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha ulinzi na usalama ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ambapo alisema ingawa katika manispaa hiyo hapajaripotiwa tukio la mauaji ya albino,pikipiki hiyo itatumika katika kuimarisha zaidi ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na vikongwe.

  Matiro alisema wataendelea kutoa msaada wa pikipiki  kwa jeshi la sungusungu katika kata 17 za manispaa hiyo na mwezi Juni mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele atatoa pikipiki 2 kwa jeshi hilo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na  viongozi wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga
  Viongozi wa Jeshi la Sungusungu halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiondoka na pikipiki waliyokabidhiwa,anayeendesha ni katibu wa jeshi la sungusungu manispaa ya Shinyanga James Deshi-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga.

  0 0
 • 05/07/15--21:00: TID APIGWA KABALI
 • Msikilize TOP IN DAR A.K.A TID kwa 
  kubofya mstari mweupe hapo chini...

  0 0  0 0

  Leo, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi anatimiza miaka 90. Tulipata fursa ya pekee kuketi naye akatueleza mambo machache kuhusu maisha yake
  UNGANA NASI


  0 0

  DSC_0023
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (wa pili kulia), Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (kushoto), Afisa utawala na fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha (kulia), Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmar pamoja na mkalimani wa Balozi wa China wakifurahi jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani) akiwasili kwenye chumba cha mikutano Wizara ya Elimu kwa ajili ya hafla fupi ya kutiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini. (Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

  Na Modewji blog team
  SERIKALI na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jana wametiliana saini mkataba utakaowezesha kutekelezwa kwa mradi wa kuwezesha walimu wa Tehama vyuoni nchini.

  Akizungumza baada ya kutiwa saini kwa mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome alisema mradi huo ni mkombozi mkubwa katika maandalizi ya kufundisha kwa kutumia Tehama nchini.

  Alisema mpango huo wenye kuwezesha walimu kujifunza Tehama unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China ambao ndio wamepitisha fedha zao UNESCO.

  Katika utiaji saini huo ambapo Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing alikuwepo, katika jumla ya uhai wa mradi ambao ni miaka miwili , miundombinu ya ufundishaji masomo ya sayansi na hesabu katika vyuo vya walimu vya Monduli na Tabora itaboreshwa.

  Katika mradi huo walimu watafundishwa elimu ya Tehama, namna ya kufundisha na kujifunza.

  Katibu mkuu Mchome alisema kwamba vyuo hivyo viwili vitawezeshwa kuwa na mtandao ambao utaunganishwa na vyuo vingine vinane vya masomo ya sayansi na hesabu kwa ajili ya kubadilishana taaluma.
  Pia vyuo hivyo vitawezeshwa kuandaa programu zenye kuelezea mfumo wa utoaji huduma za Tehama kwa ajili ya walimu wa masomo ya sayansi na hesabu.
  DSC_0037
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimina kwa furaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome (kulia) na kushoto ni Balozi wa China nchini, Mh. LU Youqing (aliyeipa mgongo kamera).


  0 0

  Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko yaliyong'oa miti na kuharibu kingo za daraja la Kikuletwa wilayani Hai.
  Mti mkubwa ulizolewa na maji na kisha kugota katika daraja la Kikuletwa.
  Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kikuletwa wakivuka katika daraja hilo.
  Baadhi ya vijana wakiangalia namna ambayo wataweza kuondoa miti hiyo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na ujumbe kutoka Tume ya haki za Binadamu, ofisini kwake jijini Dar es salaam Mei 8, 2015. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Tom Nyanduga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa katika uongozi wake mpya atasimamia maslahi ya wafanyakazi wa shirika hilo na kuwakomboa katika dimbwi la umaskini ili kuendana na mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN).

  Ameyasema hayo jijini Dar es salaam katika kikao cha pamoja cha utambulisho wake kwa wafanyakazi wa Dawasco kilichowajumuisha wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo huku akisisitiza kuwa mshahara wa chini wa mwajiri katika shirika hilo utapanda ulipo hadi kufikia 650,000.

  Ameahidi kuboresha hali ya upatikanaji wa Maji kwa maeneo sugu zaidi Dar ikiwa ni pamoja na kubuni miradi mipya na kusimamia miradi iliyopo ili kuongeza kasi ya makusanyo ya shirika na pia kuweza kulipa wafanyakazi maslahi mazuri zaidi.

  “ongezeni kasi ya utoaji huduma kwa wateja na kuboresha mawasiliano na wateja kwani wao ndio kiungo muhimu katika kufikia malengo ya shirika na malengo yetu kwa ujumla” alisema Luhemeja Alisema katika uongozi wake atatengeneza DAWASCO mpya isiyo na fitina na itakuwa ni marufuku kwa watumishi wa shirika hilo kuitana wezi bila ya ushahidi na sababu za msingi, kufanya kazi kwa mazoea .

  Luhemeja ni Afisa Mtendaji Mkuu aliyeteuliwa kuendesha shirika hilo kuanzia 01/05/2015 kwa mkataba wa miaka mitatu. Kabla ya kuja DAWASCO, Mhandisi Luhemeja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA).
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza katika kikao cha pamoja cha utambulisho wake kwa wafanyakazi wa Dawasco kilichowajumuisha wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo, uliofanyika kwenye ukumbi wa JWTZ Kurasini jijini Dar
  Sehemu ya Wfanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) wakimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wao mpya, Mhandisi Cyprian Luhemeja (hayupo pichani).

older | 1 | .... | 829 | 830 | (Page 831) | 832 | 833 | .... | 3270 | newer