Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WADAU WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA MATIBABU MKOANI RUKWA WAPEWA ELIMU YA UTARATIBU WA MIKOPO MBALIMBALI INAYOTOLEWA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akichangia na kufunga Semina maalum ya siku moja iliyoendeshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuwaelimisha wadau wa vituo mbalimbali vya kutolea huduma za matibabu Mkoani Rukwa juu utaratibu wa Mfuko huo katika kutoa mikopo ya vifaa tiba, dawa na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za matibabu. Lengo kuu la utaratibu huo ulioanzishwa na Mfuko wa Bima ya Taifa ni kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wake na watanzania kwa ujumla. Semina hiyo imefanyika leo tarehe 02/03/2015 katika ukumbi wa RDC Mkoani Rukwa, Ndugu Pangisa amewaasa wadau hao kuchangamkia fursa hiyo kuimarisha huduma katika vituo vyao.
 Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Rukwa Ndugu Abdiel Mkaro akizungumza katika semina hiyo. Ndugu Mkaro alisema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanza utaratibu wa kuwakopesha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za matibabu Mkoani Rukwa, lakini jambo la kushangaza wengi wao wamekuwa hawatumii fursa hiyo vizuri kwani baadhi yao wamediriki hata kutofuatilia maombi yao na kutelekeza barua zao ambazo wameshakubaliwa. Aliwaasa wadau hao kutumia fursa hiyo ili kuboresha huduma katika vituo vyao.
Mtoa mada mkuu katika Semina hiyo ndugu Yesaya Irira (Kulia) ambaye ni Afisa Mipango na Uwekezaji Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Makao Makuu akizungumza katika Semina hiyo ambapo amesema mikopo hiyo inatolewa kwa vituo vyote vya Serikali, vya Binafsi na vya Kidini kwa kigezo kikuu kuwa kituo hicho kiwe kimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kutoa huduma kwa wanachama wake. Aliongeza kuwa miongoni mwa taratibu za kupewa mkopo ni pamoja na Mkopaji kujaza fomu ya maombi ambapo kiwango cha Mkopo kitategemea wastani wa madai ya kituo kwa huduma zitolewazo kwa wanachama wa Bima ya Afya ambayo pia yatakuwa dhamana kuu ya Mkopo husika katika madai ya kila mwezi. Kwa Mkopo unaozidi Milioni tano Mkopaji atatakiwa kuweka dhamana yenye thamani ya mkopo na kwa upande wa mkopo wa kifaa tiba hufanyika kuwa dhamana ya mkopo mpaka marejesho ya Mkopo yatakapokamilika.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

JUST IN: Tume ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza kuahirishwa kwa zoezi la Kura ya Maoni hadi hapo itakapotangazwa tena

LORI LAFELI BREKI NA KWENDA KUPARAMIA PRADO

$
0
0
Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 255 CRN na lililokuwa na Tela lenye namba za usajili T 478 BCG likiwa limefunga njia baada ya kufeli breki lilipo kuwa kwenye njia kubwa katika eneo la Mbezi Mwisho, Jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Dereva wa Lori hilo aliejitambulisha kwa jina moja la Bw. Sendegwa, alisema kuwa alianza safari yake ya kutoka Mkoani Singida akiwa vizuri kabisa na alipofika maendeo ya Kibamba alihisi gari yake kupoteza upepo lakini kwa wakati huo alikuwa kwenye mwendo mdogo tayari na alianza kujarubu kutafuta namna ya kusimama lakini hakufanikiwa, na alipofika maeneo ya Mbezi aliona sehemu ya kuchepuka ambayo aliona ni salama kwa upande wake na ndipo alipoamua hivyo na huko alikutana na Gari dogo aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 902 DCS ambapo alilipiga pasi ubavuni na kwenda kukita kwenye baraza la moja ya nyumba zilizokuwepo kwenye eneo hilo.Hakuna aliejeruhiwa wala kupoteza maija kwenye ajali hiyo.
 Lori hilo linavyoonekana baada ya kufeli breki na kuja kusimama hapo.
 Muonekano wa Prado hiyo baada ya kupigwa pasi na Lori hilo.

RADIO DW-BONN YAMUHOJI KAMANDA RAS MAKUNJA,AZUNGUMUZIA MAFANIKIO NA CHANGA MOTO ZA MUZIKI WA KIAFRIKA BARANI ULAYA

$
0
0
Bonn, Asubuhi na mapema tu Radio Deutch Welle Idhaa ya Kiswahili inayorusha matangazo yake mjini Bonn,Ujerumani, ilimwamkia mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu ya dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni.

katika mahojiano na mtangazaji mahiri Bi. Swaumu Mwasimba wa radio DW na kipindi cha muziki na utamaduni, Kamanda Ras Makunja amezungumzia mafanikio na changamoto za muziki wa kiafrika barani ulaya.pia amezungumizia jinsi muziki wa kiswahili unavyokubalika barani ulaya.usikose kusikiliza mahojiano hayo katika tuvoti za radio DW-Kiswahili http://www.dw.de/idhaa-ya-kiswahili/habari-za-ulimwengu/s-11590

NMB yadhamini Mkutano wa Serikali za Mitaa kwa Shilingi Milioni 200

$
0
0
Benki ya NMB imedhamini mkutano mkuu wa serikali za mitaa (ALAT) utakaoanza tarehe 8 April mpaka Tarehe 11 April, 2015 katika katika hotel ya Kunduchi beach ya jijini Dar es Salaam.

NMB imetoa shilingi milioni 150 kwaajili ya kufanikisha mkutano huo na shilingi milioni 50 kwaajili ya ununuzi wa trekta litakalotolewa kama zawadi kwa meya (Mayors Award) na halmashauri iliyofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali kama utawala bora na utengenezaji wa miradi ya kiuchumi.

Udhamini huo unaifanya NMB kuwa wadhamini wakuu wa mkutano wa ALAT kwa mwaka wa pili mfululizo.

Hii ni mara ya pili kwa NMB kudhamini mkutano mkuu wa mwaka wa ALAT ambapo mwaka 2014, NMB ilitoa shilingi milioni 150 kabla ya leo hii kumwaga udhamini wa milioni 200 kwa mkutano mkuu wa mwaka huu wa ALAT.
Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi akitangaza maadhimisho ya mkutano mkuu wa 31 wa ALAT -2015. Pembeni ni Afisa Mkuu Fedha wa NMB – Waziri Barnabas na Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw. Abraham Shamumoyo.
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akikabidhi mfano wa hundi kwaajili ya udhamini wa mkutano mkuu wa ALAT – 2015 kwa mwenyekiti wa ALAT taifa na meya wa Jiji la Dar es Salaam Dr Didas Masaburi . Katikati ni Katibu Mtendaji wa ALAT – Bw Abraham Shamumoyo. 
Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB – Waziri Barnabas akitangaza udhamini wa NMB katika mkutano mkuu wa ALAT Taifa mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa Karijee jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa ALAT taifa na Mstahiki Meya wa Dar es Salaam - Dr Didas Masaburi na pembeni ni Katibu Mtendaji wa ALAT - Bw Abraham Shamumoyo.

MKUTANO WA TAKWIMU WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),kutokaTanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Uganda Bw. Ben Mungyereza akizungumza jambo wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwi mu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashari kikuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw. Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Takwimu Kenya Bw.Zachary Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WACHUNGAJI WATAKIWA KUWARUHUSU WAUMINI KUHUDHURIA TAMASHA LA PASAKA

$
0
0

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka. Kushoto ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama. (Picha na Francis Dande)
 Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka.
Mwenyekiti wa tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamashas la Pasaka. Kulia ni Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel  ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste, David Mwasota.

NA LOVENESS BERNARD

Askofu wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly,  David Mwasota amewataka wachungaji wote nchini  kuwaruhusu waumini wao kuhudhuria katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika April 5 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Askofu huyo amewataka wachungaji wawaruhusu waumini waweze kusherehekea kufufuka kwake Yesu kristo kwa kusifu  na kuabudu pamoja na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
 
Nawaomba wachungaji wawaruhusu waumini baada ya ibada waje uwanja wa taifa tumsifu muumba wa vyote kwa nyimbo na sala pamoja na waimbaji kutoka mataifa mbalimbali.

Naye Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama alisema waimbaji wameshaanza kuwasili nchini wakiongozwa na Faustine Munishi (Malebo) ambaye aliwasili jana huku Kerechi muimbaji kutoka Uingereza  akitarajiwa kuwasili Jumamosi.

Maandalizi tumekamilisha kwa asilimia 99 na waimbaji wameanza kuwasili nchini ambapo Faustine Munishi mtanzania aishie nchini Kenya na kesho tunatarajia kumpokea Ifeanyi Kerechi na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia huku Rebecca Malope na Solly Mahlangu tukuwatarajia kuwasili Aprili 3 alisema Msama.

MADEREVA WAFUNDWA NA TANROADS KUHUSU MZANI WA KISASA WA VIGWAZA

$
0
0
Eng. Japhet Kivuyo kutoka kitengo cha mzani wa Vigwaza mkoani Pwani akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea mzani huo jana jijini Dar es salaam.
Taa ya mzani wa Vigwaza ikielekeza gari lililobeba mzigo mzito kupinda kushoto kwa ajili ya ukaguzi wa kina. Changamoto kubwa iliyopo madereva hawafati taratibu za taa na wengine hawazielewi.
Kamera zilizounganishwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) eneo la mzani wa Vigwaza zikirekodi matukio mbalimbali yanayotokea katika eneo hilo ili kutambua magari yanayotii na kuvunja sheria.


KITABU CHA DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI CHATINGA MTAANI

$
0
0
Mdau wa maendeleo wa wilaya za Handeni na Kilindi, mkoani Tanga, bwana Amiri Mganga, mwenye t-shirt nyekundu, akikabidhiwa nakala ya KITABU CHA DIRA NA TUMAINI JIPYA HANDENI, kilichoandikwa na Kambi Mbwana, kutoka kwa Msemaji wa Coastal Union, Assenga Oscar ambaye pia ni Mwandishi wa habari wa New Habari 2006 Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai, Dimba, Bingwa na The African, leo jijini Tanga, Tanzania.

Kitabu hicho kinapatikana kwa Sh 3500 tu. Maeneo yanapopatikana kitabu hicho ni pamoja na Handeni Mjini kwa Ayubu Magazeti soko la zamani, Misima, Sindeni, Kwamatuku, Komsala, Korogwe, Tanga Mjini na Dar es Salaam. Kama unahitaji kitabu hicho wasiliana nasi kwa simu +255 712053949, kambimbwana@yahoo.com.
Picha na Mpigapicha Wetu.

UMOJA WA MATAIFA WAFADHILI USAMBAZAJI WA KATIBA INAYOPENDEKEZWA KWA NJIA YA SAUTI

$
0
0
Pamoja na Tume ya  Taifa ya Uchaguzi kuahirisha  tarehe ya kupiga kura ya maoni, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Elimu na Utamaduni (UNESCO), kwa kushirikiana na Kampuni ya Focus Media pamoja na Mtandao wa radio za jamii  (COMNETA), limeamua kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti nchi nzima, ili wananchi wapate elimu  kuhusu maudhui yaliyomo ndani ya Katiba na kufanya maamuzi sahihi pindi siku ya kupiga kura itakapowadia. 

Aidha, mkakati huo wa kusambaza Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti unajumuisha utoaji elimu kuhusu mfumo mpya wa kujiandikisha kwa njia ya kieletroniki (Biometric Voters Registration – BVR) pamoja na kuhamasisha wananchi ili wajitokeze kwa wingi kujiandikisha na kutimiza haki yao ya kikatiba wakati wa upigaji kura.

Akipokea, nakala za CD zenye Katiba inayopendekezwa kwa njia ya sauti, Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez, alipongeza Kampuni ya Focus Media kwa kuandaa matoleo hayo na kusisitiza radio za jamii kuzitumia ili kuwaelimisha wananchi mikoa yote juu ya Katiba inayopendekezwa.

 “Nimefurahi sana kuona hizi nyenzo za kisasa kama SD cards, kwa sababu tunaonesha kwamba radio za jamii ni njia bora zaidi za kutoa taarifa na pia zinawezesha kupata mrejesho kutoka kwa wananchi.”

Bi Zulmira Rodrigez, ameongeza kusema “Hili ni jambo zuri sana kwa jamii, na inapeleka taarifa mpaka katika njia ya chini kabisa, vijiji vilivyoko ndani kabisa.”  

Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku amewashuri watangazaji wa redio mbalimbali wliohudhuria semina hiyo amewaasa kutumia muda uliobai wa siku28 vizuri ili kuelimisha jamii maudhui ya Katiba inayopendekezwa ili wananchi wafanye maamuzi sahihi katika kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

Sekiku ameongeza kwamba kwa sasa itapatikana kupia Focus Media pro ltd kwa kupitia mitandao yote ya kijamii na redio mtandao na wananchi wanaweza kuwasiliana kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba +255 772 55 55 53
Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO nchini Tanzania Bi Zulmira Rodrigez akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii Bwana Joseph Sekiku.

BASATA YAPIGA MARUFUKU DISKO TOTO NA UKIUKAJI WA SHERIA ZA UENDESHAJI KUMBI ZA BURUDANI KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA PASAKA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa utumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu.

Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kumezwa na faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa ambayo yangedhibitika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

BASATA kama mtoaji wa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa sherehe njema ya Pasaka yenye furaha tele. 

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini

Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 61

Moto wa burudani kuwaka ufukweni Coco Beach Pasaka

$
0
0
Katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka kwa furaha,wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wataweza kupata burudani za aina mbalimbali katika tamasha kubwa la Pasaka litakalofanyika katika ufukwe wa maraha wa Coco beach chini ya maandalizi ya Vodacom Tanzania.

Akiongea juu ya tamasha hili kubwa ambalo hivi sasa limeanza kuwa gumzo ya jiji,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema mipango yote kuhusiana na tamasha hilo imekamilika kinachongojewa ni kuwasha moto wa burudani kwa wateja wa Vodacom na wananchi wote kwa ujumla.

“Kama ilivyo kawaida yetu ya kuwapatia huduma bora wateja wetu sambamba na kuwaburudisha zamu hii tumewaandalia tamasha hili ili waweze kuburudika katika kuadhimisha sikukuu ya Pasaka ambapo pia watapata fursa ya kukutana na wasanii mbalimbali wawapendao na kuwa karibu nao ukiwa ni mwendelezo wa promosheni ya Vodacom ya kuleta burudani kwa wateja inayojulikana kama Ishi Kistaa”.Alisema.

Nkurlu alisema kuwa tamasha hilo litakalofanyika siku ya Jumapili ya Pasaka litaanza asubuhi saa tano kwa burudani mbalimbali za muziki na michezo kwa ajili ya watoto ambapo baadaye jioni wasanii mbalimbali wa bongofleva na aina nyingine ya muziki watapanda jukwaani kutoa burudani kwa washabiki watakaohudhuria kwenye tamasha hilo.

Alisema wako wasanii wengi wamejipanga kutoa kuburudisha wapenzi wa muziki baadhi yao wakiwa ni Shilole  na Bob Junior na wengineo. “Wateja na mashabiki watapata fursa ya kuonana na mastaa  ambao wanawapenda pia tunawakumbusha wachukie nafasi ya kushiriki katika promoshe ya Ishi kistaa kwa kutuma neno STAR kwenda 15670”.

Alimalizia kwa kusema kuwa  hali ya amani na usalama inatarajiwa kutawala kwenye tamasha hili kwa kuwa kuna ulinzi wa kutosha kuhakikisha wananchi wanapata burudani murua kwa utulivu wakiwa na familia zao na aliahidi kuwa wateja wa Vodacom na wananchi wengine wanaokaa mbali na Dar es Salaam wakae mkao wa kula kwa kuwa mikakati inaandaliwa kupeleka burudani za aina hii katika sehemu mbalimbali nchini kwenye sikukuu mbalimbali zijazo katika siku za usoni.

bei ya Madafu leo

Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini watoa tamko dhidi ya muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao,2015

$
0
0
 Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa mawasiliano mitandaoni.  
Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.

MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015
Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015 kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa kutumia mitandao na yapi yanakubalika 
Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea habari.
 Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu. 
Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa sahihi?
 Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari. 
Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu kihisia. 
Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013. 
Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’ 
Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa habari nchini. 
Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa na kupokea habari. 
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika
 IMETOLEWA NA;
Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network-TBN)
04/03/2015.

IBADA YA IJUMAA KUU YA PASAKA KATIKA KANISA LA KKKT AZANIA FRONT JIJINI DAR LEO

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwa ameungana na Waumini wengine katika Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front la Dar es Salaam leo.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu ya Pasaka iliyofanyika leo.

Sehemu ya Waumini wa Kanisa la KKKT Azania Front jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye Ibada ya Ijumaa Kuu leo.
Yesu akiwa amebebeshwa Msalaba katika Igizo hilo.
Muumini wa Kikristo, Moses Kombe akitungikwa msalabani kama Yesu katika igizo lililofanywa na Vijana wa Umoja wa Kwaya zote za Usharika wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front, Jijini Dar es salaam, wakati wa ibada ya Ijumaa Kuu leo.

Wakulima wa Kahawa Mbozi kunufaika na bilioni 1.35 kutoka Heifer International

$
0
0
Na. Mwandishi Wetu

Shirika lisilo la Kiserekali la Heifer International limepokea ufadhili wa Shilingi bilioni 1.35 (USD 750,000) kutoka Starbucks Foundation ili kuwasaidia  wakulima wadogo wadogo wilayani Mbozi kupitia mradi wa Heifer unaojulikana kama “Mbozi Farmer Livelihood Improvement Project”. Fedha hizi zinatarajia kuziwezesha jumuiya za wakulima wadogo wadogo wa zao la kahawa wa nchi za Afrika Mashariki kuboresha na kuinua viwango vya maisha.

Fedha hizi ni sehemu ya mkakati wa Starbucks wa kujipatia kahawa yenye ubora madhubuti kwa kuwasaidia wakulima wa zao hilo,kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Mpaka sasa Starbucks Foundation imechangia  jumla ya dola za kimarekani milioni 15 ,  kwenye miradi mbali mbali ya jamii duniani.Mradi huu utakuwa ni sehemu ya Mradi wa Uendelezaji wa Sekta ya Maziwa Afrika Mashariki (EADD) nchini Tanzania na unatarajiwa kusaidia wakulima wadogowadogo wa kahawa wapatao 5,000.

Heifer na Starbucks walianza kutekeleza miradi pamoja zamani. Mwaka 2009 , baada ya Mkurungenzi Mkuu Howard Schultz kutembelea wakulima wadogowadogo wa kahawa nchini Rwanda; alisikiliza maombi ya wakulima – waliosema kwamba wakipata ng’ombe ; wataweza kupata Maziwa, lishe bora na kipato Zaidi kwa familia zao. Wafanyakazi wa starbucks walikusanyika kutafuta hao ng’ombe kwa ajili ya wakulima wa Rwanda.

NEWS ALERT: WASHABIKI WA TIMU YA SIMBA WAPATA AJALI MKOANI MOROGORO LEO, NANE WAPOTEZA MAISHA

$
0
0
Ajali mbaya imetokea leo maeneo ya Makunganya, Barabara kuu ya kutoka Morogoro kwenye Dodoma baada ya gari iliyokuwa imewabeba washabiki wa Timu ya Simba Sports Club kupoteza muelekea na kuingia porini, watu nane wamepoteza maisa na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya. 

Hili ni pigo kubwa sana kwa Timu ya Simba, tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

Globu ya Jamii inatoa pole wa Klabu ya Wekundu wa Msimbazi kuwa kuondokewa na washabiki wake hao, na Mungu aziweke Roho za Marehemu hao mahala pema Peponi, Amin.
Zoezi la uokoaji wa watu waliokuwa ndani gari hilo ikiendelea.
Muonekano wa gari hilo baada ya ajali.


PRESIDENT KIKWETE VISITS THE BILL GATES FOUNDATION AND BOEING PLANT IN SEATTLE

$
0
0
President Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation are received and later holds talks with the Chairman of the Bill and Melinda Gates Foundation, Mr Bill Gates, at the foundation's headquaters in Seattle on April 2, 2015.
President Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation are shown around the offices of the Bill and Melinda Gates Foundatio in Seattle on April 2, 2015.
President Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation visit the Boeing planes manufacturing plant in Seattle on April 2, 2015.

WAIMBAJI KUTOKA UINGEREZA WATUA KUNOGESHA TAMASHA LA PASAKA JUMAPILI UWANJA WA TAIFA.

$
0
0
 Nyakwesy Mujaya akimpa au mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Uingereza, Ifeanyi Kelechi.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Uingereza, Ifeanyi
Kelechi, akipokea ua kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Msama Promotions, Nyakwesy Mujaya, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam le kwa ajili ya kutumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka. Kulia ni Mwenyekiti wa tamasha hilo, Alex Msama.
 Msama akipeana mkono na Ifeanyi Kelechi.
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images