Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 809 | 810 | (Page 811) | 812 | 813 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

  SERIKALI imesema hakuna mtanzania aliyepoteza maisha kwa vurugu zinazoendelea nchini Afrika Kusini kutokana na wenyeji wa nchi hiyo kuwachukia wageni.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe amesema watanzania waliofariki nchini Afrika Kusini hawatokani na vurugu za wenyeji kuwakataa wageni.

  Membe amesema tatizo hilo lilianza 2008 na 2014 hiyo lilichangiwa na Mfalme wa nchini humo kuchochea fujo hizo dhidi wageni lakini Mfalme huyo amejitokeza leo na kuzungumza na wananchi hao kwa kuwaasa kuacha kuwaua wageni waliopo nchini humo.

  Amesema watanzania waliopo katika makambi ni watanzania 23 ambao wawili wamekataa kurudi na 21 wanasema wanaweza kurudi hivyo mpango wa kuwarudisha nyumbani unafanyika na serikali ina uwezo huo.

  Amesema watanzania walioko katika mataifa mbalimbali wajenge tabia ya kujiandikisha katika balozi zao pamoja na kuunda umoja ili kuweza kupata taarifa panapotokea matatizo.

  Hata hivyo amesema serikali imekuwa ikifanya mazungumzo ya karibu na viongozi wa nchini Afrika Kusini juu vurugu hizo na taarifa zimekuwa nzuri.

  Membe amesema kunahitajika kujenga uchumi imara katika nchi za Afrika ili kuwezesha vijana wengi kuajiriwa na kujiajiri na kuachana na kukimbilia katika nchi hizi zenye uchumi wakati hawana ujuzi.

  Membe amesema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC),Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU),Robert Gabriel Mugabe amelaani kitendo hicho.

  Aliwataja watanzania waliopoteza maisha nchini Afrika Kusini kwa sababu tofauti na vurugu hizo, kuwa ni Rashid Jumanne aliyeuawa kutokana na kufanya unyang'anyi,Athuman China aliechomwa kisu akiwa gerezani kwa vurugu,Ally Mohamed alikuwa na ugonjwa wa kifua kikuu TB na mwili wake umeletwa nchini jana kutoka Afrika Kusini.
   Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya hali ya usalama wa wa Watanzania waishio nchini Afrika Kusini, katika mkutano uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es salaam leo.
   Sehemu ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakifatilia kwa makini kauli ya Serikali juu ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini, iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.
  Sehemu ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Wanahabari wakifatilia kwa makini kauli ya Serikali juu ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini, iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.

  0 0

  Waziri mkuu Mstaafu ,Fredrick Sumaye akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mbalimbali wakiwemo waandaji buda mfupi kabla ya kuanza kwa mbio za Km 21 Katika gate la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro,
  Waziri mkuu Msaatfu Fredirick Sumaye akikimbia sambamba na rais wa shirikisho la riadha Tanzania,RT,Athony Mtaka(Kushoto kwake) mkuu wa mkoa wa Arusha ,Daud Ntibenda,pamoja na mkuu wa wilaya ya Karatau Omary Kwaang kuashiria kuanza kwa mbio za Ngorongoro Marathoni.
  Maratibu wa Mbio ,Meta Paul akiwa na mmoja wa wasiamamizi ,Leila wakati wakiwaandaa wanariadha kuanza mbio za Km 21 katika lango la kuingilia hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa (katikati mwenye kapelo), "akitroti" kukimbia sambamba na mamia ya watu waliojitokeza kwenye matembezi ya kuunga mkono kupiga vita dhidi ya mauaji ya watu wenye Ualbino, yaliyofanyika jana kuanzia Uwanja wa Taifa na kuishia kwenye Viwanja vya TCC Club, Chang'ombe jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake mwishoni mwa matembezi hayo ya kilomita 5, Mh. Lowassa alimuomba Rais Jakaya Kikwete, "kumwaga" wino, ili kubariki hukumu ya kifo dhidi ya waliohusika na mauaji ya Albino.
  Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Edward Lowassa (katikati) akishiriki matembezi ya kuunga mkono kupiga vita dhidi ya mauaji ya watu wenye Ualbino, yaliyofanyika jana kuanzia Uwanja wa Taifa na kuishia kwenye Viwanja vya TCC Club, Chang'ombe jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mbunge wa Ilala, Mh. Mussa Zungu.

  0 0

  Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, Focus Masawe,  akizindua Kadi maalumu na tiketi kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanaisa hilo jijini Dar es Salaam juzi
   Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, Focus Masawe,  akionyesha Kadi maalumu na tiketi kwa ajili ya harambee kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo baada ya kuzindua rasmi
   Wanakwaya wa Paroko wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala, wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi.
  Waumini wa Kanisa Katoliki Paroki ya Mwananyamala wakiimba wakati wa uzinduzi uuzaji wa tiketi na kadi Maalumu ya  harambee ya kuchangia ujenzi na ukarabati wa Kanisa hilo juzi

  0 0

  Texas Black Belts club Seminar , imeandaliwa na Sensei Ramon Veras, Dan 7, Okinawa Goju Ryu Kyokai, mjini Houston, Texas tarehe 19 April, 2015. Pia ni sehemu moja ya maandalizi na marekebisho ya mbinu na ufundi wa vipande tofauti katika mfumo mzima wa  Sanaa na tayari kwa baadhi ya washiriki kwa msafara wa kwenda kwenye chimbuko la Karate huko Okinawa, Japan.

   Sensei Rumadha Fundi, ni mmoja ya wawakilishi wa Goju Ryu Jundokan, atayoiwakilisha Tanzania kwenye msafara huo.. 
  Baada ya takriban miaka 23 sasa, sensei Rumadha Fundi “Romi”, anarejea tena chini Japan kama alivyofanya mwezi  May mwaka 1992. Safari hiyo ya mwezi  June kwenda Naha City, Okinawa kwa njia ya Los Angeles, Tokyo  na hatimaye  Naha City, Okinawa.

   Sensei Rumadha amepewa mwaliko kama mwakilishi wa Jundokan Tanzania, kwa niaba ya kuwa mteule na mwakilishi wa chama hicho cha mtindo wa Okinawa Goju Ryu, chini ya rais wake ambaye ni mtoto wa Eiichi Miyazato mwanzilishi wa chama hicho Sensei Yoshihiro Miyazato “Kancho”, na hatimae kupewa jukumu la kusambaza  Jundokan nchini kote  akiwa“Tanzania Chief Instructor ” na kupewa  madaraka ya kutowa idhini na mikanda ya wawakilishi wa Jundokan nchini Tanzania na utambulisho wa kutowa vyeti ( Dan Certificate) kutoka, Naha, Okinawa.

   Sensei Rumadha anashikilia Dan 6 toka Tanzania Karate-do Federation, na Dan 3 toka Jundokan Kyokai.Lengo na madhumuni ya sensei Rumadha ni kusambaza ufanisi wa Goju Ryu na mbinu za “Muchimi” ni undani halisi wa utumiaji mbinu kifasaha na kitamaduni kama ifanyavyo huko Okinawa, Japan. 


  Sensei Rumadha, atafanya mazoezi katika dojo ambayo mwalimu wake yeye Sensei Bomani na Master Morio Higaonna walikuwa wanafunzi hapo  miaka 45-50 iliyopita. Pia Sensei Rumadha, atatembelea sehemu zenye historia ya mwanzao wa Karate na makaburi ya waanzilishi wa Sanaa na makumbusho ya Karate na vitongoji vyake kama,  Naha, Shuri na Tomari, Okinawa , Japan.

  Nia na madhumuni makubwa ni kutaka kuiendeleza Goju Ryu Karate Tanzania na hatimae kuwa na walimu wenye utambulisho huko, Okinawa, Japan na kuleta maendeleo na maslahi ya kimaisha kama mwalimu wa Karate. 

  Pia Sensei Rumadha alisema “ Tapenda kubadilisha mfumo wa jinsi Goju Ryu inafundishwa Tanzania. Tawapa mwaliko wanafunzi wote wenye nia ya mafanikio na utambulisho toka Okinawa, kuwa chini ya uongozi wangu na kuendeleza utamaduni wa Goju Ryu. Goju Ryu ina matawi mengi na uongozi tofauti, mimi napendelea kuwa na shina la Okinawa Goju Ryu Karate – do, lililowekwa na waanzilishi wa mtindo huo; lengo ni kuwa na Goju Ryu halisi na sio mabadiliko”, alisema Sensei Rumaha.


  0 0

  Wakati Mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la kifedha la kimataifa ikiendelea hapa Mjini Washington Dc. Mawaziri wa fedha wameweka misimamo yao juu ya sera ambazo zinawekwa na Benki ya Dunia.

  Akizungumza na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuya alisema” Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika utekelezaji wa mipango ya Benki. Tumeshukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi za kiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara, kilimo pamoja na miundo mbinu ya maji na umeme”.

  “Lakini vilevile tumeonyesha wasiwasi wetu kutokana na sera ambazo Benki ya Dunia imeziweka, kama vile kuangalia sera zile za watu wa kiasili ya kiafrika, sisi tumehisi mbali ya nia nzuri na njema ya Benki hii ya Dunia, lakini inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi zetu kwa sababu sera hiyo inaweza kutumika kuigawa nchi ambayo misingi yake imekuwa ikijengwa kwa umoja kutoka uhuru”.Alisistiza Mkuya.

  Hakuishia hapo aliendelea kutoa mfano kuwa “sisi watanzania tumekuwa wamoja ingawa tuna lugha mbalimbali kutokana na makabila tofauti. Lakini tumekuwa pamoja kwa kipindi cha miaka 50.Kwa hiyo tumeona sera hiyo isije ikatumika kwa ajili ya kuwa kigezo cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini . Sisi kama wa Afrika na viongozi wa Afrika tunashirikiana kuona kuwa sera zinazowekwa hazitukwamishi”.

  Hali hii ya kudai uasilia (indigenous) imeibuka zaidi katika miongo hii miwili, wakati kukiwa kumejitokeza watu wanaodai kuwa wao hawatambuliki na hoja hii inaihusu hasa nchi ya Tanzania.

  Mawaziri wa Fedha kutoka Afrika wamejadili mambo mbali mbali ambapo ni pamoja na masuala ya maendeleo na mahusiano yao na Benki ya Dunia.

  Katika Mkutano huo wa kisheria Mkurugenzi Mtendaji ndiye ambaye amewasilisha maazimio ya Benki katika kipindi cha miezi sita.Aliongeza Mkuya.

  Aidha katika mkutano huo pia walizungimzia suala la Ebola. “Kwa kweli wamekubali kusaidia nchi zile ambazo zimekumbwa na gonjwa hili lakini wamezitaka nchi za afrika na zenyewe kushirikiana katika kupambana na gonjwa hili”.Alimalizia Mkuya.

  Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
  Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia semina iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini.

  0 0


  0 0

  Ujumbe wa Kampuni ya Push Mobile kitengo cha SimuTV  ukiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Michuzi Media Group (MMG) mara baada ya kufanya mazungumzo juu ya libeneke hilo la SimuTV.Toka kulia ni Mtendaji Mkuu wa MMG, Ankal Issa Michuzi, Mkuu wa Kitengo cha Habari MMG, Cathbert Kajuna, Meneja wa SimuTV, Patricia Michael, Meneja Uendeshaji wa Push Mobile, Jason Hill, Meneja Masoko wa SimuTV, Athanas Muhanuzi, Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa MMG, Ahmad Michuzi pamoja na Mkuu wa Uendeshaji wa MMG, Othman Michuzi. Walioketi ni Kareem Michuzi na Chalila Kibuda.
  Mkuu wa Uendeshaji wa MMG, Othman Michuzi akielezea jambo kwa Meneja wa SimuTV, Patricia Michael juu ya namna Michuzi TV inavyofanya kazi zake.Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa MMG, Ankal Issa Michuzi akionyesha kitu kwenye simu yake kwa Meneja Uendeshaji wa Push Mobile, Jason Hill na Meneja Masoko wa SimuTV, Athanas Muhanuzi.

  0 0


  0 0
 • 04/20/15--07:27: MICHEZO YA WATOTO
 •  Watoto ambao majina yao hayakufahamika mara moja wakiwa katika michezo yao ya kawaida katika sehemu ya juu kabisa na ya hatari ya kingo za Mto Mbezi eneo la Kunguru- Makongo juu jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

  0 0
 • 04/20/15--08:10: CHANDIMU
 •  Watoto wa mtaa wa kwamtenga  Makongo juu jijini Dar es Salaam wakisakata kabumbu a.k.a Chandimu kama walivyo naswa na kamera ya Globu ya Jamii.
   "Beki hasifiwagi" hapa hapiti mtu.
   Nyanda akijiandaa kudaka mpira kwa woga.
  (Picha zote na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.)

  0 0


  0 0

  HATIMAYE hatma ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba na mjumbe wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Dk Damas Ndumbaro itatolewa Mei 10 mwaka huu.

  Kikao cha Kamati ya rufaa ya nidhamu chini ya Revocatus Kuuli ilisikiliza hoja za pande mbili ambao Ndumbaro alijiwakilisha mwenyewe wakati kwa upande wa TFF iliwakilishwa na wakili wao Emmanuel Muga huku habari za ndani zikidai kuwa licha ya Ndumbaro kukata rufaa, TFF nayo imemfungulia shtaka la tatu la kuandaa mechi kinyume na taratibu.

  Kikao hicho kilipitisha taratibu za kisheria ambazo zitatumika kuamua kesi hizo ambazo ni taratibu kama zinazotumika mahakamani ikiwemo kuwasilisha hoja zao kwa mdomo na si maandishi kitendo ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili.

  Wakili wa TFF, Emmanuel Muga aliiambia Mwananchi kuwa taratibu hizo zimewekwa ili kuondoa malalamiko kwa pande zote mbili.

  "Ni taratibu tu kama za mahakama za kawaida, hii inasaidia kuepusha manung'uniko upande mmoja kulalamika kuonewa."alisema Muga.

   Awali rufaa hiyo ya Ndumbaro ilikuwa ijadiliwe Aprili 12 lakini Sekretarieti ya TFF ilizembea kupeleka barua ya wito wa kuitwa kwenye rufaa hiyo kitendo ambacho Ndumbaro alikigomea kwa kile alichoeleza kuwa hawezi kuburuzwa.

  "Mimi ni mwanasheria, kanuni na taratibu nazifahamu, nilikata rufaa TFF walitakiwa waniletee samas wiki moja kabla angalau ili nijue na nijipange sasa mtu anakukurupusha kwa simu unatakiwa kwenye kikao leo hii mimi ni mtu mzima siwezi kuburuzwa."alisema Ndumbaro.

  Kitendo hicho cha Ndumbaro kugomea kudhuria kikao, kiliilazimisha kamati hiyo ya rufaa kutoa agizo kwa TFF kumpa tarifa ya wito Ndumbaro kabla ya Aprili 14 na juzi Jumapili Ndumbaro aliudhuria kikao hicho na sasa hatma yake itajulikana Mei 10. 

  Ndumbaro alikata rufaa ya kufungiwa miaka saba na Kamati ya Nidhamu baada ya kutiwa hatia kwa  makosa mawili.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Ndumbaro kugomea agizo la TFF juu ya kukatwa asilimia 5 za mgao wa fedha za klabu kutoka kwa wadhamini wa ligi kuu ambapo baadaye shirikisho hilo lilimburuza kwa Kamati ya Nidhamu kwa kitendo chake cha kukiuka kanuni zao.

  TFF ilimshitaki Ndumbaro kwa makosa mawili ambayo moja ni kutoa taarifa zisizo sahihi kiasi cha kupotosha kuhusu uamuzi wa TFF juu ya kanuni mpya za ligi kuu 2014/15 kinyume na kifungu namba 41 kifungu kidogo cha sita huku shitaka la pili likiwa kutamka kuwa kanuni za ligi hiyo siyo halali huku akijua kuwa zimepitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF ambayo yeye ni mwanafamilia.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na watendaji , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa mkoa wa Dar es salaam leo wakati akizindua Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza na watendaji , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es salaam leo kueleza nafasi yake katika kusimamia utekelezaji wa wakati Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akiwasilisha mpango Kazi wa Kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama, Watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
  Baadhi ya watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es salaam waliohudhuria uzinduzi wa Mpango kazi wa Kupunguza Vifo vya akina mama wajawazito na Watoto chini ya miaka 5 leo wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo Mhe. Sadiki Meck Sadiki (hayupo pichani) Picha/Aron Msigwa.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki amezindua Mpango  Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam na kukemea tabia ya baadhi ya watumishi wasio waadilifu wanaotumia lugha za kuudhi, kejeli na vitendo vya unyanyasaji kwa  akina mama wajawazito wanaofika kupata huduma za uzazi katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati.

   Akizungumza  katika kikao kilichowahusisha watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa wilaya na mkoa  wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam, Mhe. Sadiki amesema watumishi wa afya  wa mkoa huo wanao wajibu wa kutekeleza majukumu yao na kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuwapatia huduma bora za afya akina mama wajawazito na watoto walio na umri chini ya miaka 5 yaliyowekwa na mkoa.


  0 0


  0 0


  0 0

  MADAKTARI bingwa kutoka hospitali ya  SPS Apollo iliyopo  Ludhiana
  nchini India wamewasili nchini na kuanza kutoa huduma ya ushauri bure
  kwa magonjwa makubwa ambayo yamekuwa yakiwasumbua watu wengi na
  kuwalazimu  kwenda kutibiwa nchini India.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kutoa huduma kwa
  matibabu Arusha, Austin Makani alisema kuwa , madaktari bingwa hao
  wanatoa ushauri kwa wagonjwa wenye matatizo ya Figo , Moyo, tumbo,
  saratani, mishipa ya fahamu, uti wa mgongo, upasuaji wa kawaida na wa
  kupunguza uzito.wanawake (MMC) ambapo ushauri huo unatolewa, Mratibu wa Kambi hiyo ya

  Austin alisema kuwa,  ujio wa madaktari hao watano kutoka  nchini
  India umeratibiwa na kituo  cha kutoa huduma kwa wanawake (MMC) kwa
  kushirikiana na hospitali ya SPS Apollo iliyopo Ludhiana nchini India
  na wamefikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa wagonjwa wengi
  wanaoenda kutibiwa nchini India wanasumbuliwa na magonjwa hayo.

  Alisema kuwa, uwepo wa madaktari hao bingwa kwa siku tatu utasaidia
  sana wananchi wa jiji la Arusha kufika na kupewa ushauri bure juu ya
  magonjwa yanayowasumbua na hivyo kuokoa gharama ya kusafiri hadi
  nchini India kufuata huduma hizo.

  ‘hapa sisi wanachofanya madaktari hawa bingwa ni kusikiliza wagonjwa
  na baada ya kupata maelezo wanapata ushauri bure wa kwenda kupima
  kulingana na ugonjwa alionao na baada ya kurudisha majibu ndipo
  tunamwandikia dawa ya kutumia na kama ugonjwa wake unahitaji kutibiwa
  India tunampunguzia  gharama  kidogo ya kwenda kutibiwa India ‘alisema
  Austin.

  Alisema kuwa, uwepo wa kambi hiyo ya matibabu jijini Arusha unatoa
  fursa pia kwa wagonjwa waliokuwa wakatibiwe nchini India kutokana na
  magonjwa yanayowasumbua na kuweza kupata ushauri wa haraka na wakti
  mwingine kuepuka gharama za kusafiri.

  Wakizungumza  katika kituo hicho, Madaktari hao bingwa ,Abhijit Singh
  na Atul Behll kutoka hospitali ya SPS Apollo India  walisema kuwa
  ,changamoto kubwa iliyopo katika nchi za kiafrika ni watu wengi
  kutokuwa na utamaduni wa kwenda kupima afya zao ,hivyo aliwataka
  wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa jirani kufika kwa wiki ili kupata
  ushauri juu ya afya zao.

  Walisema kuwa,nchini India  kuna watanzania wengi wanaopata matibabu
  kwa wao kuwafikia na kuweza kutoa ushauri bure na hatimaye kupunguza
  gharama za kwenda nchini India.kutokana na magonjwa yaliyotajwa ,hivyo wakaona kuna umuhimu mkubwa.
  SAM_2088
  Wagonjwa wakiwa wanapatiwa vipimo mbalimbali .
  SAM_2082
  Atul Behll ambaye pia ni daktari bingwa kutoka India akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.
  SAM_2097
  Mgonjwa aliyekuja kupata huduma akiwa anasaidiwa na wahudumu wa kituo hicho.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Shughuli za Kanda wa Bohari ya Dawa (MSD),  Edward Terry (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam mipango ya MSD na mambo mengine. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa MSD, Etty Kusiluka.
   Etty Kusiluka akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.

  Dotto Mwaibale
  WASIMAMIZI  wa vituo vya afya, zahanati, hospitali za wilaya, mkoa na hospitali za rufaaa wametakiwa kuwa makini katika kusimamia utoaji wa dawa na vifaa tiba ili kutoa matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuhakikisha vinatosheleza idadi ya watu katika eneo husika.

  Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja na shughuli za kanda wa Bohari ya Dawa (MSD),  Edward Terry wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam katika ukumbi wa wa idara habari maelezo.

  "Wasimamizi wa vituo vya afya na hospitali huleta maoteo ya dawa na vifaa tiba kulingana na idadi ya watu walionao kwenye maeneo yao na mara nyingi uangalia magonjwa yanayoshambulia zaidi maeneo hayo hivyo hakutakiwi kuwa na uhaba wa dawa endapo usimamizi mzuri utazingatiwa, alisema Terry.

  Akitolea mfano wilaya ya Iramba, Igunga, Bariadi, babati , Arumeru na Sumbawanga kutokuwa na tatizo la dawa ambapo hufuata kanuni na sheria za uagizaji wa dawa kutoka bohari ya dawa pamoja na kutumia vyanzo vingine vya mapato kuongezea bajeti inayotolewa na serikali.

  Pamoja na hilo  Teryy aliongeza kuwa usimamizi makini wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ndiyo utakaofanya changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye hospitali na vituo kukoma.

  "MSD imeboresha huduma na kumpatia mteja taarifa muhuimu zinazomhusu kwa kuziweka wazi taarifa hizo kwenye mtandao ambapo atapata fursa ya kupata taarifa hizo muda wowote.


  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

    
   .Mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab wakikabidhi kabati likiwa na madawa mbalimbali kwa  kituo cha Makalala kilichoko mafinga liganga.
    Mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab, wakiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi walemavu wa kituo cha Makalala kilichoko mafinga liganga.


  NA DENIS MLOWE, MUFINDI

  JAMII imewatakiwa kuacha tabia ya kuwaficha walemavu bali kutoa taarifa za watoto hao waliopo kwenye familia mbalimbali kwa lengo la kupata huduma bora  hasa katika sekta ya elimu na afya.

  Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mufindi Community Walefare Amina Rajab wakati wa kutoa msaada wa madawa mbalimbali na nguo kwa walemavu wanaolelewa na kituo cha Serikali cha Makalala kilichoko Luganga Mafinga kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Hazina Foundationi ya mjini humo, William Mungai ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema na Mgombeo ubunge jimbo la Mufindi Kaskazini.

  Amina alisema kuwa kuna wazazi wengi wana kasumba ya kuwaficha watoto wenye ulemavu bila kujua kuwa wanahaki sawa na watoto wasiowalemavu na wakipatiwa elimu wanaweza kuwa wakombozi wa familia hasa katika masomo ya ufundi.

  Alitoa wito kwa serikali kuona umuhimu wa kutumia vituo mbalimbali vinavyolea watoto wenye ulemavu kuhakikisha vinawejengea miundo mbinu rafiki na uboreshaji mipango na mfumo wa utoaji elimu, afya na usafiri kulingana na tofauti za umri wa watoto nchini.

  Aliongeza kuwa walemavu wanayo haki ya kuishi na kujitegemea iwapo jamii itawajengea uwezo badala ya kuwafungia ndani na kuwaona kama ni mkosi katika familia  ila kugundua vipaji walivyonavyo na kuiwezesha serikali kuwaingiza katika mipango mbalimbali ya kuwapatia huduma

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hazina Foundationi, William Mungai aliomba jamii kubadilika sasa na kuondokana na dhana potofu ya kuwatenga walemavu katika shughuli za kijamii

  Alisema kuwa bado elimu zaidi inahitajika kwa jamii ili kuweza kuondokana na mila zisizo na maana za kuwatenga na kuwadharau walemavu katika jamii.

  Naye Rahel Kumbo  ambaye ni Mlezi wa kituo cha Makalala kinachofadhiliwa na serikali alitoa wito kwa jamii kuwa walemavu wasifichwe majumbani na badala yake  wapelekwe hospitalini mapema ili wapate matibabu na kuwapatia elimu katika shule husika za walemavu.

  Alisema kuwa licha ya nia ya serikali kutaka watoto walemavu wapelekwe shule bado mazingira ya kujifunza katika shule nyingi hayawavutii watoto hawa hali inayosababisha baadhi yao kukacha masomo licha ya kuwa na vipaji vikubwa.

  Alisema kuwa serikali imejenga sana shule za kata lakini ujenzi wa shule za walemavu hasa upande wa sekondari umekuwa kikwazo kwa baadhi ya watoto kwa kuwa hali zao za kimaumbile zinawapa ugumu kurandana na hali ya mazingira ya shule.

  Alitoa wito kwa serikali kuwa makini na suala zima la ujenzi wa shule unaoendelea kuangalia na walemavu wanapaswa kujengewa vyoo vya kukidhi haja zao,maana hali hiyo ikiendelea walemavu watapata magonjwa mengi na kushindwa kuhudhuria masomo yao.


older | 1 | .... | 809 | 810 | (Page 811) | 812 | 813 | .... | 3278 | newer