Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

DJ PETER MOE NA GROOVEBACK DEEJAYS ALHAMISI HII @ RHAPSODY'S- TOWN


TASWIRA ZA SUNDAY CELEBRATION SEASON 6 YA GWT

0
0
Mjasiriamali mahiri Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo akitoa somo la ujasiriamali.
Wageni wakisikiliza somo la ujasiriamali kutoka kwa Shigongo.
Waimbaji wa GWT wakizidi kutoa burudani kwa washiriki wa Sunday Celebration Season 6.

KWA mara nyingine, kile Kikundi cha Kusifu na Kuabudu nchini cha Glorious Worship Team (GWT) Jumapili iliyopita kiliendelea na programu yake ijulikano kwa jina la 'Sunday Celebration' ambayo hufanyika kila Jumapili jioni.

Wiki iliyopita ilikuwa ni Sunday Celebration Season 6 ambapo burudani mbalimbali pamoja na elimu ya ujasiriamali vilitolewa kwa watu waliohudhuria katika Ukumbi uliopo Victoria Service Station, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Burudani ukumbini hapo ziliongozwa na Kundi la GWT likishirikiana na The Jordan Band huku elimu ya ujasiriamali ikitolewa na Mwalimu mahiri wa Ujasiriamali Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.(PICHA ZOTE NA GWT).
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Article 11

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI PAUL MAKONDA, APOKEA VIFAA VYA MICHEZO KUTOKA KWA WADAU WA MICHEZO NCHINI KWA AJILI YA MASHINDANO YA KINONDONI CUP

0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, wakati akipokea msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 50 kutoka Kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN) wa ajili ya mashindano ya Kinondoni Cup yatakayoanza Juni 2015 katika wilaya hiyo.
 Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy  Kinachosambazwa na Kampuni ya TSN, Khamis Tembo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Smart Sports, George Wakuganda, akizungumza katika mkutano huo baada ya kutoa mipira 50 kwa ajili ya mashindano hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akiangalia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na Kampuni ya TSN pamoja na Kampuni ya Smart Sports  ambayo imetoa mipira 50 kupitia Mkurugenzi wake, George Wakuganda.

 Suleiman Msuya

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, Paul Makonda amepokea msaada wa jezi seti 100 na mipira 50 kutoka kampuni ya Tanzania Sisi Nyumbani (TSN), ambavyo vina thamani ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya mashindano ya mpira wa netibali na mpira wa miguu yatakayoitwa Kinondano Cup.

Akizungumzia msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kinondani, Paul Makonda alisema mikakati yake ni kuhakikisha kuwa vijana wa Wilaya hiyo wanatumia vipaji vyao kujikwamua katika umaskini.

Makonda alisema mashindano hayo yatakuwa ni mpira wa miguu wanaume na wanawake, mpira wa kikapu wanawake na wanaume na mpira wa netibali ambao ni wanawake pekee.

"Nimedhamiria kuhakikisha kuwa jamii inaondokana na dhana kuwa wakazi wa wilaya hiyo ni watumia madawa na uchangudoa na njia sahihi ni kuwahusisha vijana na kutumia vipaji vyao," alisema.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huyo Meneja wa Kinywaji cha Chilly Willy ambacho ndio wametoa mtaasa huo kupitia TSN, Khamis Tembo alisema msaada huo una lengo la kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Tembo alisema kampuni ya TSN inatambua umuhimu wa michezo hivyo kupitia Chilly Willy wameona ni muhimu kutoa msaada huo wa jezi seti 100 na mipira 50 ili kufanikisha malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Smart Sport, George Wakuganda ambaye kampuni yake imetoa mipira 50 alisema wameamua kuungana na Mkuu wa Wilaya kwani wao ni wanamichezo.

Wakuganda alitoa wito kwa wadau wengine kuungana na Mkuu huyo wa Wilaya kwani jitihada zake za kuhakikisha vijana wanatoka katika dibwi la umaskini ni za maana.


PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MH. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA BRITISH AMERICAN TOBACCO

0
0
PRIME MINISTER MIZENGO PINDA SPEAKING TO BRITISH AMERICAN TOBACCO OFFICIALS IN HIS OFFICE, DAR ES SALAAM, APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA, ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA.
PRIME MINISTER, MIZENGO PINDA POSES FOR A GROUP PHOTO WITH BRITISH AMETICAN TOBACCO OFFICIALS AT HIS OFFICE IN DAR ES SALAAM ON APRILI 28, 2015. FROM LEFT IS ENREST LE ROUX, REGIONAL MANAGER EAST AFRICA- BAT AND CONNIE ANYIKA CORPORATE AFFAIRS HEAD EAST AFRICA, PM, CHRIS BURREL REGIONAL DIRECTOR EAST AND CENTRAL AFRICA, JOHAN VANDERMEULEN REDIONAL DIRECTOR AFRICA, MIDDLE EAST AND EUROPE FOR BRITISH AMERICAN TOBACCO AND TEDDY MAPUNDA BOARD MEMBER BRITISH AMERICAN TOBACCO KENYA.

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA BRAZILI

0
0

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU AAGANA NA BALOZI WA BRAZILI

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekutana na Balozi wa Brazili nchini Tanzania, Bw. Fransisco Luz na kujadiliana mambo kadhaa kuhusu maendeleo na mahusiano baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza na Balozi Luz ofisini Magogoni jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumatano, Aprili 29, 2015), Waziri Mkuu alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano ambao ameutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi cha miaka sita ambacho amekuwa akiiwakilisha nchi yake hapa nchini.

Balozi Luz ambaye amepangiwa kwenda Jordan kwenye kituo kipya, alisema anaondoka nchini akiamini kwamba mtu atakayekuja kumpokea ataendelea mambo aliyoyaanzisha ikiwemo mradi wa kufadhili utafiti na uendelezaji wa zao la pamba kwenye kituo cha utafiti wa kilimo cha Ukiriguru, Mwanza.

Balozi Luz ambaye alifika kumuaga Waziri Mkuu, alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu kwamba ubalozi huo umefanikiwa kupeleka Watanzania wawili kusomea kozi za Uzamili (Masters’ Programme) kwenye vyuo vikuu vya Brazil.

“Wanafunzi hawa wawili waliondoka Februari mwaka huu, ni kati ya wanafunzi saba waliofuzu lakini wengine watano walikosa ufadhili kutoka kwenye taasisi zao. Mmoja anasomea Geo-Physics na mwingine Oil Engineering,” alisema Balozi Luz.

Balozi Luz ambaye anatarajia kuondoka nchini mapema mwezi ujao, amepangiwa kituo kingine ambapo ataenda kuiwakilisha nchi yake nchini Jordan.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMATANO, APRILI 29, 2015.

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA DHARURA WA VIONGOZI WA NCHI NA SERIKALI.

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili kwenye Hoteli ya Rainbow, jijini Harare, Zimbabwe kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini unaojadili kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake katika Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015 na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Jijini Harare, Zimbabwe, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akitoa hotuba yake, wakati akifungua rasmi Mkutano wa dharura wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa SDC, uliofunguliwa leo Aprili 29, 2015, kuhusu Uendelezaji wa Viwanda. 

BENKI KUU YATOA TAARIFA KUHUSU upotoshaji unaoendelea juu ya Sarafu ya sh. 500/=

0
0
Asilimia 94 ya madini katika sarafu ya sh. 500 ni chuma na asilimia 6 ni Nickel, ameeleza Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki katika Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Marcian Kobello. 

Pia ndivyo ilivyoelezwa wakati wa uzinduzi wa sarafu hii mnamo mwezi Septemba mwaka jana kabla haijaingizwa katika mzunguko mwezi Oktoba 2014. 

Bw. Kobello amesema hadi sasa sarafu zenye thamani ya sh. 1,162,000,000/- zimekwishasambazwa kote nchini na kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu hiyo endapo itahitajika.

“Hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya sh. 500,” amesema Bw. Kobello na kuongeza kuwa haitegemewi kwamba mfanyabiashara yeyote anaweza kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake halisi.
“Kwa hiyo, tunapenda kuwafahamisha wananchi kwamba kuna kiasi cha kutosha cha sarafu za sh. 500 nchini na kwamba kununua sarafu hiyo kwa bei ya juu kuliko thamani yake ni kujiingizia hasara,” ameeleza mkurugenzi huyo.

Pia ameongeza kuwa Nickel sio miongoni mwa madini maarufu kwa ajili ya kutengeneza vidani vya thamani.

Imetolewa na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
Aprili 29, 2015.

SERIKALI YA NEPAL YASEMA INASIMAMIA VYEMA MISAADA

0
0
Wanajeshi wa nchini Nepal wakiwa wamebeba misaada kwaajili ya wahanga wa tetemeko la ardhi

Kwa Msaada  wa mtandao.
Serikali ya Nepal imejitetea dhidi ya malalamiko juu ya misaada ya dharura, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi  lililotokea Jumamosi  nchini humo.

Mkuu wa masuala ya dharura wa Nepal,Rameshwor Dangal,ameambia BBC serikali inajitahidi iwezavyo, lakini mkasa huo ulikumba majimbo 20 nchini humo na hivyo mahitaji ni mengi sana ndiposasa serikali inaelemewa.

Hali ya kutamauka imewakumba wengi waliothiriwa na tetemeko hilo,na wengine wameonesha malalamiko yao kwa kulumbana na polisi huko Kathmandu, mji mkuu wa taifa hilo.

Angalau sasa misaada ya bidhaa muhimu na huduma zimeanza kuwafikia waavijiji katika mji wa Kathmandu nchini humo.

Wakati huo huo, Mwanamme aliyetolewa ndani ya kifusi katika hoteli iliyoporomoka mjini Kathmandu ameelezea jinsi alivyoweza kuishi kwa saa 82 kabla ya kuokolewa.

Rishi Khanal amesema alilazimika kunywa mkojoo wake wakati akisubiri kuokolewa.

Mguu wake alikwama ndani ya kifusi lakini aliweza kuwasiliana na jamaa zake akitumia simu yake ya mkononi.

Hata hivyo hakumbuki hoteli alimokuwa, aliokolewa na makundi ya uokoaji kutoka nchini humo na Ufaransa.

Zaidi ya watu 5000 wamepoteza maisha katika janga hilo la tetemeko la ardhi huko Nepal.

Brigedia Jenerali (Mstaafu) Hashim Mbita azikwa leo kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar

0
0
Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.Picha zote na Hamis Makuka.
 Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.
Sehemu ya Maafisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wakiongoza shughuli ya kuusafirisha mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kuelekea kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam leo.

NIC YATOA MSAADA WA VIFAA VYA ELIMU KWA WATOTO WENYE UONI HAFIFU KITUO CHA ALBINO BUHANGIJA SHINYANGA

0
0
Shirika la Bima la taifa leo limetoa msaada wa vifaa 34 vya kujifunzia darasani kwa watoto wenye uoni hafifu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi(Albino),wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga. Vifaa vilivyotolewa ni darubini kiona mbali(Telescope Monocular),Kikuza Maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Ndani ya ofisi ya mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Bungaja ambaye ndiye msimamizi mkuu wa kituo cha walemavu wa ngozi,wasioona na wasiosikia cha Buhangija katika manispaa ya Shinyanga,Mwalimu Peter Ajali (katikati),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima Makange ,kulia ni Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez wakijadili jambo kabla ya kukabidhiana vifaa 34 vilivyotolewa na Shirika la Bima la taifa ikiwemo Darubini kiona mbali(Telescope Monocular),kikuza maandishi cha Kusimamisha(Stand Magnifier) na Kikuza Maandishi cha Kuweka juu ya Maandishi( Dome Magnifier).
Meneja wa Shirika la Bima la taifa tawi la Shinyanga Halima  Makange akimkabidhi  vifaa hivyo na kushikana mkono na msimamizi mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali.

ngoma azipendazo ankal

0
0
Twanga Pepeta (African Stars)- Mtu Pesa

WAZIRI MKUU PINDA AKUTANA NA DANGOTE

0
0

Mradi wa kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini wawanufaisha wakulima

0
0
Afisa kilimo wa mtandao wa kilimo hifadhi barani Afrika (ACTN) Nicholas Johanes (wa kwanza kulia aliyechuchumaa aliyeshika simu) akitoa maelezo kwa kulima(nyuma yake) kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa siku ya wakulima iliyofanyika katika kijiji cha Laela wilaya ya Sumbawanga . Wapili kushoto ni Joseph Mwangono , Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga.
Wakulima wakiangalia moja ya shamba darasa Mbeya vijini . Aliyechuchumaa ni Nicholas Johaness, afisa kilimo (ACTN)

Na mwandishi wetu 
Mradi wa  kutekeleza tija ya uzalishaji katika nyanda za juu kusini umekuwa na mafanikio kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao  kwa kutumia kilimo hifadhi lakini changamoto kubwa imeonekana ni ukosefu wa masoko .

Mradi huo ambao unafadhiliwa na mtandao wa mapinduzi ya kijani barani Afrika  (AGRA )unatekelezwa na mashirika manne katika wilaya sita za mikoa ya Mbeya na Rukwa katika mazao manne kutokana na eneo husika ambayo ni Mahindi , mpunga , Soya na maharage  kwa kutumia kilimo hifadhi .

Katika siku ya wakulima iliyofanyika kijiji cha  Laela wilaya ya  Sumbawanga , Mwenyekiti wa chama cha ushiliki mazao na masoko Laela Amcos Limited  bwana Edom Mwaisemba amesema wakulima wamelima kwa kufuata kanuni bora za kilimo na kuzalisha mazao mengi lakini kinachowakwamisha ni soko .

CBA YAHIMIZA WATANZANIA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA NYUMBA

0
0
Meneja Masoko wa kampuni ya AVIC International,Bw.He Xianlong (katikati) akimwonyesha Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo na maofisa alioambatana nao ramani za nyumba  zilizojengwa kwa ajili ya kuuzwa wakati wa ziara ya maofisa wa CBA walipotembelea mradi huo leo. CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi
Maofisa wa CBA Na Avic wakiangalia nyumba ambazo  zimejengwa kwa ajili ya kuuzwa kwa wananchi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo  na maofisa wengine wa benki hiyo wakiwasili katika eneo la Kigamboni walipofanya ziara ya kutembelea nyumba za mradi wa Avic International,CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi.Wengine pichani ni maofisa waandamizi ya Avic.
Meneja Msaidizi wa kampuni ya AVIC International,Bw.Li.Jiayin (katikati) akimwonyesha Mkurugenzi wa Benki ya CBA Tanzania,Bw.Julius Mcharo eneo la mradi  wa  uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za kuuza wakati wa ziara ya maofisa wa benki hiyo kutembelea nyumba hizo. CBA imeingia mkataba wa kutoa mikopo kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba hizo kwa ajili ya makazi.

KLABU YA MICHEZO YA RIADHA YA DAR ES SALAAM ‘DAR RUNNING CLUB’ YAANDAA MASHINDANO YA RIADHA YA MARATHON 02 MAY 2015

0
0
Klabu ya michezo ya riadha ya Dar Es Salaam “Dar Running Club” (DRC) imeandaa mashindano  ya  mbio yajulikananyo kama “Mayday marathon” yatakayofanyika tarehe 02Mei 2015 yatakayoanza na kumalizika katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay (Police Officers Mess).
Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania  Inspekta Generali wa Police Ernest Jumbe Mangu (IGP).

Akizungumza na waandishi wa habari Mlezi wa Klabu ya DRC Mkuu wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni bwana Camillus Wambura) amesema DRC ni klabu ambayo ilianzishwa rasmi kutokana na makundi mawili tofauti yenye malengo sawa kimichezo, yaani Kinondoni police jogging club kutoka Polisi mkoa wa Kinondoni na Dar Es Salaam Athletic Club yenye washiriki kutoka maeneo mbali mbali ya Dar Es Salaam wakaamua kuungana na kuwa DRC. 

DRC ina madhumuni makubwa  ya kuendeleza michezo ya riadha nchini mpaka nje ya nchi na kuhimiza afya njema kimwili na kiakili, lakini pamoja na hayo muungano huu wa klabu unasaidia sana kuimarisha mahusiano  kati ya  Polisi na raia, hii inasaidia sana katika usalama na kukuza na kuendeleza dhana ya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kwa jamii. Aliongezea…
 
Naye Captain wa DRC bi (Stella Mandago, na mratibu wa mashindano haya amesema kuwa Mashindano haya yanatarajia kushirikisha wanamichezo mbalimbali kutoka hapa nchini na  nje ya nchi pia, mashindano haya yatakuwa na washiriki watakao shiriki katika mbio za kilometa ishirini na moja nukta moja (21.1km) na kilomita kumi (10.0Km) yakiwa na lengo la kukuza na kuendeleza michezo ya riadha Tanzania na nje ya nchi ili kuwawezesha wanamichezo kufikia hatua za kimataifa na kuhimiza maisha yenye afya pia kudumisha mahusiano baina aya police na jamii.

 Klabu ya michezo ya Riadha “Dar Runing Club” inachukua fursa  hii kukukaribisha kushiriki mbio hizi zinazotarajiwa kuanza majira ya saa kumi na mbili asubuhi 12:00 katika viwanja tajwa hapo juu, aliongezea…..

Kutakuwa na zawadi kwa washindi kumi wa kwanza kwa wanawake na wanaume kama ifuatavyo kwa nusu marathoni ya km 21

 Mshindi wa kwanza  TZS 1,100,000
Mshindi wa pili   TZS 800,000
Mshindi wa tatu TZS 600,000
Mshindi wa nne TZS 350,000
Mshindi wa tano TZS 300,000
Mshindi wa sita TZS 250,000
Mshindi wa saba TZS 200,000
Mshindi wa nane TZS 1500,000
Mshindi wa tisa of TZS 100,000
Mshindi wa kumi of TZS 50,000

Kutakuwa pia na washindi wa 3 kwa mbio za Km 10 kama ifuatavyo

Mshindi wa Kwanza  TZS 500,000
Mshindi wa PIli  TZS 300,000
Mshindi wa tatu  TZS 200,000

ACHENI RUSHWA TUISAIDIE NCHI IPATE MAENDELEO -DK.MAGUFULI.

0
0
  Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli  akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa wizara Ujenzi katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza leo jijini Dar es Salaam,katika ufunguzi wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya ujenzi.
 Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi waliohudhuria katika  ufunguzi wa baraza hizo leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya waziri wa Ujenzi  pamoja na  Baraza la wafanyakazi wa wizara ya ujenzi. Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
WAZIRI wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli amewataka wafanyakazi katika wizara hiyo kuacha rushwa na badala yake wafanye kazi kwa weledi katika kusaidia nchi kuendelea katika ujenzi wa barabara.

Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo,amesema wizara hiyo imekuwa na mafanikio kutukana na wafanyakazi kujituma katika miradi mbalimbali.

Amesema madaraja na barabara  yaliyokuwa yakisumbua tangu  nchi ipate uhuru yamekamilika katika kipindi cha miaka mitano ya Rais Jakaya Kikwete na miradi mingine inaendelea ambayo Tanzania itakuwa nchi ya kuigwa katika kwa kuwa madaraja ya juu.

Aidha amesema Wizara ya ujenzi imevuka hata ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na kutekeleza miradi kwa asilimia 91.

Magufuli amesema katika sekta ya usafirisha kwa njia ya barabara ndio inabeba uchumi kutokana na kutegemea kwa asilimia 99.7 huku usafiri wa Reli,Maji na Anga ikiwa na asiliamia 0.7.

Magufuli amewataka wafanyakazi kuacha kulalamika kwani wanaweza kulalamika hata kama vitu vinavyofanywa ni vizuri na hiyo ndio umekuwa utamaduni wa watanzania.

Amesema kwa vivuko vilikuwa 15 lakini sasa viko 30 hali ambayo imerahisisha usafiri kwa wakazi wanaotumia vivuko na kufanya maeneo hayo kukua kiuchumi.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AREJEA NCHINI BAADA YA KUHUDHURIA MKUTANO WA DHARURA WA SADC, JIJINI HARARE, ZIMBABWE

0
0
 Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akimkabidhi Katibu Mtendaji wa SADC, Dkt Stargomena Tax, mfano wa funguo kama ishala ya makabidhiano ya Kituo cha Mafunzo ya Utunzaji Amani katika nchi za SADC, wakati wa Mkutano wa dharura uliofanyika jana Aprili 29, 2015 kwenye Hoteli ya Rainbow jijini Harare, Zimbabwe.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wenzake walioshiriki katika Mkutano wa dharura wa SADC, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo kwenye Hoteli ya Rainbow Jijini Harare, Zimbabwe, jana Aprili 29, 205. Makamu wa Rais amerejea nchini jana kuendelea na majukumu ya Kitaifa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Zimbabwe, huku akipunga mkono kuaga wakati akiondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Zimbabwe jana Aprili 29, 2015 kurejea nchini. Kushoto kwake ni mkewe mama Zakhia Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Adadi Rajab, wakati akiondoka kurejea nchini baada ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC, jijini Harare, Zimbabwe jana April, 29, 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na baadhi ya viongozi wenzake wakitoka kwenye ukumbi wa mkutano baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa dharura wa SADC jana.

Kufuatia makabidhiano haya, Chuo hiki sasa kitakuwa kinamilikiwa na SADC na matumizi yake yatahusisha vyombo na wataalamu mbalimbali wanaohusika na masuala ya utunzaji amani ndani ya nchi hizi, ili kupata mafunzo ya kuboresha kazi zao kufuatia migogoro kuwa mingi katika nchi mbalimbali Afrika. Picha na OMR

WAKUU WA TAASISI ZA TAKWIMU WA NCHI ZA AFRIKA WAKUTANA JIJINI DAR

0
0

th5Mtendaji Mkuu wa  Taasisi ya  Takwimu ya Bara la Afrika Bw. Joseph ILboudo akizungumza na watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu Kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala lililowahusisha wataalam na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi  za Afrika zinazozungumza lugha ya Kiingereza na Kifaransa leo jijini Dar es salaam.
th2Bw. Andry Andriantseheno kutoka UNECA akiongoza kongamano hilo la siku 2 la  watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu wa nchi za Afrika linalojadili masuala ya Uongozi na utawala na leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka Tanzania wenyeji wa mkutano huo.th3Baadhi ya watalaam na wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka katika nchi mbalimbali za Bara la Afrika wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa kongamano la Kimataifa kuhusu Uongozi na utawala linaloendelea jijini Dar es salaam.th4Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Takwimu Barani Afrika (AFRISTAT) pia mtaalam wa Takwimu kutoka nchini Cameroon Bw. Martin BALEPA akiwasilisha mada kuhusu namna nchi za Bara la Afrika zinavyoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kutumia takwimu sahihi.

IFIKAPO MACHI MWAKANI TATIZO LA UMEME JIJINI DAR ES SALAAM LITAKUWA HISTORIA

0
0
 Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
IFIKAPO machi mwakani tatizo la umeme jijini Dar es Salaam itakuwa historia  kutokana na kukamilika  kwa miundombinu  ya mitambo ya  umeme ifikapo machi mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene katika ziara ya  ukaguzi wa miradi ya umeme ya  Kurasini, Mbagala pamoja na Kinyerezi  jijini Dar es Salaam leo.

Ziara hiyo  iliyoanzia katika mitambo ya Umeme Wizarani hapo na kuelekea,Kurasini na Mbagala ikiwa na lengo la  kusogeza miundombinu ya umeme karibu na watumiaji wa umeme.

Simbachawene amesema kuwa  kuna miradi minne ambayo mpaka sasa inafanyiwa kazi kwa uhakika  inayotegemewa kusambaza Umeme kwa watumiaji bila kuwa n amatatizo ya  umeme.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  amesema kuwa matatizo mbalimbali ya  ununuzi wa Luku za umeme nayo yanafanyiwa kazi kwa  kuyahimiza makampuni nayoshirikiana na TANESCO katika uuzaji wa umeme ili waweze kuimarisha huduma hizo.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene akipewa maelekezo leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Felshesm Mramba  kuhusiana na uboreshaji wa  Mtambo wa umeme uliopo katika wizara ya Nishati na Madini.
Waziri wa Nishati na Madini,George Simbachawene  akikagua Mtambo wa umeme uliopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
 Mitammbo ya umeme iliyopo nyuma ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images