Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live

DIRA YA DUNIA NA BBC SWAHILI LEO


MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SAFA

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Afrika Kusini (SAFA) Dr.Danny Jordan kufuatia kifo cha nguli aliyewahi kuichezea timu ya Taifa ya nchi hiyo (BafanaBafana) John Lesiba "Shoe" Mashoeu kilichotokea jana Aprili 21.

Katika salamau zake kwa Dr. Jordan, Malinzi amesema nchi ya Afrika Kusini imepatwa na pigo kubwa katika tasnia ya mpira wa miguu, kufuatia kifo cha  Mashoeu aliyefariki dunia kwa ugonjwa wa Kansa ya Utumbo, na  kusema watanzania wako nao pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo.

John Lesiba "Shoe" Mashoeu aliyezaliwa Disemba 18, 1965 nchini Afrika Kusini, alikuwa ni miongoni wa wachezaji wa nchi hiyo waliotwaa Ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) mwaka 1996 nchini Afrika Kusini na baadae kushiriki fainali za Kombe la Dunia nchini Ufaransa mwaka 1998.

Wakati wa uhai wake Mashoe alipata kuvichezea vilabu vya Giant Blackpool, Kaizer Chiefs, Amazulu na Alexandria United vya Afrika Kusini, na timu Gencleribirligi, Kocaeilispor, Fenerbahce na Busrsapor za Uturuki.

Dog For Sale

$
0
0
 Puppies Details:
Specie: German Shepherd
Gender: Female
Age: 2 Month (Puppies)
Immunization: Distemper; Canine Viral Hepatitis;  Leptospirosis;  Parvovirus and Rabies
Clinic card: Available
Pedigree: Very Good
Contact: 0713353939




KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUKUTANA DAR ESSALAAM KUANZIA TAREHE 26 APRILI HADI 9 MEI, 2015

PUBLIC ANNOUNCEMENT: WIA COM GETS NEW BOSS

$
0
0

 WIA GROUP is delighted to announce the appointment of Mr. Patrick Nyindo (pictured above) as the new Managing Director of WIA Company Ltd, effective April 1st, 2015.
Patrick is an experienced professional who brings many years of knowledge, skills and leadership in telecom, information and online businesses, with a primary focus on connectivity services. 
As the Commercial Director at WIA Company, he was responsible for Business Development and Sales with a focus on growth of enterprise connectivity in various broadband and data service operations, and was actively involved in the launch and success of a number of new products, many with a strong data and benchmarking component.
Prior to joining WIA, Patrick worked for Sabre Holding, an online media platform based in the United Kingdom. 
Patrick will build on the strong foundation laid by his predecessor and lead WIA into a new phase of development, focusing on managed platforms, fiber outreach and client services.
"WIA Company’s business model and unique assets have us well-positioned to meet the rapidly growing demand for Enterprise Broadband services, I'm excited at the prospect of where WIA Company is headed as we implement our future plans to build a true Hybrid network Fiber and LTE covering up to 30 regions in Tanzania by 2017."– Patrick Nyindo.


51st Anniversary of the Union and National Day of the United Republic of Tanzania

Waziri Membe azungumza na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN eneo la Maziwa Makuu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akizungumza na Mwakilishi  Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, Bw.  Said Djinnit walipokutana kwa mazungumzo tarehe 22 Aprili, 2015. Katika mazungumzo yao waligusia masuala ya usalama katika Ukanda huo hususan hali ilivyo nchini DRC.
Waziri Membe akimweleza jambo Bw. Said Djinnit (katikati) huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilshi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Bw. Alvaro Rodriguez akisikiliza kwa makini.
Waziri Membe (kulia) akiagana na Bw. Said Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Picha na Reginald Philip

NHC NA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM ZATILIANA SAINI MKATABA WA MANUNUZI YA ENEO LA OFISI JENGO LA MOROCCO SQUARE

$
0
0
hc1
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakitiliana saini makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea. (Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii) hc2Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto), akibadilishana hati za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa, mara baada ya kusaini makubaliano ambapo DSE itanunua ofisi katika jengo la Morocco Square litakalojengwa na shirika hilo eneo la Kinondoni jijini. Mkataba huo ulisainiwa jijini leo. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BILLIONAIRE MO TO GIVE AWAY $100M THROUGH MODEWJI FOUNDATION

$
0
0
Mo-Dewji_0310-780x350
Mohammed Dewji, head of the $1.25bn MeTL Group and an MP in Tanzania, is set to launch a foundation in May to give away $100m of his fortune.

Dewji – ranked 31st richest person in Africa last year by Forbes – plans to gift around $2m from his fortune to the Mo Dewji Foundation on its launch, gradually building up the endowment fund to some $100m, he told Philanthropy Age.

“I earned my money in Africa,” said Dewji. “It is my responsibility and priority to give back.

The foundation will start with work across Tanzania, with the aim of extending its reach into other African countries. The focus areas of the foundation are still being developed, but education, healthcare, water access and enhancing purchasing power for the very poor are all being considered. 

The timeframe by which the foundation will reach its $100m target is still being decided, he added.

Mh. Anne Kilango aitaka Bodi ya Mikopo kutoa elimu zaidi kwa wadaiwa

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kulia) akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majuku ya Bodi kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela leo (Jumatano, Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Emma Sabaya (kushoto) leo (Jumatano, Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.
Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na TEHAMA wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Asangye Bangu (mwenye tai ya njano) akimweleza Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela (kulia) jinsi kumbukumbu za waombaji wa mikopo zinavyohifadhiwa katika Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015). Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA UNI WI-FI

$
0
0
Wakwanza kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga akiwa ameshilia bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti maalum kwa wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael
Afisa masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua huduma hiyo chuoni hapo jana.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza (hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.

AIRTEL YAZINDUA HUDUMA YA UNI WI-FI

$
0
0
·        Wanafunzi chuo kufurahia Uni Wi-Fi kwa kifaa kinachotumia Wi-Fi
·        Uni Wi-Fi ya Airtel kupatikana kwa laini ya mtandao wowote
 Kampuni ya simu za mkono ya Airtel Tanzania katika muendelezo wa kutoa huduma bora na nafuu nchini imezindua huduma mpya ya kisasa ya UNI Wi-Fi itakayowaweza wanafunzi vyuoni kufurahia huduma ya Intaneti yenye kasi zaidi
Akiongea wakati wa uzinduzi uliofanyika chuo kikuu cha SAUT Mwanza Meneja Mauzo wa Kanda ya Ziwa Bw, Raphael Daudi alisema “huduma ya Airtel UNI Wi-Fi tumeianzisha kwaajili ya kuwapatia wanafunzi huduma nafuu ya intaneti yenye kasi zaidi wakati wanapofanya shughuli zao za masomo au wanapoingia katika mitandao ya jamii kupata taarifa mbalimbali muhimu”
Ulimwenguni Intaneti sio kitu cha anasa tena na pia kutokana na  kasi ya  uhitaji wake kwenye mambo ya maendeleo ya uchumi na kijamii kwenye makundi tofauti vikiwemo  vyuo vya elimu ya juu Airtel tumeona ni vyema  kuja na ubunifu huu kuleta suluhisho kwenye kuwahudumia wateja wetu”
Leo huduma ya intaneti kupitia Airtel UNI Wi-Fi hapa Chuo cha St, Augustine Mwanza (SAUT) ni rahisi na nafuu kabisa kupitia Airtel
Kwa Upande wake Meneja Masoko wa Huduma hiyo Bi, Aneth Muga amesema “Airtel Uni Wi-Fi tunayozindua leo nimuendelezo wa mikakati yetu ya Airtel kutoa huduma nafuu kwa wanafunzi,  mwishoni mwa mwaka jana pia tulizindua Uni 255 vocha kwenye vyuo mbalimbali ili kuwapatia huduma ya bando za Intaneti, SMS pamoja na muda wa maongezi nafuu zaidi kuliko zote”
Leo hii Wi-Fi vocha ipo ya Siku, Wiki, Mwezi au bando la usiku kwa gharama nafuu ya hadi shilingi mia tano kwa GB 1 kwa siku.
Unachotakiwa kuwa nacho ili kufaidi huduma hii ni kuwa na kifaa chochote kinachoweza kutumia Wi-Fi kama vile smartphone, laptop, tablet, Camera, printer na utaunganishwa bila kujali unatumia laini ya Airtel au mtandao wowote.
“Leo tumeanzia hapa SAUT lakini tutahakikisha inasambaa vyuoni kote na baadae nchi nzima ili vijana na wale wote wanaokwenda na wakati waweze kufaidika nayo katika matumizi ya kimtandao” alimaliza kusema Bi Muga
Kwa upande wake mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa Chuo hicho Bw, Liberatus Ndegeulaya alisema “hapa chuoni SAUT tumefarijika sana kuona Airtel mara zote mnaanzia kwetu mnapotaka kuzindua huduma hizi rafiki kwa mawasiliano. Kwa elimu ya sasa hii Wi-FI ni muhimu sana inarahishia wanafunzi wetu na hata sisi walimu katika ufundishaji”
Natoa wito kwa wanafunzi wote kuitumia Airtel Wi- Fi kama nyenzo ya kufikia mmalengo ya elimu yao
Nae Raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura aliishukuru Airtel huku akiitikia wito wa kuitumia huduma hiyo kwa manufaa ya kupandisha kiwango cha elimu nchini  sambasamba na ukuaji wa teknolojia mbalimbali.
“Asanteni Airtel kwa ubunifu huu na kuleta Airte Wi-Fi sisi wanafunzi tutahakikisha tunajiwekea utaratibu wa kuitumia katika utaratibu unaofaa na wenye manufaa ya kwa elimu nan chi yetu’ alisema Wambura Raisi wa wanafunzi SAUT
 Afisa masoko wa Airtel bw, Prospa Mwanda akitoa maelekezo ya jinsi huduma mpya ya Airtel Wi-Fi inavyofanyaka kazi kwa kasi kwa Raisi wa wanafunzi chuo kikuu cha SAUT mwanza Bw, Sogone Wambura (wakwanza kulia) na Makamu wa Raisi wa chuo hicho Bi, Pearl Mecar (kati) mara baada ya Airtel kuzindua huduma hiyo chuoni hapo jana.
  Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga akionyesha kwa wanafunzi wa SAUT Mwanza (hawapo pichani) muonekano wa vocha za huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti iliyozinduliwa chuoni hapo jana maalumu kwaajili ya kuwapa wanafunzi intaneti nafuu na yenye kasi zaidi.
 Mshauri wa wanafunzi chuo cha St. Augustine Mwanza (SAUT) akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) kuitumia vyema huduma iliyozinduliwa na Airtel ya Wi-Fi intaneti ili kutimiza uhitaji wao katika masomo na kuongeza ufaulu chuoni hapo. Hafla ya uzinduzi ilifanyika chuoni hapo jana
Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga (kulia) akiwa ameshikilia bango linaloonyesha huduma mpya ya Airtel Wi-Fi intaneti  maalum kwa wanavyuo iliyozinduliwa rasmi kwa mara ya kwanza Mwanza katika chuo cha St Augustine (SAUT) pamoja nae anaefuata ni raisi wa serikali ya wanafunzi Sogone Wambura, Mshauri wa wanafunzi chuoni hapo bw,Liberates Ndegeulaya na Afisa masoko wa Airtel Mwanza Bw, Emanuel Raphael

KITUO CHA HUDUMA ZA SHERIA ZANZIBAR (ZLSC) CHATOA Mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama ya Kadhi juu ya ulinzi wa Mtoto Zanzibar

$
0
0
 Kituo cha huduma za Sheria kimetoa Mafunzo kwa Maafisa wa Mahakama ya Kadhi juu ya ulinzi wa Mtoto Zanzibar leo hoteli ya Mazsons, Shangani, Zanzibar. Juu nia baadhi ya Mashekh wakisikiliza mada katika mkutano uliondaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
MRATIBU wa mafunzo  ZLSC Gabriel Mkama akitoa maelekezo katika mafunzo hayo.
Sheikh Khamis Abdul hamid akiwasilisha maada ya malezi ya mtoto.
Afisa habari wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Suleiman Abdulla akitoa ufafanunuzi.
Sheikh akichangia katika mkutano huo.

ZIFF 2015 ANNOUNCES OFFICIAL FILM SELECTION

KAMATI YA MAWASILIANO NA UJENZI YA BARAZA LA WAWAKILISHI YATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO INAYOTEKELEZWA NA IDARA YA NJIA ZANZIBAR

$
0
0
 Wajumbe wa kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza la Wawakilishi wakitembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa  na Idara ya Ujenzi wa Barabara (UUB). Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakwanza  (kushoto) Mahmoud Muhammed Mussa akiwa na wajumbe wenzake na watendaji wakuu wa UUB wakikagua barabara ya Chaani iliopo Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja.
 Mhandisi Mkuu  wa UUB  Eng. Cosmas Masolwa akitoa maelezo  kwa wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi  ya Baraza la Wawakilishi juu ya ukarabati unaoendelea wa  kuihami njia ya Chaani kwa kuwekewa kifusi kabla ya kukamilishwa  ujenzi wake kwa kiwango cha lami hap baadae.
 Sehemu ya barabara ya Chaani  iliyotembelewa na Kamati  hiyo  ambayo inafanyiwa matengenezo ya kutiwa kifusi  ili weze kupitika huku ikisubiri ujenzi wake kwa kiwango cha lami hapo baadae. 
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

Mhe Anne Kilango Malecela aitaka Bodi ya Mikopo kutoa elimu zaidi kwa wadaiwa

$
0
0

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja Upangaji Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Emma Sabaya (kushoto) leo (Jumatano, Aprili 22, 2015) jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

 Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na TEHAMA wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Asangye Bangu (mwenye tai ya njano) akimweleza  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela (kulia) jinsi kumbukumbu za waombaji wa mikopo zinavyohifadhiwa katika Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015). Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Hamisi Chagonja akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Anne Kilango Malecela jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Aprili 22, 2015). Naibu Waziri alifanya ziara ya kikazi katika Bodi hiyo na kukutana na uongozi wa Bodi.

DUKA LA NAKIETE LATOA MSAADA HOSPITALI YA SINZA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada kutoka Kwa  Mkurugenzi wa Duka la Dawa la Nakiete Bi Batilda.
Duka la Dawa la Nakiete Limetoa msaada katika Hospitali ya Sinza.Vitu Mbalimbali vilitolewa na duka hilo vyenye Dhamani ya Shilingi milioni 6.Mkurugenzi wa Nakiete Akieleza zaidi kuhusu msaada huo amesema hiyo ni sehemu ya faida waliyopata kwa Mwaka uliopita wakaona ni vema kurudisha sehemu ya faida hiyo kwa jamii.Alisema Hospitali inakabiliwa na changaamoto nyingi lakini wao wameona wasaidie kile kidogo walichopata. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipokea Msaada 

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akiwa katikati ya wakinamama alipowatembelea kuwajulia hali na kuwapa zawadi.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akiwa wodi ya wazazi Akimpa Mmoja wa wakinamama waliojifungua jana sehemu ya zawadi zilizotolewa na Duka la Nakiete Ambapo zaidi ya wakinamama 40 waliokuwa wamelezwa katika wodi hiyo walinufaika
Baadhi ya wakina mama waliotembelewa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh Makonda 

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akishukuru kwa Msaada huo amewapongeza kwa moyo waliouonyesha wa kujitolea kwajili ya wananchi maskini wa tanzania.Aidha Mkuu wa wilaya amesema Nakiete wameonyesha mfano kwa kujitolea kwasababu wa Pamoja na kulipa kodi bado wameona umuhimu wa kujitolea kwa jamii ya tanzania tofauti na wachache wanaoikosesha serikali kwa kukwepa kodi na bado hata hawawakumbuki hata Wananchi maskini wa tanzania.

NHIF NA PSPF WATOA ELIMU KWENYE MKUTANO MKUU WA VIONGOZI WA CWT MKOA WA LINDI

$
0
0
 Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Fortunata Raymond akitoa elimu kuhusu maboresho yanayoendelea kufanywa na mfuko mbele ya viongozi na wawakilishi wa chama cha walimu mkoa wa Lindi,wakati wa mkutano wa mwaka wa chama hicho,ambapo alisema kwa sasa katika kukabiliana na changamoto ya huduma ya dawa mfuko umeanzisha mkopo wa dawa na vitendanishi kwa vituo vilivyosajiliwa na mfuko, ambapo bodi ya wakurugenzi iliridhia kutolewa kwa mikopo hiyo tangu mwezi Oktoba.2014.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Chamikumbi mkoani hapa.
 Wajumbe wa mkutano wa mkuu wa chama cha waalimu mkoa wa Lindi wakimsikiliza meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya (hayupo pichani)Fortunata Raymond wakati akifafanua mikakati mbalimbali inayotekelezwa na mfuko katika kuhakikisha wanachama wa mfuko wanapata huduma stahiki na bora zaidi.

 Fabiani Erioh mwakilishi wa shule za msingi Lindi vijijini kwenye mkutano mkuu wa viongozi wa CWT, akitoa hoja baada ya mada zilizowasilishwa kutoka kwa mwezeshaji wa mfuko wa Taifa wa Bima ya afya.
 Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Lindi Ramadhan Mtumwa akifafanua mafao yanayotolewa na mfuko huo mbele ya viongozi wa CWT mkoani hapa,ambapo alibainisha ubora mafao hayo kama vile fao Elimu,fao la uzazi,mikopo ya nyumba sanjari na mkopo wa kuanza maisha pale mwanachama wa mfuko anapopata ajira,hivyo alitoa wito kwa wanachama kuiona kuwa ni fursa. 
Kutoka kulia ni meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Fortunata Raymond akichukua dondoo za hoja kutoka kwa wanachama wa mfuko,kushoto ni meneja wa PSPF Ramadhan Mtumwa mkoani Lindi akifuatilia kwa karibu.

Serikali ya Tanzania na Korea ya Kusini zakubadilishana uzoefu katika masuala ya uwekezaji

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda akifungua kongamano kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
Baadhi ya wajummbe kutoka nchini Korea ya Kusini wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati alipokuwa fungua kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
 Baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia mjadala wakati wa kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Korea ya Kusini ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu.
Picha ya pamoja ya wajumbe kutoka Tanzania na Korea ya Kusini walioshiriki kongamano la siku moja lililofanyika leo jijini Dar es salaam kuhusu masuala ya uwekezaji ili kubadilishana uzoefu na kushirikiana katika kuinua uchumi wa nchi zote mbili kwa kushirikisha sekta ya Umma na sekta binafsi katika kujiletea maendeleo endelevu. Kutoka kushoto walioketi ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Prof. Adolf Mkenda. Picha na Wizara ya Fedha

NDONDO CUP YANUKIA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Mkoani Arusha mwishoni mwa juma hili kunataraji kufanyika michuano ya NDONDO CUP itakayoshirikisha jumla ya timu nane kutoka mkoani hapa.

Lengo la michuano hiyo ni kuwakutanisha wapenda soka mkoa wa Arusha pamoja na kuwapa nafasi wa  mashabiki wa mchezo huo Mkoani hapa kukutana sehemu moja.

Michuano hii itaanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa ya tarehe 24/04/2015 na kufika tamati siku ya jumapili.
Mshindi wa kwanza katika michuano hii atapata zawadi ya fedha taslimu shilingi laki tano (500,000) pamoja na kikombe, mshindi wa pili atajipatia fedha taslimu shilingi laki tatu (300,000).

Timu zitakazoshiriki katika michuano ya NDONDO CUP 2015 ni FFU OLJORO, TANZANITE SPORTS FOUNDATION, RED STAR, TANZANITE VETERAN, LEMARA BOYS, NJIRO SPORTS, SMALL NYOTA na UMBRELA GARDEN.

Ratiba katikIMA MICHUANO HIYO NI KAMA IFUATAVYO

FFU OLJORO VS TANZANITE SPORTS CLUB, TANZANITE VETERAN VS RED STAR, LEMARA BOYS VS UMBRELA GARDEN, NJIRO SPORTS VS SMALL NYOTA
Michezo yote itapigwa siku ya ijumaa kwa mfumo wa bonanza na nusu fainali itakuwa siku ya jumamosi wakati mchezo ya fainali utapigwa siku ya jumapili.

Michuano hii itafanyika katika uwanja wa AICC uliopo karibu na round about ya KIJENGE. muda ni kuanzia saa 4 asubuhi mpaka 12 jioni.

Katika michuano hii kutakuwa pia na burudani toka kwa bingwa wa kucheza na baiskeli dunia (BMX CHAMPION) VICK GOMEZ, pamoja na wasanii wa Bongo flava akiwemo G NAKO, CHABA, KINGS, na mchekeshaji KATARINA.

Kwa mawasiliano zaidi 0759858586
Akida Kilango – mratibu wa mashindano
Viewing all 110114 articles
Browse latest View live




Latest Images