Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 821 | 822 | (Page 823) | 824 | 825 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopo Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
  Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5,  Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo ya  tatu ya kujishindia pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.  
  Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akionyesha nyaraka za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima na Mrs Mkola Mlima pamoja na Wafanyakazi wa Ubalozi wakiwapokea wageni katika kuadhimisha sherehe za miaka 51 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  Sherehe hiyo iliyofanyika katika Hotel ya InterContinental Iliyopo Kuala Lumpur ilihudhuriwa na wageni 300 wakiwepo Mabalozi, wawakilishi na viongozi mbali mbali kutoka sekta binafsi na fedha waliopo hapa Kuala Lumpur na baadhi ya wanafunzi na watanzania walioweza kushiriki.

  Serikali ya Malaysia iliwakilishwa na mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Biashara ya Kimataifa na Viwanda Mheshimiwa Seneta Dato' Lee Chee Leong".
   

  0 0

   Mhandisi wa Sunnrgy,Erick Mhema akielezea wadau mbalimbali kifaa cha kuvuta maji kutokana na kutumia Nishati ya jua (Solar Energy),wakati wa mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
   Kamishina wa Nishati na Petroli wa Wizara ya Nishati na Madini,Mhandisi Hosea Mbise akizungumza na waandishi na vyombo vya habari katika mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na  Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Mhandisi wa Sunnrgy,Erick Mhema akizungumza na waandishi na vyombo vya habari katika mkutano wa Wadau wa Nishati ya Jua na Upepo iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
  Baadhi ya wadau wakifatilia mada kutoka kwa watalaam wa kampuni ya Sunnrgy iliyofanyika leo katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII

  0 0

   Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamad akitoa maelezo na kuwakaribisha washiriki wa warsha ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Shangani mjini Zanzibar.
   Mfamasia Mkuu Zanzibar Habib Ali Shariff akitoa maelezo kuhusu mfumo huo mpya wa kielectroniki ulivyoanza kufanyakazi Zanzibar.
   Waziri wa Afya Zanzibar Rashid Seif ambae alikuwa Mwenyekiti wa warsha hiyo akitoa muongozo kwa washiriki .
   Mkurugenzi Usimamizi wa Mifumo ya kielectroniki kutoka Shirika la John Snow Incoparated (JSI) akizungumzia uimarishaji wa mfumo na mafanikio yake kwa washiriki wa warsha hiyo.
   Meneja wa Zoni ya Unguja ya mfumo mpya wa usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki Biubwa Khamis (aliesimama) akitoa uzoefu wa usambazaji wa  mfumo zamani na huu wa sasa katika warsha hiyo.
  Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha ya siku moja ya usambazaji dawa kwa njia ya kielectroniki iliyofanyika Park Hyatt Hotel Mjini Zanzibar.
  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  SALAAM ZA RAMBIRAMBI ZILIZOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI NDUGU ABUDLRAHAMAN KINANA WAKATI WA KUAGA MWILI WA BRIG. GEN. HASHIM MBITA (Mst)
  TAREHE 29 APRILI, 2015 – LUGALO DAR ES SALAAM


  Ndugu Rais, Amiri Jeshi Mkuu na Ndugu Waombolezaji,

  Maisha ni safari na kila safari huwa na mwisho wake,  Tuko hapa kwa kuwa safari ya Brig. Gen. Hashim Mbita duniani imefika ukingoni.  Tumekusanyika hapa siyo kuhuzunika bali kujivunia safari ya mafanikio makubwa ya Mwanamapinduzi, Mpiganaji, Mwanadiplomasia, Mwanahabari, Mwanasiasa na Mzalendo wa mfano.

  Mwanasayansi mashuhuri Albert Enstain aliwahi kusema kuwa, thamani ya mtu itapimwa kwa mchango wake kwa jamii siyo kwa kile alichokipata kutoka kwa jamii yenyewe.  Hakuna ubishi, Brig. Gen Mbita alitoa mchango mkubwa kwa Watanzania na Waafrika.  Aliipenda na kulitumikia Taifa lake.  Alishiriki kikamilifu kulijenga na kuliimarisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika miaka ya awali na aliongoza Chama cha TANU kwa ufanisi.  Lakini mchango na umahiri wake ulidhihirika katika kuiongoza Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika.

  Kwa kumbukumbu zilizopo kila kazi na jukumu alilopewa Brig. Gen. Mbita iwe Jeshini, Serikalini, katika Chama, katika kuongoza Ukombozi na baadaye kuandika historia ya Ukombozi, aliteuliwa kwa makusudi maalum na kwa malengo maalum.  Alipelekwa Uingereza kutoka Ikulu kwa lengo la kusaidia kulijenga Jeshi la Wananchi Tanzania liwe la kizalendo baada ya maasi ya mwaka 1964. Kwa kuamini kuwa Chama imara ndicho kinachotoa uongozi bora kwa Taifa, Brig. Gen. Mbita aliteuliwa kuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa TANU ili kuleta ufanisi na nidhamu katika Chama.

  Kuna msemo maarufu jeshini usemao Kamanda aliye jasiri anaweza kuwa na bahati. Lakini hakuna Kamanda anayeweza kuwa na bahati bila ya kuwa jasiri. Ujasiri aliokuwa nao Brig. Gen. Mbita ndiyo iliyokuwa sababu ya kuteuliwa kwake kuiiongoza Kamati ya Ukombozi wa Afrika.   

  Alishiriki kuvijenga vikosi vya Frelimo (Msumbiji), ZANU-PF (Zimbabwe), SWAPO (Namibia), ANC (Afrika Kusini), MPLA (Angola), MOLINACO (Comoro), PAIGC (Guinea Bissau, Cape Verde)  na vyama vingine.  Aliviandaa vikosi hivi kupambana na majeshi makubwa yenye silaha nzito na za kisasa na yenye nguvu nyingi.  Lakini mwaka 1994, Brig. Gen Mbita alihitimisha kazi ya Ukombozi wa Afrika kwa ushindi mkubwa.

  Chama Cha Mapinduzi kinatambua na kuthamini mchango na kazi kubwa iliyofanywa na Brig. Gen. Mbita katika kukiendeleza na kukiimarisha Chama cha TANU na baadaye Chama Cha Mapinduzi. Katika maisha yake kazini na hata baada ya kustaafu aliendelea kutoa ushauri, maoni na wakati mwingine kutoa uzoefu wake ndani ya Chama. 

  Tutauenzi mchango wake, tutajifunza utendaji wake, tutajitahidi kuiga mwenendo wake na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na ardhi na mwenye kutupa na kutuondolea uhai, ili amuonee huruma mja wake huyu.  Brig. Gen. Mbita atabaki kuwa na nafasi muhimu katika historia ya mapambano dhidi ya ukoloni, ubeberu, ubaguzi wa rangi na uonevu.

  Alikuwa kiongozi mwenye msimamo na mwenye kuelewa mambo mengi lakini msikivu. Inawezekana Watanzania wengi hatukumjua kwa kuwa hakushughulika kujulikana. Alikuwa jasiri na vile vile alikuwa na wingi wa unyenyekevu. Ujasiri wake ulidhihirika katika kufanikisha majukumu aliyokabidhiwa lakini unyenyekevu ulimzuia kujinadi.   

  Alitanguliza utumishi na kujiepusha na utukufu. Nafasi alizoshika zilikuwa za juu na zenye kuheshimika.  Kama angependa angeweza kupata umaarufu mkubwa katika nafasi aliyokuwa nayo lakini hiyo haikuwa hulka yake.  Maisha na Utumishi wake ni darasa kamili kwetu sote.

  Tunawashukuru viongozi waliokuja kuwakilisha vyama mbalimbali kuungana na Watanzania kumuenzi Brig. Gen. Hashim Mbita.  Wanafalsafa wanatuambia ushindi wa kumbukumbu za wale tutakaowakumbuka zitadumu katika mioyo ya watu na katika historia ya Taifa walilolitumikia. Sihitaji kuwashawishi Ndugu waombolezaji wenzangu kukiri kuwa Brig. Gen Mbita atabaki kwenye mioyo yetu na kuendelea kukumbukwa na wananchi wengi wa Bara la Afrika alioshirikiana nao kuwarudishia Uhuru wao na heshima yao.

  Kwa kumalizia, kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole kwa Mama Mjane, Watoto, Ndugu na Jamaa, Marafiki na kwa Jeshi la Wananchi Tanzania.

  Mwenyezi Mungu amfungulie milango ya Pepo.

  Imetolewa na:
   
  Idara ya Itikadi na Uenezi
  Chama Cha Mapinduzi
  30/04/2015

  0 0

  Book Launched: Photographic Journey - 50 years of United Republic of Tanzania 
  Deputy  Minister of Finance, Hon Adam Milama launched the much anticipated book,  Tanzania Photographic Journey - 50 years of  United Republic of Tanzania (The Union between Tanganyika and Zanzibar 1964 -2014 ) at Serena Hotel this week.
  The book celebrates and covers the historic journey of the 50 years of the United Republic Of Tanzania. The book, which comprises of over 444 pages describing in detail the historic journey of Zanzibar and then Tanganyika (Tanzania Mainland), covering the rich historical background and the political journey prior to the Union in 1964 and also the political journey of the factual events from 1964 until 2014.
  Javed Jafferji who is the publisher of the book said" It took 17 months to publish this book and it is the best book I have worked in the last 25 years out of 70 books i have published. I am proud that this book will remain a reference manual  for generations of Tanzanians to come"
  This book has been blessed by both the existing Presidents, Dr Jakaya Mrisho Kikwete and Dr. Ali Mohamed Shein by both having agreed to do the foreword for this book. Furthermore, it remains to be the only book that carries the foreword of both the Presidents of the United Republic of Tanzania and Zanzibar respectively and furthermore they are the current Presidents in power.
   Left JAVED JAFFERJI and Right Simai Mohammed Said.
   Launching of the book.
  Presenting a copy to Daimond who appears in the book as Icons of Tanzania.
   Presenting a Book to Mama Zakia Meghji.
   Signing of the book.
   Diamond proudly showing  the book.

  0 0

  Heads of State and government of the Southern African Development Community (SADC), meeting in Harare, Zimbabwe yesterday condemned the recent attacks against African migrants in parts of Durban and Johannesburg in South Africa. The summit meeting was reacting to a briefing by South Africa President Jacob Zuma on the nature of the xenophobic attacks and measures taken by his government to restore peace.

  According to a communique issued after the meeting, "Summit commended the measures that the government of South Africa has put in place and resolved to work together to deal with the situation and ensure it does not recur." The attacks affected the citizens of SADC member countries of Zimbabwe, Mozambique, Malawi, Zambia and Tanzania, which were forced to evacuate their people.

  The violence heightened tension between South Africa and its neighbours, some of whom threatened retaliatory measures. But briefing the media after the summit yesterday, The SADC Chairman, President Robert Mugabe, said the situation should not be blamed on South Africa alone. He said an virtually unchecked influx of migrants from neighbouring countries was stretching resources to the limit in South Africa, where the majority blacks were living in dire conditions.

  "Only the whites are living well there. Our people should not have the instinct to rush to Johannesburg in the false hope that it is heaven," he said. The SADC Chair said one way to arrest the influx was for SADC member countries to improve their economies and attract their youth to stay and work at home. Hundreds of Zimbabweans, Malawians, Mozambicans and Zambians were evacuated following the attacks, but millions more, who are largely unskilled, remain in South Africa.

  Twenty six Tanzanians were facilitated by the government to return home last week and the Tanzania High Commission in Pretoria is looking for others who may wish to return home. There was no Tanzanian among eight foreigners reported to have been killed in the attacks.

  President Zuma has been quoted in the media as saying he would address the root causes of the xenophobic attacks, which he said were poverty, unemployment and immigration. An estimated 53 percent of the South African population lives below the poverty line, according to the United Nations. (Ends) .


  0 0

   Mhe, Balozi Liberata Mulamula akiwa na wageni wake Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na mama Sitti Mwinyi mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Bethesda, Maryland.
    Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akisaini kitabu cha wageni
   Mama Sitti Mwinyi akisaini kitabu cha wageni mara walipowasili nyumbani kwa balozi
    Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na mama Sitti Mwinyi wenye nyuso za furaha baada ya kukaribishwa nyumbani.
    Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na mama Sitti Mwinyi wakitambua familia ya balozi kwenye picha .


  Baadhi ya ujumbe ulioambata na  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Afisa wa ubalozi wa Tanzania Washington DC, Swahiba Mndeme

  0 0


  Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif (kulia) akimuelekeza mshindi wa droo ya tatu ya mwezi wa Aprili, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam namna ya kuchomeka ufunguo wa pikipiki katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la kampuni hiyo zilizopo Bamaga-Mikocheni jijini Dar es Salaam leo. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
  Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif (kulia) akimkabidhi mshindi wa simu ya kisasa aina ya Solar 5,  Richard John, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar es Salaam mara baada ya kuibuka mshindi wa droo hiyo ya  tatu ya kujishindia pikipiki na simu ya mwezi wa Aprili inayoendeshwa na kampuni hiyo. Katikati akishuhudia ni Bw. Gideon Fumbuka ambaye naye alijinyakulia simu kisasa aina ya P40. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.  
  Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akionyesha nyaraka za pikipiki kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa katika ofisi za kampuni jijini Dar es Salaam. Pamoja naye katika makabidhiano ni Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif, kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

  Mshindi wa droo ya bahati nasibu ya kujishindia pikipiki inayoendeshwa mwezi huu wa Aprili na StarTimes Tanzania, Mary Luis Tumsifu, mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo na mfugaji pia, mkazi wa Kijitonyama, jijini Dar es Salaam  akichezesha droo ya bahati nasibu kumpata mshindi wa nne. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.


   Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania,  Zuhura Hanif akipiga simu kumjulisha mshindi ushindi wake.

  Na Dotto Mwaibale

   MKAZI wa Kijitonyama Dar es Salaam, Mary Luis Tumsifu (40) ambaye anajishughulisha na biashara ya kuuza vyakula vya mifugo na ufugaji amekabidhiwa zawadi ya pikipiki baada ya kuibuka mshindi katika droo ya tatu ya mwezi ya bahati nasibu inayoendeshwa na StarTimes Tanzania.
  Akizungumza wakati anakabidhiwa pikipiki yake Tumsifu amebainisha kuwa amefurahia sana zawadi hiyo kwani hakutegemea kama angeweza kushinda kwani alilipia kutazama vipindi anavyovipendelea.
  “Sikutarajia kama nitajishindia pikipiki lakini tayari ndiyo bahati imekwishaniangukia mimi. Ni kweli nilikuwa nafahamu kuhusu bahati nasibu hii kupitia njia mbalimbali kama vile kutumiwa ujumbe mfupi pamoja na matangazo. 
  Kwa kawaida huwa nalipia kifurushi kile kikubwa cha shilingi 30,000/- cha Kili. Mimi ni mpenzi sana wa ‘Series’na mwanangu anapenda kuangalia chaneli ya watoto ya ‘Nickelodeon’. Hivyo huwa sina budi kulipia ili mimi na mwanangu tufarahie vipindi tunavyovipenda.” Alisema  Tumsifu
  “Mimi ni mfanyabiashara wa vyakula vya mifugo lakini pia ni mfugaji. Kusema kweli hii zawadi imekuja kipindi ambacho sijaitarajia hivyo nashindwa hata kuelezea nitaitumia kwa namna gani. Naweza kuifanya kama biashara au mimi mwenyewe nikajifunza na kuwa dereva bodaboda.”  Alisema kwa masihara huku akicheka.
  Akizungumzia kuhusiana na imani waliyonayo wateja juu ya bahati nasibu hii kuwa ni uzushi, Tumsifu alifafanua kuwa, “Kwanza kabisa ningependa kuwatoa hofu na kuwahakikishia wateja na watanzania kuwa kitu kama hicho hakipo. 
  Kwa mfano mimi sifahamiani na mtu yeyote StarTimes, huwa nalipia vifurushi vya mwezi kama wateja wengine lakini nimebahatika nimeshinda. Hivyo basi nawaomba wengine pia waondoe mawazo hayo na kushiriki pindi wanapoambiwa wafanye hivyo.”
  “Nashukuru sana kwa zawadi hii, ninaahidi nitaitumia vema ili inisaidie katika shughuli zangu. Wito wangu, kwanza kabisa kwa StarTimes, nawapongeza kwa huduma bora wanazotupatia wateja wao tena kwa bei nafuu, ninawaomba wazidi kuboresha zaidi, wasikilize maoni yetu ili tuzidi kufurahia.” Alihitimisha. Tumsifu
  Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif aliwataka wateja wa kampuni hiyo kuchangamkia hii fursa kwa kujiunga zaidi na vifurushi ili waweze kuburudika na pia kushinda.
  “Ningependa kutoa wito kwa wateja wetu kujiunga zaidi kwani zawadi bado zipo na pongezi kwa waliojishindia. Zawadi hizi tunazozitoa ni sehemu ya mpango wa StarTimes kurudisha fadhila kwa wateja wake kuwa waaminifu na kutuunga mkono tangu awali tulipoanza kufanya kazi. 
  Tunafahamu kuwa hiki tunachokitoa hakitoshi hata chembe lakini tunachoweza kuwaahidi ni kuwapatia huduma bora na nafuu kwa asilimia mia moja.” Alihitimisha Hanif
  Mbali na kukabidhiwa kwa mshindi huyo, StarTimes pia walichezesha droo kumtafuta mshindi wa nne wa pikipiki ambapo Bw. Samson Mollel, mkazi wa Arusha ambaye amenunua king’amuzi cha kulipia cha NYOTA kinachouzwa kwa shilingi 34,000 siku moja kabla ametajwa kuwa ni mshindi. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kuanzia Jumamosi iliyopita, Aprili 24, 2015, taarifa iliyotolewa Dar es Salaam, leo, Alhamisi, Aprili 30, 2025 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) imesema.


  Taarifa hiyo imewataja wajaji hao kuwa ni Jaji  Augustine Gherabast Mwarija na Jaji Stella Ester Augustine Mugasha, ambao wote wamekuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania tokea walipoteuliwa Novemba 28, 2006.

  Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mwarija alikuwa Jaji Mfawadhi, Kitengo cha Biashara, Mahakama Kuu, Dar Es Salaam. Kabla ya kuwa Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani kati ya mwaka 2003 na 2006.

  Aliajiriwa kama Hakimu Mkazi Daraja la Tatu Februari 2, mwaka 1987, baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka 1986.

  Naye Jaji Mugasha, kabla ya uteuzi wake, alikuwa Jaji Mfawidhi, Dar es Salaam. Alikuwa Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na awali Kanda ya Moshi tangu 2009 hadi alipohamishiwa Mahakama Kuu, Dar Es Salaam.

  Aliajiriwa kama Wakili wa Serikali mwaka 1983 baada ya kupata Shahada ya Sheria mwaka huo huo, 1983.


   Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.  30 April, 2015


  0 0

  Mradi wa kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini umekuwa na mafanikio kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao kwa kutumia kilimo hifadhi lakini changamoto kubwa imeonekana ni ukosefu wa masoko . 
  Mradi huo ambao unafadhiliwa na mtandao wa mapinduzi ya kijani barani Afrika (AGRA )unatekelezwa na mashirika manne katika wilaya sita za mikoa ya Mbeya na Rukwa katika mazao manne kutokana na eneo husika ambayo ni Mahindi , mpunga , Soya na maharage kwa kutumia kilimo hifadhi . 
  Katika siku ya wakulima iliyofanyika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga , Mwenyekiti wa chama cha ushiliki mazao na masoko Laela Amcos Limited bwana Edom Mwaisemba amesema wakulima wamelima kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuzalisha mazao mengi lakini kinachowakwamisha ni soko . ‘’ Kwa mfano mwaka jana tulipata tani 2,500 lakini tukashindwa wapi tutapata soko . 
  Tunauomba mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) kwasababu umetufundisha jinsi ya kulima na tumelima kikamilifu kwa kufuata kanuni bora na tunaweza kupata hadi tani 3,500 kwa hiyo tunauomba ututafutie soko’’ alisema bwana Mwaisemba . 
  Bwana shamba kutoka taasisi ya kilimo , biashara tegemezi ya mazao mengi ya mkoani Ruvuma(RUCODIA) bwana Evaresto Joshua amesema kwa kuondoa changamoto ya soko wamekubaliana na mashirika mengine ya mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) , CNV na micro finance limited kuwatumia mawakala wa pembejeo pia kununua mazao . 
  Changamoto ya matumizi bora ya mbegu pia imejitokeza katika siku hiyo ya wakulima ambapo wakala wa mbegu SEEDCO Tanzania Limited imewashauri wakulima kutotumia mbegu kutoka nje ambazo hazijapimwa na taasisi za ndani ya nchi . 
   ‘’ Tunajaribu kuwasisitiza wakulima kuhusu matumizi bora ya mbegu bora . Lakini zaidi tunasisitiza uagizaji na ununuzi wa mbegu ambazo zinatoka nchi za jirani ziwe zimepimwa na taasisi mbali mbali za nchini mwetu ‘’ alisema bwana Joshua Zuberi , afisa mauzo kutoka wakala wa mbegu SEEDCO Tanzania Limited . 
   Nao wakulima wamesema kilimo hifadhi kimewasidia kuhifadhi udongo na pia kupunguza gharama za kilimo na kuongeza uzalishaji ikilinganishwa na awali . ‘’ Unakuta mwanzoni heka moja ulikuwa unatumia shilingi 500,000 lakini kwa sasa hivi angalau inapungua hadi shilingi laki mbili . Unaposema kupunguza gharama ni sehemu zote kuanzia uandaaji wa shamba . Kwa mfano kuandaa shamba kunahitaji kutumia moto lakini sasa hivi tunahifadhi udongo tunafukia mlemle ndani ‘’ alisema bwana Ezebius Chapita , mkulima kijiji cha Lula . 
  Faida nyingine za mradi huu ni kusogeza huduma ya ugani karibu kwa namna ya kwamba sio kila kijiji kina afisa ugani lakini kutokana na mafunzo haya ya kilimo hifadhi tumeweza kuwasaidia wakulima viongozi kutoa taarifa za ugani kwa wakulima wetu na pale inaposhindikana wanaweza kuwasiliana na sisi kwa kuwasaidia zaidi .’’ alisema Nicholas Johanes , afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika ( ACTN) 
   Naye Joseph Mwangono , afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga ambaye alimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Sumbawanga katika sherehe hizo alisema kumekuwa na mafanikio kutokana na wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo
   ‘’ Kwa upande wa zao la mahindi wengi sasa wanapanda kwa kutumia mistari ,wanatumia mbolea na wanapalilia kwa wakati tatizo tu linakuwa soko la zao hilo la mahindi . Kwa zao la maharage zamani walikuwa wanapanda kwa kumwagilia lakini sasa hivi wanapanda kwa mistari na kutumia mbolea ‘’ alisema bwana Mwangono . 
   Kanuni za kufuata katika kutumia kilimo hifadhi ni pamoja na kufunika udongo kwa kutumia mazao funika au mabaki ya mazao , kutosumbua udongo na kupanda bila kulima kwa kutumia zana maalum . Kwa mujibu wa ACTN , mafanikio ya kwanza katika maeneo maalum Tanzania ni pamoja kupunguza mmonyoko wa udongo kwa zaidi ya asilimia thelathini .
  Afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) Nicholas Johanes (wa kwanza kulia aliyechuchumaa  aliyeshika simu) akitoa maelezo kwa kulima(nyuma yake) kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa siku ya wakulima iliyofanyika katika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga . Wapili kushoto ni Joseph Mwangono , Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga 
   Wakulima wakiangalia moja ya shamba darasa Mbeya vijini. Aliyeinama mbele yao ni Nicholas Johaness , afisa kilimo (ACTN)
  Bango la mradi

  0 0

   Afisa masoko wa Airtel tanzania Prospa Mwanda akionyesha kwa wanafunzi wa chuo Kikuu dodoma (UDOM) jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi Intaneti  inavyofanya kazi mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo chuoni hapo jana. Airtel Tanzania chuoni hupo imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu

   Meneja masoko wa Airtel Uni Wi-Fi Bi Aneth Muga anaepiga picha ya selfie ili waitume kwa kutumia huduma ya Airtel Wi-Fi intaneti kwa baadhi ya uongozi wa wanafunzi na mshauri wa wanafunzi chuoni hapo mara baada ya Airtel kuzindua huduma yao ya  intaneti Wi-Fi yenye kasi zaidi  maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho
   Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) bw, Dick Manong akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UNI Wi-Fi jana chuoni hapo ambapo itawasaidia wanafunzi kupata intaneti kwa gaharama nafuu ya yenye kasi zaidi.
  kutokana na ukweli kwamba Dodoma ni mji mteule na wenye kuendelea kwa kasi hapa nchini na pia ni mji uliobahatika kuwa miongoni mwa mji wenye chuo kikubwa hapa Tanzania, Airtel Tanzania mkoani huko imezindua huduma ya UNI Wi-Fi Intaneti yenye ubora zaidi na itakayopatikana kwa wananfunzi kwa gharama nafuu
  UNI WI-FI itawezesha wanafunzi zaidi ya 60,000 katika Chuo Kikuu cha Dodoma kupata huduma ya kimtandao ya Intaneti iliyo bora na nafuu pamoja na  kukidhi mahitaji ya wote waishio chuoni hapo.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Airtel Bi , Adriana Lyamba alisema: "Leo hii tunazindua Airtel UNI WI- FI huduma ya internet inayopatikana kwa bei nafuu kwa ajili ya wanafunzi na  pia tumeongeza mnara wa pili  wa simu   ambao tunaamini utaimarisha mtandao wetu hapa UDOM na kuinua uchumi  wa nchi yetu na kwa watu wanaoishi karibu na maeneo haya 
  Tunafuraha kubwa kwa Airtel kuweza kuboresha Maisha ya wanafunzi hapa chuoni  kwani spidi hii itawawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti wao, kupata habari mbalimbali za  taaluma au kijamii  kupitia mtandao wetu wa Airtel " 
  Meneja Masoko wa Airtel UNI WI-FI, Bi, Aneth Muga, alisema "Airtel wifi itakuwa inapatikana kwa mwanafunzi yoyote hapa  UDOM, kwa kutumia simu zao za mkononi, laptop, kamera na kwa mwanafunzi yoyote aliyepo UDOM bila kujali mtandao wa simu wanaoutumia.
  Wanaweza kununua UNI Wi-FI vocha ambayo inapatikana  masaa 24 , kwa kifurushi cha siku , wiki,  mwezi na kifurushi cha usiku mzima.
  Fikiria! Unaweza kufurahia kifurushi cha 1 GB kwa shilingi  500 tu! Alisisitiza Bi, Muga. 
  Kwa upande wake mgeni rasmi ambae ni mshauri wawanafunzi chuoni hapo (UDOM) Bw, Dick Manongi   alisema: ". Tunawashukuru sana Airtel Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa huduma hii kubwa na ya bei nafuu hapa chuoni. Nina hakika kwamba, huduma hii itaimarisha uwezo wa kujifunza na kuendelezea wanafunzi  urahisi wa kujipatia Habari mbalimbali zinazoendelea hapa nchini na hata nje ya nchi ".
  Ningependa kuwaomba wanafunzi wote kutumia fursa hii kubwa ili kuweza kuongeza ujuzi wao kitaaluma na katika Maisha yao ya baadae. 
  Uzinduzi wa Airtel Uni Wi- Fi katika chuo kikuu cha Dodoma umekuja mara baada ya Airtel Tanzania kuzindua huduma kama hiyo katika chuo kikuu cha Saint Augustine (SAUT) jijini Mwanza na mipango mingine inaendelea kufikia vyoo vingine hapa nchini.

  0 0

  Mwanamuziki mkongwe na mtunzi Tshimanga Kalala Assosa

  ​UZINDUZI WA KITABU NA KAVASHA CLUB...
  Jumapili hii tarehe 03-May-2015, mwanamuziki mkongwe Tshimanga Kalala Assosa atazindua kitabu kilichokuwa kikisubiriwa na watu wengi sana kwa muda mrefu mno.
  Ni kitabu cha "Jifunze LINGALA kwa Kiswahili".
  Uzinduzi huo utaambatana na tukio kubwa sana la wana Dar Kavasha Club pamoja na chakula cha jioni cha pamoja (dinner).
  Ni ndani ya ukumbi wa MRC Jumapili (03-May-2015) kuanzia saa 12 hadi saa 3 jioni. MRC ndio ukumbi ambao "Club Raha Leo Show" ya TBC1 ilikuwa inafanyikia.
  Tshimanga Kalala Assosa amepata kupiga bendi nyingi kubwa hapa Afrika kama Negros-Success (akiwa na Bolhen na Bavon Marie), Orchestre Lipua Lipua, Orchestre Les Kamale (akiwa na Nyboma, Mulembu na Kizunga) pamoja na Fukafuka zote za Congo DRC. Kwa hapa Tanzania amefanya kazi na Mlimani Park Orchestra, Marquis Original, Orchestre Makassy, Orchestre Mambo Bado, Legho Stars na Bana Maquis.
  Mgeni rasmi wa tukio atatangazwa.
  Wote mnakaribishwa. Wahi bila kukosa. Kiingilio ni BURE.

  0 0
 • 04/30/15--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Juwata Jazz Band - Nidhamu ya kazi

  0 0

  The DJ and  MC with some fans pose for our photographer tonight at the Golden Crest 8th floor roof top bar in Mwanza happening now. 

  0 0

   Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.
  Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifaania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal. Picha na OMR

  0 0

  HUWEZI KUPITWA NA DANGA CHEE! Usiwaze, kwenye simu yako ya mkononi fuatilia popote ulipo ukiwa na SIMU.tv. Kujiunga piga *149*01# chagua Shangwe, kisha SIMU.tv(MPYA) kisha Video hitajika kisha Habari kisha Michuzi TV kwa walio na laini za Vodacom. 
  Kwa yeyote mwenye simu au tablet ya Android pata app ya SIMU.tv kwenye Google play; bofya hapa: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.SIMU.tv.


  0 0


  0 0


  0 0

  Na Teresia Mhagama.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage ameanza rasmi ziara ya kikazi katika kanda ya kusini ambapo ameanza ziara hiyo kwa kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika wilaya ya kitanesco ya Makambako, Mhandisi Abdulrahman Nyenye, amesema kuwa uzinduzi wa mradi huo ni kielelezo cha utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme vijijini awamu ya pili inayotekelezwa na TANESCO kwa kushirikiana na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage akibonyeza kitufe kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (wa kwanza kushoto) akiangalia kikundi cha utamaduni cha mkoani Njombe mara baada ya kuzindua rasmi transfoma yenye uwezo wa 50KVA itakayohudumia wateja 200 katika kijiji cha Maguvani wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe.Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mhe. Deo Sanga.
  Mbunge wa Njombe Kaskazini, Mhe. Deo Sanga (wa pili kulia) akieleza hali ya nishati katika Jimbo lake mara baada ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (katikati) kuwasili katika Ofisi za Tanesco, wilaya ya kitanesco ya Makambako mkoani Njombe akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo cha kufua umeme mkoani Ruvuma. Wa pili kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) katika wilaya ya kitanesco ya Makambako, Mhandisi Abdulrahman Nyenye.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage (mwenye shati la mistari) akiangalia jinsi wateja wanavyohudumiwa katika ofisi za Tanesco, Makambako, mkoani Njombe. Naibu Waziri alitembelea ofisi hizo akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya umeme inayotekelezwa katika Kanda ya Kusini pamoja na kuzindua kituo cha kufua umeme mkoani Ruvuma.

older | 1 | .... | 821 | 822 | (Page 823) | 824 | 825 | .... | 3285 | newer