Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 812 | 813 | (Page 814) | 815 | 816 | .... | 3348 | newer

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa ufafanuzi  kuhusu zoezi linaloendelea kuhusiana na Vyama vya Kijamii vilivyosajiliwa chini ya Sheria ya Vyama, Sura 337 kuwa ni la kubaini vyama vile ambavyo havitekelezi matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama husika na pia vile ambavyo havilipi ada ya mwaka kama sheria ya Vyama inavyoelezea.

   Vyama ambavyo vitabainika kukiuka matakwa ya kisheria kama yaliyotajwa hapo juu ndio vitakavyofutwa kutoka katika Daftari la Msajili wa Vyama vya Kijamii.  Orodha ya Vyama vitakavyofutwa itaanza kutolewa kwa awamu kuanzia wiki hii na kwa kuanzia, orodha hiyo itahusu Vyama vilivyosajiliwa mkoni  Dar es Salaam.
   Kufuatana na orodha tuliyonayo kiasi cha vyama 10,000 vya Kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila mwaka kama sheria inavyotaka.  Hii ina maana kuwa vile ambavyo vinatekeleza matakwa hayo ya kisheria havitafutwa.
  Kwa taarifa hii napenda kueleza kuwa sio Vyama vyote vya Kijamii na Taasisi za Dini vitakavyofutwa na wala hakuna mpango wa kuanza upya zoezi la Usajili wa Vyama vya Kijamii.  
  Aidha ni vyema ikaeleweka kuwa zoezi linaloendelea kwa sasa halihusiani na Taasisi zinazoelezewa kujiingiza katika masuala ya kisiasa na pia ieleweke kuwa Wizara yetu haihusiki na usajili wa NGO.  Imetolewa na Isaac J. Nantanga 
  MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI 


  0 0

   Winchi likinyanyua basi baada ya ajali ambapo watu 10 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa kutokana na ajali ya basi la Unique na lori kugongana uso kwa uso  mkoani Shinyanga leo.
   Zoezi la kunyanyua mabaki ya basi hilo likiendelea
   Simanzi yatawala eneo la ajali
  Winchi likiwa kazini huku wanahabari wkirekodi tukio la kunyanyuliwa basi hilo

  0 0
 • 04/22/15--13:30: Article 3


 • 0 0

   Mfanyabiashara maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
   Alhaji Dangote akiwa na viongozi wa Kijiji cha Mgao pamoja na wananchi akikagua uwanja heka mbili na nusu aliyopewa kwa ajili ya kujenga makazi yake katika kijiji hicho
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja aliopewa  na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na miradi mingine ya maendeleo.
   Msafara wa Alhaji Dangote ukielekea eneo patakapojengwa Bandari.


  0 0

  The six-days Art Exhibition opened officially at the University of Dar es Salaam was described as “professional advancement” with an important role in the field of art. 
   The Vice Chancellor of the University Prof. Rwekeza S. Mukandala observed these remarks when performing the opening ceremony of the exhibition where not less than 134 art works were displayed in the Nkurumah Hall of the University. 
   Speaking to hundreds of professional artists, budding artists from the Fine & Performing Arts Department and members of the public, he said that art works should not only be produced for commercial reasons but should also be for the sake of love of art. He emphasized that efforts should be made to train more experts in this field. 
   The Fine & Performing Arts Department in the University was forty years old and the venue where the Art Exhibition was being held, Nkurumah Hall, had attained the status of Heritage Site. 
  The exhibition was a collection of some 134 paintings in numerous medias, sculptors made with different materials, photography etc. Simple yet attractive paintings, meticulously prepared sculptors with selling prices ranging from TShs. 30,000/= to TShs. 6,720,000/= were on display in the hall. Prominent Artists like Vita Malulu, Muzu Sulemanji, Raza Mohamed, Fred Halla, Suitbert Komba (TASUBA) and many others were present and their works on display. 
   The master piece (my assessment) was a set of three sculptors fabricated by mild steel wires and plastered with discarded black plastic bags portraying a “feasting time for a vulture and hyena on a carcass of buffalo”. 
  The effect of splashed red oil paint (blood) on the half eaten victim and the dramatic fight for the meat chunk was so dramatically made that time and again admirers were seen taking photographs. 
  Strange enough, the title of the show piece was “Election Time” costing TShs. 6,720,000/= for a complete three piece, installation size 3 x 3 metres on the floor. The Artist is called Vita Malulu and has his own studio under the name of Nafasi Art Space at Kijitonyama in dar es Salaam. 
  Principal of the college, Prof. Imani Sanga delightfully described the budding artists as seeds planted and germinated, ready to bring out their best works.
   Veteran Artist Raza Mohamed with of his works in Nkurumah Hall at University of Dar es salaam
   Principal tutor of College of Arts and Culture Bagamoyo Suitbert Komba with his Makonde Carving
   Vice Chancellor Prof. Rwekaza S. Mukandala observes some of the 134 art works exhibited immediately after performing the opening ceremony.
  Artist Vita Malulu with his master piece plastic on wire sculpture of wild animals on feasting time, being most expensive of all art work. STORY & PICTURES: ABDUL HAI

  0 0


  0 0

   Afisa Masoko wa Benki ya Exim (Tawi la Karatu), Bi. Rosemary Meglan (kulia) akikabidhi kasha la gurudumu kwa Waziri Mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye ambaye alikua mgeni rasmi katika mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika Karatu, Manyara hivi karibuni. Benki ya Exim ilikua miongoni mwa wadhamini wa mbio hizo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo.
  Afisa Masoko wa Benki ya Exim (Tawi la Karatu), Bi. Rosemary Meglan (kulia) akikabidhi vipeperushi vyenye taarifa za huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa Waziri Mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye ambaye alikua mgeni rasmi katika mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika Karatu, Manyara hivi karibuni. Benki ya Exim ilikua miongoni mwa wadhamini wa mbio hizo. Wengine ni wafanyakazi wa benki hiyo

  0 0

  Yafuatayo ndio maelezo yake haya:

  "Kwa nianze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu anawezesha yote na kutujalia uhai...

  "Waheshimiwa Mabibi na mabwana,vijana na wazee,watoto na wakubwa, Baba zangu na mama zangu na wanadau wote wanaoishi Moshi na wenyeji wa Moshi walio ndani na nje ya Moshi. Mimi mtoto wenu,mdogo wenu na  Kijana wenu.  DAUDI BABU MRINDOKO

  "Nina heshima kubwa na unyeyekevu kwenu ,Pia nawashukuruni sana kwa kunishawishi niweze kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo
  la Moshi Mjini katika uchaguzi mkuu 2015,nafasi ambayo Ubunge ! ambayo mimi mwenyewe kwa tafsiri ya Ubunge yaani utumishi,mtetezi,msemaji,mwakilishi n.k
  katika baraza la kutunga sheria na katiba yaani Bunge, na katika tafsiri hii ya majina ya kazi hii lazima mtumishi awe mkweli,muwazi na aliyeweka mbele kwanza maslahi ya walio mchagua. 
  "Waheshimiwa Mabibi na mabwana, vijana na wazee, watoto na wakubwa ,Baba zangu na mama zangu Kunishawishi kwenu Kulinifanya niwe kimya kiasi na nikiwa najiuliza maswali mengi kichwani ! Lakini maswali makubwa yalikuwa 3 (a) Nashawishiwa na jamii nichukue fomu kwa kuwa mimi ni kijana mwenywe uwezo wa kuifanya kazi hii?

  (b)Nashawishiwa kwa kuwa kijana niliozaliwa na kuelimishwa na wanao nishawishi? yaani wanachi wa Moshi mjini na ndio wananitambua tabia na uwezo wangu wa kikazi.

  "Swali lingine nililojiuliza ni: Hivi mtoto au kijana mwenye adabu ,Nidhamu na heshima kwa wazee na wakubwa zake walikuwa katika jamii wakimteua au kumtuma kufanya kitu au jambo tena kwa faida na maslahi ya jamii,itakuwa vema kijana huyo akatae? au asikubali kutumwa huko? 
  "Baada ya kujiuliza maswali hayo na mengineyo nimepata jibu ambalo ni: 
           NAKUBALI WITO WENU NA USHAWISHI WENU
  Kuwa nitachukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge 2015 jimbo la Moshi Mjini. Mmenishawishi nami nashawishika na kuthubutu kuchukua fomu ya kugombea ubunge,kwa kuwa siwezi kuwa mvunjifu au mtovu wa adabu kukataa wito na ushawishi wenu ambao wazee wangu,vijana  wenzangu,mama na baba zangu wa Moshi mjini
  mmeniteua kwa kunishawishi niweze kuja kuwa mtumishi wenu mbunge.

  "Kwa kuwa mmenizaa, mmenilea, mmenisomesha mpaka elimu ya juu na mmenishawishi kwa kuwa mnaniamini mimi ni mmoja wenu katika maisha ya kila siku katika jamii yetu Moshi,yanafahamu wazi mahitaji yetu,kero zetu na kipi jamii yetu haitaki na kipi? Jamii yetu inataka hapa jimboni Moshi Mjini,Marekebisho gani ?yanatakiwa hapa Moshi mjini
  ili palete tumaini jema na maana kamili wa wakazi wote jimboni hapa Nayafahamu yote.
  "Nanyi mmemshawishi Kijana Daudi Babu Mrindoko,mtoto wenu  kwa hakika mmetuma mtumishi anayeguswa na yanayowagusa, anayekerwa na yale mnayokelwa ! anafurahishwa na yale mnayofurahia
  "Kwani mwenzenu katika jamii jimboni Moshi mjini.
  Nawashukuruni sana na Asante sana kwa Kunishawishi, Nimeshawishika Nangojea wakati ukifika nami nifuate taratibu zote za kuchukua fomu kupitia Chama tawala"

  "NAKUBALI NITACHUKUA FOMU 2015,KWA NIA YA USHIRIKIANO WETU TULETE MABADILIKO MOSHI MJINI YENYE MASLAHI KWA WOTE"
                  
                         Mungu Ibariki Tanzania!

  Usikose kujiunga nae at www.facebook.com/mrindoko.mwidadi

  0 0

  Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (Katikati) akiongea katika halfa ya kumpongeza mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Airtel Trace Music Stars Afrika kwa kuibuka mshindi wa mashindano hayo na kuiwakilisha vyema Tanzania . halfa hiyo ilifanyika katika ofisi za BASATA Ilala Dar es Saalam. kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.
  Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Vivian Msao Shalua (kulia)akipokea tuzo aliyoipata Nalimi Mayunga mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Afrika. Shughuli hii imefanyika jana katika halfa ya kumpongeza Mayunga kwa kuiwakilisha vyema Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars iliyofanyika katika ofisi za BASATA. Akishuhudia kushoto ni meneja uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando.

  Baraza la sanaa Tanzania BASATA leo limempongeza mwakiliwa wa Tanzania katika mashindano ya Airtel Trace kufatia ushindi alioupata katika mashindano ya muziki yaliyoshirikisha washiriki 13 toka nchi za Afrika .

  Mwisho mwa mwezi wa tatu BASATA ilimkabidh bendera Mayunga na kumpa kibali cha kwenda kushiriki mashindano hayo yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya  na kumtakia kila  laheri katika mashindano hayo ambapo mwakilishi huyu aliweza kufanya vizuri na kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Star wa Afrika.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban  Ki Moon akiwa na  Viongozi wa Madhehebu  mbalimbali ya Dini mara baada ya  viongozi hao wa dini kuzungumza katika mkutano wa ngazi ya juu uliojadili  pamoja na mambo mengi kuongezeka kwa vurugu zitokanazo na itikadi kali za kidini na ukereketwa wa kupindukia na  nini kifanyike kukabiliana na  changamoto hiyo. katika picha hii yupo pia Rais wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutessa ambaye ndiye aliyandaa mkutano huo.
  Na  Mwandishi Maalum, New York
   Kufuatia ongezeko la  makundi ya dini  yenye itikadi , matukio ya  kigaidi,  kukosekana  kuvumiliana na maridhiano,  Katibu Mkuu wa     wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amewageukia viongozi wa  madhebu ya  mbalimbali  dini  duniani akiomba busara zao na uongozi wao.

  Amesema, busara na uongozi wa madhehebu  hayo ya dini  unahitajika sana  katika kuhubiri na kueneza kuvumiliana,  maridhiano,  stahimili,  kuheshimiana na kujenga utamaduni wa kuzungumza   miongoni wa  jamii bila ya kujali dini zao au rangi zao.

  SOMA ZAIDI HAPA

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akipata maelezo kwa wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite One, Faisal Juma Shabhai na Hussein Gonga, kuhusiana na uchimbaji wa madini ya Tanzanite, baada ya kutembelea kituo cha kampuni hiyo, katika maonesho ya nne ya kimataifa ya madini ya vito, yanayoendelea Mount Meru hotel.


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu (kushoto) amekutana na wafanyabiashara wa Sweden kwenye mkutano ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika Mashariki(Swedish East Africa Chamber of Commerce)

  Mhe. Balozi Dora Msechu amewahamasisha Wafanyabiashara wa Sweden kuwekeza Tanzania kwa kuwaeleza fursa za uwekezaji zilizopo na mikakati ya Serikali ya Tanzania ya kuboresha miundombinu.
  Sehemu ya Wafanyabiara hao wa nchini Sweden wakiwa kwenye kikao na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu.

  0 0

   Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.

  Na Fredy Mgunda,Iringa

  Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa, Hassani Mtenga amewataka wananchi wa tarafa ya Pawaga katika jimbo la Isimani kuendelea kumwamini Mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea haki kwa kuwaletea maendeleo.

  akizungumza katika mkutano huo, MTENGA amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.

  Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa Vijijini wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji hicho.

  katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA
  akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa
   tarafa ya pawaga
  wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema kuwa kijiji hicho hakina mganga wa kutoa huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi limekuwa kubwa.

  Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa hassani mtenga amewata viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea kukijengea imani chama chao.

  Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo mikubwa katika vijijini.

  Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.

  “Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.

  0 0

   Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yesaya Mwakifulefule  akikabidhi  msaada wa vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mashahriki Bi. Christina Mndeme kwa ajili ya ukarabati wa maabara za shule katika wilaya hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mashahriki Bi. Christina Mndeme akizungumza jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya   Meneja wa Kanda ya Mashariki ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yesaya Mwakifulefule  kukabidhi  msaada wa vifaa vya ujenzi kwa kwa ajili ya ukarabati wa maabara za shule katika wilaya hiyo.
  Picha ya pamoja baada ya makabidhiano hayo.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) ahudhuria Kongamano Kubwa la Biashara kati ya Comoro na Tanzania, litakalofanyika tarehe 23 Aprili, 2015 Visiwani Comoro.

  Lengo kuu la kongamano hilo ni “kuongeza kiwango cha biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro kwa kutambua fursa zilizopo kati ya nchi hizi mbili na kurasimisha biashara ambayo kwa sasa hairatibiwi”.

  Kongamano hilo ambalo litawakutanisha viongozi, maafisa wandamizi wenye dhamana ya kuendeleza biashara kutoka Tanzania na Comoro pamoja na wadau wa Sekta Binafsi, litafungua rasmi fursa ya kutangaza na kuuza bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwa wafanyabiashara watakaopenda kufanya hivyo kutokana na nafasi nyingi za biashara na uwekezaji zilizopo katika Visiwa vya Comoro.

  Miongoni mwa mada ambazo zitazungumzwa katika kongamano hilo ni pamoja na; Mada kadhaa kuhusu fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania na Comoro, mazingira ya biashara za uwekezaji nchini Tanzania na Comoro, fursa zinazopatikana katika nchi hizo na usaidizi wa kiserikali katika kurahisisha baishara. Aidha, itakuwapo fursa ya mazungumzo ya kina kati ya wafanyabiasha wa Comoro na Tanzania (business to business discussions).

  Aidha, zipo fursa nyingi za uwekezaji katika uzalishaji na usindikaji wa bidhaa za kilimo, pamoja uwekezaji katika sekta ya huduma za afya, elimu, mawasiliano na nishati endapo fursa hizi zitatangazwa na kuwekwa miundombinu ya uhakika ya usafiri kati ya Tanzania na Comoro bidhaa za Tanzania zitapata soko la uhakika visiwani Comoro.

  Kongamano hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutoka Tanzania, limeandaliwa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini Comoro, kwa kushirikiana na kampuni ya 361 degrees ya Dar es Salaam.

  Kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya Uendelezaji wa Biashara Tanzania (TANTRADE) ambao wanahamasisha na kuwakaribisha wafanyabiashara wa Tanzania, Exim Bank, Shirika la Ndege la Air Tanzania, Jumuiya ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Wakulima ya Comoro (UCCIA); na Mamlaka ya Kuendeleza Vitega uchumi vya Comoro (INM).
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (Mb) akibadilishana mawasiliano na baadhi ya wafanyabiashara waliowasili Visiwa vya Comoro kwa ajili ya kushiriki katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro, linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili, 2015. Kushoto (mwenye miwani) ni Balozi wa Tanzania Visiwa vya Comoro Bw. Chabaka Kilumanga.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu( Uwekezaji na Uwezeshaji) Mhe. Mhandisi Christopher Chiza (mwenye tai) akishiriki kucheza ngoma ya asili ya Comoro mara baada ya kuwasili visiwani humo.

  0 0  0 0

  Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia.

  =====  ====
  UTEUZI WA MWENYEKITI WA BARAZA LA TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikiwete, amemteua Mhandisi, Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia,  kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tume ya
   Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10 Aprili 2015.  

  Uteuzi huo ni kwa mujibu wa Kifungu Na. 4 cha Sheria Na. 7 ya Mwaka 1986 iliyounda Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia. Mhandisi Kanali Mstaafu Joseph Leon Simbakalia kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Export Processing Zones Authority (EPZA).

  Imetolewa na:

  John Mngodo
  KAIMU KATIBU MKUU
  Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia


  0 0
 • 04/23/15--05:26: UKARABATI
 •  Mafundi wakiendelea na kazi yao ya kuweka karavati katika Makutano ya Mtaa wa Chimala na Albert Luthuli, mbele ya Ocean Road Hospital, jijini Dar es salaam.


  0 0

  Na Veronica Mheta, Arusha

  WAKANDARASI wameaswa kuacha tabia ya kujenga majengo ya serikali pamoja na wananchi chini ya viwango kwalengo la kupata faida kubwa na kuleta hasara kubwa katika nchi.

  Aidha serikali inafanya kila linalowezekana ili kulipa madeni ya wakandarasi wazalendo ikiwemo kupata mikopo ya riba nafuu kwaajili ya kuwezesha wakandarasi kupata zabuni za ujenzi wa majengo makubwa zaidi yanayojengwa na wageni kutoka nchi za nje.

  Kauli hiyo ilitolewa jana Jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Mussa Iyombe wakati alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa nne wa mwaka wa Chama cha Makandarasi Wazalendo Tanzania (ACCT) unaofanyika kwa siku mbili .

  Alisema si vyema wakandarasi kufanya kazi kwa kutaka faida kubwa na kupelekea hasara kwa wananchi pamoja na serikali kwani ufanyaji kazi kwa kulipua unashusha heshima katika fani hiyo sambamba na kuleta hasara kwa serikali kwani baadhi ya majengo yanajengwa chini ya viwango.

  Pia alisema hivi sasa serikali imefanya mazungumzo na Gavana wa Benki Kuu (BoT) kwaajili ya kuwasaidia wakandarasi waweze kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka serikalini itakayowasaidia kupata fedha na kujenga majengo makubwa zaidi badala ya wageni kutoka nje ya nchi kupata zabuni za kujenga majengo hayo huku wakandarasi wazalengo wakiambulia asilimia 40 tu ya ujenzi.

  “Naomba msibabaike na faida kubwa na kuleta hasara kwa Taifa angalieni uzalendo lakini najua mnaidai serikali fedha nyingi ila tuko mbioni kuwalipa madeni yenu na pia hivi sasa serikali itatoa mikopo yenye unafuu ili muweze kujenga majengo makubwa ya kisasa badala ya wageni kujenga maana wakipata faida wanarudisha kwao huku wakandarasi wazalendo wakiambulia kazi za matengenezo madogo madogo”.

  Naye Mwenyekiti wa ACCT, Mhandisi Milton Nyerere alisema kuwa chama hicho kipo katika hatua ya kuanzisha chuo cha ufundi kwaajili ya kukuza uwezo kwa kuendesha mafunzo ya fani mbalimbali za kikandarasi kwa mafundi wa makampuni ya makandarasi ili kupunguza changamoto ya wataalam wanayokumbana nayo kwenye utekelezaji wa miradi.

  Aliongeza kuwa chama hicho kinajumla ya wanachama 78 na kimekuwa na mahusiano mazuri na Bodi ya Wakandarasi (CRB)na wadau mbalimbali katika uimarishaji wa ubora wa kazi sambamba na kuanzisha taasisi ya fedha benki kwaajili ya makandarasi wazalendo ili kuwasaidia kupambana na changamoto ya mitaji.

  0 0

  Kiongozi wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) katika Makazi ya Mishamo, Adolph Bishanga akimkabidhi chandarua na shuka raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses (kulia) baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na UNHCR kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.
  Mkuu wa Makazi ya Ulyakulu, Abdulkarim Mnacho (kushoto) akimpongeza raia mpya wa Tanzania, ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kapemba, Kata ya Mishamo, wilayani Mpanda, Ageva Moses baada ya kujifungua mtoto wa kiume wakati akiwa katika kituo cha kupokelea cheti cha uraia katika Kijiji cha Ifumbula wilayani humo. Licha ya maafisa wa Serikali pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) kutoa maelekezo kuwa wagonjwa na wasiojiweza wote wakiwemo mama wajawazito kusubiria vyeti hivyo nyumbani watakapopelekewa lakini baadhi ya raia hao wapya wasiojiweza wanafurahia kuja wenyewe katika vituo vya kupokelea vyeti.


older | 1 | .... | 812 | 813 | (Page 814) | 815 | 816 | .... | 3348 | newer