Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 792 | 793 | (Page 794) | 795 | 796 | .... | 3285 | newer

  0 0

  IMG_1562

  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na Mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Na Mwandishi Maalumu, 
  Trollhattan-Sweden
  MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote barani Ulaya unaopicha vyakula vya Kiafrika.
  Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
  Balozi Msechu alimpongeza  Chef Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.
  Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
  IMG_1477
  Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
  IMG_1567
  Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.


  0 0

  Mkurugenzi wa Mtedaji wa Jembe ni Jembe ambaye ni mmiliki wa Jembe FM Radio, Dr. Sebastian Ndege, kwa mara ya kwanza hii leo amezungumza na wakazi wa mkoa wa Mwanza kupitia masafa mapya ya 93.7 Jembe FM kuwakaribisha kuwa sehemu ya familia ya redio hiyo sanjari na kuelezea mipango na mikakati ya kituo hicho. 
  Dr. Ndege amesema kuwa Jembe FM imepania kuwa sehemu ya uchangiaji wa ukuaji wa maendeleo ya jiji la Mwanza lenye hazina za kitalii, uvuvi, madini na sekta mbalimbali za uchumi, viwanda biashara kwa kuhakikisha inapenya kihabari na kuainisha changamoto mbalimbali za jamii husika ikiwa ni sambamba na kutoa ushauri kwa nini kifanyike. ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA YALIYOJIRI TANGU AWALI KUPITIA JEMBE FM.
  Mkurugenzi wa Mtendaji wa Jembe ni Jembe ambaye ni mmiliki wa Jembe FM Radio, Dr. Sebastian Ndege (kulia) akitambulishwa hewani na moja kati ya watangazaji wa kituo hicho Timoth Ngalula (kushoto). 

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDA

  0 0

   Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali  Pengo, akiubusu msalaba, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu katika   Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam,  Katikati aliyeshikilia msalaba huo  ni Padri Audax Kaasa wa kanisa hilo.(PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
   Mtoto Benedicta Mushi, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Masaka English Medium  akiubusu msalaba, wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu,  kulia kwa mtoto huyo ni Baba mzazi Philip Mushi
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, akikomunika Ekaristi Takatifu  katika Kanisa  Kuu Katoliki  la Mt. Joseph Dar es Salaam
  Meneja Miradi Jimbo la Mtama Wilaya ya Lindi, Paul Maokola akibusu mkono wa  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali  Pengo,  wakati wa Ibada ya Ijumaa Kuu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam  kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Mtama, mkoani  Lindi  Bernad Membe

  0 0

  President Jakaya Mrisho Kikwete addresses a meeting of the World Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete addresses a meeting of the World Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete chats with Carmen Hummel who had asked him a question on how his childhood was during a meeting of the World Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete is mobbed by excited stidents after addressing a meeting of the World Affairs Council in Seattle on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete greets members of the Tanzanian Community based in Seattle during his one-day visit of the city on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete greets members of the Tanzanian Community based in Seattle during his one-day visit of the city on Thursday April 2, 2015
  President Jakaya Mrisho Kikwete greets members of the Tanzanian Community based in Seattle during his one-day visit of the city on Thursday April 2, 2015


  STATE HOUSE PHOTOS.

  0 0

  Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla Aprili 3,2015 alichangiwa fedha kiasi cha sh 2,319,500 na wananchi wa kijiji cha Manyinga na vijiji vya jirani kwa ajili ya kuchukua fomu ya kuwania Ubunge mara muda utakapofika.

  Tukio la kuchangiwa fedha za kuchukulia fomu lilichagizwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe aliyefanya ziara ya kukagua hospitali teule ya Bwagala na kisha kuongea na wananchi kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.

  Alipopanda jukwaani, Dk. Stephen Kebwe alisema "nionavyo mnafuraha sana na mnampenda sana Mbunge wenu", wananchi wakamjibu kwa sauti Makalla ni jembeee.

  Kusikia hivyo, Dk. Kebwe akawatania kama kweli mnampenda Amos Makalla basi onyesheni kwa kumchangia ili achukue fomu, hapo ndipo umati ulipolipuka na kuanza kuwasilisha michango.

  Akiwashukuru wananchi hao, Mbunge wa Mvomero alisema amepokea msaada huo kwa heshima kubwa na kwa maana kubwa ikiwepo imani kubwa waliyoonyesha wananchi hao kwake.

  Amewaahaidi kugombea tena Ubunge na zaidi amewaomba ushirikiano na amewahakikishia utumishi uliotukuka.

   Aidha katika tukio lingine amewakabidhi Wawakuda Saccos ya Kijiji cha Dakawa msaada wa computer na printer yenye thamani ya sh 2,000,000 .

  Akishukuru Mwenyekiti wa Wawakuda Saccos, ndg. Mohamed Mkupete alimshukuru sana mbunge kwa msaada wa computer ambayo walimuomba wiki moja iliyopita na leo ametembelea"mheshimiwa Makalla wewe ni mtu makini na huna longolongo ndani ya wiki moja umetekeleza tunakushukuru sana".
  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla wakiongozana wakati wakiwa kwenye ziara ya kutembelea hospitali teule ya Bwagala, Turiani Mkoani Morogoro.
  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akiwa na Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla wakiwajualia hali wagonjwa waliolazwa kwenye hospitali hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Dk. Stephen Kebwe akipokea mchango wa wananchi wa Jimbo la Mvomero waliomchangia Mbunge wao wa Mvomero, Amos Makalla ili achukua fomu za kuwania Ubunge wa Jimbo hilo wakati utakapofikia.

  0 0

  Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa kwa mmoja wa walezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akikabidhi sehemu ya msaada kwa kwa mmoja wa walezi wa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'.Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka. Baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund' wakibeba sehemu ya msaada uliyotolewa kwao na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwa kituo hicho ikiwa ni maandalizi ya Siku Kuu ya Pasaka.Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Kushoto ni MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza. Meneja wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dar es Salaam Kusini, Adolf Matondo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi sehemu ya msaada kwa watoto wa kituo cha watoto yatima kilichopo Mbagala, Chamazi jijini maarufu kwa jina la 'Yatima Group Trust Fund'. Kushoto ni MKuu wa Kituo hicho, Wilfrida Lubanza.


  0 0


  0 0


  Wanakikundi wa women with vision wakiongozwa na mwenyekiti wao Herieth Makombe  wakiwa katika kituo cha msimbaz centre walipofika na kutoa misaada ya baadhi ya mahitaji katika kuwakumbuka watoto yatima katika msimu huu wa sikukuu za pasaka 


  Baadhi ya mahitaji ambao walitoa katika kituo cha msimbaz centre katika kuawajali watoto yatima wa vituo vya msimbaz centre na mburahati.

  0 0

  Naomba nifafanue kuhusu propaganda inayoenezwa na maafisa wa TCRA kupitia CloundsFM kuhusu Sikika na Mswada wa ‪#‎CyberCrimeBill‬.

  Sikika haikuhudhuria mkutano wa wadau unaodaiwa kufanyika Dodoma kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na leo maafisa wa TCRA.

  Sikika haikutoa maoni kuhusu Mswada wa miamala ya kielektoniki kama ilivyodaiwa na Mh Peter Serukamba na pia leo maafisa wa TCRA.

  Sikika ilituma maoni ya pamoja ya wadau kwa niaba ya wadau kuhusu #CyberCrimeBill kwa njia ya email kwa Mkiti Kamati Mh Peter Serukamba.

  Maoni hayo hayakutumika kuboresha #CyberCrimeBill bali kuongeza tu orodha ya wadau wanaoda iwa "kushiriki" kwa lengo la kuonesha kuridhia.

  Kwa kuwa maoni ya wadau hayakuzingatiwa na kwamba ‪#‎CiberCrimeBill‬ iliyopitishwa ina mapungufu mengi, Sikika na wadau bado wanaipinga.

  Mwisho tunaomba jina la Sikika lisiendelee kutumika kuhalalisha upitishwaji wa sheria hii.

  Irenei Kiria
  Mkurugenzi wa Sikika
  4 Aprili 2015.

  0 0

   Mtangazaji wa Radio 93.7 EFM ya jijini Dar es salaam, Samira Kiango (pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Tasnia ya Habari za Mitandao (Social Media), Clarence Mulisa kutoka Global Publishers (kulia), Fredrick Bundara kutoka Bongo Five (pili kushoto) pamoja na Othman Michuzi MTAA KWA MTAA BLOG chini ya Michuzi Media Group, mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha Mezani, kilichokuwa kikijadili swala zima la Muswada wa Sheria za Makosa ya Mtandao 2015, kilichoruka hewani mapema leo asubuhi.Alieketi ni Johnbosco Kamili wa EFM.


  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetuma salama za rambirambi kwa familia za washabiki wa timu ya Simba waliopoteza maisha katika ajali ya gari jana mkoani Morogoro wakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga kuishangilia timu yao dhidi ya Kagera Sugar.

  Meneja Uhusiano wa Vodacom Matina Nkurlu katika taarifa yake aliyoitoa kwa niaba ya kampuni amesema kuwa msiba huu ni mzito kwa watanzania na wapenzi wa soka kwa ujumla.

  “Vodacom Tanzania kama mdhamini Mkuu wa ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara tumeguswa sana na msiba huu na tunatoa pole kwa familia zilizopoteza jamaa zao katika ajali hii na tunawaombea moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,vilevile tunatoa pole kwa majeruhi wote wa ajali hii na tunawaombea wapone haraka na kurejea katika hali zao za kawaida”.Alisema.

  Ajali hiyo iliyotokea katika eneo la Mkundi katika manispaa ya Morogoro juzi imesababisha vifo vya watu saba na wengine zaidi ya 18 kujeruhiwa.

  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro.Leonard Paul amekaririwa akisema kuwa chanjo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva aliyekuwa analiendesha gari hilo.
  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akiongea na waandishi wa habari( hawapo pichani) wakati alipokuwa akituma salama za rambirambi kwa niaba ya kampuni kwa familia za mashabiki wa timu ya Simba waliopoteza maisha yao kwa ajali ya gari jana Mkoani Morogoro wakiwa safarini kuelekea mkoani Shinyanga kuishangilia timu yao dhidi ya Kagera Sugar.

  0 0   Baadhi ya Vyakula mbalimbali vikishushwa kwenye gari kwa ajili ya kuvikabidhi vituo vya wataoto waishio katika mazingira magumu vipatavyo saba,msaada huo una thamani ya shilingi milioni sita.
   Bwa.Alex Msama akikabidhi msaada vitu mbalimbali vikiwemo vyakula kwa Msimamizi wa kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa,Bi.Halima Ramadhan,kilichopo Boko jijini Dar.


  NA LOVENESS BERNARD.

  Kampuni ya Msama Promotions imetoa msaaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 7 vya kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi misaada hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Alex Msama alisema kuwa misaada hiyo ni sehemu ya mapato yatokanayo na Tamasha la Pasaka.

  ‘’Misaada hii ni mapato ya Tamasha la Pasaka mwaka jana  ,tumewapa watoto zawadi hizi ili washiriki vema katika kusheherekea sikukuu ya Pasaka na wajisikie kama watoto wengine’’, alisema Msama.

  Kwa upande wake mmoja wa walezi wa vituo hivyo Honoratha Michael ambaye ni mlezi wa kituo cha Honoratha kilichopo Temeke, alisema kuwa anaishukuru  Kampuni ya Msama Promotions kwa kuwapa misaada hiyo wanaomba nawatu wengine wajitolee kuwasaidia.

  ‘’Tunamshukuru Msama na kampuni yake na hatuna cha kumlipa zaidi ya kumuombea Baraka kutoka kwa Mungu baba pia tunawaomba watanzania wengine wajitolee kwani tunazo changamoto nyingi katika vituo vyetu’’alisema Honoratha.

  Misaada hiyo iliyotolewa jijini Dar es Salaam imegharimu million sita imewanufaisha watotowa vituo vya Honoratha (Temeke),Malaika kids (Kinondoni),  Umra(Magomeni),Mwandaliwa( Boko), Zaidia (Sinza)na kituo cha Rahman kilichoko Magomeni.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF jana ijumaa alipokea ugeni wa makamu wa Rais wa FIFA ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini Jordan, HRH Prince Ali Bin Al Hussein. (picha ya Rais Jamal Malinzi na HRH Ali imeambatanishwa)

  Jioni Prince Ali Bin AliHussein na ujumbe wake walifanya mazungumzo na Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Jamal Malinzi  katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Kempsinki) iliyopo jijini Dar es salaam.

  Katika mazungumzo hayo, zaidi waligusia maeneo kadhaa ya ushirikiano kati ya TFF na Chama cha Mpirwa wa Miguu nchini Jordan (JFA), hasa katika maeneo ya maendeleo ya mpira wa vijana, makocha na waamuzi.

  HRH Prince Ali Bin Al Hussein ambaye ni mgombea wa nafasi ya urais FIFA mwaka huu, ameondoka leo mchana kurudi nyumbani kwake Jordan.

  0 0

  Nguli wa soka wa timu ya taifa ,Uholanzi na vilabu vya Ajax na Barcelona,Johan Cruyff (Kulia) akiongozana na mwenyeji wake,Rayco Garcia mara baada ya kuwasili katika uwanja a ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)


  Dixon Busagaga (Kushoto) wa Globu ya Jamii na Busagaga's Orijino Blog akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa ziara hiyo ya magwiji wa Barcelona.


  0 0  0 0

  As part of its African Women To Watch series, global TV network Bloomberg TV, has just featured the worlds most powerful child and the youngest filmmaker in the world - Child Education Advocate Zuriel Oduwole. Broadcast across Africa and Europe, it highlights her incredible journey and her mission, and vision for Africa and the continents young Girls, at just 12 years old.

  0 0

  Shika ndinga kwa wilaya ya Kinondoni imefanyika leo Aprili 4,2015 katika uwanja wa Garden Kinondoni jijini Dar es salam,ambapo wasikilizaji wa Radio EFM waliopata nafasi ya kushiriki baada ya kujibu maswali mbalimbali kupitia vipindi vya redio  walishindana kushika ndinga ili kuweza kujishindia ndinga ya biashara.

  Washiriki wa shindano kwa Wanawake walikua 21 na wanaume 20 ambapo kati ya hao ni Wanawake Watano  na Wanaume watano waliofanikiwa kuendelea mbele katika raundi nyingine ambapo watashiriki katika fainali na washindi wengine kutoka katika Wilaya ya Ilala na Temeke.

  Mtiririko wa kushika ndinga ulikuwa ni kusimama kwa miguu miwili wakiwa wameshika ndinga  na baada ya kama dakika tano wanaume wengi walianza kushuka baada ya kushindwa kuhimili vigezo vilivyowekwa na wanawake walisimama imara kwa muda na badae wao walianza kushindwa kwa wingi kuliko wanaume. 

  Ndani ya lisaa la kwanza tu washindi watano wanawake walipatikana  hivyo zoezi hilo kubaki wanaume tu, ambao baada ya muda kidogo walibadilishiwa zoezi la kushika ndinga kwa mguu mmoja na mwingine kuuinua usishuke chini chini hapo ndipo washindi Watano Wanaume walivyopatikana.

  Washindi kwa upande wa Wanawake ni KHADIJA RASHIDI, SWAUMU IDDI, HAPPY AMBROS, NYABUHO Peter na  HABIBA,
  Na kwa upande wa Wanaume ni ABDUL Said , KASSIM Said, ERNEST EDWARD, MUBARAK RAMADHANI pamoja na MBWANA KASANGA.


  0 0
  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi akimpa pole Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mazishi ya baba mzazi wa mkewe, Marehemu Mzee Abdallah Rehani yaliyofanyika kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam, Aprili4, 2015.
  Waombolezaji wakizika mwili wa baba mzazi wa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda , Marehemu Abdallah Rehani kwenye Makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam, Aprili 4, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishiriki katika mazishi ya Baba Mkwe wake , Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad akishiriki katika mazishi ya Baba mzazi wa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Marehemu Abdallah Rehani kwenye makaburi ya Segerea jijini Dar es salaam Aprili 4, 2015.


  0 0
 • 04/04/15--14:29: HERI YA SIKUKUU YA PASAKA
 • LEO NI SIKU KUBWA SANA KWA WAKRISTO WOTE DUNIANI AMBAO WANAUNGANA PAMOJA KATIKA KUMBUKIZI YA KUFUFUKA KWA BWANA YESU KRISTO NA KUPAA MBINGUNI AMBAYO ILIITWA PASAKA. HIVYO GLOBU YA JAMII INAWATAKIA HERI NA FANAKA WADAU WOTE KATIKA SIKUKUU HII YA PASAKA.

older | 1 | .... | 792 | 793 | (Page 794) | 795 | 796 | .... | 3285 | newer