Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 814 | 815 | (Page 816) | 817 | 818 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitegemei kuona kura ya Maoni ya Katiba Mpya ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu unakumbwa na vurugu zinazoweza kuepukwa mapema. 
  Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania { TBC } mapema wiki hii Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba vyombo vya Dola vitakuwa makini muda wote kabla na baada ya matukio hayo mawili katika kuhakikisha amani inaendelea kudumu muda wote. 
  Balozi Seif Ali Iddi alisema suala la ulinzi na usalama ndani ya Taifa hili linamgusa kila Mwananchi anayepaswa kuwajibika muda wote kwa kuwafichua watu au vikundi vinavyoashiria kutaka kujiandaa kufanya vurugu kwa kuchafua amani inayohitajika na kila mtu. 
  Alisema kura ya maoni sambamba na uchaguzi mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano n mambo ambayo yamo ndani ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yakitekelezwa katika lengo la kuimarisha Utawala Bora kwa mujibu wa Maazimio ya Umoja wa Mataifa Tanzania ikiwa ni Mwanachama wake. 
  Akizungumza pia na Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar { Zanzibar Leo } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Zanzibar imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kuimarisha miundo mbinu ya kiuchumi ndani ya Kipindi cha Miaka mitano iliyopita. 
  Balozi Seif alisema miradi ya Bara bara zilizomo ndani ya mpango wa ujenzi Unguja na Pemba hivi sasa zimekamilika na juhudi zinaelekezwa zaidi katika kuimarisha huduma za maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya Mijini na Vijijini ambayo bado yanakabiliwa na upungufu huo. Alifahamisha kwamba zipo baadhi ya changamoto ikiwemo Bajeti ndogo ambayo haikidhi mahitaji halisi katika kukamilisha baadhi ya miradi ya Maendeleo hasa katika sekta za Elimu, Huduma za Maji pamoja na miradi ya Jamii. 
  Akijibu Swali la Mafuta na Gesi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Suala hilo linasubiri Katiba Mpya ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa ambalo limetolewa katika Mambo ya Muungano. Alisema endapo Katiba hiyo itapita kwenye Kura ya Maoni inayotarajiwa kupigwa baadaye mwaka huu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatengeneza Sera na Sheria inayohusu mambo ya Mafuta na gesi ili kuweka wazi uanzishwaji wa miradi itakayotokana na Sekta hiyo.
   Alifahamisha kwamba upo muelekeo unaoonyesha kuwepo kwa nishati hiyo hapa Zanzibar kutokana na kujitokeza kwa Wataalamu na Makampuni ya Mafuta na Gesi yanayotaka kushirikiana na Zanzibar katika kufanya utafiti wa nishati hizo.
   - Ripota wa Shirika la Utangazaji Tanzania {TBC } Marine Hassan akiporomosha maswali kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati wa mahojiano yao kuhusu maadhimisho ya Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanbzibar Balozi Seif akijibu maswali aliyoulizwa na Wanahabari wa Shirika la Magazeti ya Serikali la Zanzibar leo Hafsa Golo aliyepo Kati kati na Tatu Makame wa kwanza kushoto.

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini Bi. Liz Lloyd alipomtembelea Wizarani kwa ajili ya mazungumzo na Mhe. Maalim. 
  Mhe. Maalim akimtambulisha kwa Bi. Llyoid Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya. 
  Mhe. Dkt.  Maalim akizungumza na Bi. Lloyd
  Ujumbe alioambatana nao Bi. Lloyd wakifuatilia mazungumzo.
  Bi. Lloyd nae alipata wasaa wa kuchangia hoja wakati wa mazungumzo na Dkt.  Maalim 
  Mazungumzo yakiendelea.
                                       Picha na Reginald Kisaka.

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil wa pili kutoka kushoto akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mwamini Malemi wa kwanza kutoka kushoto pamoja na Viongozi wa Baraza la Wafanyakazi wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Wajumbe wengine wa Baraza hilo wakielekea kwenye ukumbi wa Police Officer’s Mess jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufungua kikao hicho kilichoketi jana kujadili utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2014/2015 na Malengo ya mwaka 2015/2016.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil watatu kutoka kushoto akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mwamini Malemi wa pili kutoka kushoto pamoja na Viongozi wa Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo wa pili kutoka kulia Amani Mashaka Katibu wa Baraza hilo na wa kwanza kutoka kulia Ndugu Jenitha Ndone ambaye ni Katibu Msaidizi wa Baraza hilo pia, wakiimba pamoja na wajumbe wengine (hawapo pichani ) wimbo wa ‘Mshikamo Pamoja’ katika kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Police Officer’s Mess jijini Dar es Salaam kikao kilichoketi jana kujadili utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2014/2015 na Malengo ya mwaka 2015/2016.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil watatu kutoka kushoto aliyeketi akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mwamini Malemi watatu kutoka kulia pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo wa kwanza kutoka kushoto walioketi ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Pius Nyambacha, wapili kutoka kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Ernest Mangu wa pili kutoka kulia ni Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza John Minja kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza hilo waliposhiriki kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Police Officer’s Mess jijini Dar es Salaam kikao kilichoketi jana kujadili utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2014/2015 na Malengo ya mwaka 2015/2016.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mbarak Abdulwakil katikati akifurahia jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP)Ernest Mangu wa kwanza kutoka kulia na baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo wakati aliposhiriki Kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Police Officer’s Mess jijini Dar es Salaam kikao kilichoketi jana kujadili utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2014/2015 na Malengo ya mwaka 2015/2016.

  0 0


  diamond_platinumz-slider-2
  ZURII HOUSE OF BEAUTY AND BONGO DEEJAYS PRESENT!!
  Londons Rugby 7's After Party, Appearing Live, Bongo Flava recording artist from Tanzania most famous for his song "Number One". Diamond Platnumz will be preforming with his WCB dancers and special guests at the Royal Regency Banquet Hall for one night only.
  THE ROYAL REGENCY
  501 HIGH STREET NORTH
  MANOR PARK 
  For Front Row V.I.P Tables and Info Please Contact our Ticket Hotline: 07853482158 or 07421167123
  Dont be left out, tickets are running out quickly. We are counting down to the most Epic event of the Year!!

  IN SUPPORT OF ALBINO CRUELTY IN TANZANIA. TOGETHER WE SAY: "IMETOSHA"

  Follow the link below or clck "Buy Tickets" to get your tickets A.S.A.P

  http://buytickets.at/zurii-house-of-beauty-and-bongo-deejays/26052


  Buy tickets for Diamonds are forever UK live concert


  0 0  0 0

  Mshindi wa kitita cha shilingi milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Irene Mrema (kushoto) mkazi wa Kawe Jijijini Dar es Salaam akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi yake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud”Jaymillions”kulia baada ya kuibuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo ambayo imeongezwa muda mpaka Mei 7 mwaka huu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
  Balozi wa Promosheni ya JayMillions Hillary Daud”Jaymillions”(kushoto)akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- Mshindi wa kitita hicho mkazi wa Kawe jijini Dar es salaam Irene Mrema(kulia) alichojishindia kupitia promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Rosalynn Mworia.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mlimani city jijini Dar es Salaam. Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.  0 0


  Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akimpiga kanzu mchezaji wa Ruvu Shooting, Abdulahman Musa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 5-0.

   Timu zikiingia uwanjani.


   Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwatoka wachezaji wa Ruvu Shooting. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  JAMII imeaswa kutumia elimu sahihi ya matumizi ya vyandarua katika kuweza kupambana na ugonjwa wa malaria.

  Hayo ameyasema leo Kaimu Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,amesema jamii imetakiwa kutumia elimu sahihi katika kupambana na malaria.

  Amesema malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asilimia 10 mwaka huu hiyo imetokana na juhudi za wizara ya afya na mashirika mbalimbali kutoa elimu juu kujikinga ugonjwa huo ambao awali ulikuwa ikichangia vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutokana na kutokana na kukosa vyandarua.

  John amesema katika madhimisho ya siku ya malaria ambayo itaadhimishiwa jijini Dar es Salaam yatakwenda sambamba na uzinduzi  wa ugawaji wa vyandarua milioni 24 vilivyotolewa na Wizara ya Afya ikiwa lengo kupambana na ugonjwa wa malaria. Amesema mikoa ambayo iko katika viwango vya juu vya ugonjwa wa Malaria ,Lindi,Geita ,Kigoma pamoja na Mara hali ambayo elimu inahitajika kwa mikoa hiyo katika matumizi sahihi ya vyandarua  kuweza kufikia asilimia sifuri.

  John amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Maralia ni Wekeza kwa Maisha ya Baadae ,Tokomeza Malaria na maadhimisho hayo itatumika sehemu ya kuelimisha juu ya kutambua dalili za malaria kuwahi katika kituo cha kutolea huduma,ili kupima na kudhibitisha uwepo wa vimelea kabla ya kuanza kutumia dawa kwa kuwa sio kila homa inasababishwa na Malaria.
   KAIMU Katibu Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akiandika maswali aliyeulizwa na waandisshi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maadhimisho ya siku ya malaria duniani iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani  -Tanzania ,Dk.Ritha Njau ,Kulia ni Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara,Dk.Abdulrazq Badru.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Michael John akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza siku ya malaria duniani inayoadhimishwa kila mwaka Aprili 25 iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam,Kushoto ni  Naibu Mkurugezi Kituo cha Utafiti cha Ifakara (IHI),Dk.Abdulrazq Badru.
   Meneja wa Mpango wa Kudhibiti Malaria wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,DK.Ben Mandike akisisitiza jambo  kwa waandishi  habari juu ya maadhimisho  ya siku ya malaria Duniania  iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.
  Watalaam na watafiti wa malaria wakifatilia mada mbalimbali katika mkutano wa tano wa taarifa ya miaka mitano ya utafiti wa Malaria na hali halisi ya sasa iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti cha Ifakara na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini ,Dar es Salaam.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akizungumza mbele ya wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi (hawapo pichani),wakati akizindua  chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa.
   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akiwa amembeba mtoto mara baada ya kumpa chanjo.
  wakazi wa kijiji cha Sawala wilayani Mufindi wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi Mboni Mhita,mara baada ya kuzindua  chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Iringa
   Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA akimpa chanjo mmoja wa watoto katika kijiji cha Sawala wilayani Mufindi mkoani Iringa

  Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wazazi na walezi Mkoani Iringa kutosikiliza maneno ya uzushi kuwa chanjo zinazotolewa kwa Watoto nchini huwa zinamadhara, badala yake wajitokeze kwa wingi kwenye vituo vya kutolea chanjo ili kuwakinga watoto na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi mbali mbali.

  Taarifa ya ofisi ya habari na mawasiliano ya halmashauri ya Wilaya  ya Mufindi, imeeleza kuwa ,Mkuu  wa wilaya aliyasema hayo katika kijiji cha Sawala Wilayani Mufindi Mkoani iringa wakati akimwakilisha Mkuu wa  Mkoa wa Iringa kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5.

  Mhita amesema endapo wazazi na walezi watasikiliza maneno yasiyo na ukweli wowote, watakuwa wanahatarisha afya za watoto wao kwani kuzikosa chanjo hizo muhimu kwa ustawi wa Mtoto kutasababisha washambuliwe na maradhi, kitu ambacho kinahatarisha uhai wa Mtoto.

  Amesema chanjo ni mkakati muhimu na muafaka katika kutokomeza maradhi na kupunguza vifo vya watoto lakini pia kupunguza gharama kubwa ambazo Familia na taifa kwa ujumla lingetumia katika kutibu maradhi yatokanayo na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.

  Wataalam ya afya wamethibitisha kuwa, chanjo huzuia  takribani vifo milioni mbili hadi tatu kila mwaka kutokana na maradhi yanayokigwa kwa chanjo ikiwa ni pamaoja na Ndui, Polio, Kifaduro na Pepopunda,ujumbe wa chanjo mwaka huu unasema Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya huku kauli mbiu ikisema Chanjo ni zawadi ya Maisha.

  0 0


  Changamkia Fursa "Ardhi Ni Mali"
  Eneo Linauzwa Lipo Kimara Mwisho, Mita 300 Kutoka Morogoro Road Au Stendi Ya Mabisi Ya Mwendo Kasi, Eneo Lina Ukubwa Wa Heka Moja Na Lina 

  Nyumba Moja Ndogo Na Restaurant Ya Makuti... Linafaa Kwa Makazi Na 
  Biashara. 

  Kwa Mnunuzi Piga Simu Nambari +255 757 343333 Au 786 582078. 

  0 0
 • 04/24/15--18:07: yale yaleee...
 • Mabasi yakipimana ubavu katika barabara kuu kuelekea Morogoro hivi karibuni.  Kwa mtaji huu ajali zitaisha kweli?

  0 0


  0 0


  Na DORICE Kigombe wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa kushirikiana na Idara mbalimbali za Serikali na wadau wa Amani Raia ,wamefanya matembezi/Routmatch ya pamoja kuzunguka mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma .Matembezi yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa Dodoma Capt. Mstaafu CHIKU GALAWA.

  Washiriki wa zoezi hilo ni Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ), Jeshi la Magereza, Uhamiaji, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Wafanya biashara, Raia wema na watumishi raia wa Vyombo vya ulinzi na Usalama Mkoani Dodoma.

  Lengo la zoezi hili la pamoja ni kudumisha ushirikiano, mahusiano mema ya idara mbalimmbali za serikali na raia wema. Akiongea na washiriki wa zoezi hilo, Mh. Mkuu wa Mkoa Capt. Mstaafu CHIKU GALAWA alisema “mazoezi ni afya, ushirikiano ni furaha na kukuza Udugu. Aliwapongeza wote walioshiriki zoezi hilo na kuagiza kuwa litakuwa zoezi endelevu na litashirikisha Idara nyingi zaidi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Dodoma,  Mkuu wa Mkoa Dodoma Capt. Mstaafu Chiku Galawa akiwa na wajumbe wakuu katika Routmatch leo.

  Askari polisi wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika Routmatch leo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Capt. Mstaafu Chiku Galawa akizungumza na washiriki wa Routmatch baada ya kuhitimisha zoezi katika viwanja vya bwalo la Polisi Dodoma leo.

  0 0
 • 04/25/15--05:17: Wanasubiri kuvuka Barabara
 • Watoto ambao majina yao hayakupatikana mara moja wakiwa wamesimama kando ya Barabara ya Chang'ombe kusubiri kupungua kwa magari ili wavuke, kwenye makutano ya barabara Mandela na Chang'ombe jijini Dar es salaam leo. 

  0 0

  Askofu msaidizi wa Kanisa Katiloki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe (Kulia) akizungumza na Watoto waliopata Sakramenti ya Kipaimara katika Kanisa Katoriki la Kimara jijini Dar es Salaam jana.
  Mtoto Angel Machellah (mbele) akiwa na watoto wenzie wakijiandaa kuingia kanisani wakati wa kupokea Sakramenti ya Kipaimara iliyofanyika katika Kanisa Katoriki Parokia ya Kimara Dar es Salam jana.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari, iliyofanyika jana usiku April 24, 2015 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milion tatu na Laki Nane (M.3.8) mshindi wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi, Mkinga Mkinga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na Generali Ulimwengu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni kumi (M. 10) Mwandishi wa habari wa siku nyingi mkongwe, Generali Ulimwengu, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015. Kushoto ni Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Robert Mihayo na (kulia) ni Mke wa Generali Ulimwengu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo mshindi wa pili wa jumla katika kinyang’anyiro cha Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT), Mwandishi wa habari wa Gazeti la The Citizen, Lucas Liganga, wakati wa hafla hiyo ya utoaji tuzo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, jana usiku Aprili 24, 2015.  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Tanzania Sylvester Ambokile Mwakinyule wakati alipowasili kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo liliopo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kutoka kushoto) Kamishna Mkuu wa UhamiajiTanzania Sylvester Ambokile Mwakinyule na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia hatua za utengenezaji wa PassPort za Uraia wa Tanzania wakati alipotembelea sehemu mbali mbali baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Perera A.Silima na (kulia) Inspekta wa Uhamiaji Hassan Suleiman Ameir.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Asistance Inspekta Khamis Ali Haji (katikati)wakati alipotembelea katika chumba cha kumbukumbu za picha kwa Wananchi walioomba Passpoti za Uraia baada ya kulifungua Jengo la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar leo Kilimani Mjini Zanzibar akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. [Picha na Ikulu].

  0 0

  Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba shindano la urembo nchini maarufu kwa jina la Miss Tanzania limefunguliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kwamba Kampuni ya Lino International Agency LTD ambayo ni waendeshaji wa shindano hilo imewataka mawakala wake kuanza maandalizi ya shindano hilo.

  Taarifa hizo za kufunguliwa shindano hilo zilienda mbali kwa kueleza kwamba mawakala wametumiwa kalenda ya mashindano hayo kwa mwaka huu.

  Baraza linapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

  1.Wananchi wapuuze taarifa hizo kwani kusimamishwa kwa shindano la Miss Tanzania bado kuko palepale kama ilivyoelezwa katika barua ya BASATA ya tarehe 22/12/2014 waliyoandikiwa Lino International Agency LTD ambayo pamoja na mambo mengine iliwataka warekebishe kasoro kadhaa zilizojitokeza. Walisimamishwa kwa misimu miwili ya mwaka 2015 na 2016 ili kujipanga upya na kurekebisha kasoro husika.

  2.BASATA kama msimamizi na mratibu mkuu wa sekta ya Sanaa nchini ndilo lililolisimamisha shindano hilo baada ya kubaini mapungufu mengi. Kusimamishwa kwa shindano hili ilikuwa ni kwa njia ya kuufahamisha umma na kwa maana hiyo kama shindano litafunguliwa njia hiyo-hiyo ya  kutoa taarifa kwa umma itatumika na si vinginevyo. 

  3.BASATA linatoa wito kwa Lino International Agency LTD kutumia muda wake mwingi kufanyia marekebisho mapungufu yaliyojitokeza ili mashindano haya yatakaporejea yawe na mikakati na hadhi kuliko ilivyo sasa. 

  4.Aidha, Baraza linawataka wasanii na wadau wote kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika kuendesha shughuli za Sanaa sambamba na kufuata mifumo sahihi ya mawasiliano.

  Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

  Godfrey Mngereza
  KATIBU MTENDAJI

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  SERIKALI  imeitaka jamii kutumia vyandarua  kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vyandarua hivyo vitumike kwa ajili ya kufugia Kuku au kuvulia Samaki.  Hayo yamesemwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick wakati wa maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka.  Sadick amesema wafadhili mbalimbali wamekuwa wakiweka nguvu katika kupambana na Malaria hivyo ni wajibu jamii kutumia Vyandarua hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa kwani kufanya hivyo kutaongeza uzalishaji wa uchumi katika nchi kutokana na kuwa na afya iliyo bora.  Katika maadhimisho hayo Mkuu Mkoa huyo amezindua mpango wa ugawaji wa Vyandarua milioni 24 kwa nchi mzima ikiwa ni jitihada za Serikali na wadau mbalilmbali kupambana na ugonjwa wa Malaria.  Amesema tangu kuanza kampeni hiyo ya kupambana na Malaria utafiti unaonyesha Malaria imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2012 na kufikia asiliamia 10 mwaka huu ambapo kupungua huko kumekwenda sambamba na kupungua kwa vifo vya wajawazito pamoja na vifo vya watoto chini ya miaka mitano(5).  Sadick amesema Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Wizara ya Kazi zinatakiwa kuweka utaratibu kwa makampuni mbalimbali kupambana na Malaria na sio kuwa sehemu ya hiari kwani kufanya hivyo kutaongeza ufanisi katika makampuni pamoja na viwanda.
  Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani ambayo hufanyika Aprili 25 kila mwaka, yaliyoanzia katika viwanja vya Msasani na kuishia viwanja vya
  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vyandarua katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam .
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akitoa hotuba yake katika maadhimisho ya siku ya Malaria Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
  Mtoto Noel Peter akiwa amelala kwenye kitanda kilichowekwa Chandarua ikiwa ni ishara ya kampeni ya kupambana na Malaria katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam leo.

  BOFYA  HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 814 | 815 | (Page 816) | 817 | 818 | .... | 3348 | newer