Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 815 | 816 | (Page 817) | 818 | 819 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akizungumza na halaiki ya vijana wa chama hicho muda mfupi baada ya kuifunga kambi ya mafunzo ya vijana hao iliyofanyika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
  Mamia ya wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, wakimshangilia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (hayupo pichani), katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Lagangabilili wilayani humo juzi.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Lagangabilili Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu juzi.
  Wazee wa kabila la wasukuma wakimuombea kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ili yeye na chama chake aweze kutawala nchi. Mbowe alisimikwa na kupewa zana za kitemi za kabila hilo na kuitwa jina la Mayego kabla ya kuanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Lagangabilili wilayani Itilima mkoani Simiyu juzi.

  0 0

  TETEMEKO la ardhi limetokea nchini Nepal muda mchache uliopita na na kupoteza maisha ya watu  ya 900 na kuangusha Mnara wa Karne ya 19 Mjini, Kathmandu pamoja na kusababisha maporomoko ya theluji kutoka katika milima. 

  Taarifa zinadai kuna uharibifu katika maeneo ya nje ya kitovu cha tetemeko hilo lenye ukubwa wa kipimo cha richter cha 7.9 maili 50 kutoka Pokhara mji wa pili kwa ukubwa nchini Nepal. 

  Tetetemeko hilo la ardhi ni kubwa kabisa kuwahi kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha miaka 81 na pia limesababisha athari katika majimbo ya nchi jirani kaskazini mwa India na Bangladesh. 

  Kunauwezekano vifo hivyo vinaweza kuongezeka katika Bonde la Kathmandu ambalo lina watu milioni 2.5.

  Naibu balozi wa Nepal mjini New Delhi Prasad Pandey amesema inahofiwa kuwa mamia ya watu wamekufa na kuna ripoti ya kuwepo kwa uharibifu mkubwa kila sehemu kubwa na kwamba sio tu katika baadhi ya maeneo ya Nepal bali ni nchi nzima imeathirika. 

  Nepal ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kurekodiwa nchini humo hapo mwaka 1934 likiwa na kipimo cha 8.0 ambapo watu 8,500 walipoteza maisha yao.
  Baadhi ya Waokoaji wakiwa wamsaidia mmoja wa waathirika wa Tetemoko hilo aliekuwa amefukiwa kwenye kifusi ya moja ya majembo yaliyoporokoma kutokana na tetemeoko hilo.
  Sehemu ya athari za tetemeko hilo.
  Jitihada za kuokoa waliofunikwa na kifusi zikiendelea.
  Wananchi wa Nepal wakishitikiana kwa pamoja kuvuta kamba. 

  Ramani inayoonyesha sehemu iliyokumbwa na tetemeko hilo.
  Picha zote kwa hisani ya Mtandao wa Daily Mail

  0 0

  Kiungo mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’ na kipa, Juma Kaseja ni kati ya wachezaji watakaoiongoza timu ya Dar City kesho Jumapili Aprili 26,2015 kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Vikawe iliyopo Mkoani Pwani.

  Kwa mujibu wa mratibu wa mchezo huo, Athuman Tippo ‘Zizzou’, mchezo umeandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo mkoani Pwani.

  Tippo alisema kikosi cha Dar City kitajumuisha pia baadhi ya Waandishi wa Habari za Michezo na kubainisha kuwa mechi hiyo itachezwa kesho Jumapili kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Vikawe uliopo Kibaha, Mkoani Pwani.

  “Kikubwa tunataka kuhamasisha michezo huko Vikawe na katika kutimiza hilo, tumepanga kucheza mchezo mmoja wa kirafiki na wakazi wa huko kwa kuwatumia wachezaji, waandishi na watangazaji maarufu nchini,” alisema Tippo.

  Kikosi cha Dar City kinaundwa na wachezaji kama Manyika Peter, Juma Kaseja , Athuman Idd "Chuji" , Haruna Moshi "Boban",Idd Moshi,Kahabuka, George Magere Masatu, Charles Palapala,Mwinchumu Babel, Tippo Athumani "Zizzou", Shaffih Dauda, Saleh Ally,Kamba Lufo,Mbwiga wa Mbwiguke, Ibrahim Massoud "Maestroal",Clifford Mario Ndimbo, Abou Amokachi,Shearer Pamoja na Juma Assey
  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa pamoja na viongozi wa elimu nchini wametembelea Singapore kujifunza jinsi nchi hiyo ilivyofanya mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo.

  Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, unalenga kuendeleza wanafunzi katika kuwapatia stadi muhimu zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi.

  Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, umeweka mkazo zaidi katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanatoa ujuzi kwa mhitimu kuweza kufanya kazi katika kada ya kati. Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa, asilimia 29.4 ya wahitimu wanajiunga na vyuo vikuu; asilimia 28.2 wanajiunga na vyuo vya elimu ya ufndi na asilimia 46.4 wanajiunga na vyuo vya utaalamu mbalimbali (Polytechnic).

  Katika ziara hiyo Dkt Kawambwa na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea chuo kikuu cha Taifa cha Singapore (National University of Singapore), Chuo cha Elimu ya Ufundi (Institute of Technical Education) na Chuo cha Ufundi stadi (Republic Polytechnic) ambapo katika vyuo hivyo walipata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi pamoja na walimu.
  Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt Shukuru Kawambwa akielezea Jambo katika Mkutano kati ya viongozi wa elimu kutoka wa Tanzania na Viongozi wa Wizara ya Elimu ya nchini Singapore.
  Viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo kutoka Tanzania na Viongozi wa Elimu wa Singapore wakiwa katika mkutano wa pamoja katika kubadilisha mbinu na mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuboresha na kuleta mageuzi katika mifumo ya elimu wa nchi hizi mbili.
  Waziri wa Elimu na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Chuo kikuu cha Taifa Singapore. Ujumbe wa Tanzania ulitembelea chuo hicho ili kujionea na kujifunza ambavyo elimu ya ngazi ya chuo kikuu inavyotolewa nchini Singapore.

  0 0

  Mbunge  wa Ludewa Deo Filikunjombe akishirikiana,viongozi wa CCM , wananchi na mafundi  wa mradi wa umeme kubeba nguzo za  umeme katika  kitongoji cha Ngalawale Ludewa kijijini kama  sehemu ya kuhamasisha wananchi kushiriki maendeleo.
  mbunge Filikunjombe akiwa  chini ya shimo akishiriki  kuchimba shimo la nguzo ya  umeme  kitongoji cha ngalawale  kijiji  cha ludewa wengine ni diwani wa kata ya  Ludewa MONICA MCHILO ,katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na katibu mwenezi  wa CCM ludewa FELIX Haule  wakishirikiana na mbunge  wao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kundi la Watanzania 25 limerejea nyumbani kutoka Afrika Kusini leo tarehe 26 Aprili, 2015 kufuatia mashambulizi ya wazawa dhidi ya wageni. Kundi hilo la kwanza kurejea nyumbani liliwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere saa 11 alfajiri na Ndege ya Fast Jet.

  Watanzania hao walikuwa wanaishi katika kambi za dharura za Isipingo na Phoenix zilizopo jijini Durban. Walisindikizwa kurudi nyumbani na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Bw. Elibahati Lowassa. Zoezi la kuwarejesha wananchi hao lilisimamiwa na kuratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.

  Wakati huo huo, Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umepata taarifa kuwa kuna Watanzania wengine wapatao 20 wanaishi kwenye Kambi ya Hillbrough jijini Johannesburg. Ubalozi umetuma Afisa kwenda katika kambi hiyo ili kufanya uhakiki wa taarifa hizo kwa madhumuni ya kuwarejesha nyumbani Tanzania haraka iwezekanavyo.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
  25 Aprili 2015

  0 0

  Mhamasishaji kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Ester Riwa katikati akizungumza na Vijana wa Kata ya Selela (hawapo pichani) wakati wa semina ya Ujasiriamali, Ujuzi, Stadi za Maisha na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana jana katika Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele na kulia ni Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara hiyo Bi. Amina Sanga.
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Bi. Mesha Singoyo akifafanua jambo kwenye semina ya vijana wa Kata ya Selela kuhusu Ujasiriamali, Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana iliyofanyika jana katika Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha.
  Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga (kulia) akizungumza na wanakikundi cha Naisho wanaomiliki mradi wa kunenepesha ng’ombe na kuziuza wakati wa kutembelea miradi ya vijana wa Kata ya Selela Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni mhamasishaji kutoka Wizara hiyo Bibi. Ester Riwa na wanne kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Mbeya Bw. Laurean Masele.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Mwandishi Wetu.

  MASHINDANO ya mchezo wa Darts Taifa yamezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Moshi iliyopo Manzese kwa kushirikisha mikoa mitano ya Tanzania.

  Akizindua mashindano hayo Katibu Tawala wa Wilaya ya kinondoni, Selestine Onditi ”kwanza aliwapongeza viongozi wa chama hicho kwa juhudi za pekee za kufanya mashindano hayo yafanyike kwa mwaka wa 2015,lakini zaidi aliwashukuru wachezaji kwa moyo wa kupenda mchezo kujigarimia kuacha kazi zao kutoka mikoani ikiwa pamoja na wenyeji Dar es Salaam kuja kushiriki mashindano hayo ya Taifa kwa kujilipia gharama zote za ushiriki hiyo inatia moyo sana kuwa ni dhahiri mnaopenda mchezo”.
  Alisema Onditi michezo ni afya,michezo ni furaha na michezo ni kufahamiana basi aliwataka washiriki wote watumie nafasi hii ya kukutana katika kuyafanikisha haya yote.

  Onditi alitoa wito kwa wafadhili kuwa wasiegemee kwenye mpira wa miguu tu kuna michezo mingi kama Darts na mingine wajitokeze wadhamini kwani kwa kutumia wapenda michezo kama hawa waliojitolea kutoka mikoani kwa gharama zao kuja kushiriki mashindano ya Taifa ni nafasi ya pekee wewe mfanyabishara kutangaza biashara yako.

  Mwisho aliwatakia mashiondano mema yenye amani kuwa waanze salama na wamalize salama na mwisho warejee majumbani salama salimini.
  Nae Mwenyekiti wa Chama cha Darts Taifa, Gesase Waigama alizitaja zawadi kuwa ni Vikombe na Pesa taslimu kwa mfumo wa mashindano utakaotumika ni wa Singles(mmoja mmoja), Doubles(wawili wawili) na Timu.

  Mwisho Katibu wa Chama cha Darts Taifa, Kalley Mgonja aliitaja mikoa iliyofanikiwa kufika jijini Dar es Salaam kwa ushiriki wa mashindano ya Taifa kuwa ni Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha na wenyeji Dar es Salaam.

  0 0


  0 0

  Waziri mkuu wa zamani na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akitoa salamu zake kwenye sherehe za miaka 51 ya muungano ambazo ziliandaliwa na jumuiya ya watanzania wanaoishi katika Falme za kiarabu (UAE) .Sherehe hizo zimefanyika leo Jumamosi ya mkesha wa kuamkia tarehe 26 siku ya muungano, katika hoteli ya Shangrila mjini Dubai

  0 0

   Katika mahojiano ya Ras Makunja kiongozi wa Ngoma Africa band iliyopo kule nchini ujerumani na Zenj FM katika kipindi maalumu cha muziki wa dansi kinaongozwa na mtangazaji mahiri bwana Mustapha Mussa (pichani kulia) siku ya Jumamosi 25 April 2015.

  Mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja akihojiwa kwa njia ya simu alikuwa akijibu maswali ambayo majibu yake yamesikika kama ni pumzi mpya ya uhai wa muziki wa dansi Tanzania na miziki mingine kama vile taarabu na muziki wa kizazi kipya,Kamanda Ras Makunja ametoa wito kwa wasanii wa Tanzania wasisite wala kuogopa kutoa kazi zao nje ya mipaka ya nchi kwani Tanzania inajulikana kuwa ina muziki mzuri na unao kubalika kimataifa "Wanamuziki Msiogope tuone kazi zenu nje mnatisha na kukubalika" alitoa wito
  Mkuu huyo wa Ngoma Africa Band aka FFU kamanda Ras Makunja,ambaye pia
  aliwasifu sana wanamuziki wa wakongwe wazamani kuwa ndio kioo cha wanamuziki wengine.
  Alipoulizwa umri wa bendi ya Ngoma Africa kamanda Ras Makunja amesema bendi inatimiza miaka 22 na imekuwa sawa na muzimu wa muziki unao mtisha hata yeye mwenyewe unamtisha ! pia alichambua changamoto zinazoukabili muziki wa dansi nyumbani Tanzania,ni pamoja na baadhi ya vituo vya redio kutopiga mara kwa mara nyimbo za bendi za dansi,pia aliwaomba wanamuziki na bendi za muziki wa dansi kufupisha nyimbo zisiwe ndefu mno,na aliwaomba kuacha tabia ya kulalamikia kitu au hali fulani baadala yake kujitaidi kuutangaza
  muziki wa dansi katika kila hali na kuvifuata vyombo vya habari sio kusubiri.
  fuatilia mahojiano hayo katika Redio Zenj FM ya Zanzibar.
  pia unaweza kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com
  0 0

  Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya Pan Africa Power Solutions (T) Limited imetoa msaada wa vyandarua 700 vyenye viwatilifu kwa vituo vya afya vilivyopo kwenye kata za Wazo, Kunduchi na Kawe kwenye wilaya ya Kinondoni katika kuadhimisha ya siku ya Malaria duniani. 
  Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa IPTL na PAP, Katibu na mshauri mkuu wa sheria wa kampuni hizo, Bw. Joseph Makandege alisema: “IPTL inakubaliana kabisa na kauli mbiu ya mwaka huu ya Siku ya Malaria Duniani inayosema, Wekeza katika mapambano dhidi ya Malaria sisi kama IPTL/PAP tunaamini kuwa kuwekeza katika mapambano dhidi ya malaria kunabaki kuwa ‘nyenzo kubwa’ katika afya duniani kwa sababu kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kunaongeza upatikanaji wa rasilimali watu.” 
  Sambamba na msaada huo wa vyandarua pia kampuni ya IPTL imetoa elimu kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo na wakazi wa maeneo ya Kunduchi kuhusiana na ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na namna unavyoambukizwa, njia za kujikinga na matibabu sahihi ya ugonjwa huo. 
  “Kwa niaba ya Mwenyekiti Mtendaji wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP), Bw. Harbinder Singh Sethi na kwa niaba ya Menejimenti, IPTL/PAP leo inatoa vyandarua 700 ambavyo vitagawiwa vituo vyote vya afya katika kata za Wazo na Kunduchi, vikiwa ni vituo vinavyozunguka mitambo yetu ya kufua umeme iliyopo Sala Sala karibu na Tegeta,” Aliongezea Bw. Makandege. 
  Msaada huo ambao umelenga kuwanufaisha wagonjwa wanaolazwa, wanopumzishwa, kina mama wajawazito, na kina mama wanaojifungua katika vituo vya afya vya kata ya Wazo na Kunduchi. Malaria ni tatizo kubwa la afya nchini Tanzania, ambapo takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa Malaria inachangia vifo vya kila mwaka vya kadri ya watu 60 elfu, huku asilimia 80 ya vifo hivyo huwapata watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. 
  “Takwimu hizi si nzuri katika uhai wa uchumi wa nchi yetu. Hivyo basi, kila mtu hana budi kuhakikisha kuwa anatimiza wajibu wake katika kutokomeza Malaria hapa nchini. Sisi kama kampuni ya IPTL/PAP tumeanza. Hatutarudi nyuma. Tutakuwa bega kwa bega na serikali katika mapambano haya,” Alisisitiza Bw. Makandege 
  Bodi ya IPTL, ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Bwana Harbinder Singh Sethi, imeamua kujikita katika Nyanja za Afya, Michezo na Elimu katika awamu yake ya kwanza ya utekelezaji wa programu yake ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii (Corporate Social Responsibility – CSR)
   Kina baba hawakuwa nyuma katika kuunga mkono jitihada za kupambana na Malaria kwa kuungana na kina mama kupokea msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu uliotolewa na Kampuni za IPTL/PAP katika kata za Wazo na Kundunchi
   Mama huyu na mtoto wake aliye chini ya miaka 5 ni miongoni mwa watu waliopo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa Malaria wasipotumia vyandarua vyenye viwatilifu. Mama huyu ni miongoni mwa wananchi walionufaika na msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu uliotolewa na IPTL/PAP kwa wakazi wa Wazo na Kunduchi.
  Kina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ni sehemu ya walengwa wakuu wa msaada wa vyandarua vyenye viwatilifu ulipotolewa na makampuni ya IPTL na PAP. Hapa kina mama wenye watoto wadogo wakiwa kwenye foleni ya kupokea msaada kata ya Wazo.

  0 0

   Amb. Dr. Sezibera(in the middle with black suit)
  along with Ugandan 
  CEOs
  The EAC Secretary General’s CEO Forum was held yesterday at the Kampala Serena Hotel. Hosted by the East African Business Council (EABC) in collaboration with Private Sector Foundation Uganda (PSFU), EAC Secretariat and Trade Mark East Africa, the Forum brought together over 150 key business leaders, owners and Chief Executive Officers (CEOs) of private businesses in Uganda to dialogue on issues impacting doing business in Uganda and the region as a whole and strategize on the way forward.  
  Addressing participants, Uganda’s Minister of State for East African Community Affairs, Hon. Shem Bageine urged the business community to lay emphasis on sustainable investments for sustainable economic growth, employment creation particularly to the young generation and poverty reduction to create positive impact on the community.

  Hon. Bageine urged the private sector to regularly attend and participate in the Sectoral Council meetings and those related to trade, finance, investment, industry, monetary, and other matters, “as this would help you to own and drive the EAC integration process to your benefit sustainably”.

  He pointed out that Partner States had put in place conducive conditions for the private sector to thrive such as the rule of law, modern infrastructure, a stable macroeconomic environment, an educated, skilled and healthy workforce, gender equality and access to financial services. He called for strengthening the teaming up of public and private sector to support the transformation of the EAC region.

  Hon. Dr. Mutende, Uganda’s Minister of State for Trade and Cooperatives said in creating the enabling environment to trade, the Community was on the right direction but he called for effective implementation and enforcement of the regional laws and policies so as to make them effective and beneficial to all stakeholders and the citizens in the bloc.

  Dr. Mutende said that non-tariff barriers (NTBs) resulting from poor implementation of administrative procedures and enforcement of laws had caused the business community a lot of losses that could be avoided.

  The Minster sighted some of the NTBs as those related to lack of coordination among institutions involved in testing goods, existence of several weighbridges, un-harmonized border management institutions’ working hours, un-harmonized road users charges, numerous charges to protect certain products particularly dairy products, and unnecessary restrictions to other companies’ bids to tender for supply of goods and services across the borders.

  The Hon. Minister asserted that NTBs were greatly impacting the intra-EAC trade and “we need to rethink strategies to eliminate them”, adding that “we need to have a policy that encourages Private-Public Sector Partnership in capital investment which will lead to substantial reduction of cost of doing business in the EAC region”.

  The Secretary General of the East African Community Amb. Dr. Richard Sezibera informed his guests that due to the growing portfolio of the EAC projects and programmes, and also in order to diversify the EAC resource base and cut on donor dependency, there was need for the Community to tap into the potential funding from the private sector through the establishment of an EAC Private Sector Fund. 

  Amb. Sezibera informed Uganda’s business community that the ongoing initiative to set up a $20 Million EAC Private Sector Fund was to boost the participation of the private sector in the ongoing market integration. “The idea behind the fund is to see how we can ensure that the private sector plays a bigger role in the integration of EAC. The fund will be used to address various challenges facing the private sector within the EAC” disclosed the EAC official.

  The Secretary General briefed his audience on the latest positive developments taking place in all the four pillars of the regional integration noting that the process was on track and gaining momentum each passing day.

  The EABC Executive Director, Mr. Andrew Luzze highlighted the status and progress on the implementation of agreed recommendations of previous EAC SG CEO Breakfast Meetings and noted that 31 issues remained unresolved


  0 0


  0 0  0 0

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa pamoja na viongozi wa elimu nchini watembelea Singapore kujifunza jinsi nchi hiyo ilivyofanya mageuzi makubwa katika mfumo wa elimu na mafunzo. 
  Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, unalenga kuendeleza wanafunzi katika kuwapatia stadi muhimu zinazohitajika kwa maendeleo ya nchi. 
  Mfumo wa elimu wa nchi hiyo, umeweka mkazo zaidi katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi ambayo yanatoa ujuzi kwa mhitimu kuweza kufanya kazi katika kada ya kati. 
  Takwimu za elimu zinaonyesha kuwa, asilimia 29.4 ya wahitimu wanajiunga na vyuo vikuu; asilimia 28.2 wanajiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na asilimia 46.4 wanajiunga na vyuo vya utaalamu mbalimbali (Polytechnic). 
  Katika ziara hiyo Dkt Kawambwa na ujumbe wake walipata nafasi ya kutembelea chuo kikuu cha Taifa cha Singapore (National University of Singapore), Chuo cha Elimu ya Ufundi (Institute of Technical Education) na Chuo cha Ufundi stadi (Republic Polytechnic) ambapo katika vyuo hivyo walipata nafasi ya kuona shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanafunzi pamoja na walimu.
  Waziri wa Elimu na ujumbe wake wakiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Chuo kikuu cha Taifa Singapore. Ujumbe wa Tanzania ulitembelea chuo hicho ili kujionea na kujifunza ambavyo elimu ya ngazi ya chuo kikuu inavyotolewa nchini Singapore
  Viongozi wa wizara ya Elimu na Mafunzo kutoka Tanzania na Viongozi wa Elimu wa Singapore wakiwa katika mkutano wa pamoja katika kubadilisha mbinu na mikakati mbalimbali ambayo inaweza kuboresha na kuleta mageuzi katika mifumo ya elimu wa nchi hizi mbili
   Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt Shukuru Kawambwa akielezea Jambo katika Mkutano kati ya viongozi wa elimu kutoka wa Tanzania na Viongozi wa Wizara ya Elimu ya nchini Singapore.   0 0
 • 04/26/15--13:30: Article 0


 • 0 0
 • 04/25/15--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Christian Bella & Malaika Band - Nakuhitaji

  0 0

  Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akimwelezea Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya jinsi gani vitabu vyake vinavyoweza kumkwamua mwananchi wa hali ya chini na kumfikisha juu katika kumboreshea maisha mapya. Akijitolea mfano wake mwenyewe alipoanzia shimoni Kariakoo mpaka kufika nchni Marekani na sasa kualikwa katika mikutano mikubwa ya kutoa semina ya jinsi gani unavyoweza au kampuni inavyoweza kuwa namba moja katika sekta ya biashara.
  Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akichangia jambo na Katibu Mkuu wa Rais mstaafu Bwn. Abdallah Makame (kulia) aliokua akiongea na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi siku ya Ijumaa April 24, 2015 jijini Washington, DC nchini Marekani.
  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakishikilia bango la kitabu chake kipya kitakachotoka hivi karibuni.

  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akimkabidhi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi moja ya vitabu vyake.

  Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akiagana na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Picha na Vijimambo, Kwanza Production  0 0


  Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mhe Freeman Mbowe, akihutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mongella mjini Nansio Ukerewe jana.
   Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe Joshua Nassari wakihutubia wananchi wa Makambako, mkoani Njombe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana  kwenye Uwanja wa Azimio, ikiwa ni sehemu ya operesheni ya mafunzo kwa viongozi kukiandaa chama kwenda kushinda dola na kuongoza serikali.
   Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu akihutubia wananchi
    Gari iliyowapeba Naibu KAtibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Mhe. Salum Mwalimu na Mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe Joshua Nassari ikiwasili katika mkutano wa hadhara Makambako, mkoani Njombe
  Sehemu ya wananchi kwenye mkutano huo

older | 1 | .... | 815 | 816 | (Page 817) | 818 | 819 | .... | 3348 | newer