Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 790 | 791 | (Page 792) | 793 | 794 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akipanda mti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye kilelele cha maadhimisho ya upandaji miti yaliyofanyika kimkoa wilayani Kinondoni leo. Wa tatu kulia anayeshuhudia upandaji miti huo ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
   Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
   Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa Manispaa Kinondoni jinsi ya upandaji wa mimea mbalimbali pamoja na miti kwa kutumia matairi ya magari yaliyotumika.
   Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamebeba miche ya miti wakielekea kuipanda katika maeneo mbalimbali shuleni hapo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  A Panel discussant from Parliament of Tanzania Hon. Suzan Lyimo makes her points during the IPU committee on UN Affairs at the 132 Inte- Parliamentary Union in Hanoi, Vietnam yesterday.
  A Panel discussant from Parliament of Tanzania Hon. Suzan Lyimo (left) makes her points during the IPU committee on UN Affairs at the 132 Inte- Parliamentary Union in Hanoi, Vietnam yesterday.
  The Special Invited Guest during the discussion on “The Convention on the Rights of the Child 25 Years on: Are Children’s Lives Better? Organized by the IPU Standing Committee on Democracy and Human Rights during the 132 Assembly, Hon. Lediana Mafuru Mng’ong’o (MP) from Tanzania noting some comments from the delegates after presenting her paper on Right to Nutrition in Hanoi, Vietnam, yesterday.
  Delegates of the 132 Assembly of the IPU in Hanoi VietNam. Photo By Owen Mwandumbya

  By, Owen Mwandumbya,
  Hanoi, VietNam

  Members of the Inter-Parliamentary Union (IPU) have expressed their satisfaction on the committed done by the Parliament of Tanzania on taking the necessary action to cooperate with the United Nation Agencies for building a strong and committed Parliament through capacity building programs coordinated by the UN.

  The comments was made by the Parliamentarians during the discussion on report of the field visit of the Advisory Group to the IPU Committee on United Nations Affairs to Tanzania conducted in 2008 to gather first-hand information about the progress made in the One United Nations reform and, more generally, to gain a better understanding of the complexities of UN field operations during the 132 IPU Assembly, in  Hanoi, Vetnam.


  0 0

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti wa kampuni hiyo, Gaurav Dhingra wakionyesha ishara dole wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
  Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampunihiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI

  MAONESHO YA KIMATAIFA YA VITO YA ARUSHA
  TAREHE 21-23 APRILI, 2015

  Wizara ya Nishati na Madini (MEM) kwa kushirikiana na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wanawaalika wadau wote wa Sekta ya Madini na wamiliki wa leseni za biashara ya madini, Masonara na wachimbaji wa madini ya vito kushiriki kwenye Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Vito ya Arusha (Arusha Gem Fair-AGF 2015). Maonesho haya yatafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya Arusha, kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili, 2015.

  Maonesho ya AGF kwa mwaka 2015 yanalenga kuendeleza azma ya kuifanya Arusha kuwa kituo cha madini ya vito Afrika. Pia maonesho haya yatawakutanisha washiriki (exhibitors) zaidi ya 100 kutoka nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini na wanunuzi wa kimataifa zaidi ya 1000 pamoja na wadau mahiri wa tasnia ya vito. Maonesho haya yanadhamiria kuendeleza biashara ya madini ya vito katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

  Mabanda ya maonesho yanapatikana kwa gharama za Dola za Marekani 1,000. Kamati ya Maonesho inasimamia ugawaji wa mabanda hayo kwa ushindani (first come-first be served).

  Taarifa kuhusu usajili zinapatikana katika Ofisi za Madini za Kanda zilizo katika Miji ya Arusha, Mwanza, Dar es salaam, Mtwara, Mpanda, Shinyanga, Mbeya, Musoma, Songea na Singida au Ofisi za TAMIDA. Wanunuzi wanatakiwa kujisajili kupitia tovuti ya maonesho: www.arushagemshow.com; au kwa barua pepe ya maonesho: info@arushagemshow.com; au kwa njia ya simu zifuatazo 0786366968, 0767498869 na 0767223387.

  KATIBU MKUU

  0 0


  0 0

  TWIGA STARS KUIVAA SHE-POLOPOLO.

  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10, Aprili  mwaka huu, itashuka dimbani  Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The She-Polopolo).

  Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika mwaka huu.

  Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).

  Mshindi wa jumla katika mchezo huo atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya nchini Congo - Brazzavile kuanzia Septemba 13 mwaka huu.


  VPL KUENDELEA JUMAMOSI
  Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na michezo mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.

  Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

  Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo Mlandizi.

  Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya  Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.


  KILA LA KHERI YANGA.

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru Bulawayo.

  Malinzi amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.

  Endapo Young Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh ya Tunisia.
       
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).

  0 0

  AutoSueco Tanzania (Volvo) has appointed Alen Nkya as new Commercial Manager CE, a unit whose primary function is to run overall Construction Equipment business which also comprises of mining machines. He joins from April, this year.

  In a statement released today states that Mr. Nkya has over 10 years' experience in the industry. Formerly a Sales Manager CE at Hyundai, he has an outstanding track record of achievements in Marketing, Business Development and Customer Relations.
  “I'm looking forward to this new challenge,” said Mr. Nkya. “Tanzania is one of the key markets with great potentials, so we must prosper in here and not just stay."

  AutoSueco is a subsidiary of Nors Group, the leading supplier of Trucks, Construction Equipment, Power Generators and Industrial Engines. Established since 1949 with HQ in Porto, Portugal; it has several brands worldwide.

  0 0

  NA MWANDISHI WETU, TANGA.

  Timu ya Coastal Union imeanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu za wapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.

  Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala salama.

  Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.

  Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.

  Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.

  Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao.
  wachezaji wa Coastal Union wakiwa na mazoezi jana kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly chini ya Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu "Julio".
  Kocha Mkuu wa Coastal Union ya Tanga,Jamhuri Kihwelu "Julio"amimnyajua mlinda mlango wa timu hiyo,Shabani Kado mara baada ya kumalizika mazoezi ya timu hiyo.

  0 0
 • 04/02/15--04:29: Bei ya Madafu leo

 • 0 0

  Aprili Mosi kila mwaka huwa ni siku ya kupanda miti kitaifa na mwaka huu 2015 mkoa wa Kagera ulipewa heshima ya kuadhimisha siku hiyo ambapo iliadhimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi na kushirikisha wadau mbalimbali pamoja na wananchi wanaojihusisha na kupanda miti na kutunza misitu.

  Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Celestine Gesimba kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo maadhimisho hayo yalianzia katika Kijiji cha Bugolola eneo la Omukajunguti kwa kupanda miti 2100 kwa kushirikisha washiriki wote na wananchi wa kijiji hicho.

  Kauli mbiu ya siku hiyo ilikuwa ni “Misitu ni Mali Panda Miti.” Katika Hotuba yake Naibu Katibu Mkuu Bw. Gesimba alisema wizara yake siyo kwamba inahamasisha wananchi kupanda miti ili kulinda mazingira tu bali wananchi wapande miti ili kunufaika nayo kwani ni mali inayoingiza kipato kikubwa kwa mwananchi mmoja mmoja.

  Bw. Gesimba alisema wananchi wanatakiwa kupanda miti kwa wingi kwani miti isipopandwa itasababisha maafa makubwa hapo mbeleni kama inavyoanza kuonekana kwa sasa mfano, ukosefu wa mvua au mvua kutonyesha kwa wakati, joto jingi, kuyeyuka kwa theruji mlima Kilimanjaro.
  Bw. Gesimba alimalizia hotuba yake kwa kusema kuwa kutotunza misitu kumesababisha baadhi ya sehemu kuwa jangwa au kusababisha ugonjwa wa malaria mfano Lushoto mkoani Tanga ambako hakukuwa na ugojwa huo miaka ya 1970 na 1990. Aidha alitahadhalisha misitu kutoweka kabisa kwani   kila baada ya dakika sita (6) nusu kiolmeta ya misitu hutoweka duniani.


  0 0

  Jikekizz la nguvu la kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Radio 93.7 EFM.
  Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yussuf Mwenda akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila walipo kutana katika ofisi za EFM asubuhi ya leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mtangazaji wa kipindi cha Joto la Asubuhi, Dennis Ssebo akiwa na Mkurugrnzi Mkuu wa Radio 93.7 EFM, Francis Ciza.


  0 0

  Tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Pasaka ambayo inaanza kesho Ijumaa Kuu, Jeshi la Polisi nchini, linatoa tahadhari kwa wananchi, kuwa makini katika suala zima la ulinzi na usalama wa maisha na mali zao. 

  Uzoefu unaonyesha kwamba, katika kipindi kama hiki cha sikukuu kuna baadhi ya watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vya uhalifu. Hata hivyo, Jeshi la Polisi katika mikoa yote limejipanga vizuri kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vyovyote vya uhalifu vitakavyojitokeza na pale vitakapoonyesha dalili ya kujitokeza viweze kudhibitiwa kwa haraka.

  Aidha, ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote, yakiwemo maeneo ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.

  Vilevile, Jeshi la Polisi linawataka madereva na watu wote watakaokuwa wakitumia barabara, kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kuepuka kwenda mwendo kasi, kujaza abiria kupita kiasi na kutumia vilevi wawapo kazini. Wamiliki wa kumbi za starehe wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao hususani katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.

  Aidha, wazazi wawe makini na watoto wao, kutokuwaacha watembee peke yao ama kwenda disko toto bila kuwa chini ya uangalizi wa watu wazima ili kuepusha ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

  Wananchi wakumbuke kutokuacha makazi yao bila uangalizi na endapo italazimu kufanya hivyo watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu watoe taarifa haraka kwenye vituo vya polisi vilivyo karibu yao, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

  Mwisho, Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya biashara hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, mahoteli na maeneo ya benki. Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji wa wahalifu hao endapo uhalifu unatokea. Tunawatakia watanzania wote Pasaka njema.

  Imetolewa na:-
  Advera Bulimba -SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,Salim Abdullah akisaini makubaliano ya kuendeleza utafiti  tasisi hiyo kulia ni Mkuu wa Taasisi ya Kinga na wa China,Dk.Ning Xiao  katika hafla iliypfanyika leo jijin Dar es Salaam.(Picha Emmanuel Massaka).
   WAZIRI wa Afya  na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid akizungumza hafla ya makubaliano na Serikali ya watu wa China ( Kulia),Naibu Waziri  na Kamisheni ya Taifa ya Afya na Uzazi wa Mpango,na  Usimamizi wa Tiba Asili iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Wadau mbalimbali wakishuhudia kutiliana saini kati ya Serikali na China katika suala zima la kuwekeza katika utafiti wa Tiba asili.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

  Serikali imesema itaendeleza kufanya utafiti wa tiba asili ikiwa ni pamoja na kuanzisha baraza la tiba asili ,kutokana na kuwepo kwa mafanikio ya kutumia dawa hizo.

  Hayo aliyasema leo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Rashid wakati akisaini makubaliano na Kamisheni ya Taifa ya Afya na Uzazi wa Mpango na  Usimamizi wa Tiba Asili ya China,katika kuendeleza Wizara ya Afya  katika nyanja ya utafiti,ujenzi  wa kituo cha Moyo.

  Amesema makubaliano hayo  yataongeza  chachu kwa Wizara ya Afya na  Ustawi wa Jamii, katika maeneo ambayo kwa sasa Wizara imeongeza mkazo katika utafiti,hivyo kutokana na makubaliano   yaliyofanyika kutaongeza kasi.

  Dk.Seif amesema kuwa madaktari kutoka nchini china wamekuwa wakija katika kutoa huduma nchini hali ambayo inaonyesha ushirikiano katika sekta ya afya katika kuhudumia wananchi.

  Amesema katika matumizi ya dawa za asili nchi ya China iko mbali ambapo wameweza kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa virusi vya ukimwi.

  0 0

  Na Avila Kakingo Globu ya jamii

  MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania (TCRA) wamekanilisha mfumo wa kidijitali kwa nchi nzima.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungy, amesema Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza maazimio ya nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC ) na yale ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

  Amesema mfumo wa analojia ulizimwa rasmi Desemba 31,2012,kwa mujibu wa makubaliano ya nchi mwanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo tulianza kuzima mitambo hiyo na kuwasha ya dijitali kwa baadhi ya mikoa hapa nchini.

  Mungy amesema mpaka sasa mikoa yote ya Tanzania inatumia mfumo wa kidijitali ambapo inatumia mifumo minne tofauti ambayo ni Satelaiti, mfumo wa mitambo ya utangazaji kupitia kebo,mfumo wa utangazaji wa dijitali kwa mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi pamoja na mfumo wa utangazaji wa intaneti.
  Meneja Mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano (TCRA), Innocent Mungy (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo juu ya mafanikio waliyoyapata katikmfumo wa Dijitali.Kushoto ni Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Christopha Assenga na kulia Semu Mwakyanjala Afisa Mawasiliano mkuu TCRA.

  0 0

  Kamati ya ufundi ya Trade Facilitation and Ports Community Systems ya Shirikisho la Bandari ulimwenguni " International Association of Ports and Harbours (IAPH)" inakutana Paris , Ufaransa kujadili mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kutayarisha Mpango Kazi 2015-2017 wa Kamati hiyo, kupitia na kuandaa taarifa itakayowasilishwa kwenye World Ports Conference itakayofanyika Hamburg, Ujerumani June 2015 , ambapo pia tuzo kwa bandari bora zitatolewa. Ndg. Phares Magesa ni mjumbe wa Kamati hiyo na pia ni mmoja wa majaji wanne duniani watakaoamua na kutoa tuzo hizo. Mkutano wa Kamati hii unafanyika katika ofisi za makao makuu ya bandari ya Paris.
  Wajumbe wakiwa kwenye kikao
  Majadiliano yakiendelea.

  0 0
 • 04/02/15--07:31: APPRECIATION
 • Late Alhaj Abdulrahman I. Mongi 
  12th June 1939 – 11th March 2015

  Dear friends and family;

  We would like to convey our sincere appreciations and thanks for your help and cooperation during the difficult times that we have been facing.  Thank you for being there and supporting us.  May GOD bless and richly reward you, “For great is your reward in Heaven”.  Matthew 5:11b.  Our sincerest appreciation is to our Almighty God for giving us the gift of the life of our Father here on earth, we will rejoice in this gift by Worshiping and Praising the Lord in all the days of our lives.  
  “A tree is known by its fruit; a man by his deeds.  A good deed is never lost; he who sows courtesy reaps friendship and he who plants kindness gathers love”.

  Sincerely yours,

  Mrs. Omerga A. Mongi and the Children


  0 0

  Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili nakutoa msaada wa mashuka na nguo kwa watoto waliolazwa Hospitalini hapa. Bi. Davutoglu amesema ameguswa kutoa msaada huu kwa watoto waliolazwa na kuwatakia kupona haraka ili waendelee kukua vizuri katika jamii wanazotoka. 
  Watatu kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto akipokea msaada wa mashuka na nguo za watoto kutoka kwa Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu. Wa kwanza kulia ni Prof. Fatmah Alatar, Mhadhiri kutoka Uturuki ambaye kwa sasa yuko Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Muhimbili (MUHAS), akifuatiwa na Dkt. Jenifa Swai Daktari Bingwa wa Watoto ambapo wa kwanza kushoto ni Muuguzi Anna Mponeja, ambaye ni Meneja wa Jengo la Watoto akifuatiwa daktari wa watoto Dkt. Helena Kakumbula.
  Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Bi. Yesim Davutoglu akitoa msaada kwa akina mama wenye watoto waliolazwa wodini.
  Prof. Atalar na mke wa Balozi Bi. Davutoglu wakitoa msaada kwa mtoto “Musa” anayekadiliwa kuwa na umri wa miezi 18, ambaye hana wazazi. Mtoto huyu aliletwa na Polisi Hospitali ya Taifa Muhimbili miezi miwili iliyopita baada kuokotwa huko Mabibo akiwa ametelekezwa yeye na dada yake mwenye umri wa miaka mitano. Kwa sasa mtoto huyu anaendelea vizuri sana.

  0 0

  flavy
   Kwa mara nyengine tena Mwanamitindo afanyae kazi zake za uanamitindo nchini Marekani Flaviana Matata amepata deal ya kutangaza vipodozi vya Kiko Milano vya nchini Italy
  Flaviana na wanamitindo wenzie wanatangaza kampeni iyo iliyopewa jina la Modern Tribe.

  0 0  0 0older | 1 | .... | 790 | 791 | (Page 792) | 793 | 794 | .... | 3278 | newer