Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

WAKANDARASI WAASWA KULINDA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI-OSHA

$
0
0
 Mkuu wa kitengo cha sheria wa Wakala wa usalama na afya mahali pa kazi(OSHA),Joyce  Mwalubungu, akizungumza na wakandalasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri mkuu wa ufundi wa ujasiliamali na miradi kwa vijana Jelous Chirove akizungumza na wakandarasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkaguzi mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano katika jengo la Kazi House jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakandarasi waliohudhuria kwenye warsha iliyoandaliwa na wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA) iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)



Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

 MAKANDARASI wametakiwa  kuwajibika kwa kuwahudumia wafanyakazi wao wakiwa sehemu ya kazi kwa kulinda afya na usalama  wakiwa kazini.
Hayo yamesemwa  na Mkaguzi Mkuu wa Wakala wa Usalama na afya  Mahala Pakazi (OSHA),Akwilina Kayumba wakati wa Warsha ya Wakandarasi iliyoandaliwa  na Wakala wa Usalama na Afya sehemu ya kazi  uliofanyika leo katika Ukumbi wa Shirika la Kazi Duniani, jijini Dar es salaam.

Warsha kwa hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa Makandarasi  katika kuelekea kuadhimisha siku ya usalama na Afya Mahala Pakazi  Duniani ya afya  Duniani itakayofanyika Aprili 28 mkoani Dodoma.
Amesema sekta ya ujenzi ina wafanyakazi wengi hivyo inatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu katika kuepuka ajali ambazo zinaweza kutokea wakiwa kazini pamoja na magonjwa.

Kayumba amesema katika maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Mahala Pakazi Duniani,Wakala usalama na afya Mahala Pakazi kwa maadhimisho hayo itakuwa  siku ya maombolezo,majeruhi,magonjwa na vifo vya wafanyakazi mahala  pakazi.

Amesema kauali mbiu ya maadhimisho ya siku usalama na Afya Mahala Pakazi  Duniani mwaka huu ikiwa na kauli mbiu ‘Tushirikiane sote kudumisha usalama na afya sehemu ya kazi’.

MANISPAA YA ILALA YAELEZEA UBORESHAJI WA UKUSANYAJI WA MAPATO YAKE

$
0
0

Meneja Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo. Kulia ni Meneja Kodi Majengo, Stellah Mgumia na Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano. 
 Meneja Kodi Majengo wa Manispaa hiyo, Stellah Mgumia akitoa ufafanuzi mbalimbali wa ukusanyaji wa mapato.
 Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika wa Manispaa hiyo, Francis Luambano (kushoto), akizungumza na wanahabari katika mkutano huo.Picha na (Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA KYERWA LUTENI KANALI BENEDICT KITENGA (MSTAAFU) LEO MKOANI MOROGORO

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete (pichani kati) na Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda (pichani shoto) wakishuhudia askari wa jeshi la Wananchi (JWTZ) wakipiga risasi hewani kama sehemu ya heshima ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya mpya ya Kyerwa mkoani Kagera leo,Marehemu Luteni Kanali Benedict Kitenga (mstaafu) huko kwenye makaburi ya Mlima Kola Kigurunyembe mkoani Morogoro. PICHA NA IKULU.

JK MGENI RASMI UZINDUZI WA KITABU CHA HISTORIA YA NCHI “PHOTOGRAPHIC BOOK”

$
0
0
Mchapishaji wa Kitabu kipya chenye historia ya nchi tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964,Javed Jafferji (kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Uzinduzi wa Kitabu hicho   April 24 mwaka huu katika Hoteli ya Serena  jijini Dar es Salaam,Mhariri Mkuu wa Kitabu Simai Mohammed.
Mhariri Mkuu wa Kitabu kipya chenye historia ya nchi tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Simai Mohammed  akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Uzinduzi wa Kitabu hicho April 24 katika Hoteli ya Serena  jijini Dar es Salaam,Mchapishaji wa Kitabu kipya aved Jafferji. (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

Na Bakari Issa,Globu ya Jamii
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Jakaya M.Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Kitabu kipya chenye historia ya nchi tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Kitabu hicho chenye kurasa 444 kinaelezea historia ya nyuma ya kisiwa cha Zanzibar pamoja na Tanzania Bara na safari ya kisiasa tangu mwaka 1964,kinatarajiwa kuzinduliwa kesho April 24 katika Hotel ya Serena,saa 12 jioni  jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wandishi wa Habari,Mhariri Mkuu wa Kitabu hicho, Simai Mohammed amesema kitabu hicho kinazungumzia undugu ulioko kati ya kisiwa cha Zanzibar pamoja na Tanzania Bara,pamoja na matukio muhimu ambayo yamewagusa Watanzania kama Vita vya Kagera pamoja na kifo cha Mwalimu Julius K.Nyerere.

Mchapishaji wa Kitabu hicho,Javed Jafferji amesema kitabu hicho kimechukua miezi  17 kuchapishwa,vilevile kimeelezea historia fupi ya Rais wa Tanzania, Dkt.Jakaya M.Kikwete  pamoja na wa Tanzania visiwani,Dkt.Ali Mohammed Shein.

Jafferji aliongeza kuwa  amefurahishwa sana na Kitabu hicho kutokana na kuelezea historia ya nchi yetu pamoja na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

MANISPAA YA ILALA YADHAMIRIA KUBORESHA UKUSANYAJI WA MAPATO YAKE

Habari njema kwa WanaBlogu waTanzaniania juu Uandikishaji Wanachama TBN

$
0
0
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' - TBN kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa. Wahusika ni wamiliki na waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.

Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo. Kwa wa kazi wa Dar es Salaam wenye sifa ambao wanataka kujiunga fomu hizo zinapatikana kwenye Ofisi za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN. Fomu zitatolewa siku za kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia zinapatikana Ofisi za Michuzi Media, mjini Jengo refu karibu na Hospitali ya Ocean Road ghorofa ya pili. 

Kwa wanachama wa mikoani utaratibu unafanywa namna ya kusambaza fomu hizo mara moja na wanachama watalipa moja kwa moja benki ya NMB kwenye akaunti ya TBN. Utaratibu unafanywa kupata viongozi wa kanda wa muda watakaoratibu usajili kwa kushirikiana na viongozi wa muda wa TBN taifa. Viongozi wa muda wa mikoa na kanda watapewa maelekezo namna ya kusimamia na kuratibu zoezi la kujiunga uwanachama wa TBN. 

Mikoani TBN itagawanyika kwa kanda, yaani Kanda ya Pwani (ikijumuisha mikoa ya Tanga na Pwani yenyewe), Kanda ya Zanzibar (ikijumuisha Unguja na Pemba), Kanda ya Dar es salaam, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Simiyu), Kanda ya Kusini (jumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma), Kanda ya Kati (mikoa ya Dodoma, Tabora, Morogoro na Singida), Kanda ya Magharibi (inayojumuisha mikoa ya Kigoma na Rukwa), Kanda ya Ziwa (yenye mikoa ya Kagera, Geita, Mara na Mwanza), na Kanda ya Kaskazini (inayojumisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara).

Kwa wahitaji unaombwa kuchukua fomu yako mapema kwani usajili wa wanachama wa TBN utafanyika kwa muda wa wiki tatu kisha zoezi hili litafungwa ili kutoa fursa kwa viongozi na kamati husika kutathmini wanachama waliopatikana na litafunguliwa tena baada ya miezi sita.

NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Utaratibu unafanywa wa kuichapa kwenye soft coppy na zitatumwa mikoani kwa gharama za TBN. 

Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470 
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)

Shindano la TMT 2015 lazinduliwa rasmi leo, Mwanza kufungua pazia kesho

$
0
0

Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.
 Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MAADHIMISHO SIKU YA MALARIA DUNIANI KITAIFA KUFANYIKA MNAZI,MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Tanzania itaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Malaria duniani Aprili 25 mwaka huu ili kutathmini mafanikio ya utekelezaji wa mikakati  mbalimbali ya kupambana na ugonjwa huo hapa nchini.

Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mwaka 2015, leo jijini Dar es salaam amesema maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za ugonjwa wa Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.

Amesema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam chini ya kauli mbiu isemayo Wekeza kwa Maisha ya Baadaye, Tokomeza Malaria huku msisitizo mkubwa ukilenga kuikumbusha na kuielimisha jamii kuepuka athari na madhara yanayotokana  na ugonjwa huo.

Bw. Mushi amesema maadhimisho ya mwaka huu  yamelenga kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutambua dalili za malaria na kuwahi kwenye vituo vya kutolea huduma pindi wasikiapo dalili za ugonjwa huo ili waweze kupima afya zao  na kupatiwa matibabu.

“Ugonjwa wa malaria kwa muda mrefu umekuwa na athari kwa nguvu kazi ya taifa na utekelezaji wa mikakati mbalimbali, hivyo ni wajibu wetu kushirikiana kuwaelimisha wananchi kuwahi katika vituo vya afya pindi wasikiapo dalili za malaria” Amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji Mpango wa Udhibiti wa Maambukizi ya Malaria Dkt. Linda Nakara akizungumza kuhusu maadhimisho hayo amesema kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na wadau mbalimbali wa huduma za afya kufanya maonyesho ya huduma wanazotoa kwa jamii.
Ameongeza kuwa wadau hao pia wataendesha shughuli za uchunguzi wa vimelea vya malaria kwa kutumia vipimo vinavyotoa majibu kwa haraka (MRDT) na matibabu ya ugonjwa wa malaria kwa wale watakaogundulika kuwa na malaria.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani mwaka 2015 alipokutana na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. Maadhimisho ya mwaka huu yanalenga kuwakumbusha na kuwaelimisha wananchi juu ya athari za Malaria na mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Mwakilishi wa FAO nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akimkaribisha Mwakilishi wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (F.A.O) nchini Bi. Diana E. Tempelman alipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa Shirika hilo hapa nchini. 
Mhe. Dkt. Mahadhi akizungumza na Bi. Diana kwa kumpongeza kwa uwakilishi wake mzuri wa Shirika la FAO hapa nchini
Bi. Diana nae akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri kwa Ushirikiano mzuri aliokuwa akiupata kutoka Wizarani wakati wote akiwa hapa nchini.  
Picha na Reginald Philip

News alert: Majina yatakayowania Tuzo za Watu 2015 yatangazwa

$
0
0
Majina yaliongia kwenye hatua ya tano bora kwenye Tuzo za Watu 2015 yametangazwa rasmi Ijumaa hii. Hiyo ni baada ya siku kadhaa za kuhesabu mapendekezo yaliyokuwa yakitumwa na wananchi kwa kipindi cha wiki tatu tangu kuzinduliwa kwa tuzo hizo.

Zoezi la kupiga kura linafunguliwa rasmi Jumamosi hii, April 24.

Haya ndio majina matano yaliyoingia kwenye tano bora:


Mtangazaji wa redio anayependwa TZW1         

Dida – Times FM
D’Jaro Arungu – TBC FM
Diva – Clouds FM
Mariam Kitosi – Times FM
Millard Ayo – Clouds FM

Kipindi cha redio kinachopendwa TZW2

Ala     za Roho – Clouds FM
Amplifaya – Clouds FM
Hatua Tatu – Times FM
Papaso – TBC FM
XXL – Clouds FM


Mtangazaji wa runinga anayependwa TZW3     

Abdallah ‘Dullah’ Ambua - EATV  
Salama Jabir – EATV/Maisha Magic
Salim Kikeke – BBC Swahili
Sam  Misago - EATV
Zamaradi Mketema – Clouds TV


Kipindi cha runinga kinachopendwa TZW4

Friday Night Live – EATV
In My Shoes – EATV
Mkasi – EATV
Planet Bongo – EATV
Take  One – Clouds TV

Blog/Website inayopendwa TZW5

Muongozaji wa video anayependwa TZW6

Abby Kazi
Adam Juma
Khalfan
Hanscana
Nisher


Muongozaji wa filamu anayependwa TZW7

Jacob 'JB' Stephen
Leah Mwendamsoke
Timothy  Conrad
Vincent ‘Ray' Kigosi
William Mtitu


Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa TZW8

Elizabeth 'Lulu' Michael
Irene  Uwoya
Jacqueline  Wolper
Riyama  Ally
Wema Sepetu


Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa TZW9
Hemedi  Suleiman
Jacob   'JB'    Stephen Mzee
King Majuto
Salim ‘Gabo’ Ahmed
Vincent  'Ray' Kigosi

Mwanamuziki wa kike anayependwa TZW10
Lady  Jaydee
Linah
Mwasiti
Shilole
Vanessa  Mdee

Mwanamuziki wa kiume anayependwa TZW11 
Alikiba
Barnaba
Diamond  Platnumz
Jux
Ommy Dimpoz

Filamu inayopendwa TZW12
Chausiku
Kigodoro
Madam
Mshale wa Kifo
Sunshine

Video ya muziki inayopendwa TZW13
         
Akadumba -  Nay  wa        Mitego
Kipi Sijasikia – Profesa Jay
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz   
Wahalade -  Barnaba
XO - Joh  Makini

Membe awahimiza Watanzania kuchangamkia fursa za kibiashara na kuwekeza katika Visiwa vya Comoro

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) amewahimiza wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji Visiwani Comoro kwani uhusiano baina ya nchi hizi mbili umeimarika. 
 Mhe. Membe alitoa kauli hiyo wakati akilihutubia Kongamano la Biashara baina ya Tanzania na Comoro lililoandaliwa na Balozi za Tanzania na Comoro kwa kushirikiana na sekta binafsi za nchi hizo mbili jijini Moroni, Comoro tarehe 23 Aprili, 2015. 
 “Watanzania tunathaminiwa sana hapa kutokana na mchango wetu mwaka 2008 tulipokikomboa Kisiwa cha Anjouan kutoka kwa Kanali Bacar. Sasa Serikali ya Umoja wa Visiwa vya Comoro imeimarika na uhusiano wetu umeshamiri. Wanatukaribisha sisi kwanza kushirikiana kibiashara, tuchangamkie fursa hii” alisema Waziri Membe. 
 Vilevile, Mhe. Membe alisifu jitihada za ofisi za ubalozi wa nchi hizi mbili kwa kuitikia wito wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara kwa kuandaa kongamano hilo la kihistoria. 
 “Rais Kikwete alipofanya ziara yake hapa mwaka 2014, aliahidi kukuza uhusiano wetu na kutoa wito wa kushirikiana kibiashara kwa manufaa ya nchi zetu. 
Nawapongeza sana Balozi Kilumanga na Balozi Fakih kwa kushirikiana na sekta binafsi na kutekeleza hili kwa wakati”alisema Waziri Membe, ambaye aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano hilo. Kwa upande wake, Rais wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Ikililou Dhoinine alisema kuwa yeye na Serikali yake wanathamini mchango mkubwa wa Tanzania kwa watu wa Comoro na hivyo atahakikisha uhusiano wetu unakua kwenye nyanja zote, Serikalini, sekta binafsi na hata baina ya watu wa nchi zote mbili. 
 Aidha, baada ya ufunguzi rasmi wa kongamano hilo, wafanyabiashara wa Tanzania walikutanishwa na wenzao wa Comoro kwenye makundi madogo madogo ili kuibua changamoto zinazokwaza biashara baina ya nchi hizo. Mikutano hiyo inatarajiwa kuibua njia bora zaidi ya kuwezesha biashara baina yao na kuimarisha uhusiano baina ya watu wake. 
 Akiwa jijini Moroni, Mhe. Membe alipata fursa ya kutembelea fukwe za bahari ambazo ni vivutio vikubwa vya utalii kwenye nchi hiyo ya visiwa akiwa na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Alanrif Said Hussane, Waziri wa Mambo ya Nje wa Visiwa vya Comoro. 
 Serikali ya Tanzania ilifungua ofisi zake za ubalozi mwaka 2013 ambapo inawakilishwa nchini humo na Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania, mwenye makazi yake Moroni. 
Kwa upande wa Serikali ya Comoro ilifungua Ubalozi wake nchini Tanzania mwaka 2014 na inawakilishwa na Mhe. Ahamed El Badaoui Mohamed Fakih Balozi wa Comoro mwenye makazi yake Dar es salaam. 
 Kongamano hilo la siku mbili lililofunguliwa na Mhe. Ikililou Dhoinine, Rais wa Visiwa vya Comoro, lilifanyika kwenye ukumbi wa bunge jijini Moroni, mojawapo ya visiwa vitatu vinavyounda Umoja wa Visiwa vya Comoro, na kuhudhuriwa na wafanyabiashara takriban mia moja kutoka Tanzania. 
Visiwa vingine vinavyounda umoja huo wa Comoro ni Ngazija (Grand Comoro), Anjouan na Moheli huku mji mkuu ukiwa Moroni.
 meza kuu ya viongozi wa Tanzania na Comoro, katikati ni Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Dk. Ikililou Dhoinine, akiwa na Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania na kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Kongomano la Biashara wakifuatilia 
 Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Dk. Ikililou Dhoinine, akizungumza na Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi rasmi tarehe 23 Aprili 2015 Moroni.
 Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akihutubia kongomano kubwa la biashara baina ya Tanzania na Comoro jijini Moroni Alhamis tarehe 23 Aprili 2015.
Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akihutubia kongomano kubwa la biashara baina ya Tanzania na Comoro jijini Moroni Alhamis tarehe 23 Aprili 2015.

VIJANA WA NCCR-MAGEUZI WAMCHUKULIA FOMU MGOMBEA URAIS WA CHAMA HICHO,DK.MIHANGO

$
0
0
Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi,Faustine Sungura akizungumza na Wandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi,leo jijini Dar es Salaam,(kushoto) ni Katibu wa Vijana wa  Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa Mawazo Atanas.

 Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya Urais Katibu wa vijana wa  chama cha NCCR-Mageuzi taifa Mawazo Atanas kwa niaba ya  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk George Mihango,jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa kumkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya urais Katibu wa Vijana wa  Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa,Mawazo Atanas kwa niaba ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.George Mihango,leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii)

Na  Avila Kakingo,Globu ya Jamii

UMOJA wa Vijana wa Chama cha NCCR-Mageuzi  wamemchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Urais kwa chama hicho,Dk.George Mihango ambaye ni Mhadhiri wa  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Chama hicho, leo jijini Dar es Salaam,Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura,amesema vijana wa chama hicho wamemshawishi Mhadhiri huyo kwakuwa anavigezo vyote vya kugombea nafasi hiyo.


Sungura,amesema kuwa milango iko wazi kwa wanachama kuja kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho katika uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni.


Aidha amesema,wakati umefika kwa  vijana waliozaliwa baada ya uhuru sasa wanaweza kugombea nafasi za uongozi katika  chama hicho, kutokana na uwezo wanaonyesha katika vitu mbalimbali.



Nae Katibu wa Vijana wa  Chama cha NCCR- Mageuzi Taifa,Mawazo Atanas amewashukuru vijana wa chama hicho kwa kusaidia kumchagua Mhadhiri wa Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam,Dk.George Mihango kuchukua fomu kwaajili ya kugombea nafasi ya Urais katika chama hicho ambaye atachuana na wagombea mbalimbali katika nafasi hiyo.

MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 51 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR YAKAMILIKA, WANANCHI WAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI

$
0
0
Serikali imesema kuwa maandalizi ya Sherehe za Miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yamekamilika na kwamba sherehe hizo zitafanyika katika uwanja wa Uhuru Aprili 26 mwaka huu. 
 Akitoa ufafanuzi kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya sherehe hizo kwa niaba Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam leo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema amesema maadhimisho ya mwaka huu yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani Na Umoja ,Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki Uchaguzi Mkuu. 
 Amesema Tanzania katika kipindi cha miaka 51 ya Muungano imepata mafanikio makubwa katika Nyanja mbalimbali za maendeleo ya jamii, uchumi, Siasa,Ulinzi, Usalama na Uhusiano wa Kimataifa. 
 Bi. Mjema amefafanua kuwa maadhimisho hayo yataongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye atakuwa mgeni rasmi na kupambwa na michezo ya Halaiki, ngoma za asili, vikundi vya burudani na Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya ulinzi na usalama. 
 Pia yatapambwa na Wimbo maalum utakaoimbwa na vijana wa halaiki na ndege vita za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zitakazopita mbele ya mgeni rasmi Kama sehemu ya shamrashamra ya sherehe hizo. 
 Ametoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuhudhuria maadhimisho hayo na kufafanua kuwa milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kuanzia saa 12:30 asubuhi ili kuwawezesha wananchi kuingia kushuhudia sherehe hizo. Aidha, ameutaka uongozi wa SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya usafiri (Daladala) kuelekeza magari yao ya abiria kwenda uwanja wa Uhuru ili kurahisisha huduma ya usafiri kwa wananchi.
Askari watakaoshiriki kwenye Gwaride la heshima litakalohusisha vyombo vya ulinzi na usalama wakati wa maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakiwa wamebeba bendera za Majeshi ya Tanzania ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe hizo uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.
skari wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
 Askari wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Maji wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
 Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kitengo cha Mawasiliano wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo jijini Dar es salaam. 
Askari wa Kikosi Maalumu cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (Komando) wakipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa kasi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe za miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. 

Tigo yazindua internet ya 4G LTE jijini Dar es salaam leo

$
0
0
Tigo launches bid to become biggest 4G network in Tanzania
Speaking at the launch, Tigo Interim General Manager Cecile Tiano said: “This once again demonstrates our company’s commitment to the digital lifestyle transformation and its leadership in delivering cutting edge technology and innovation in this market.” 
 The 4G LTE network means faster speeds to surf and download content from the Internet and make Skype calls. It also significantly enhances the customer experience for video streaming or conferencing. 
The new technology is about 5 times faster than the 3G technology currently available in the market. The 4G LTE technology is a standard for wireless communication of high-speed data. It has the capacity to efficiently transfer large amounts of data at an unparalleled speed. 
It can also accommodate more applications such as video conferencing, high definition content, video blogs, interactive games and video downloads on social networking sites. 
 With the surging use of smartphones among the Tanzania population, 4G technology will enable Tigo customers to enjoy a world class experience of increased speed and quality of internet access through the network. “Today’s launch covers Masaki and Mlimani City areas within Dar es Salaam but our plan is to fully cover the city by end of July, ensuring quality coverage in Kinondoni, Ilala and Temeke in places such as Upanga, Posta, Tegeta, Mbagala, Tabata, Kimara, Mbezi, Ukonga, Salasala, Mikocheni, Msasani, Sinza and so on,” Ms Tiano explained. 
 “We will also launch 4G in Arusha, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza and Tanga by end of August. This will make us by far the biggest 4G network in Tanzania,” she added. 
 The 4G technology launch is part of Tigo’s commitment to continue improving the quality and coverage of its network and bring world class products and services to Tanzanians. 
Tigo recently announced plans to invest US $120 million in 2015 on its network expansion and improvement. The investment includes scaling up its 3G sites and fibre network countrywide to make the internet accessible to more users.
Ag Tigo Tanzania General Manager Cecile Tiano making her key-note speech during the launch of the fastest Network in Tanzania 4GLTE in Mlimani City, Dar es Salaam. 

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akihutubia hivi sasa kwenye uzinduzi wa 4G LTE ya internet iliyozinduliwa leo na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo, katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na Balozi Ami Mpungwe mara baada ya uzinduzi wa 4G LTE ya internet iliyozinduliwa leo na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Tigo Tanzania. Katikati ni Maafisa wa Kampuni ya Tigo.
Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA AWASILI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi ya Rasaisei English Medium ya mjini Dodoma baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 24, 2015. Wapili kulia ni Rubani wa Ndege za serikali, Narzis Kisimbo , kulia ni Mwalimu Esther Minja na kushoto ni mwalimu Emmanuel Kubyo.Wanafunzi hao walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kwa ziara ya kujifunza.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Aprili 24, 2015.Kutoka kushoto ni Rubani Naeziz Kisimbo, Mhandisi, Dioniz Majogo na Afisa Uendeshaji, Mohammed Mwilima. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

introducing "Shauri yako" by SLIMSAL ft. G. Nako

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI APENDEZESHA SHEREHE YA CHAUKIDU SILVER SPRING, MARYLAND NCHINI MAREKANI

$
0
0
Meza kuu toka kushoto ni Rais wa CHAUKIDU Prof.Lioba Moshi, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi wakuhudhuria sherehe ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani. Mhe. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi sherehe iliyofanyika Silver Spring, Maryland nchini Marekani siku ya Alhamisi April 23, 2015 na kuhudhuriwa na wadau wa Kiswahili kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo Wamarekani wanaozungumuza lugha ya Kiswahili.
Dr. Hamza Mwamoyo mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of Amerika (VOA) akimsabahi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi huku wakipata picha ya kumbukumbu wenginine kwenye picha ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
Farida(kulia) wa Farida Catering akiwaelekeza Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula aina ya vyakula alivyopika katika kuhitimisha sherehe ya CHAUKIDU siku ya Alhamisi April 23, 2015 Silver Spring, Maryland nchini Marekani. Hii ni mara ya pili kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuonja mapishi ya Farida Catering mara ya kwanza ilikua katika shere ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyika mwaka 2013 Capitol Heights.
Pia

MASPIKA WA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA JIJINI DAR KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YANAYOHUSU NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0
Na Bakari Issa,Dar es Salaam

Maspika wa Bunge wa Afrika Mashariki wamekutana jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala mbalimbali yanayozihusu nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki likiwemo suala la Ugaidi pamoja na vurugu zinazotokea ,maendeleo hususan Barani Afrika.

Katika Mkutano huo wenye jina la ‘Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki’ulihuduliwa na Maspika wa nchi za Tanzania,Kenya,Uganda, Rwanda pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki(EALA),Mhe.Daniel Kidega.

Akizungumza katika makutano huo,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano huo,Mhe.Anne Makinda amesema mkutano huo una lengo la kuangalia maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki pamoja na mambo mazuri yaliyoko katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo tabu kama suala la Ugaidi.

Spika wa Bunge la Uganda,Mhe.Rebecca Kadaga amesisitiza juu ya ushirikiano baina ya nchi za Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati na mipango juu ya ulinzi wa nchi za Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Spika wa Bunge la Kenya,Mhe.Justine Muturi amewahasa wananchi wa Afrika kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi za Afrika Mashariki na kuwahasa vijana wa nchi hizo kutojihusisha na vikundi visivyofaa.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya Afrika Mashariki,Mhe.Anne Makinda (katikati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya uwepo wa mkutano huo hapa nchini. Wengine pichani toka kulia ni Mh. Justine Muturi (Spika wa Bunge la Kenya), Mh. Rebecca Kadaga (Spika wa Bunge la Uganda), Mh. Donatille Mukabalisa (Spika wa Bunge la Rwanda) pamoja na Mh. Daniel Kidega (Spika wa Bunge la Afrika Mashariki).

MATEMBEZI YA ASUBUHI KWA WATUMISHI WA TAASISI MBALIMBALI MKOANI DODOMA

$
0
0
Kesho siku ya Jumamosi tarehe 25 Aprili, 2015, kuanzia saa 12:00 hadi saa 2:00 asubuhi, kutakuwa na zoezi la matembezi ya miguu kwa watumishi wa taasisi mbalimbali Mkoani Dodoma.


Matembezi hayo yataanzia viwanja vya bwalo la polisi Mjini Dodoma na kufuata uelekeo wa barabara ya Bunge la Tanzania, Barabara ya Dodoma Inn, Mtaa wa Nyerere na kurudi viwanja vya Bwalo la Polisi ambapo ndio kituo cha mwisho. 
Matembezi hayo yataongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa. Vilevile yatahudhuriwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma. 
Watumishi wa taasisi mbalimbali za Mkoani Dodoma wamealikwa kuhudhuria matembezi hayo. Taasisi hizo ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kama Jeshi la Polisi, Magereza, JWTZ, JKT, Uhamiaji na Majeshi ya Akiba. Taasisi nyingine ni kama TAKUKURU, Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira-DUWASA. Taasisi nyingine ni Mabenki, Wamachinga, TCCIA (M), Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Tume ya Utumishi wa Maadili ya Umma na CWT. 
Zoezi hili la matembezi limeanzishwa kwa Malengo ya kutoa fursa kwa watumishi wa taasisi mbalimbali Mkoani Dodoma kujumuika kwa pamoja katika mazoezi ya kutembea na litakua zoezi endelevu. Matembezi haya yatakuwa yakitumika kuhamasisha masuala ya kimkoa na kitaifa na yatakuwa yakifanyika kila Jumamosi ya Kwanza na ya mwisho ya kila mwezi.

Imetolewa na:
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Aprili 24, 2015

MFUKO WA CHANGAMOTO ZA MILLENIA (MCAT) YAKABIDHIN RASMI KAMBI YA KANDA ILIYOPO MKOANI RUKWA KWA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (Millenium Challenge Account - MCAT) Eng. Salum Sasilo (kulia) akimkabidhi funguo Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kama ishara ya makabidhiano rasmi ya kambi ya Kianda iliyokuwa ikitumiwa na Mkandarasi Aasleaf Bam International katika ujenzi wa barabara ya lami kuunganisha Mikoa ya Rukwa na Mbeya katika mradi wa Laela - Sumbawanga wenye jumla ya Kilomita 95. Chuo hicho Kikuu cha MUST kimedhamiria kubadilisha kambi hiyo yenye jumla ya ekari 118 na majengo ya kudumu zaidi ya 18 kuwa moja ya Kampasi zake itakayobobea katika sekta ya uhandisi ujenzi hususani ujenzi wa barabara.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa salamu zake katika hafla hiyo ambapo ameitaka taasisi ya MUST kuhakikisha kuwa inatunza miundombinu waliyokabidhiwa na kuiendeleza kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini kwa vizazi vilivyopo na vijavyo. Aliongeza kuwa dhamira ya Serikale yake ya Mkoa ilikua ni kuona kambi hiyo inakabidhiwa kwa moja ya taasisi kubwa za elimu nchini ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaamn na taasisi zingine ili kuinua sekta ya elimu nchini lakini imekuwa bahati kwa chuo cha MUST kupata nafasi hiyo ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya chuo chao na elimu kwa ujumla. Amekiomba Chuo hicho kuona uwezekano wa kuipa Kampasi hiyo ya Kianda jina la Rukwa kwa ajili heshma ya maeneo hayo ambayo yapo Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Sumbawanga. 
Meza kuu.


 Picha ya pamoja.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya katikati akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya - MUST Prof. Joseph Msambichaka kulia na Meneja Mradi wa Kampuni ya Aasleaf Bam International iliyojenga barabara ya Lami ya Laela - Sumbawanga Ndugu Russel Rourke muda mfupi baada ya zoezi la makabidhiano ya kambi hiyo ya Kianda.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images