Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA VUNJO MKOANI KILIMANJARO

0
0
   Wananchi wa Kata ya Makuyuni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye aliwaambia kwa miaka mingi sasa jimbo la Vunjo limekuwa linarudishwa nyuma na ushabiki wa kisiasa na kuwataka wananchi hao kufanya maamuzi sahihi mwaka huu kwa kuichagua CCM.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wapo kwenye ziara ya siku tisa mkoani Kilimanjaro ya Kutekeleza,Kukagua na Kuhimiza Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010.
 katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisikiliza moja ya swali lililokuwa likiulizwa na mmoja wakazi wa himo,Bi.Pepetua Shayo kuhusiana na mradi wa maji uliopo katika eneo hilo,ambapo baadhi ya wananchi wamechukuliwa maeneo yao bila kulipwa fidia yoyote.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwenye mradi wa vijana wa kijiji cha Oria ,kata ya Kahe Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Naibu Kamanda wa UVCCM , Moshi Vijijini,Innocent Shirima alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Oria,Kata ya Kahe Magharibi,jimbo la Vunjo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye uwanja wa polisi Himo ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa muda umefika sasa wa kufanya maamuzi ya msingi kwa kuchagua kiongozi anayeweza kuleta maendeleo katika Jimbo la Vunjo.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye viwanja vya polisi himo na kuwaambia wananchi hao wapinzani hawana tena ubavu wa kuongoza kwani kwa zaidi ya miaka mingi sasa wamepata nafasi na hamna walichokifanya kwa wananchi hao wa jimbo la Vunjo.
PICHA NA MICHUZI JR-VUNJO-MOSHI VIJIJINI

TASAF YAWAFUNDA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

0
0
 Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF unaendelea kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari ili waweze  kutumia vyombo vya habari vilivyoko kwenye maeneo yao kutangaza habari za Mpango wa kunusuru kaya masikini unaoratibiwa naMfuko huo.

Akifungua mafunzo hayo yanayoendeshwa kwa utaratibu wa Kikao Kazi Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amesema kazi ya kutokomeza umaskini nchini inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.

Bwana Mwamanga amesema tangu TASAF ianze kutekeleza Mpango wa kunusuru kaya masikini kumekuwa na mafanikio makubwa hususani katika maeneo ya walengwa ambao wameanza kuboresha maisha yao na katika baadhi ya maeneo walengwa wameanza kukuza shughuli za kiuchumi huku wengine wakiweza kuhudumia kaya zaokinyume na hali ilivyokuwa huko nyuma.

Amewasihi waandishi wa habari kuwatembelea walengwa wa Mpango huo ili kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na Mpango huo wa uhawilishaji fedha na kisha kutangaza mafanikio yaliyokwisha patikana huku akisisitiza kuwa hata pale penye changamoto zionyeshwe ili marekebisho yafanyike kwa manufaa ya walengwa
Zifuatazo ni baadhi ya picha za washiriki wa kikao kazi hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo kikuu Huria Mjini Mtwara.
 Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bwana RenatusMongogwela (mwenye shati nyeupe)akizungumza na ujumbe wa TASAF ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Ladislaus Mwamangawa, kwanza kushoto kwa kaimu katibu tawala.
 Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga aliyesimama akifungua kikao kazi cha watendajiwa TASAF kutoka maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa kunusuru kaya maskini na waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi (hawapopichani) 
 Washiriki wa kikao kazi cha watendaji wa TASAF  na waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga(hayupo pichani).
 Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF bwana  Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Mkurugenzi Mtendajiwa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF makao makuu baada ya kufungua kikao kazi cha waandishi wa habari wa mikoa ya Mtwara na Lindi.


BBC DIRA YA DUNIA LEO

WARSHA YA WADAU KUHUSU HUDUMA ZITOLEWAZO NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAFANYIKA JIJINI DAR

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewazo na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uainishaji wa matakwa ya wadau,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo jijini Dar es Salaam, Machi 24, 2015.
Mkurugenzi wa Huduma za Utafiti na Matumizi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dkt. Ladislaus Chang'a akitoa ufafanuzi kwenye warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uainishaji wa matakwa ya wadau,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo jijini Dar es Salaam, Machi 24, 2015.
Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu huduma zitolewaza na Mamlaka ya Hali ya Hewa na Uainishaji wa matakwa ya wadau.

WAKUU WA MAJESHI YA ULINZI WAKUTANA UMOJA WA MATAIFA

0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
 Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinachangia wanajeshi au Polisi katika operesheni za kulinda Amani chini ya Umoja wa Mataifa, wanakutana hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa katika mkutano unaoelezwa kuwa wa kihistoria. 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake amewasili jijini New York siku ya Jumatano tayari kuhudhuria na kushiriki mkutano huo ambao utafunguliwa siku ya alhamisi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon . 
 Kwa mujibu wa Waandaji wa Mkutano huu ambao ni Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa, ( DPKO) wameeleza kuwa Zaidi ya Wakuu wa Majeshi 100 watashiriki mkutano huu ambao ni wa kwanza wa aina yake kuwakutanisha Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi kwa wakati mmoja. Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi wanatarajiwa pamoja na mambo mengine, kujadili na kubadilishana mawazo juu ya umuhimu wa operesheni za ulinzi wa Amani katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiulinzi na kiusalama yanayoikabili dunia hivi sasa. 
Vile vile wakuu hao watautumia mkutano huu ambao hautakuwa wazi ( closed meeting)kuongeza uelewa na ufahamu juu ya mazingira ya uendeshaji wa operesheni za ulinzi wa Amani , na wanatarajiwa kutoa mchango wa mawazo yao juu ya namna ya kuboresha utendaji na ufanisi wa operesheni za ulinzi wa Amani. 
Katika miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, jumla ya misheni 68 za ulinzi wa Amani zilianzishwa na mpya kabisa ikiwa ni ile iliyoanzishwa ( 2014)katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ( MINUSCA). 
Jumla ya wanajeshi 93,000 na polisi 13,000 kutoka nchi 120 wanahudumu katika misheni 16 ambazo ziko katika mabara manne.Ambako pia kuna raia 17,000 wanaotoa huduma mbalimbali zikiwamo za misaada ya kibinadamu katika misheni hizo. 
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange ameambatana na Brigedia Jeneral MG Luwogo, Brigedia Jenerali HS Kamunde, Lt. Col GM Itang’are na Maj CA Ngh’abi
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange akiwa na,  kutoka kushoto,  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na kulia kwake,  Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu,  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  yupo hapa Jijini New York ambako atahudhuria na kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi ambao nchi zao zinatoa wanajeshi au polisi katika operesheni za ulinzi wa amani  chini ya Umoja wa Mataifa
 Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na ujumbe wake  katika picha ya   pamoja na Mabalozi Tuvako  Manongi na  Ramadhan Mwinyi.
Maafisa wa Uwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa wakiwa katika picha ya pamoja na  Mkuu wa  Majeshi ya Ulinzi, pamoja na Mabalozi

SUDAN KUSINI WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA KUBADILISHANA UZOEFU NA WATENDAJI WA SEKTA YA UJENZI NCHINI

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia), akizungumza na viongozi wa ujumbe wa Serikali ya Sudan Kusini waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga, akizungumza katika kikao cha mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na viongozi wa Sudan Kusini. (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Barabara wa Wizara ya Ujenzi Eng. Venny Ndaymukama, anayemfuatia ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara za Mkoa Eng. Laurent Kyombo.
Naibu Waziri wa Usafirishaji, Barabara na Madaraja wa Sudan Kusini Mh. Simon Mijok, akitoa salamu za Serikali yake kwa viongozi wa Wizara ya ujenzi, kutokana na ziara ya mafunzo ya siku tatu inayoendelea hapa nchini.

hellofood Tanzania extends its services to Mbezi Beach

0
0
Hellofood Tanzania an online food delivery company will now be extending its services to Mbezi Beach. The company has been operating in Dar es Salaam in sub-regions such Masaki, Mikocheni, Upanga, Ilala, Oysterbay, City center, Kariakoo, Kinondoni, Makumbusho, Morocco, Namanga.

The Country Manager of Hellofood Tanzania Ms. Sherrian Abdul said “for the last couple of months most of our customers have been requesting for our services in Mbezibeach, and starting today, our Mbezi beach customers can enjoy delicious cuisines from their neighborhood restaurants at the comfort of their homes through hellofood”.

Hellofood Tanzania offers customers a chance to order food from the best restaurants in their areas through their mobile app or website.Ordering food from hellofood is as easy as few clicks away. Type in your area, choose your favorite restaurant and food and then sit and relax while hellofood brings the food to you.

“We have signedthe best restaurants in Mbezi beach to cater for our customers’ food needs. We want our customers to enjoy delicious food without needing to leave the house” Ms Abdul explained. Restaurants that will begin delivering to Mbezi beach via hellofood include Amsterdam Treat, Marrybrown, Limerick, Mbezi garden, Jangwani Sea Breeze, Nelly’s Inn, Tamu Coffee,Velisa’sand many more.

Hellofood is launching its operations in Mbezi beach this Thursday on 26th March 2015 at Amsterdam Treat from 6pm onwards.”Come dance and have a good time! We will have karaoke and other prizes to win from hellofood” said Ms. Abdul.

hellofood together with its affiliated brand foodpanda and Delivery Club is the leading global online food delivery marketplace, active in more than 40 countries on five continents. The company enables restaurants to become visible in the online and mobile world and provides them with a constantly evolving online technology.

For consumers, hellofood offer the convenience to order food online and the widest gastronomic range, from which they can choose their favorite meal on the web or via the app. hellofood operates in Brazil, Mexico, Argentina, Chile, Colombia, Peru, Saudi Arabia, Jordan, Lebanon, Qatar, Nigeria, Morocco, Kenya, Ghana, Senegal, Ivory Coast, Rwanda, Tanzania, Uganda and Algeria.

foodpanda operates in India, Thailand, Indonesia, Pakistan, Singapore, Malaysia, Brunei, Vietnam, Taiwan, Bangladesh, Kazakhstan, Azerbaijan, Cambodia, Hong Kong, Philippines, Russia, Poland, Ukraine, Hungary, Romania, Bulgaria, Georgia and Serbia. Delivery Club operates in Russia.


The Africa Internet Group introduces and accelerates the online shift in Africa – for its people and its culture. It is committed to running successful and vibrant internet companies which boost the evolution of African online culture. AIG is the parent group of eight successful and fast-growing companies in more than 30 African countries, accounting for a team of over 6000 people.

AIG cares about entrepreneurship and brings together all the key elements required to build great companies: team, concept, technology and capital. Its network of companies includes JUMIA, Zando, Kaymu, hellofood, Lamudi, Carmudi, Jovago and Easy Taxi.

NMB YAZINDUA MATAWI MAPYA TABORA NA SHINYANGA

0
0
Benki ya NMB hivi karibuni imezindua matawi mapya mawili yaliyopo kwenye mikoa ya Tabora na Shinyanga. Hii ni habari njema kwa wakazi wa maeneo hayo na kwa wateja wa benki ya NMB kwa ujumla ambapo awali walitembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za kibenki.

Kuongeza matawi hayo yanamaanisha NMB imewafikia wateja wake katika kila wilaya nchini.

Uzinduzi wa matawi hayo NMB Kaliua na NMB Kishapu yamezidi kuongeza idadi ya matawi ya NMB yaliyotapakaa nchi nzima kuwa zaidi ya 170.

Tawi la NMB Kaliua liko karibu na kutuo cha reli cha Kaliua wakati tawi la Kishapu lipo umbali wa kilometa 49 kutoka barabara ya Shinyanga – Mwanhuzi kutoka Urambo.

Tembelea matawi haya ufurahie huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na benki yako ya NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi - Bw. Abraham Augustino (kushoto) akishangilia pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga - Mhe. Ally Rufunga baada ya kufungua pazia kuashuria ufugunguzi rasmi wa tawi la NMB Kishapu. 

Tawi la NMB Kishapu.

Rais Kagame awasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kushiriki Mkutano wa Uwekezaji wa Ukanda wa Kati

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akisalimiana na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Kagame yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 
Rais Kagame akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Elizabeth Jackson kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania. 
Rais Kagame akikagua gwaride la heshima.

WANAWAKE JITOKEZENI KUWANIA NAFASI YA URAIS- TGNP

0
0
Mwanaharakati  wa TGNP  kutoka kijiji  cha   Ifiga kata ya Ijombe Mbeya  Bi . Flora Mathias Mlowezi akifafanua  jambo  wakati  wa mafunzo ya  wanahabari juu ya wajibu  wa  wanawake na  vijana kujitokeza katika kuwania nafasi za  uongozi
washiriki  wa  mafunzo ya  TGNP kwa  wanahabari wa mikoa ya nyanda za juu kusini wakisikiliza kwa makini mada mbali mbali zilizokuwa  zikitolewa katika mafunzo  hayo.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

Tuzo za watu zaja kivingine, vipengele vyaongezeka

0
0
Mhariri mkuu wa Bongo5 Bw. Fredrick Bundara (kushoto) akiwa pamoja na Mhariri msaidizi, Sandu George wakizungumza leo na waandishi wa habari katika uzinduzi wa Tuzo za watu 2015.
Kampuni ya Bongo5 Media Group,  imezindua msimu mpya na wa pili wa Tuzo za Watu Tanzania zilizoanzishwa mwaka jana ili kuwatuza watu kwenye sekta ya burudani na habari wanaofanya vizuri.

Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari leo, mhariri mkuu wa mtandao wa Bongo5, Fredrick Bundala amesema tuzo za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuongeza vipengele vitatu vipya.

“Mwaka huu tuzo zimeongezewa nguvu zaidi. Kutoka vipengele 11 tulivyokuwa navyo mwaka jana hadi vipengele 1. Mwaka huu tumeongeza vipengele vitatu muhimu,” amesema Bundala.

Amevitaja vipengele vilivyoongezeka kuwa ni pamoja na muongozaji wa filamu anayependwa, tovuti/blogu inayopendwa na mfadhili maarufu anayependwa.

“Kwenye jamii yetu kuna watu maarufu ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jamii hususan watu wasio na uwezo ama wanaoshi katika mazingira magumu. Tumeona ni muhimu pia kuwatambua watu hawa ambao huamua kujinyima na kugawana kile wanachokipata ili kuwasaidia watu wanaohitaji msaada,” ameongeza.

Amesema zoezi la kuanza kupendekeza majina ya washiriki limeanza rasmi Alhamis hii ambapo wananchi wanaweza kuwapendekeza kupitia website ya www.tuzozetu.com ama kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu kwa kuandika neno TZW, code ya kila kipengele na jina la anayependekezwa kwenda 15678.

TAYARI KISHALIA HAPA.....

0
0
 Gari la kubeba wagonjwa la Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es salaam lenye nambari za usajili SM 9058 likiwa limeigonga kwa nyuma gari nyingine aina ya Toyota Mark II lenye nambari za usajili T 230 ATW kwenye makutano ya mtaa wa Uhuru na Msimbaji.
Madereza wa magari yote mawili wakiwa kwenye maelewani mara baada ya kutokea ajali hiyo,mchana wa leo.

MH. MWAKYEMBE AFUNGUA SEMINA YA MAJAJI NA MAWAKILI JIJINI DAR

0
0
Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa Hotuba ya ufunguzi kwa Wajumbe (hawapo pichani) kwenye Semina ya Majaji na Mawakili ya Umuhimu wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika usimamizi wa haki inayofanyika Machi 26, 2015 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afrika Mashariki, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati ya walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria Semina ya Majiji na Mawakili ya umuhimu wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika usimamizi wa Haki inayofanyika Machi 26, 2015 kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

NEWS ALERT: ASKOFU GWAJIMA ATAKIWA KUHOJIWA NA JESHI LA POLISI KUHUSU TUHUMA ZA KASHFA NA MATUSI DHIDI YA KALDINARI PENGO

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtaka Askofu JOSEPHAT GWAJIMA wa Kanisa la Ufufuo na Uzima afike haraka katika kituo cha Polisi cha Kati ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa mahojiano kuhusu tuhuma za kashfa na matusi.

"Tumepokea malalamiko ya kukashifiwa na kutukanwa hadharani Mwadhama Kaldinari Polycarp Pengo ambaye ni kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kama vile WhatsApp na mingineyo kuna sauti iliyorekodiwa (audio) na picha za video (Video Clip) zikimuonyesha Askofu Gwajima akimkashfu na kumtukana kwa maneno makali Kaldinari Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine".

Baada ya tukio hilo juhudi mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika hali ya kawaida ili kumpata Askofu Gwajima bila mafanikio na hivyo yeye mwenyewe sasa anatakiwa aende akaripoti haraka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam bila kukosa.

Ni muhimu sana kwa Askofu Josephat Gwajima kuripoti yeye mwenyewe badala ya Kutafutwa au kukamatwa ili ajibu tuhuma hizo kutokana na nafasi yake katika jamii.

Jalada la uchunguzi limefunguliwa na upelelezi wa shauri hili unaendelea ili sheria ichukue mkondo wake.

Imetolewa na: 
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO

0
0

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa nje ya maduka yao mara baada ya kuamua kuyafunga kwa kile wanaochodai kufanya mgomo kwa lengo la kumuunga mkono Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Johnson Minja ambaye kesi yake inasikilizwa mkoani Dodoma.


Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa baadhi ya maduka yaliyoko Double road.


Maduka yaliyopo katika jengo la Halmashauri ya manispaa ya Moshi lenye ghorofa mbili pia hali ilikuwa hivi.


Pilika pilika zilizozoeleka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi hazikuonekana katika kituo hicho,kufuatia mgomo wa wafanyabiashara wa maduka kutofungua kwa kile kinachodaiwa kuungana kwa wafanyabiashara hao katika mgomo.




NCHI ZA UKANDA WA KATI WA UCHUKUZI ZASHAURIWA KUCHUKUA NIDHAMU YA UTEKELEZAJI YA BRN

0
0
Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN),  Omari Issa amewashauri Wakuu wa Nchi za Ukanda wa Kati wa Uchukuzi kuwa mifumo ya ufuatiliaji na utekelezaji itakayoharakisha ukamilishaji wa miradi iliyoko katika nchi zao.

Alisisitiza kuwa bila kuwa na mifumo ya ufuatiliaji, baadhi ya nchi zinaweza kumaliza kwa wakati miradi yake; huku nchi nyingine zikichelewa kukamilisha miradi iliyo upande wake. Hali hii inaweza kuzivunja moyo nchi ambazo zitakuwa zimekamilisha miradi yake, hasa ikizingatiwa kwamba miradi yote ya Uchukuzi ya Nchi za Ukanda wa Kati inategemeana.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa Majadiliano ya Wakuu wa Nchi za Mpango wa Uharakishaji wa Ujenzi wa Miundombinu katika Ukanda wa Kati, Bw. Issa alisema Tanzania imetekeleza miradi mbalimbali katika mwaka wa kwanza wa BRN kuliko ilivyotarajiwa kwa kutumia bajeti kidogo kutokana na nidhamu ya utekelezaji chini ya mfumo huo wa BRN, unaosisitizia katika kuweka vipaumbele, ufuatiliaji madhubuti na utatuzi wa changamoto. Nidhamu hiyo imesaidia kutatua changamoto zilizokuwa na zinazooendelea kujitokeza; na kuifanya Tanzania iweze kutekeleza kwa ufanisi miradi yake ya kipaumbele ikiwemo ile iliyo katika sekta ya uchukuzi.

KAYMU YAFUNGUA KITUO UUZAJI WA BIDHAA KWA NJIA YA MTANDAO

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kampuni ya Kaymu imefungua tawi lake Kariakoo kwa ajili ya wafanyabiashara na wanunuzi kwa njia ya mtandao pamoja na uhifadhi wa bidhaa kabla hazijasafirishwa kwenda maeneo husika, hali ambayo itasaidia kuwapunguzia usumbufu wauzaji waliokubaliana na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja wa Kaymu Tanzania, Erfaan Mojgani amesema kufungua huduma kwa njia ya mtandao ni kurahisisha uendeshaji biashara pamoja na kuondoa usumbufu kwa mteja wa bidhaa husika.

Amesema kampuni ya Kaymu inaendesha huduma kwa njia mtandao katika nchi 17 za Afrika ambapo wafanyabiashara wanajisajili katika kampuni hiyo kwa ajili ya kufanya biashara kwa njia ya mtandao kwa wateja kuchagua na kufanya manunuzi kwa bei ambayo kila mtanzania anaweza kumudu.

Kwa upande wa Mfanyabiashara wa Viatu katika Maduka ya kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) amesema amekuwa na mafanikio katika kupata bidhaa kupitia Kaymu.

“Tumefurahishwa sana na hatua ya Kaymu kufungua kituo chake hapa Kariakoo,kwani italeta mafanikio kwa wafanyabiashara kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano”alisema Lucas.
Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan Mojgani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu ya upatikanaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya Mtandao kwa wanunuzi na wafanyabiashara katika masoko yaliyopo katika mtandao wa kaymu. 
Mfanyabiashara wa Viatu katika Maduka ya Kariakoo,Zacharia Lucas (Cha Classic) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Dar es Salaam (hawapo pichani) juu ya  faida ya kuuza bidhaa zake katika mtandao wa Kaymu.Katikati ni Meneja wa Kampuni Kaymu nchini,Erfaan Mojgani pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji wa Kampuni Kaymu,Ulumbi Bryceson. 

ECASSA YAIKUTANISHA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA KATI

0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akitoa mada katika warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii ya Africa Mashariki na Kati (ECASSA)  inayoendelea nchini Mauritius.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF Tanzania, Abubakar Rajab, akimkabidhi zawadi  Mh. Fazila Jeewa waziri wa masuala ya hifadhi ya jamii nchini Mauritius mara baada ya waziri huyo kufungua rasmi warsha juu ya uendeshaji wa bodi za mifuko ya hifadhi ya jamii iliyoandaliwa na taasisi ya hifadhi ya jamii ya Africa mashariki na kati (ECASSA)  inayoendelea huko nchini Mauritius.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

CHUO CHA CBE KUANZA KUTOA SHAHADA YA ELIMU KATIKA MASUALA YA BIASHARA

0
0
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Prof. Emanuel Mjema akizungumza wakati wa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari waliokutana kupitia Mtaala wa kufundishia mafunzo ya taaluma ya Ualimu katika Biashara leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mafunzo ya awali wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Esther Mbise akitoa ufafanuzi kwa wadau wa Elimu kuhusu uandaaji wa mtaala wa kufundishia walimu wa masomo ya Biashara leo jijini Dar es salaam.
Menejimenti na watendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa wadau na wataalam wa elimu kutoka Taasisi za Elimu, vyuo, walimu wa masomo ya Biashara wa shule za Sekondari na vyuo na wadau mbalimbali wa Elimu leo jijini Dar es salaam.

KUTOKA BUNGE MJINI DODOMA LEO

0
0
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge)Mhe.Jenista Mhagama akisoma Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania kwa mara ya pili katika Bunge,Mjini Dodoma.
Mhe.Lediana Mng’ong’o Viti Maalum CCM akitoa maoni yake katika kipindi cha uchangia wa mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania,ndani ya Bunge Mjini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mhe. Edward Lowassa (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mhe. Muhammed Seif Khatib ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge.

Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images