Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live

Mpiganaji Kyaloeichi Oko Kessy afariki dunia

$
0
0
Mwandishi mkongwe wa habari, Kyaloeichi Oko Kessy (62) amefariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Pugu jijini Dar es Salaam.

Mpwa wa marehemu Tumaini Msengi amesema hayo leo kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amekuwa akitibiwa katika hospitali mbalimbali za jijini Dar es Salaam hadi jana ambapo mauti yalimkuta.

Kabla hajaanza kuugua Kessy alikuwa mwandishi wa kujitegemea akiandika zaidi uchambuzi na makala katika vyombo mbalimbali vya habari nchini yakiwemo magazeti ya Motomoto,Shaba,Rai, na mengineyo mengi pia alikuwa ni mtunzi wa vitabu vya aina mbalimbali.

Msengi ameeleza kuwa marehemu ameacha watoto wawili na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa mdogo wake Chanika nje kidogo ya jiji na mazishi yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Marehemu ni mzaliwa wa kijiji cha Rosho Kilema mkoani Kilimanjaro.

onesho la Zari White party lazua gumzo jijini Dar,ni kuhusu kiingilio chake.!

$
0
0
 Watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando pamoja na Hudson Kamoga wa Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wakifanya mahojiano na Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na kwingineko Diamond Platnum akiwa na mchumba wake Zari the bosslady,kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo ya maisha yao na pia kuhusu onesho lao la Zari White Party wanalotarajia kulifanya usiku wa leo pale Mliman City,Jijini Dar.

Onesho hilo ambalo lilizua gumzo kila kona ya jiji la Dar likijulikana kwa jina la The White Party leo ndio kilele chake,kiingilio chake ukikisikia lazima usisimke,Kiingilio cha Onesho hilo kimevunja rekodi,haijawahi kutokea,kwa maana ya kwamba kiingilio kimepangwa kwa madaraja kuanzia Elfu hamsini,laki moja,milioni moja na milioni tatu,na huwezi amini tiketi sold out kitambo,imagine.

Katika mahojiano hayo Zari alieleza kuwa amefurahi kuonana na mtu kama Diamond,kijana anaejiamini,anaejituma na ni msanii anaefanya kazi zake kwa kujituma na juhudi kubwa,mwenye upendo na mapenzi ya kweli kutoka moyoni,alisema Zari huku akitoa tabasamu laini na kuongeza kuwa hajutii kumpata Diamond katika maisha yake.

Kwa upande wake Diamond nae alikiri wazi kumpenda Zari katika nyanja zote,amesema kwa sasa amekuwa na furaha kila wakati, kwa kuwa hivi karibuni anatarajia kupata mtoto wa kike kutoka kwa mchumba wake Zari. 
 Mtangazaji wa Clouds 360 Hudson Kamoga akimuuliza swali Bi.Zari ambae ni Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na kwingineko. 
 Diamond akirekebisha jambo kwa mpenzi wake
 Ooh..relax baby.
 Ooh Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha Zari The Bosslady kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia Clouds FM na Clouds TV.

Balozi Njoolay akabidhi barua ya pongezi kwa Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari

$
0
0
Tarehe 28 Aprili 2015 Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay, alimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete. 

Rais Mteule Jenerali Buhari alimshukuru Rais Kikwete kwa salamu hizo na kukiri kwamba alikwishapokea simu ya pongezi kutoka kwake mara tu baada ya matokeo kutangazwa. Wakati wa mazungumzo yake na Balozi Njoolay, Generali Buhari aliisifu Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu na kusema kuwa anaamini kwamba Tanzania itaendelea kuwa kitovu cha amani na utulivi Barani Afrika. Imetolewa na Ubalozi Tanzania, Abuja
Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay (kulia) akimkabidhi Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.
Balozi wa Tanzania, Nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais Mteule wa Nigeria Generali Mstaafu Muhammadu Buhari, mara baada ya kukabidhi barua ya pongezi toka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete

KILA LA KHERI YANGA - MALINZI

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini - TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CC) timuYoung Africans katika mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Etoile du Sahel utakaochezwa kesho nchini Tunisia.

Katika salamu zake Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa barani Afrika wanapaswa kupambana kuhakikisha wanasonga mbele katia hatua inayofuata.

Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi wa jumla kwa mchezo wa huo, atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI UKISHIRIKIANA NA PROIN PROMOTIONS WAZINDUA RASMI MANUNUZI YA FILAMU ZA KITANZANIA ONLINE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika, Karibiani na Pasifiki Balozi Dr Patrick Gomes (kushoto) akisalimiana Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala P baada ya kuzindua Utaratibu wa Uuzaji wa Filamu za Tanzania kwenye Mtandao. Uzinduzi huo humefanyika Makao Makuu ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki Jijini Brussels Ubeligiji.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[kushoto] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Rais Jakaya Kikwete apokea hati za Utambulisho za Mabalozi wa Nchi nne Ikulu Jijini Dar es salaam

WAFANYAKAZI WAHIMIZWA KUJITOKEA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwahamasisha wananchi wote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga Kura ili kuweza kupiga kura ya maoni na kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Hayo yamedhihirika leo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei 1, 2015 zilizofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wizara mbali mbali ikiwemo taasisi binafsi zilibeba mabango yenye ujumbe kuhamasisha wafanyakazi.
Mpaka sasa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura linaendelea vizuri katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 Wafanyakazi wa Mamlaka  ya anga nao  hawakuwa nyuma na mabango yao.
 Wafanyakazi wa Ofsi ya Rais - Ikulu...

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BODI YA MIKOPO YAANZA KUPOKEA MAOMBI YA MIKOPO KUTOKA KWA WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2015-2016

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Bw. George Nyatega

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo (Ijumaa, Mei 1, 2015) imetoa mwongozo kwa wanafunzi wahitaji wanaotarajia kuomba mikopo na ruzuku kwa ajili ya mwaka wa masomo 2015/2016 unaotarajiwa kuanza miezi michache ijayo.

Kwa mujibu wa mwongozo huo, ambao unapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz), waombaji wote wamepewa takribani miezi miwili kuwasilisha maombi yao kuanzia Jumatatu, Mei 4, 2015 hadi Jumanne, Juni 30, 2015.

Aidha, wanafunzi wote wahitaji wa mkopo na ruzuku wanapaswa kufanya na kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia mfumo maalum (Online Loans Application and Management System) ulioanzishwa na HESLB kwa ajili ya kupokea maombi hayo. Mfumo huo unapatikana kupitia tovuvi ya Bodi au kwa kufungua kiunganishi chake (http://olas.heslb.go.tz).

Pamoja na mambo mengine, mwongozo huo unafafanua kuwa waombaji wa mara ya kwanza (First Time Applicants) wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tshs 30,000/- kwa na kisha kutumia namba ya muamala (Transaction ID) kuingia katika mtandao na kuanza kujaza fomu za maombi.

“Waombaji wa mara ya kwanza wanapaswa kulipa ada ya maombi ya Tzs 30,000/- ambayo inalipwa mara moja tu na haitarudishwa kwa nia ya M-Pesa,” inasema sehemu ya mwongozo huo uloiotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo.

Aidha, mwongozo huo umesisitiza kuwa wanafunzi wenye mikopo na wanaoendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu hawapaswi kuwasilisha maombi tena.

Bodi imewasihi waombaji na wadau wengine kuusoma na kuuzingatia muongozo huo wakati waote wanapofanya na kuwasilisha maombi.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu. Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.

SHEREHE ZA MEI MOSI ZILIVYOFANA JIJINI DAR LEO

$
0
0
Bendi ya Jeshi la polisi wakiwa katika maandamano ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika katika uwanja vya uhuru jijini Dar es salaam leo.Picha zote na Avila Kakingo
Wafanyakazi wa Kampuni ya uchapishaji wa Magazeti ya Daily, Sunday News na Habari leo (TSN) wakipita na bango lao wakati wa kuadhimisha siku ya Wafanyakazi (Mei Dei), leo jijini Dar es salaam.
 Maandamano ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei mosi), yaliyofanyika katika uwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam leo.
Hawa ni wachama wa chama cha wafanyakazi mashambani na kilimo Tanzania tawi la TPAMU makao makuu wakiwa katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam leo.
 wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam wakiwa na kauli mbiu ya DOWUTA kauli moja na Nguvu imara,wakiwa katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkowa wa Dar es salaam, Mh. Said Meck Sadick akitoa hotuba katika kilele cha siku ya Wafanyakazi iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam.

JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 65

Rais Kikwete aongoza Sherehe za Mei Mosi jijini Mwanza leo

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa pamoja na viongozi wengine wakiimba wimbo wa mshikamano katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) iliyofanyika kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo.

Picha zaidi zitawajia baadae kidogo.

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO NA TUCTA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu toka kwa Gratian Mukoba, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wakati wa kilele cha Mei Mosi Uwanja wa CCM Kirumbna jijini Mwanza leo mei 1, 2015. Picha na IKULU

PRESS STATEMENT BY THE SECRETARY GENERAL OF THE EAST AFRICAN COMMUNITY ON THE SITUATION IN BURUNDI

$
0
0
The Secretary General of the East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera commends the Government of Burundi on the preparations undertaken so far towards the General Elections to be held in May, June and July 2015.

  The Community wishes the People of Burundi free, fair and peaceful elections and calls upon all friends of Burundi to offer their support to the success of the electoral process.

The Secretary General notes that Burundi has made substantial progress in establishing and maintaining peace and stability in the last decade and the forthcoming elections provide an opportunity to consolidate and enhance the country’s social and economic development.

He further recalls that on March 09, 2015 all political actors signed a code of good conduct in which they committed to refrain from pursuing violence in the electoral process.

The EAC notes that the attainment of peace and stability in Burundi amounts to peace and stability in the entire region and urges all regional and international stakeholders to actively engage in the attainment of these objectives.

The Secretary General notes with concern that some Barundi are seeking refuge in neighboring countries due to fear of election related violence. He commends Partner States that receive them and urges the International Community to offer support.

He further urges the Government of Burundi and all actors to ensure that the electoral process does not lead to humanitarian crisis.

The Secretary General calls upon the government of Burundi to continue with the dialogue process that brings together all key actors and stakeholders in Burundi with a view to deliberate on all key issues of potential impact to the realization of a peaceful, free and fair electoral process.

The Community reiterates its continued commitment in supporting the people of Burundi in the attainment of free and fair elections and promoting dialogue among all parties involved when called upon.

Makabidhiano ya Pampu ya Maji Kisima cha Kaburi Kikombe na Utilianaji Saini ya Mradi wa Uchimbaji Kisima Bomani Ukiwa na Thamani ya Shilingi milioni mia tatu

$
0
0
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akitiliana saini ya makubaliano ya Mrai wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya Bamani na Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akibadilishani Mikatabani ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya Bomanii Unguja Mradi huo utagharimu shilingi milioni Mia tatu, akibadilisha na Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Eng.Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini ya Makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima, mradi unaosimamiwa na Tanzania Youth Icon.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

BAN KI MOON SALUTES PRESIDENT KIKWETE

$
0
0
The following is a congratulatory message from Ban Ki Moon, Secretary General of the United Nations to H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania on the occasion of the Union Day which was cerebrated of 26 April 2015.

“You’re Excellency,

I am Pleased to offer you and the Government and people of the United Republic of Tanzania my warmest congratulations on the occasion of the Union.
   This year marks the 70th anniversary of the United Nations, offering a time for reflection, for renewing our commitment to our founding mission, and for redoubling our efforts towards peace, development and human rights for all.

Our efforts this year on sustainable development should make a significant and lasting contribution to the global good.

Every country has its unique characteristic and culture, and makes a unique contribution to our joint endeavors. I will continue to count on your country’s active engagement and leadership. Only by working in common cause will succeed in advancing our shared goals.”

Please accept, Excellency, the assurance of my highest consideration.

Ban Ki Moon, 
Secretary-General of the United Nations

ngoma azipendazo ankal

SHEREHE ZA MEIMOSI ZILIYOFANA MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
Wafanyakazi wa Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika  mjini Moshi. 
Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCLwakipita katikamaonesho ya Mei Mosi
Chuo cha wauguzi Kibosho pia walipita mbele ya mgeni rasmi kuonesha nini wanafanya katika sherehe hizo za Meio Mosi.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Dar es Salaam Charity Goat Races 2015

$
0
0
The 2015 Dar es Salaam Charity Goat Races will be held at The Green on Kenyatta Drive, Msasani Peninsula, on Saturday 30 May 2015.
Make sure you get your tickets for this year's raffle -the prizes are bollygood.

MTI WAPANDWA KATIKATI YA BARABARA JIJINI DAR

$
0
0
 Kamera yetu imeweza kuinasa taswira hii ya mti uliopandwa katikati ya Barabara ya Sokoine Drive karibu kabisa na lango kuu la kuingia kwenye Kanisa la KKKT Azania Front, Jijini Dar es salaam. hii inaonekana ni namna gani kampeni ya upandaji miti inavyokubalika hapa mjini.Picha na Othman Michuzi.

LUKU YAZUA GUMZO NCHINI

$
0
0
Pichani ni baadhi ya wakazi wa maeneo mbali mbali ya jiji la Dar, wakiwa kwenye foleni ya kununua umeme wa luku kwenye kituo cha Sayansi, Kijitonyama baada ya kupatwa na kwikwi kwa siku kadhaa zilizopita kwenye vituo vingine pamoja na kwenye mitandao ya simu.ila sasa Tanesco wametoa taarifa na kusema mambo yako mswano kwa sasa.

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) 
 TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA LUKU KWA BAADHI YA MAWAKALA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatoa ufafanuzi juu ya tatizo lililojitokeza kwa baadhi ya mawakala wa LUKU kushindwa kutoa huduma ya kuuza umeme. Hali hiyo inatokana na Kampuni ya Selcom ambaye ni wakala wa kuuza na kuyaunganisha baadhi ya makampuni ya simu kwa Tanesco kusitishiwa huduma kutokana na kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake kimkataba.

Wakati suala hili likiendelea kushughulikiwa na mamlaka zinazohusika tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, huduma zinaendelea kupatikana kupitia Kampuni ya MAXCOM katika Vituo mbalimbali, ATM za CRDB na NMB, NMB Mobile pamoja na ofisi zote za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) nchi nzima hadi siku ya Jumamosi na Jumapili na siku za Sikukukuu kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku.

Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.
Viewing all 110031 articles
Browse latest View live




Latest Images