Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

Balozi Mulamula azungumza na wanaDiaspora katika kongamano la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani

0
0

Mhe.Liberatus Mulamula

Balozi wa Muungano ya Jamhuri ya Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberatus Mulamula, alipozungumza  katika kongamano  la mapambano dhidi ya gojwa la saratani duniani, aliwataka wanaDiaspora wa nchi za kiAfrika kuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na watalaamu wa vitengo vya afya duniani ili kuboresha upatikana wa huduma za afya barani Afrika. Mhe. Balozi Mulamula, ambaye pia ndie aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo alizungumzia faida za kutumia Teknolojia  ili kuboresha mawasiliano kati ya wataalam, utafiti na  elimu . 
Nia mojawapo ya  kongamano la Global Health Catalyst Cancer Summit 2015 ni kuboresha huduma mahiri za saratani barani Afrika kwa  kutumia ( Information and Communication Technologies (ICTs);Teknolojia ya mawasiliano kati ya wataalam wa gojwa la saratani wa nchi za nchi za ng'ambo  na wataalam waliopo barani Afrika.Mhe. Balozi L. Mulamula, alikabidhi Tunzo Maalum kwa Bigwa wa Tiba ya Saraatani Dr. Twalibu Ngoma. Dr.Ngoma ni miongoni mwa wataalam wa kuigwa ambaye amepata elimu ya juu nje ya nchi na kureja nyumbani ili kuboresha upatikanaji wa huduma na elimu ya saratani nchini Tanzania.


WANACHAMA WA TUICO TAWI LA MUWSA ,WAPATA VIONGOZI WAPYA

0
0
Viongozi na wananchma wa Chama cha Wafanyakazi TUICO tawi la MUWSA wakiimba wimbo wa Solidarity.
Viongozi wapya wa Chama cha Wafanyakazi (TUICO) tawi la MUWSA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa kuongoza tawi hilo kwa kipindi cha miaka mitano. 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

AIRTEL YAKARABATI DARASA SHULE YA MSINGI USHINDI

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa tatu kulia), akimkabidhi Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o, Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kulia) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), akifungua mlango wa Darasa la Chekechea lililokarabatiwa kwa udhamini wa Wafanyakazi wa Airtel, kama sehemu ya huduma kwa jamii, katika Shule ya Msingi Ushindi iliyopo Mikocheni ‘B’, jijini Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Mwenyekiti wa Shule hiyo, Jumanne Konara, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Elias Katunzi, Mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mikocheni ‘B’, Suleiman Sagong’o na baadhi ya wafanyakazi wa Airtel.

NANI KUIBUKA KINARA WA TUZO ZA FILAMU TANZANIA!

0
0
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba(kulia) akielezea jambo kwa wana habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza walioingia katika hatua ya mwisho ya kushindania Tuzo za Filamu Tanzania leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wana habari uliofanyika katika hotel ya New Africa ya jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tuzo hizo Caroline Gul na mmoja wa wadhani kutoka International Eye Hospital Dr. Recep Yujel.
Jaji mkuu katika mchakato wa mchujo Issa Mbura kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa ufafanuzi wa vipengere 11 vilivyoainishwa kushindaniwa. 
 Afisa Masoko kutoka EATV/EA Radio Happy Shame ambao ni moja ya wadhamini wa tuzo hizi akitoa neno kwa niaba ya wadhamini wa Tuzo za Filamu Tanzania.
  Mwakilishi kutoka Push Mobile Bwana Ezekiel akielezea namna ya upigaji kura ili kupata washindi tuzo hizi kubwa nchini.

World Parliaments sharpen ways on achieving sustainable development goals

0
0
Tanzania delegation at the 132nd Inter- Parliamentary Union (IPU) Assembly which is taking place from 28 March to 1st April, 2015, in Hanoi, Viet Nam.


By Owen Mwandumbya
Hanoi, Viet Nam

Parliamentarians from across the world are calling upon all Parliaments and MPs to use their individual and collective power to make sustainable development a key for developments among IPU members states and have a concrete ways on which parliaments can implement the new sustainable development goals (SDGs) when they are adopted later this year.  

The call was made by Parliamentarians who are attending the 132nd Inter- Parliamentary Union (IPU) Assembly in Hanoi, Viet Nam which kicks off on 28 March and expected to end on 1st April, 2015 with the adoption of a declaration on the implementation of the new sustainable development goals (SDGs).

More than 600 MPs from 113 countries among them whom are Speakers, Presidents, and leader of delegation from Parliament and National Assemblies across the world are among the participants.

TANGAZO: Kamishna wa Madini awatangazia wamiliki wa leseni za madini wenye malimbikizo ya ada za leseni kuzilipia haraka

MAALIM SEIF ASHIRIKI MAZISHI YA MFUASI WA CHAMA CHA CUF ALIEFARIKI KWA AJALI, UNGUJA

0
0
Na: Khamis Haji (OMKR)

Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amehudhuria mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) aliyefariki katika ajali ya barabarani iliyotokea wakati akirudi katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja.

Marehemu ambaye ni mkaazi wa Kinuni, Wilaya ya Magharibi Unguja amesaliwa katika Msikiti Ngamia, Kilimahewa na kuzikwa Kianga, mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.

Aidha, Maalim Seif amewatembelea na kuwawafariji baadhi ya wafuasi wa chama hicho waliojeruhiwa na watu wasiojuilikana wakati walipokuwa wakirudi katika mkutano huo walipofika eneo la Fuoni.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu wa CUF bibi Pavu Juma, katika tukio hilo vijana waliokuwa katika gari eneo la Fuoni Taveta wakiwa na mapanga, nondo na mawe walianza kuwarushia mawe wafuasi wa CUF waliokuwa kwenye magari wakitokea katika mkutano Makunduchi na kuwajeruhi wafuasi 24 wa chama hicho.

Amesema baadhi ya majeruhi hao wamepata majeraha makubwa na wamelazwa katika hospitali ya Mnazimmoja, na wengine wamesafirishwa hadi Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mapema akiwatembelea baadhi ya majeruhi huko Mwembemakumbi, Katibu Mkuu huyo wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema watu waliowajeruhi wafuasi wa CUF wamefanya hivyo baada ya chama chao kukosa Sera za kuwaeleza Wananchi na sasa wameamua kufanya hujuma ambazo amesema hazitowasaidia.

Amerejea wito wake wa kuwataka wanachama na wafuasi wa CUF wawe watulivu na kwamba chama hicho kinafuatilia kwa karibu hujuma zote zinazofanywa dhidi yao.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akishiriki katika mazishi ya Hemed Salum Hemed (38) mkaazi wa Kinuni Zanzibar aliyefariki katika ajali ya barabarani wakati akitoka mkutanoni Makunduchi. Mazishi hayo yamefanyika Msikiti Ngamia, Kilimahewa.
Katibu Mkuu wa CUF, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali mmoja kati ya watu waliojeruhiwa na watu wasiojulikana katika maeneo ya Fuoni Taveta, wakati wakirejea kutoka mkutano wa CUF Makunduchi. Amemtembelea kijana huyo Shamis Ali Khamis nyumbani kwao Muembe Makumbi mjini Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).

JUST IN: Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki (Electronic Transanctions) 2015


MALI MPYA IMEWASILI NDANI YA DUKA LA J&M VIRGO

0
0
 DUKA LAKO PENDWA LA J&M VIRGO LIMESHUKA MALI MPYA NA ZA UHAKIKA KABISA KWAKO WEWE MTANZANIA TOKA MAJUU ILI UWEZE KUNG'AA KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA PASAKA

J&M VIRGO WENYE UHODARI WA KUUZA VIWALO VYA NGUVU NA VYA KISASA JIJI LA DAR ES SALAAM ,WANAPATIKANA PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA.FIKA ILI UWEZE KUJIPATIA VITUZZ NA VIWALO VYA KIJANJA,POCHI BABKUBWA,MOKA MATATA NA MICHUCHUMIO YA HAJA KWA KINA DADA.

KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO

 Gauli la mtoko wa Jioni kwa kina Dada.
Moka za nguvu kwa kina baba.

WATEJA WA VODACOM WAAMBIWA CHONDE WASIWE WANAZIMA SIMU ZAO

0
0
Wateja wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuacha simu zao zikiwa hewani ili waweze kupata mawasiliano kwa urahisi muda wowote na mahali popote wanapokuwa. 
Wito huo ulitolewa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa droo ya 45 ya Promosheni ya Jaymillions ambayo imemuwezesha mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kitita cha shilingi Milioni 100/- ingawa alipopigiwa simu na maofisa wa kampuni hiyo mbele ya waandishi wa habari na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Mrisho Millao simu ya mteja huyo ikawa haipatikani. 
“Tunaelewa zipo sababu zisizoweza kuzuilika ambazo zinaweza kusababisha simu ya mteja isiwe hewani lakini vilevile kuna baadhi ya wateja wana utamaduni wa kuzima simu ambao unaweza ukasababisha mteja akose mawasiliano ya muhimu kama mteja wetu huyu leo ambaye tulitaka kumpa taarifa ya kujishindia kitita chake kupitia promosheni yetu ya Jaymillions”. Alisema kwa mjibu wa taratibu za Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa namba hiyo ya ushindi kutopatikana wataendelea kufanya jitihada za kumtafuta mshindi kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari na kuendelea kumpigia mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili kuona kama kuna wakati atakuwa hewani. 
Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari mwaka huu ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi wawili wa milioni 100/-(akiwemo mshindi wa leo),washindi wanne wa Milioni 10/-na washindi 38 wa Milioni moja.
Nkurlu pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions katika kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.
 Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Mrisho Millao (kushoto) akihakiki namba ya simu anayooneshwa na  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) wakati wa kuchezesha droo ya 45 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ambapo mshindi wa pili wa kitita cha shilingi milioni 100 alipatikana. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au Auto kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya 45 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ambapo mshindi wa pili wa kitita cha shilingi milioni 100 alipatikana. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au Auto kwenda 15544. Kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini,Mrisho Millao



Global Health catalyst Cancer Summit 2015

0
0
Wataalamu na washiriki katika mkutano huo uliofanyika Boston, Massachutes.
Mwanzilishi wa http://www.nesiwangu.com/ ; mtandao unahusika na utoaji wa Elimu Afya kwa lugha ya kiswahili  Bi. harriet Shangarai, alizungumzia faida za kutoa Elimu Afya kwa kutumia lugha ya asilia na  kusema kuwa baadhi ya wasomaji wake walitafuta huduma ya haraka baada kujisomea na  kuelewa dalili  zenye kuashiria hitilafu katika mifumo mbali mbali mwilini.

Bi. Harriet alizungumzia faida zitokanazo na Teknolojia ya mawasiliano ambayo ni fursa kubwa kwa Wanadiaspora kutoa mchango wao wa kielimu kwa jamii na kujenga mawasilino ya karibu na wataalam wa afya nchini mwao ili kwa pamoja waweze kushirikiana katika  kuziba  mapengo yaliyomo kwenye uwanja wa huduma na elimu ya afya.
Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA

AMI hospital faces imminent closure

0
0

AMI Hospital or Trauma Center at Msasani Dar es Salaam is facing imminent closure after it failed to comply by Tanzania Court of Appeal order that wanted it to deposit in court USD 1,514,000 plus a monthly rent to a tune of USD 64,000 per month following a tenancy agreement dispute.

A panel of three Court of Appeal judges, Justices Mbarouk Mbarouk, Salum Massati and Katherine Oriyo ordered African Medical Investments (T) Ltd (AMAI) to make the deposits a month after the ruling which was issued on the 12th day of February 2015, an order that has not been honored. 

The court made their ruling on civil application No. 185 of 2014 filed by AMI in protest against execution of a ruling on main commercial suit No. 104 of 2013 that it lost to its Landlord (local business man Navtej Singh Bains) in respect of a building where the company is conducting its business.

AMI Hospital had lost the case filed by the landlord for failure to pay rent for the past 26 months in a legal battle at the Tanzania Commercial Court in November 2014 and were issued with a Notice for Eviction by the landlord.
AMI subsequently filed for Bankruptcy protection to the High Court of Tanzania last Friday stating that it was operating insolvently having incurred losses for the past two years.

AMI Plc Chief Executive Officer (CEO), Mr Theunis Peter Botha, also a Director and CEO of the local AMI Hospital in Tanzania, filed the Bankruptcy application in the High Court of Tanzania.

 AMI Tanzania is wholly owned by its London Company AMI Plc which was kicked out of the London Stock Exchange in February 2014 for trying to sell its assets in Maputo without shareholder disclosure.

Through a notice released last week on Wednesday (25th March), Mr Lawrence Ochola, a Kenyan National working as Hospital Accountant, appealed for all stakeholders to stay cool and that AMI Hospital is operating normally.

“The management of AMI hospital –Dar es Salaam wishes to take this opportunity to acknowledge to its various stakeholders that we are aware of their fears and concerns that have been elicited by news that appeared in a section of local media to the effect that AMI has filed for bankruptcy.

In a bankruptcy petition filed last week before the High Court's Main Registry, the company alleges that it has been incurring losses in terms of billions to the extent of having several outstanding liabilities and debts which are now exceeding its ability to pay to different creditors.

"The petitioner (AMI) incurred a net loss of 1.146 million US dollars in the year ended February 28, 2013, while in the year ended February 28, 2014, the petitioner incurred a net loss of 775,000 US dollars," reads a section of the petition document.

It is stated that the company was also required to pay outstanding dues to institutes, notably the National Social Security Fund (NSSF) and the Tanzania Revenue Authority (TRA) and individuals.

According to the petition, given the value of the assets of the company and the amount of money owed to it by creditors, there was no way it would be able to raise enough funds for paying them as well as meeting her obligations.  

There are also records showing that Lancet Laboratory (T) Ltd filed for an urgent application against AMI Hospital eviction claiming over TSh 150m owed to them by AMI Hospital.

Inside information has it that several creditors are now in a limbo as the Hospital owes over $4m to them including the biggest creditor being the Landlord Mr N Bains, Doctors, Staff, TRA, Pharmaceutical suppliers and other suppliers.

Learned counsel Dilip Kesaria, who represented the Landlord, asked the court to issue a final notice of eviction which has been outstanding since September 2014 against AMI Hospital.

NMB NA DSE WAZINDUA SHINDANO LA UWEKEZAJI KWA WANAFUNZI WA VYUO VYA JUU NCHINI

0
0
Soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa kupitia udhamini wa benki ya NMB imezindua shindano la uwekezaji lijulikanalo kama ‘DSE Scholar Investment Challenge’ linalowahusisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu ambapo washindi wanatarajia kuibuka na kitita cha shilingi milioni 2 na nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo.

Shindano hilo ambalo litadumu kwa miezi mitatu, litawakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu ambao watapewa mitaji ya kielectroniki (Virtual Capital) ya shilingi milioni moja na wao kufanya uwekezaji kwa njia ya kununua hisa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.

Washindi watatu watakaopatikana, watagawana kitita cha shilingi milioni 2 ambapo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 1, mshindi wa pili laki 6 na mshindi wa tatu atapata shilingi laki nne. Washindi watapatikana kutokana na faida watayoipata katika uwekezaji wao kwenye soko la hisa na ushiriki wao kwenye majadiriano yanayoonyesha njia walizotumia kufikia faida walizopata. Shindano hili litafanyika kwa njia ya mtandao wa simu.

Hii ni mara ya pili kufanyika kwa shindano hili kuendelea kupata udhamini mzuri kutoka benki ya NMB, Lengo la shindano hili ni kuwahamasisha wanafunzi kujenga utamaduni wa kuwekeza na kutunza akiba katika taasisi za fedha.
Afisa kutoka DSE – Aleck Ngoshani akiwasilisha mada kwa wanafunzi wa CBE wakati wa semina za kuwahamasisha wanafunzi kushiriki shindano la DSE na jinsi watakavyoweza kufanya uwekezaji kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Wanafunzi wa chuo cha biashara cha CBE wakisikiliza mada kutoka kwa maafisa wa DSE jinsi ya kushiriki shindano la DSE Scholar Investment Challenge.

TUME YA KUREKEBISHA SHERIA TANZANIA YAFANYA KIKAO CHAKE CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI DAR ES SALAAM

0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambaye ni Katibu wa Tume Bi. Agnes Mgeyekwa akitoa hotuba fupi katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi TUMESHERIA.
Mwenyekiti wa TUGHE tawi la TUMESHERIA Bw. Fredy Kandonga akizungumza katika kikao cha Baraza.
Mwenyekiti wa Tume Mh. Jaji Aloysius Mujulizi akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi.

USAID gets accolades for supporting WMAs

0
0
On Monday, March 30, the Authorized Association Consortium (AAC) of Wildlife Management Areas (WMAs) kicked off a 2-day Constitution and Strategic Plan Workshop at the Kurasini Training and Conference Centre in Dar es Salaam. At the opening of the workshop, Acting Wildlife Director Herman Kerario expressed gratitude to the United States Agency for International Development (USAID) for its longstanding support for WMAs in Tanzania. Pictured is a token of appreciation, a custom beaded Maasai rungu stick and Maasai cloth, presented to USAID Deputy Office Director for Economic Growth Randy Chester by Chairman of Enduimet WMA Komolo Simel.

The AAC is an important platform for discussions on how to advance the cause of the community-owned and managed conservation areas called WMAs. USAID has supported WMAs in Tanzania since 1998, through policy and institutional development and implementation in areas with critical wildlife habitat.

SAKATA LA ASKOFU GWAJIMA, MAASKOFU KUTINGA KWA IGP LEO KUMUOMBEA MSAMAHA

0
0
 Maaskofu na wachungaji wa makanisa ya kipentekosti wakiingia ukumbini katika Hoteli ya Tamari iliyopo Mwenge tayari kwa kutoa tamko lao.
Katibu wa Maaskofu wa makanisa ya Kipentekosti Dk. Damas Mukassa akisoma tamko la maaskofu hao Dar es Salaam jana, kuhusu sakata la kukamatwa kwa Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima ambalo leo hii wanatarajia kwenda kumuona Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu kuzungumzia suala hilo. Kulia ni Askofu Dk.Mgullu Kilimba na Askofu Mwaviga Mwafululila.
 Askofu Dk. Paul Shemsanga akizungumza katika mkutano huo ambapo maaskofu hao walitoa tamko lao.

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MILIONI 10 UJENZI WA KANISA LA KKKT USHARIKA WA MATOSA

0
0
 Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Rabisante Lema akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei baada ya kukabidhi hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miundombinu ya kanisa hilo wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa. Jumla ya shilingi milioni 50 zilipatikana katika harambee hiyo. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) akimkabidhi hundi ya sh. millioni kumi Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Matosa Kimara jijini Dar es Salaam, Mhandisi Simon Kihunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kanisa hilo, wakati wa harambee iliyofanyika kanisani hapo, ambapo jumla ya shillingi milioni 50 zilipatikana. 
Godwin Semunyu akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charls Kimei baada ya kutoa mchango wake. Kulia ni Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Rabisante Lema.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

BBC DIRA YA DUNIA

MAHAFALI YA PILI YA PROGRAM YA HAKI ZA BINADAMU UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA DAR

0
0
 Rais wa Foundation For Civil Society, Dk. Stigmata Tenga akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya pili ya Program ya Haki za Binadamu Afrika Mashariki yaliyofanyika katika Chuo cha Bagamoyo (UB) jijini Dar es Salaam.
Rais wa Foundation For Civil Society, Dk. Stigmata Tenga (kulia) akimkabidhi cheti muhitimu wa kozi ya haki za binadamu Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika  Chuo Kikuu cha Bagamoyo, Comfort Maembe, kozi hiyo iliandaliwa na Chuo Kikuu cha Bagamoyo kwa kushirikiana na Akiba Uhaki Foundation ya Kenya na kufanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Picha na Francis Dande).

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

ALIYEKUWA KATIBU WA MBUNGE WILAYA YA ROMBO AJIUNGA NA CCM

Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images