Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" kesho (Jumatatu), usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda

$
0
0
NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. 
Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda

Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO

$
0
0
 Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
 Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
 Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
 Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto

NYALANDU: UMOJA WETU NDIO UTATUFANYA TUSONGE MBELE

$
0
0
Waziri wa maliasili na utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na aliyewahi kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Joshua Kileo (Kulia)  baada ya ibada katika kanisa la KKKT Mjini Kati siku ya Jumapili.
************
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema pamoja na mitihani mikubwa ambayo taifa inakabiliana nayo, umoja wa Watanzania utaifanya nchi isonge mbele kama taifa linalozingatia sheria na demokrasia.
Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili ya Pili ya Pasaka iliyofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mjini Kati jana, Nyalandu alisema nchi itafanikiwa kupita mitihani hiyo kama wananchi wataimarisha umoja kati yao.
“Nchi inapita huku kukiwa na mambo mengi makubwa kufanya…kila mmoja anahitaji amani na hiyo tunaweza kuipata au kufanikiwa kupita salama iwapo tutakuwa na umoja.
“Nchi yetu itasimama, itashinda mitihani ambayo tunayo kama ya uandikishaji wa wapiga kura katika daftari la kudumu, upigaji wa kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu,” alisema.
Mapema katika mahubiri yake kanisani, Mteolojia Solomoni Dereva, aliwaomba Watanzania kuliombea taifa kwa Mungu ili liweze kupita kwa utulivu katika kipindi hiki chenye mambo makubwa.
“Tumuombe Mungu pia atuletee viongozi wazuri, wenye sifa ambao watatutoa hapa tulipo na kutufikisha mbele zaidi katika maendeleo,” alisema.
Alisema kiongozi mzuri ni sawa na mchungaji mwema ambaye huanza kuchunga nafsi yake dhidi ya matendo maovu kama rushwa na ubinafsi na pia huchunga familia yake na ofisi aliyokabidhiwa ili kuwatumikia wananchi.

ZITTO ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO WALEMAVU WA NGOZI, MACHO NA MASIKIO SHINYANGA

$
0
0
Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akizungumza na mtoto mwele ulemavu wa ngozi kwenye kituo cha kuwahifadhi cha Buhanginja Mkoani Shinyanga jana
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira, katikati akiwa na viongozi wenzake Taifa  wakitembelea mabweni  kwenye kituo cha  Buhanginja Mkoani Shinyanga 




Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, akizungumza na watoto walemavu wenye albinism,walemavu wa macho na kusikia waliopo kwenye kituo cha kuwahifadhi cha Buhanginja Mkoani Shinyanga

Balozi seif atembelea Karafuu Beach Resort Spa iliyoungua kwa moto Ijumaa usiku

$
0
0
Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Karafuu Beach Resort  Spa ya Michamvi Wilaya ya Kati umeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wananchi wa Kijiji cha Michamvi Wilaya ya kati kwa juhudi walizochukuwa katika kusaidia kuuzima moto mkubwa uliotokea juzi mnamo saa 10.00 za alfajiri. 
Meneja wa Hoteli hiyo Bwana Zakaria Juma alitoa pongezi hizo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika Hotelini hapo kuangalia athari ya moto huo kwa lengo la kutoa Pole pamoja na kuufariji Uongozi na Wafanyakazi wa Hoteli hiyo. 
Bwana Zakaria Juma alisema licha ya baadhi ya vitu na vifaa vya Hoteli hiyo kuathiriwa na moto huo lakini juhudi na uungwana ulioonyeshwa na Serikali pamoja na Wananchi ambao ulipelekea kutopotea kwa kitu chochote kilichobakia kwenye kizaa zaa hicho umeleta faraja kwao pamoja na wageni waliokuwemo kwenye Hoteli hiyo. 
Meneja huyo wa Karafuu Beach Resort Spa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba moto huo ambao hadi sasa haujatambulika chanzo chake pamoja na hasara iliyopatikana umeteketeza vyumba 35, Ghala, Duka, Sehemu ya Mapokezi na Mkahawa wa Hoteli hiyo. 
Alisema vyumba 70 kati ya 135 vya hoteli hiyo vimesalimika baada ya juhudi zilizochukuliwa kwa pamoja kati ya Wananchi na Wafanyakazi wa Hoteli hiyo kwa kujaribu kuzunguushia mabati eneo la kusini la Hoteli hiyo.
 “ Hoteli yetu imejigawa katika maeneo mawili ya vumba na huduma zote. Lipo lile tunaloliita Masai ambalo ndio lililoteketea kwa moto na jengine lililosalimika ni lile liitwalo Bondeni “. Alifafanua Bwana Zakaria Juma. 
Alifahamisha kwamba Uongozi wa Juu wa Hoteli hiyo umefikiria kuandaa mpango maalum wa kufanya matengenezo mapya ya eneo lililoathirika na kuendelea kutoa huduma kama kawaida ifikapo mwezi wa saba mwaka huu. Bwana Zakaria Juma alisisitiza kwamba huduma za kupokea wageni zinaendelea kama kawaida katika eneo la Bondeni ambalo halikuathirika na moto huo. 
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole na kuwafariji wafanyakazi na Uongozi wa Hoteli hiyo aliwataka kuwa wastahamilivu katika kipindi hichi kigumu ambacho kimeleta usumbufu kwa wageni wao. 
Balozi Seif ameupongeza Uongozi wa Karafuu Beach Resort Spa kwa umakini wake wa kuuwekea Bima mradi wao jambo ambalo litasaidia kupunguza machungu kutokana na hasara hiyo. 
Hata Hivyo Balozi Seif alitahadharisha kwamba ipo haja kwa Uongozi huo kufikiria namna ya ya kubadilisha matumizi ya makuti katika uwezekaji wa majengo ya Hoteli hiyo ambayo ni hatari wakati linapotokea janga la moto. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia wawekezaji wa miradi yote ya Kiuchumi na maendeleo kwamba itakuwa pamoja katika kuisaidia wakati inapopata matatizo .
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa na mwenyeji wake Meneja wa Karafuu Beach Resort Spa Bwana Zakaria Juma wakiangalia baadhi ya majengo yaliyoteketea kwa moto alfajiri ya siku ya Ijumaa.
 Maneja wa Hoteli ya Karafuu Beach Resort Bwana Zakaria  Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif katika maeneo yaliyoathirika na moto kwenye Hoteli yake iliyopo katika Kijiji cha Michamvi Wilaya ya Kati.
 Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto usiku wa kuamkia juzi na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
 Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua kwa moto
Baadhi ya Majengo ya Haoteli ya Karafuu Beach Resort Spa ya Michamvi yaliyoungua. 

Harakati za kuanzishwa kwa Kariakoo Family Foundation (KFF)

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kariakoo Family Foundation (KFF) Mohamed Bhinda akiongoza kikao cha Kamati ya Utendaji katika kuandaa rasimu ya katiba ya chama hicho kinachotarajiwa kusajiliwa  hivi karibuni kama taasisi isiyo ya kiserikali kwa nia ya kukutanisha upya wadau wote waliozaliwa, walioishi na wenye asili ya Kariakoo katika Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam. Mkutano huu umefanyika leo jioni Kinondoni Studio. Kulia kwa Bhinda ni katibu wa chama hicho Senpai Wahid
 Mtunza hazina wa KFF Yahaya Sameja akielezea namna chama hicho cha jamii ya wana Kariakoo kitavyoweza kujiendesha kwa njia za ada, michango na misaada ya wafadhili katika kuendeleza wanachama, ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika shida na raha. Kushoto ni Mwenyekiti wa KFF Mohamed Bhinda na kati ni Makamu Mwenyekiti Tatu Lumelezi
 Wana KFF wakipata mlo wa mchana wakati wa mapumziko
Jopo la kamati ya utendaji ya KFF baada ya mkutano wao leo

Msama afafanua yanayojiri Kituo cha Honoratha

$
0
0

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu taarifa za upotoshwaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Honoratha kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu taarifa za upotoshwaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusiana na Kituo cha Kulelea Watoto Yatima cha Honoratha kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam.

NA LOVENESS BERNARD

MKURUGENZI wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, amesikitishwa na taarifa za upotoshaji zilizotolewa hivi karibuni kuhusu kituo cha kulea watoto yatima cha Honoratha kilichopo wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msama ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, amesema kuwa Kituo hicho ni moja ya vituo anavyovihudumia kila mwezi na hakina tatizo la kuwalaza watoto madarasani, kwani wana vyumba kwa ajili ya malazi na kwamba, picha zilizoonyeshwa  zilipigwa watoto hao wakiwa darasani. 

‘’Nimesikitishwa na taarifa hizi, kwani Honoratha ni moja ya vituo ambavyo ninavihudumia, changamoto zao nazifahamu...Kinalea watoto vizuri na baadhi yao wengine tunawasomesha vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini,” alisema Msama.

Aidha, Msama amevitaka vyombo vya habari kuandika habari za ukweli na uhakika ili kuepuka usumbufu  utakaojitokeza kwa wahusika, ikiwamo kwa mlezi na watoto wanaoishi katika kituo hicho ambao walipata adha baada ya taarifa hiyo kutoka.

Alisisitiza kuwa, taarifa hizo hazina ukweli wowote kwani hata mlezi wa kituo hicho hawakufanya mahojiano naye, ikiwamo kumuuliza kwa nini watoto hao walilala darasani mchana huo.

Msama amekuwa akisaidia vituo mbalimbali vya kulea yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia vyanzo vyake mbalimbali ikiwamo mapato yanayotokana na Tamasha la Pasaka.

Introducing new song "My Self" by Sky Go


The Tanzania Association of Greater Manchester (TAGMA) presents...TANZANIAN NIGHT(USIKU WA MTANZANIA)

$
0
0

DATE: Saturday, 25th April 2015.

TIME: Doors open from 4:00 pm. 5:00pm prompt start till late.
VENUE: Greater Manchester Fire and Rescue Service Training Center,
Cassidy Close,
Manchester,
M4 5HU.
EVENT: Tanzanian Union Day (51 years)
DRESS CODE : African Attire
TICKETS: £10 each for adults and free for children.

Your entrance ticket will enable you to receive a plate of Tanzanian food for adults, children will eat for free.


A cash bar will be available. There will be children's games and Raffle prizes to be won. Tanzanian music will be provided (Bongoflava, Taarabu, mduara etc)

Come one, Come all.


Regards,



Bravo Mkony
Chairman
TAGMA



For more information please call or text : 07880994315

MSAGA SUMU NA YAMOTO BAND WALIVYOTIKISA BONANZA MAALUM

MAKALA YA SHERIA: NI MAKOSA KISHERIA TAASISI YA FEDHA KUUZA NYUMBA YA DHAMANA KWA BEI YA KUTUPA

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.
Kumekuwa  na  tabia  ya  taasisi  za  fedha  kuuza  nyumba   au  viwanja vya  watu  walivyoweka  rehani   na kushindwa  kulipa  mkopo   kwa  bei  ya  kutupa. Kwakuwa  taasisi  za  fedha  huamini  kwamba  wana  deni na  mtu  na ameshindwa  kulipa  hela  zao  na  pengine  kwakuwa  tayari  wamekamilisha  taratibu  zote  za  kisheria  za  kuuza  basi  huamua  kuuza  mali  ya  mtu  kwa  bei   ambayo    ni  ndogo   kiasi  cha  kustaajabisha.  

 Ni  kawaida  kukuta  nyumba ya  milioni  mia  ikiuzwa  hata  milioni kumi  na  tano  ili  kulipia  deni  la  milioni  kumi  na mbili  au  kumi  na  tano.  Watu  wanapaswa kuelewa  kuwa hili  si  sawa  na  sheria  imekataza    jambo  hili. Thamani  ya  nyumba  au  kiwanja  iko  palepale  hata  kama  mtu  ameshindwa  kulipa  mkopo.  Si  kweli  kuwa  kwakuwa  sheria  imeruhusu  kuuza  mali  ya  mtu  anaposhindwa  kulipa  mkopo   basi  imeruhusu   kuuza  bei  yoyote  ile  ilimradi  muuzaji  amepata   kiasi  anachodai.  Hili  si  kweli  kama  tutakavyoona  hapa  chini. 

1.WAJIBU  WA  TAASISI  YA  FEDHA  KATIKA  KUUZA  NYUMBA  YA  DHAMANA.  . 
Kwa  kujua  hili  la  kuuza  mali  za  watu  bei  ya  kutupa  Sheria  ya  ardhi  kifungu  cha  133  ( 1 ) kikasema  kuwa  muuzaji  wa  nyumba  iliyowekwa  rehani   ana  wajibu  mkubwa  na  wa  hali  ya  juu  kuhakikisha  anachukua  tahadhari  na  anakuwa  mwangalifu  kwa  kiwango  cha  juu  kuhakikisha    wakati  anapouza   ardhi   ya  mtu anaiuza  kwa  bei  nzuri   na  bei  ambayo  inakubalika  kuwa  bei  inayostahili  kwa  wakati husika.  

Huu  ni  wajibu  wa  kisheria  alionao  muuzaji  au  mnadishaji  wa  ardhi  ya  dhamana.  Kifungu  hicho  kinasema  kuwa  suala  la  kuuza  mali  ya  dhamana  kwa  bei  inayokubalika  ni  haki  ambayo  aliyeshindwa  kulipa  deni  anamdai  muuzaji/mnadishaji.  Kwa  hiyo  wewe   unayedaiwa  unamdai  huyo  mnadishaji  anayetaka  kuuza  nyumba  yako  haki  ya  kuuza  hiyo nyumba   katika  bei  inayokubalika ( reasonable  price). 

2. NYUMBA/KIWANJA  KIUZWE  BEI  GANI  KWA  MUJIBU  WA  SHERIA ? 
Sheria   ya  ardhi  haikutaja  moja  kwa  moja   ni  kiasi  gani nyumba   ya  mtu  au  kiwanja  kinatakiwa kuuzwa. Hii  ni  kutokana  na  utofauti  wa  thamani  wa  mali  hizo  na  hivyo  isingekuwa  rahisi  kusema  kuwa  bei  ya  mwisho  ya  nyumba  au  kiwanja  ni  kiasi  fulani.  Ili  kuliweka  sawa  hili  kifungu  hichohicho  cha  133( 2 ) kikasema  kuwa   nyumba/kiwanja  cha  mtu   hakitakiwi  kuuzwa    25%    ya   bei  ya  soko   ya  nyumba  au  kiwanja   hicho  kwa  wakati  huo  au  chini  yake.

KINANA ASHIRIKI JOGGING KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.

$
0
0

MEYA WA KINONDONI YUSUPH MWENDA AKUTANA NA WAFANYABIASHARA SOKO LA MBURAHATI AAHIDI KUANZA KWA MRADI WA UJENZI WA SOKO JIPYA MWEZI UJAO

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akimsikiliza kwa makini mfanyabiashara wa Kuku katika soko la Mburahati, Mkude Higilo (kulia) wakati alipofanya ziara sokoni hapo kukutana na wafanyabiashara kuzungumzia mradi wa ujenzi mpya wa soko hilo mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge. 
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na mmoja wa wafanyabiashar wa soko la Mburahati wakati wa ziara yake sokoni hapo ambapo alikutana na wafanyabiashar hao kwa ajili ya kuzungumzia mradi w wa ujenzi mpya wa soko hilo mwishoni mwa wiki, Dar es Salaam.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akisisitiza jambo kwa viongozi wa soko la Mburahati wakati alipofanya ziara sokoni hapo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kukutana na wafanyabiashara kuzungumzia mradi wa ujenzi mpya wa soko hilo. Kushoto kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge, Katibu wa wafanyabiashara wa soko hilo, Fikiri Pazi na wafanyabiashara wengine.

BREAKING NEWZZZZZ: Tanzania's Mayunga Nalimi is the winner of Airtel TRACE Music Star grand finale!

$
0
0

 You chose Mayunga Nalimi! Tanzania's contestant seduced you and the judges Akon, Lynnsha and Devyne Stephens. After a finale full of unexpected developments, Mayunga has been one of the only to keep his calm during his performances. That's probably why he fainted just after he heard final verdict!
Mayunga has quickly attracted judges' eyes with great live and acapella performances. He also took advantage of Laurna and Jitey failures in the last round of the finale to take the title back home. 
He will now join Akon in the studio to work on his first single.

A new superstar is born!

Former Tanzania President Benjamin MKAPA moderating The Tana High Level Forum on Security in Bahir Dar-Ethiopia, 18 April 2015


Ngoma azipendazo ankal special request by John Kitime, Abdul Salvador & Kawelee Mutimwana

$
0
0
Masafa marefu na Tancut Almasi Orchestra

Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) sehemu ya kwanza

$
0
0
Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo, nani alimfanya ashawishike na fani hii? Maisha yake kimahusiano je? Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake? KARIBU

WAKAAZI 10 TEMEKE WAINGIA KWENYE FAINALI YA SHIKA NDINGA YA 93.7 EFM

$
0
0
                      Pichani ni uwanja wa Mwembe Yanga Temeke wakati wa  Shindano la Shika ndinga ya 93.7 EFM kwa wilaya hiyo  lililofanyika Jumamosi  tarehe 18 mwezi wa nne mwaka 2015 ambapo washiriki kumi kutoka wilaya hiyo wamefuzu kuingia fainali ya shika ndinga kwa mkoa wa Dar-es-salaam kati yao watano wakiwa wanawake na wengine watano ni wanaume.Shindano hili kwa wilaya hii lilikuwa la aina yake ukilinganisha na wilaya zingine kwa maaana washiriki walishika ndinga huku mvua kubwa ikinyesha jambo ambalo liliongeza ushindani baina yao.

Shika ndinga ni shindano la aina yake linaloandaliwa na redio ya 93.7 EFM kama namna ya  kutoa shukurani kwa wasikilizaji kwa ushirikiano wao ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa redio hiyo ,ambapo washiriki wanatakiwakusikiliza redio ya EFM na kujibu maswali mbalimbali kuhusiana na redio hiyo ili kupata nafasi ya kushika ndinga ya gari ya biashara inayojulikana kama kirikuu kwa muda uliopangwa bila kutikisika, kuyumba ama kutetemeka na mshindi kujishindia gari hiyo ya biashara.


Mchakato wa shindano nzima ulikuwa hivi, wanaume walishika  ndinga  moja na wanawake pia walishika ndinga moja wakiwa wamesimama kwa miguu miwili kwa masaa kadhaa na badae walishika ndinga wakiwa wamesimama na mguu mmoja na hatimaye watano katika kila kundi walifanikiwa kuingia kwenye fainali ambayo itawahusisha washindi wa shika ndinga wa wilaya zote tatu yani ilala , kinondoni na temeke ambao kwa pamoja watashindana kujishindia ndinga ya biashara .fainali ya shika ndinga itafanyika jumapili ya tarehe 26 mwezi huu wa nne hivo watu wengi wajitokeze ili kushuhudia shindano hili la aina yake.


JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM KATA YA SINZA YAWASHUKURU WANACHAMA WAKE KWA KUKIPA USHINDI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiwahutubia wanaccm wa Kata ya Sinza katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru kufuatia kukipa ushindi chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Cholaje akihutubia katika mkutano huo.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia), akielezea mafanikio ya maendeleo ya wilaya hiyo pamoja na changamoto zilizopo. Kushoto ni Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Cholaje.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Askofu Dk Alex Malasusa amuingiza kazini Msaidizi wake Mch. Chediel Lwiza

$
0
0
1a
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa akimuingiza kazini Msaidizi wake Mch. Chediel Lwiza wakati wa Ibada iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wachungaji pamoja na waumini mbalimbali wa KKKT.
2aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akimuingiza kazini Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Godfrey Nkini wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam
4aMkuu wa KKKT Askofu Dk Alex Malasusa akimpongeza Msaidizi wake aliyemaliza muda Mch. George Fupe wakati wa Ibada iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images