Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 775 | 776 | (Page 777) | 778 | 779 | .... | 3283 | newer

  0 0


  Chaka Khan - Ain't Nobody

  0 0

   Akina mama wakiusimamisha msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ili waeleza tatizo la kutopatikana maji tangu wazaliwe katika Kijiji cha Shimbumbu, Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na akina mama waliobeba ndoo tupu ikiwa ni ishara ya kuelezea tatizo la maji linalowakabili wakazi wa Kijiji cha Shimbumbu  Jimbo la Arumeru Mashariki,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

  Wakazi wa eneo hilo wamedai kuwa wamekuwa na tatizo hilo la maji tangu wazaliwe kiasi cha kuwafanya walazimike kubadilishana maji na kokoto zinazotokana na kuuvunja mlima wa mawe uliopo kijijini hapo.

  Komredi Kinana ambaye katika ziara yake ameambatana na Katibu wa Itikadiu na Uenezi, Nape Nnauye, amewaahidi wananchi wa eneo hilo kuwasaidia kukamilisha mradi wa maji utakaogharamiwa na Serikali ili mlima huo unusurike. Eneo hilo kwa hivi sasa linaoongozwa na Mbunge Joshua Nassari wa Chadema.
   Akina mama wakiwa na ndoo wakati wa mkutano na Komredi Kinana karibu na mlima unaopasuliwa mawe kupata kokoto za kubadilishana maji.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbuguni,jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha.
   Komredi Kinana akihutubia katika mkutano uliofanyika Kata ya Mbuguni, alikozaliwa yeye.
   Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Mbuguni, alikozaliwa yeye.

  PICHA NA MICHUZI JR-ARUMERU MASHARIKI


  0 0  0 0

  Tokyo,Japan. Mwanamuziki mahili wa muziki wa dansi Ally Choki ambaye pia ni kiongozi wa bendi ya Extra Bongo aka "Wazee wa Kizigo" anatarajiwa kutingisha jukwaa siku ya Jumamosi Machi 21,2015 ambapo wanamuziki wa Eagle's Vission watakuwepo kumsindikiza Ally Choki anayefuatana na Super Nyamwela.

  Katika onyesho hilo wakongwe wawili wa muziki wa dansi watanzania wanaoishi Japan,Fresh Jumbe Mkuu na Abbu Omary watakuwepo jukwaani kuwapa baraka zote wadogo zao Ally Choki na Super Nyamwela katika ukumbi wa Sehemu inaitwa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City pembeni kiduchu ya Jiji la Tokyo.

  Madhumuni ya ziara ya Ally Choki na Super Nyamwela ni kuangalia ushirikiano na uwezekano wa soko la muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" ili muziki huo uweze kushika kasi kubwa na soko Japan na mashariki ya mbali kwa ujumla,Pia uwezekano wa bendi ya Extra Bongo kufanya ziara za kimataifa. Wadau msikose kujitokeza kwa wingi katika Onyesho hili waswahili usema 'Chereko Chereko na mwenye mwana"
  Fresh Jumbe akifanya yake katika moja ya shoo zake huko Japan.


  0 0  0 0  0 0

  This weekend provides SuperSport’s football fans with the chance to enjoy two of the biggest rivalries in world football that could also have a huge impact on the fortunes of the clubs involved.

  Liverpool host Manchester United at Anfield on Sunday having gone unbeaten in the Premier League for three months since their visit to the Theatre of Dreams last December turned into a nightmare 3-0 loss.

  Hours later, the latest chapter in the story of Spain’s El Clasico will be written when Real Madrid travel to Barcelona having slipped behind their great rivals in the La Liga title race in recent weeks.

  Liverpool-Manchester United will be broadcast on SuperSport 3 at 15:30 EAT and Barcelona-Real Madrid will air on SuperSport 3 at 22:40 EAT.

  There will be no love lost on Merseyside, with these two great foes going head-to-head for a place in the Uefa Champions League next season. United occupy that fourth and final qualification spot, two points ahead of Brendan Rodgers’ side.

  And former Evertonian Wayne Rooney will be eager to land another knockout blow against Liverpool and continue his rich vein of form that has seen him score four goals in his last four appearances.

  Real Madrid look to have the momentum in the La Liga title race but have faltered in the last few weeks to allow Barca to grab a one-point lead in the championship.

  If they extend that to four it would be a big step towards lifting the trophy with a few months left of the campaign.

  And no modern day El Clasico would be complete without the mouth-watering prospect of a head-to-head battle between Lionel Messi and Cristiano Ronaldo.

  One thing we should expect is goals – both sides have scored at least once in this fixture in the last 17 meetings.

  More sport news at: www.supersport.com
  Twitter.com/SuperSportTV

  0 0

  Mchungaji wa mifugo akinywesha maji mifugo yake kwenye eneo lenye maji ambalo Waizri Prof. Maghembe amepiga marufuku kunywesha kwenye eneo hilo.

  Na Hussein Makame-MAELEZO, Musoma

  WAZIRI wa Maji Profesa Jumanne Maghembe amewaonya wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji kwamba kufanya hivyo kunahatarisha uhai wa vyanzo hivyo.

  Ametoa onyo hilo kwa nyakati tofauti wakati akiwa kwenye shughuli za kuweka mawe ya msingi kwenye miradi ya maji kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya ya Serengeti mkoani Mara ambako Maadhimisho ya Wiki ya Maji kitaifa yanafanyika. 

   Akiwa katika kijiji cha Rung’abure, Waziri alishuhudia baadhi ya wafugaji wakinywesha mifugo yao kwenye maeneo ya vyanzo vya maji huku baadhi wakilima karibu na chanzo cha maji.


  0 0

  Design of TAZARA Flyover
  CONSTRUCTION of TAZARA flyover is expected to start in May, this year, following recent signing of a deal with the government of Japan to access a grant of over 26.3bn/- for the project.

  This was said in the National Assembly on Wednesday by the Minister for Works, Dr John Magufuli, when responding to a supplementary question by Ms Rita Mlaki (Special Seats - CCM), who sought to know the government’s resolve to decongest Dar es Salaam city.

  “Last week, the government signed an Exchange of Notes with the government of Japan to access a grant of over 26.3bn/- for the improvement of the third phase of the TAZARA intersection,” he said, adding that the additional grant brings total amount for the project to 76bn/-.

  Dr Magufuli said that the funds under the Exchange of Notes and related grant agreement will serve as additional support for successful construction of the TAZARA flyover, after the 5.64bn/- that was secured in July 2014 and 52.55bn/- in June 2013.

  He said that the funds will enable the Japanese government make available the funds for procurement of goods and services for the implementation of the project.

  Magufuli insisted that this assistance will contribute much to the improvement of road infrastructure necessary in reducing congestion, especially during peak hours.

  The specific aim of the project, Magufuli said, is to improve road transport sector in Dar es Salaam and that the project intends to reduce transportation costs within and outside the city.

  He further said that the government was committed to construct ring roads in the city and another flyover will soon be built at the Ubungo junction.

  Earlier in her basic question, Ms Mariam Nassoro Kisangi (Special Seats - CCM), demanded to know the government resolve to develop ambitious Kigamboni City project.

  She also wanted to know if the government was ready to build a modern airport that will complement a new city. Responding, Deputy Minister for Transport, Dr Charles Tizeba, reiterated the government’s commitment to develop Kigamboni City, under the Kigamboni City Development Authority.

  However, he said Kigamboni City was within Dar es Salaam city, which is served by Julius Nyerere International Airport (JNIA).

  Dr Tizeba said JNIA is capable of handling 30 aircraft per hour after the completion of the second phase of expansion and renovation of infrastructure at the airport, which was carried out between 2008 to 2011. However, Dr Tizeba said JNIA is currently handling only eight aircrafts per hour which is below its capacity.

  0 0

  11072283_933753296658934_392071823375109477_n
  ..burudani kutolewa na Baby J, Coconut na Zanzibar One Modern taarab
  Na Andrew Chale
  Machi 22 mwaka huu Kisiwa cha Unguja, Zanzibar kinatarajiwa kuwa na tukio moja kubwa litakalowakutanisha Wanawake mbalimbali na kusheherekea siku ya Mwanamke Dunia, ndani ya ukumbi wa Bwawani Hoteli.

  Katika tukio hilo, linatarajiwa kuwa pia na shamra shamra ikiwemo za mitindo ya mavazi kutoka kwa gwiji wa mitindo Nchini, Mama Asia Idarous Khamsin atakaye onesha mavazi mbalimbali siku hiyo akiwa sambamba na Mbunifu wa mavazi wa Zanzibar, Matilda Revelian wa Matty Designs.
  Sherehe hizo zimeandaliwa na kikundi cha akina mama cha Zanzibalicious Women Group, chenye maendeleo makubwa kwa sasa hapa nchini.
  IMG_9704
  Usiku huo utapambwa na burudani mbalimbali akiwemo mwanamuziki Baby J. Wengine ni bendi ya Coconut na Zanzibar One Modern taarab.

  Aidha, Asia Idarous Khamisin amekisifia kikundi kilichoandaa halfa hiyo ya siku ya Mwanamke Duniani kwa Zanzibar, kwani ndio kwa mara ya kwanza Zanzibar wanawake na kusheherekea siku hiyo ya mwanamke duniani.
  Usiku huo kiingilio kinatarajia kuwa sh. 35,000 kwa viti vya kawaida na sh 50,000 kwa upande wa V.I.P.

  Aidha, kwa wadau wanaotaka tiketi wanaweza kutembelea katika maduka yaliyopo Mlandege Al Bashaer Tour, Magereza Ms Saloon, Michenzani Sas Saloon au kupitia mawasiliano ya simu ya namba: 0777418324, au 0777868766, 0715080399

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akipata maelezo ya mradi wa Maji Taka katika Manispaa ya Sumbawanga kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Sumbawanga (SUWASA) Ndugu Zakaria Ngunda alipofika kutembelea mradi huo tarehe 19/03/2015. Ujenzi wa mradi wa Maji Taka umeshakamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni magari matatu kwa ajili ya kuzolea taka za vyooni zitakazomwagwa katika mtambo huo  ili uanze kufanya kazi. Miradi yote mikubwa ya Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga inagharimu zaidi ya fedha za Kitanzania shilingi bilioni 30.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na Wakandarasi wanaojenga mradi Maji Safi na Maji Taka Mjini Sumbawanga ambao ni Techno Fab na Mkandarasi mshauri GKW ambapo amewataka kuongeza kasi kumaliza mradi huo ambao upo nyuma ya wakati. Amemuagiza Mkandarasi anaejenga kukamilisha ujenzi huo kwa kipindi cha miezi miwili ijayo licha ya kuomba kuongezewa muda wa miezi sita ili aweze kukamilisha kazi hiyo. 
   Mradi wa Bwawa la kuchujia Maji Taka Mjini Sumbawanga ukiwa umekamilika. 

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mh. Zitto Kabwe

  0 0

  Kamishna wa Polisi Elice Mapunda akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Katikati ni Msemaji wa Jeshi hilo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Advera Bulimba. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Polisi Diwani Athumani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akimpongeza Kamishna wa Polisi Elice Mapunda mara baada ya kula kiapo mbele yake kufuatia kupandishwa cheo na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Polisi Diwani Athumani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu baada ya kupandishwa cheo na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Naibu Kamishna wa Polisi kuwa Kamishna wa Polisi. Hafla hiyo fupi ilifanyinyika jana Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).

  Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) na maafisa wengine 14 kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP).

  Maofisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) kuwa Kamishina wa Polisi (CP) ni pamoja na Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na Diwani Athumani.

  Maofisa wengine waliopandishwa cheo kutoka Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kuwa Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) ni pamoja na Godluck Mongi, Ally Lugendo, Salum Msangi, Faustine Shilogile, Maulid Mabakila, Albert Nyamhanga, Daniel Nyambabe, Salehe Ambika, Robert Boaz na Gabriel Semiono. Pia wamo kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo, kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola, kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas na kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Maria Nzuki.

  Aidha, mhe. Rais amempandisha Juma Yusuf Msige kutoka cheo cha kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP).

  Kufuatia kupandishwa vyeo kwa maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu katika hafla fupi ya kuwaapisha makamishina hao wapya, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

  Aidha, IGP Mangu amewapongeza maofisa wote waliopandishwa vyeo na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa ili kuwa chachu ya mabadiliko katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao. IGP Mangu aliongeza kuwa, cheo ni dhamana na kuwataka kuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao na usimamizi kwa walio chini yao.

  Imetolewa na:
  Advera Bulimba -SSP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60, akimlisha keki Katibu Muhtasi wake Bi. Fatuma Ngodoki jijini Dar es Salaam leo huku watumishi wengine wakishuhudia.
  Mwanasheria katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Charles Mmbando akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60.
  Mhasibu katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Job Kiwory akimiminia kinywaji kisicho na kilevi Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara hiyo Bw. Joseph J.K. Ndunguru, ambaye anastaafu leo (Ijumaa, Machi 20, 2015) baada ya kutimiza miaka 60. Kulia ni Mwanasheria katika Wizara hiyo Bw. Charles Mmbando.
  Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria kwa Umma katika Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Joseph J.K. Ndunguru (mwenye tai) katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dar es Salaam leo (Machi 20, 2015). Bw. Ndunguru anastaafu utumishi wa umma leo baada ya kutimiza miaka 60. (Picha: Wizara ya Katiba na Sheria)

  0 0


  0 0

  Katika kile kinachooneka na ni kujipanga vyema, kampuni gwiji la mawasiliano duniani Huawei imeanza kutangaza kuja na kitu kipya na kikubwa zaidi hivi karibuni.  Tunaweza kusema huu ni mwaka wa Huawei, au tuseme huu ni msimu wa Huawei kufanya yao kwani ni mwezi huu huu wamezindua bidhaa kali na tumeanza kusikia minong’ono ya kuwa ku na mengine yanakuja.  

  Tofauti na tulivyozoea kuwa wanatangaza uzinduzi wa bidhaa ila sasa hivi wanakuja na “kishkwambi”. Hakuna ajuaye kishkwambi ni nini kwani inaweza kuwa ni bidhaa mpya au inaweza kuwa ni zawadi kwa wapenzi wake laki ni inaonekana wazi kuwa ni jambo kubwa.
  Alipoulizwa na mwandishi wa habari hii, Meneja Bidhaa wa kampuni hiyo, Joseph Lyimo alisema kuwa ‘kishkwambi’ ni habari ya mjini, maalumu kwa wapenzi wao na kuwaomba watanzania wote watembelee kurasa zao za mitandao ya kijamii kujua zaidi pia tovuti maalumu ya kishkwambi hapahttp://huawei.kishkwambi.co.tz/
  Kampuni ya Huawei yenye makao makuu yake nchini China, imekuwa mstari wa mbele kufikisha teknolojia ya kisasa kwa watu duniani kote. Kwa hapa nchini wamekuwa wakitoa simu za bei nafuu na hivyo kufanya watanzania wengi kupata teknolojia hiyo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua eneo la chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Bunda katika katika ziwa Victoria kwenye kijiji cha Nyabehu mkoani Mara ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji, Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Mbunge wa Bunda na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasira.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji wa Bunda katika kijiji cha Nyabehu mkoani Mara ,Machi 20, 2015 ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya Maji. . Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe na kushoto ni Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora. Wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephene Wasirra.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua moja kati ya mashine tisa za kusukuma maji katika mradi wa Maji wa Bunda uliopo kwenye ziwa Victoria katika kijiji cha Nyabihu wilayani Bunda ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji Machi 20, 2015. Kulia kwake ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  The former Apple CEO and founder of Obi Mobiles Mr. John Sculley discusses a point during their visit of Tanzania Investment Centre (TIC) to explore investment opportunities. This company is now eying the East African market.
  The former Apple CEO and Obi Mobiles co-founder Mr. John Sculley explains something during the visit of Tanzania Investment Centre offices today, 20 March 2015. On his left is Mrs. Diane Sculley.
  The meeting between Ministry of Communication, Science and Technology, Tanzania Investment Centre, COSTECH and the former Apple CEO and Obi Mobiles co-founder Mr. John Sculley and his delegation at Tanzania Investment Centre offices today, 20 March 2015.
  The Deputy Minister for Communication, Science and Technology, Hon. January Makamba explains something to the former Apple CEO and Obi Mobiles co-founder John Sculley (Middle) and Mrs. Diane Sculley (First Left) when they visited TIC Offices today, 20 March 2015.
  The Deputy Minister for Communication, Science and Technology, Hon. January Makamba poses with the Executive Director of Tanzania Investment Centre, Ms. Juliet Kairuki and Obi Mobiles co-founder and former Apple CEO John Sculley (Third Right). First Left is Mr. Sculley’s wife Diane Sculley.
  The former Apple CEO and Obi Mobiles co-founder Mr. John Sculley and his team leaving Tanzania Investment Centre offices after their meeting with Ministry of Communication, Science and Technology, Tanzania Investment Centre and COSTECH.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu hoja mbali mbali zilizoletwa na kamati ya soko la  Kilombero ikiwa pamoja na kupandishiwa kodi bila utaratibu maalum.Ndugu Kinana anatarajia kuhutubia kesho katika mkutano wa hadhara ndani ya uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini humo.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Arusha kwenye soko la Kilombero ambapo walisalimu wananchi waliojitokeza kwa wingi.
   Wananchi na Wafanyabiashara mbalimbali katiko soko la Kilombero wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao ikiwemo pia na kuyasikiliza matatizo mbalimbali yanawakabili katika soko hilo.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali wakila chakula kwa Mama Lishe wa soko la Kilombero,jijini Arusha,pichani kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Vijana,Mh.Catherine Magige.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakinywa kahawa mara baada ya kumaliza kuwasalimu na kuzindua shina la wakereketwa wajasiliamali Oysterbay, Unga ltd, Arusha.

  PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA.


  0 0

  Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10 kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.

  Akizunguma na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani. 

  Amesema watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.

  Matembezi hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.

  Akizungumzia Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki matembezi hayo.

  mdimu amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee kuwepo.

  "Hatulengi masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia katika familia"amesma Mdimu.

  Amesema harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'Konyagi', David Mgwassa akizungumza alipokuwa akitoa ahadi ya kampuni hiyo kuchangia shilini milioni 10 kuunga mkono Imetosha Foundation na kampeni yake ya kupinga mauaji ya watu wenye ualbino.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
  Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi 29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika "Jhikoman".
  Sehemu ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.

older | 1 | .... | 775 | 776 | (Page 777) | 778 | 779 | .... | 3283 | newer