Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109939 articles
Browse latest View live

MH. RIDHIWANI KIKWETE ATEMBELEA SHUGHULI ZA MAENDELEO JIMBONI KWAKE

$
0
0
Na John Gagarini,Globu ya Jamii - Chalinze

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete jana alianza ziara kwenye Jimbo hilo ambapo ametembelea shughuli mbalimbali pamoja na kujua changamoto zilizopo kwenye Jimbo lake.

Ridhiwani alitembelea kata ya Pera na kuzungumza na wakazi wa vitongoji mbalimbali ambavyo vinaunda kata hiyo ambapo leo ametembelea kata ya Kibindu nako alipata fursa ya kuzungumza na wakazi wa vitongoji vilivyopo kwenye kata hiyo.

Mbunge huyo atakuwa na ziara ya wiki moja kutembelea kata mbalimbali za Jimbo hilo na kujionea shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa shule za msingi na sekondari, barabara, zahanati na kufanya mikutano ya hadhara ya wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete Akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kitongoji cha Malivundo wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiongea na moja ya wanafunzi wa shule ya Msingi Malivundo wakati wa zaiara yake kutembelea shughuli za maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka mchanga kwenye mashine ya kufyatulia matofali alipotembelea ujenzi wa shule ya Msingi wakati wa ziara yake ya kutembelea shughuli za maendeleo.


CHUO CHA TAKWIMU MASHARIKI MWA AFRIKA KUTILIANA SAINI YA MKATABA WA MAKUBALIANO YA MAFUNZO YA WATALAAM WA TAKWIMU NA CHUO CHA TAKWIMU CHA INDIA

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akimwelezea Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal kuhusu chumba cha kompyuta kilichopo chuoni hapo wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015. 
Naibu Balozi wa India nchini Balvinder Humpal akiangalia vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wakati wa kuangalia maadalizi ya kutiliana saini ya Mkataba wa Makubaliano ya Mafunzo ya Watalaam wa Takwimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika na Chuo cha Takwimu cha nchini India utakaosainiwa tarehe 28 Machi, 2015.

KAMPUNI YA East Africa Unique Co.LTD KUENDESHA SEMINA KWA WAFANYABIASHARA

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kampuni ya East Africa Unique Co.LTD imeandaa semina itakayo anza mwezi April mwaka huu kwa wafanyabiashara juu ya kuwajengea uwezo wenye miradi itakayo kuwa na uaminifu na kujituma kulingana na uwezo pamoja na ukomo wao.

Akizungumza leo na Waandishi wa Habari,Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Rodgers Mbaga amesema Kampuni hiyo ambayo inashughulika na ushauri,mawasiliano ya masoko imebuni na kupanga Maonyesho ya Kukuza Uwekezaji-TIPEC kwa lengo la kuweka msukumo zaidi kwenye uwekezaji na hatimaye kuinua uchumi.

Amesema kampuni hiyo imepanga kuwainua wafanyabiashara nchini katika program ambazo wanazifanya kutokana na kukosa mwamko katika fursa za uwekezaji nchini.

Amesema semina hiyo itakuwa na kiingilio cha dola za kimarekani 100 kwa mtu na kushiriki mara moja katika kila jumatano ya mwisho wa mwezi.

Kampuni hiyo inatarajia kufanya gulio Juni 3 hadi 4 mwaka huu na kuweza watu kuandika miradi yao na kwa ajili ya kuwea kupata washirika wa kuendesha mawazo yao zaidi ya miradi 100itakuwapo katika maonyesho hayo na makampuni 100 yatashiriki na gharama za ushiriki dola za kimarekani 1000 na 3000.
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya TEPAC Rodgers Mbaga (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu kuwepo kwa mkutano na maonesho ya kukuza uwekezaji yatakayofanyika Juni 3 hadi 5 Mwaka huu. Kushoto ni Meneja miradi wa kampuni hiyo Tony Swaheh na kulia ni Ofisa mwandamizi ukuzaji masoko wa TEPAC Stephen Kobero. Picha na Agnes Alcardo.

RAIS KIKWETE AFUNGUA MAFUNZO YA WAKUU WAPYA WA WILAYA,MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mafunzo ya wakuu wa wilaya wapya yanayofanyika katika ukumbi wa hosteli ya St.Gaspar mjini Dodoma leo jioni.Kushoto ni Waziri wa TAMISEMI Mh.Hawa Ghasia,Watatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa na kulia ni Naibu waziri TAMISEMI Mh.Aggrey Mwanri.
Baadhi ya wakuu wa wilaya wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo kwa wakuu wapya wa wilaya mjini Dodoma leo jioni.(picha na Freddy Maro).

MAAFISA UTUMISHI KUTOKA MIKOA YA LINDI NA MTWARA WAPATA ELIMU JUU YA MAENDELEO YA MFUKO WA PENSHENI WA GEPF

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Halima Dendegu akifungua rasmi semina maalum kwa Maafisa Utumishi kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara Juu ya Maendeleo ya Mfuko wa Pensheni wa GEPF,uliofanyika Mkoani Mtwara.Katika hotuba yake ya Ufunguzi,Mh. Dendegu ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mfuko wa GEPF kwa kuifikisha elimu hiyo katika mikoa hiyo ya kusini.
Meneja Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF,Bw. Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada juu ya maendeleo ya Mfuko wa GEPF, mafao mapya yatolewayo pamoja na faida za kuwa mwanachama,wakati wa semina maalum kwa Maafisa Utumishi kutoka Mikoa ya Lindi la Mtwara.

Imetosha Movement Kufanya Matembezi Hisani Machi 28

$
0
0
Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu (kulia) akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni. Baadhi ya wajumbe wa kamati ya taasisi ya 'Imetosha Movement' na viongozi wakizungumza na vyombo vya habari hivi karibuni.

  Na Mwandishi Wetu 

  ASASI ya Harakati za Imetosha ilioanzishwa kupinga mauaji na vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye u-albino inatarajiwa kufanya matembezi makubwa ya hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu kwa uma juu ya imani potofu zinazoendelea za mauaji ya albino. 

 Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Kujitolea wa Harakati za 'Imetosha Movement', Henry Mdimu amesema matembezi ya hisani kuchangia fedha zitakazowezesha kutolewa kwa elimu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa juu ya imani potofu zinazoendelea na mauaji ya albino yanatarajia kufanyika Dar es Salaam Machi 28, 2015. 

 Alisema matembezi hayo yataanzia katika Viwanja vya Leaders na kuzunguka maeneo yaliyopangwa kisha kurejea viwanjani hapo kwa ajili ya shughuli maalumu ya kuchangisha fedha kwa ajili ya harakati maalumu za imetosha zitakazo kwenda kwa jamii ya kawaida na kueneza elimu ikiwa ni juhudi za kuhamasisha kila mwana jamii kupaza sauti na kusema 'Imetosha Mauaji ya Albino'. 

 "...Baada ya taratibu kukamilika, matembezi sasa yatafanyika Tarehe 28 Machi kuanzia saa 12 Alfajiri, kutoka Leaders Club tutazunguka na kurudi hapo, karibuni sana tuchangie harakati hizi zenye lengo zuri kwa mustakabali wa Taifa letu lenye sifa ya amani na utulivu," alisema Mdimu katika taarifa yake. 

 Aidha akizungumzia uvumi ulioenea hasa katika nchi za nje, unaodai kwamba serikali imekataza watu wenye ulemavu wa ngozi kuandaa matembezi au maandamano alisema taarifa hizo hazina ukweli wowote na kuongeza kuwa kuna taratibu za kufuata kabla ya uandaliwa shughuli hizo. "...Hili suala sio kweli, ili ufanye mambo kama haya ni lazima upitie taratibu za kisheria ili upate kibali. 

Hii ni nchi na ina taratibu zake kwa hiyo tulipaswa kuzifuata na ndio kilichosababisha hata matembezi yetu kuahirishwa. "Tulikuwa tunafuata taratibu na leo rasmi tumepata usajili wa Imetosha...sasa imetosha imekuwa taasisi kamili inayoitwa IMETOSHA MOVEMENT. 

Napenda kuchukua wasaa huu kuwashukuru marafiki wote wanaoniunga mkono, na kunipa moyo, msinichoke kwa sababu safari bado ni ndefu," Hata hivyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni kujitokeza katika matembezi hayo ya hisani ili kuunga mkono juhudi sa mapambano ya kukomesha mauaji na vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa watu wenye ualbino maeneo mbalimbali ya nchi.

WAZIRI MKUU KUTANA NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI JAPAN

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Bibi wa Kijapan, Midori Uno,machi 17, 2015 kwenye hoteli ya New Otani jijini New York , ambaye aliishi Tanzania miaka ya 60 baada ya Uhuru wa Tanganyika akifanya kazi kwa kujitolea. Hisasa Bibi Uno ni bingwa wa lugha ya kiswahili na amekwishaandika Kamusi ya Kijapan na Kiswahili pamoja na vitabu kadhaa.
Waziri mkuu, Mizengo Pinda na mkewe wakitia saini kitabu cha wageni kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo nchini Japan baada ya kuwasili ubalozini hapo kuzungumza na Watanzania waishio Japan Machi 17, 2015. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza muda wake, Salome Sijaona na Wapili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, Batilda Buriani na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Mahadh Maalim.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania waishio nchini Japan.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA LONGIDO MKOANI ARUSHA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako kwenye ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya Kuhimiza,kuimarisha na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 ikiwemo pia na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.
Wananchi wa kijiji cha Eworendeke wakiwa wamekusanyika wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia wilayani humo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ujenzi wa nyumba ya watumishi wa Afya katika kijiji cha  Lesingeita,wilayani Longido.Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Longido Mh.Lekule Laizer. 
Mzee Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli yake ya Longido kama ionekanavyo pichani.
Pichani ni jengo la kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL),ambapo  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliweka jiwe la msingi na kushiriki kupaka rangi kwenye majengo hayo.

PICHA NA MICHUZI JR-LONGIDO ARUSHA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Usalama wa Raia, Demokrasia na Haki za Binadamu Bi. Sarah Sewall atembelea zanzibar

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Usalama wa Raia, Demokrasia na haki za Binadam Bi. Sarah Sawell akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) alipofika katika kituo cha Vijana muembe madema Mjini Zanzibar.

Na Abdulla Ali-Maelezo Zanzibar 
Serikali ya Marekani imeamua kuwatembelea Vijana wa Bara la Afrika kwa lengo la kukaa nao pamoja na kuzungumza nao juu ya Changamoto na Matatizo yanayowakabili vijana hao. 
 Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Usalama wa Raia, Demokrasia na Haki za Binadamu Bi. Sarah Sewall wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi ya Kituo cha Vijana iliyopo nyuma ya Kituo cha Polisi Madema, Wilaya ya Mjini Unguja. 
 Amesema vijana wanakabiliwa na matatizo mengi kwa sasa yanayowafanya kukata kabisa tamaa ya maisha na badala yake kujiingiza katika vitendo viovu ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya, wizi, ujambazi na wengine kuweza kutumiwa na makundi maovu yasiyo na tija kwao. 
 Aidha amesema kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ndio tatizo kubwa zaidi duniani jambo ambalo lilimfanya Rais wa Marekani Barack Obama wiki 3 zilizopita kuitisha mkutano wa pamoja wa Dunia ili kujadili masuala ya vijana ambapo Taasisi Mbalimbali za Kiserikali na Binafsi Duniani zilishiriki katika mkutano huo. 
 Amefahamisha kuwa lengo la ziara yake barani afrika ni kuyaendeleza kwa kuyafikisha kwa vijana yale yote yaliyojadiliwa katika mkutano huo ili kuwaonesha njia ya mafanikio vijana hao pamoja na kuwapa msaada pindi utakapohitajika. Akizungumzia kuhusiana na mauaji ya Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) nchini Tanzania amesema Serikali yake imeshachukua hatua mbalimbali katika kulinda haki za binadamu duniani kote kwa kuwapatia ulinzi na usalama wakiwemo hao albino ila juhudi zaidi za kuwalinda zinatakiwa kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha kuwa albino wanakuwa katika usalama zaidi. 
 Akigusia kuhusu mchakato wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini Tanzania amesema Serikali ya Marekani imekuwa ikitoa msaada mkubwa kwa Serikali ya Tanzania wakati wa uchaguzi hivyo itaendeleza na jitihada hizo ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa katika hali ya usalama na amani na kuepukana na vurugu zisizo za lazima. 
 Nae Mwenyekiti Mtendaji wa Vituo vya Vijana Tanzania Nd. Abdalla Miraji Othman amesema vituo vyao kwa sasa vinakabiliwa na Changamoto nyingi ikiwemo usafiri pamoja na posho na mishahara kwa wafanyakazi wa vituo hivyo kwani huwa havitolewi kwa wakati jambo ambalo linarejesha nyuma kwa kiasi kikubwa jitihada zao za kuwaokoa vijana kutokana na vitendo viovu. Akitoa wito wake Nd. Othman amesema ipo haja kwa Benki za Kitanzania kupunguza masharti ya kutoa mikopo pamoja na Riba ili vijana wamudu kuchukua mikopo katika Benki hizo kwa lengo la kujiajiri na hatimae kujikomboa kimaisha. Amesema Ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Usalama wa Raia, Demokrasia na Haki za Binadamu Bi. Sarah Sewall ilikua ni ya Siku 1 Visiwani Zanzibar ambapo ziara hiyo inatrajiwa kufanyika takriban bara lote la Afrika kwa lengo la kukutana na vijana na kuzungumza nao juu ya masuala mbalimbali.

WAFUNGWA GEREZA KUU UKONGA, DAR ES SALAAM MAHIRI KWA USHONAJI WA NGUO ZA AINA MBALIMBALI MAGEREZANI

$
0
0

Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakikata vitambaa vya nguo kabla ya kuanza kushona nguo za Wafungwa Magerezani. Wafungwa hao hujifunza Stadi mbalimbali za ujuzi ambazo huwasaidia kujipatia kipato mara tu wanapomaliza kifungo chao.

Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakiendelea na ushonaji wa nguo za aina mbalimbali kama wanavyoonekana katika picha. Jeshi la Magereza nchini linatekeleza ipasavyo jukumu lake la Urekebishaji kwa kuwapatia ujuzi wa fani mbalimbali Wafungwa wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao Magerezani.

Aina za nguo mbalimbali ambazo tayari zimeshonwa kwa Ustadi Mkubwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam. Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam limejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kutekeleza ipasavyo Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa kwa Vitendo

Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ismail Mlawa akiongea na Wanahabari(hawapo pichani).Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

ally rehmtulla's eleganza on march 21, 2015 live @ Dar es salaam serena hotel

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 18.03.2015.

ACACIA'S 2014 CEO EXCELLENCE AWARDS

$
0
0
Chief Executive Officer with Acacia Gold Mine Plc, Brad Gordon, (R), presents the 2014 CEO Excellence Award, to the Security Manager Operations of Bulyanhulu Gold Mine, Assistant Commissioner of Police (rtd), Abdallah Msika, during the Acacia Mining Plc Excellence Award ceremony held at the mining site, in Kahama District, Shinyanga region late on Tuesday, March 17, 2015. The CEO award, is awarded to a person leads by example and is an inspiration to others. Always lives the desired behaviors and is a role model, passionate about their work in Acacia. Witnessing the event, in Bulyanhulu Gold Mine General Manager Michelle Ash
Acacia’s Chief Executive Officer, Brad Gordon, (R), presents the Best Site OHS Performance Safety Award, to Abel Yiga on behalf of North Mara Gold Mine’s General Manager, Gary Chapman, during the 2014 Acacia CEO Excellence Award held at Bulyanhulu Gold Mine in Msalala District Shinyanga region, Tuesday March 17, 2015.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 17/03/2015

WATEJA WA AIRTEL WAENDELEA KUNUFAIKA NA TOYOTA IST ZA YATOSHA ZAIDI

$
0
0
Staff Sargent wa Polisi wilaya ya hanang, Janet Mungolya akimkabithi funguo mshindi wa gari aina ya Toyota IST Bwn Mohamed Ahmed Khamisi mara baada kuibuka mshindi wa droo ya wiki ya nne ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. Bi Emiliana ni mfanya biashara ndogo ndogo na mkazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara akishuhudia ni meneja mauzo wa Airtel kanda ya kaskazini bwana Brighton Majwala.
Staff Sargent wa Polisi wilaya ya hanang, Janet Mungolya akimkabithi funguo mshindi wa gari aina ya Toyota IST Bi Emiliana Tarmo HHaway mara baada kuibuka mshindi wa droo ya wiki ya tano ya promosheni ya Airtel yatosha Zaidi. Bi Emiliana ni mkulima na mkazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara akishuhudia ni meneja mauzo kanda ya kaskazini bwana Brighton Majwala.
Mshindi wa gari aina ya Toyota IST kupitia promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi bwana Mohamed Ahmed Khamisi akiwasha gari lake mara baada ya kukabithiwa gari yake katika halfa iliyofanyika katika uwanja wa mnada wa edasak wilaya ya Hanang mkoani Manyara.


miss tanga 2014 awasaidia vifaa vya shule wanafunzi wasio na uwezo

$
0
0
MREMBO wa mkoa wa Tanga 2014/15,Diana Festo ametoa zawadi za vifaa vya shule kwa wanafunzi wasio jiweza katika shule za msingi Wilayani Pangani,ili kufanikisha azma yake ya kuwataka wanafunzi kutambua umuhimu wa elimu na kuweka juhudi na kuzingatia masomo..

Shule ambazo zilipata nafasi ya kutembelewa na Mrembo huyo na kufanikiwa kupata vifaa hivyo ni ni shule ya msingi Pangani,Funguni, Mwela na shule ya msingi Mwembeni ambazo zote zinapatikana katika wilaya hiyo ya Pangani,huku vifaa vilivyokabidhiwa vikiwa ni Madaftari,Pencel,Rula pamoja na Kalamu ambazo ndio nyezo kuu za kujifunzia.

Pia Mrembo huyo alitembelea kituo cha watoto yatima na waishio katika mazingira magumu chini ya uangalizi wa mawatawa (Sisters) kiitwacho CASA DELA JOIR (wakoregina wa familia takatifu) kilichopo tanga mjini maeneo ya Bombo Hospital,ambapo pia aliwapatia watoto walio shule vifaa vya shule.
Mrembo wa mkoa wa Tanga 2014/15,Diana Festo  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Pangani wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi hizo.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Pangani,akimtambulisha mrembo huyo kwa wanafunzi wa Darasa lake.

U.S. Marines and Sailors train Selous Park Rangers

$
0
0
Selous Game Reserve, TANZANIA.  Ambassador Mark Childress observed on Monday a training of 50 Park Rangers by a team of U.S. Marines and Sailors.  This month long training is aimed at helping the Rangers combat illicit trafficking across the reserve.  The Marines and Sailors are from Special-Purpose Marine Air-Ground Task Force Crisis Response-Africa and are helping to develop small unit tactics, patrolling techniques, night operations, and logistical capabilities to increase the Rangers’ effectiveness within the game reserve.  

During the visit on Monday, the Ambassador observed classroom instruction and field training focused on patrolling techniques.  At the event, the Ambassador highlighted the exceptional reputation of the U.S. Marines in the United States and their effective collaboration with the Tanzanian Park Rangers.  He remarked that the training was progressing well, and reiterated continued U.S. support for the Rangers’ efforts to stop illicit traffickers. 

The Marines will return to Tanzania for follow up training programs later this year.  In addition to military training, the U.S. Government is providing training on such topics as anti-money laundering and more effective prosecution of poachers and illicit traffickers.  In January, the United States and Germany handed over a significant amount of field equipment for use by the game wardens patrolling the reserve. 

The equipment included small and large tents, torches, maps, binoculars, cameras, uniforms and boots.  These efforts are part of a larger Tanzania-wide wildlife conservation program worth $40 million over the next four years that will complement parallel efforts among international partners such as the Paul Allen Foundation, which is funding a new VHF system to allow game scouts to communicate across secure channels.  

To request more information about this event, please email Japhet Sanga (SangaJJ@state.gov), Senior Information Specialist at U.S. Embassy Dar es Salaam.
U.S. Marine training Selous Park Rangers on patrolling techniques. The training is being conducted by U.S. Marines and Sailors from March 2-27 in the Selous Game Reserve and will help develop small unit tactics, patrolling techniques, night operations, and logistical capabilities to increase the Rangers’ effectiveness within the game reserve.
U.S. Marine Lance Cpl. Kyle McAuliffe helps a team of Tanzanian park rangers shoot an azimuth on a compass before conducting a simulated reconnaissance patrol and land navigation exercise at the Selous Game Reserve in Matambwe, Tanzania, March 11, 2015. (U.S. Marine Corps photo by Lance Cpl. Lucas J. Hopkins/Released).

HAPPY BIRTHDAY MAMA MZAZI WA BLOGGER FATHER KIDEVU

$
0
0
TAREHE ya leo ni ndio aliyo zaliwa Mama mzazi wa Blogger na Mpigapicha nguli Tanzania, Mroki Mroki, Bi. Mary O.Nathan  (pichani) wa Kinyenze, Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ambaye leo anatimiza miaka 63 tangu kuzaliwa kwake tarehe kama ya leo. 



Kipekee anamshukuru Mungu kwa kumjalia umri huo alionao hivi sasa. Anawashukuru wote ambao wamechangia yeye kuishi vyema. Anaishukuru sana Familia yake yote kwa umoja na upendo walio nao jambo mabalo anasema linamfanya aishi kwa furaha na amani. 



Aidha watoto wake wote wanampa Pongezi za dhati na Kumuombea Mungu amjalie zaidi Afya njema, akimpa zawadi ya Hekima na Busara katika kipindi hiki cha maisha yake ya utu uzima ambao Busara yake na Hekima vinahitajika sana ndani ya Familia yake na Jamii kwa ujumla.


Wajukuu zako na Vitukuu wako pia wanakusalimia sana na wanakuimbia kale kawimbo ka Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!! Happy Birthday Bibi!!!


Happy Birthday Bibi!!! Dear Bibi Happy birthday to youuuuuuuu!!!!

Wananchi na majirani zako wa pale Kijiji cha Kinyenze ,Kata na Tarafa ya Mlali , Wilayani Mvomero mkoani Morogoro pia wanakutakia heri na fanaka.


HAPPY BIRTHDAY MAMA TUNAKUPENDA SANA NA TUNAJIVUNIA KUWA NA MAMA WA NAMNA YAKO, MUNGU AKUJALIE HEKIMA NA BUSARA ZAIDI KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.



BY: FAMILIA YAKO.

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI JAPAN

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakizungumza na Viongozi wa kampuni ya Japan ya kuengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu ya NEC ambayo inashirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika suala la ufundi na vifaa, wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo jijini Tokyo Machi 18, 2015. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEC Kaono Yono.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya kutengeneza vifaa vya mawasiliano ya simu, Kaono Yono baada ya kuzungumza na viongozi wa kampuni hiyo . Kampuni hiyo nashirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika suala la ufundi na vifaa, wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni hiyo jijini Tokyo Machi 18, 2015. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEC Kaono Yono.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akigana na Rais wa Shirika la Misaada la Kimataifa la Japan (JICA), B. Akihiko Tanaka baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani jijini Tokyo Machi 18, 2015.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akizungumza na Mbunge wa Bunge la Japan kutoka Chama Tawala cha Liberal Democratic Party, Koya Nishikama (katikati) kwenye Ofisi za Bunge la Japan jijini Tokyo Machi 18, 2015. Wengine pichani ni maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Japan.
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akiagana na Mbunge wa Bunge la Japan kutoka Chama Tawala cha Liberal Democratic Party, Koya Nishikama baada ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Bunge la Japan jijini Tokyo Machi 18, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Membe amwakilisha Rais Kikwete kwenye hafla ya kumwapisha Waziri Mkuu mpya wa Lesotho

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wa katikati alipokuwa anaingia kwenye uwanja uliotumika kumwapisha Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisili jijini Maseru jana. wengine katika picha, kutoka kulia ni Bibi Talha Mohammed, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambaye pia anawakilisha Lesotho. kutoka kushoto ni Maafisa wa Serikali ya Lesotho.
Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Mosisili (kushoto) akikabidhiwa Bendera ya nchi hiyo na Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Thom Thabane kama ishara ya kukabidhiwa rasmi madaraka ya uwaziri Mkuu.

Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisili akitoa neno la shukrani baada ya kuapishwa.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 109939 articles
Browse latest View live




Latest Images