Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 785 | 786 | (Page 787) | 788 | 789 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akifungua mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo. 
  Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiwahutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam leo.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Aloyce Ntukamazima akitoa mada kwa maofisa na mameneja wa Rasilimali Watu nchini, kuhusu mafao na maendeleo ya mfuko huo, kwa sasa mfuko huo pamoja na mambo mengine wanachama wake wananufaika na Fao la Elimu, Fao la kuanza maisha kwa waajiriwa wapya, Fao la Kujikimu na Fao la Uzazi.
  Baadhi ya maofisa na mameneja wa Rasilimali Watu nchini, wakimsikiliza Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF, Aloyce Ntukamazima , alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu hatua kadhaa zilizofikiwa na mfuko huo hadi sasa ikiwemo ongezeko la Fao la Elimu, Fao la kuanza maisha kwa waajiriwa wapya, Fao la Kujikimu na Fao la Uzazi.

  0 0

   Taswira mbalimbali zikionyesha hali ya kufungwa kwa maduka jijini Mbeya kufuatia mgomo wa wafanya biashara unaoendelea nchi nzima.
  eneo lote la Soko la Mwanjelwa kimyaaaa
  mitaa yote kufuli tuuu.
  wafanya biashala wakiwa wameketi nje ya maduka yao.


  0 0

  Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars - pichani)) leo asubuhi imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya taifa ya Malawi (The Flames) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

  Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum. 
  Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo. 
  Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho. 
  Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi. 
  Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo. 
  Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba  Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0
 • 03/28/15--08:16: KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO
 •  Waziri wa Fedha Saada Mkuya  akihitimisha Muswada  wa Sheria ya Bajeti wa Mwaka 2014, Bungeni mjini Dodoma leo Machi 28, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi, Angela Kairuki, Bungeni mjini Dodoma leo Machi 28, 2015. 

  0 0


  0 0
 • 03/28/15--08:46: DMV ALL STARS WATUA VOA
 • IMG_6367Sunday na Ebreezy, Domi, Aj Ubao na Prince Heri.Jiandae kusikiliza mahojiano yao katika Jukwaa la Vijana la VOA. IMG_6371Aj Ubao na Domi wakijiandaa kupiga acapella. IMG_6379San Tized na Prince Heri katika acapella. Kwa picha zaidi ungana na www.sundayshomari.com IMG_6384

  0 0


  0 0

  Mdau mohammed Mgori (Mtarajiwa) anapenda kutoa shukurani kwa ndugu, jamaa, jirani na marafiki kwa kuweza kufanikisha kufanikisha Harusi ya dada yake Ashura Mgori iliyofanyika tarehe 27 March 2015. 
  Anasema asanteni sana sana 
  Allah awalipe kila Mmoja wenu.

  0 0

  Kampuni ya Pernod Ricard kupitia kinywaji chake cha- Jameson Irish Whiskey iliandaa hafla maalum ya kuonjesha kinywaji chake katika mgahawa wa High Spirit Lounge, jijini Dar es salaam jana.Hafla hiyo iliandaliwa na Balozi wa Jameson Kanda ya Afrika- Nelson Aseka. 

  Bwana Aseka, ambaye amepewa mafunzo maalum kutoka kwa wataalam wa kinywaji cha Jameson Irish Whiskey nchini Ireland na mwenye miaka mingi kuwa Balozi wa kinywaji hich alisema, “Jameson inaongoza duniani kwa mauzo katika kitengo cha whiskey kutoka Ireland na imeanza kupata umaarufu nchini Tanzania.

  Sababu kuu ya Jameson kuongeza umaarufu wake ni kupitia mbinu zinazotumiwa katika utengenezaji wa kinywaji hiki ambayo inaipa ladha nzuri zaidi. Jameson imezidi kupata ongezeko la mauzo na ubora kwa miaka 24 sasa na inatarajia kuendeleza jambo hili kwa kuingia katika soko la Afrika Mashariki”.

  Naye Meneja Ukuzaji Bidhaa wa Pernod Ricard, Bwana Adam Kawa alisema, “ Hii ni moja kati ya hafla nyingi ambazo Pernod Ricard itaandaa katika soko la Tanzania na sio tu kwa kinywaji cha Jameson bali kwa vinywaji vingine kama vile: Ballentine’s, Absolut Vodka, Chivas, Beefeater na Malibu. Na kama mlivyoona katika hafla ya leo tutaendelea kuwafanyia wateja wetu hafla zinazowapatia uzoefu zaidi juu ya bidhaa zetu”.
  Balozi Mkuu wa kinywaji cha Jameson Whisk, Nelson Aseka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywaji hicho na jinsi namna kinavyotengenezwa.Hafla hiyo iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaam.
  Meneja masoko wa Jameson Whisk,Adam Kawa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywa hicho iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika hafla ya kuonja Jameson Whisk iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (kushoto ni Dkt,K.Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital (kulia) Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo alipotembelea mashine ya Xray baada ya kuifungua Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo (wa kwanza kulia) Dkt,K.Ravindranath Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Daktari Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Global Hospital Dkt,K.Ravindranath(wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Vigor Turky Salim Hassan Turky wakiangalia mashine ya kufanyia Upasuaji wakati alipotembelea Hospitali ya Global Hospital iliyopo Mtaa wa Vuga Mjini Unguja leo baada ya kuifungua rasmi.


  0 0

  Dr. Teresia Olemako of WWF Tanzania showing Journalists (not in picture) the work spots for vetiver grass planting to rehabilitate the Environment and prevent soil erosion alongside Msimbazi river banks near Vingunguti area in Dar es salaam on the 27th March, marking the Earth Hour 2015 in Tanzania.
  Some of Ilala Municipal Employees actively planting vetiver grass alongside Msimbazi river near Vingunguti area in Dar es salaam to prevent soil erosion and rehabilitate the Environment, Earth Hour March 2015 in Tanzania.
  Some of Ilala Municipal Employees busy with vetiver grass planting preparations along Msimbazi river near Vingunguti area in Dar es salaam to curb soil erosion and rehabilitate the Environment. Earth Hour in Tanzania March 2015.

  0 0


  Na Faustine Ruta, Mwanza.
  Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) pichani leo jioni imefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili Wenyeji wao Tanzania Timu ya (Taifa Stars) mchezo utakaochezwa kesho jumapili saa 10.30 jioni katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

  Wakibadilishana Mawazo wakati Wachezaji wa Malawi wanajifua mara ya mwisho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo.

  Tiketi za mchezo tayari zimeshaanza kuuzwa katika vituo vya Uwanja wa Nyamagana na uwanja wa CCM Kirumba kwa bei za sh. 5,000 kwa mzunguko, sh. 12,000 kwa jukwaa kuu na sh.20,000 kwa viti vya jukwaa kuu maalum. 
  Taifa Stars inashika nafasi ya 100 katika msimamo wa viwango vya FIFA vilivyotolewa mwezi Machi, huku Malawi (The Flames) wakishika wakiwa nafasi ya 91 kwenye vinago hivyo. 
  Akiongea na waandishi wa habari leo kaika hoteli ya La Kairo iliyopo Kirumba jijini Mwanza, kocha msaidizi wa Taifa Stars Salum Mayanga amesema kikosi chao kipo katika hali nzuri , na sasa kilichobakia ni mchezo wenyewe wa kesho jumapili.


  Mayanga amesema vijana wake wote 22 waliopo kambini wapo fiti, wamefanya mazoezi kwa siku tano katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, wachezaji wapo kwenye ari na morali ya juu, kikubwa wanachosubiri ni kesho tu kushuka dimbani kusaka ushindi. 
  Aidha Mayanga amewaomba wapenzi wa mpira wa miguu waliopo jijini Mwanza na mikoa ya jirani ya kanda ya ziwa, kujitokeza kwa wingi kesho uwanjani kuja kuwapa sapoti vijana kwa kuwashangilia muda wote wa mchezo. 
  Tayari waamuzi na kamishina wa mchezo wameshawasili jijini Mwanza, mwamuzi wa kati atakua ni Munyazinza Gervais kutoka nchini Rwanda, akisaidiwa na mshika kibendera wa kwanza Hakizimana Ambroise (Rwanda), mshika kibendera wa pili Niyitegeka Bosco (Rwanda), mwamuzi wa akiba Martin Saanya kutoka Morogoro huku na Kamishina wa mchezo ni Afred Rwiza kutoka Mwanza.

  0 0

   Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akizungumza jambo na Rais wa Zimbambwe,Mh.Robert Mugabe mara mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchaa.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo  na Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha..
    Makamu wa Rais Dk Gharib Bilal akimpomkea mgeni wake,Rais wa Zimbabwe,Mh.Robert Mugabe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa KIA,mapema leo mchana.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo mjini Arusha.
   Baadhi ya Wanahabari wakihangaika kupata taswira ya kuwasili kwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye alipokelewa na Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal na viongozi mbalimbali wa Kitaifa na Kidini
   Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akiwasili mapema leo mchana
  kwenye uwanja wa ndege wa KIA.Rais Mugabe anatarajiwa kufungua  Kongamano la Viongozi Vijana wa Afrika na China litakaloanza leo katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.

  PICHA  NA MICHUZI JR-ARUSHA
  0 0


  0 0

   
  Mgeni Rasmi wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China, Rais wa Zimbabwe,Robert  Mugabe akihutubi usiku huu kweye kongamano hilo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,ambapo Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China linafanyika na mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
  Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe (aliyeshikwa  mabepa) akiwasili usiku huu kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kufungua kufungua  Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China.
   RAIS Jakaya Kikwete  akipewa tunzo  ya Heshima ya juu ya Kuhamasisha Amani na Utulivu katika Bara la Afrika na Rais wa Umoja wa Vijana Afrika (PAYU),Francine Furaha Muyumba .Tuzo hiyo imetolewa na Umoja wa Vijana  wa  Umoja wa Afrika,pichani kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh.Mboni Mhita
    Rais Jakaya Kikwete akitoa salamu zake kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.
    Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe,kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana 
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowasili jioni ya leo kwenye moja ya ukumbi wa mikutano katika hotel ya Ngurdoto mjini Arusha,kwa ajili ya kutoa salamu kwa washiriki wa   Kongamano la tatu la Viongozi Vijana wa Afrika na China,ambalo mgeni rasmi ni Rais wa Zimbabwe,Robert Mugabe.Pichani kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Mh.Stephen Masele.

  PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.


  0 0

  Dkt. Amosy Ephreim M'Koma, Mtanzania, Bingwa katika fani ya Upasuaji (Colon and Rectal Surgery). ametambuliwa na Jarida kubwa la watalaam mabingwa wa upasuaji duniani la "World Journal of Surgical Procedures" kutokana na  shughuli zake za utafiti (Surgical Sciences) katika Chuo Kikuu cha Vanderbilt University huko North Nashville, Tenesee. Dkt. M'Koma amekuwa taarifa kuu katik toleo la sasa la Jarida hilo (BOFYA HAPA) lenye bodi ya wahariri 275 ambao wote ni mabingwa wa upasuaji toka sehemu mbali mbali dunia.  Globu ya Jamii inampa hongera sana Dkt M'Koma kwa fanaka hiyo ambayo kupatikana kwake ni lazima uwe jembe kweli kweli kwenye fani hiyo.
  Kumjua zaidi daktari pingwa 

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
  Matembezi yakiendelea.
  Wadau kutoka sekta mbali mbali wakishiriki kwenye Matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
  Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Jeshi la Magereza nchini limemfukuza  kazi askari wake wa Gereza Bariadi, Mkoani Shinyanga (pichani) kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia kinyume na Sheria za Nchi.

  Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana Machi 28, 2015 na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B. 6499 Wdr. Edmund Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28, 2015 kwa kosa la kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni 22(xlix) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.

  Aidha, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali vitendo hivyo kwani ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi la Magereza huku akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.


  Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
  Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
  Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
  DAR ES SALAAM
  Machi 29, 2015.

  0 0

  Mkuu Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mussa Jallow (wa tano kulia) akikabidhi msaada wa pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Thomas Diwani Mponda katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, kompyuta, kofia na mafuta maalumu ya ngozi vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
  Ofisa Mkaguzi wa Sheria za Ndani za Benki wa NBC, Lilian Kawa (katikati) akikabidhi msaada wa kofia kwa Katibu wa Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Aicha Joakim Ngure (wa tatu kushoto) katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na mafuta maalumu ya ngozi ili kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na tatizo unaotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.
  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Kibaha, Asia Chambega (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mafuta maalumu ya ngozi kwa mmoja wa wawakilishi kutoka Chama Cha Albino Tanzania Mkoa wa Pwani, Haika Ngowo, katika hafla ambayo NBC pia ilikikabidhi msaada wa hundi ya shs milioni 3.2, pikipiki, kompyuta na kofia vikiwa na lengo la kuwasaidia na matatizo yanayowakabili kutokana na hali hiyo inayotokana na kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Wengine ni baadhi ya maofisa wa NBC na kutoka chama cha albino.


older | 1 | .... | 785 | 786 | (Page 787) | 788 | 789 | .... | 3270 | newer