Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI BABATI MKOANI MANYARA

0
0
1aMkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
2aWaziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
3aMratibu wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya mipaka inasababishwa na wanasiasa. 


KINANA KUHITIMISHA ZIARA YAKE JIJINI ARUSHA LEO.

0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami,Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua barabara hiyo.
 Ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami ukindelea ambapo Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua. 
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea kiwanda cha General Tyre eneo la Themi,jijini Arusha,ambapo Kiwanda hicho Serikali imeamua kukifufua na kuanza kuzalisha upya bidhaa zake kupitia shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),pichani kati ni Kaimu Mkuregunzi wa NDC,Bwa.Mlingi Mkucha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangolo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza malalamiko ya baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha shirika la General Tyre,ambao Ndugu Kinana ameahidi kuyafanyia kazi na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata haki yao.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sambamba na viongozi wengine wa chama hicho wakitembelea kiwanda cha nguo cha Kiltex,ambapo kimefungwa na kusimamisha uendeshaji wake,ambapo kwa miaka mitatu kiwanda hicho  kiligeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia nafaka,hku mitambo yake yote ikiwa imeondolewa na kupelekwa kusikojulikana,
 Mlinzi Mkuu wa Kiwanda cha Kiltex,Mathias Mahundi akifafanua jambo kwa  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,na kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Asnah Mwilima.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizunguza na Halmashauri kuu ya CCM Wilaya,mapema leo jijin Arusha,ambapo pia alipokea taarifa za kazi ya chama na serikali.

RASIMU YA MWISHO YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

FINAL DRAFT OF THE PROPOSED CONSTITUTION

TASWIRA ZA HALI ILIVYO JIJINI DAR LEO KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

0
0
Hivi ndivyo hali ilivyo katika maeneo mengi hapa jijini Dar,kutoka na Mvua zinazoendelea kushesha.Kwa Mujibu wa Mamlaka ya Hali ya hewa nchini,inaeleza kwamba Vipindi vya mvua hii inayozidi milimeta 50 ndani ya masaa 24 itaendelea kuwepo katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa pwani wa nchi ikihusisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Dar es Salaam pamoja na kisiwa cha Unguja,hiyo ni kutokana na kuwepo na kuimarika kwa ukanda wa mvua (Inter Tropical Convergency Zone –ITCZ) katika maeneo hayo.
Barabarani huko nako mambo ni kama hivi.
Huku mitaani ndio usiseme,maana njia zote zimejaa maji.

nyumba, magari mawili yateketezwa kwa moto katika vurugu eneo la Olasiti jijini Arusha leo

0
0
Vurugu kubwa zinaripotiwa kutokea leo maeneo ya Olasiti jijini Arusha baaada ya habari ambazo bado kuthibitishwa rasmi zimeanza kufuatia mtu mmoja kukuta mfanyakazi wake wa kike akiwa  amelala  na anayedaiwa kuwa mpenzi wake ndani ya nyumba anayofanyia kazi. 
Inasemekana baba mwenye nyumba alikasirika sana kwa kitendo hicho na akampiga huyo kijan hadi akafa. Ndipo marafiki wa huyo anayedaiwa kuuwawa wakakusanyika nyumbani hapo na kuchoma moto nyumba na magari mawili kabla askari wa kutuliza ghasia kufika na kupambana nao kwa masaa kadhaa. Habari kamili na rasmi itawajia mara baada ya kupatikana
Nyumba hiyo ikiungua moto
Sehemu ya nyumba hiyo na gari 
Moja ya magari yaliyochomwa moto
Gari lingine lililochomwa moto
Majirani na wapita njia wakiangalia nje ya nyumba hiyo.
Picha na Gadiola Emmanul wa Tanzania Bloggers Network

WAZIRI MKUU AKIWA BUNDA

0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bw. Sanya William ambaye ni mlemavu na wanawe Mussa, Nasma na Dickson baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Bunda alikonda kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Bunda ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji Machi 20, 2015. 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Viongozi wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu wakati aliposimama kwa muda mfupi kwenye makazi ya Mkuu wa wilaya hiyo akiwa njiani kwenda Mwanza akitokea Bunda alikoweka jiwe la Msingi la Mradi wa maji wa Bunda Machi 20, 2015.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Busega, Paul Mzindakaya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

BONDIA IBRAHIMU CLASS 'KING CLASS MAWE' APOTEZA MCHEZO WA KWANZA NAMIBIA

0
0
BONDIA IBRAHIMU CLASS "King Class Mawe" mwenye rekodi namba moja nchini Tanzania na ni namba 216 kwa Dunia  amepoteza mpambano wake wa kwanza nchini Namibia kwa kupigwa kwa pointi na bondia Julius Indongo mwenye rekodi ya Namibia namba moja na Duniani ni namba 76 kwa ubora

mpambano huo uliofanyika machi 20,mwaka huu katika ukumbi wa Windhoek Country Club Resort,Windhoek, Namibia.

Mpambano huo ulianza kwa kasi ya ajabu ambapo bondia Class alimkalisha chini Indongo na kuhesabiwa na mpambano kuendelea kwa mashambulizi ya zamu kwa zamu kila upande,hata hivyo mpaka mwisho wa mchezo Class alipoteza mpambano uho kwa point.

mpambano huo ni wa pili kwa Class kucheza nje ya nchi baada ya ule wa kwanza kupigana nchini Zambia mwaka jana na kurudi na ubingwa wa WPBF Africa.

Kabla ya kuchaguliwa kwenda kupigana nchini Namibia,Class alimdunda bondia Cosmas Cheka na kunyakuwa mkanda wa U.B.O Africa na kumfanya amiliki mikanda miwili ya Africa mpaka sasa. 

Mpambano huo anaupoteza baada ya miaka mitano iliyopita kuwapiga mabondia mbalimbali, Class ananolewa na jopo la makocha linalongozwa na Habibu Kinyogoli 'Masta',Kondo Nassoro pamoja na Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye humpa ushauli anapokuwa ulingoni jinsi ya kukabiliana na mpinzani anaecheza nae.

LOWASSA: MASHEKHE WA BAGAMOYO MMENISHAWISHI KUGOMBEA URAIS 2015

0
0
MASHEIKH wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.MSIKILIZE HAPA.

Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu,"alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za Elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii. 
Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.
 Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.

Wajasiriamali wa soko lililoungua Arusha wamshukuru Nyalandu

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiongea na waandishi wa habari na Wajasiriamali wa soko la vinyago lililoungua moto Mkoani Arusha, mara baada ya kutoa kiasi cha shilingi milioni 100 kupitia Tanapa Ili ziweze kusaidia ujenzi wa soko hilo. Makabidhiano hayo yalifanyika jana Mkoani Arusha.

MAMA SALMA KIWETE AKABIDHI GARI LA WAGONJWA KWENYE HOSPITALI YA MKOMAINDO HUKO MASASI

0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na mmoja wa wauguzi katika hospitali ya Wilaya ya Masasi, Mkomaindo, mara baada ya kuwasili hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatembelea wagonjwa tarehe 19.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwelekeza Bibi Zauda Amuli,18, mkazi wa Mtaa wa Moroco namna ya kumnyonyesha mtoto wake mchanga aliyezaliwa tarehe 17.3.2015 katika hospitali ya Mkomaindo huko Masasi tarehe 19.3.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimchukua mtoto mchanga kutoka kwa mama yake Bibi Malisela Amandus, 24, anayeishi mtaa wa Silabu huko Masasi wakati Mama Salma alipotembelea hopitalini hapo kuwajulia hali wagonjwa tarehe 19.3.2015.

WAFANYABIASHARA MANISPAA YA SUMBAWANGA WALALAMIKIA KODI MBALIMBALI SERIKALINI, MKUU WA MKOA WA RUKWA AWATAKA KUWA WAZALENDO KULIPA KODI KWA HIARI KUJENGA NCHI YAO

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisikiliza risala ya umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga iliyokuwa ikisomwa kwake na Mwenyekiti wa umoja huo Ndugu Willington Kiziba Ndyetabura (Kulia). Katika risala hiyo yalikuwepo malalamiko mbalimbali ikiwemo ya matumizi ya mashine za EFD ambapo ni pamoja na gharama kubwa za mataengenezo, Ada ya ukaguzi wa majanga ya moto(Fire), Kupanda mara mbili kwa kodi ya mapato kwa wafanyabiashara wadogo na Ulinzi na Usalama kwa wafanyabiashara. Wafanyabiashara hao walihoji n ivigezo gani vilivyotumika kupandishwa kwa kodi hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza na umoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Sumbawanga tarehe 19/03/2015 katika mkutano wa pamoja wa kusikiliza kero zao mbalimbali uliofanyika katika ukumbi wa Upendo View katikati ya Mji wa Sumbawanga. Wafanyabiashara hao waliomba kuonana na Mkuu huyo wa Mkoa ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wafanyabiashara hao kuwa wazalendo kwa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia maendeleo ya Mkoa na taifa kwa ujumla.

 Katika kujibu kero zao mbalimbali alisema kuwa, zile kero ambazo haziwezi kutatuliwa mpaka yafanyike mabadiliko ya sheria atayachukua na kuyafikisha sehemu husika na pindi marekebisho yatakapohitajika yatafanyiwa kazi, aliwataka pia wafanyabishara hao watii sheria mbalimbali za kodi ikiwemo kuchangia ada ya ukaguzi wa majanga ya moto ili kuimarisha jeshi la zimamoto ambalo linahitaji maboresho makubwa kwa usalama wa wananchi na malizao.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZEE WA CUF MJINI ZANZIBAR LEO

0
0
 Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wazee wa CUF katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, Zanzibar, leo
  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wazee wa CUF katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani, Zanzibar, leo
 Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui, akizungumza na wazee wa CUF katika ukumbi wa salama hoteli ya Bwawani.
Sehemu ya wazee wa CUF wa Wilaya sita za Unguja waliohudhuria mkutano huo (picha na Hassan Hamad, OMKR)

Prof Jay atangaza nia ya Kugombea jimbo la Mikumi

Redio Times, Valentino Hotel kudhamini mafunzo TASWA

0
0
Meneja Mkuu wa Royal Valentino Hotel iliyopo Kariakoo Dar es Salaam, Kapara Hamis (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na semina ya waandishi chipukizi wa habari za michezo inayoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), itakayofanyika Jumatano ijayo. Kulia ni Mkurugenzi wa Redio Times FM, Rehure Nyaulawa ambaye redio yake pamoja na hoteli hiyo ndiyo wadhamini wa semina hiyo. Mwingine ni Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Egbert Mkoko. (Na Mpigapicha Maalum).

Na Mwandishi Wetu
REDIO Times FM ya Dar es Salaam imejitokeza kuwa mdhamini mkuu wa semina ya waandishi wa habari za michezo chipukizi  itakayafanyika Jumatano wiki ijayo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Egbert Mkoko alimkshukuru Mkurugenzi Mkuu wa Redio Times FM, Rehure Nyaulawa na Meneja wa Valentino Royal Hotel, Kapara Hamis kwa kukubali kugharamia semina hiyo ya siku moja.

“Naomba nitamke kuwa Redio Times FM ndiyo wadhamini wa semina yetu ya siku moja itakayoshirikisha waandishi wa habari za michezo chipukizi, ambapo Valentino Royal Hotel pia ya Dar es Salaam watakuwa wadhamini washiriki wa semina yetu, ambayo itafanyikia hotelini kwao,” alisema Mkoko.

Aliwashukuru wadhamini hao kwa moyo wa kujitolea na kuiomba pia hoteli hiyo iliyopo Kariakoo, Dar es Salaam kuendelea kuipa ushirikiano TASWA na wanamichezo kwa ujumla katika masuala mbalimbali ya udhamini.

Mkoko alisema siku zote chama chake kimekuwa kikipigania kuandaa mafunzo kwa wanahabari wa michezo kama sehemu mojawapo ya kukuza weledi na kwamba wana matumaini Aprili watafanya nyingine kama hiyo na pia Mei mwaka huu watafanya nyingine.

Alisema wataalamu wa michezo mbalimbali kama vile soka, riadha, netiboli, kikapu watapata fursa ya kutoa mada kuhusiana na michezo yao, ambapo pia waandishi wa habari za michezo waliobobea wameitwa kuwaweka sawa chipukizihao, ambao wameteuliwa kutokana na mapendekezo ya wahariri wa habari za michezo wa vyombo husika.

 “Hii ni awamu ya kwanza kwa waandishi wachanga na baadhi ya wa kada ya kati ambao jumla yao ni 40, baada ya hapo tutaendesha mafunzo ya namna hii kwa waandishi waandamizi na wahariri wa habari za michezo.

“Tunaamini baada ya hapo kutakuwa na mabadiliko ya namna fulani, kwani watu tuliowaandaa nina hakika washiriki watashiba vizuri,” alisema na kuongeza kuwa pia kutakuwa na mtoa mada kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kwa upande wake Nyaulawa alisema redio yake ikiwa ni mdau mkubwa wa habari na michezo kwa ujumla amekuwa akipigania mafunzo kwa wanahabari wa michezo kama sehemu mojawapo ya kukuza weledi.

“Tunaamini waandishi wanapoboresha uandishi wao inachangia kwa kiasi kikubwa kukuza heshima ya vombo vya habari, hivyo tunaomba wadau mbalimbali washirikiane na TASWA inapoandaa mambo kama haya, sisi tumeanza na wengine wasaidie,” alisema.

Naye Kapara wa Valentino Royal, alisema hoteli yake imekuwa ikitumiwa pia na timu mbalimbali zinapotoka nje ya nchi kufikia hapo, hivyo kwa namna ya pekee waandishi wa habari za michezo ni wadau wao, ndiyo sababu hawakusita kukubali kudhamini mafunzo hayo.

Jumapili hii njoo ushuhudie mchuano wa nguvu wa ma-DJ wakali club bilicanas

0
0
Jumapili hii njoo ushuhudie mchuano wa nguvu kutoka kwa ma Dj wakali wa bongo watakaochuana pale juu ni @djzeroxxl @chokadj na @djvasley hii ni ndani ya @bilznightclub pekee! Unakosaje kushududia ni Dj gani atapagawisha zaidi? Airtel watatoa zawadi kibao 🎁🎁🎁Kiingilo ni buku 10 tu TAG kuwajulisha washkaji 👍 FOLLOW: @airtel_tanzania

how the rich get richer

Balozi Seif afunguwa Kongamano la Wanawake na Uongozi katika Katiba inayopendekezwa,Zanzibar leo

0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akilifunguwa Kongamano la Wanawake na Uongozi katika Katiba inayopendekezwa lililofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi akitoa nena la shukrani kwa Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Uongozi.
Mtangazaji wa Zamani wa Kituo cha Matangazo ya Televisheni Zanzibar Karume House Bibi Neema Mussa Maisara akiipitia Katiba iliyopendekezwa kwenye Kongamano la Wanawake na Uongozi hapo Grand Palace Malingi Mjini Zanzibar. Kulia yake ni msanii maarufu Zanzibar Bi Tele, Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Zanzibar Bibi Salama Aboud Talib na Makamu mwenyekiti Mstaafu wa UWT Zanzibar Bibi Mvita Mussa Kibendera.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI YA KUCHANGIA UJENZI WA KANISA LA KIGANGO CHA MT. DOMINIC SAVIO TEMEKE MIKOROSHINI, DAR ES SALAAM

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki na kuongoza matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokelewa na mwakilishi wa Askofu Titus Mdoe, Padri Mushi (mwenye kanzu nyeupe) na baadhi ya viongozi wa Kanaisa wakati alipowasili eneo la mwisho wa matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa hafla fupi ya matembezi ya hisani ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kigango cha Mt. Dominic Savio, lililopo Temeke Mikoroshini. Matembezi hayo yamefanyika leo Machi 21, 2015 asubuhi kuanzia Chang’ombe Polisi hadi Temeke Mikoroshini, jijini Dar es Salaam.

MAANDALIZI MBIO ZA MAGARI YAKAMILIKA,SASA KUFANYIKA JUMAPILI HII MAENEO YA KIA

0
0
Baadhi ya magari yakiingia uwanjani kwa ajili ya ukaguzi wa mwisho kabla ya mashindano.

Mafundi wakiweka mafuta ya ndege katika moja ya magari yanayoshiriki mbio hizo.
Magari yanaotajwa kutoa ushindani mkali katika mbio hizo.Mamboz na Madebe linalotajwa kufungwa injini mpya ambayo bado kilometa zake zinasoma 0.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images