Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Tanzania yaikabidhi Malawi msaada kwa ajili ya Wahanga wa mafuriko

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Patrick Luciano Tsere (kulia) akikabidhi  Dawa za Binadamu na Mahindi  kwa Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna  anayeshughulikia masuala ya Maafa aktika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi  ikiwa  ni sehemu ya msaada wa Tani 1,200 za Mahindi na Dawa za Binadamu zilizotolewa na Serikali ya Tanzania kwa nchi hiyo kufuatia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo mwezi Januari 2015. 
manajdhdfdufdhuf Bw. Paul Chiunguzeni, Katibu Mkuu na pia Kamishna anayeshughulikia masuala ya Maafa katika Ofisi ya Makamu wa Rais wa Malawi akitoa hotuba ya shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa msaada huo wa Mahindi na Dawa za Binadamu.
Mhe. Balozi Tsere akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Chiunguzeni. Wengine katika picha ni Mwambata wa Jeshi katika Ubalozi wa Malawi nchini Tanzania, Ufulu Kalino (kushoto) akifuatiwa na Kanali Rugeumbiza kutoka JWTZ ambaye alikuwa msimamizi wa zoezi la usafirishaji wa msaada huo kutoka Tanzania na Luteni Kanali B.B. Kisinda (wa tatu kulia) kutoka JWTZ ambaye alikuwa Kiongozi wa Msafara pamoja na Makamanda wa JWTZ.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

NAFASI ZA KAZI SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

SAMAKI SAMAKI KUCHANGIA ELIMU KWA WATOTO YATIMA

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Mgahawa wa Samaki Samaki umeanzisha mpango wa kuchangia Elimu kwa watoto yatima kwa kila mtu atakayekula katika migahawa ya samaki samaki itatolewa sh.1000 kwa bei halisi na sio kukatwa mteja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,Afisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki,Edward Lusala amesema Samaki Samaki imefikisha miaka nane tangu kuanza kwake na wameona kuna umuhimu wa kuchangia katika kundi la watoto yatima.

Amesema kuwa wanawafundisha ufundi watoto yatima ili kuweza kufikia hatua ya kujiajiri wenyewe katika sekta uchongaji wa vinyago pamoja na mitumbwi.

Lusala amesema kundi la watoto yatima linahitaji kuangaliwa kwa karibu ili kuweza kufikia malengo yao kwa kuwasaidia katika sekta mbalimbali.
Afisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki,Edward Lusala (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, juu ya kuchangia sh.1000 kwa kila mtu ambaye atakula chakula katika migahawa ya Samaki Samaki na fedha hiyo itatumika kwa kusaidia Elimu kwa watoto yatima.Kulia ni Meneja Masoko wa Samaki Samaki,Njama Matumbo na kushoto ni Meneaja Mauzo wa Coca Cola Kwanza Dar es Salaam,Ruqaiya Alibhai

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BENKI YA DUNIA (WB) MAPEMA LEO

0
0
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (mbele ) akiongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Benki ya Dunia na watalaam wa Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili maendeleo ya miradi ya nishati nchini inayofadhiliwa na Benki hiyo, changamoto zake na kupata mapendekezo ya kuboresha miradi hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi , Philippe Dongier (kushoto) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) mikakati ya Benki hiyo katika kuisaidia Tanzania katika sekta ya nishati kwenye kikao hicho.

WABUNGE WAPYA WAAPISHWA LEO MJINI DODOMA

0
0
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Dkt. Grace Puja akila kiapo ndani ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo Machi 27, 2015.
Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Innocent Sebba akila kiapo ndani ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma leo Machi 27, 2015.

ASKOFU JOSEPHAT GWAJIMA AJISALIMISHA POLISI KWA MKUU WA UPELELEZI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limeanza kumhoji Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima baada ya kujisalimisha kama alivyotakiwa kufanya hivyo na Kamishana wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Askofu Gwajima alifika kituo kikuu cha Polisi saa nane na dakika kumi na tano mchana wa tarehe 27/03/2015. Mara baada ya kufika kituoni hapo alielekezwa kwenda kumuona Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Constantine Masawe ambaye alikuwa akisubiri kufika kwake.

Tuhuma zinazomkabili Askofu Gwajima ni pamoja na kumkashfu na kumtukana hadharani Kiongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Taratibu za mahojiano zimekwishaanza kwa mujibu wa sheria na mtuhumiwa atapewa haki zote anazostahili kama vile kuwa na ndugu yake wa karibu, rafiki yake anayemwamini au wakili wake. 

Kama ilivyo kawaida utakusanywa ushahidi kutoka pande zote za shauri hilo ili kubaini ukweli wa jinsi tukio hilo lilivyotokea na athari zake.

Baada ya hapo hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kupata maoni ya kitaalamu na ya kisheria ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Ili ufanisi upatikane katika upelelezi wa shauri hili, ni muhimu kupata ushirikiano kutoka kwa kila atakayetakiwa kulisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha haraka upelelezi wa shauri hili ambalo sasa limepata mvuto mkubwa katika jamii.

Imetolewa na:
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

MADEREVA 21 WA KAMPUNI YA MAJINJAH LOGISTICS LTD WAPATIWA MAFUNZO CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI (NIT) WAHITIMU WAPEWA VYETI.

0
0
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Majinjah Logistics Ltd wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka kushoto mstari wa mbele (wa pili) Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete,Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe,Mhandisi, Charles Kisunga na Dereva wa kike wa Majinjah,Grace Andrew.
 Wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wao na viongozi wa NIT.
Wanafunzi wahitimu wa mafunzo ya Udereva wa Kampuni ya Majinjah Logistics wakiwa
 Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu,bDk,Ethel Kasembe (kulia) akikakabidhi vyeti wahitimu.
  Mhandisi, Charles Kisunga wa NIT akizungumza,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Majinjah Logistics,Benjamin Mwandete (kushoto) Mkuu wa Idara ya Tafiti,Machapisho na Masomo ya Elimu ya Juu (NIT),Dk,Ethel Kasembe (wa pili kulia) na Mkuu wa Kampuni ya Majinjah,Geoffrey Mwambona.
Kwa taarifa kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Hon. Mayor of Ilala District officiates Standard Chartered's Tree Planting event

0
0
Standard Chartered Bank’s Finance Team members this morning held a tree planting event which was officiated by the Mayor of Ilala District Hon. Jerry Silaa. 
The event was also attended by the Bank’s Audit Team members and other high ranked officials from the Ilala Municipal Office – Environment department. The team planted sixty trees along the Barack Obama road, one of the most busy roads in Dar es Salaam. 
Given its location near the public beach, the area is also frequented by many people during weekends. The trees will, therefore, not only help in conserving the environment, but will also be a great source of shade for many people who frequent the area. 
 Hon. Silaa commended the Bank for its ongoing efforts to conserve the environment. In addition to applauding the tree planting initiative, he also commended the Bank’s Digitization move, citing the use of eStatements and Online Banking as a great example of the Bank’s contribution to Environmental conservation. 
 On her part, the Bank’s Head of Finance, Ruth Zaipuna, used the opportunity as a platform to reiterate the Bank’s support towards conserving the environment, covering the Bank’s various initiatives, and reminded participants on the various individual actions towards environmental conservation, such as not leaving tap water running and switching off their PCs at close of day, which collectively make a big contribution towards conserving the environment.
 Standard Chartered Bank’s Finance Team members applaud the Mayor of Ilala, Hon. Silaa as he plants a tree. Ruth assists in watering it as John assists in firming it up with soil. 
 ‘Environment First!’ – Standard Chartered Bank’s Finance team joins together in a group photo with the Honourable Mayor and officials from the Environment Department at the Ilala Municipal Council.
 PPPs – Standard Chartered Bank’s Head of Finance, Ruth Zaipuna, plants a tree assisted by the Honourable Mayor.
This is how we do it! Members of staff planting trees.

MAONI YA MDAU KWA UONGOZI WA MAKUMBUSHO YA TAIFA

0
0
Hivi punde nimetoka Makumbusho ya Taifa na Nyumba ya Utamaduni iliyopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha  (IFM)  jijini Dar es salaam. Hapo kulikuwa na matukio makubwa mawili.  Moja la sherehe za siku ya wanawake na Nyingine kwenye viwanja ikiwahusisha wanafunzi wa shule mbali mbali.
Muda mfupi kabla sijaondoka kuna wanafunzi  wawili wa Jangwani Sekondari walidondoka na kupoteza fahamu mmoja akiwa ameng’ata ulimi babisa, Hali hii ya sintofahamu iliwashtua wengi waliokuwa  karibu na tukio hili. Ilikuwa ni wanafunzi wenyewe waliochukuwa jukuamu la kuwasaidia wenzao. Pembeni ya tukio hili la kusikitisha niliwaona viongozi wa Makumbusho wakiwa chini ya mti mkubwa wakizungumza mambo yao bila hata kushtuka na kutoa msaada.
Hii inasikitisha sana, Nimeona niufahamishe umma hasa wenye maeneo ya kukodisha kwa shughuli za kijamii, kwamba msipuuzie wateja wenu wanapopatwa na matatizo kama nilivyo shuhudia pale makumbusho ya Taifa. Kwa kweli ni aibu sana kwa uongozi wa hapo...Ni aibu kwa kuwa mabinti waliopoteza fahamu ni sawa na watoto wao tu, ukiachana na kuwa ni wateja wa Makumbusho.
Nawapongeza vijana wachache wa Makumbusho hiyo waliojitolea kwa moyo kusaidiana na wanafunzi hao kuhakikisha waathirika wanakimbizwa hospitali. Pia Mtangazaji Sauda Simba Kilumanga  ambaye alijitoa sana kama mama kuhakikisha wanafunzi hao wanapatiwa msaada. 
Mungu awabariki wote na ninawaombea Mungu wanafunzi waliopelekwa hospital wapone haraka.

Mimi Mdau wa Makumbusho ya Taifa.

Kampuni ya Kaimu yawezesha wananchi kununua na kuuza vitu mtandaoni Tanzania

NIMR yataja madhara ya pombe na tumbaku

LORI LAGONGA TRENI JIJINI DAR LEO

0
0

 Lori la Mizigo lenye namba za usajili T 535 CCT mali ya Kampuni ya Coast Millers Limited watengenezaji wa Unga wa Ngano wa Nyati, likiwa nje ya barabara ya Kawawa eneo la Karume mara baada ya kuigonga Treni ya TRL mapema leo asubuhi.

Sehemu ya mashuhuda wa tukio hilo.
Askari Polisi wakiwa eneo la tukio. 

Allan Kingdom: The rapper with Tanzanian blood attracting international attention

0
0
After helping hip-hop megastar Kanye West debut new song “All Day” last week, Allan Kingdom is making headlines around the world. Few rappers get the chance to collaborate with hip-hop’s self-proclaimed savior, so this support from West means a lot—and as we learned on Tuesday, Kingdom didn’t just help Kanye in the song’s live performance butappears on the studio version of the track, too.
All of this is leading many to question, who is Allan Kingdom? Although many in The Current’s audience are familiar with Kingdom’s work, all this national attention is piquing new interest.
Complex, a web magazine and national hip-hop news source, focuses on Kingdom in a new video report; he’s a 21-year-old artist, born Allan Kyariga, who’s lived in St. Paul since the age of nine. The son of a South African father and a Tanzanian mother, he grew up listening to African music before discovering artists like André 3000, Pharrell, and Kid Cudi. Now, he’s a graceful, inventive rapper who’s releasing both solo material and collaborations with others.
Kingdom’s music often has a hazy, floating feel, with spacious soundscapes punctuated by ambient percussion; his style evokes a sense of vulnerability that sometimes underscores, sometimes contrasts with his lyrics. When Kingdom started making music, he told David Campbell when he visited The Current’s studios last fall, he “couldn’t find a producer that fit exactly what [he] wanted to do,” so he started designing beats for himself. Since then, he’s spent a lot of time in his bedroom, writing and perfecting songs on his computer.
 Allan with his Tanzanian mom Lau Kyariga in Minnesota. Lau owns the famous Arise Beauty Supply store at Msasani Kwa Mwalimu in Dar es salaam and the mega hit hair product Ebenezer that is sold world wide
 Allan is met with his mom Lau Kyariga at the airport in Minnesota returing from London where he went to perfome at the BRIT Awards with Kanye West
Allan in the studio

MAMLAKA ZINAZOHUSU OPERESHENI ZA ULINZI WA AMANI ZIWE WAZI- JENERALI MWAMUNYANGE

0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amelishauri Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuweka bayana na kwa uwazi mamlaka ( mandate) ambayo misheni ya kulinda Amani itapaswa kutelekeza kule inakopangiwa kwenda. 
 Ametoa ushauri huu siku ya Alhamisi wakati alipokuwa akitoa mchango wake kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinachangia katika operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa. 
Katika mkutano huo uliokuwa wa siku moja, na kuhudhuriwa na Wakuu wa Majeshi na Maafisa wa Ngazi za Juu ,kutoka nchi 108, Jenerali Mwamunyage amesema; “ Wakati wa utoaji wa idhini na mamlaka kwa misheni ya kulinda Amani, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, linatakiwa kumwita mbwa kwa jina lake kama lilivyo.Mbwa aitwe kwa jina lake. Elezeni bayana na kwa uwazi mamlaka na idhini za utekelezaji za ya misheni ” 
Na kuongeza, “ iwekwe wazi, kama ni misheni ya kulinda Amani, basi ielezwe ni ya kulinda Amani, na kama ni ya matumizi ya nguvu basi na iwe hivyo”. Amesisitiza Mkuu wa Majeshi 
Amesema kwamba, kwa kutamka jina halisi /mamlaka ya misheni pale inapoundwa, Baraza Kuu la Usalama linakuwa linapeleka ujumbe ulio sahihi kwa pande zote zinazohusika pamoja na nini wakitarajie. 
Jenerali Mwamunyage ameuleza washiriki wa mkutano huo mkutano wa kwanza wa aina yake kuwakutanisha Wakuu wa Majeshi zaidi ya mia moja, wakati mmoja na mahali pamoja. Kwamba, uwazi huo pia utasaidia kuweka bayana hatua za utekelezaji zinazofanywa na walinzi wa amani kwenye eneo la utekelezaji. 
Vile vile Mkuu wa Majeshi ya Tanzania ameshauri pia kuwa misheni ambayo tangu kuundwa kwake zilikuwa na mamlaka ya kutumia nguvu, ni vema zisiendelee kutambuliwa hivyo pale mamlaka ya misheni hiyo yanapobadilika kutoka matumizi ya nguvu na kuwa misheni ya kulinda Amani au jina lolote lile. Tanzania inawanajeshi wake katika Misheni mbalimbali ikiwa ni pamoja na UNAMID ( Darfur) UNFIL, ( Lebanon) MONUSCO ( DRC) na katika maeneo mengine. 
Vile vile Tanzania ina Polisi na Askari Magereza ambao nao wanahudumu katika misheni mbalimbali. 
Akizungumzia kuhusu mkutano huo ambao ulifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Ban Ki Moon na kufungwa na Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson. Jenerali Davis Mwamunyange amesema, mkutano kama huo unapashwa kuitishwa mara kwa mara kwa kuwa unawawezesha wakuu wa majeshi kubadilishana uzoefu wao katika utekelezaji wa operesheni za ulinzi wa Amani na hasa kwa kuzingatia kwamba nchi wanachama ndio wanaotoa wanajeshi wao na ndio haswa wanaokumbana na changamoto mbalimbmali za utekelezaji wa dhamana hiyo. 
Awali akifungua mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon pamoja na kuwashukuru Wakuu hao wa Majeshi kwa mchango wao katika eneo hilo la ulinzi wa Amani, amesema operesheni ya kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa, licha kwa kwamba ni dhamana inayohitajika sana lakini pia inakabiliwa na changamoto mbalimbali. 
Akazitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni upugufu wa raslimali fedha, zana, vifaa na teknolojia za kisasa lakini pia ugumu na hatari wanazokumbana nazo walinzi wa Amani, ambapo hivi sasa mbinu za kigaidi na uvamizi kwa walinzi wa Amani ni baadhi ya changamoto na hatari wanazokumbana nazo. 
Katibu Mkuu, amewataka wakuu hao wa majeshi kuongeza ushirikiano wao kwa Umoja wa Mataifa na hasa katika kutafuta mbinu za kukabiliana na changamoto za kiulinzi na kiusalama ambazo duni hivi sasa inakabiliana nao. Akaongeza kuwa kujitokeza kwa idadi kubwa ya wakuu hao wa majeshi ya ulinzi kushiriki mkutano huo, kumeipa faraja kubwa Umoja wa Mataifa. 
Naye Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson, akihitimisha mkutano huo, amewataka wakuu hao wa majeshi na serikali zao kuendelea na majadiliano ya mchakaTo wa kuundwa kwa majeshi ya ulinzi ya kikanda, majadiliano ambayo yanatakiwa kuendelea kuelekea mkutano wa Operesheni ya Ulinzi wa Amani utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu. 
 Wakuu hao wa Majeshi ya Ulinzi pamoja na kutoa mchango wa mawazo yao, pia walipata fursa ya kupata maelezo kutoka kwa Viongozi wakuu waandamizi wanaoongoza Idara zinazozohusu Operesheni ya Ulinzi wa Amani.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange akiwa katika ukumbi  wa Baraza la Uchumi la Umoja wa Mataifa maarufu kama ECOSOC ambapo ndipo ulipofanyika  mkutano wa kihistoria wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi na Maafisa wa ngazi za juu  kutoka nchi  zinazochangia katika  Operesheni za Ulinzi wa Amani  chini ya Umoja wa Mataifa. Akichangia majadiliano ya mkutano huo. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi amelishauri  Baraza Kuu la Usalama na  UN kuweka bayana na kwa uwazi  mamlaka ya misheni  inazoziunda. Pamoja naye ni  Brigedia Jenerali MG. Luwogo na Brigedia Jenerali HS Kamunde.
 Mkuu wa Majeshi ya  Ulinzi,  Jenerali Davis Mwamunyage akiwa ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akibadilishana mawazo na  mmoja wa Maafisa wa ngazi ya juu  kutoka Idara ya Masuala ya Siasa katika UN muda  mfupi  kabla ya  Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi hawajapiga picha ya  pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 
 Jenerali Davis Mwamunyange akiwa na ujumbe wake katika picha hii ambayo wapiga mbele ya bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  muda mfupi  baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku moja wa wakuu wa majeshi ya  ulinzi kutoka nchi 108 kutoka kushoto ni  Kanal Adolf Mutta, Brigedia Jenerali Luwogo, Mkuu wa  Majeshi  Jenerali  Mwamunyange,  Brigedia Jenerali Kamunde,  Meja Ngh'abi, na  Luten  Kanal Itang'are
 "...Mnatuwakilisha vema?" ndilo swali ambalo   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,  Jenerali Mwamunyange alilowauliza watanzania hawa wawili,  Afisa wa Usalama wa UN Bw. Jacob Mwashiozya na  Bw.  Joseph Msami, wa Idhaa ya Kiswahili  ya Umoja wa Mataifa walipokuwa  wakisalimiana naye na ujumbe wake  mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiingia kwa staii ya aina yake wakati alipokwenda kufungua mkutano wa kwanza wa aina yake  kufanyika  katika Umoja wa Mataifa,  ambapo Wakuu wa Majeshi  ya ulinzi kutoka  nchi zaidi ya 100 walikutana kwa wakati mmoja na mahali pamoja kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu operesheni za ulinzi wa amani za umoja wa mataifa.

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI WA KAMPUNI YA LOTUS

0
0
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni Lotus,Bwana Matthieu Boone. alipomtembelea ofini kwake mjini Lembeke, Ubelgiji .

AZAM, SIMBA, YANGA ZAPIGWA FAINI

0
0
Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es salaam, kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Vodacom.

Katika mechi namba 107 iliyowakutanisha wenyeji Ndanda FC dhidi ya Coastal Unioni, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu ya Vodacom  kutokana na washabiki wake kumrushia chupa za maji mwamuzi msaidizi Anold Bugado.

Mechi namba 108 iliyochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, (Stand United dhidi Simba SC), wenyeji timu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kutokana na timu yake kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika ishirini.

Mchezo namba 117 uliozikutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya  Simba imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kukataa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.

Nayo klabu ya Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(11) baada ya timu yake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano kwenye mchezo dhidi ya Simba SC, huku mshambualiji wake Dany Mrwanda  akipigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(12) kwa kutopeana mikono na wachezaji wa timu hiyo.

Mchezaji Haruna Niyonzima wa Yanga amepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 37(f) kwa kupiga teke meza ya   mwamuzi wa akiba baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu. Suala la mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe kumshika korodani beki wa Simba SC Murshid Juuko limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu.

Kipa wa timu ya Simba SC, Ivo Mapunda amepewa onyo kwa kufunika tangazo la mdhamini wa Ligi Kuu  (Vodacom) kwa kutumia taulo lake wakati wa mechi dhidi ya Yanga, hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake iwapo atarudia kufanya tukio la aina hiyo.

Nao wachezaji Salum Abubakar wa Azam FC na Richard Maranya wa JKT Ruvu wamepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kila mmoja na kusimamishwa mechi tatu kwa mujibu wa Kanuni ya 37(3) kwa kupigana uwanjani kwenye mechi namba 123 ambapo walitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Klabu ya Kagera Sugar imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) baada ya timu yake kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo namba 130 dhidi ya Young Africans uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.

Mechi namba 132 iliyozikutanisha Azam na Ndanda SC kwenye uwanja wa Chamazi, klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) baada ya washabiki wake kuwamwagia maji na kuwarushia chupa za maji washabiki wa Azam.

Aidha klabu ya Stand United imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(8) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi namba 134 dhidi ya timu ya Mbeya City,  pia imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(9) kwa kutoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo huo.

Kiongozi wa Stand United, Muhibu Kanu amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu baada ya kuondolewa kwenye benchi na mwamuzi wa mchezo dhidi ya Mbeya City kutokana na kutumia lugha ya kuhamasisha vurugu kwa timu yake na kupinga uamuzi wa refarii.

Katika mchezo namba 135 uliochezwa jijini Tanga na kuwakutanisha wenyeji Mgambo Shooting dhidi ya Yanga SC, Yanga SC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) kutokana na washabiki wake kuvamia uwanja baada ya mechi namba 135 dhidi ya Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

INDIA YADHAMIRIA KUKABILIANA NA WIZI KUPITIA MASHINE ZA ATM

0
0
Katika Mkutano uliofanyika Nchini India, Mbali na maelezo ya jitihada na dhamira kubwa katika kuwekeza katika maswala ya teknolojia kupitia kampeni yao ya DIGITAL INDIA, Pia nchi imepata kuelezea dhamira yao ya kuwekeza zaidi kwa kutoa misaada ya kimasomo ( Scholarships ) kwa wale watakao kuwa wakisomea masomo yatakayo wezesha kukuza na kufanikisha jitihada zao za Digital India.

Aidha, Kwa Upande mwingine – Wameweza kukubali tatizo linalo ambatana na ukuaji wa technolojia ni uhalifu mtandao huku ikielezwa watumiaji wa simu wamefikia asilimia 97% ya raia wa nchini humo, kitu ambacho kinapelekea matumizi mtandao kuingiwa na dosari ya kipekee.

Itakumbukwa India kupitia taarifa inayosomeka kwa "KUBOFYA HAPA" waziri mkuu wan chi hiyo alihimiza wananchi wake kujikita zaidi katika kutengeneza namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao ambapo pia iweze kutumika kutoa misaada kwa nchi nyingine.

Katika Kikao cha siku mbili, Kubwa la kiusalama mtandao ni dhamira kubwa ya moja kati ya washiriki wa mkutano huo kuonyesha dhamira yao kubwa ya kukabiliana na tishio la uhalifu kupitia mitandao ( Hasa Wizi wa fedha kupitia ATM) linalo tikisa mataifa mbali mbali hivi sasa.

TUME YA USHINDANI NCHINI (FCC) YAKAMATA BIDHAA BANDIA JIJINI ARUSHA

0
0
Afisa Mkaguzi wa Tume ya Ushindani(FCC), Michael David akizungumza na waandishi wa habari kwenye Kituo cha Polisi jijini Arusha baada ya kufanikiwa kukamata Simu bandia 215 za mikononi na vifaa vingine vyenye jina la Samsung wakati sio halisi.
Baadhi ya Simu,Chaja na mifuniko yenye nembo ya kampuni ya Samsung vilikamatwa kwenye maduka mbalimbali jijini Arusha.
Afisa Mkaguzi wa Tume ya Ushindani(FCC), Michael David akionesha moja ya bidhaa bandia zilizokamatwa leo.Amewataka wananchi kununua bidhaa halisi kwa Mawakala waliohidhinishwa ili kuepuka madhara ya kiafya.

SEND OFF YA BI. ASNA ALLY MUAZINI YAFANA SANA

0
0
  Bi Harusi  mtarajiwa Asna Muazini akiwa katika pozi na tabasam katika Hafla yakuagwa kwake (SEND OFF) iliyofanyika hivi punde katika ukumbi wa DDC Keko jijini Dar es Salaam
   Bi Harusi  mtarajiwa Asna Muazini akiwa na wapembe wake  katika pozi wakati wa  Hafla yakuagwa (SEND OFF) iliyofanyika hivi punde katika ukumbi wa DDC Keko  Dar es Salaam, kushoto ni Wardat Saidi Juma anaye somea Uwandishi wa Habari huko Zanzibar maeneo ya Vuga na kulia ni Mwanafunzi wa Shule ya Lumumba Zanzibar Mwanahija Suleimani Yusufu.
  Bi Harusi  mtarajiwa Asna, akijianda kuwakadidhi Keki wazazi wake.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

WANAFUNZI WA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA(TPSC) TAWI LATANGA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO PSPTB

0
0
Na Mwandishi wetu
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imepokea ugeni wa wanachuo sabini wa mwaka wa pili wanaosoma stashahada ya ununuzi na ugavi waliokuja kwenye ziara ya mafunzo kutoka Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tanga. 

Ziara hiyo ya mafunzo ililenga kujua kazi mbalimbali za Bodi ya wataalam wa ununuzi na Ugavi (PSPTB). Mkurugenzi mkuu Mtendaji wa PSPTB Dr Clemence Tesha, aliupokea ugeni huo, na kuwashukuru kwa kuona nia ya kufanya ziara ya mafunzo. Aidha aliwaelezea umuhimu wa kuzingatia maadili , kujifunza kwa bidii ili kupata maarifa na ujuzi unaoweza kuhimili soko la ushindani la ajira . 

Wanachuo pia walielezewa juu ya taratibu za mitihani ya Bodi yenye ngazi ya cheti cha awaliAwali, msingi Msingi na Taaluma. Aidha aliwaelezea taratibu za kusajii kwa ajili ya kufanya mitihani ya kitaaluma mara baada ya kumaliza masomo yao na kwamba mhitimu wa stashahada ya ununuzi na ugavi kwa chuo kinachotambuliwa na Bodi anaanzia ngazi ya kwanza ya mitihani ya taaluma. 

Mitihani ya taaluma ina ngazi tano, ambazo huhitimishwa kwa wanafunzi kufanya mitihaniutafiti. Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa wanachuo hao kujua taratibu za kujisajili kama wataalum wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwani ni hitaji la sheria iliyounda Bodi. 

Aidha walifahamishawa kwamba kuna ngazi mbalimbali za usajili ambazo zinatambua kiwango cha ujuzi na uzoefu wa mtaalam. “ fanyeni usajili mara mmalizapo chuo ili kutumia fursa za ajira katika fani yenu “ ” alisisitiza. 

Tambueni kwamba taaluma ya ununuzi na ugavi inaongozwa na misingi ya maadili ambayo inawataka kutambua kuwa mnawajibika kwa umma wa watanzania, taaluama yenu, mwajili wako. Misingi hii ya wajibu ndio inayoifanya taaluma hii iwe ya kipekee. “maadili huanzia.
New Picture (3)
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa PSPTB, Dr Tesha akitoa hutuba ya ufunguzi kuwakaribisha wanachuo wa mwaka wa pili wa stashahada ya Ununuzi na Ugavi kutoka chuo cha TPSC Utumishi wa Umma tawi la Tanga.
New Picture (4)
Wanachuo wakimsiliza Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bodi Dr. Tesha.
New Picture (5)
Mkurugenzi ya Mafunzo, Bw. Godfred Mbanyi akielezea juu ya madaraja ya mitihani ya Bodi na taratibu za kufanya mitihani.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images