Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 817 | 818 | (Page 819) | 820 | 821 | .... | 3282 | newer

  0 0

   Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki akisalimiana na baadhi ya Wakufunzi wa chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi.
   Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahmani Kaniki (kushoto) akiwasili katika chuo cha Polisi Moshi (CCP) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua mafunzo yanayoendelea chuoni hapo.Katikati ni Mkuu wa Chuo hicho, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi na Mkuu wa Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Omar Rashid (Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Moshi.
  Wakufunzi wa Chuo cha Polisi Moshi (CCP) wametakiwa kuendelea kutoa mafunzo kwa weledi ili kuweza kupata askari bora ambao watashirikiana na jamii katika kupambana na uhalifu hasa katika kipindi hiki ambapo kumeibuka uhalifu mpya kwa njia ya mitandao na unaovuka mipaka.
  Wito huo umetolewa jana mjini moshi na Naibu Inspekta Jenerali wa  Polisi, Abdulrahman Kaniki wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi chuoni hapo ambapo alizungumza na wakufunzi hao na kuweka mikakati mbalilmbali ya kuboresha mafunzo katika chuo hicho.
  Naibu IGP Kaniki alisema, askari wakipata mafunzo bora wataongeza mbinu zitakazowezesha kukabiliana na  uhalifu huo na hivyo kuendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao kwa kushirikiana na jamii ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
  “Ili kuhakikisha kwamba raia wa Tanzania na mali zao wanalindwa ipasavyo, Jeshi la Polisi hatuna budi kuendelea kubuni mbinu mpya za kukabiliana na uhalifu wa kila aina unaobadilika mara kwa mara na hilo linawezekana kwa kuendelea kuwapatia askari wetu mafunzo yenye viwango vya kupambana na uhalifu unaokua kwa kasi”alisema Kaniki.
  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Polisi moshi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Matanga Mbushi alisema wanaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa mafunzo wanayotoa yanalenga katika mitaala ambayo wamekuwa wakiiboresha mara kwa mara ili kuendana na wakati kulingana na mazingira ya uhalifu unaotokea katika jamii.
  Alisema, mbinu za uhalifu zimekuwa zikibadilika kila siku hivyo, na wao kama chuo wamejikita kuhakikisha kuwa askari wanaopita katika chuo hicho wanazipata mbinu mpya na hivyo kuwa zaidi ya wahalifu ili waweze kupambana nao.

  0 0


    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na washiriki wa Kongamano la  Takwimu barani Afrika baada ya kufungua mkutano wa kwenye Hoteli ya Firaffe Ocean View jijini Dar es salaam.  Kushoto kwake  ni Mkurugenzi wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa, Dr. Albina Chuwa,  kulia  ni Irena Krizman kutoka  Slovenia na wapili kulia ni  Pali Lehohla kutoka Afrika ya kusini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


   Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kulia ni  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah. (Picha na Francis Dande)
   Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kusaidia matibabu ya watoto 400 wenye matatizo ya kupinda miguu. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans 
    Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji wa dola 100,000 ili kuisaidia matibabu ya watoto wenye matatizo ya kupinda miguu katika mpango wake wa kufanikisha matibabu ya watoto 400 wanaosumbuliwa na ugonjwa  huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0
 • 04/27/15--05:23: SHUKURANI

 • FAMILIA YA MAREHEMU MZEE ADAM ABDALLAH WA BOKO KWA MPEMBA DAR-ES-SALAAM,WANAPENDA KUTOA SHUKRANI ZAO ZA DHATI KWA NDUGU,JAMAA,MAJIRANI WOTE WA BOKO KWA MSAADA WA HALI NA MALI WALIOUTOA KATIKA KIPINDI KIGUMU CHA MSIBA WA NDUGU YAO -IBRAHIM ADAM ABDALLAH ULIOTOKEA TAREHE 18-4-2015 NA KUZIKWA TAREHE 19-4-2015 KATIKA MAKABURI YA KISUTU.

  SHUKRANI ZA PEKEE KWA MADAKTARI WA HOSPITALI YA MWANANYAMALA WALIOTOA MSAADA WA KUJARIBU KUOKOA MAISHA YAKE,WAUMINI NA MASHEIKH WA MSIKITI WA BOKO NA MSIKITI WA SHADHIR KWA KUMUOMBEA MAREHEMU.

  TUNAWASHUKURUNI SANA KWA  YOTE.

  AROBAINI YA MAREHEMU IBRAHIM ADAM ABDALLAH ITAFANYIKA TAREHE 30 MAY 2015 SAA SABA MCHANA LUMUMBA/AMANI NHC FLAT.APT NO 202.

  INNA LILLAHI WA INNLILLAHI RAJIUN.
  RIP MY YOUNG BROTHER.

  0 0

  Wakazi wa Mloganzila wa Kata ya Kwembe  wilayani Kinondoni wakiwa katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam leo.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia Madai  kwa  Wakazi  wa Mloganzila –Kwembe,Fedrick Schone akitoa malalamiko yao katika Ofisi za wizara ya  Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushoto ni Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki akisikiliza madai ya wananchi wao leo jijini Dar es Salaam. 
   Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki  akizungumza na baadhi ya wananchi  katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi juu ya wananchi walioenda kudai fidia za maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA)

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WAKAZI wa Mloganzila wa Kata ya Kwembe  wilayani Kinondoni leo wameandamana katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,jijini Dar es Salaam.

  Kuandamana huko kumetokana na serikali kuchelewa kutoa majibu juu ya fidia ya ardhi pamoja na mapunjo ya fidia yaliyotokana na  nyumba ,mashamba katika eneo hilo lililochukuwa na mradi huo.

   Maandamano yalikuwa ya aina yake kutokana na kuwa na misafara ya magari matatu na kuingia mmoja moja na kisha kujaa katika mlango mkuu wa wizara hiyo na kuanza kupiga kelele kwa kile walichodai hatima yao ya kulipwa ili waendelee na maisha yao.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia Madai  kwa  Wakazi  wa Mloganzila –Kwembe ,Fedrick Schone kufika kwa wanachi katika ofisi ni katokana na kuwepo kwa kalenda nyingi zisisotoa suluhu ya mgogoro wao wa madai.

  Amesema  kamati yao imekosa kuaminika kutokana na kupeleka majibu ambayo yamekuwa yakiibua maswali mengi kwa wananchi waliochuliwa maeneo yao.

  Akizungumza  wananchi hao,Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki amesema madai yao watashughulikia ndani ya siku saba kwa kwenda kuzungumza na wananchi hao baada ya kujadili na Waziri wake.
  Amesema kuwa suala hilo limefika na kudai anawapa barua juu ya utekelezaji ndani katika kuweza kufikia suluhu na kuwataka kuondoa wasisi wa jambo hilo.

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi leo amefungua kozi ya walimu wakufunzi wa mpira wa miguu chini inayofanyika katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

  Malinzi amesema kozi hiyo ni muhimu kwa mustakabali wa soka la Tanzania, walimu wakufunzi watasaidia kuwafundisha walimu wengine wa mpira, ili kuweza kufundisha mpira kwa watoto wadogo ambao ndio hazina ya baadae.

  Malengo ya TFF ni kuhakikisha timu ya vijana ya U17 inafuzu kwa fainali za Mataifa Afrika 2017 nchini Madagscar, na baadae kuwa na kikosi bora wakati tunapotarajia kuwa wenyeji wa fainali za U17 Afrika mwaka 2019 "alisema Malinzi".

  TFF ina program mbili za kuwaandaa vijana wenye umri chini ya miaka 13, 15 kwa kuwaweka kambini na kucheza michezo ya kirafiki mikoani na kufanya ziara katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Bostwana na Afrika Kusini.

  Aidha Malinzi amewaomba walimu wakufunzi kuwa karibu na makocha wa timu za Taifa, na kuwapa ushauri makocha hao ili kuweza kuwasaidia katika kuboresha vikosi vyao na maendeleo ya soka la Tanzania kwa ujumla.

  Naye Rais wa CECAFA na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodgar Tenga alimshukuru Malinzi kwa kuweza kufungua kozi hiyo ambayo inawakutansisha walimu wakufunzi wa mpira miguu kutoka sehemu mbalimbali nchini.

   Akiongea kwa niaba wa walimu wakufunzi, Dr. Mshindo Msolla alisema wanaishukuru TFF kwa kuandaa kozi na kuomba kuendelea kushirikishwa katika mipango mbalimbali ya soka nchini ikiwa ni pamoja na kutambulika kuanzia katika ngazi za juu mpaka katika maeneo waliyopo.

  Kozi hiyoiliyoanza leo jumatatu itamalizika Mei 2 mwaka huu, inawajumuisha walimu 18, wenye leseni A, B na C za CAF kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar.

   IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

    Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha ACT-Tanzania na kuwa ACT-Wazalendo bila ya kufuata utaratibu. Kulia ni Katibu Muenezi wa chama hicho, Fredy Kisena na Katibu Mkuu wa chama hicho, Leopold Mahona.
   Viongozi wa chama hicho wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto Kaimu Katibu wa chama hicho, mkoa wa Dar es Salaam, Peter Katunka, Kaimu Katibu Mkuu, Leopold Mahona, Mwenyekiti, Kadawi Lucas Limbu na Katibu Muenezi Fredy Kisena.
    Mwenyekiti wa ACT-Tanzania,  Lucas Kadawi Limbu.
   Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.(Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)

  Na Chalila Kibuda

  MWENYEKITI wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas Kadawi Limbu amemlalamkia Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu Francis Mtungi kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la chama hicho na kuwa ACT-Wazalendo.

  Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam loe na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.

  "Tunashangazwa na jaji Mtungi kwa kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata taratibu huku akijua fika kuna kesi ya msingi ipo mahakamani kuhusu mwenendo wa chama hicho. Alisema Limbu

  Aliongeza kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama hicho kwani haiwezekani na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.

  "ACT-Tanzania ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.

  Alisema ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu na kumpatia mtu madaraka ya kiongozi mkuu na kubadilisha jina lake huku msajili wa vyama akishuhudia.

  Alisema msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho kilichobadilishwa jina akiwa katika ziara ya kichama mikoani aliyoianza tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ACT-Wazalendo.

  Limbu alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia mbaya na chama cha ATC-Tanzania.

  (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

  0 0

     Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO Ajijini Dar es Salaam leo kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni  Afisa masoko  wa NHBRA Zubeda Salum.
    Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina  ya kwanza ya kigae  cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa kulia ni  Afisa masoko  wa NHBRA Zubeda Salum.
   Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akionyesha aina  ya pili ya kigae  cha kupaulia nyumba,kushoto ni kaimu afisa Habari wa NHBRA Frimin Lyakurwa.
    Baadhi ya wandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa kuonyesha aina mbalimbali za vigae vinavyoweza kutengenezwa na kila mwananchi hapa nchini katika ukumbi wa Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

  Na Avila Kakingo,Globu ya Jami.
  WAKALA Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA) wamegundua njia rahisi ya kuboresha makazi kwa kutumia vigae kwa gharama nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kuzimudu. 

  Hayo yamesemwa na  Meneja  wa Utafiti na Maendeleo wa NHBRA Injinia Elias Kwemana akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa habari MAELEZO jijini Dar es Salaam leo. Kwemana amesema kuwa utengenezaji wa vigae hivyo ni rahisi na gharama hafuu kwani bidhaa zote za kutengeneza vigae hivyo zinapatikana hapa hapa  nchini.

  Hifaa hivyo  vinavyotumika kutengenezea vigae hivyo ni mchanga sementi na  nyuzi za katani bidhaa  hizo zote zinapatikana hapahapa nchini, ikiwa kuna  mashine inayotumika kushindilia mchanga uliochanganywa na sementi nayo ni gharama nafuu ukilinganisha na faida zinazopatikana.

  Kwemana amesema kuwa  njia ya kutengeneza vigae hivyo vitasaidia  kutumika kama njia nyingine ya kupaua nyumba zetu ambapo vigae hivyo huu kaa muda mrefu kuliko kutumia Nyasi au Bati.

  0 0

   Wanajeshi wa nchini Nepal wakiendelea kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika tetemeko la ardhi  mjini Kathmand nchini Nepal.
   Baadhi ya miili ya watu waliopoteza maisha katika 
  katika tetemeko la ardhi  mjini Kathmand nchini Nepal.
  Kwa msaada wa mtandao
  MAMLAKA ya nchini Nepal imesema kuwa zaidi ya watu 3300 wamesemekana kufairki dunia kutokana na Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea jumamosi katika mji wa Kathmandu nchini  humo.
  Waokoaji wanchi hiyo wamesema wanaendelea kuchunguza zaidi kwa kuyafikia maeneo ya mashamba mbalimbali katika mji Kathmandu, inawezekana Idadi ya watu waliopoteza maisha kuwa kubwa zaidi jinsi muda unavyozidi kwenda.
  Mamia ya watu wanaoishi karibu na milima inasemekana kuwa wameachwa bila makazi kutokana na tetemeko la ardhi katika nchi hiyo.
  Shirika la umoja wa mataifa linalosimamia watoto (UNICEF) limesema kuwa kalibia watoto milioni moja hawana mahala pakulala, wanakabiliwa na ukosefu wa maji  safi pamoja na mazingira safi katika nchi hiyo.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Swiden Nchini Tanzania, Lennarth Hjelmaker, wakati alipowasili kwenye Taasisi ya ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kimataifa la Mafunzo ya pamoja kwa Mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia, yaliyoanza leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Nchi 14 za Afrika na washiriki kutoka Vyuo 15 vya nchini Sweden.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kimataifa la Mafunzo ya pamoja kwa Mabadiliko ya Kisayansi na Teknolojia, yaliyoanza leo jijini Arusha. Mafunzo hayo yameshirikisha washiriki kutoka Nchi 14 za Afrika na washiriki kutoka Vyuo 15 vya nchini Sweden.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo, baada ya ufunguzi rasimi.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadick, ameitaka  Bohari ya Dawa MSD kuendeleza kasi ya huduma zake za kupambana na ugonjwa wa malaria kwakuwa ni  moja ya taasisi  zilizo mstari wa mbele kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo.
  Akizungumza jana katika banda la MSD ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Malaria duniani Sadick alisema MSD imekuwa ikifanya jitihada kuhakikisha ugonjwa wa malaria unakoma na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vinapungua.
  Alisema jitihada hizo za MSD zimechangia matokeo ya kupungua takwimu za vifo vya mama na mtoto mchanga chini ya miaka mitano vitokanavyo na ugonjwa wa malaria hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha malengo ya millennia ya kupunguza vifo hivyo yanafikiwa.
  Alisema kutokana na MSD kuhakikisha dawa za malaria zinapatikana katika kila kituo cha afya, Zahanati na Hospitali ni wajibu wa wananchi kuhakikisha wanafanya  matumizi sahihi ya dawa hizo ili kutibu ugonjwa huo.
  “MSD inasaidia serikali kufikia lengo la kupunguza ugonjwa wa malaria tumeelezwa jinsi gani MSD inahakikisha dawa za malaria hazikosekani katika vituo vya kutolea huduma lakini pia imepanua  wigo kwa kutoa elimu kwa vitendo jinsi ya kupambana na ugonjwa huo kwa  kuhakikisha kinga dhidi ya malaria   inaanzia kwa wafanyakazi wake na wanapewa vyandarua vyenye dawa wao na familia zao,”alisema
  Sadick aliwataka wananchi kuacha kutumia dawa hizo katika matumizi yasiyo sahihi ikiwemo dozi moja ya dawa kutumiwa na watu zaidi ya mmoja kwakuwa kufanya hivyo kunasababisha matibabu ya wagonjwa wa malaria kutokukamilika na kusababisha vifo.
  Alisema pia kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi  katika vyandarua vya msaada ambapo utumika kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki hivyo mapambano dhidi ya ugonjwa huo kutokufanikiwa.
  “ Jitihada hizi za MSD na wafadhili mbalimbali katika kuweka  nguvu ya  kupambana na Malaria ni wajibu wa  jamii kuziunga mkono kwakuwa matumizi ya misaada hiyo ikiwemo Vyandarua ikitumiwa  kwa malengo yaliyokusudiwa  kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuimarika kwa afya ya wananchi wake,”alisema.
  Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo alizindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalimbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.
   Ofisa wa Kitengo cha Udhibiti Ubora wa MSD, Richard Makalla (kulia), akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki alipotembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo. Kushoto ni Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga na ofisa kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.
   Muenekano wa banda la MSD katika maadhimisho hayo.
   Ofisa Huduma kwa Wateja Kanda ya Dar es Salaam wa MSD, Florida Sianga (kushoto), akimuelekeza jambo kijana aliyetembelea banda la MSD katika maadhimisho hayo.

  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu akikagua moja ya vitanda na hema linazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akicheza na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

  HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  NMB imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla katika makampuni ya biashara yanayojali zaidi jamii kwa kutoa sehemu kubwa ya faida yake kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii ya kitanzania.

  Ushindi huo umetokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti wa huduma za maendeleo ya jamii - Research Centre for Social Development Services kwa kushirikiana na kampuni mwenza ya konsalt limited imetoa tuzo hiyo kwa NMB baada ya kujiridhisha kuwa ndiyo benki inayoongoza kwa kusaidia jamii zaidi.

  NMB imeyapiku makampuni na benki zingine 9. NMB hutoa asilimia moja kwaajili ya kuchangia maendeleo hususani madawati mashuleni, vifaa mahosipitalini, kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kuchangia jamii kipindi cha majanga kwa kuchangia vifaa mbalimbali kwa wahanga.

  Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Mtarajiwa wa NMB Bi. Ineke Bussermaker alisema “NMB imedhamiria mchango kwa jamii sio tu katika huduma za kibenki kwa wateja bali pia kutoa sehemu ya mafanikio yetu ili kuisadia jamii katika maeneo makuu matatu - kutoa elimu kuhusu huduma za kifedha, kuchangia katika sekta ya Afya, misaada mashuleni na mchango kwenye matukio ya maafa”.
   Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB-Bi Ineke Bussermaker akipokea tuzo ya Mshindi wa jumla kama taasisi inayochangia zaidi huduma za jamii kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara -Abdala Kigoda.
  Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB - Bi Ineke Bussermaker pamoja na Waziri wa Viwanda-Abdala Kigoda wakipata picha baada ya makabidhiano ya tuzo hiyo.  

  0 0

   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
   Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof. Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.
    Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua  Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.


  0 0


  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba  katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi. 

  Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:

  1.    FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

  2.   ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

  3.   PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS,   Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.

  Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.

  Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
  1.    Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”

  2.   Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi Tanzania zinazowasaidia  kwa lengo la kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.

  3.   Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops) zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja na uhalifu huo wa kimataifa.

  4.   Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap) za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.

  5.   Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au manunuzi mengine za ATM.
  Pia watuhumiwa hao wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za majina, anwani, pamoja na namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki mbalimbali kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya, Uingereza na Nigeria.

  Uchunguzi ziadi unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili kubaini mtandao wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.

  TAHADHARI KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE
  Pamoja na kuibuka na wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na kutoa fedha katika mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi hili la wizi kwa njia ya mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina hii kwa ushirikiano kati ya wamiliki wa mabenki  na wateja wao.  

   Jeshi la Polisi linashauri (pamoja na maelekezo mengine ya benki) njia sahihi ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha kwamba miamala yote inayofanyika katika akaunti za benki ni lazima ifahamike kwa mteja kwa njia zifuatazo:

  1.    Mteja ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.
  2.   Mteja atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi kilichoingizwa au makato au maingizo yoyote kwa muda ule ule.

  Aidha tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na wasikubali kutoa nambari za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari zao za siri hata kwa mtu ambaye ni ndugu wa karibu sana.
  Mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

  S. H. KOVA,
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
  DAR ES SALAAM.

  0 0

   Simon Msuva (kushoto) akishangilia na Amis Tambwe baada ya Tabwe kuipatia timu yake bao la katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshida 4-1. (Picha na Francis Dande)
   Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Amis Tambwe.
   Mshambuliaji Wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Polisi Moro, Hassan Mganga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Shabiki wa Yanga akifurahia bao la pili la timu yake.
   Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezona Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
   Amis Tambwe akipokea mpira baada ya kufunga"Hat Trick"
   Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akishangilia baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
   Mashabiki wakishangilia.

  0 0
 • 04/27/15--10:07: TASWIRA KUTOKA MORO-DAR • 0 0

  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatina muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.

  Ulega ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani kilwa.

  Ulega amesema Serikali kupitia mfuko wa uchangiaji wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.

  Awali, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Bima ya Afya, Rehani Athumani alimweleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa kampeni hiyo iliyozinduliwa leo itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

  Rehani alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.

  Naye mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga aliwaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Afya wa Jamii katika mikoa hiyo. 

  Aliomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.

  Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.
  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa, wakati uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akielezea namna kampeni hiyo inavyofanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15, katika uzinduzi uliofanyika leo katika Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.
  Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mashuka 150 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani(kulia) kwa ajili ya Zahanati za Wilaya ya Kilwa.


  0 0

  Na Mwandishi wa Wizara
  ya Mambo ya Nje.
  Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wameanza kikao cha siku mbili jijini Harare, Zimbabwe leo kufanya matayarisho ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo, utakaofanyika hapo tarehe 29 Aprili, 2015.

  Kikao cha Mawaziri, kinachoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. Simbarashe Mumbengegwi, kinatayarisha agenda ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi, ambao utajikita kwenye Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa nchi za SADC. Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mkutano huo, utakaofanyika chini ya Mwenyekiti wa SADC, Rais Robert Mugabe.

  Katika kikao cha Mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, anawakilishwa na Naibu wake, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, ambaye aliwasili Harare jana. Washiriki wengine ni Waziri wa  Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Gerson Lwenge.

  Mbali na mkakati wa maendeleo ya viwanda na mpango wa utekelezaji wake, Mawaziri watajadili Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Miundombinu na uanzishwaji wa Soko Huria la Utatu baina ya nchi za SADC, EAC na COMESA.

  Kikao cha Mawaziri kilitanguliwa na Kikao cha Maafisa Waandamizi, kilichosimamiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Musa Uledi.

  Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe, Simbarashe Mumbengegwi akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili Mkakati na Mwongozo wa kuelekea Maendeleo ya Viwanda katika Kanda ya SADC. Mhe. Mumbengegwi amefungua mkutano huo jijini Harare, Zimbabwe  huku akiwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa ya kifo cha Bregedia Jenereli Hashim Mbita ambaye alitoa mchango mkubwa katika ukombozi  wa nchi za Kusini mwa Afrika. Mhe. Mumbengegwi aliwaomba wajumbe wote wa mkutano kusimama ili kumuombea dua Bregedia Hashim Mbita.
  Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Mb) wa katikati akiomba dua kumkumbuka Brigedia Hashim Mbita. Kulia kwa Mhe, Kigoda ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao pia wakimuombea dua Brigedia Jenerali Hashim Mbita.
  Meza kuu nayo ikimuombea  Brigedia Jenerali Hashim Mbita. Kwa habari zaidi na picha BOFYA HAPA 

older | 1 | .... | 817 | 818 | (Page 819) | 820 | 821 | .... | 3282 | newer