Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SIMBA SC KUFUATIA AJALI WALIYOPATA WASHABIKI WAKE

0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, ametuma salamu za rambi rambi kwa Rais wa klabu ya Simba SC Bw. Evans Aveva kufuatia vifo vya mashabiki wa klabu hiyo, viliyotokea jana katika ajali ya barabarani eneo la Makunganya mkoani Morogoro.

Katika salamu zake Rais Malinzi amesema, TFF imezipokea kwa masikitiko taarifa hizo za ajali na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, wanawapa pole wafiwa wote na mwenyezi Mungu awape nguvu majeruhi waweze kupata nafuu na kupona kwa uharaka zaidi.

Aidha Rais  Malinzi ameagiza michezo yote ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania itakayochezwa  wikiendi hii nchini, kusimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka mashabiki waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

IJUE HISTORIA YA KHANGA

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA KINONDONI AKABIDHI ZAWADI ZA PASAKA KWA YATIMA

0
0
NA MWANDISHI WETU,
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amekabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali vyenya thamani ya shilingi milioni 2.5 kwa vikundi vitatu vya kulea watoto yatima, Dar es Salaam jana kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka.

Akikabidhi msaada huo Meya Yusuph Mwenda aliwataka watanzania kuwa na moyo wa kusaidia watoto hao hususan katika msimu wa Sikukuu ikiwa ni njia mojawapo ya kuwafariji watoto hao.

“Hakuna anayependa kuona watoto hawa wanaongezeka mitaani, Na Serikali inafanya juhudi kubwa kuondoa tatizo la watoto hawa hasa wanaotelekezwa mitaani lakini peke yake haiwezi, ni lazima wananchi muunge mkono juhudi hizo.” Alisema Mwenda.

Alisema kuwa badala ya watu kusherehekea Sikukuu majumbani mwao ni vema wakajumuika na watoto hao ili kuwafanya nao wajisikie wapo na wazazi wao. 

Msaada aliotoa Meya huyo ni pamoja na Mchele, Sukari, Mafuta, Unga wa Ngano, Unga wa Sembe, Sabuni za miche na unga, Mbuzi na vitu vingine.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha Kiwohede- Bunju kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, kwenye hafla iliofanyika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Meya Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akikabidhi msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa watoto wa kituo cha kule watoto yatima cha Malaika kwa ajili ya kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa vikundi hivyo.

Rais Kikwete atoa Mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani. PICHA NA IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua jambo wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson International Centre) tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC nchini Marekani. 
Sehemu ya wahudhuliaji katika mhadhara huo wakimpigia makofi Rais Kikwete (hayupo pichani). 
Serikali ya awamu ya nne inajivunia mafanikio iliyoyapata tangu kuingia madarakani Mwaka 2005 na kuweka msingi imara wa nchi katika kutekeleza Mkakati wa Maendeleo wa Mwaka  2025 (Tanzania Development Vision 2025) ambao  unalenga  kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye  uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo tarehe 3 Aprili, 2015 jijini Washington DC wakati akitoa mhadhara katika kituo cha Kimataifa cha Woodrow Wilson (Woodrow Wilson Centre.

 "Naamini mrithi wangu atayaendeleza na kujifunza kutokana na mafanikio haya na kuendeleza kutoka pale tutakapoachia" Rais amesema na kuongeza kuwa pia anatarajia kuwa Tanzania itakuwa na sera na sheria ya kusimamia Gesi na mapato yake kwa vile inatarajiwa kuanza kupatikana ifikapo Mwaka 2020. 

Katika mhadhara huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Mabalozi, wasomi na viongozi wa taasisi hiyo, Rais  Kikwete ameelezea mafanikio na changamoto katika uongozi wake wa miaka 10 katika elimu, siasa, uchumi na maendeleo ya jamii. 

 "Najivunia kuweza kuendelea kuliweka Taifa katika hali ya Umoja pamoja na changamoto zote, tumepambana na vitisho pale vilipojitokeza na pia tumetoa mchango mkubwa katika harakati za kisiasa zilizopelekea vyama viwili kutiliana saini maridhiano na kupata muafaka Mwaka 2010". 

 Rais ameelezea na kuongeza kuwa makubaliano hayo yalipelekea Zanzibar kufanya uchaguzi kwa amani na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa baina ya vyama vya CCM na CUF. "Natumaini tutafanya uchaguzi huru, haki na amani ili niweze kumkabidhi Urais mrithi wangu katika hali ya utulivu" Rais ameongeza.

 Imetolewa na; 

 Premi Kibanga
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Washington DC - Marekani4 Aprili, 2015.

Introducing "Njoo Uichukue" (Official Video) by Mrisho Mpoto

HISTORIA YAANDIKWA MJINI ADDIS ABABA- WHEN PRINCE OF SWAHILI BLUES MET THE LEGENDARY KING OF ETHIO JAZZ

0
0
 Hannival akipapasa zeze la Kihabeshi
 Timu kamili ya Ethio-Swahili  Fusion wakishambulia
 Juma Setumbi akipongezwa na mkongwe Dr Mulatu
 Leo Mkanyia akimkaribisha rasmi King of Ethio Jazz Dr Mulatu
 Dr Mulatu na Leo wakishambulia jukwaa
 Wadada wa Kihabeshi wakitwanga Swahili Blues kihabeshi habeshi. Kwa habari kamili na picha BOFYA HAPA

JUMUIYA YA WATANZANIA DMV KUUNGURUMISHA SHEREHE ZA MUUNGANO DMV- SATURDAY APRIL 25, 2015

0
0
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa DMV unapenda kuwajulisha watanzania wote kukaa mkao wa kula , kwa ajili ya sherehe za muungano zitakazofanyika, Jumamosi April 25, 205.
Jiandaeni kwa Hafla na Vivutio mbali mbali. Michezo, Utamaduni, Nyama Choma nk. DMV Patakuwa Hapatoshi.


Wadhamini Wanakaribishwa


Wasiliana na uongozi kupitia


President: Iddi Sandaly 301-613-5165
Vice President: Harriett Shangarai 240-672-1788
Secretary: Saidi Mwamende 301-996-4029

Assistant Secretary: Bernadetta Kaiza 240-704-5891
Treasurer: Jasmine Rubama 410-371-9966

Assistant Treasurer: Gerald Mude 202-644-1829

info@watanzaniadmv.org


Waziri Membe atoa wito kwa Watanzania kuwasaidia watu wasiojiweza kwenye jamii

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)  akimtazama kwa furaha mmoja wa watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Kigogo Mburahati, Jijini Dar es Salaam. Waziri Membe alikitembelea kituo hicho wakati wa Siku Kuu ya Pasaka. 
Mhe. Membe pamoja na Mkewe Mama Dorcas Membe wakipata maelezo juu ya watoto waishio katika kituo hich kutoka kwa Sista Mary Bakhita.
Waziri Membe akitoa  msaada kwenye kituo hicho
Picha zaidi BOFYA HAPA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kuwasaidia watu wasiojiweza waliopo kwenye jamii wakiwemo watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ametoa wito huo hivi karibuni alipotembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima na Wazee cha Nyumba ya Furaha na Amani kilichopo Mburahati Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Membe alisema kuwa katika jamii za watu kumekuwa na makundi ambayo yanahitaji msaada mkubwa kutoka kwa watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine wamejaaliwa kipato kidogo na afya. Alisema kuwa ni wajibu wa watu wa aina hiyo kuwasaidia wale wanaohitaji kama vile watoto yatima, walemavu, wazee na wajane.

Waziri Membe ambaye alikuwa amefuatana na Mke wake, Mama Dorcas Membe aliguswa sana na historia ya baadhi ya watoto yatima aliowatembelea kituoni wakiwemo wale waliotupwa jalalani na kuokotwa wakiwa kwenye hali mbaya.

 “Lipo kundi linalopata mateso na matatizo katika jamii zetu tunazoishi. Ni vizuri Watanzania tukajenga utamaduni wa  kutembelea sehemu kama hizi ili kujionea wenyewe hali halisi. Kwa kweli ni hali ya kusikitisha kuona baadhi ya watoto walitupwa na kuokotwa jalalani na wengine tayari wakiwa wamepata majeraha ya kung’atwa na mbwa. Hivyo ni wajibu wetu sote kuwasaidia kwa chochote kidogo tunachojaaliwa kupata”, alisema Waziri Membe.

Aidha, Mhe. Membe aliwapongeza na kuwasifu Masista wa Shirika la Mama Theresa  ambao ndio wasimamizi wa kituo hicho kwa kuwalea watoto, vijana na wazee wenye matatizo mbalimbali na kuwaomba waendelee kujipa moyo katika kazi hiyo kwani ni njia moja wapo ya kumtumikia Mungu.

Awali akimkaribisha Waziri Membe kituoni hapo, Sista Mkuu wa Kituo hicho, Sista Mary Bakhita, alisema kuwa wamefurahia sana ziara hiyo ya Mhe. Membe hususan katika Siku Kuu ya Pasaka kwani ni faraja kubwa kwao kwa Watoto na Wazee wanaolelewa kituoni hapo.

“Tumefarijika sana kula pasaka pamoja nawe Mhe. Waziri. Watoto na Wazee hawa wanajisikia vizuri pale wanapotembelewa na tunaomba uendelee na moyo huo huo”, alisema Sista Bakhita.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Membe na familia yake walitoa zawadi mbalimbali kwa kituo hicho ikiwemo vyakula, sabuni na fedha kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali kituoni hapo.

-Mwisho-

Sherehe za pasaka kanisa la kkkt azania front jijini Dar es salaam

Mbunge wa Mtera Mhe. Livingstone Lusinde alipochangia mjadala wa kuanzishwa kwa baraza la Taifa la vijana bungeni mjini Dodoma

TAARIFA KWA UMMA YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHUSU UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KURA YA MAONI

0
0

Kama inavyofahamika, chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ya mwaka 2010, jukumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kusimamia na kuendesha Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara. Aidha, Sheria ya Kura ya Maoni imezipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar jukumu la kuendesha Kura ya Maoni kwa ajili ya kuhalalisha Katiba Inayopendekezwa. Kwa mujibu wa Katiba na Sheria, Tume hizi huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mamlaka nyingine yeyote. 

Ni jambo linaloeleweka kwamba, zoezi lolote la Uchaguzi huanzia na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Wapiga Kura wote wenye sifa za Kikatiba na Kisheria ya Kupiga Kura ni lazima kwanza waandikishwe katika Daftari na kupata Kadi kama Kitambulisho kinacho thibitisha kuwa ameandikishwa na ndicho atakachotumia kujitambulisha siku ya kupiga kura. Hivyo, ni muhimu sana kuwa na Daftari la Wapiga Kura linaloaminika ili kuhakikisha kuwa wote wanaopiga kura kweli ni wale tu walioandikishwa. 

Kutokana na chaguzi zilizopita, za mwaka 2010, Chaguzi Ndogo za Igunga, Arumeru Mashariki, Kalenga na Chalinze, Daftari lililokuwa linatumika limekuwa lilalamikiwa Tume imelalamikiwa sana hivyo, linahitaji kuboreshwa. 

Hivyo, Tume ilifanya tafiti za kutosha katika nchi mbalimbali ikiwemo wenzetu wa Zanzibar na tuliridhika kwa dhati kuwa, Kuboresha Daftari kwa mfumo wa BVR unafaa. Hata hivyo, kwa Tanzania mfumo huo utatumika kwa Kuandikisha Wapiga Kura tu na siyo kwa shughuli nyingine za Mchakato wa Kupiga Kura. 


Kwa kuwa kazi ya kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ni ya msingi kabla ya zoezi la Kupiga Kura, Tume wakati wote imesisitiza kuwa jukumu lake la kwanza ni kukamilisha kazi ya Kuboresha Daftari. Mengine yatafuata baada ya hapo.

Kama inavyofahamika, zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari, 2015 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mkoani Njombe. Zoezi lilianza kwa kutumia vifaa 250 vya BVR vilivyokuwa vimefika nchini na ndivyo pia vilitumika wakati wa Zoezi la Majaribio katika maeneo ya Kawe Dar es Salaam, Kilombero Morogoro na Mlele Mkoani Katavi. 

 Pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika matumizi ya mfumo huu, kwa ujumla zoezi limeendelea vizuri. Mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana. Kwa mfano katika maeneo fulani ya Kata mbili tumeongeza muda ili kumaliza Uandikishaji kwa wananchi waliojitokeza. 
Inatarajiwa kwamba, zoezi litakamilika Mkoani Njombe tarehe 18/04/2015. Hadi kipindi hiki kwa Kata ambazo Tume imeishapita, hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza Kituoni ambaye aliachwa kuandikishwa. 

Tume inawahakikishia wananchi kuwa wakati ambapo vifaa vingine vya BVR vinaendelea kupokelewa na Tume wanachi wote watakaojitokeza katika Mikoa mingine nchini wenye sifa wataandikishwa. Baada ya zoezi kukamilika Mkoani Njombe, kwa tarehe zitakazo ainishwa, Tume itaendelea na Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Mikoa ya Ruvuma, iringa, Mtwara, na Lindi. 

Kama ilivyofanyika Mkoani Njombe ni tegemeo la Tume kuwa Mikoa inayofuata itawahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yao na kujiandikisha kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye Mikoa husika. Ni upotoshaji kwa wananchi kwamba mistari/foleni ni dalili ya ubovu wa mfumo wa BVR badala ya kuonyesha kwamba ndiyo kukolea kwa demokrasia nchini. 

Mara kwa mara, Tume imeulizwa itakuwaje kama tarehe 30 April, 2015 inakaribia na Tume haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi.

haijakamilisha Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi kwa jumla hali itakavyokuwa.
Kwa muktadha huo leo tarehe 02/04/2015, Tume inapenda kuwaarifu wananchi kama ifuatavyo;
i. Kwa vile kazi ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ya msingi kabla ya Zoezi la Kupiga Kura na kutokana na uzoefu tuliopata Mkoani Njombe, Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura bado halijakamilika Mkoani Njombe na katika Mikoa mingine. 

ii. Kwa vile zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijakamilika, Tume haitaweza kuendelea na zoezi la upigaji wa kura ya maoni.  
Hivyo, kwa heshima na taadhima Tume inawaarifu kuwa Zoezi lililotangazwa awali la Kura ya Maoni kufanyika tarehe 30 Aprili, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.



Introducing HARAKATI TV show Hosted by KALAPINA on Clouds TV every sturday @ 7 - 730pm: EPISODE 1 -2015

FILIKUNJOMBE AIPONGEZA NEC ASEMA JK ATAKUMBUKWA DAIMA NA WATANZANIA

0
0


mbunge  wa  jimbo la  ludewa Deo Filikunjombe akishiriki ibada ya pasaka na  waumini wa kanisa  la RC MAVANGA.
PAROKO WA MAVANGA AKIMKABIDHI MBUNGE FILIKUNJMBE  ZAWADI YA  KUKU BAADA YA MBUNGE  HUYO  KUTOA ZAWADI  MBALI MBALI KATIKA MAKANISA YA LUDEWA ZIKIWEMO BATI 300 NA VITI.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Wafanyakazi wa Benki ya CBA washerehekea pasaka na watoto yatima

0
0
Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Centre kilichopo jijini Dar es Salaam,Sister Anna Marandu (Kulia) akipokea msaada wa chakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa kituoni hapo kutoka kwa Meneja wa benki ya CBA tawi la barabara ya Nyerere, Nuru Mwangulangu wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali na kucheza na watoto leo ikiwa ni moja ya shamrashamra za kkuwapa burudani katika kipindi hichi cha Sikuu ya Pasaka.Wengine pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Msimbazi wakifurahia zawadi mbalimbali zilizotplewa kwa ajili yao na benki ya CBA,waliosimama ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ambao wametembelea kituo hicho kwa ajili ya kuitoa zawadi mbalimbali na kucheza na watoto ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja na msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Msimbazi kilichopo jijini Dar es Salaam.Sr.Anna Marandu na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto hao leo ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Pasaka.

The Avenue Mawazohuru S04 EP12 katika mahojiano na Millard Ayo


WAZIRI MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE NA SERIKALI KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI KUDUMISHA AMANI,UTULIVU NA UADILIFU NCHINI

0
0
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akionyesha tuzo yake mbele ya umati wa watu (hawapo pichani),aliyotunukiwa kwa mchango wake mkubwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii,katika tamasha la pasaka.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika tamasha la 15 la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutubi maelfu ya watu waliohudhuria Tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba  amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.

Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.

Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.

Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza  na Zambia.
 Mwanamuziki wa Kimataifa wa nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope akicheza na shabiki wake kwa staili ya pekee kabisa,huku uwanja ukilipukwa na mayowe kila kona.
 Mwimbaji nguli wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu pichani kulia akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa kwa pamoja  katika lamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
 Mdau wa muziki wa Injili Emmanuel Mbasha akipa kitu cha Selfie na rafiki yake ndani ya uwanja wa Taifa wakati wa tamasha Pasaka lililofanyika April 5 jijini Dar na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.
 Kwaya ya Kijitonyama wakiimba katika tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
  Sehemu ya umati wa Watu waliohudhuria tamasha la 15 la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe wakimkaribisha jukwaani Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe pichani kulia ni Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly.

TASWIRAZZZ MWANANA ZA JIJI LA DAR

ALI KIBA AFUNIKA SHOO YA MWANA DAR LIVE, ACHEKECHA NA KUCHEKETUA

0
0
MSANII wa kizazi kipya anayetamba na wimbo wa Chekecha Cheketua, Ali Saleh ‘Kiba’ amewapagawisha vilivyo mashabiki wake waliojitokeza katika shoo ya Mwana Dar Live kwenye Sikukuu ya Pasaka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani, Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Ali Kiba akiwa sambamba na mdogo wake Abdul Kiba waliangusha bonge la burudani huku wakiimba nyimbo zao zote kwa kutumia vyombo vya jukwaani ‘live band’.

Shoo hiyo ilisindikizwa na Isha Mashauzi akiwa na Mashauzi Classic, Msaga Sumu na Pamela Daffa 'Pam D' ambao walitoa burudani ya nguvu na kuzikonga nyoyo za mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo.

Mwanamuziki Ali Kiba akizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika Dar Live katika shoo yake ya Mwana Dar Live iliyokuwa ikipigwa kwa 'Live Band'.

Ali Kiba na mdogo wake Abdul Kiba wakichekecha na kucheketua.

Mashabiki wa Ali Kiba wakishow love.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Masauni Akibidhiwa Cheti cha Mchangio wake kwa Vijana Dhidi ya Amani kutoka UNESCO NA YUNA

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na Mlezi wa Jumuiya ya Tanzania Yuoth Icon (TAYI) Mhe.Eng Hamadi Yussuf Masauni akikabidhiwa Cheti cha Mchango wake kwa Vijana kuhusiana na Amani kutoka kwa Mratibu wa UNESCO kwa Vijana Tanzania Ndg Simba Mwinyi Simba kwa kutambua mchango wake kwa Vijana Zanzibar kudumisha amani, hafla hiyo mefanyika katika Kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema Zanzibar    
Mhe.Eng Hamad Masauni akionesha Cheti baada ya kukabidhiwa wakati wa Kongamano la Vijana wa TAYI . 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

MWILI WA HAYATI MZEE MGAWE UMEWASILI TANZANIA

0
0
IMG-20150406-WA0061Maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania wakipokea mwili wa hayati mzee Eddis Mgawe ulipowasili leo Jumatatu kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam Tanzania (JIA) kutoka Washington Dc. Mzee Mgawe alikuwa ni kamishna mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini na alifariki dunia wiki iliyopita nchini Marekani alikokuwa anawatembelea wanae.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images