Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 816 | 817 | (Page 818) | 819 | 820 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Katika shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora​ nchini Marekani imeifunga bao jirani zake timu ya Tanganyika USA bao 7-1.
   Kikosi cha timu ya Tanganyika 
  Tanganyika na Zanzibar kama ishara ya Muungano

  0 0

  Rais mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiingia chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya mjengo wa Ubalozi Washington, DC siku ya Ijumaa April 24, 2015 kulikokua na kikao cha Mabalozi wa heshima kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Liberata Mulamula kwa ajili kuongelea maswala mbalimbali zikiwemo changamoto za utalii na uwekezaji nchini Tanzania na jinsi gani ya kukabiliana nazo, mbali na Mabalozi hao wa heshima na marafiki zao wengine waliohudhuruia kikao hicho ambacho kilikua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano ni wawakilishi wa Taasisi za Diaspora za Kitanzania zinazopigana kusaidia maswala ya uwekezaji na Utalii kwa nchi yao Tanzania. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pia aliongozana na mkewe Mama Sitti Mwinyi.
  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Mabalozi wa heshima wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani.

  Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa  taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.

  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani anyoamtambulisha mbele ya mabalozi wa heshima na kwamba yeye Rais mstaafu ndiye aliyefanya mageuzi ya mfumo wa uchumi Tanzania tunaoendelea nao hivi sasa.

  Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na Mabalozi wa Heshima kuwashukuru kwa kuipenda na kuitangazaTanzania nchini Marekani na kuwaasa wasichoke kwa wao wamekua chachu ya maendeleo ya nchi aipendayo Tanzania.

  Mbalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi zinazotangaza Utalii na uwekezaji Tanzania wakimsuikiliza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
   Picha ya pamoja.
  Mayor De  Andre Windom wa mji wa Highland Park jimbo la Michigan akipata picha na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimuaga Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakati walipokua waiondoka baada ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kumaliza kufunga kikao cha Mabalozi wa Heshima Ubalozini hapo. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production. Picha zaidi BOFYA HAPA


  0 0


  Sitti Abbas Mtemvu, jina alilopewa kutoka kwa Bibi yake mzaa Baba, ambae nae wakati wa enzi zake alipewa jina hilo kutokana na umahiri wake wa kughani akifananishwa na msanii na mtunzi maarufu aliepata kutokea akiitwa Siti Binti Saad. Umahiri wa bibi ulimfanya kuwahi kushinda tuzo mbalimbali za sanaa wakati huo katika ukumbi maarufu wa burudani ulioitwa Anatoglou…….Nae alipozaliwa alipewa tunu, tunu ya jina la Sitti.

  Haya ni machache latika kitabu chake kipya kikiitwa – Chozi la Sitti……Kwa nini ukose kuwa sehemu ya HISTORIA?


  02.05.2015kuanzia saa moja usiku @Mlimani City Conference Hall…..Pata tiketi yako SASA: 0685 01 07 17. 


  0 0
 • 04/26/15--03:33: Article 16


 • 0 0

   Serikali kupitia Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imetiliana saini ya makubaliano na Kampuni ya UDA Rapid Transit kuendesha huduma ya usafiri ya mradi huo katika kipindi cha mpito. 
  Katika mkataba huo wa miaka miwili kampuni hiyo itatakiwa kununua mabasi 76 yenye urefu wa mita 12 na 18 ili kuanza kutoa huduma hiyo katika barabara za mradi jijini Dar es Salaam miezi minne kuanzia sasa. 
  Wakati DART ikiwakilishwa na Mtendaji Mkuu wake, Bi. Asteria Mlambo, kampuni hiyo iliwakilishwa na Bw.Robert Kisena na Bw. Sabri Mabruki na kushuhudiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki na viongozi wengine. 
  Bw. Kisena ni Mwenyekiti wa Simon Group Ltd, kampuni inayoendesha Usafiri Dar es Salaam (UDA). 
  Akizungumza katika halfa ya utiaji saini mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Bi. Ghasia alisema tukio hilo ni la kihistoria katika mchakato wa mfumo wa mabasi yaendayo haraka. 
  “Tumefikia hatua nzuri kwa nchi yetu kuwa serikali imeweza kushirikiana vyema na wadau wa usafiri kupata kampuni ya kuendesha huduma ya usafiri kipindi cha mpito,”alisema. 
  Alisema pamoja na kwamba mradi mzima haujakamilika, serikali imeamua kuanza na huduma ya mpito katika barabara ya Kimara hadi Kivukoni ambayo imekamilika kwa asilimia 90 na kuwa sasa kazi inayofanyika ni ya kuweka taa za barabarani. 
  Alifafanua kuwa usafiri katika barabara hiyo utakuwa wa uhakika na wa kisasa kwa vile basi moja la urefu wa mita 18 litakuwa na uwezo wa kubeba watu 150 wakati yale ya mita 12 yatakuwa na uwezo wa kubeba abiria 80 kila moja. Kampuni ya UDA Rapid Transit imeundwa na Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) na wamiliki wa daladala. 
  Waziri huyo aliitaka kampuni hiyo kuendelea kujenga mshikamano ili kupata uwezo wa kushindana katika zabuni ya kuendesha huduma ya kudumu ya mradi huo baada ya kipindi cha mpito kuisha. Mwakilishi wa Kampuni ya UDA Rapid Transit ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Daladala (DARCOBOA), Bw. Mabruki alisema wao wamejipanga kutoa huduma nzuri ya usafiri kipindi cha mpito. 
  “Tunaishukuru serikali kwa kutuwezesha wadau wa usafiri kufikia tulipo,” alisema. Alisisitiza kuwa katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa kampuni yao itakuwa imeleta mabasi mawili yenye sifa zinazotakiwa kwa ajili ya kufundishia madereva na hadi kufikia Septemba 15 mwaka huu mabasi yote 76 yatakuwa yameshaletwa. 
  Pia alisema kampuni yao inatarajia kujisajili katika soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) ili kuwapa fursa wananchi kununua hisa katika kampuni hiyo na kuwa sehemu ya wamiliki. 
  Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Sadiki alisema mradi huo ni mkubwa hivyo wananchi pamoja na madereva wanatakiwa kuyathamini basi hayo na kulinda miundombinu yake. Alikemea tabia ya udokozi kama ilivyojitokeza kwa taa za barabarani na mifuniko na vyuma mbalimbali vya mradi na wizi uliofanyika katika reli ya Kati wakati treni ya kisasa ilipoanza safari ya kwanza ya uzinduzi wake. 
   Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alisema huduma ya mabasi hayo katika kipindi cha mpito itapunguza adha ya usafiri katika jiji la Dar es Salaam ambapo hali imekuwa mbaya. 
  “Jiji hili linakua kwa haraka na mahitaji ya usafiri yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa,” alisema. 
  Alisema inakadiriwa kuwa hadi kufikia mwaka 2025 jiji hili litakuwa na wakazi milioni 11.5 hivyo uboreshaji miundombinu ni jambo lisiloepukika.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Hawa Ghasia akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kutiliana saini ya makubaliano ya kuanza kwa utekelezaji wa kipindi cha mpito cha huduma ya mabasi yaendayo haraka mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kampuni ya UDA Rapid Transit itaendesha mradi huo.  Kulia kwake ni Kamishna wa Kanda Maalumu ya Kipolisi Dar es Salaam, Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki.

   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bi. Asteria Mlambo (wa pili kushoto), na wawakilishi wa kampuni ya UDA Rapid Transit, Bw. Robert Kisena (wa tatu kulia) na Bw. Sabri Mabruki (wa kwanza kushoto) wakitiliana saini ya makubaliano ya kuanza kwa utekelezaji wa kipindi cha mpito cha huduma ya mabasi yaendayo haraka mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Pamoja na viongozi wengine wanaoshuhudia ni waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi.Hawa Ghasia (wa pili kushoto waliosimama); Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) na Kamishna wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia).

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Bi. Asteria Mlambo (wa pili kushoto) akibadilishana hati na mwawakilishi wa kampuni ya UDA Rapid Transit, Bw. Robert Kisena (wa pili kulia) kuhusu makubaliano ya kuanza kwa utekelezaji wa kipindi cha mpito cha huduma ya mabasi yaendayo haraka kuanzia mwezi wa tisa mwaka huu.  Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Kushoto ni muwakilishi mwingine wa kampuni hiyo, Bw. Sabri Mabruki.  


  0 0


  MNAMO TAREHE 24.04.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MTAA WA SOGEA KATIKA MJI MDOGO WA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA, VIJANA WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. MATHEW ANGANILE MWAFONGO @ RASI (27) MKAZI WA TUNDUMA NA MWENZAKE AITWAYE SALEHE TABULEI SICHALWE (22) MKAZI WA MAJENGO TUNDUMA WALIKAMATWA NA POLISI BAADA YA WANANCHI WA ENEO HILO KUWATILIA MASHAKA KUWA NI WAHALIFU, HII NI KUTOKANA NA MVAO WAO AMBAO ULIKUWA UMEFICHA SURA ZAO.


  VIJANA HAO WALIKUWA WAKITUMIA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.855 CDQ AINA YA T-BETTER NA WALIKUWA NA BEGI MOJA AMBALO MMOJA WA VIJANA HAO ALIKUWA AMELIVAA MGONGONI.


  POLISI WALIPOWAPEKUA KATIKA BEGI HILO WALIKUTA VISU VIWILI, MANATI MBILI, MAWE AROBAINI YA KURUSHWA KWA MANATI NA NATI NNE ZA KURUSHWA KWA MANATI, KOFIA MBILI ZA JESHI, BUTI JOZI MBILI, MIWANI MIKUBWA INAYOTUMIWA NA POLISI KATIKA MISAFARA, SHEEN-GUARD JOZI NNE (VIFAA MAALUM VYA KUVAA KWENYE MAGOTI NA VIWIKO VYA MIKONO), MAKOTI MAWILI MAREFU, VIFAA VYA KUFANYIA MAZOEZI YA “PUSH UP” NA KAMBA YA KUFANYIA MAZOEZI YA KURUKA.


  AIDHA KATIKA BEGI HILO KULIKUTWA PIA T-SHIRT MOJA YA CHADEMA, BENDERA MBILI NDOGO ZA CHADEMA, KITAMBAA/KILEMBA KIMOJA NA BARUA TATU ZA KUWATAMBULISHA WATUHUMIWA KWENDA KUTOA MAFUNZO KWA RED BRIGADE HUKO MAENEO YA KATA YA CHITETE, MSANGANO NA KAMSAMBA  WILAYANI MOMBA. 

  KATIKA KUHOJIWA, WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KUWA WANAENDA KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WA RED BRIGADE KATIKA KATA HIZO TAJWA HAPO JUU. KUTOKANA NA MATISHIO TULIYONAYO YA USALAMA NA VIASHIRIA VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UTULIVU NCHINI, WATUHUMIWA HAO WALIFIKISHWA POLISI MKOA KWA MAHOJIANO ZAIDI NA BAADA YA UCHUNGUZI, JALADA LITAPELEKWA KWA MWANASHERIA WA SERIKALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANAWASHUKURU WANANCHI KWA KUCHUKUA TAHADHARI ZA KIUSALAMA KWA KUTOA TAARIFA HARAKA. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA HARAKA KATIKA VYOMBO VYA USALAMA PALE WANAPOTILIA MASHAKA MTU/WATU AU VITENDO VYA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU ILI HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.


  Imesainiwa na:

  [AHMED Z. MSANGI – SACP]


  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  0 0

  On 25th April 2015, the Embassy of the People’s Republic of China in the United Republic of Tanzania holds the “Excellent Employee of Chinese Company Awards” ceremony, honoring the excellent Tanzanian and Chinese employees in Chinese companies for their outstanding performance. 
   H.E. Amb. Dr. LU Youqing, Ambassador of China to Tanzania, Mr. WU Xiaoyi, Senior Consultant, Mr. LI Xuhang, Political Councilor, Mr. LIU Dong, Cultural Councilor, Mr. Lin Zhiyong, Chief Economic & Commercial Representative and other staffs of Chinese embassy, Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga, Deputy Minister for Labor and Employment of Tanzania, Dr. Aggrey Mlimuka, Chairman of the Association of Tanzania Employers (ATE), all the awarded employees, representatives of Chinese companies and friends from both Chinese and Tanzanian media attended the ceremony. 
   There are 37 employees of Tanzania nationality won the Awards for long-term Dedication or Loyalty to their jobs, 25 employees of Chinese nationality won the Outstanding Contribution Awards and 3 Chinese companies won the Best Employer Awards. 
   Nowadays, the Tanzania-China economic cooperation is of unprecedented scale and reaches all fields. By the end of 2014, Chinese investment to Tanzania reached US$ 4 billion. More than 500 Chinese companies invested in Tanzania, created at least 150,000 jobs and there are about 300,000 people engaged in the work related with China-Tanzania bilateral trade. 
  In the vigorous bilateral economic and trade cooperation, a large number of employees from Tanzania and China have made outstanding achievements. They love and cherish their jobs and enjoy personal progress along with the Chinese companies’ development. 
  Some of them have been working in Chinese companies for 10 to 20 years, some even 30 years. Some of them regard Chinese company as their home and the whole family work and move with the projects.
  In some Tanzania families, children dreamed to work for Chinese companies as what their parents do. The employees working in Chinese companies not only obtained knowledge and techniques but also enjoyed life quality improvement. Many of them have become technical backbone or senior management personnel of Chinese companies and are undertaking the responsibility of training other local staffs. 
  They are playing an important role to the Tanzania-China economic cooperation. The Embassy of China in Tanzania hopes that everyone could learn from the award winners and produce positive energy to push forward the process of Tanzania-China economic cooperation, industrial tie-in and capacity relocation. Let’s carry on and disseminate Tanzania-China Friendship, engage in and promote our economic cooperation, and write the new chapter of Tanzania-China comprehensive and cooperative partnership featuring mutual benefit and win-win outcome.
  H.E. Amb. Dr. LU Youqing, Ambassador of China to Tanzania, presents to one of the reciepients the Excellent Employee of Chinese Company Awards
  Group photo after the presentations:  H.E. Amb. Dr. LU Youqing, Ambassador of China to Tanzania, Mr. WU Xiaoyi, Senior Consultant, Mr. LI Xuhang, Political Councilor, Mr. LIU Dong, Cultural Councilor, Mr. Lin Zhiyong, Chief Economic & Commercial Representative and other staff of Chinese embassy, Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga, Deputy Minister for Labor and Employment of Tanzania, Dr. Aggrey Mlimuka, Chairman of the Association of Tanzania Employers (ATE), all the awarded employees,
   
  H.E. Amb. Dr. LU Youqing, Ambassador of China to Tanzania, Mr. WU Xiaoyi, Senior Consultant, Mr. LI Xuhang, Political Councilor, Mr. LIU Dong, Cultural Councilor, Mr. Lin Zhiyong, Chief Economic & Commercial Representative, Hon. Dr. Milton Makongoro Mahanga, Deputy Minister for Labor and Employment of Tanzania, Dr. Aggrey Mlimuka, Chairman of the Association of Tanzania Employers (ATE), with  the awarded employees, 

  0 0

   Hatimaye Washindi wa shindano la Shika Ndinga la 93.7 EFM wamepatikana baada ya mchuano mkali uliofanyika jana Aprili 25, 2015 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe jijini Dar es salaam. 
   Fainali hiyo iliwahusisha washiriki 10 kutoka katika wilaya zote tatu za mkoa wa Dar-es-salaam watano kati yao wakiwa wanawake watano wakiwa ni wanaume. 
  Shindano hilo lilihudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akiwa kama mgeni rasmi, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na Mstahiki Naibu Meya wa wilaya ya Temeke Mhe. Juma mkenga. Mhe Sadik alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa vijana na kuinua hali zao za uchumi.
  Mkuu wa Mkoa huyo pia aliwaasa washindi kutumia ndinga walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa upande wake Mhe. Paul Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza katika mashindano kama haya maana zaidi ya kuburudisha yanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti. 
  Washindi waliojishindia ndinga kwa upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka wilaya ya Temeke mwenye umri wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya ya Ilala mwenye umri wa miak 26 ambao kwa pamoja wamesema shindano halikuwa rahisi na wanafuraha kubwa ya kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao
  Aidha wameishukuru redio ya 93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali wasikilizaji wake.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akiongea na Dennis Ssebo wa 97.3 EFM kwenye hafla hiyo jana katika uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda 
  Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa likioneshwa
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimkabidhi ndinga yake mshindi  Stella Joseph kutoka wilaya ya Ilala
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadik akimpongeza mshindi Gabriel Robert kutoka wilaya ya Temeke bada ya kumkabidhi ndinga 
  Mojawapo ya ndiga zilizoshindaniwa

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipunga mkono kuwasalimia wananchi wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es salaam, leo  kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akienelea kuwapungia mkono kwa furaha kuwasalimia wananchi
   Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwa na Viongozi wengine wakisimama kutoa heshima wakati ikipigwa mizinga 21, uwanjani hapo. 

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akikagua gwaride la heshima, wakati wa sherehe za Maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR

  0 0


  Habari zilizotujia hivi punde zinasema Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam. 

  Kwa mujibu wa taarifa za kifamilia, mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam siku itayotajwa kesho na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.

  Msiba upo nyumbani kwa marehemu Chang'ombe jirani na TCC Club jijini Dar es salaam.

  Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa Nelson Mandela.
  Mjane wa marehemu Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita, Ngeme Mbita (katikati) akiwa na waombolezaji wengine nyumbani kwa marehemu, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo.  Brigedia Mbita amefariki leo katika Hospitali ya Lugalo. (Picha na Francis Dande).


  0 0

  Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni yenye makao yake nchini ujerumani inawatakia kila la heri watanzania wote walio nyumbani na nje ,Heri ba na baraka, Amani,Mshikamano na Upendo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamuhuri yetu ya muungano wa Tanzania. Tudumishe Muungano wetu daima millele. Mungu Ibaraki Tanzania . 

  sherekea muungano kwa muziki at www.ngoma-africa.com


  0 0

   Mandhari ya nje ya Hoteli ya Kisasa ya Shangani Hotel Apartments iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego usiku jana mjini Mtwara. Pia ulizinduliwa Mgahawa wa kisasa ambapo wageni waalikwa walifaidi kula chakula cha usiku kilichopikwa na wapishi waliobobea kwa mapishi yenye vionjo vya kila aina.

  Wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo itakayozidi kuongeza hadhi ya Mji wa Mtwara ni, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara, Seleman Mtalika na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Fatma S. Ally.Pia waliwepo wageni wengine kutoka taasisi mbalimbali pamoja na wafanyabishara. Hoteli hiyo inamilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji Akida Zidikheri.
  Akida Zidikheri (kushoto) mmiliki wa Shangani Hotel Apartments na . Said Aboud (kulia)pamoja na Mstahiki Mayor wa Manispaa ya Mtwara, Selemani Mtalika ndani ya mgahawa huo wa kisasa uliopo katika hoteli hiyo.
   Mmiliki wa Shangani Hotel Apartments, Akida Zidikheri wakiwa ndani ya moja ya Apartments pamoja naMkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego (kulia), na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara  Fatma S. Ally (kushoto).

  0 0
 • 04/26/15--13:48: YALE YALEEEE.......
 •  Hivi ni lini uendeshaji wa aina hii utasitishwa hapa nchini, Maana haiwezekani mtu anaendesha gari iliyobeba abiria na anaamua kuyapita mabari mengine na ili hali mbele kuna magari mengine yanakuja. huu ni uzembe wa hali ya juu na unapaswa kukomeshwa kabisa. hii ni jioni ya leo katika Kijiji cha Vikindu, Mkoani Pwani na hiyo gari Namba zake za usajili ni T 386 AVR, Toyota Hiace.
  Sasa ona anavyolazimisha kurudi kwenye nyia husika.

  0 0


  0 0

  Na Felix Mwagara, Mishamo

  ZOEZI la ugawaji wa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa waliokuwa Wakimbizi wa Burundi zaidi ya 152,572 walioingia nchini mwaka 1972 linatarajiwa kumalizika wiki hii katika Makazi ya Mishamo mkoani Katavi.

  Wakimbizi hao ambao waliomba uraia wa Tanzania mwaka 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, sasa watakuwa raia halali wa Tanzania kwa kuwa na uwezo wa kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo za Udiwani na Ubunge.

  Akizungumza wakati wa ugawaji wa vyeti hivyo, Mkuu wa Makazi ya Mishamo, Fredrick Nisajile alisema ugawaji wa vyeti hivyo ulianza Novemba 24 mwaka jana, katika Makazi ya Katumba yaliyopo mkoani Katavi, ambapo watu 56,554 walipewa vyeti vya uraia na baadaye zoezi la ugawaji likahamia katika Makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora, ambapo watu 43,453 tayari wamepewa vyeti hivyo.

  Nisajile alisema katika makazi yake ya Mishamo ambapo ugawaji wa vyeti hivyo unaendelea na unatarajiwa kumalizika ifikapo Aprili 30 mwaka huu, ambapo katika makazi hayo zaidi ya raia wapya 52,565 wanatarajiwa kupewa vyeti vyao.

  “Mpaka leo hii (jana) katika makazi haya ya Mishamo kama unavyoshuhudia ndugu mwandishi umati wa watu wakizidi kuingia katika kituo hiki, mpaka sasa tayari tumegawa vyeti 131,351 kwa raia hawa wapya, na tunatarajia ifikapo wiki ijayo Aprili 30 tutakuwa tumemaliza ugawaji wa vyeti hivi katika vijiji vyote, na zaidi ya raia wapya 152,572 katika Makazi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo watakuwa wamepewa vyeti hivi na zoezi litakuwa limekamilika” alisema Nisajile.

  Alisema Serikali ndiyo inatoa vyeti hivyo kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), ambapo wote kwa pamoja wamejipanga kikamilifu ili ugawaji huo unamalizika salama na kwa umakini wa hali ya juu.

  Hata hivyo, Nisajile alisema kuwa, makazi yake ya Mishamo yana vijiji 16, hivyo kabla ya kuanza kugawa vyeti hivyo, huwa wanatoa elimu kwa kuwahamasisha wakazi wa kijiji ambacho kinatarajia siku ya pili yake kwenda kugawiwa vyeti hivyo. Alisema katika uhamasishaji huo, yeye Mkuu wa Makazi anaambatana na Maafisa Uhamiaji na UNHCR ili waweze kuhamasisha mambo mbalimbali kuhusiana na umuhimu wa vyeti hivyo.

  Aliongeza kuwa, vyeti hivyo vinatolewa kwa mtu mmoja mmoja ambapo raia mpya anatakiwa aje na karatasi ya uthibitisho wa picha za wanafamilia ili kuiwezesha Serikali na UNHCR kutambua kabla ya kutoa cheti kwa wahusika hao na kila anayepewa cheti hicho anatakiwa kusaini.

  Zoezi la ugawaji wa vyeti vya uraia kwa raia hao wapya lilikuwa la miezi mitano, ambapo lilianza Novemba 24 mwaka 2014, na Aprili 30 wiki hii, linatarajiwa kukamilika.
  Afisa Uhakiki, Neema Chilipweli (kushoto) akiihakiki familia ya Yohanna Bukuru (watatu kulia), pamoja na mkewe na watoto wao sita kutoka Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda Vijijini, Mkoa wa Katavi, ikiwa ni hatua ya awali ya uhakiki ili familia hiyo iweze kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania. Zaidi ya watu 152,572 katika Makazi ya Mishamo, Katumba na Ulyankulu waliokuwa wakimbizi wa Burundi wa mwaka 1972 walioomba uraia 2008 na kupewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2010, wanastahili kupokea vyeti hivyo kama raia wapya wa Tanzania. Hata hivyo, Makazi ya Katumba na Ulyakulu tayari wamekamilisha zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo, na sasa ni zamu ya raia wapya wa Makazi ya Mishamo ambapo wiki hii zoezi la ugawaji wa vyeti hivyo nchini, linatarajiwa kukamilika. Serikali ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) katika ugawaji wa vyeti hiyo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti) akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Usalama wa Hotel ya New Afrika Hotel ya Jijini Dar es Salaam, Bw. Isack Kabugu kuhusu hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo ambayo ilileta athari katika majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo Jumapili April 26, 2015.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel (mwenye koti) akijionea athari mbalimbali zilizosababishwa na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo hatua iliyosababisha uharibifu wa majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo Jumapili April 26, 2015.
  Mafundi mitambo wa katika hoteli ya New Afrika ya Jijini Ddar es Salaam akiangalia athari zilizotokana na hitilafu ya kiufundi iliyotokea katika mtungi wa kuhifadhi moto katika Hoteli hiyo ambayo ilileta athari katika majengo ya ofisi zilizopo jirani na hoteli hiyo ikiwemo ofisi ya Idara ya Habari na Ofisi ya Bodi ya Filamu Tanzania zilizopo chini ya Wizara hiyo Jumapili April 26, 2015. (Picha na MAELEZO)

  0 0
 • 04/26/15--14:47: WASICHANA WERUWERU WAASWA
 • Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa pili kutoka kushoto) akimkabidhi chetu cha uhitimu mmoja wa wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo. Wengine ni Wajumbe wa Bodi ya Shule.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru Rosalia Tarimo (wa pili kutoka kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Akifuatilia ni Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa kwanza kushoto) ambaye pia alikuwa ni Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo. 
  Ofisa Mkuu wa Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (wa tatu kutoka kushoto – mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru na wageni wengine waalikwa wakati wa mapokezi yake kama Mgeni Rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Ofisa huyo aliwakilisha wafanyakazi wa Vodacom kupitia Vodacom Foundation ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kusaidia wasichana katika elimu ambapo kampuni hiyo pia ilitoa msaada wa mashine ya kutoa nakala na kuchapisha nyaraka kwa shule hiyo.


  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiwahutubia wakazi wa Mtaa wa Kilimahewa Juu iliyopo uliopo Kata ya Wazo Dar es Salaam jana, alipofika kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu muda mrefu.
   DC Makonda akizungumza na viongozi wa Manispaa ya Kinondoni na wakata ya Wazo kuhusu mgogoro huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na   Bashir  Yakub.

  Kifungu  cha 18  cha  Sheria  ya  Kanuni  za  adhabu  sura  ya  16  kimeeleza  hatua  ya  mtu  kujikinga  mwenyewe,  kumkinga  mwenzake  ,  mali  yake  mwenyewe  na  mali  ya  mwenzake. Kujikinga( defence)  maana  yake  ni  kujilinda  au  kujitetea  inapokwa  imekutokea  dharula   ya  kuvamiwa  na  mtu  au  watu  waovu. Uovu  ni  uovu  si  lazima  awe  mwizi .  Hata  mtu  asiyekuwa  mwizi  lakini  amekuvamia  kwa  nia  ovu iwe  nyumbani, kazini  au  sehemu  nyingine  yoyote  basi   ni  adui   unayepaswa  kujikinga  naye.

  1.KUJIKINGA  NI  HAKI  YA  KILA  MTU.

  Haki  ya  kujikinga  na  adui  si  tu  imeelezwa  katika  kifungu  nilichotaja  bali  pia  ni  haki  ya  msingi  ya  kikatiba.  Haki hii  pia  huingia  katika  zile  haki  ambazo  huitwa  haki  za  kuzaliwa ( in born right).  Haki  za  kuzaliwa  ni  zile  haki  ambazo  sio  lazima  ziwe  zimeandikwa  katika sheria  fulani  halafu  ndipo  mtu  azitekeleze .  Ni  haki  ambazo  hata  kama  hazikuandikwa  popote   mtu  ni  lazima  azipate  tu. Kwa  mfano  haki  ya  kula  au  ya  kuishi. 

  Haihitaji  iwe  imeandikwa  popote  katika  katiba  au  penginepo  ili   uweze  kula  au kuishi.  Ni  kitu  ambacho  hutokea  moja  kwa  moja( automatic). Ni  kitu  ambacho  huandikwa  kama  haki  katika  sheria  lakini  hata  kisingeandikwa  ilikuwa  ni  lazima  kiwepo. Halikadhalika   ndivyo  ilivyo  katika  haki   ya  kujikinga ( defence) kwani  haihitaji kuwa  imeandikwa popote   kuwa  mtu  akikuvamia  kukudhuru   ujikinge  naye.  Inakuja  tu  moja  kwa  moja  mtu  akitaka  kukudhuru  ni  lazima  ujilinde  kwa  kutafuta  namna  ya  kujiepusha  naye. 

  2. INARUHUSIWA  KUJIKINGA  HADI  KUUA.

  Kifungu  cha  18c cha  sheria  hiyohiyo  ya  kanuni  za  adhabu   kinasema  kuwa   mtu  anaweza  kujikinga  mwenyewe, mali  yake  , kumkinga  mtu  mwingine, mali  ya  mtu mwingine  dhidi  ya  hatari   au  shambulio  mpaka  kufikia  hatua  ya  kuua  au  kusababaisha  madhara  makubwa  ya  kimwili. Madhara  makubwa  ya  kimwili  ni  pamoja  na  kukata  kiungo  cha  mtu  mfano  mguu,  mkono,  au  kusababnisha  madhara  mengine  kama  kusababisha  kidonda  kikubwa  na   hali  nyingine  zote zinazofanana  na  hizo.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Umoja wa Watanzania wanaofanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(WATJAM)yenye makao yake makuu jijini Arusha katika kuhadhimisha Sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo wametembelea hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru kufanya usafi na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 3.7 milioni

  Mwenyekiti wa umoja huo,James Kuleiye amesema wao kama watanzania wameona waitumie siku ya leo kufanya shughuli za kijamii na kuwa karibu na taasisi hiyo kwa lengo kujenga mahusiano mema.

  Misaada iliyotolewa ni Maji maluumu ya wagonjwa ,Mashuka 50,Vifaa tiba vya kupima mapigo ya moyo(Presha) na vifaa mbalimbali vya usafi.

  Mganga Mkuu wa hospitali hiyo,Aziz Msuya ameshukuru umoja huo kwa moyo wa uzalendo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo licha ya kueleza changamoto inayoikabili hospitali hiyo ya kutokuwa na Wodi ya kuwalaza wagonjwa waliofanyiwa Upasuaji.

  Amesema vifaa hivyo vitakua msaada mkubwa kuboresha afya ya mama na mtoto kwani kila mwezi jumla ya wanawake 300 hujifungua huku 50 wakijifungua kwa upasuaji.
  Umoja wa Watanzania wanaofanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(WATJAM)yenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwasili kwenye hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru kufanya usafi na kutoa misaada mbalimbali kwaajili ya kuadhimisha Siku kuu ya Muungano wa Tanzania leo.
  Watanzania wanaofanyakazi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)yenye makao yake makuu jijini Arusha wakifanya usafi kuzunguka mazingira ya hospitali hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Mganga Mkuu wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru,Arusha,Dk Azizi Msuya(kushoto)akipokea sehemu ya zawadi zilizotolewa na Wafanyakazi wa EAC ambao ni Watanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa umoja huo,James Kuleiye yenye thamani ya Sh.3.7 milioni.


older | 1 | .... | 816 | 817 | (Page 818) | 819 | 820 | .... | 3348 | newer