Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 774 | 775 | (Page 776) | 777 | 778 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Na. Johary Kachwamba-MAELEZO, DODOMA

  SERIKALI kupitia Mamlaka ya Maeneo ya EPZ pamoja na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) imeweka matayarisho na utaratibu wa kuvutia wawekezaji eneo la Tanga.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene alipokuwa akijibu swali la msingi la Mhe. Omari Nundu, Mbunge wa Tanga Mjini.

  “tayari Mamlaka ya EPZ imetenga hekta 1,363 katika eneo la Neema mkoani Tanga kwaajili ya ujenzi wa viwanda na uthamini wa mali umekamilika” alisema Mhe. Mbene

  Aidha Mhe. Alisema NDC ina eneo la hekta 50 huko Kange Mkoani Tanga ambalo maandalizi ya kuliweka tayari kwaajili ya kuvutia uwekezaji yanaendelea.

  Juhudi za kuvutia uwekezaji ili kuanzishwa viwanda vipya zimefanyika pia ambapo kuna viwanda vingi vimeanzishwa ikiwa ni pamoja na Kiwanda cha Maweni cha Saruji, Athi River cha Chokaa, Neelkanth cha chokaa, Tanga Pharmaceutical and Plastics LTd, Peepe Tanzania Ltd, Pemba Flour Mill na vinginevyo. 

  “kiwanda cha Saruji cha Tanga na Tanga Fresh ni baadhi ya viwanda vilivyoboreshwa mkoani Tanga ambavyo vinafanya kazi na kuongeza uzalishaji. Kiwanda cha Tanga Dairies Ltd, Tanga kilifufuliwa na sasa kinafanya kazi” alisema Mhe. Mbene

   “Serikali imetambua kuwa tatizo la kiwanda cha mbao linatokana na gharama kubwa ya kupata malighafi kutoka Mufindi, Iringa hadi Tanga. Kutokamilika kwa makabidhiano baina ya mwekezaji na Msajili wa Hazina wa Hati zinazomwezesha mwekezaji kuendelea na kazi kumechelewesha uzalishaji katika kiwanda cha chuma. Wizara inafuatilia kwa karibu masuala hayo” aliongezea Mhe. Mbene

  Mazungumzo kati ya Serikali na wamiliki wa viwanda vya Mbao na Chuma yalifanyika na kukubaliana jinsi ya wao kuanza upya kutekeleza wajibu wa kimkakati.

  0 0

   The East Africa Auto-Mobile Service Company Operations Manager, Mr. Dean Stout speaks to the journalists in Dar es Salaam recently, on the importance of vehicles inspection especially for the cars imported from Japan.
  Tanzania Bureau of Standards (TBS), Engineer Tumaini Mtitu speaks to the attendees of the Car Inspection Seminar prepared by the East Africa Auto-Mobile Service Company in Dar es Salaam recently, on the importance of vehicles inspection especially for the cars imported from Japan

  Representatives from a Japanese automobiles firm have called upon Tanzanians to import vehicles that have been inspected, illustrating that by doing so they will be avoiding unnecessary additional costs.

  Mr Stout Dean Lawrence, The International Operations Manager for the Japan-based East Africa Automobile Service Company Limited said in Dar es Salaam on Tuesday that importing uninspected vehicles pose as a risky doing as it may lead to further inconveniences to the buyer.

  “Buyers should have a clear understanding that not all vehicles from Japan come in commendable quality, buyers should have the tendency to buy vehicles that has passed through inspection so as to maintain the quality and avoid incurring inconveniences,” he clarified.

  Recently the company signed a three-year agreement with Tanzania Bureau of Standards (TBS) that enables it to have the mandate to conduct pre-shipment inspection of motor vehicles being exported from Japan to Tanzania.

  According to the firm’s Tanzania country manager, Mr. Josia Nguku, East Africa Automobile Company Limited will inspect all the vehicles and make sure that there is value for money in what Tanzanians import.

  0 0


  0 0

   Mwimbaji wa siku nyingi wa nyimbo za injili nchini, Jennifer Mgendi, ameachia albamu yake mpya mapema wiki hii.

  Akizungumza na blogu hii  Mgendi amesema albamu hiyo ina jumla ya nyimbo saba ambazo ni Wema ni Akiba, Nani kama Mungu?, Nakungoja aliomshirikisha Mchungaji Abiudi Misholi, Kimbilia Msalabani, Nakuhitaji Roho, Tenda nishangae na Wastahili.

  Akizungumzia video ya albamu hiyo, Mgendi amesema maandalizi ya video yameanza na video itazinduliwa Juni 28 katika kanisa la DCT Tabata Shule katika tamasha litakaloambatana na shukurani ya kutimiza miaka 20 tangu aanze uimbaji. 

  Mbali na uimbaji Jennifer pia ni muandaaji wa filamu mbalimbali za kidini hadi sasa akiwa na filamu tano Joto la roho, Pigo la faraja, Teke la Mama, Chaimoto na Mama Mkwe.

  0 0


  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Nchi Maendeleo,Biashara na Ushirikiano wa Ireland Bw.Sean Sherlock wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiri wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waziri wa Nchi Maendeleo,Biashara na Ushirikiano wa Ireland Bw.Sean Sherlock wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na Ujumbe aliofuatana nao.[Picha na Ikulu,Zanzibar.]

  0 0

  Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Robert Mongi (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waliofika hospitalini hapo kukabidhi msaada wa simu 150 aina ya ZTE zitakazotumiwa na wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
  Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation Reenu Verma (kulia) akimfungulia boksi lenye moja ya simu kati ya 150 aina ya ZTE, Mratibu wa Mradi wa MDOTS unoafanya utafiti wa tiba ya ugonjwa wa siko seli (Sickle Cell) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt Robert Mongi wakati wa makadhiano ya msaada wa simu hizo zilizotolewa na mfuko huo kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa wamebeba maboksi yenye simu aina ya ZTE walipofika kukabidhi msaada wa simu 150 zilizotolewa msaada na Vodacom Foundation katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya wagonjwa wa siko seli kujirekodi na kutuma video wakati wakimeza dawa za ugonjwa huo na kuzituma katika hospitali hiyo kila watumiapo dawa hizo kwa ajili ya kujua kama wanafuata matumizi sahihi ya dawa hizo.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(pichani) kesho tarehe 20 Machi, 2015 saa 8:00 mchana atawavisha vyeo Maafisa wa Jeshi la Magereza wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam waliopandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria.

  Kwa Mamlaka aliyopewa kisheria na Tume ya Polisi na Magereza ya Mwaka 1990, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini atawavisha vyeo hivyo katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.

  Tume ya Polisi na Magereza katika Kikao chake Namba 2/2014/2015 kilichofanyika tarehe 16 Machi, 2015 chini ya Mwenyekiti Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Pereira Ame Silima(Mb) imewapandisha vyeo Maafisa 292 wa ngazi mbalimbali kuanzia tarehe 16 Machi, 2015.

  Maafisa hao waliopandishwa vyeo ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza kuwa Kamishna Msaidizi wa Magereza 11, Mrakibu wa Magereza kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza 41, Mrakibu Msaidizi wa Magereza kuwa Mrakibu wa Magereza 83 na Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kuwa Mkaguzi wa Magereza 157.

  Imetolewa na; Inspekta Lucas Mboje, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
  Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
  DAR ES SALAAM
  19 Machi, 2015.

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na ujumbe wa baraza la wafanyabiashara waUturuki,uliofika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza biashara kati ya Zanzibar na Uturuki.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania Atakan Giray, Ofisini kwake Migombani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokea zawadi zungumza na mwenyekiti wa baraza la wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania Atakan Giray, Ofisini kwake Migombani.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa baraza la wafanyabiashara wa Uturuki na Tanzania, Ofisini kwake Migombani. (picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0

  Mwandishi Wetu

  Wakati bondia Mohamed Matumla Jr akiwa katika mazoezi ya mwisho mwisho kumkabili Wang Xin Hua wa China, wenzake Thomas Mashali na Karama Nyilawila wametoleana uvivu huku kila mmoja akijigamba kutwaa ubingwa watakapozichapa Machi 27 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

  Matumla Jr atazichapa na Hua pambano la super bantam la ubingwa wa dunia wa (WBF World Eliminate) pambano maalumu kwa mabondia hao la kutafuta tiketi ya kucheza pambano la utangulizi kwenye lile la nguli wa masumbwi duniani, Manny Pacquiao na Floyd Mayweather la Mei 2. 

  Kama Matumla atampiga Hua kwenye pambano lao la Machi 27 na kuonyesha kiwango kizuri atapata nafasi ya kucheza pambano la utangulizi kuwasindikiza nguli hao wa masumbwi duniani watakapovaana Mei 2 jijini Las Vegas.

  Akizungumza katika mazoezi yake yanayoendelea kwenye gym ya Oil Com, Keko jijini Dar es Salaam chini ya kocha wake ambaye ni baba yake mzazi, Rashid 'Snake Man' Matumla, bondia huyo alisema hataki kupoteza nafasi ya kucheza kwenye pambano la Mayweather na Pacquiao.


  0 0

  9
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba na kuingia ndani kukagua nyumba hizo.
  20
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akipewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC maelezo ya uendelezaji wa eneo la Usa-river lililonunuliwa na NHC kwa ajili ya kujenga Jiji la kisasa hapo jana.
  19
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi akiondoka eneo la Meru Residential arpatments alipomaliza kukagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC na kuuzia wananchi hapo jana.


  0 0


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, PSPF, Adam Mayingu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemiah Mchechu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.


  0 0

  Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo
  Diwani wa Kata ya Nachingwe, Lindi Mjini, Omary Chitanda (katikati) akiuliza swali kwa mtaalamu wa mradi huo.

  *Taasisi ya Miradi na Maendeleo ya Miundombinu (UTT-PID) ilianza kazi zake Julai 1, 2013. Taasisi hii ilirithi kazi za miradi zilizokuwa zinafanywa na Taasisi mama yaani UTT.

  Andrew Chale ,Bagamoyo

  Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Lindi Machi 17, wametembelea miradi mbali mbali ya UTT-PID iliyopo Dar es Salaam ikiwemo ule wa Bagamoyo wa New Mapinga Satellite.

  Madiwani hao waliweza kujifunza mambo mbalimbali dhidi ya mradi huo ulivyoandaliwa na kufanya kazi na namna ulivyopangiliwa kwa ustadi mkubwa.

  Katika ziara hiyo inayotarajia kumalizika Machi 19, mwaka huu. Madiwani hao wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Lindi, Frank Magali alipongea juhudi za UTT-PID kwa kufanikisha ziara hiyo kwani wamejifunza mengi na pindi watakaporejea Lindi, watakuwa mfano wa kuigwa.

  “Kule kwetu Lindi pia tuna mradi uliopo katika hatua mbaali mbali na UTT-PID tayari wamesha pima baadhi ya viwanja katika mfumo kama huu wa kisasa tunaojifunza hapa hivyo itatusaidia sana kwa sasa” alisema Meya Magali.
  Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani)
  Diwani wa Kata ya Nachingwea, Manispaa ya Lindi, Omari Chitanda akielezea namna alivyojifunza kwenye mradi huo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani).


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika wakifungua maji ya bomba kwenye Zahanati ya Kijiji cha Mpiji Magohe mara baada ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji hicho manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua Tenki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea mkoani Dar es salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Said Meck Sadiki akizindua Tenki la kuhifadhia maji katika kijiji cha Mpiji Magohe, manispaa ya Kinondani jijini Dar es salaam leo wakati wa mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji yanayoendelea mkoani Dar es salaam.


  0 0

  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,DIGP, Abdulrahmani Kaniki akikagua gwaride la wakaguzi wasaidizi wa polisi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
  Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,DIGP, Abdulrahmani Kaniki akimvisha cheo wp 2704 ssgt Batuli kuwa mkaguzi msaidizi wa jeshila polisi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
  Wahitimu wa kozi ya mkwaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wakipita kutoa heshima kwa mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi.
  Wahitimu wa kozi ya mkwaguzi msaidizi wa jeshi la polisi wakiimba kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya maofisa hao katika chuo cha polisi Moshi. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  0 0

  Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mapema leo katika eneo la Soweto jijini Mbeya,Chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mara moja.Picha na Fadhiri Atick Mr.Pengo,Mbeya.
  Juhudi za kuuzima moto huo zikiendelea kufanywa na baadhi ya majirani wa eneo ilipo nyumba hiyo,huku wakiendelea kukisubiria kikosi cha Zimamoto.
  Hakuna kilichobaki ndani ya Nyumba hiyo.


  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa kampuni ya Brussels Airline Mhe. David Lyssens (kulia) baada ya kumaliza kikao naye ofisini kwake Brussels. Kushoto ni Bwana Geoffrey Kabakaki Mchumi Mhandamizi Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Balozi Kamala ameiomba kampuni hiyo kuingia kwenye biashara ya usafiri wa anga Tanzania.

  0 0


  0 0

  Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama.Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama.Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo.Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na benki hiyo. Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na benki hiyo.


older | 1 | .... | 774 | 775 | (Page 776) | 777 | 778 | .... | 3353 | newer