Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 807 | 808 | (Page 809) | 810 | 811 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Na Ramadhani Ali –Maelezo Zanzibar 
  Waislamu wa Zanzibar wanaotegemea kutekeleza Ibada ya Hijja mwaka huu wameshauriwa kukamilisha mipango ya safari hiyo mapema ili kuziwezesha Taasisi zinazosafirisha mahujaji kuweza kukamilisha taratibu mpya zilizowekwa na Serikali ya Saudi Arabia. 
  Akizungumza katika Kongamano la mahujaji watarajiwa lililofanyika ukumbi wa Beit al Yamin Malindi, Afisa kutoaka Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Ustaadh Khalid Mohammed Mrisho amesema Serikali ya Saudi Arabia imefanya mabadiliko makubwa ya taratibu za maandalizi ya Hijjah kuanzia mwaka huu. 
  Amesema wamefanya maamuzi hayo baada ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na mahujaji kutokana na vitendo vya udanganyifu vilivyokuwa vikifanywa na baadhi ya Taasisi zinazosafirisha mahujaji kutoka mataifa mbali mbali duniani. 
  “Baadhi ya viongozi wa Taasisi zinazosafirisha mahujaji walikuwa wakiwatoza fedha mahujaji wao kwa ajili ya kulipia Viwanja vya ndege vya Makka na Madina lakini walikuwa hawalipi na mahujaji kuzuiliwa kwa saa kadhaa,”alisema Ustaadh Khalid. 
  Taasisi nyengine alisema zilikuwa zinawaahidi mahujaji kuwakodia nyumba nzuri za karibu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina lakini wanapofika huko huwekwa kwenye nyumba mbovu na wengine hukosa huduma ya chakula. Amesema katika kukabiliana na matatizo hayo Serikali ya Saudia Arabia kuanzia sasa imeziagiza Taasisi zinazosafirisha mahujaji kufanya taratibu zote za maandalizi ya safari, makaazi na matembezi kwa njia ya mtandao na kulipa gharama zote wakiwa nchini mwao. 
  Amesema iwapo taratibu hizo hazikukamilika hujaji atakosa visa ya kuingia Saudi Arabia na atakuwa amekosa kutekeleza ibada ya Hijjah kwa mwaka huo. Ameongeza kuwa mwaka huu nchi hiyo imeweka hadi tarehe 27 Juni kuwa ni siku ya mwisho kukamilisha taratibu za mahujaji na baada ya tarehe hiyo mtandao huo utakuwa umefungwa na itakuwa hakuna njia nyengine. 
  “Lengo la uwamuzi huo wa Saudi Arabia ni kuwaondoshea mahujaji usumbufu usiowalazima wakati wa kutekeleza ibada hiyo,”alisisitiza Ustaadh Khalid. Amewakumbusha mahujaji watarajiwa kuwa waangalifu na mizigo yao wakati wa safari na wanapokuwa nchini humo na watakaporejea kuchukua kiwango cha mizigo kinachokubalika kwenye ndege. 
  Akifungua Kongamano hilo lililoandaliwa na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar (UTAHIZA) Mwenyekiti wa Bodi Sheikh Khamis Abdulhamid amewasisitiza waislamu wenye uweze kutekeleza ibada ya hijja ili kukamilisha uislamua wao. 
  Mwaka huu Tanzania imepewa nafasi 3,000 kupeleka mahujaji nchini Saudi Arabia ambapo ibada hiyo hutekelezwa kila mwaka mwezi wa mfunguo tatu.
   Ustaadh Seif Shaaban akisoma Qur-an tukufu ikiwa ni ufunguzi wa kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Taasisi za Hjja Zanzibar (UTAHIZA) lililowashirikisha mahujaji watarajiwa katika ukumbi  wa Beit al Yamin Malindi Mjini Zanzibar. 
   Katibu wa UTAHIZA Ustaadh Ali Adam akitoa historia ya Umoja huo na kazi zake katika kongamano lililofanyika Malindi Zanzibar.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar  Sheikh Abdulhamid akifungua Kongamano la mahujaji watarajiwa katika ukumbi wa Beit al Yamin Malindi Zanzibar, kulia ni Mwenyekiti wa Umoja huo na kushoto Sheikh Othman Maalim.
   Ustaadh Khalid Mohammed Mrisho akiwasilisha mabadiliko ya taratibu mpya za Ibada ya Hijja katika kongamano la mahujaji watarajiwa lilifanyika Malindi Zanzibar.
   Baadhi ya mahujaji watarajiwa wakimsikiliza Sheikh Othman Maalim alipowasilisha mada ya umuhimu wa kutekeleza ibada ya hija na madhara ya kuchelewesha kutekeleza ibada hiyo katika kongamano liliofanyika Malindi Mjini Zanzibar.
  Hujaji mtarajiwa Abass Imtiyaz akiuliza swali katika kongamano lililoandaliwa na Umoja wa Taasisi za Hijja Zanzibar katika ukumbi wa Beit al Yamin Malindi Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanziba.

  0 0

  ***Mchungaji Kiongozi Ipyana Mwakabonga***

  0 0

  Othman Khamis Ame, OMPR -  ZNZ
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alionya kwamba wananchi wanalazimika kujenga utamaduni wa kuthamini kazi za wabunifu na wasanii kwa kuona fahari kuzilipia bila ya shuruti pale wanapozitumia jambo ambalo ni uungwana na kinyume chake inahesabika kuwa ni wizi. 
  Alisema Serikali kupitia Ofisi ya Hakimiliki, Bodi ya Hakimiliki na Jumuiya ya Hakimiliki Zanzibar { COSOZA } itaendelea kusimamia kazi za wabunifu na wasanii ili kuona kuwa maslahi, nguvu na jasho lao halipotei bure kutokana na ulaghai unaoendelea kufanywa na watu wanaozipora kazi zao. 
  Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa Wabunifu na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar. 
  Alisema Serikali itaendelea kuchukuwa hatua za kisheria za kuwadhibiti wezi hao wasiojali jasho la wenzao, lakini kazi hiyo inaweza kufanikiwa kwa ufanisi zaidi endapo wabunifu na wasanii wenyewe watatoa ushirikiano kwa taasisi zinazosimamia maslahi yao katika kudhibiti wizi wa kazi zao. 
  Alifahamisha kwamba Serikali haipendi kuwabughudhi wananchi wake katika biashara hata kidogo lakini hulazimika kuchukuwa hatua za kisheria mara moja pale ambapo uvunjaji wa sheria unapobainika ili haki ipatikane kutokana na sheria inavyochukuwa mkondo wake. 
  Akitoa Taarifa Msimamizi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Zanzibar Bibi Mtumwa Khatibu Kheir alisema huo ni mgao wa pili wa Mirabaha kwa wabunifu na wasanii wapatao elfu 1124 wa zanzibar. 
  Bibi Mtumwa alisema Ofisi ya Hakimiliki imefanya kazi kubwa na nzuri kwa kushirikiana na kamisheni ya Utalii pamoja na Mamlaka ya Uwekezaji vitega uchumi Zanzibar { ZIPA } katika kuziunganisha kwa wateja kazi za wabunifu na wasanii. Mapema akimkaribisha Mgeni rasmi Balozi Seif, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis Bakar alisema vipaji walivyokuwa navyo wabunifu na wasanii wa Zanzibar ni vyema vikaenziwa na kuheshimiwa kwa faida ya Taifa kwa jumla.
  Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi   wa Kamati ya ugawaji Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na wasanii bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo Ukumbi wa Salama  Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.

  Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar Khamis,Msanii Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo.

  Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi, Mjumbe wa Kamati ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na Mchangiaji bora wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim. Picha na – OMPR – ZNZ.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management wakiwasikiliza walimu wa kujitolea kutoka Restless Development(walioko mbele yao) kuhusu maarifa ya kupata kazi 
   

   Wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management wakifundishwa na walimu wa kujitolea kutoka Restless Development Gemma Bunn (wa kwanza kushoto )na Jonathan Aquilina ( wa pili kulia ) kuhusu maarifa ya kupata kazi. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
  .

  0 0

   Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akisalimiana na mwakilishi kutoka UNICEF katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC.
   
   Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akisikiliza kwa makini hoja iliyokuwa ikitolewa na mwakilishi kutoka CIFF katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC.

   Wajumbe kutoka nchi mbali mbali Duniani wakimsikiliza Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum Mkuya ( hayupo kwenye picha) alipokuwa akiwasilisha mada na kuchangia hoja mbalimbali katika mkutano uliohusu Lishe bora kwa mtoto mjini Washington DC.
   Waziri wa Fedha  Mhe. Saada Salum akitoa mada na kuchangia hoja mbalimbali zinazohusu Tanzania katika mkutano wa Lishe mjini Washington DC. 

  Lishe bora ni msingi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya nchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano ambao ulikuwa unazungumzia kuhusu suala la Lishe (Nutrition).
  "It is important to understand consequences including adverse effects on the child's physical and mental development from conception until it reaches the age of two. These effects are irreversible," he said."Ni muhimu kuelewa madhara yatakayompata mtoto ikiwa mama hata mnyonyesha mtoto huyo ikiwa ni pamoja na athari mbaya juu ya mwili na maendeleo ya mtoto kutoka mimba mpaka kufikia umri wa miaka miwili  kama mtoto hatapat Madhara haya ni kubatilishwa.," Alisema  Mkuya.

  Mkuya aliongeza kuwa, “ Tanzania tunajitahidi sana kupambana na janga hili kwani mama kushindwa kumnyonyesha mtoto kwa miezi sita kunaweza kusababisha utapiamlo na kusababisha kuathiri mamilioni ya watu katika Tanzania, hasa watoto, na hivyo kusababisha magonjwa kuenea na kunyong’onyesha maendeleo ya kimwili na ki akili”.

  “Kwa kuruhusu hali hiyo kunachangia kupunguza uwezo katika kuboresha uwezo wakufikiri, kupunguza nguvu ya  kujifunza na kuwa mbunifu, kuongezeka kwa umaskini, na kasi ndogo katika kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi”.Aliongeza Mkuya.

  Takwimu za mwisho za utafiti wa mambo ya afya  zina onyesha kuwa asilimia 59 ya watoto wenye umri wa miezi 5-59 wana upungufu wa madini,asilimia 33 ya watoto chini ya miaka sita wana upungufu wa vitamin A.  Asilimia 11 ya wanawake wenye umri wa kuzaa yaani  miaka 15-49 wana uzito wa chini, asilimia 41 wana uzito wa chini na upungufu wa madini, wakati asilimia 58 ya mama wajawazito wana upungufu wa madini pia.

  “Katika Tanzania mikoa ambayo inafanya vizuri katika kupambana na utapiamlo ni mkoa wa Kilimanjaro, Mjini magharibi na Mkoa wa Dar es salaam.”  Alisema Mshauri  Lishe wa Rais Jakaya Kikwete”.Dr. Wilbald Lori.

  Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na janga hili, hivyo katika mikutano hii mikakati mbalimbali inapangwa ya jinsi ya kulimaliza kabisa tatizo hili.

  Mikutano hii bado inaendelea na hali ya hewa mjini hapa ni baridi kiasi. 
  Imetolewa na Msemaji :Wizara ya fedha

   Ingiahedi C.Mduma

  Washington DC
  0 0
 • 04/18/15--07:59: TAARIFA KUTOKA TFF LEO
 • MAKUNDI YA RCL
  Jumla ya vituo vitatu vitatumika katika hatua ya makundi kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) itakayoanza Mei 2 mwaka huu , vituo hivyo ni Lindi, Manyara na Sumbawanga huku kila kituo kikiwa na timu tisa;

  Lindi ni Babati Shooting Stars (Manyara), Changanyikeni FC (Dar es Salaam), Coast United FC (Mtwara), FFU Football Club (Dar es Salaam), Kilimanjaro FC (Kilimanjaro), Matai FC (Rukwa), Sabasaba United FC (Morogoro), Small Boys (Singida) na Super Star (Pwani).

  Manyara ni Alliance Schools (Mwanza), Bariadi United (Simiyu), Baruti FC (Mara), Lukirini FC (Geita), Madini SC (Arusha), Mtwivila City FC (Iringa), RAS Kagera FC (Kagera), Small Prisons (Tanga) na Watumishi FC (Shinyanga).

  Sumbawanga ni Abajalo FC (Tabora), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Gunners FC (Dodoma),  Lucent FC (Ruvuma),  Market Place FC (Lindi), Mwanga United (Kigoma), Nyundo FC (Katavi), Tomato FC (Njombe) na Zakhem FC (Dar es Salaam).

  Timu mwenyeji zimeondolewa katika vituo vyao na kupelekwa vituo vingine ili kuondoa masuala ya uzalendo, na kuhakikisha fair play inakuwepo.

  Kila kundi lina timu tisa, na timu itakayoongoza kituo kwa mechi za ligi ya mkondo mmoja ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Ndugu,

  Ninafuraha isiyokadirika kwa hatimaye kufanikisha kazi niliyoianza takriban miaka minne iliyopita kuandika kitabu kinachoainisha mawazo yangu juu ya Tanzania tuitakayo, Tanzania ya mabadiliko, Tanzania ya mapinduzi kuelekea kupata maisha bora kwa kila mtu. Ndani yake nimejaribu kuelezea, kwa kadri nilivyojaaliwa, jukumu la kizazi chetu ni nini haswa? Misingi ya ukombozi wa kiuchumi na kijamii ni ipi haswa? Nini chanzo cha umaskini na utajiri wa nchi? Nini kifanyike ili tuvune na kufaidika na utajiri tulionao? Nini vipaumbele na mbinu za ukombozi tunaoutaka sana sasa? Ni nini yanapaswa kuwa mabadiliko tunayoyatarajia? 

  Katika kitabu hiki naweka mapendekezo ya mfumo mpya wa kuendesha uchumi kwenye nchi zinazoendelea za Afrika kutokana na misingi ya utamaduni asilia wa kiafrika, nazungumzia nguzo nane za mfumo huu, ambao nimeuita 'African Socialism with Capitalist Characteristics'. Kanuni hizi zilizosheheni muundo wa fikra zangu, uliwahi kuitwa 'Kigwanomics' na rafiki yangu Michael L. Wilson (Ph.D.) wakati tukijadili mambo mbali mbali ya kiuchumi na mustakabali wa Africa tunayoitaka akiufananisha na mawazo ya watu wengine mashuhuri duniani waliowahi kusimamia mabadiliko kwenye nchi zao na kufanikiwa, kama Ronald Reagan (Reaganomics) ama Thaksin Shinawatra (Thaksinomics). Nami nilipenda kuazima style hii na kukiita kitabu changu, Kigwanomics.  

  Katika kitabu hiki utasoma uchambuzi wa mawazo ya waandishi mashuhuri duniani kama akina Mchumi Prof. Paul Collier (The Bottom Billion n.k.), Dr. Chika Onyeani (The Capitalist Nigger), Why Nations Fail (Drs. Robertson and Acemoglu), What went wrong with Africa (Roel van der Veen), Dead Aid (Dr. Dambisa Moyo), Towards the African Renaissance (Prof. Cheikh Anta Diop) na wasomi wengine wa Africa.  

  Imani yangu ni kwamba nimetoa changamoto ya namna mpya ya kufikiria juu ya mapinduzi ya upili (Secondary revolution) kuelekea Tanzania iliyozaliwa upya (Tanzanian Renewal). Lengo kuu la mawazo yangu kwenye kitabu hiki ni hili. Kama ukisoma na ukaona upya wa mawazo yangu, na haja ya kuiunda upya Tanzania Tuitakayo basi nitakuwa nimefanikiwa. 

  Kitabu kitazinduliwa rasmi taratibu zitakapokamilika na tutakujulisha. Nimeandika kitabu changu kwa lugha ya kiingereza, na tayari kuna timu, inayoongozwa na Ndg. Prince Bagenda, inafanyia kazi tafsiri ya kiswahili, na kuna wataalamu wanaofanya kazi ya kuandaa 'popular version' ya kitabu hiki kwa lugha ya kiswahili ili kufikisha mawazo haya kwa haraka na kwa watu wengi zaidi. Ikikamilika kazi hii ndipo tutatangaza siku, mahala na saa ya kukizindua rasmi. Kwa sasa kinauzwa kwa bei ya 'promotion' ya TZS 5,000 kwa kila nakala, kwenye maduka ya TPH Bookshop na maduka yote ya Uchumi Supermarkets, Mlimani City (MAK Bookshop), pia kipo kwenye mikono ya wamachinga kwenye njia panda zote kubwa za jijini Dar es salaam, kimefika Iringa (Lutengano Investment), Vyuo Vikuu vyote iringa, Dodoma na Mwanza (Pia Kwa Ibrahim Campbell jirani na CRDB Mwanza Branch). 

  Nakutakia usomaji mwema. Natanguliza Shukrani zangu za dhati na fanaka. 

  Wakatabahu,
  Hamisi Kigwangalla.
  Mwandishi. 


  0 0

  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
  Jumla ya Pikipiki 10 zenye thamani ya Sh.Million 42 zimegawiwa kwa Maafisa 10 wa Afya wa Wilaya za Unguja na Pemba. Pikipiki hizo ni Msaada kutoka Shirika la Watu wa Marekani USAID kupitia Taasisi ya JSI wenye lengo la kusaidia Sekta ya Afya Zanzibar. 
   Akikabidhi Pikipiki hizo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amewataka Maafisa Waliokabidhiwa kuzitumia vyema ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Amesema ana imani kubwa kuwa zitasaidia kwa kiasi kikubwa Usimamizi na usambazaji mzuri wa Dawa katika kila Wilaya ya Zanzibar. 
   "Kwa kweli pamoja na kuwashukuru Wahisani wetu USAID na JSI tunaamini sasa Usimamizi na Usambazaji wa Dawa utakuwa bora na kwa wakati maana Pikipiki hizo ni usafiri wa Rahisi" Alisema Naibu Mahmoud. 
   Amewataka Maafisa hao kutoishia kusambaza Dawa tu bali wapitie kila kituo cha Afya kutafuta Matatizo na kuyaripoti Sehemu husika ili yaweze kushughulikiwa. 
   Aidha Naibu Mahmoud amewashauri Viongozi wa Wizara ya Afya kutoa Motisha kwa Watendaji wanaoweza kukabidhiwa Vitendea kazi na kuvitunza vyema. Kwa upande wao Maafisa waliokabidhiwa Pikipiki hizo wameishukuru Serikali kwa Juhudi zake za kutafuta mbinu mbali mbali za kukabiliana na Changamoto na kuzifanyia kazi. 
   Mmoja wa Maafisa hao Mayasa Othman Shariff kutoka Wilaya ya Chake Chake amesema Pikipiki hizo zitawarahisishia kazi zao ikiwa ni pamoja na kusambaza na kusimamia Dawa sambamba na kupeleka Ripoti mbali mbali sehemu husika. Mfamasia Mkuu Dkt. Habib Ali Shariff alisema miongoni mwa Changamoto zinazokabili Sekta ya Afya ni pamoja na Usimamizi mbaya wa Dawa hivyo Pikipiki hizo zitasaidia kupambana na Changamoto hiyo. 
   Hafla ya Kukabidhiwa Pikipiki hizo ilifanyika katika Viwanja vya Bohari kuu ya Madawa Maruhubi Zanzibar ambapo Wilaya zote 10 za Unguja na Pemba zilipatiwa Pikipiki moja na kukabidhiwa Maafisa wa Afya wa Wilaya husika. Wizara ya Afya imekuwa ikifanya Juhudi mbali mbali za kukabiliana na Changamoto za Sekta ya Afya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutafuta Wafadhili kutoka Nchi tofauti ambapo Shirika la Watu wa Marekani USAID ni mdau muhimu wa kusaidia Sekta hiyo Zanzibar.
   Mfamasia Mkuu wa Zanzibar Dkt. Habib Ali Sharif akizungumza na Mafisa wa Afya wa Wilaya kabla ya kukabidhiwa Pikipiki kwaajili ya usambazaji wa Dawa Wilayani, pikipiki hizo zimetolewa na Shirika la watu wa Marekani (USAID) hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika Bohari Kuu la Madawa Maruhubi Mjini Zanzibar. 
   Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) akimkabidhi Pikipiki Afisa wa Afya wa Wilaya Nd. Khamis Daud Ali katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Maruhubi.
   Mafisa wa Afya wa Wilaya wakiwa kwenye Pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa.

  Mafisa wa Afya wa Wilaya wakiwa kwenye Pikipiki zao mara baada ya kukabidhiwa. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.
   Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.  “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.
  Wajumbe wa Imetosha

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

   Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa akiruka daluga la Beki wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho uliopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. Hadi mwisho wa mchezo matokeo ni 1-1.Picha zote na Othman Michuzi.
  Mchezaji wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Bounedjah Baghdad akiangalia namna ya kuwatoka wachezaji wa Yanga, Mbuyu Twite na Amissi Tambwe wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho uliopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. hadi mwisho wa mchezo matokeo ni 1-1.
   Wachezajiwa Timu ya Yanga, wakishangilia ushindi sambamba na mashabiki wao.
  Kiungo wa Timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia, Franck Kom aruka juu kuwania mpira wa kichwa wakati wa mchezo wa Kimataifa wa Kombe la Shirikisho uliopigwa leo kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam. 


  0 0

  SAM_2053
  Meneja masoko wa benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe kushoto,Meneja masoko Moshi Eliud Marko katikati wakimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika kijiji cha kituri kata ya kileo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro hundi ya shilingi Milioni tano yenye thamani ya zaidi ya mifuko 300 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa Hosteli ya wasichana katika shule hiyo ,msaada huo ni sehemu ya kamapeni ya Book by Book inayoendeshwa na benki ya CBA ikilenga kusaidia serikali katika juhudi za Elimu(Picha na Pamela Mollel wa Jamiiblog)
  SAM_2042
  Meneja masoko wa Benki ya CBA Tanzania Solomon Kawishe akizungumza na wanafunzi(hawapo pichani) kuhusu nia yao ya kuwasaidia msaada huo wa saruji kwaajili ya kujenga hosteli ni kutokana na idadi ya wanafunzi 944 kuwa na changamoto kubwa ya ufaulu hasa jinsia ya kike huku akiwaasa wanafunzi hao kuwa Elimu ndio urithi pekee wa kuweza kuharakisha maendeleo Tanzania hivyo jamii inategemea kupata watu muhimu wakuwasaidia kama madaktari,wafanyakazi wa mabenki na hata walimu wa kuendeleza elimu
  SAM_2038
  Meneja masoko Moshi Eliud Marko akiwa anasisitiza wadau mbalimbali wa makampuni makubwa kujitokeza kusaidia kuinua Elimu ili kupunguza umaskini Nchini
  SAM_2033
  Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kifaru Abdallah Mwomboke iliyopo katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro akiwa anatoa neno lake la  shukrani kwa Benki ya CBA kwa kufika na kuguswa kusaidia hosteli ya wasichana katika shule hiyo kutokana na wengi wameshindwa kuendelea na masomo shuleni baada ya kuingizwa katika mahusiano na wanaume hali ambayo inawawia vingumu kuweza kumudu masomo.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kigogo na vijana waliopo katika kundi maalumu kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya wakati akizindua ibada makundi maalumu iliyoanzishwa katika kanisa hilo Dar es Salaam jana.
   Msaidizi mstaafu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), George Fute (kulia), akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kwa kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hiyo.
   Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo ambaye ndio muasisi wa ibada hiyo ya makundi maalumu,  Richard Ananja akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Msaidizi mstaafu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), George Fute.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Na Ripota Maalum.

  Serikali ya Uingereza imebuni mbinu ya kuwasaidia vijana wa Tanzania katika kukabiliana na vikwazo katika soko la ajira kwa kuwapa maarifa na mikakati ya kujiajiri na kujinadi kwa waajiri .

  Vikwazo vinavyowakabili vijana katika soko la ajira ni pamoja na kutokuwa na maarifa ya kupata kazi na tabia ambazo zitawawezesha kuwa karibu na wafanyakazi wenzao,kutoa maamuzi magumu , kutatua matatizo kuweka heshima na mwisho kuwa wawakilishi bora wa taasisi wanayotumikia .

  Kwa kutambua changamoto hizo Uingereza imetuma walimu wa kujitolea kutoka taasisi ya Restless Development Organization (ICS)kuwafundisha vijana mikakati ya kujinasua na matatizo hayo .

  Wakizungumza katika mafunzo waliyoyatoa katika chuo cha Kilimanjaro Institute of Technology and Management (KITM) walimu hao wa kujitolea wamesema wanawafundisha vijana namna ya kuandika wasifu wao wenye maelezo ya mtu binafsi kuhusu elimu, ujuzi na kujiajiri wenyewe .
  Kiongozi wa walimu (ICS) Gemma Bunn aliliambia gazeti hili kwamba sababu ya kuwapo hapa nchini ni kwa kutambua kuwa Tanzania ina vijana zaidi ya asilimia 50 ambao hawawezi kupata ajira na wengi hukwama kutokana na vigezo kama hivyo .


  0 0

  Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa safari mpya kati ya Kilimanjaro, Tanzania na Entebbe, Uganda. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi asiye mtendaji wa Fastjet Tanzania, Lawrence Masha.
  Meneja Mkuu wa shirika la Ndege la Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (kushoto aliyeinama) na Mkurugenzi asiye mtendaji wa Fastjet, Lawrence Masha (Kulia aliyeinama) wakikata keki kwa pamoja katika uzinduzi wa safari mpya ya ndege hiyo kati ya Kilimanjaro, Tanzania na Entebbe, Uganda. Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Mshauri Kibiashara wa Fastjet, Ian Petrie (Kulia) na Mkurgenzi mtendaji wa Simba Travelcare, Uganda, Declan Peppard (Kushoto).
  Meneja Mkuu wa shirika la Ndege Fastjet Afrika Mashariki, Jimmy Kibati (wapili kushoto) akipongezana na mkurugenzi asiye mtendaji wa Fastjet Lawrence Masha (watatu kushoto) katika uzinduzi wa safari mpya kati ya Kilimanjaro, Tanzania na Entebbe, Uganda. Uzinduzi huo ulifanyika katiKa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Mshauri Kibiashara wa Fastjet, Ian Petrie (Kulia) na Mkurgenzi mtendaji wa Simba Travelcare, Uganda, Declan Peppard (Kushoto).

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kutangaza huduma wanazozitoa kwa wananchi ili jamii iweze kunufaika na huduma hizo kwa wakati na  gharama nafuu.

  Akizungumza na Menejimenti ya TEMESA jijini Dar es salaam leo, Eng. Iyombe amesisitiza Wakala huo kuwa na wafanyakazi wenye weledi, waliokabidhiwa mamlaka kamili na wabunifu ili kuhuisha huduma zinazotolewa kwa wananchi na kujiongezea mapato.

  “Hakikisheni mnatumia wataalamu mlionao kuleta tija kwa Wakala na kwa Serikali kwa ujumla ili mfikie malengo yenu na kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwahudumia”, alisisitiza Eng. Iyombe. 

  Aidha Eng. Iyombe ameagiza TEMESA kuimarisha uhusiano wake na jamii hasa sekta binafsi ili kubadili mtazamo uliopo sasa kuwa Wakala huo unatengeneza magari ya Serikali peke yake na hivyo kushindwa kuteka soko la sekta binafsi.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magesa amemshukuru Katibu Mkuu kwa kuwapatia vifaa mbalimbali na mitambo na kuahidi kuwa vitatumika vizuri ili kuimarisha utendaji kazi wa TEMESA.

  “Asilimia 100 ya mapato kwa baadhi ya mikoa tunayaacha mikoani ili kufufua mitambo iliyoko na kuboresha huduma za Ufundi, hivyo tumieni fursa hii kubuni miradi mingi ya kuongeza mapato”, amesema Eng. Magesa.

  Ubunifu, kujitangaza na kutoa motisha kwa wafanyakazi inachangia ari ya kufanya kazi ambapo TEMESA mkoa wa Pwani na Tanga imeelezwa kufanya vizuri na hivyo kuhudumia taasisi mbalimbali binafsi na za umma.

  0 0

  Wasanii wanaounda kundi la Original Komedi wakipata maelezo kutoka kwa Bw. Lonick Nkinda, Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF juu ya huduma zinazotolewa na Mfuko huo, wasanii hao walitembelea Makao Makuu ya PSPF ili kujionea utendaji wa Mfuko huo.
  Msanii wa kikundi cha Original Komedi Bw. Emmanuel Mgaya akijaribu kufungua moja ya mitambo inayotumika kuhifadhia kumbukumbu za wanachama wa PSPF ili kuona ubora wa huduma za Mfuko huo.
  Wasanii wa kundi la Original Komedi wakiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na watendaji wengine wa Mfuko huo baada ya kufanya ziara ya siku moja kujionea utendaji wa Mfuko huo.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa wasanii wa kundi la Original Komedi baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya Mfuko, pichani wasanii hao wakiwa katika jengo jipya la PSPF lililopo katika Barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu (kulia) akiongea wasanii wa kikundi cha Original Komedi walipotembelea Makao Makuu ya PSPF kwa ajili ya kujionea ubora wa huduma zinazotolewa na Mfuko huo.

  0 0


  Mchungaji Wilbert Nfubhusa akihubiri kwenye mkutano mkubwa wa neno la Mungu wa Wasababto waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland. Kulia ni Michael Mwasumbi akitafsiri mahubiri kwa lugha ya Kiingereza.Mkutano huu umehudhuriwa na Watanzania kutoka majimbo mbalimbali wakiwemo wengine kutoka Tanzania.
   Mhe. Liberata Mulamula. Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiushukuru uongozi wa Wasabato nchini Marekani kwa kuweza kufanikisha mkutano wao na kuweza kumleta mchungaji Wilbert Nfubhusa na kuelezea amefurahishwa kwa makaribisho mazuri na kuwatakia mkutano mwema huku akiomba Mwenye Mungu aushushie baraka zake.

  Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimtambulisha mdogo wake  Joycelyne Rutageruka ambaye amekuja kumtembelea Mhe. Balozi toka nyumbani Tanzania nae akitoa neno kwenye mkutano mkuu wa Wasabato wa Watanzania waishio nchini Marekani uliofanyika siku ya Jumamosi April 18, 2015 Silver Spring, Maryland.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA  

  0 0

  Mkongwe kwenye Muzuki wa Kizazi Kipya Nchini Tanzania Juma Khassim Kiroboto Maarufu kama Juma Nature @Sir_Nature amesema Kuwa Siku za Karibuni Zijazo atamuoa Mpenzi wake Ambaye anatokea Arusha.
  Akifanya Mahojiano na @DjHaazu wa @MamboJamboRadio Arusha Tanzania, Juma Nature amesema kuwa amekaa bila Mke wa ndoa kwa kipindi Kirefu sana tangua aachane na alikuwa Mkewe ambaye Alibahatika Kuzaa Mtoto mmoja na yeye aitwaye FURAHA na kwa sasa anaamini ni Muda Muafaka wakufikia Hatua Nyingine ya Kuitwa Baba wa Familia.
  Katika Mazungumzo hayo @Sir_Nature amesema pia kwamba Mwanaye Furaha anaishi na mama yake ila yeye kama Baba anamgharamia mwanaye Kila kitu ikiwa ni Pamoja na Shule Bora huku akisema kuwa yeye na Mzazi mwenzake huyo hawana Shida wako Sawa japo Mzazi mwenzake huyo alipata Bwana Mwingine na Kuolewa.
  Katika Point nyingine Pia Nature amewaomba Mashabiki wake wakae Tayari kwani Karibuni anaachia Wimbo wake Mpya wenye Mahadhi ya Kwaito aliosema utaitwa GUSA UNASE.

  MSIKILIZE  JUMA NATURE AKIONGEA NA @DjHaazu KWA KU-CLICK LINK HII ----> JUMA NATURE - AKIZUNGUMZA NA DJHAAZU

older | 1 | .... | 807 | 808 | (Page 809) | 810 | 811 | .... | 3283 | newer