Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 786 | 787 | (Page 788) | 789 | 790 | .... | 3286 | newer

  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Tusiime kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ambapo wanafunzi hao walipata nafasi ya kumuuliza maswali na kuyajibu kabla hajafungua maabara ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo. Wengine wanaoonekana ni wageni alioambatana nao na walimu wa Tusiime.
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Akisikiliza maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa kidato cha pili sekondari ya Tusiime, Khadija Suleiman kuhusu namna ya kuchuja maji wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akipata maelezo kutoka kwa Angela Shanira wa kitado cha tano sekondari ya Tusiime Tabata kuhusu masuala mbalimbali ya kisayansi kwenye maabara ya shule hiyo wakati Waziri alipofungua rasmi maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba na mahafali ya tano ya kidato cha sita ya shule hiyo.
  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akikata utepe kuzindia maabara ya kisasa ya sayansi na maktaba ya shule ya sekondari Tusiime kabla yajatoa vyeti kwa wahitimu wa kitado cha tano wa shule hiyo. Wengine ni kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. John Mbogoma kulia kwa Waziri ni Mkurugenzi wa shule hizo, Albert Katagira, Meneja wa shule Jane Katagira, na Mkuu wa shule ya sekondari Tusiime, Emil Rugambwa.

  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Zimbabwe's President Robert Mugabe in Arusha shortly before president Mugabe officiated the opening of the 3rd Africa-China Young Leaders Forum yesterday.
  The President of Pan African Youth Union Ms.Francine Muyumba presents a Leadership Excellence Award to President Dr,Jakaya Mrisho Kikwete in recognition for his outstanding leadership in the continent especially in promoting youth development.(photos by Freddy Maro)

  0 0

  Viongozi mbali mbali pamoja na Timu zote mbili wakiwa wamesimama kwa dakika chache kumkmbuka Kiongozi wa mpira wa Miguu, Aliyetangulia mbele ya haki, Kocha wa zamani wa Timu ya Taifa Star, Marehemu Sylvester Marsh aliyefariki dunia hivi karibuni katika Hospitali ya Muhimbili na kuzikwa Mjini Mwanza.
  Wachezaji wa Malawi wakipongezana baada ya kupata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Esau Kanyenda kwa kufanya 1-0.
  Mshambuliaji wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Thomas Ulimwengu akitafuna namna za kuuchukua mpira uliomilikiwa na Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Malawi wakati wa mtanange wao uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanzawa. Mchezo huoulimalizika kwa kufungana bao 1 -1
  Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe akionyeshana uwezo wa kutunishiana misuli na Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Malawi wakati wa mtanange wao uliopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanzawa. Mchezo huoulimalizika kwa kufungana bao 1 -1.


  0 0


  0 0
  0 0

  Wananchi wa kijiji cha Mwaniko -Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano huo wa hadhara.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano huo  uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (wa nne kushoto akiwa ameongoza na viongozi mbalimbali wa chama,walipokuwa wakiwasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mwaniko Ugweno wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akishiriki usafi wa mazingira katika Mtaa wa Mlalakuwa na wakazi wa Mtaa huo wakati wa operesheni maalum ya kuweka safi mazingira.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni akioneshwa sehemu mbalimbali za Mto Mlalakuwa wakati wakiufanyia usafi.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kulia) akikabidhi viroba kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni B, Sixbert Thomas kwa ajili ya kuzuia maporomoko ya ardhi katika Mto Mlalakuwa, wakati wa operesheni hiyo.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa, Abraham Shoo (kushoto) wakati wa operesheni maalum ya kusafisha mazingira katika Kata za Manispaa hiyom Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Nicodemus Masika.


  0 0

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar Dkt Issa Haji Zidi akizungumza na vijana katika mjadala kuhusu uzazi wa mpango katika uislamu ulioandaliwa na Kitengo cha Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto kwenye ukubi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Mkufunzi kutoka Chuo cha Sayansi ya Afya ya Mbweni Asha Ali Khamis akionyesha moja ya dawa za kisasa za uzazi wa mpango katika mjadala huo.
  Mmoja wa washiriki wa mjadala kuhusu uzazi wa mpango katika uislamu Dosa Omar Machano akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa uzazi wa mpango.
  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada zilizowasilishwa katika mjadala kuhusu uzazi wa mpango katika uislamu uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Mafunzo Kilimani.
  Mshiriki wa mjada huo kutoka Mkoa Kaskazini Unguja Asha Makame Mohd akichangia mada zilizowasilishwa. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akisalimiana na Ofisa mtendaji Mkuu wa kampuni ya Property International Abdulhalim Zahran, alipowasili Hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam kwa ajili ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akihutubia Viongozi na watendaji wa kampuni ya Property International inayomilikiwa na watanzania wanaoishi Nchini Dubai wakati wa uzinduzi rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” na Jarida linalotolewa kila wiki Property International Magazine, uzinduzi huo umefanyika jana katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akizindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” uzinduzi huo umefanyika jana katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Property International LTD Mr. Mohammed Sharif baada ya kuzindua rasmi mpango wa PILA-1 “JENGA KWA MPANGO EPUKA MAKAAZI HOLELA” katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha (kulia) akiwapungia mikono wanachama alipokua akiingia katika Ukumbi wa Diamondi Jubilee Dar es Salaam jana. (kushoto) ni  Kiongizi MKuu wa chama  hicho,Zitto Kabwe.
   Mwenyekiti wa Chama cha  Alliance for change and Transparecy (ACT)  Anaa Elisha Akiwashukuru wanachama wote walioshiriki walio kiunga Mkono chama hicho nawaliotoka vyama vingine wakiwemo viongozi na Taasisi Mbalimbali.
  Baadhi ya wajumbe na Viongozi wa Chama hicho wakimsikiliza Zitto Kabwe alipo kua akizindua Mkutano wa Chama hicho(wa tatu kushoto) ni Baba wa  Kiongizi MKuu wa chama  hicho na akiliyekua Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zitto Kabwe.
  Wafuasi wa chama hicho wakijiandikisha na kupatakadi ya Uanachama.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  DSC_0065
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati) akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.

  Na Mwandishi wetu
  UMOJA wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.

  Kauli hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.

  Ripoti hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii- ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .

  Katika hotuba yake amesema kwamba Umoja wa Mataifa unaona juhudi za serikali katika kuwakwamua wananchi katika umaskini na kutokana na hali hiyo wataendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na utafiti wenye kulenga kutoa suluhu kwa changamoto za maendeleo ya wananchi.
  DSC_0207
  Mshehereshaji wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.


  0 0

  IMG_6523Bw.harusi David Kanumba akiwa na mkewe Nadege na wakwe zake mara baada ya kufunga ndoa siku ya Jumamosi Machi 28,2015, katika kanisa la Faith Ministry International Atlanta Georgia. IMG_6563Bw.harusi na Bi harusi wakiwa Bw.Togo na mkewe na mwisho kulia ni mchungaji Mwinamila. IMG_6569Bw.harusi na bi.harusi wakiwa na Best man Oscar na Matron Renee . 

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza taarifa ya Maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kituo cha Kisasa cha Uchunguzi wa Magonjwa kinachojengwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa udhamini wa Serikali.
  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bw. Rehani Athuman (aliyesimama) akitoa ufafanuzi wa maswali ya waandishi.
  Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Bw. Deusidedit Rutazaa akielezea ujenzi wa mradi huo wakati waandishi walipotembelea.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Machi 29, 2015 amewasili jijini New York, Marekani kwa mwaliko wa Umoja wa Mataifa.

  Miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete amefunguia rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa, na Jumatatu Machi 30, 2015 amealikwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Jamii (ECOSOC - UN).
  Rais Kikwete akilakiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Dkt Mahadhi Juma Maalim alipowasili jijini New York, Marekani. 
  Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa WAZIRI wa Kazi na Ajira, Mhe. Gaudensia Kabaka anayefuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee ...
  Jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
  Rais Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la ghorofa sita la Ofisi za Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  DSC_0035

  Mwanamuziki Lady Jay Dee akitoa burudani na Machozi Band Ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu ndani ya kiota chake cha Mog Bar & Restaurant (Nyumbani Lounge) katika show anazofanya mara moja kwa mwezi kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi ambapo Ijumaa hiyo alimualika Msanii machachari wa Bongo Flava Ali Kiba kwa ajili ya kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota hicho.
  DSC_0204
  Msanii nyota nchini, Ali Kiba akitoa burudani ya aina yake ndani ya kiota cha M.O.G Bar & Restaurant baada ya kutikia mualiko wa msanii mwezake Lady Jay Dee na kufanya Live Music bila kutumia CD na kuwafanya mashabiki kupagawa zaidi.


  0 0

  Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mfanyakazi aliyeitumikia benki hiyo kwa kipindi kirefu cha miaka 27, Said Kilala wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo (COO) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya.
  Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla katika vipengele vyote wa shindano la kumtafuta mfanyakazi mahiri katika idara hiyo, Mwanaisha Ayosi wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya.


  0 0

  Mkuu wa Vodacom Tanzania,Kanda ya Tanganyika George Venanty(kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni ya Associate AEG Winnie Nyamubi(kulia) wakielezea matumizi ya Umeme Jua”Solar Power” wakati wakukabidhi msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation kwa wahanga wa maafa ya mvua kwenye kijiji cha mwakata wilayani Kahama Mkoani Shinyanga mwishoni mwa wiki.

  Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga(kulia) akipokea msaada wa Umeme Jua ”Solar Power”kwa niaba ya wahanga wa maafa ya mvua uliotolewa na Vodacom Foundation kutoka kwa Mkuu wa Vodacom kanda ya Tanganyika,George Venanty.

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii “Vodacom Foundation” leo imekabidhi msaada kwa wahanga wa mvua wa Kahama mkoani Shinyanga. Msaada huo unatokana na mchango wa kampuni na michango ya wateja wake walioguswa na tukio hilo kupitia  namba  maalumu ya kupokea msaada ya kusaidia majanga mbalimbali ya 155990.

  Mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama mkoani Shinyanga mapema mwezi uliopita ilisababisha vifo vya watu 42 na wengine mamia kujeruhiwa na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake jana Machi 29, 2015 wakati akifunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la China na Afrika, Chen Lin, baada ya Makamu kufunga rasmi Kongamano la tatu la Vijana wa Tanzania na China, lililohusu masuala ya Uongozi, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakati akiondoka ukumbini hapo baada ya kufunga rasmi Kongamano la tatu ya Viajana wa Tanzania na China, lililofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi akizungumza na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam ambapo ameruhusu upimaji wa vipande vya ardhi na utoaji wa hatimiliki za ardhi uliokuwa umezuiliwa tangu kutangazwa kwa mradi huo.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Willium Lukuvi akisisitiza jambo wakati wa mkutano na wadau kuhusu mpango wa uendelezaji wa mji mpya wa Kigamboni, Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Meck Sadiki. Sehemu ya wadau hao ni pamoja na viongozi wa taasisi za Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s), madhehebu mbalimbali ya dini na taasisi za elimu na ulinzi na huduma mbalimbali zilizopo katika eneo hilo la Kigamboni.


  0 0

  Mratibu wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) Mussa Shanyangi (wa pili kulia), akiwaonesha Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Habari na Teknolojia Francis Fungameza namna mashine ya kukata mawe inavyofanya kazi.
  Baadhi ya Wanafunzi katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) waki polish mawe wakati wa mafunzo. Wanafunzi hao wako katika mafunzo ya ukataji na unga’rishaji madini katika kituo hicho.
  Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa   Yahya (kushoto) akimweleza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering Oswald Modu(wa tatu kulia) wakati wa ukaguzi wa jingo la kituo hicho kabla ya makabidhiano rasmi kufanywa.
  Baadhi ya wanafunzi wa kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Wakiwa katika mafunzo ya kunga’risha madini. Kituo hicho kitawezesha shughuli za Uongezaji Thamani kufanyika chuoni hapo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 786 | 787 | (Page 788) | 789 | 790 | .... | 3286 | newer