Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 781 | 782 | (Page 783) | 784 | 785 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Bondia wa zamani wa uzito juu Duniani,Francois Botha (kulia) akiwa na Mtangazaji machachari wa Michezo hapa nchini kupitia Kituo cha Redio EFM,Maulid Baraka Kitenge mara baada ya kufanya nae Mahojino katika kipindi cha Sports Headquartes mapema leo asubuhi.Botha yupo jijini Dar tayari kushuhudia pambano la Kimataifa la Masumbwi la Mtanzania Mohamed Matumla na Mchina Wang Xin Hua ambao litakalopigwa katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Ijumaa Machi 27,2015. 


  0 0

  Afisa Habari Mwandamizi wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu(AfCPHR)Sukhdev Chatbar(kulia)akizungumza na Waendesha Mashtaka kutoka Darfur nchini Sudan waliotembelea Mahakama hiyo kujifunza namna inavyotekeleza wajibu wake.
  Msajili wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu,AfCHPR)Dk Robert Enno(kushoto)akimsikiliza Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Jimbo la Darfur,Sudan,Yassir Ahmed Mohammed.
  Msajili wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu,AfCHPR)Dk Robert Enno(kushoto)akinzungumza na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Jimbo la Darfur,Sudan,Yassir Ahmed Mohammed na ujumbe wake.


  0 0
 • 03/25/15--02:48: In the loving memory
 • In the loving memory of our dearest father Late Dr Ole Loisiligaki Ole Lengine

  Today 28th March 2015 marks one year since your soul departed. You were a dad who was so special; and who was loved very much and brought so much happiness to the many hearts you have touched.

  ‘’Work hard and always work as team” That was your favourite quote; and we promise to live with it.

  You were always kind and caring, life has never be the same since you have been gone.

  As we commemorate you one year since you have gone we have joined our hands and sing your favorite song ‘’Mahali ni pazuri’’

  You are remembered by your lovey wife Mrs Endesh Ole,your mother Elizabeth ,your daughter Esther,your sons Peter, Emmanuel, and Martin, your in-laws, relatives, friends and the whole team of EKENYWA HOSPITAL.

   "I am the resurrection and the life. The one who believes in me will live, even though they die” JOHN 11:25.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwajua watu waliohusika kuchoma moto ofisi za chama hicho jimbo la Dimani na baadaye wafikishwe mbele ya mkono wa sheria.

  Maalim Seif amesema hayo wakati alipotembelea ofisi hizo zilizoteketezwa kabisa kwa moto, tukio lililofanywa na watu wasiojuilikana juzi usiku, huko katika eneo la Kisauni Wilaya ya Magharibi Unguja.

  Katibu Mkuu wa CUF amesema tukio hilo ni la kusikitisha lililolengwa kuchafua hali ya amani na utulivu iliyopo Zanzibar, baada ya kufikiwa maridhiano ya kisiasa yaliyosababisha wananchi kuishi kwa amani.

  “Polisi hili ni tukio bay asana na hili sio la kwanza, kama mtawaachia watu hawa waendelee kufanya haya wataipeleka nchi hii pabaya”, amesema Maalim Seif alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea eneo hilo.

  Aliwataka Polisi katika kufanya kazi yao kwa weledi na wasiingize mitazamo ya kisiasa hata kama kitendo hicho kimefanyiwa CUF, bali walichukulie ni tukio la kihalifu lililopangwa linalohitaji kufanyiwa kazi kwa kina.

  Aidha, aliwataka wananchi hasa wanachama na wafuasi wa CUF wawe watulivu na wala wasilipike kisasi kwa sababu kitendo cha kulipa kisasi kitawafanya nao wanachangia vitendo vya kihalifu.
  “Tunawaomba wanachama wa CUF wawe watulivu katika kipindi hichi na kamwe wasichokozeke kulipiza kisasi, wakifanya hivyo nao watakuwa wanachangia matukio ya kihalifu”, alionya Katibu Mkuu wa CUF, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais.

  Amesema matukio ya kuchomeana moto ofisi na kushushwa bendera za vyama yameshapitwa na wakati Zanzibar yalijitokeza katika miaka ya 1990 hadi 2005 na yalikomeshwa baada ya maridhiano ya kisiasa, hivyo hayapaswi tena kukaribishwa Zanzibar.

  Katika hatua nyengine, Maalim Seif ameitaka Kamati Tendaji ya chama hicho ibuni njia za kulijenga haraka jengo hilo la ofisi ya jimbo la Dimani katika eneo hilo hilo, ili iweze kutumiwa na wanachama wa eneo hilo.

  Mapema akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa CUF, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Salum Bimani alisema mashuhuda wa tukio hilo walisema watu wasiojuilikana walifika katika ofisi hizo majira ya saa nane usiku wakiwa na gari  na waliposhuka waliingiza matairi ya gari ndani ya ofisi na baadaye kuilipua.

  Bimani alimweza Maalim Seif kuwa kiasi cha shilingi milioni 135 zimepotea kufuatia hujuma hiyo.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuangalia ofisi ya (CUF) jimbo la Dimani iliyochomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuni.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitembelea Ofisi ya (CUF) jimbo la Dimani kuangalia uharibifu uliofanywa baada ya ofisi hiyo kuchomwa moto na watu wasiojulikana hivi karibuni. (picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua (kushoto), akikabidhi bendera ya taifa kwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati), ni Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga.
  Meneja Masoko wa Airtel, Anet Muga. akiongea wakati wa tukio la kumuaga na kumkabithi bendera ya taifa kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha nchi katika fainali za Afrika za Airtel Trace Music Stars zitakazofanyika Jumamosi Machi 28, nchini Kenya na kushirikisha nchi 13, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi za BASATA jijini Dar es Salaam jana. pichani katikati ni Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Nsao Shalua akifatiwa na mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi.
  mshindi wa Airtel Trace Music Stars, Mayunga Nalimi akiwa ameshika bendera mara baada ya kukabithiwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Sanaa na Masoko wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya muziki ya Airtel Trace Music Stars yatakayofanyika Jumamosi hii nchini Kenya.

  Barasa la Sanaa Tanzania leo limemkabithi bendera mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Bwana Nalimi Mayunga anayeondoka leo nchi kwenda kuhudhuria mashindano ya Airtel Trace Afrika yatakayoshirikisha washiriki toka nchi 13 barani Afrika yanayofanyika nchini Kenya siku ya Jumamosi tarehe 28 March 2015.

  Mayunga aliibuka mshindi katika kinyanganyiro cha kusaka Wakali wa vipaji vya mziki kupitia shindano la Airtel Trace Music lililozinduliwa na kampuni ya Airtel Tanzania Mwaka Jana mwezi wa kumi na kushirikiksha washiriki mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali nchini ambapo fainali ya kumsaka mshindi ilifanyika mwanzoni mwa mwezi wa februari na kumwezesha Mayunga kuwashinda washindani wengine watano na katika fainali hizo na kuondoka na kitita zawadi ya shilingi million 50.


  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wanatarajiwa kuwasha moto  ndani ya ukumbi mpya wa kisasa  ujulikanao kwa jina la Flomena uliopo  wilayani hai mkoani Kilimanjaro usiku wa jumatatu ya pasaka .


  Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo  Swaum kileo alisema kuwa ameamua kuwaleta bendi hiyo katika uzinduzi huo ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa mkoa wa kilimanjaro na mikoa jirani katika sikukuu hiii ya pasaka.
  Alisema kuwa  bendi hii inamda mrefu sana aijafika wilayani hai ivyo wameamu kuileta ili wakazi wa wilaya hiyo nao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo.


  Alitaja kiingilio cha onyesho hiyo kuwa ni shilingi 10000 za kitanzania huku akiwataja wathamini wa onyesho hilo kuwa ni Swaum fashion ,Tbl , libeneke la kaskazini blog pamoja , faraja saloon  pamoja na Radio five.

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisaini Kitabu cha Maombolezo katika Ubalozi wa Singapore Ubelgiji. Singapore imempoteza Mhe. Lee Kuan Yew aliyewahi kuwa Kiongozi wa Singapore na ambaye aliwezesha nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi tajiri Diniani.

  0 0

  Na. Johary Kachwamba-MAELEZO, DODOMA

  SERIKALI imeweza kushawishi mashirika ya kimataifa ya ndege kuongeza idadi ya safari pamoja na kiwango cha mzigo kinachosafirishwa kutoka Tanzania kwenda nje ya nchi, ikiwemo bidhaa za matunda.

  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene alibainisha hayo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Muhammad Sanya, Mbunge wa Mji Mkongwe aliyehoji mpango wa Serikali katika kutafuta soko la matunda nje ya nchi.

  Mhe. Mbene alisema TanTrade kwa kushirikiana na Chama cha Wazalishaji Maembe (AMAGRO) inaratibu mpango wa kutoa mafunzo ya uzalishaji bora, ufungashaji na kujenga kituo cha kuchambua na kupanga ubora wa maembe ili kuuzwa kwenye soko la kimataifa.

  Aidha kampuni ya AMAGRO inaendelea kuhamasisha kilimo cha maembe aina ya tommy na alphonso ili kuuza soko la nje.

  “mkoani Tanga tumeanzisha program ya Muunganisho wa Ujasiriamali Vijijini (MUVI) katika vijiji 9 ili kuzalisha machungwa yasiyo mbegu kwa matumizi ya ndani na soko la nje ” alisema Mhe. Mbene

  Tayari kampuni ya Africado inayozalisha maparachichi Wilayani Hai na Kampuni ya Rungwe Avocado  ambapo yote yanawakilisha wakulima wadogo, yanazalisha na kuuza maparachichi soko la nje ya nchi.

  Aidha Mhe. Mbene alisema Serikali imeanzisha kampuni ya GS1 Tanzania inayoratibu mfumo wa ufuatiliaji wa mnyororo wa bidhaa ambao ni msingi mkubwa katika kupata soko la bidhaa yoyote nje ya nchi.

  “Serikali inaendelea kutangaza bidhaa za Tanzania kupitia maonesho ya Biashara ya ndani, kikanda na kimataifa” aliongezea Mhe. Mbene

  Mkakati wa Mauzo ya Nje (National Export Strategy) wa Mwaka 2009 ulibainisha mikakati ya kuongeza mauzo ya matunda, maua na mbogamboga. Kutokana na hali hii thamani ya mauzo ya matunda nje imeongezeka kutoka Dola za kimarekani 7,440,290 mwaka 2010 hadi Dola za kimarekani 32,116,895.22 mwaka 2013.

  0 0


  • Education and training opportunities in Mozambique and Tanzania

  With some of the largest offshore gas fields in the world, no local supply chain and an immediate and significant demand for skilled workers, East Africa can benefit from the expertise of the UK’s oil and gas sector.

  Twelve UK organisations – from business and academia – with an interest in the oil and gas sector, headed to Mozambique on 18 March and arrive in Tanzania on 24th and partnerships in these exciting new pioneering markets.

  Led by Scottish Development International (SDI) and supported by UK Trade and Investment (UKTI) and Aberdeen City Council, the mission follows a visit last year to Aberdeen by President Kikwete who saw UK expertise in the oil and gas sector at first hand.

  Participating in the mission will be the University of Aberdeen, who in partnership with the University of Dar es Salaam have been awarded €2 million by the European Union to help develop higher education in Tanzania and create a sustainable oil and gas sector in the East African country.

  The money will be used to fund a three-year project that will promote learning, research and knowledge-sharing between the Universities in conjunction with the Aberdeen Institute of Energy (AIE), and academics and students at UDSM. Stakeholders from the public and private sector will also benefit from this arrangement.

  Operators in Tanzania are expected to invest billions in an onshore Liquified Natural Gas plant that will provide jobs and export earnings. This means that as well as capacity building, operators will substantially invest in education and training - around 25,000 people will require training at a technical and vocational level as well as higher education in the East African region.

  The global reputation of the UK’s Oil & Gas education and training providers means the UK is well placed to support Tanzania to develop its local capacity and skills to manage its own resources. As such, five of the 12 organisations on the mission are education and training companies from the university, college and private sector.

  March to explore opportunities The mission also complements the newly announced UK investment of £25 million into the joint UK and German government ‘Skills for Oil and Gas Africa’ (SOGA) initiative, which is also supported by BG Group, and aims to upskill local workers to give them an opportunity to benefit from jobs in and around the industry in Tanzania and the region.

  The British High Commissioner to Tanzania, HE Dianna Melrose, said: “"The UK has a global reputation for Oil & Gas skills development. UK training providers can help ensure Tanzanians benefit from new work opportunities created by gas development."
  From left Richard Boulter (DFID), Ms Dianna Melrose-British High Commissioner, Mr.Bikash Dawahoo-Prosperity Officer and Representative from TCCIA.

  0 0

  Meneja Mauzo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa ukanda wa Temeke, Patrick Swai akizungumza na waandishi wa habari (hawapi pichani)wakati akizitangaza bar tano zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano la uchomaji nyama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”,kwa mkoa wa Dar es salaam.

  0 0

  Kumbukizi maalum ya tarehe 20 Machi 2015 ya wanafunzi watano wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani imetukumbusha msiba mkubwa wa watu 50 katika ajali moja ya basi na lori ya tarehe 11 Machi 2015.

  Wakati tukiendelea kuwaombea marehemu na majeruhi na kutoa pole kwa wafiwa na wahanga wakati umefika sasa tutangaze #AjaliBarabaraniJangalaTaifa tuwajibike kuzipunguza.

  Kumbukizi katika ukumbi wa Nkurumah ilihusisha ibada, nyimbo maalum na kusomwa kwa wasifu wa wanafunzi walioaga dunia wakiwa wadogo familia zao na taifa likiwahitaji na hatimaye salamu kutoka makundi mbalimbali.

  Niliguswa na salamu za Chuo cha Fani za Jamii zilizosomwa na Mkuu wa Chuo cha Fani za Jamii aliyeeleza kwamba mabasi sasa yanaua kuliko magonjwa mengi.

  Alipendekeza utafiti ufanyike UDSM kuchangia kupunguza hali hiyo kwa kuzingatia kwamba Chuo Kikuu hicho kina fani mbalimbali (multi disciplinary).

  Alieleza kwamba kwa upande wa uhandisi waangalie iwapo teknolojia ya mabasi yenye spidi inawiana na barabara zetu kuu ambazo nyingi ni za njia moja. Huku fani ya jamii iangalie masuala ya maadili kufanya madereva wa mabasi kujifunza kwamba wanabeba binadamu sio wanyama.


  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard K. Membe (Mb) akimpokea Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Rais Museveni yupo nchini kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Ukanda wa Kati kuhusu Uwekezaji na Viwanda unaofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuanzia tarehe 25 hadi 26 Machi, 2015.
  Rais Museveni akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe akimpokea Rais wa Burundi Mhe.Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimatafa wa Mwalimu Julius Njerere.
  Rais Nkurunziza akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Balkis Mvungi kama ishara ya kumkaribisha nchini Tanzania.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Ltd Bw.Brian Thomson leo alipokuwa akiangalia ramani ya ujenzi wa Barabara za Kiashange -Kijini-Mbuyutende na Matemwe-Muyuni Mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa na Kampuni hiyo ambayo inasimamia mradi wa (Amber Golf&Beach Resort).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia ramani ya ujenzi wa Barabara za Kiashange -Kijini-Mbuyutende na Matemwe-Muyuni Mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa na Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Ltd ambayo inasimamia mradi wa (Amber Golf&Beach Resort) wakati alipotembelea ujenzi wa barabara leo (wa tatu kushoto) Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Ltd Bw.Brian Thomson na (wapili kulia) Bi Naila Jidawi msemaji Mkuu wa Kampuni hiyo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Wananchi wakati alipotembelea ujenzi wa Barabara za Kiashange -Kijini-Mbuyutende na Matemwe-Muyuni Mkoa wa Kaskazini Unguja inayojengwa na Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Ltd, ambayo inasimamia mradi wa Amber Golf&Beach Resort.


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifunga Mkutano wa Taasisi ya Research on Poverty Alleviation in Tanzania (REPOA) kwenye hoteli ya BahariBeach Jijini Dar es salaam Machi 25, 2015.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama machapisho mbalimbali kuhusu uwekeza wa gesi wakati alipotembelea banda la British Gas (BG) baada ya kufungau mkutano wa Taasisi ya Utafiti wa Kuondoa Umaskini (REPOA) kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es slaam Machi 25, 2015. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa REPOA, Profesa Samuel Wangwe, wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya REPOA, Profesa Meja Jenerali Mstaafu, Yodon Kohi na kulia ni Adam Prince kutoka Bkampuni ya British Gas. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Benki ya NMB imeendela kuwapiga msasa wateja wake wa mtandao wa NMB Business Club Wilaya ya Ilala kwa kuwapa mafunzo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara zao, fedha za kigeni, bidhaa na huduma zitolewazo na benki ili kuwawezesha kuendelea kuwa vinara wa biashara.

  Katika semina hiyo iliyowakutanisha wajasiriamali zaidi ya 300, iliwapa fursa vilevile wanachama wake kubadilishana mawazo na wenzao hasa katika ulimwengu wa biashara.
  Kaimu mwenyekiti wa NMB Business Club Wilaya la Ilala-Dar es Salaam Bw. Chatele Eliakimu Sando akielezea jinsi wana NMB Business Club Wilaya ya Ilala walivyonufaika na klabu hiyo tangu kuanzishwa kwake na wanavyoendelea kufurahia huduma na bidhaa kutoka benki ya NMBAkitoa shukurani kwa niaba ya wanachama wake kwa uongozi wa benki ya NMB kwa kuandaa semina ambazo zinatoa mafunzo yanayowajenga wanachama wa NMB Business Club.
  Afisa Bidhaa wa NMB-Chacha Borondo akielezea kuhusu bidhaa na huduma zitolewazo na NMB
  Sehemu ya wanachama hao wakibadilishana mawazo.
  Mhazini wa NMB Kanda ya Dar es Salaam kitengo cha Hazina, Joseph Funuguru akitoa mafunzo juu ya fedha za kigeni kwa wateja wa NMB walio katika mtandao wa NMB Business Club katika semina hiyo.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Afrika Kusini.

  MWENYEKITI mpya wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau, ameongoza wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara nchini ya Afrika Kusini.

  Wakiwa nchini humo walitembelea Bandari ya Durban, ambapo walifanya mazungumzo na viongozi wa juu wa bandari hiyo wakiongozwa na Meneja wake Vusi Khumalo.

  Mwidau ambaye ameambatana na wajumbe kadhaa wa PAC akiwemo Makamu Mwenyekiti Deo Filikunjombe, Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage pamoja na Mbunge wa Mbinga Mashariki, Gaudence Kayombo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau akiwa na Meneja wa Bandari Durban nchini Afrika Kusini, Vusi Khumalo wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kikazi nchini humo, Machi 24 na 25 mwaka huu.
  Mwidau akiwa na wajumbe wa PAC, Ismail Rage pamoja na Gaudence Kayombo wakipata maelezo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa SIR SERETSE KHAMA Nchini Botswana kwa ajili ya kuhudhuria kwenye kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal, akiwa na ujumbe wa Tanzania kwenye kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana. kulia Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Ghariba Bilal kulia, Rais wa Botswana Mhe. Seretse Khama katikati na Rais wa Gabon Mhe. Ali Bongo Ondimba wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kongamano la Kimataifa kwa Viongozi wakuu wa Nchi, kuhusu biashara haramu ya wanyamapori Duniani. Kongamano hilo limefanyika leo March 25,2015 kwenye Hoteli ya Mowana iliyopo katika mbuga ya wanyama Kasane Nchini Botswana.


  0 0

  East African Community Headquarters, Kampala, Uganda, 25 March 2015: Uganda’s Vice President His Excellency Edward Ssekandi this morning represented HE Yoweri Kaguta Museveni at the official opening of the 5th Annual East African Health and Scientific Conference and International Health Exhibition and Trade Fair at the Kampala Serena Hotel in Uganda.

  In a statement read by his Vice, President Museveni commended the EAC Secretariat and the Partner States for initiating the process of establishing Regional Centers of Excellence (CoEs) in the Health sector namely Nephrology and Urology in the Republic Kenya, Oncology in the Republic of Uganda, Cardiovascular in the United Republic of Tanzania and Biomedical Engineering and eHealth in the Republic of Rwanda.
  Uganda’s Vice President His Excellency Edward Ssekandi addresses the participants at the Conference.
  He said this initiative will enhance EAC Competitiveness through highly skilled health workforce in biomedical sciences and also enable the East African citizens access quality and specialized services within the region.

  The first phase of the project is expected to cost USD 72.75 million and will be supported by the African Development Bank.  The CoEs are expected to deliver high quality and skilled personnel in the specialized fields and reduce medical tourism, which costs EAC Governments an estimated of USD 150 million annually for treatment of Non-Communicable Diseases abroad.

  At the same occasion, the Deputy Secretary General of the East African Community in charge of the Productive and Social Sectors Hon. Jesca Eriyo, who represented the Secretary General Amb. Dr. Richard Sezibera, informed the delegates that there was strong evidence that an investment in people’s health was a key asset for society and for the economy as a whole.

  Deputy Secretary General of the East African Community Hon. Jesca Eriyo make her remarks during the Conference.
  “As you may be aware, the Health sector is also leading in creating Job opportunities and a driver of innovation and technology” noted Hon. Eriyo, adding that “As such, health systems strengthening have an important role in achieving Millennium Development Goals to ensure sustainable and inclusive growth in the Health Sector and Economy at Large.


  0 0

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete delivers his keynote address during the opening session of the Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning. Third left seated is President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda, fourth left is Burundi’s President Pierre Nkurunzinza, and second left is DRC’s Minister for Transport Justin Kaumba Mwana Ngongo.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete speaks with President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda(left) and President Pierre Nkurunzinza of Burundi shortly before the commencement Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning.

  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete welcomes President Yoweri Kaguta Museveni of Uganda and Pierre Nkurunzinza of Burundi for the Central Corridor Presidential Round Table and High Level Industry and investor Forum held at Julius Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam this morning.(photos by Freddy Maro).

  0 0

   Simon Msuva (kushoto) akimkumbatia Mrisho Ngasa huku Danny Mrwanda. Kulia ni Danny Mrwanda baada ya kuifungia kimu yake bao la tatu ambapo Yanga ilishinda 3-1. (Picha zote na Francis Dande)
   Mshambuliaji wa Yanga, Danny Mrwanda akichuana na Damas Makwaya wa JKT Ruvu (kushoto), katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa leo.
  Msuva akimtoka beki wa JKT Ruvu, Mohamed Faki akiambaa na mpira.
   Mrisho Ngasa (kushoto) akichuana na Mohamed Faki.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 781 | 782 | (Page 783) | 784 | 785 | .... | 3284 | newer