Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 783 | 784 | (Page 785) | 786 | 787 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Picha juu na chini ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Bingwa, Dimba na Mtanzania kutoka Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Sharifa Mmasi pichani akisoma kitabu cha Dira na Tumaini Jipya Handeni kilichoandikwa na Kambi Mbwana, ambaye ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Handeni Kwetu linalofanyika kila mwisho wa mwaka wilayani Handeni, mkoani Tanga. 

  Na Mwandishi Wetu, 
  Dar es Salaam
  MWANDISHI wa Habari za Michezo ambaye pia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha la Utamaduni la Handeni Kwetu, Kambi Mbwana, ameandika kitabu chake kinachojulikana kama ‘Dira na Tumaini Jipya Handeni’, kilichoanza kupatikana mapema wiki hii jijini Dar es Salaam na wilayani Handeni, mkoani Tanga.
  Kitabu hicho kimeelezea kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa Handeni, kama vile shida ya maji, elimu na migogoro ya ardhi kwa ajili ya kushirikisha mawazo ya viongozi wa serikali, wadau na wananchi ili kukabiliana na tatizo hilo wilayani humo na mikoa ya jirani ambapo changamoto hizo zinashabihiana kwa kiasi kikubwa.
  Kwa habari kamili BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Imeripotiwa na Hiroshi Takeuchi Tokyo,Japan, 

  Wanamuziki wa kongwe wa muziki wadansi Abbu Omar Njenga aka Abbu Omar na Fresh Jumbe Mkuu wenye ngome yao nchini Japan,siku ya jumamosi 21 Machi 2015 walitia fora kwa kushiriki jukwaani na kumpa baraka zote mwanamuziki Ally Choki katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,Tokyo, Japan. 

  Wakongwe hao waliobobea katika muziki kwa maiaka mingi Abbu Omar Njenga mpiga gitaa au mpini na mtunzi aliyewahi kutamba na bendi za UDA JAZZ na mwaka 1981 alijiunga na Simba wa Nyika nchini Kenya na hatimaye kujikita nchini Japan kwa miaka mingi na mwenziwe mkongwe Fresh Jumbe Mkuu aliewahi kuwa mwimbaji mtunzi wa bendi za Dar International (Super Bomboka),DDC Mlimani Park "Sikinde na pia Juwata Jazz band aka Msondo Ngoma.
  Wakongwe hawa ni mfano wa kuigwa pamoja na kuwa wameliteka soko la muziki wa kiafrika nchini japani na kungineko lakini wapo mstari wa mbele kuwaunga mkono na kuhakikisha kuwa wanamuziki wa nyumbani Tanzania waingiapo Japan wanateka soko. Pia mnaweza kujumuika na mmoja wao at https://www.facebook.com/omar.abbu
  Abbu Omar Njenga aka Profesa Abbu Omar na Fresh Jumbe Mkuu kazini
  Camarade Ally Choki
  Ally Choki na Super Nyamwela
  Profesa Abou Omar
  Fresh Jumbe Mkuu

  0 0
 • 03/26/15--13:00: TUZO ZA WATU TANZANIA 2015

 • Washindi wa Tuzo ya Watu Tanzania 2014


  0 0


  THE COMPANY IS NOW UNDER NEW MANAGEMENT. 
  LOGISTICS LINK OF KENYA HAS TAKEN OVER THE COMPANY AND PROMISES TO  KEEP THE PRICES  LOW, PLUS  EXCELLENT CUSTOMER SERVICE!
  WE ARE INVITING YOU FOR A BUSINESS DINNER AT THATCHED HOUSE PUB ON FRIDAY 27/03/2014 FROM 18:00HRS TO 22:00
  WELCOME FOR DRINKS AND NYAMA CHOMA TOGETHER.

  VAN ON A CONTAINER SERVICE
  SMALL VANS £850
  LARGE VANS i.e sprinter £980
  NEW CONTAINER SHIPMENT SERVICE FOR CARS
  WE NOW SHIP CARS ON CONTAINERS TO MOMBASA/DAR ES SALAAM
  WE LOAD ONLY TWO VEHICLES ON A 40' CONTAINER
  WE DONT LOAD ANYTHING ELSE
  NO CARGO OUTSIDE CARS
  YOU CAN LOAD ANYTHING INSIDE YOUR CAR AND LOCK IT
  4 X 4 /SALOON TO MOMBASA /DAR IN A CONTAINER £750
  SMALL VANS £850
  LARGE VANS ie sprinter £980
  NO LOADING CHARGES
  EVERY CAR HAS ITS OWN BILL
  WE WILL OFFLOAD FOR YOU IN MOMBASA/DAR AND GIVE YOU 21 DAYS FREE STORAGE

  MAXIMUM SECURITY
  5 WEEKS TRANSIT TIME
  CONTAINER VESSEL SAILS EVERY FRIDAY
  HAKUNA TENA KULALAMIKA VITU KUIBIWA KWA GARI
  YOU ARE WELCOME TO WITNESS THE LOADING!
  THIS IS OUR CONTAINER SO YOU DONT DEAL WITH THE CONTAINER, WE TAKE CARE OF THE CONTAINER.
  YOU JUST GET YOUR CAR   CUSTOMS CLEARED

  Tell (+44) 01375 855917    SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali 
  LYDIAH SEYMOUR ; 07950491707

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimraribisha Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Kanda ya Kati (Central Corridor Conference) ulioanza jana na kumalizika leo Machi 26, 2015.
  Rais Paul Kagame wa Rwanda akipeperusha bendera kuashiria kuzinduliwa kwa safari za treni za mizigo kuelekea Rwanda katika stesheni ya reli ya Dar es salaam akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete leo Machi 26, 2015.


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake, Rais Paul Kagame wa Rwanda, leo, Alhamisi, Machi 26, 2015, wametembelea Bandari ya Dar es Salaam na baadaye Rais Kagame ameanzisha safari ya treni maalum za kusafirisha mizigo ya Rwanda kutoka Tanzania.

  Rais Kagame amewasili nchini asubuhi ya leo na kufungua Mkutano wa Wawekezaji katikaUjenzi wa Miundombinu Ukanda wa Kati (High Level Investors Forum – Central Corridor Development Acceleration Programme) uliofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere mjini Dar es Salaam.

  Mara baada ya hotuba ya ufunguzi na kipindi cha maswali kutoka kwa washiriki na majibu kutoka kwa viongozi wa nchi tano zinazounda Shirika la Uwezeshaji wa Usafiri wa Ukanda wa Kati (The Central Corridor Transit Transport Facilitation Agency (CCTTFA), viongozi hao wawili wamekwenda Bandari ya Dar es Salaam.

  CCTTFA lilianzishwa Septemba 2, mwaka 2006, na Makubaliano yaliyotiwa saini na nchi tano ambazo zinanufaika na usafiri wa Ukanda wa Kati – Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Rwanda na Uganda.

  Katika Bandari ya Dar es Salaam, Rais Kagame na mwenyeji wake wameanza kwa kutembelea ofisi mpya za Mpango wa Ukusanyaji Ushuru kwa Pamoja (Single Customs Territory)miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), mpango ulioanza kutumika Julai mwaka jana, 2014. Chini ya Mpango huo, kila nchi inashughulikia mizigo yake yenyewe, ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi yake.

  Rais Kagame na mwenyeji wake wametembelea ofisi za Mamlaka ya Kodi ya Rwanda (RRA) na Mamlaka ya Kodi ya DRC ambako walipewa maelezo kuhusu faida za mpango huo.

  Miongoni mwa mambo mengine, marais hao walielezwa kuwa chini ya Mpango huo, waagizaji wa mizigo ya Rwanda, kupitia Bandari ya Dar es Salaam, sasa wanajaza fomu moja tu badala ya tatu na sasa mizigo ya Rwanda inachukua siku mbili tu kutoka Bandari ya Dar es Salaam hadi Kigali, badala ya siku kati ya tano na 10 kabla ya kuanzishwa Mpango huo.

  Nchi ambazo tayari zimefungua ofisi zao katika Bandari hiyo kutekeleza Mpango huo ni Tanzania yenyewe, Burundi, DRC na Rwanda. Uganda inakamilisha maandalizi ya utekelezaji na Zambia imeonyesha nia ya kujiunga na Mpango huo, kwa sababu inapitishia mizigo yake katika Bandari ya Dar es Salaam, hata kama siyo mwanachama wa EAC.

  Kutoka kwa ofisi za Single Customs Territory, viongozi hao wamekwenda kwenye Bandari ya Dar es Salaam ambako wamepatiwa maelezo kuhusu jinsi utendaji wa Bandari hiyo ulivyoboreka katika miaka miwili iliyopita.

  Aidha, viongozi hao wameelezwa jinsi gani pia utendaji wa kampuni binafsi ya upakiaji na upakuaji mizigo ya TICTS inavyofanya kazi na ilivyoboresha utendaji wake katika sehemu nne za meli kutia nanga (berths) ambako inafanyia kazi yake katika Bandari hiyo yenye sehemu 11 za kupakia na kupakulia mizigo.

  Katika Bandari hiyo, marais hao wameelezwa kuwa katika miaka mitano iliyopita, kiwango cha mizigo inayopitia katika Bandari hiyo kimekuwa kinaongezeka kwa wastani wa asilimia 12.8 kila mwaka.

  Wameelezwa pia kuwa mwaka jana, kiasi cha tani milioni 14.6 ya mizigo kilipitia katika Bandari hiyo zikiwemo kontena 621,000 na kuwa kati ya mizigo hiyo kiasi cha asilimia 34, sawa na mizigo tani milioni 5.020 ilikuwa mizigo kwa ajili ya nchi za jirani.

  Aidha, viongozi hao wameelezwa kuwa muda wa kontena kukaa Bandarini hapo sasa ni siku tisa tu badala ya siku 21 Februari mwaka 2008, muda wa meli kukaa nje ya Bandari ikisubiri kuingia Bandarini ili ipakuliwe, sasa ni siku moja unusu badala ya siku tatu unusu za mwaka 2013.

  Marais Kagame na Kikwete pia wameelezwa kuwa usalama wa mizigo ya waagizaji sasa umeongezeka mno, kiasi cha kwamba halijakuwepo tukio hata moja la wizi wa mizigo ya wateja yakiwemo magari na spea zake kwa miaka mitatu mfululizo sasa.

  Bandari ya Dar es Salaam ambayo huhudumia mizigo ya nchi saba – ya Tanzania yenyewe, Malawi, Zambia, DRC, Burundi, Rwanda na Uganda pia huendesha Bandari kwenye maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa.

  Jana, Jumatano, Machi 25, 2015, Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na wawakilishi wa nchi za DRC na Uganda pia walianzisha safari za treni za namna hiyo kwenda katika nchi zao.

  Rais Kagame ameondoka nchini kurejea kwao leo baada ya kuanzisha safari hizo na mkutano wenyewe kuhusu Ukanda wa Kati, ambao pia ulihudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, umemalizika jioni ya leo.

  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu – Dar es Salaam.


  26 Machi, 2015  0 0


  “Zanlink ambayo sasa inatumia teknolojia ya FIBER, inapenda kuwatangazia kuwa imeanzisha kifurushi cha huduma ya mtandao katika fiber, ambacho kinaitwa “Home Pack”. 
  Huduma ya kifurushi hiki kinapatikana kwa wateja wanaokaa maeneo ya Stone town, Mlandege, Mbweni, Chukwani, Mazizini, Kiembe Samaki na Mombasa. Maeneo mengine yatafuata karibuni

  Kifurushi hiki kinapatikana kwa bei nafuu na ni mahususi kwa watumiaji wa majumbani wa huduma ya mtandao (internet), kina spidi ya 512 kbps muda wa mchana na spidi ya 2 mbps muda wa usiku na wikend. Kwa maelezo zaidi unaombwa ufike ofisi yetu iliyopo  mtaa wa Vuga baina ya Sinema ya zamani ya Majestik na ofisi za zamani za SUZA.

  Sasa unaweza kujiunga na kufurahia huduma ya uhakika na ya bei nafuu kwenye Fiber.” 


  “Get FIBER”

  “Zanlink which is now on Fiber, is happy to inform you that it has launched fiber business internet packages which have high speeds to meet your daily business bandwidth requirements. These service plans are currently available to customers within the Stone town, Mlandege, Mbweni, Chukwani, Mazizini, Kiembe Samaki and Mombasa areas. Other areas will follow soon.

  Due to the importance bandwidth speeds for business use, we have plans that have data caps with speeds ranging from 2 mbps to 4 mbps as well as various unlimited bandwidth plans to ensure you have the highest speeds available. For more information on how to get FIBER, please visit our office along Vuga Street, right between the Old Majestic Cinema and the former SUZA office building and get “Fibered”.
  0 0

  Baada ya Mji wa Ibaraki kutoa magari mawili ya kubeba wagonjwa na moja la huduma ya zimamoto mwezi Februari, 2015, Miji mingine ya Japan nayo imeunga mkono jitihada hizo.
  Pichani Mhe. Salome Sijaona, Balozi wa Tanzania Japan na Mhe. Toshima Suzuki, Meya wa Mji wa Tochigi wakionyesha mkataba wa makubaliano wa msaada wa magari 10 ya huduma, gari 6 ni kwa ajili ya Zimamoto na 4 kubeba Wagonjwa. Gari mbili (moja la wagonjwa na moja la huduma ya zimamoto) zimetolewa Machi 24 na mji huo kwa mwaka 2015 na gari nyingine 8 kwa kipindi cha mwaka 2016/17.

  Vile vile Mjiwa wa Hakusan - Ishikawa Prefecture umetoa gari mbili za huduma ya Zimamoto Machi 25, 2015 na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kwa mwaka ujao wa fedha.
  Kulia ni Afisa wa Ubalozi, Bw. Francis Mossongo, akipokea Nozzle ya gari ya zimamoto kutoka kwa Bw. Noriaki Yamada, Meya wa Mji wa Hakusan kama ishara ya kupokea gari hizo.
  Picha ya Gari zilizopokelewa kutoka kikosi cha zimamoto cha mji wa Kanazawa. Gari hizo zitakabidhiwa kwa kikosi cha Zimamoto Tanzania.
  Vile Vile Ubalozi umeshizikiana na Hakusan Chamber of Commerce ya mji wa Hakusan kuanzisha aina mpya ya kahawa kwa jina la Hakusan-Kilimanjaro Coffee. Lengo ni kuunganisha na kutangaza mlima ya Kilimanjaro na Mlima Hakusani. Chini ni picha ya Kahawa hiyo. Kila kikombe kimoja kinachouzwa kiasi cha Yen 10 (sawa na Tsh. 150) inatumika kwa ajili ya kulinda mazingira ya milima hiyo miwili ikiwa ni pamoja na kupanda miti.

  Juu ni mfano wa kahawa hiyo ikiwa kwenye vifungashio viwili tofauti.

  Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania Japan
  26. Machi 2015

  0 0


  0 0
 • 03/27/15--01:58: Bei ya Madafu leo

 • 0 0
 • 03/27/15--02:00: BBC DIRA YA DUNIA

 • 0 0

  Mkurugenzi wa Mipango wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Jason Rwiza, akielezea namna TANROADS inavyofanya kazi za ujenzi wa barabara hapa nchini kwa ujumbe wa viongozi kutoka Sudan Kusini katika ofisi za Wakala hao jijini Dar es salaam jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Barabara wa Sudan Kusini Eng. Kenyata Warille, akifafanua namna Mamlaka yake inavyofanya kazi za ujenzi wa barabara nchini kwao. (Nyuma wa kwanza kulia) ni Mwakilishi wa JICA wa Sudan Kusini Tomoki Kobayashi, akifatilia kwa makini.
  Naibu Waziri wa Usafirishaji, Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mh. Simon Mijok (Wa kwanza kulia), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi wa Sudan Kusini Eng. Gabriel Makur, baadhi ya vitabu walivyopewa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa ajili ya kuwasaidia kuboresha taasisi zao za ujenzi.


  0 0

  Mpenzi wa Michuzi tv, sasa tunapatikana kwenye SIMU.tv. Kujiunga na SIMU.tv, ukiwa na simu au tablet ya Android, nenda kwenye Google playstore uandike SIMU.tv au bofya linki hii: https://play.google.com/store/apps/details?id=com.SIMU.tv . Utaweza kudownload BURE app ya SIMU.tv. Ukishadownload, nenda kwenye categories, ukifika hapo elekea kwenye TV channels na utakuta Michuzi TV kama inavyoonekana hapa chini. 

   Fuatilia Michuzi tv muda wowote na mahali popote ulipo kwenye SIMU.tv.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa kikao kazi cha siku moja ya maafisa na wakuu wa idara za Halmashauri za miji na Manispaa za mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, iliyofanyika makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam, Alhamisi Machi 26, 2015.
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo, Profesa Hermans Mwansoko akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha siku moja kwa maafisa na wakuu wa idara za Halmashauri na Manispaa za Dar es Salaam na Pwani, kilichoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na kufanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam, Alhamisi Machi 26, 2015
  Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Contatina Martin, akizungumza kwenye kikao hichoMkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Gabriel Silayo, akitoa mada kuhusu uwekezaji wa Mfuko huo, wakati wa kikao kazi hicho


  0 0


  0 0  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akizungumza wakati wa kukabidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad akimkabidhidhi Ripoti yake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Musa Assad(kushoto)ikulu jijjini Dar es Salaam leo.Kulia anayeshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa waandamizi kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuju wa Hesabu za Serikali mufa mfupi kabla ya mkuu wa taasisi hiyo Profesa Musa Assad(Watatu kushoto) kuiwasilisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watano Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Milionea kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Ibrahim Ibrahim (kushoto) akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10/- Zuwena Rajabu(kulia)aliyeibuka mshindi wa kitita hicho kupitia Promosheni hiyo wiki hii.Anayeshuhudia katikati ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu.Hafla hiyo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es Salaam,Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
  Milionea kupitia Promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Ibrahim Ibrahim (kushoto) na Meneja wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(katikati)wakimpongeza Mshindi wa Promosheni ya Jaymillions,Zuwena Rajabu baada ya kumkabidhi hundi yake yenye thamani ya kitita cha shilingi Milioni 10/-alizojishindia kupitia promosheni hiyo.Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.


  0 0

  Mwenyekiti  wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana (hawapo pichani) kuhusu maandalizi  ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 5, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi, Jimmy Charles. (Picha na Francis Dande)
  Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Jimmy Charles akifafanua jambo.

  Na Mwandishi Wetu


  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Aprili 5 mwaka huu jijini Dar es Salaam.  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika kwa asilimia 97 hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.


  Alisema wameshakamilisha maandalizi ya tamasha hilo, ila kinachosubiriwa ni waimbaji  wa kimataifa Ephraim Sekeleti wa Zambia, Ifeanyi Kelechi kutoka Uingereza, Rebeca Malope na Thori Mahlangu wote kutoka Afrika Kusini pamoja na Faustine Munishi ‘Malebo’ kuanza kuwasili nchini.

  “Tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani tutakata keki, kupiga fataki kama ishara ya kutakiana amani, upendo  na mshikamano na tutaiombea nchi yetu  kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba mwaka huu’’alisema Msama.

  Msama aliongeza kuwa tamasha la mwaka huu litabeba ujumbe mahsusi wa ‘amani na upendo ndio amani kwa watanzania’, aidha tamasha hilo pia litatumika kupiga vita maauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Albino’

  Aliongeza kuwa ukiachia mgeni Waziri Membe, pia wageni mashuhuri watahudhuria tamasho hilo akiwemo rais mstaafu ali Hassani Mwinyi ambalo linatimiza miaka 15 tangu kuanzishwa.

  0 0

  Kondakta (ambaye jina lake halikufahamika - kulia) wa Basi  UDA  lenye namba za usajili T 558 CVP akizungumza na mmoja wa abiria na kumuomba asubiri ili awapandishe kwenye gari nyingine la kampuni hiyo, baada ya gari hilo kugonga gari ndogo lenye namba za usajili wa T 498 DCU katika kipita shoto cha Samora na Azikiwe, jijini Dar es salaam leo.
   Askari wa Usalama Barabarani wakiwa katika eneo la tukio
   Askari wa Usalama Barabarani katikati akiongea na Dereva wa UDA. 
  Gari ndogo inavyoonekana baada ya kugongwa na UDA leo.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)

  0 0

  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa tatu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya wa kwanza kushoto wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirikia la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu nyumba hizo ambazo ni za ghorofa moja zitauzwa baada ya kukamilika ujenzi wake kwa njia ya fedha taslimu na njia ya Mikopo ya benki. 
  Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi katikati akiweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa Mjini Sumbawanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama na Serikali Mkoani Rukwa tarehe 26/03/2015.
  Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Ndugu Nehemia Mchechu katika hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za makazi za shirika hilo Mjini Sumbawanga.


older | 1 | .... | 783 | 784 | (Page 785) | 786 | 787 | .... | 3272 | newer